Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 771 | 772 | (Page 773) | 774 | 775 | .... | 3348 | newer

  0 0

  H.E Michael D. Higgins, President of Ireland
  H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Michael D. Higgins, President of Ireland on the occasion of the National Day of Ireland on 17th March 2015.

  The message reads as follows;

  “H.E. Michael D. Higgins,

  President of Ireland

  Dublin

  IRELAND

  Your Excellency and Dear Colleague,

  It is my pleasure and privilege to extend to you and through you to the Government and people of Ireland my heartfelt congratulations on the occasion of your country’s National Day.


  Tanzania cherishes the good relations and co-operation that happily exist between our two countries.  

  On this historic day, I take the opportunity to reaffirm my country’s commitment and desire to continue working with you and your Government in strengthening further the existing ties of friendship and co-operation for the mutual benefit of our two countries and peoples.


          Please accept, Your Excellency, my best wishes for your continued good health and prosperity for the people of Ireland”.  Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam


  16th March 2015


  0 0  0 0

   WAHARIRI 22 wa Vyombo vya habari mbali mbali nchini jana walifanya ziara kwenye Kiwanda cha Kampuni ya  Bia Tanzania(TBL) wakiongozwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF).

  Katika ziara hiyo Wahariri hao walipata maelezo mbali mbali kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Roberto Jarrin kuhusu hali ya kibiashara ya kampuni hiyo pamoja na bidhaa zinazozalishwa kisha kutembelea mitambo ya kutengeneza Bia.

  Meneja wa Kiwanda cha Bia Mbeya, Waziri Jemedari aliwaambia Wahariri Changamoto ambazo Kiwanda hicho kinakabiliana nazo kuwa ni pamoja na umeme wa grid ya taifa kuwa na nguvu ndogo ya kutokutosha kuendesha mitambo, ubovu wa barabara ya kuingilia kiwandani pamoja na upatikanaji wa maji.

  Akitoa Shukrani kwa niaba ya Wahariri, Mwenyekiti wa TEF, Absolom Kubanda, aliishukuru Kampuni ya TBL kwa kuwathamini na kuwaalika katika ziara hiyo na kuongeza kuwa watakuwa mabalozi wazuri kutangaza hali halisi waliyoiona kiwandani hapo tofauti na maneno ya watu mitaani.

  Alisema watu wengi hudhani mazingira ambayo vinywaji vinatengenezwa hayafai jambo ambalo sio la kweli kutokana na kujionea wenyewe mlolongo mzima tangu uoshaji wa chupa hadi kinywaji kinavyojazwa kuwa katika hali ya usafi.
  Kwa upande wake Meneja uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Editha Mushi alisema lengo la kuwaalika Wahariri wa Vyombo vya habari ni kudumisha uhusiano baina ya TBL na Vyombo vya habari.

  Aliongeza kuwa lengo lingine ni kutoa mrejesho kwa jamii juu ya hali ya kibiashara ilivyosasa na awali kupitia kwa Wahariri wa Vyombo vya habari ili iwe wazi kwa kila mtu.


        Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Bia(TBL) na SUBMiller East Africa Operesheni, Roberto Jarrin, akiwasilisha Mada kwa Wahariri wa Vyombo vya habari nchini waliofanya ziara katika kiwanda cha Bia Tawi la Mbeya.


     Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari akitoa maelezo kuhusu kiwanda hicho kwa Wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Mwandishi Maalum,  New York

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban  Ki Moon  amemteua Jaji Mkuu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Mohamed Chande Othman (pichani)   kuongoza jopo  huru la wataalam watakaopitia taarifa mpya  kuhusu kifo cha   Bw. Dag  Hammarskjold ambaye  aliwahi kuwa   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

  “ Katibu Mkuu anayofuraha ya  kutangaza kwamba amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa   jopo huru la wataalamu. Bw.  Mohamed Chande Othman kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ambaye atakuwa mkuu wa jopo hilo. Wajumbe wengine ni  Bw. Kerryn Macaulay kutoka Australia na Bw.  Henrik Ejrup  Larsen kutoka Denmark” inasomeka taarifa  iliyotolewa   na   Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu

  Uteuzi wa Jopo hilo unatokana na Azimio   namba 69/246 la Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa lililopitishwa  tarehe   29 mwezi Desemba  2014  ambalo lilimtaka   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuteua jopo la wataalam huru ili kuchunguza na kutathimin thamani ya taarifa mpya ( probative value)zinazohusiana  na kifo  cha Katibu  Mkuu  Dag Hammarskjold pamoja  na watu waliofuatana naye.

