Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA INAYOENDESHWA NA UTT AMIS YAPATA FAIDA KUBWA

$
0
0
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa UTT AMIS Bw.Simon Migangala akiongea na waandishi wa habari jana Dar es salaam kuhusiana na ufanisi wa mifuko kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

UTT AMIS ndiyo waendeshaji na waanzilishi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja nchini.Mpaka sasa wanaendesha mifuko mitano ya uwekezaji ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa wekeza Maisha,Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye zaidi ya shilingi bilioni 227.

Bwana Migangala aliwaambia waandishi wa habari kuwa kwa ujumla ukuaji wa mifuko umekua mzuri na umewezasha kutoa faida nzuri kwa wawekezaji wake zaidi ya 100,000 kwa kipindi cha miezi sita iliyopita. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Naibu Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Moshi vijijini ampongeza Rais Kikwete

$
0
0
Na Bakari Issa,Dar es Salaam

Naibu Kamanda wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),Wilaya ya Moshi vijijini,Innocent Melleck amempongeza Rais Jakaya Kikwete na Serikali kwa ujumla kwa kuwajali wananchi wa kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga waliopatwa na janga la kubomokewa na nyumba zao kutokana na mvua iliyoambatana na mawe makubwa na upepo mkali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Melleck amesema kitendo cha Rais Kikwete kuahidi kuwajengea nyumba wananchi hao kinaonyesha namna anavyowajali wananchi hao.

Melleck ambaye  amejitolea kuingia katika kinyanganyiro cha kuwania ubunge jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),amesema Serikali ya Rais Kikwete imewasaidia wananchi waliopatwa na majanga mbalimbali wakiwamo wananchi wa Mbagala na Gongo la Mboto waliolipukiwa na mabomu.

Aidha,Melleck amewapongeza viongozi wa CCM kwa juhudi kubwa zinazofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Abrahamani Kinana na Katibu Mwenezi na Itikadi,Nape Nnauye ambao wamefanya kazi kubwa ya kuimarisha Chama huko mikoani na kuweza kuwa viongozi wa kwanza kuzunguka na kuwafikia wananchi.

Pia,Melleck amesema viongozi wamekuwa kiungo kikubwa sana kwa vijana na kutoa mwanga mpya wa nafasi za vijana katika nafasi za uongozi kuwa kubwa pasipo kuwa na upendeleo wowote,na kusema kuwa juhudi na ushirikiano wao ndiyo unaoleta taa ya kijani kwa vijana kuanzia ngazi za chini hadi ubunge.
Naibu Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Moshi vijijini, Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari.

Idara ya Uhamiaji yaendelea kupambana na uhamiaji haramu nchini

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

IDARA ya Uhamiaji nchini,Imesema inaendelea kupambana na uhamiaji haramu nchini na kuwataka wananchi waendelee kutoa taarifa za wahamiaji haramu na hatua zinachukuliwa dhidi ya wahamiaji hao.

Hayo ameyasema,Naibu Kamishina wa Idara ya Uhamiaji na Msemaji wa Mkuu wa Idara hiyo,Abbas Irovya ,amesema idara ya uhamiaji inaendelea kupambana na wahamiaji haramu na kufanya uhamiaji haramu kupungua.

Irovya amesema kuwa kuna gazeti moja la wiki jina tunalihifadhi liliandika habari yenye kichwa cha habari kisemacho uhamiaji wanauza nchi kutoka kwa mtoa taarifa Ajazi Ahmed Raia wa Pakistani,idara hiyo inasema mtu huyo aliondolewa nchini tangu mwaka jana.

Amesema Ajazi Ahmed alikuwa kazi yake nchini ni kuingiza wahamiaji haramu ambapo alihukumiwa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kifungo cha miaka 18 au faini ya Sh.milioni tano ambapo mtuhumiwa alilipa kwa taratibu za kimahakama na kuondolewa nchini kwa kushirikiana na ubalozi wa Pakistan nchini.

