Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 769 | 770 | (Page 771) | 772 | 773 | .... | 3286 | newer

  0 0  0 0

  Mbunge  Filikunjombe  akisisitiza  jambo  wakati  akitoa  salamu  zake kwenye  mazishi ya SR. Instrude maria
  Katibu mwenezi wa CCM mkoa  wa  Njombe Bw Honolatus Mgaya kushoto  na  mbunge wa Ludewa  Deo Filikunjombe  kulia  wakishirikiana na wananchi  wa  Njombe  kubeba jeneza na SR. Maria. 
   Mbunge  Filikunjombe katika usikivu mkubwa

   Na Matukiodaima BLoG

  Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewaomba viongozi wa dini nchini kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali wakiwemo wabunge ili kuwatumikia wananchi kwa kutanguliza hofu ya Mungu  ya  kwatumikia  wananchi waliowachagua

  Kauli hiyo aliitoa Jana wakati wa mazishi ya aliyekuwa mtawa wa kanisa la Romanikatoliki Parokia ya Imiliwaa Marehemu SR. Insetrud Maria

  Alisema kuwa viongozi wa dini wamekuwa wakifanya kazi ya kuliombea Taifa na watu wake ila wanasiasa na viongozi wa serikali wamekuwa wakiwatumikia wananchi kimwili hivyo kuna haja ya viongozi wa dini kuendelea kufanya kazi ya kuwaombea viongozi .


  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0
 • 03/15/15--01:58: Article 16
 • Vijana wa Yamoto Band waikonga mioyo ya mashabiki wao wa Tabata kwa kupiga show kali sana ndani ya Dar West ikiwa ni wiki moja tu imepita tangu warejee kutoka UK Londoni ambako walikuwa na Ziara.
  Kayumba ni Zao kutoka Mkubwa na Wanawe akifungua show kwa kuimba kabla ya Vijana wa Yamoto Band.
  Mwanadada Marope kutoka Mkubwa na wanawe akitoa Burudani katika Ukumbi wa Dar west Tabata jana.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  JE UNA MALALAMIKO JUU YA BILI YAKO YA MAJI YA KILA MWEZI, UNA DENI SUGU LA DAWASCO, UNA TAARIFA ZA WATU WANAOHUJUMU MIUNDO MBINU YA MAJI, UNAHITAJI KUUNGANISHIWA HUDUMA YA MAJI NYUMBANI KWAKO SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO) LINAKUKARIBISHA MTEJA, MWANANCHI, TAASISI NA MASHIRIKA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI YANAYOANZA RASMI TAREHE 16 HADI 22 MACHI 2015 NCHINI KOTE YENYE KAULI MBIU YA “MAJI KWA MAENDELEO ENDELEVU”

  KATIKA KUADHIMISHA WIKI YA MAJI DAWASCO KAMA MTOA HUDUMA MKUU WA HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJITAKA JIJINI DAR ES SALAAM IMEANDAA DAWATI MAALUM KWA WATEJA WAKE NA WANANCHI KWA UJUMLA KATIKA SEHEMU KUU TATU: DAWASCO KINONDONI (ILIYOPO NYUMA YA JENGO LA AIRTEL), DAWASCO MAKAO MAKUU (BARABARA YA SOKOINE DRIVE), NA DAWASCO BOKO.

  MADAWATI HAYA YATATUMIKA KUJIBU MASWALI NA KUTOA UFUMBUZI WA MATATIZO YA WANANCHI WANAOHUDUMIWA NA DAWASCO, KUTOA ELIMU JUU YA HUDUMA ZA MAJI ZITOLEWAZO NA DAWASCO, KUONGEZA UELEWA JUU YA SERA YA MAJI, KANUNI, MIONGOZO, ULINZI WA MIUNDOMBINU YA MAJI NA MATUMIZI SAHIHI YA DIRA ZA MAJI n.k

   MADAWATI HAYA YATAKUWA WAZI WIKI NZIMA KUANZIA TAREHE 16 HADI 22 MACHI KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI HADI SAA 12:00 JIONI KILA SIKU.

  KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU HUDUMA KWA WATEJA 022 5500240-4 NA 0658-198889
  IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
  DAWASCO-MAKAO MAKUU

  0 0

  Mfanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha mauzo, Erica Mwaipasi (kulia) akizungumza na baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku tatu wa Chama cha Watumiaji wa Elimu ya Kompyuta katika Sayansi inayohusu Utafiti wa Uhai na Viumbe hai Afrika (ASBCB) uliofanyika jijini Dar es Salaam. NBC ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine ulijadili jinsi elimu hiyo inavyoweza kusaidia ufumbuzi wa tiba ya magonjwa mbalimbali ya binadamu.
  Maofisa wa Benki ya NBC Kitengo cha Mauzo, Erica Mwaipasi (kulia) na Prosper Massano (katikati) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vision Investments, Ally Nchahaga katika mkutano wa siku tatu wa Chama cha Watumiaji wa Elimu ya Kompyuta katika Sayansi inayohusu Utafiti wa Uhai na Viumbe hai Afrika (ASBCB) uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi. NBC ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine ulijadili jinsi elimu hiyo inavyoweza kusaidia ufumbuzi wa tiba ya magonjwa mbalimbali ya binadamu.


  0 0

  Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusiana na ujio wa mwimbaji nyota kutoka Afrika Kusini Thori Mahlangu (Obrigado). (Picha Francis Dande)
   Msama akifafanua jambo.
   
  Na Loveness Mboje

  RAIA  wa Afrika Kusini ambaye ni Mwanamziki wa nyimbo za injili, Thori Mahlangu (Obrigado), amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji wa kimataifa watakaotumbuiza katika Tamasha Pasaka litakalofanyika Aprili 5.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema kuwa sambamba na mwimbaji huyo ataambatana na waimbaji wengine 16 kutoka nchini humo huku Faustine Munishi maarufu kwa jina la Malebo na Solomon Mukubwa  kutoka nchini Kenya nao watakuwepo.

  Msama alisema kuwa viingilio vya tamasha hilo kwa watoto vitakuwa shs. 2,000 viti vya kawaida shs.5,000 VIP B, shs. 10000 VIP A shs. 20,000 kwa watu wakubwa na kuongeza kuwa mara baada ya tamasha hilo, Aprili 12 itakuwa ni zamu ya wakazi wa jiji la Mwanza katika Uwanja wa  CCM Kirumba.

  Aidha kwa upande wa waimbaji wazawa  Msama amesema kuwa mwimbaji Joshua Mlelwa ambaye alikuwa mwimbaji wa Upendo Group  naye atapamba tamasha hilo ambalo linasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki.

  Tamasha hilo linatimiza miaka 15 tangu lianzishe
  na linatarajiwa kihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka nchi za Kenya, Uganda,Rwanda, Afrika Kusini Uingereza na wenyeji Tanzania.

  0 0

  The Entrepreneurs Organisation (EO) Tanzania Founding Team with Chapter President, Nicholas Thiede, EO East Africa President Sriram Bharatam (centre) and incoming Global Chairman Gilberto Crombe signals the launch of EO’s newest chapter in Tanzania. EO is a global business network of over 11,000 business owners in 144 countries.

  2015 – The Entrepreneurs' Organization (EO), a global business network of over 11,000 business owners in 144 chapters across 46 countries, launched its newest chapter in Dar-es-Salaam, Tanzania today.

  Founded in 1987 by a group of entrepreneurs, EO enables business owners to learn from one another, leading to greater business success and an enriched personal life. EO’s vision is to build the world's most influential entrepreneur community.

  As a global business owner network & association, EO helps to transform the lives of the entrepreneurs who transform the world. EO educates, transforms, and inspires by providing invaluable resources in the form of events, leadership-development programs, and business owner education opportunities designed for business growth.

  Over 100 members and guests, including EO members from across East Africa, leading Tanzanian entrepreneurs, thought leaders and VIPs, joined incoming EO Global Chairman, Mr. Gilberto Crombé, to launch the first Tanzanian chapter at the Hyatt Regency Hotel, Dar-es-Salaam.

  Mr. Crombé said “The launching of our newest chapter in Dar-es-Salaam is the perfect highlight to a pan African Tour which took an in-depth, strategic look at the entrepreneurship ecosystems across Lagos/Nigeria, Nairobi/ Kenya & Dar-es-Salaam/Tanzania. Leading business owners the world over value support from a peer-to-peer community like EO, which inherently becomes attributed to both their personal and professional successes.” The keynote address, “Boosting Entrepreneurship in Tanzania,” was given by Patrick Ngowi, Founder & CEO of Helvetic Group and winner of KPMG’s Top 100 Mid-Sized Companies 2013, as well as being on Forbes’ 30 Most Promising Young Entrepreneurs in Africa 2014.

  Nicholas Thiede, a long-standing EO member and founding President of the Dar-es-Salaam chapter said, “Dar- es-Salaam is home to many of the country’s leading businesses led by highly dynamic entrepreneurs. As a formal network of business owners, EO will enable peer-to-peer exchanges and learning experiences that transcend boundaries such as business sector, business life cycle or geography. Our member companies range from the well established to start-ups, and while the minimum criteria is $1m in turnover per year, most of our member companies are significantly larger.”

