Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 770 | 771 | (Page 772) | 773 | 774 | .... | 3353 | newer

  0 0
 • 03/15/15--23:38: NesiWangu Show...Albinism
 • Karibu katika kipindi cha NesiWangu.
  Katika kipindi hiki, Harriet Shangarai amezungumza na wanaharakati wa masuala ya Albinism. Sehemu ya kwanza ni mazungumzo na Daisy Makwaia wa Albino Charity Organization na sehemu ya pili ni mazungumzo yao na mwanaharakati mwenye Albinism Babu Sikare wa Afrobino Ltd
  Karibu

  0 0

  0D6A5197
  Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan akikabidhi kiti maalum cha kujisaidia pamoja na kiti cha magurudumu kwa mama huyo mlemavu.Na modewji blog team


  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan (CCM) ametoa msaada wa kiti cha magurudumu kwa Rehema Nditi mkazi wa Magomeni Mwembe Chai kama msaada kutokana na taabu aliyokuwa akiipata.

  Idd Azzan ametoa msaada … ambapo baada ya kuona Rehema Nditi kupataa tabu ya kukosa kiti hicho.Mbunge huyo amekua akisaidia maendeleo mbalimbali ikiwemo shughuli za kijamii ndani ya jimbo lake hilo.

  Aidha, Mh. Iddi Azzan ametoa rai kwa Watanzania kuungana nae katika kuchangia pesa kwa ajili ya kununua Bajaji ambayo itafanya biashara ili waweze kuendesha maisha ya kila siku.
  “Watanzania tuungane kumchangia mama huyu kiasi chochote ilikununua bajaji kwa ajili ya kufanya biashara ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku kupitia kipato cha biashara hiyo ya Bajaji” alieleza Idd Azzan.

  Kwa upande wake, Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania, Kinachoerushwa na kituo cha Channel Ten, Hoyce Temu amefungua michango hiyo kwa kutoa kiasi cha Tsh. 500,000/- ili kuhamasisha na wengine kuchangia.

  Michango hiyo inaweza kuwasilishwa kwenye ofisi za Mbunge wa jimbo la Kinondoni ama unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Rehema Nditi kupitia namba TIGO PESA +255 719-543075 AU M-PESA +255 754 097 527
  0D6A5129

  0 0


  0 0

  Balozi Juma Volter Mwapachu
  KAMPUNI tanzu ya Bharti Airtel inayoongoza katika utoaji wa huduma za simu za mkononi ikifanyakazi katika nchi 20 Asia na Afrika, leo imemteua Balozi Juma Volter Mwapachu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel Tanzania.

  Balozi Mwapachu ni Katibu Mkuu aliyepita wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, nafasi aliyoishika kati ya Aprili 2006 na Aprili 2011. Kabla ya uteuzi huu, Mwapachu alikuwa Balozi Mwakilishi Ufaransa na UNESCO.

  Mwapachu ni mhitimu wa shahada ya sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Pia ni mhitimu wa Diploma ya Juu ya Sheria ya Kimataifa, Masuala ya Diplomasia ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Sheria za Kimataifa na Diplomasia huko New Delhi, India.

  Pia ana shahada mbili za heshima katika fasihi na sayansi ya siasa za UDSM na Chuo Kikuu cha Taifa Rwanda.

  Akizungumzia uteuzi huo, Christian de Faria, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa, alisema: “Ni faraja kwetu Balozi Mwapachu kuiongoza Bodi yetu ya Wakurugenzi nchini Tanzania. Uzoefu wake mkubwa utaongeza thamani kubwa kwa Bodi yetu na kutoa miongozo bora ya kimkakati katika shughuli zetu nchini Tanzania. Tunaamini pia kuwa atadumisha mahusiano na wadau mbalimbali nchini.”

  Kwa upande wake, Balozi Mwapachu alisema: “Ninaipokea kwa heshima kubwa fursa hii ya kujiunga na Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel, na kwa pamoja na wajumbe wenzangu wa Bodi hii ya wakurugenzi wa Airtel, tutashirikiana kujenga kampuni thabiti yenye misingi imara ili kuendelea kutoa huduma bora ya mawasiliano nchini Tanzania.