Amesema kutokana na taarifa hizo wananchi wametakiwa kuupuza habari hizo kutokana na kukosa msingi dhidi ya  mtu huyo ambapo aliondolewa nchini kutokana na usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Irovya amesema wahamiaji haramu wamekuwa wakitoka nchi 47 zikiwemo nchi za Afrika huku Ethiopia ikiongoza kwa kuwa na wahamiaji wengi kuliko nchi nyingine na wengine wana kesi wako katika magereza yetu nchini.

“Tuko hapa kwa kutoa huduma taarifa hizo hazina ukweli na kama kuna mtu katumika kutoka idara yetu hatua zitachukuliwa dhidi yake kutokana na utaoaji taarifa za uongo kwa jamii kutoka katika chombo cha serikali,amesema Naibu Kamishina Irovya.
Naibu Kamishina wa Idara ya Uhamiaji na Msemaji wa Mkuu wa Idara hiyo,Abbas Irovya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari,kwenye ofisi za Uhamiaji,jijini Dar es salaam leo.

Mpigie kura Kijana Mayunga katika #‎AirtelTRACEStar

KITUO CHA YATIMA CHAMAZI CHAELEMEWA NA KARO ZA WANAFUNZI

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Save Vulnerable, Fredy Kayula (kulia) akimpatia Kiongozi wa kituo hicho, Mchungaji Amani Kayuni, (wa kwanza kushoto) msaada wa nguo, chakula na vifaa vingine kwa watoto wasiojiweza katika kituo cha Yatima Group Trust Fund kilichopo eneo la Chamazi,Mbagala wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watoto wanaolelewa kwenye Kituo cha Watoto Yatima cha Chamazi Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
---

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Kituo cha Watoto Yatima cha Chamazi Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, kimesema kinakabiliwa na changamoto ya kulipia karo wanafunzi waliopo elimu ya msingi,Sekindari na Chuo Kikuu na kutaka msaada kwa jamii kuweza kuwasaidia ili waweze kusoma.

Hayo aliyasema Mkuu wa Kituo hicho,Winfrida Lubanza wakati akipokea msaada kutoka Taasisi ya Save Vulnerable Foundation(S.V.F)kwa kushirikiana na Kanisa la EAC lilopo Sinza jijini Dar es Salaam,Winfrida amesema kituo kina miradi mbalimbali wanayoendesha ambayo ni michanga hawawezi kotokana na uchanga huo.

Amesema changamoto zingine ni chakula pamoja na kuweza kupata ukuta katika kituo hicho ambapo msaada mkubwa wanategemea kutoka katika jamii zikiwemo taasisi ,makampuni pamoja na mtu binafsi kutoa msaada katika jamii hiyo iweze kusonga mbele na kufikia malengo yao.

Mwenyekiti wa SVF, Fredy Kajula amesema wataendelea kutoa msaada kwa watu wa jamii hiyo kutokana na program zilizopangwa watoto walio katika mazingira magumu.
Kajula amesema msaada huo nguo ,mchele ,unga wa mahindi pamoja na vifaa vya mashuleni ambavyo vimechangiwa na kanisa pamoja na taasisi hiyo.

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AIPONGEZA JICA KWA UFADHILI WA MIRADI MBALIMBALI YA BARABARA NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe (kushoto), akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu Mwakilishi Mkuu wa zamani wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Yasunori Onishi, ofisini kwake jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini.Mwakilishi huyo ameishukuru Wizara ya Ujenzi kwa ushirikiano aliopata katika kipindi chote alichohudumu nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkuu mpya wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Toshio Nagase (kulia) Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe akifurahi jambo na Ujumbe kutoka wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) wakati ugeni huo ulipotembelea ofisini kwake kwa lengo la kutoa pongezi za JICA kwa Wizara ya Ujenzi kutokana na utekelezaji mzuri wa miundombinu ya barabara.Picha na Habari kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

---
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe amelipongeza Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan (JICA) kwa ufadhili wa miradi mingi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara iliyokamilika na inayoendelea nchini.