  0 0

  Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Jijini Arusha, Boniventure Mshongi (kushoto) akimkabidhi kikombe Mchoma nyama wa Bar ya Milestone Park, Lawrence Kimonge mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma yaliyofanyika katika Uwanja wa Nanenane mwishoni mwa wiki jijini Arusha .Katikati ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa.
  Mashabiki wa Bar ya Milestone Park ya jijini Arusha wakiwa wamembeba juu mchoma nyama wa bar hiyo mara baada ya kutangazwa bingwa katika mashindano ya Safari Lager Nyama Choma mkoani humo yaliyofanyika katika Uwanja wa Nane nane mwishoni mwa wiki

  Na Mwandishi Wetu.Arusha.

  MILESTONE PARK Bar jijini Ausha wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki katika Nanenane na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.


  0 0

  Wafanyakazi wa Benki ya UBA (United Bank for Africa), wakishindana kuvuta kamba wakati wa mazoezi waliofanya jijini Dar es Salaam jana kutokana na utalatibu waliojiwekea kwakila baada ya miezi mitatu hufanya mazoezi pamoja na wateja wao.
  Mwalimu wa mazoezi ya viungo kutoka Chama cha walimu wa mazoezi hayo, FIAT, Ray Mwamakula (kushoto) akiwaongoza wafanyakazi wa Benki ya UBA (United Bank for Africa), kufanya mazoezi Dar es Salaam jana.
  Mwalimu wa mazoezi ya viungo kutoka Chama cha walimu wa mazoezi hayo, FIAT, Ray Mwamakula (kushoto) akiwaongoza wafanyakazi wa Benki ya UBA (United Bank for Africa), kufanya mazoezi Dar es Salaam jana.

  0 0


  0 0


  Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.
  Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.

  Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam.
  Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam.

  Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.
  Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.

  Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu.
  Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu.

  Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege.
  Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. 

  KAMPENI maalumu za kupinga mauaji ya watu wenye u-albino nchini inayojulikana kama 'Imetosha' iliyoanzishwa na balozi wa kujitolea, Henry Mdimu, chini ya Imetosha Foundation zimezidi kushika kasi baada ya makampuni ya IPTL na PAP kutoa shilingi milioni 10 kusaidia kampeni hizo.

  Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege jana alimkabidhi balozi Mdimu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kama ishara ya kuunga mkono kampeni hizo za kutoa elimu kutokomeza imani potofu zilizojengeka kwa baadhi ya wanajamii juu ya watu wenye albino.

  Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Makandege alisema matukio ya mauaji au kukatwa viungo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino yamefika hatua ya kutisha nchini Tanzania, hususani katika kanda ya ziwa hivyo kuna kila sababu kila mmoja bila ubaguzi kushiriki kusaidia mapambano hayo.
  Alisema ulemavu wa ngozi waliyonao watu wenye albino ni mapungufu ya kibaiolojia ambayo ni mapenzi ya Mungu hivyo imani potofu zinazoendelea hazina budi kupigwa vita kwa nguvu zote.
  Aidha kampuni za IPTL na PAP zimeyataka makampuni mengine nchini na watu binafsi kuungana kwa kuchangia harakati hizi za imetosha ili kusaidia kampeni ya imetosha kupita mikoa ya kanda ya ziwa kupaza sauti na kuielimisha jamii juu ya uwepo wa imani potofu zinazoendeleza mauaji ya watu wenye u-albino.
  Kwa upande wake Balozi wa Imetosha, Mdimu aliishukuru kampuni za IPTL na PAP kwa moyo wauliouonesha wa kusaidia harakati hizo na kumtaka kila Mtanzania kwa nafasi yake kusaidia kupaza sauti kwamba imetosha mauaji na unyanyasaji wanaoupata watu wenye ualbino. Alisema mauaji haya yanamgusa kila Mtanzania na kuendelea kuichafua nchi yetu hivyo kumtaka kila mmoja kupaza sauti yake kupinga vitendo hivyo.
  Machi 28, 2015 Imetosha Foundation inatarajia kufanya matembezi ya hisani kuchangisha fedha zaidi ili kusaidia kampeni za kukomesha mauaji ya watu wenye u-albino kabla ya kuanza rasmi safari za kuzunguka katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na wasanii waliojitolea kueneza elimu hiyo kwa jamii moja kwa moja.  0 0