  Bw. Dag Hammarskjold na ujumbe wake alipoteza maisha katika ajali ya  ndege iliyotokea mwaka 1961 wakati akitokea  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

  Baadhi ya  Majukumu ya Jopo hilo huru la wataalamu pamoja na mambo mengine  yatakuwa kupitia na kutathmini thamani ya  taarifa mpya ambazo Kamisheni ya Hammarskjold imeziwasilisha   kwa Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Vile vile  litatathmini   taarifa mbalimbali ambazo zimetolewa na  nchi wanachama na vyanzo vingine.


  Jopo hilo la wataalam huru litaanza kazi yake mwisho mwa mwezi huu wa March ( 30 March) na  linatarajiwa  kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu  Mkuu si Zaidi ya  tarehe 30 mwezi June mwaka huu.


  0 0

  Na   Bashir  Yakub.

  Suala  la matunzo  ya  watoto/mtoto  lim ekuwa  ni suala  ambalo  wasomaji  wengi  wamekuwa  wakiniuliza sana. Wengi  wao  wanaouliza  ni  wale  ambao  wamezaa  nje  ya  ndoa  na  hivyo  kuna  utata  wa  matunzo  ya  watoto  na  wale  ambao  wamekuwa wana ndoa  lakini  sasa  tayari  wametengana  aidha  kwa  talaka  au  bila  talaka.  Niseme  tu kwa  ufupi  kuwa  suala  la  matunzo  ya watoto  linajumuisha  mambo  mengi  nami  nitaeleza  baadhi  tu.


  1.HUWEZI  KUMLAZIMISHA  MTOA  MATUNZO  KUTOA  AMBACHO  HANA.

  Kumekuwepo  na  tabia  ya  wazazi  hasa  upande  wa   wazazi  wa  kike   kuwalazimisha  wanaume  ambao  wamezaa  nao  na  kutengana  nao  kutoa  matunzo  ya  watoto  kwa  kiwango  cha  juu  kabisa  ambacho  pengine   kinazidi  hata  kipato  cha   mtoaji. Hili  si  sawa.  Ni  kweli sheria  inamlazimisha  mwanaume  kutoa  matunzo  ya  mtoto    lakini  haimlazimishi  kutoa  kuliko  anachopata. Sheria   haiseme  kwakuwa  mwanamke  anaishi  na  mtoto  wa  mtu  basi mwanaume   ndio  sasa afanywe  kitega  uchumi.  Inafikia  hatua  mwanamke  hafanyi  kazi  yoyote  isipokuwa  anategemea  ile  pesa  ya matunzo  ya  mtoto  ndio  iwe  kila  kitu  katika  maisha  yake.

  Hii  ndio  sababu  hata  akipewa  kiasi   kinachotosha  haoni  kama  kinatosha  kwakuwa kinakuwa  na  njia  nyingi  kama  saluni, nguo za kuvaa,  pesa  ya  upatu, michango  ya  harusi  na  kitchen  party  na  kila  kitu  kinachohusu  maisha  yake binafsi.  Ieleweke  wazi  kuwa  kwa  mujibu  wa  sheria  pesa  ya  matunzo  ya  mtoto  haihusiki  na  haya.  Pesa  ya  matunzo  ya  mtoto  ni  pesa  ya  matunzo   ya  mtoto  kama   neno  lenyewe  lilivyo  na  linavyojieleza si  vinginevyo.


  2.INARUHUSIWA  KUKATAA  IKIWA  UNALAZIMISHWA  KUTOA  MATUNZO YANAYOZIDI  UWEZO WAKO.

  Ikiwa  mwanaume  analazimishwa  kutoa  kuliko  kipato  chake  basi  anaruhusiwa  kukataa  hata  kama  amri  hiyo  imetolewa  na  mahakama. Wengine  huandikishana  polisi  lakini  bado  haibadili  maana  kwakuwa  mtu  anatakiwa  kutoa  kulingana  na  uwezo wake  au  kipato  chake. Wapo  wazazi  hasa  wa kike   ambao  huwalazimisha  wanaume  kutoa  matunzo ya  kuwasomesha  watoto   international  schools  wakati  kipato  cha  mwanume  ni  shule  ya  kata. Sheria  inachokataza  ni  kukataa  kabisa   kutoa matunzo  ya  mtoto  lakini  haimlazimishi  mtu  kutoa  kilichomzidi.  Au  wengine  hulazimisha  kuwekewa  mpaka  wafanykazi  wa  ndani( house girl)  wakati  kipato  cha  mwanaume   hakiruhusu  jambo  hilo.