  “Sekta ya mawasiliano ina mchango mkubwa katika kukua kwa uchumi wetu ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wananchi kila mahali. Pia ukuaji wa teknolojia ya hali ya juu na ubunifu katika masoko ikisaidiwa na mfumo mzuri wa usimamizi wa sekta hii ni dhahiri kutakuwa na uwezekano kwa sekta hii ya mawasiliano kuendelea kutoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya taifa.”

  Balozi Mwapachu ana uzoefu mkubwa katika masuala ya kuongoza bodi mbalimbali kwani amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) na Shirika la Reli Tanzania (TRC). Pia alikuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya East African Breweries Limited, Kenya.

  Kwa sasa yumo katika bodi kadhaa za taaasisi binafsi ndani na nje ya nchi. Ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Uzoefu wake wa kiuongozi katika mashirika na sekta binafsi Tanzania na eneo la Afrika Mashariki utaleta tija katika uongozi wake wa Airtel Tanzania.

  0 0

  1
  Mwasibu wa Kampuni ya Nivanaa Quality service and catering, Bi.Magreth Tairo akizungumza wakati wa kuzindua kampuni hiyo,kwenye kiota cha  City Louge jijini Dar es salaam.Kampuni hiyo inajishugusha na upikaji wa vyakula katika sherehe mbalimbali yenye makao yake makuu Kinondoni Manyanya Dar es Salaam.
  2
  Wadau walioudhuria katika hafla hiyo wakifuatilia uzinduzi huo.
  3
  Timu nzima ya waanzilishi na wamiliki wa Kampuni ya Nivanaa Quality service and catering wakiwa kwenye picha ya pamoja.


  0 0

  Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) wanaoishi kwenye Hostel za Mabibo,wakiangalia moja ya majengo ya Hostel hizo likiwa limeshika moto asubuhi hii.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na msaada wa haraka unahitajia ili kuokoa mali zilizopo kwenye Jengo hilo.
  Hakuna anaeamini anachokiona,kwani imekuwa ni tukio la ghafla sana.
  Baadhi ya Wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye Jengo hilo wakiwa nje,huku wakiwa hawajui la kufanya wakati moto huo ukiendelea kuwaka.
  Moshi unazidi kufuka na moto unaongezeka.

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) katikati akiingia katika viwanja vya Salender Bridge Club wmara baada ya kumalizika kwa matembezi ya amani yaliyolenga kuhamasisha umma kuhusu kujali afya zao jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno. Kulia ni Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro.
  Baadhi ya wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania na wananchi wakishiriki matembezi ya amani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini Dar es Salaam. 


  0 0

   Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe wa pili   kushoto na viongozi wa Halmashauri  wakikabidhiana daraja la mto Kitewaka kwa  ajili ya  kujengwa kisasa baada ya  serikali  kukabidhi fedha za ujenzi huo Tsh miloni 240
   Mbunge  Filikunjombe akilitazama daraja la mbao la mto Kitewaka ambalo litajengwa  kisasa. 
   Viongozi wa kanisa la Anglikana na wa CCM Ludewa  wakiongozana na mbunge Filikunjombe  mwenye kofia.


  0 0

  Waziri mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya vyakula vya Kitanzania vilivyosindikwa kitalaamu, Afisa Mtendaji Mkuu na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Sumitomo ya Japan,Bw.Michihiko Kanegae baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo, Machi 16, 2015. Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam hivi karibuni. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Masuala ya Miundombinu ya Umeme wa kampuni hiyo, Tsutomu Ben Akimoto.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake wakiagana na Afisa Mtendaji Mkuu na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Sumitomo Corporation Corporation ya Japan,Bw.Michihiko Kanegae (wapili kushoto) baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo, Machi 16, 2015. Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyrezi jijini Dar es salaam hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan aliyemaliza kuda wake, Salome Sijaona, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Batilda Burian.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata Maelezo kutoka kwa Ofisa wa Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, Noriko Tanaka kuhusu Treni inayofanyakazi bila dereva katika jiji la Tokyo wakatia lipotembelea Ofisi za Kampuni inayoendesha treni za aina hiyo ili kujifunza namna ya kusafirisha abiria kwa njia ya reli katika majiji Machi 16, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Mbunge na Naibu Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Bw.Shigeki Iwai kuhusu kipeperushi chenye picha zinazoonyesha kilimo cha chai kuzunguka mlima Fuji nchini Japan katika mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo Machi 16, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  Watanzania wametakiwa kuisoma katiba inayopendekezwa kwa umakini ili kuweza kufanya maamuzi sahihi katika kuandika historia mpya ya nchi.