   Vijana wa Kigoma wakiwa na bango wakimsubiri Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" alipokwenda jimboni huko kutoa Ahsante kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
   Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" alipokwenda jimboni huko kutoa Ahsante kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
   Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akitoa  Ahsante kwa wananchi wa jimboni kwake kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
    Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akiwa amebebwa na  wananchi wa jimboni kwake alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
    Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akicheza ngoma na  wananchi wa jimboni kwake alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
    Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akihutubia  wananchi wa jimboni kwake alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili
    Mhe. Zitto Kabwe "Mirumbani" akikabidhi gari la wagonjwa katika kituo cha Afya cha kijiji cha Nyarubanda  jimboni kwake alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwa vipindi viwili.
  Kusoma hotuba ya Mhe Zitto Kabwe leo BOFYA HAPA

  0 0

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Makao makuu ya ofisi hizo  Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne  Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali  kama zinavyopatikana kwenye  tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji  watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga  na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbali mbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.Kulia ni Katibu msaidizi wa Baraza hilo Ramadhani Samainda.
  .Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Primus Nkwela (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari pichani katika Makao makuu ya ofisi hizo  zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, wakati akiutangazia Umma juu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne  Oktoba 2014. na wengine wenye sifa mbalimbali  kama zinavyopatikana kwenye  tovuti ya baraza hilo:www.necte.go.tz.Waombaji  watakao omba kabla ya tarehe 10 Aprili 2015 wataruhusiwa kujiunga  na mafunzo mnamo Aprili 15 2015 kwenye vyuo mbalimbali kama vinavyopatikana kwenye tovuti yao.

  0 0


  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale ametangaza kuanza rasmi kwa majaribio ya kupima magari kwenye Mzani wa Kisasa wa Vigwaza mkoani Pwani ambapo majaribio hayo yataendelea hadi siku ya tarehe 17/03/2015. 
  Kwa mujibu wa Eng. Mfugale, mara baada ya majaribio kukamilika siku hiyo kituo cha Mzani wa Kibaha katafungwa rasmi na magari yataendelea kupimwa kwenye kituo kipya cha Vigwaza ambacho kina uwezo wa kupima gari moja likiwa linatembea kwa muda usiozidi sekunde 30 tofauti na mzani wa zamani uliokuwa unatumia dakika moja na nusu. 
  Eng. Mfugale amewataka madereva kufata taratibu zifuatazo katika Mzani huo mpya utakaokuwa unapima magari yakiwa kwenye mwendo yani weigh-in-motion i) Magari yanayotakiwa kupimwa kwa mujibu wa sheria ni yote yanayoanzia tani tatu na nusu.(3.5) Magari yanatakiwa yaendeshwe kwa kupita upande unaostahili kisheria yaani hayatakiwi kukanyaga mstari mweupe katika barabara.
  Eng. Mfugale aliongeza kuwa usipofata utaratibu huu katika Mzani taa nyekundu mbele ya itawaka na dereva kuelekezwa kwenye mzani mkubwa hata kama hujazidisha uzito na utatakiwa kulipa tozo la dola za Kimarekani 2000 kuashiria kwamba dereva anakwepa mzani. 
  Eng. Mfugale alisema kuwa adhabu hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya Usalama Barabarani namba 30 ya mwaka 1973 na kanuni zake za mwaka 2001 kifungu namba 6(b) ii) Madereva wanatakiwa wazingatie mwendo wa kilomita 50 kwa saa iii) Madereva wahakikishe kuwa matairi ya magari yao yanapita juu ya plates za weigh-in motion na kuachana mita 30 yanapokaribia kupita eneo la Mzani ili kuondoa usumbufu wakati wa upimaji 
   Pia Eng. Mfugale ametoa angalizo kuwa gari lolote litakalozuia magari mengine kwenye barabara ya maingilio ya Mzani au kwenye mzani wakati wa upimaji kutokana na ubovu wa magari hayo yatatozwa faini kiasi cha Tsh. 300,000/= au kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja na hiyo ni kwa mujibu wa kifungu 50(1) (f)(g)(h)(i) cha Sheria ya barabara namba 13 ya mwaka 2007. 
  Mwisho Eng. Mfugale amewashauri wamiliki wa magari kuhakikisha kuwa madereva wao wanakuwa na wasaidizi watakaowasaidia kupeleka nyaraka za gari na mzigo ili kurekodiwa kwenye ofisi za mzani. 
  Mzani wa Vigwaza ni wa kwanza kujengwa nchini na una uwezo wa kuchambua na kubaini magari Weigh-in- Motion yaliyozidisha uzito huku yakiwa yanatembea. 
   Pia kituo hicho cha Vigwaza kina Mzani mkubwa multi deck wenye uwezo wa kupima gari lolote kwa mkupuo. Pia barabara za kuingia kwenye mzani mkubwa zenye urefu wa km 1.8 zimejengwa kwa zege lenye uwezo wa kudumu kwa miaka 50. Picha na Stori kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini GCU-Wizara ya Ujenzi
   Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akiwaonyesha Waandishi wa Habari namna ya upimaji wa magari katika Mzani mpya wa Vigwaza ambao umeanza kufanya kazi kwa majaribio.
  Magari yakiwa yameanza kupima kwenye Mzani mpya na wakisasa wa Vigwaza. Mzani huu unapima gari moja kwa muda wa sekunde 30 tofauti na Mzani wa zamani wa Kibaha uliokuwa unatumia dakika moja na nusu.