  Huu  nao  ni  unayanyasaji  kwa  upande  wa  wanaume  na  haukubaliwi  na  sheria.  La  msingi  ni   kuwa  iwapo  utalazimishwa  kutoa  kuliko  uwezo  wako   we  kataa.  Na  kama  uamuzi  huo  umetolewa  na  mahakama  basi kataa  kwa  kukata  rufaa  kupinga  kabisa  jambo  hilo. Sheria  inaposema  matunzo  ya  watoto  haisemi  kuwa  watu  watoe  kuliko uwezo  wao  hapana. Sheria  ni  haki   na  haki  huzingatia  ukweli  na  hali  halisi  ya  jambo. 

  0 0

   Wajumbe wakifuatilia majadiliano kuhusu uwezeshaji wa wanawake, ambazo wazungumzaji wakuu  walikuwa ni Balozi Tuvako Manongi,  Waziri K. Kellie kutoka Canada  na Waziri Asa Regner kutoka Sweden katika mchango wake, Balozi Manongi alisema mifuko ya uwezeshaji ambayo imeanzishwa nchini Tanzania ni  moja ya  mafanikio ambayo  imeweza kuwakwamua wanawake kuondokana na  umaskini.   Baadhi ya mifuko hiyo ni  Mfuko wa  Maendeleo  ya Wanawake kwa Tanzania Bara na  Mfuko wa  Maendeleo  ya wanawake  wajasiriamali Tanzania Visiwani.pia alielezea miradi mbalimbali ya uwezeshaji wa wanawake ambayo  inafadhiliwa na wadau wa maendeleo kama vile Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji ya Umoja wa  Mataifa ( UNCDF) unaofadhili  mradi wa kuzalisha umeme  huko  Mkoani Iringa. Majadiliano hayo yaliandaliwa kwa ubia wa UN- Women,  UNCFD na  UNDP
   Katibu Mkuu kutoka  Serikali ya Mapunduzi Zanzibar Bi. Asha Ali Abdullah akifuatilia majadiliano kuhusu wajibu wa wanaume na wanavulana katika kufikia usawa wa kijinsia
   Katibu Mkuu Bi. Anna  Maembe naya akifuatilia majadiliano kuhusu wajibu wa wanaume na wavulana katika kufikia usawa wa kijinsia
   Ajenda  kuhusu wajibu wa  wanaume na wavulana katika kufikia usawa wa kijisia  ulivutia wadhiriki wengi kama inayoonekana katika picha hii.
   Mawaziri Mhe. Zainabu Omar Mohammed, kutoka Serikali ya Mapunduzi Zanzibar na  Mhe Sophia Simba kutoka Serikali ya Muungano wakiwa na mwenyeji wao  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi.
   Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Balozi Tuvako  Manongi akizungumza  katika moja ya  mikutano ya pembezoni  ya Kamisheni  kuhusu  dhadi ya wanawake.  Balozi Manongi alikuwa mmoja wa wazungumzaji walioalikwa kuzungumzia  uwezeshaji wa wanawake kwa kupitia vyanzo mbalimbali   kama  vile mifuko ya maendeleo  na mitaji  mingineyo ili  waweze kujitegemea kwa  katika kumiliki mitaji ya kiuchumi kama sehemu moja wapo ya kuondokana na umasikini. wazungumzaji wengine katika  mkutano  huu  kutoka kushoto ni    Dr. K. Kellie Leitech, Waziri  Ajira na Hadhi ya Wanawake  kutoka Canada,    Bi.Asa Reigner, Waziri wa Watoto, Wazee na Usawa wa Kijinsia kutoka Sweden ( watatu kutoka kushoto).

   Na Mwandishi Maalum, New York

  Mkutano  wa 59 wa Kamisheni  kuhusu  Hadhi ya Wanawake ( CSW) umeingia wiki  ya pili  ambapo wajumbe  wameendelea kujadiliana na kubadilishana   uzoefu kuhusu mada mbalimbali zinazohusu hadhi ya  mwanamke na mtoto wa kike.

  Jana Jumatatu  miongoni mwa majadiliano  ambayo yamevutia  wajumbe wengi  yalihusu wajibu wa wanaume na wavulana katika kufikia usawa wa kijinsia.