Eng. Iyombe ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam wakati akiagana na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Bw. Yasunori Onishi, ambae amemaliza muda wake na kumpisha Mwakilishi Mkuu mwingine Bw. Toshio Nagase.

Serikali yajidhatiti Kudhibiti Makosa ya Utakatishaji fedha haramu Nchini- AG Masaju

$
0
0
Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi za Mwanasheria Mkuu za Singida,Pwani na Dar es Salaam wakifuatilia mafunzo kwa makini.
Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya ufunguzi wa kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (hayupo pichani) kushoto ni Bw. Denis Mongula kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Bi Rhoda Martin ,Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya Dodoma akitoa neno la shukrani mara baada ya mafunzo hayo kufunguliwa rasmi.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon 2015 yazinduliwa mjini Bagamoyo leo

$
0
0
Mkurugenzi wa kampuni ya 4Beli, Gilbert Herman (kulia) akihutubia wakati uzinduzi wa mashindano ya Mbio Ndefu ya Bagamoyo Historical Marathon 2015 yanatarajiwa kutimua vumbi Juni 14 mwaka huu mjini Bagamoyo Mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Bagamoyo, Pwani leo. Wengine kutoka kushoto ni, Kaimu Ofisa Michezo Wlaya ya Bagamoyo, Hamisi Kimenya, Mwenyekiti wa Riadha Tanzania Mkoa wa Pwani, Joseph Luhende na Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Hudumaza Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Eliudi Eliakimu aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi na Uhakiki wa Ubora wa Hudumaza Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Eliudi Eliakimu aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo katika uzinduzi huo akisoma hotuba ya mheshimiwa waziri.
Kaimu Ofisa Michezo Wilaya ya Bagamoyo, Hamisi Kimenya (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon yanaandaliwa na kampuni ya 4Beli ya jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti chama cha Riadha Mkoa wa Pwani, Joseph Luhende (wa pili kushoto) akizungumzia maendeleo ya riadha katika mkoa huo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mbio Ndefu ya Bagamoyo Historical Marathon 2015 yanatarajiwa kutimua vumbi Juni 14 mwaka huu mjini Bagamoyo Mkoani Pwani.
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua taarifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Bagamoyo Historical Marathon mjini Bagamoyo, Pwani leo.

Rais Kikwete afungua Kituo Cha Taifa Cha Kumbukumbu Dodoma

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Taifa Kumbukumbu huko kisasa mjini Dodoma leo.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, watatu kushoto ni Mwenyekiti wa BungeMh. Zungu na kulia ni Waziri wan chi Ofisi ya Rais Utawala BoraMh.George Mkuchika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kufungua rasmi Kituo cha Taifa Cha Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia jalada la mwaka 1940 ambapo alisoma utendaji kazi wa Babu yake Chifu wa Kabila la Wakwere Mrisho Kikwete wakati huo.Jalada hilo ni moja ya majalada ya zamani yaliyohifadhiwa kutumia teknolojia ya kisasa katika Kituo Cha Taifa Cha Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini Dodoma.Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa kituo hicho Rais Kikwete ametoa agizo la kuanzishwa maktaba za Viongozi wa kitaifa hususan marais wastaafu ili kuhifadhi vyema historia ya nchi.(picha na Freddy Maro).

TASWIRA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia akijibu swali la Mhe.Haroub Shamis Mbunge wa jimbo la Chonga kuhusu jinsi gani serikali inawasaidia waadishi kuandika habari za kibiashara,Mjini Dodoma.
Mhe.Victor Kawawa akichangia hoja juu ya Muswada wa sheria ya udhibiti wa Ajira za wageni wa mwaka 2014 uliyosomwa na Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka, leo tarehe 18/03/2015 bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janet Mbene akijibu swali la Mhe.Philipa Mturano Mbunge wa viti maalum lililokuwa likihoji ni namna gani Serikali imejipanga kuthibiti biashara ya vyuma chakavu kutokana na kuwepo na wizi wa mabomba.