  Hayo aliyasema leo Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Asha-Rose Migiro wakati akikabidhi katiba inayopendekezwa kwa makundi mbalimbali,Migiro  amesema nchi itaandika historia mpya baada ya kupata katiba mpya.

  Alisema wananchi wakisoma katiba kwa umakini kutasaidia kufikia matarajio katika kutengeneza ramani ya nchi kwa kuvuka miaka 50 ya katiba mpya.

  Migiro amesema kuwa wamechapisha katiba inayopendekezwa kwa watu wenye ulemavu wa kuona kwa alama ya nukta nundu na baada ya kupita kwa katiba watapewa kwani ni haki yao kuwa nayo.

  “Kujitokeza kwenu ni ishara ya kuunga mkono kwa katiba inayopendekezwa hivyo ni wajibu wenu kutoa elimu ili waweze kufanya maamuzi wakati wa kupiga kura ya maoni”amesema Dk.Asha-Rose.

  Aidha wamechapisha nakala hizo kwa herufi kubwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)ili nao waweze kusoma na kuelewa na kuweza kufanya maamuzi.

  Migiro amesema wamechapisha nakala na kugawa kwa nchi nzima ambapo kila kata inapata nakala 300 na Zanzibar zinagaiwa chini ya ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.

  Baadhi ya wadau waliopokea nakala hizo wamesema watafikisha,lakini hawawezi kuwaamulia katika maamuzi yao
  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba Inayopendekezwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015). Dkt. Turuka alipokea kwa niaba ya Makatibu Wakuu wenzake.
  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba Inayopendekezwa mwakilishi wa Baraza Kuu la Taasisi na Jumuiya za Kiislam Sheikh Mussa Kundecha katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).


  0 0
 • 03/16/15--07:54: Article 11
 • Women representatives from provinces of Gitega, Karuzi, Muramvya, Kayanza and Mwaro in a group photo with members of the panels of eminent persons from the EAC and COMESA region.
  HE Dr. Speciosa Wandira-Kazibwe, Former Vice President of the Republic of Uganda, current member of the African Union (AU) Panel of the Wise and Eminent Person (left) emphasising on a key issue from her presentation on the experiences, challenges and lesson learnt from women, leadership and conflict management. To her left is Mr. Adelin Hatungimana, Senior Programme Officer of ACCORD Burundi.

  As part of its objective to increase the participation of women in the electoral process in Burundi, the EAC Secretariat, together with joint efforts from the Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA), held plenary discussions to women groups in the town of Gitega, Burundi from 11th – 12th March, 2015.

  The participants were drawn from the provinces of Gitega, Karuzi, Muramvya, Kayanza and Mwaro, in the northern and central parts of the country.


  0 0

  Na Ripota Maalum,Tanga

  TIMU ya Coastal Union imewasilia jijini Tanga ikiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha inawanyamazisha wapinzani wao Azam FC ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara mchezo unaotarajiwa kucheza kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani wikiendi ijayo.
  Akizungumza leo na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa sasa nguvu zao watazielekeza kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye mjini hapa.
  Amesema kuwa dhamira yake aliyoipanga ni kuchukua pointi tatu muhimu dhidi ya Ruvu Shooting haikuweza kutimia na kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 hivyo atahakikisha inatimia kwenye mechi hiyo.

  Amesema timu hiyo imerudi salama mkoani hapa na tayari wameshaanza kujipanga imara kuhakikisha mechi hiyo timu inapata ushindi n kutokana na uimara wa kikosi chao
  Aidha amesema kuwa wachezaji wa kikosi hicho wameimarika zaidi na wapo imara kuweza kupambana kufa na kupona ili kuchukua pointi tatu muhimuzo zitawasogeza kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo.

  Hata hiyo amewataka wapenzi na mashabiki wa soka mkoani hapa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuipa hamasa timu hiyo kuweza kutimiza ndoto zake.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Charles Kitwanga, akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kuimarisha ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini unaofanyika jijini Mwanza
  Baadhi wa washiriki wa mkutano wa kuimarisha ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga anayeshughulikia Nishati (hayupo pichani).
  Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Migodi Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha taarifa wakati wa mkutano wa kuimarisha ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini unaofanyika jijini Mwanza.