  Katika majadiliano hayo ilielezwa kwamba ili kufikia usawa wa kijinsia,  basi  hapana  budi kuhakikisha kwamba wanaume na wanavulana wanashirikishwa  kikamilifu katika safari hiyo.

  Imeelezwa  katika majadilianao hayo kuwa Ushiriki wa wanaume na wavulana  kutaongeza kasi ya kufikiwa kwa usawa wa kijinsia, na kwamba  jukumu hilo haliwezi likawa la wanawake  peke yao.

   Baadhi ya nchi zilichangia  uzoefu wao wa namna gani  zinatekeleza  dhana hiyo ya kuhakikisha kwamba wanaume na  wavulana  wanatimiza wajibu wao kwa   kuhakikisha kwamba  jamii  yote inakuwa na uelewa na ushiriki sawa katika  kufikia lengo la kuwa na usawa wa  jinsia.

  Pamoja na   majadiliano kuhusu mada hiyo, wajumbe wanaoshiriki mkutano huu  pia wameendelea na  majadiliano ya mada  nyingine nyingi zilizokuwa zinafanyika katika kumbi mbalimbali za mikutano hapa Umoja wa Mataifa

  Baadhi ya  mada hizo ni ile iliyohusu : kubadlisha kanuni za jamii,  ili kufikia usawa wa kijinsia, matarajio  na fursa.

  Ajenda kuu ya  Mkutano  wa 59 wa Kamisheni kuhusu  hadhi ya wanawake,  unaohudhuriwa na  wajumbe   kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa,  Taasisi za UM na  wawakilishi kutoka Asasi Zisizo za Kiserikali, ni Azimio la  Beijing na  Jukwaa la utekelezaji,  miaka 20 baada ya kufanyika mkutano wa  nne wa kihistoria wa wanawake, mkutano uliofanyika mwaka 1995 Beijing, China.

  Kupia Ajenda hiyo  ya   Beijing+20) wajumbe wanajadili  changamoto za utekelezaji wake na mafanikio katika   usawa wa kijinsia na uwezeshaji  wa wanawake.

   Wajumbe pia wanajadili matokeo ya kikao maalum cha 23 cha Baraza Kuu  la Umoja wa Mataifa, tathmini  ya miaka mitano baada ya kupitishwa kwa jukwa la utekelezaji, tathmini iliyoainisha hatua Zaidi na mipango  inayotakiwa kutekelezwa  ili kufika  lengo la usawa wa kijinsia na uwezeshaji.

  Vile vile mkutano huu  unajadili fursa kwaajili ya kufikia usawa wa kijinsia  na uwezeshaji  kupitia ajenda mpya za maendeleo baada ya 2015.
  0 0

  1Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)  Mh. Hawa Ghasia akizungumza mapema leo katika siku ya kwanza ya mafunzo ya Wakuu wa Wilaya wapya ishirini na saba yanayoendelea katika ukumbi wa hoteli ya St. Gaspar mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri, Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne A. Sagini na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Elimu) Bw. Zuberi Samataba.


    Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne A. Sagini akitoa mada kuhusu kazi na majukumu ya Wakuu wa Wilaya katika semina hiyo iliyoanza leo tarehe 16 hadi 19 Machi 2015.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja, ambaye pia ndiye mwezeshaji mkuu wa mafunzo hayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Dodoma. UONGOZI Institute ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Rais inayoshughulikia mafunzo kwa viongozi waandamizi serikalini pamoja na kufanya utafiti na ushauri wa sera kwa serikali.

  Mshiriki wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Shaban Kissu akichangia mada wakati wa mafunzo. Mada moja wapo zilizojadiliwa leo ni kuhusu mahusiano na mawasiliano baina ya serikali kuu na mamlaka za serikali za mitaa.

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda akizungumzia kuhusu changamoto mbali mbali za Wakuu wa Wilaya. Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na maadili na sheria za kazi.

    
  Baadhi ya wahudhuriaji wa kundi la Wakuu wa Wilaya wapya ishirini na saba wakifuatilia kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) katika mafunzo ya Wakuu wa Wilaya Wapya yanayoendelea mjini Dodoma.