THIS FRIDAY @ RHAPSODY'S (Viva Towers- Town) MUSIC BY GROOVEBACK DEEJAYS

Usalama wa kutosha Tamasha la Pasaka

$
0
0
Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka, Khamis Pembe, akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5.  Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama. (Picha na Francis Dande).
 Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5. Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.

NA LOVENESS BERNARD

KAMATI ya Tamasha la Pasaka, imewahakikishia usalama wapenzi wa muziki wa Injili na Watanzania kwa jumla katika tamasha hilo litakalokata utepe Aprili 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Kamati hiyo, Khamis Pembe, alisema tayari wamewasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna (CP), Suleiman Kova.

Alisema maandalizi ya Tamasha la Pasaka yamekamilika asilimia 90 na mwaka huu litakuwa la aina yake.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Alex Msama, alisema mwaka huu tamasha linaadhimisha miaka 15 tangu lianzishwe na wanatarajia kumwalika Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kujumuika nao, kwani ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati linaanzishwa.

Msama aliwataja waimbaji wengine watakaokuwepo katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na John Lisu na Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama huku wakiwa katika mazungumzo na mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Rose Muhando, kutokana na maombi ya wapenzi wengi wa tamasha hilo.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI MKOANI ARUSHA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi kwa kupeleka zege kwenye eneo husika wakati wa ujenzi wa daraja la Kisongo,ambalo lilikuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana na barabara ya eneo hilo kulika na mmomonyoko wa udongo.
Ujenzi wa daraja la Kisongo ukiendelea kwa kasi,ambapo pia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alikagua na kushiriki ujenzi wake.
Baadhi ya wananchi wa Kisongo wakipita juu ya barabara ambayo imeanza kuathirika na mmomonyoko wa udongo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege wakati wa ujenzi wa kituo cha afya cha Manyire,ujenzi wa kituo hicho unatarajia kuisha mwaka huu ambapo kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 500 zitakuwa zimetumika kukamilisha ujenzi huo. 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM ya sasa haitofanya makosa, na kuwahakikishia kila atakayefanya makosa itabidi aubebe msalaba wake. 
 Mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Ndugu Goodluck Ole Medeye akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nduruma ambao walikuwa na malalamiko juu ya mradi wa maji wa Nduruma kuonekana kupelekwa mashambani badala ya maeneo wanayoishi wananchi.Ndugu Kinana wa pili kushoto alikuwepo kusikiliza malalamiko hayo na kuwapatia majibu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngaramtoni ambapo alitoa sababu mbali mbali za dalili za kufa kwa upinzani nchini.
Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo,Said Mwishehe akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya mkutano wa hadhara kufanyika ndani ya jimbo la Arumeru Magharibi,pichani shoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza.Ndugu Kinana yupo kwenye ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.


PICHA NA MICHUZI JR-ARUMERU MAGHARIBI ARUSHA.

EU WAMPA TUZO MAMA HELEN- KIJO BISIMBA

$
0
0
MAMA
Umoja wa Ulaya umemtunuku Mama Helen Kijo- Bisimba (pichani) kutokana na mchango wake kwa ajili ya kutetea na kulinda haki za binadamu nchiini.
Tuzo hiyo, ilitolewa juzi na EU siku ya Jumanne wiki hii jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Maendeleo Ulaya 2015.

Balozi wa Umoja wa Ulaya bwana Filberto Sebregondi alitoa tuzo hizo na kusema kuwa lengo lake ni kusimamia haki kwenye masuala ya kiulimwengu ikiwemo kupambana na umasikini na kuhamasisha raia kujihusisha na maendeleo.