  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Vijana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo anayesimamia Kitengo cha Uratibu na Uwezeshaji Dr. Steveni Kissui (aliyesimama) akifungua mafunzo ya jinsi ya kujikwamua na umasikini kwa Vijana wa Manispaa ya Singida,Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa.
  Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa aliyesimama akivifundisha vikundi mbalimbali vya vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida mjini namna ya kuandika miradi ya maendeleo,mafunzo hayo yamefanyika Wilayani humo ikiwa ni juhudi za Serikali kuwakwamua vijana katika matatizo yanayowakabili.


  0 0

  Mhe. Bernard Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Julius James Shirima, mshindi wa Tuzo ya Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola upande wa Afrika. Kwenye mazungumzo mafupi, Mhe. Membe alimpongeza Shirima kwa tuzo hizo na aliahidi kumpa ushirikiano kupitia Wizara anayoiongoza ili vijana wengi wa Kitanzania wanufaike na mchango wa Shirima na pia waige mfano wake na kuendelea kupeperusha vema bendera ya Tanzania.
  Julius Shirima, mshindi wa Tuzo za Vijana wa nchi za Jumuiya ya Madola akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Bernard Membe, ambaye alifanya naye mazungumzo mara baada ya kumaliza kuendesha kikao cha Mawaziri wa Kikosi Kazi cha Jumuiya ya Madola mjini London hivi karibuni. Wengine kwenye picha ni Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Bernard Membe, Julius Shirima, Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Balozi Celestine Mushy Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa.


  0 0
 • 03/16/15--08:50: Kutana na Linah uishi Kistaa
 • 0 0


  0 0

  Waziri nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI,Mh. Hawa Ghasia akizungumza mapema leo katika siku ya kwanza ya mafunzo ya Wakuu wa Wilaya wapya ishirini na saba yanayoendelea katika ukumbi wa hoteli ya St. Gaspar mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri, Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne A. Sagini na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Elimu) Bw. Zuberi Samataba.
  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne A. Sagini akitoa mada kuhusu kazi na majukumu ya Wakuu wa Wilaya katika semina hiyo iliyoanza leo tarehe 16 hadi 19 Machi 2015.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja, ambaye pia ndiye mwezeshaji mkuu wa mafunzo hayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Dodoma. UONGOZI Institute ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Rais inayoshughulikia mafunzo kwa viongozi waandamizi serikalini pamoja na kufanya utafiti na ushauri wa sera kwa serikali.


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha wajumbe saba wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam .Wajumbe wa tume hiyo walioapishwa leo ni pamoja na Mwenyekiti wake Bwana Edrissa Mavura,Paul Herbert Kinemela(Kamishna), Bwana Mathias Bazi Kabundunguru(Kamishna),Bwana Njaa Ramadhani(Kamishna)Bwana Jones Kyaruzi Majura(Kamishna), Bwana Jaffari Ally Omari(Kamishna) na Bibi Suzane Charles Ndomba.Pichani ni wajumbe wa tume hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wanne kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Edrissa Mavura.(Picha na Freddy Maro).

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akiwa na ujumbe wa Kampuni ya Surbana International Pty Ltd ya nchini Singapore ofisini kwake. Kampuni hiyo imeingia mkataba na Tanzania katika uandaaji wa mpango kabambe (Master plan) wa Jiji la Arusha.
  Katibu mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akifafanua jambo katika kikao kifupi ofisini kwake, baina ya Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willium Lukuvi, National Housing Coorporation na ujumbe wa Kampuni ya Surbana International Pty Ltd ya nchini Singapore.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akipokea zawadi ya picha, ambayo alipigwa alipokuwa ziarani Singapore, anayemkabidhi ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Surbana International Pty Ltd,Pang Yee.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Angela Kairuki akipokea zawadi ya picha ambayo alipigwa alipokuwa ziarani Singapore, anayemkabidhi ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Surbana International Pty Ltd,Pang Yee.

older | 1 | .... | 770 | 771 | (Page 772) | 773 | 774 | .... | 3353 | newer