  0 0

  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ofisi ya Mkoa wa Lindi,Fortunata Raymond akitoa Mada ya Maboresho yanayotekelezwa na Mfuko hususani kitita cha Mafao kwa Wanachama katika Kata namichiga Wilayani Ruangwa ambapo pia aliwataka kutumia Mkutano huo kubainisha Changamoto hasi na Chanya zitakazowezesha Maboresho Ya Huduma Za Matibabu Sambamba Na Sekta Ya Afya Kwa Ujumla,Kushoto Katikati Ni Mtendaji Kata Ya Namichiga Richard Nnonjela Na Kushoto Kabisa Ni Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Msingi Namkonjera Iliyopo Kata Ya Namichiga.
  Watumishi Wa Kada Mbalimbali Ambao Ni Wanachama Wa Mfuko Wa Taifa Wa Bima Ya Afya Waliopo Wilayani Ruangwa Katika Kata Ya Namichiga Wakimsikiliza Meneja Wa Mfuko Wa Taifa Wa Bima Ya Afya Hayupo Pichani Wakati Wa Utekelezaji Wa Mpango Wa Elimu Ya Kata Kwa Kata Sambamba Na Upimaji Wa Afya Kwenye Magonjwa Yasiyoambukiza Ambapo Alisema Yamekuwa Ni Ya Gharama Kubwa Kwa Kuwa Wengi Hawafahamu Dalili Zake Hivyo Uyafahamu Wakati Tayari Yameshafikia Hatua Kubwa Ya Madhara Na Wakati Mwingie Kuchangia Vifo,Hivyo Ofisi Ya Mkoa Wa Lindi Umekuwa Ukitekeleza Kwa Nia Ya Kuongeza Uelewa Na Wanaobainika Kuwa Na Viashiria Kupata Ushauri Wa Kitaalamu Kutoka Kwa Madaktari Wanaotoa Huduma.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizindua mradi wa Maji ya Kisima mtaa wa Mongolandege, Ilala jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoani Dar es salaam. Mradi wa Kisima hicho umegharimu kiasi cha shilingi milioni 78.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akifungua moja ya bomba la maji la mradi wa Maji ya Kisima mtaa wa Mongolandege, Ilala jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoani Dar es salaam.
  Bi. Martha Singano, Mkazi wa Mongolandege akipokea ndoo ya maji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki mara baada ya kuzindua mradi wa Maji ya Kisima katika mtaa huo.


  0 0  Na Paparazi wa Globu ya jamii Ughaibuni,

  Bendi Maarufu ya Muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni usiku wa Jumamosi ya 14 Machi 2015 walifanikiwa kufanya mavitu yao jukwaani na kuliweka jiji la Stuttgart,chini ya himaya na muziki wao,katika onyesho la Africa Unite Party.

  pamoja na ulinzi ulioandaliwa lakini kikosi cha Ngoma Africa band kilikuwa "Fit on Fire",sheria za ughaibuni zinawaruhusu kutinga na viwalo ..kila nchi inautaratibu na sheria zake
  Kamanda Ras Makunja (pili kushoto) akiongoza mashambulizi.
  Nyomi si la kawaida.
  Kamanda Mkuu wa Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni,Ibrahim Makunja a.k.a Kamanda Ras Kamunja akiokwa na kikosi kizima.
  0 0

  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi tarehe 15.3.2015 kuanza ziara ya kikazi ya siku 5 kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Kata ya Tulieni Mjini Lindi wa Chama Cha Wananchi (CUF) Ndugu Shaibu Rajabu Matola (Kikaptura) aliyeamua kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi wakati wa mkutano mkubwa uliofanyika kwenye Kata ya Mikumbi tarehe 16.3.2015.
  Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa Mama Salma Kikwete akikabidhi bati 100 na vifaa vya bendi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Angaza iliyoko katika Manispaa ya Lindi tarehe 16.3.2015. Anayepokea kwa niaba ya shule hiyo ni Mkuu wa Shule Mwalimu Upendo Muro (wa tano kutoka kulia) akiwa pamoja na Ndugu Ashimun Mzava, Afisa Elimu Sekondar, Manispaa Lindi wa nne kutoka kulia) na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo. Aliyesimama wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bwana Abdallah Ulega.


  0 0


  0 0

  Na May-Zuhura Simba

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa ili jamii iweze kukua kwa kasi na kupata maendeleo haina budi kuwekeza katika sayansi na teknolojia.

  Aliongea hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  “ubunifu katika sayansi na teknolojia ni kitu muhimu katika kupata uvumbuzi wa vitu mbalimbali muhimu vinavyoleta maendelao kwa jamii husika hivyo kuna umuhimu wa kuwafungia wanasayansi katika atamizi ili kupata matokeo mazuri ya utafiti” alisema Balozi Sefue.