Wengine waliotunukiwa tuzo katika hafla hiyo pamoja na Mama Bisimba ni wanamziki Keisha Shaban, Fareed Kubanda (FID Q), na Balozi Ami Mpungwe, pamoja na Paul Ndunguru ambae ni msanii na mchoraji.

EU imekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu hususani ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ikiwemo vitendo vya ukeketaji, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe.
Vilevile, EU imekuwa mstari wa mbele kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kupinga adhabu ya kifo.

MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA SHEREHE YA KUTIMIZA MWAKA VIKUNDI VYA WAMA HUKO NACHINGWEA/AKABIDHI MADAWATI

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Nachingwea kuhudhuria sherehe za kutimiza mwaka za vikundi vya WAMA kwenye Mradi wa Mwanamke Mwezeshe tarehe 18.3.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaonyesha waalikwa zawadi mbalimbali alizopewa na wanavikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe mkoani Lindi. Sherehe hizo zilifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Elimu Nachingwea tarehe 18.3.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti kwa Ndugu Fatuma Mchia, Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi vya WAMA Kwenye Mradi wa Mwanamke Mwezeshe kwa kuvuka lengo kwa kuingiza wanavikundi wengi kwenye mradi huo.


MAAFISA RASILIMALI WATU TOKA WILAYA YA ILALA WAGUSWA NA KUJIUNGA KWA WINGI KATIKA MPANGO WA HIARI WA KUJIWEKEA AKIBA (VSRS) KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA GEPF

$
0
0
Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF.Bw.  Aloyce Ntukamazina akiwasilisha mada juu ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji katika Mfuko wa GEPF,wakati wa semina kwa Maafisa Rasilimali Watu kutoka Wilaya ya Ilala iliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock,jijini Dar es salaam.
 Meneja wa GEPF mkoa wa Ilala,Bw Jafari Meraji akisisitiza jambo juu ya faida zipatikanazo katika mpango wa hiari wa kujiwekea akiba (VSRS)
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo Bw Sebastian Enosh ambaye ni Meneja Rasilimali watu kutoka DIT akitoa mchango wake pamoja na ushauri kwa Mfuko wa GEPF.
Pichani baadhi ya washiriki wa semina hiyo maalum wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na maafisa wa GEPF.
Maafisa Rasilimali watu wakipata maelekezo ya kujaza fomu na kujiunga na mpango wa hiari wa kujiwekea akiba kutoka kwa Afisa Masoko wa GEPF Bw Avit Nyambele.

EUROPEAN UNION PROVIDES OVER €56,000 TO HELP THE VICTIMS OF THE HAIL STORMS IN TANZANIA

$
0
0
19 March 2015, Dar-es-Salaam – To bring urgently needed assistance to the victims of the hail storms that hit Shinyanga region earlier this month, the European Commission is providing humanitarian funding through Tanzania Red Cross Society.

Up to 5,000 people were affected by the storms, 3,500 of whom have been uprooted from their damaged or destroyed houses. Strong winds ripped off roofs, killing 47 people and injuring 112, the majority of whom were children.

The people affected urgently require food, shelter, clean drinking water and sanitation services as well as basic items such as blankets, buckets, kitchen sets, mattresses, mosquito nets, soap and school material.

The EU-funding of EUR €56,184 is being channelled through the Red Cross who operates with funding from the Disaster Relief Emergency Fund (DREF).

The hail storms accompanied by strong winds and heavy rainfall hit the villages of Mwakata, Magung’unhwa and Nhumbi in Msalala district, Shinyanga region, some 1,000 kilometres North-West of Dar- es- Salaam.

Bunge lapitisha Muswada wa Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni nchini

$
0
0
Na. Anitha Jonas na Johary Kachwamba -MAELEZO, DODOMA

WAZIRI wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka amesoma Muswada wa Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni nchini wa mwaka 2014 kwa mara ya pili ikiwa muswada huu umelenga masuala mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kiuchumi pamoja na mahitaji ya kiteknolojia ambayo ni kichocheo kikubwa  cha uhamiaji wa nguvu kazi kutoka nchi moja kwenda nyingine.

 Mhe.Kabaka alisema kwa sasa zipo mamlaka nyingi zinzotoa vibali vya ajira kwa wageni kwa kuzingatia sheria zinazosimamia maswala ya Uhamiaji, Uwekezaji, Elimu, Biashara na Wakimbizi, hivyo hali hii ya kuwepo na mamlaka nyingi zinachangia  kusababisha usumbufu kwa wawekezaji na kokosekana kwa uwajibikaji pamoja na kuwepo na udanganyifu.

“Kutungwa kwa sheria hii kunalenga kutelekeza kwa manufaa ya nchi yetu mikataba ya kikanda inayoruhusu uhamiaji huru wa nguvu kazi hususani inayohusu itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afika Mashariki na Ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika SADC” alisema Mhe. Kabaka.

Katika kutekeleza mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu uhamiaji na nguvu kazi, utaratibu wa kutoa vibali vya ajira kwa wageni umekuwa ukitumika ili kuhakikisha nguvu kazi ya wageni hao inaleta manufaa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na pia katika kulinda ajira za wananchi.

Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani Mhe.Celina Paresso Mbuge wa Viti Maalum-CHADEMA aliishauri Wizara ya Kazi na Ajira kushirikiana na wizara mtambuka kama Wizara ya Viwanda na Biashara na Idara ya Uhamiaji, kufanya ukaguzi wa vibali vya ajira hasa katika maeneo ambayo raia wa kigeni wanafanya shughuri zao bila kuzingatia sheria za nchi.

“Tanzania tuna maliasili nyingi, lakini dunia ya leo na ijayo itatawaliwa na wenye maarifa, kwa maana ya sayansi, teknolojia, elimu na ujuzi” alisema Mhe. Paresso

“kuwa na maliasili peke yake haitoshi, hatuna budi tujinoe kwa elimu na ujuzi, na hasa elimu inayomuwezesha mtu aajirike au ajiajiri” aliongezea Mhe. Paresso

Endapo Mhe. Rais ataridhia, Sheria hii itaanza kutumika tarehe 1 Julai, 2015. Kutungwa na kuanza kutumika kwa Sheria ya Ajira ya Wageni Nchini kutakuwa na matokea chanya ikiwema uratibu mzuri wa ajira za wageni nchini, kuongezeka kwa ajira za watanzania na kuongezeka kwa ujuzi kwa wafanyakazi wa Tanzania.

WAFANYAKAZI KUTOKA CLOUDS MEDIA GROUP WALIPATA FURSA YA KUTEMBEA MAKAO MAKUU YA MFUKO WA PENSHENI YA PSPF NA KUJIONEA WENYEWE UBORA WA HUDUMA NA BIDHAA ZA MFUKO

$
0
0
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Godfrey Ngonyani (kushoto) akimkabidhi zawadi mtarishaji wa kipindi maarufu cha Power Breakfast Bw. Phillip Mwihava baada ya kumalizika kwa semina ambayo PSPF iliandaa maalum kwa watendaji kutoka Clouds Media. Lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha kwanini PSPF inaendelea kuwa chaguo la kwanza kwa waajiriwa wapya hapa nchini. Anayeshuhudia Bibi. Neema Muro, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF.
Afisa uhusiano Mwandamizi wa Clouds Media Bw. Kelly Michael (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa semina iliyoandaliwa maalum kwa watendaji wa Clouds Media, kulia ni Said Mohamed maarufu kama Bonge naye akifatilia kwa makini semina hiyo iliyolenga kuwaelimisha juu ya huduma na bidhaa mbalimbali za PSPF.
Watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na wageni wao kutoka Clouds Media wakiwa katika picha ya pamoja baada ya semina iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya watendaji wa Clouds Media.