  Aidha aliongeza kuwa nchi kama Korea na Singapore waliwekeza katika sayansi,technologia na ubunifu na hivyo kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa jamii zao.

  Vilevile alisisitiza kuwa ubunifu ukisimamiwa dhabiti utasaidia katika kuleta mageuzi kwenye sekta muhimu ikiwemo elimu, afya,biashara,kilimo na miundombinu na hivyo kutatua matatizo ya kijamii.

  “Mfano mzuri ni Max malipo ambalo ni zao la vijana wa kitanzania waliokuwa wamewekwa katika atamizi na kuleta uvumbuzi huu kwa kutumia sayansi na teknolojia ” alisema Balozi Sefue.

  Aidha aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo,makampuni binafsi, na serikali kushirikiana kwa pamoja kufungua vituo atamizi zitakavyosaidia vijana kuvumbua teknolojia mbalimbali.
  Mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na wajumbe wa warsha wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya ubunifu wa sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya ubunifu wa sera ya Taifa katika Sayansi na Teknolojia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(katika) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu(kushoto), na Naibu Katibu Mkuu wa Hiyo John Mngodo,warsha hito iliandaliwa iliandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.


  0 0


  0 0

  Hiki ni kipindi kitakachozungumzia baadhi ya mambo ambayo yametawala kwenye mitandao ya kijamii.
  Kitawajia punde
  USIKOSE kukifuatilia

  0 0


  0 0


  0 0

  Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mororogoro leo imetengua adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka na badala yake atatumikia kifungo cha nje na kulipa fidia ya Shilingi milioni moja.

  Cheka alikuwa akikabiliwa na kosa la kumpiga na kumjeruhi Bahati Kibanda, ambaye alikuwa ni meneja wa baa yake iitwayo Vijana Social Hall iliopo mjini Morogoro.

  Cheka anatumikia kifungo chake cha nje kwa kufanya kazi za serikali kwa muda wa masaa manne kila siku kwa kipindi chote cha kifungo hicho.
  Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka akipatiwa maelekezo kutoka kwa askari.Picha na Maktaba.

  0 0

  Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress akisisitiza jambo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya uongozi bora kwa vijana yaliyoanzishwa na Rais wa Marekani, Barrack Obama kupitia taasisi ya Mandela Fellowship, Ohio University na Institute for International Journalism.
  Mkurugenzi wa mafunzo ya Yali Connect Camp, Dk. Yusuf Kalyango akizungumza na wahitimu 18 wa mafunzo hayo.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Joshua Nassary akipozi katika picha na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress mara baada ya kukabidhiwa cheti cha uhitimu.
  Vijana kutoka mataifa manne wakimsikiliza Balozi wa Marekani nchini Tanzania (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi bora kwa viongozi vijana wa baadaye yaiyomalizika hivi karibuni jijini.


  0 0

  MJUMBE wa kamati ya utendaji ya Simba, Musleh Al Rawah amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijin Dar es salaam leo kwa shtaka la kumjeruhi mtoto wa mwenyekiti  wa Yanga, Yusuph Manji.

   Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Genis Tesha alidai kuwa Al  Rawah alifanya kosa hilo, Machi 8, 2015 kwenye Uwanja wa Taifa uliopo Chang'ombe .

  Tesha alidai kuwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa Al Rawah alimpiga teke Meheub Manji na katika sehemu nyingine mbalimbali za mwili ukiwamo uso na kumsababishia majeraha mazito.

  Al Rawah ambaye ni mfanyabiashara na mmoja wa viongozi ndani ya klabu ya Simba anayetetewa na Wakili Damas Ndumbalo, alilikana shtaka hilo na upande wa mashtaka ukadai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika,hata hivyo baada ya mshtakiwa kusomewa shtaka hilo, upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa hauna pingamizi na dhamana.

  Kwa upande wa Wakili Ndumbalo naye aliomba mteja wake apewe dhamana.

  Hakimu Frank Moshi akitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo, alimtaka awe na mdhamini  mmoja ambaye anatoka katika taasisi inayotambulika na serikalini.

  Baada ya mdhamini kujitokeza upande wa mashtaka ulizifanyia uhakiki barua hizo ndani ya saa moja kama ilivyoelekezwa na mahakama na mshtakiwa akaachiwa huru.  Kesi imeahirishwa hadi Aprili 20,2015 kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi umekamilika ama la.

older | 1 | .... | 771 | 772 | (Page 773) | 774 | 775 | .... | 3348 | newer