Na Mwandishi Wetu

Mwanzoni mwa wiki hii wafanyakazi wa Clouds Media Group walipata fursa ya kutembelea Makao Makuu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa lengo la kujengewa uwezo juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na PSPF. Ziara hiyo iligawanyika katika sehemu mbili, ya kwanza ilikuwa ni semina na ya pili ilikuwa kutembelea maeneo mbalimbali ya PSPF ili kuweze kujionea utendaji kazi wa Mfuko huo ambao kwa sasa ndio changuo la kwanza kwa waajiriwa wapya nchini.

Semina hiyo iliendeshwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bibi. Neema Muro ambaye aliwaeleza kwa kina juu ya bidhaa na huduma zinazotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF. Bibi. Muro alisema Mfuko wa PSPF una mafao ya muda mfupi ambayo ni fao la uzazi, mkopo wa elimu, fao la kujitoa, mkopo kwa mwajiriwa mpya, mkopo wa nyumba na mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu. Aliyataja mafao ya muda mrefu kuwa ni fao la uzeeni, fao la ulemavu, fao la mirathi na fao la kufukuzwa au kuachishwa kazi.

Pia Mkurugenzi huyo alieleza kwamba PSPF ina mpango wa uchangiaji wa hiari ambao mwanachama wake ni mtu yeyote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea na anaweza kuwa katika sekta rasmi na hata katika sekta isiyo rasmi, kima cha chini cha kuchangia nia shilingi 10,000 tu kwa mwezi. Mafao yanayotolewa chini ya mpango huu ni pamoja na Fao la elimu, Fao la ujasiriamali, fao la uzeeni, fao la kifo, fao la ugonjwa au ulemavu na fao la kujitoa.

Kwa upande wa uwekezaji, Bibi Muro alisema Mfuko una vitega uchumi vya muda mrefu ambavyo ni pamoja na jengo la Golden Jubille Towers lenye ghorofa 21 ambalo ndio Makao Makuu ya PSPF, Jengo la PSPF Commerial Towers ambalo lina ghorofa 35, jengo hili ni refu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati. Pia PSPF imewekeza katika ujenzi wa Chuo cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.

Mfuko pia umejenga nyumba kwa ajili ya kukopesha wanachama wake na watanzania wengine katika mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam, Shinyanga, Mtwara,Tabora na Iringa. Baada ya semina hiyo wageni hao kutoka Clouds Media Group walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya PSPF kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa Mfuko huo na pia kutembelea baadhi ya maeneo ya uwekezaji wa Mfuko.

Baada ya ziara hiyo, kiongozi wa timu kutoa Clouds Media, Bw. Kelly Michael alisema, “ ziara hii imetupatia elimu ya kutosha juu ya PSPF…hakika kuna mengi tulikuwa hatuyajui lakini sasa tunaweza kumepata uelewa wa kutosha juu ya Mfuko huu,”.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania awasilisha mada kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje

$
0
0
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu akiwasilisha mada kuhusu  "Exchange Rate Developments in Tanzania and Implications for the Economy" kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa Semina fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam tarehe 18 Machi, 2015.  Katika mada yake Prof. Ndulu  alielezea pamoja na mambo mengine umuhimu wa Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake nje ili kudhibiti mfumuko wa bei na kuipandisha thamani  Sarafu ya Tanzania dhidi ya sarafu nyingine hususan Dola ya Marekani, kuimarisha upatikanaji wa fedha za nje kama dola na kuvutia zaidi wawekezaji nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akifuatilia uwasilishwaji wa mada kutoka kwa Prof. Ndulu (hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Irene Kasyanju na kulia ni Balozi Mstaafu Elly Mtango.    
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akiwa na  Katibu wa Waziri Membe, Bw. Thobias Makoba  wakimsikiliza Prof. Ndulu ambaye hayupo nchini.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images