  0 0

  Timu ya Yanga leo imeichapa Bad 5-1 timu ya Fc Platinum ya nchini Zimbabwe katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la shirikisho,katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
   Picha na habari zaidi zitawajia punde.

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Swissport Tanzania Bw. Gaudence Temu (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya utendaji wa kampuni yake mara baada ya mkutano mkuu wa kampuni hiyo kumalizika uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Pamoja nae kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Swissport, Bw. Juan Jose Andres Alvez na Bw, Jeroen L. de Clercq ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo nchini Kenya. 

  KAMPUNI ya Swissport Tanzania Plc imepata ongezeko la faida kwa asilimia 73 (baada ya makato ya kodi na gharama nyingine zote), mafanikio yaliyotokana na maendeleo makubwa ya Sekta ya Usafiri wa Anga hapa nchini.

  Kampuni hiyo  inayotoa huduma zake kwenye viwanja vya ndege vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro  pamoja na ule wa Mtwara, ilitangaza mafanikio hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake mkuu  wa thelathini.

  Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Bw Juan Alvez alitaja sababu za mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa mashirika ya ndege yanayofanya safari zake katika viwanja vya ndege vya Tanzania na ongezeko la wingi wa safari kwa mashirika yaliyopo.

  “Ongezeko hili la asilimia 73 ni matokeo ya ongezeko la faida kutoka sh. bilioni 7.496 mwaka 2013 hadi kufikia sh. Bilioni 12.937 iliyoripotiwa  mwaka 2014,’’ alisema.

  Akifafanua zaidi Bw Alves alisema jumla ya abiria 1,111,156 walihudumiwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 23 ikilinganishwa na idadi ya abiria 905,347 waliohudumiwa katika kipindi cha mwaka 2013.

  Kufuatia mafanikio hayo ambayo pia yameonekana kwenye idara nyingine ikwemo ya ubebaji wa mizigo, Bw Alves alisema wana hisa wa kampuni hiyo  wana kila sababu ya kutabasamu kwa kuwa watapokea Sh287.50 ya gawio kwa kila hisa ikilinganishwa na sh 166.58 ya mwaka 2013 ili kuhakisi ongezeko hilo la asilimia 73.

  Akizungumzia uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo kwa 2014, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Gaudence Temu alisema kampuni hiyo ilifanikiwa kununua vifaa vya usaidizi ardhini (GSE) vyenye thamani ya sh. Bilioni 1.7huku akiongeza kuwa vifaa hivyo tayari vimeshafika na vimeanza kutumika.

  “Ongezeko lingine la sh. bilioni 2.7 katika uwekezaji  linatarajiwa kufanyika ndani ya mwaka huu na litahusisha mabasi mawili ya kubebea abiria katika viwanja vyetu sambamba na kifaa cha kupakia na kushusha mizigo mizito chenye uwezo wa hali ya juu,’’ alibainisha Bw. Temu.

  Kampuni hiyo inajumuisha pia wanahisa wa Kitanzania wapatao 11,500 ambao wanamiliki asilimia 49 ya hisa zote huku asilimia 51 zikiwa zinamilikiwa na kampuni ya Swissport International.


  0 0  0 0

  Katika mwendelezo wa kuwa karibu na wateja wake benki ya NMB imezindua mtandao utakaowaunganisha wateja wake wakubwa ‘Executive Network’ kwa jiji la mbeya ikiwa na lengo la kuwafanya kufurahia zaidi huduma za kibenki kutoka NMB. 
   Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya na kuwakutanisha wafanyabiashara zaidi ya 100 kutoka vitongoji mbali mbali ikiwemo Kyela, Mbozi,Tunduma, Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe waliopata fursa ya kuwa kwenye mtandao wa wafanya bishara wa NMB. 
   Mtandao huu unaounganisha wateja wakubwa wa NMB vile vile umezinduliwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo; Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya ikiwa ya nne.
  Afisa Mkuu wa Wateja  Wakubwa na Serikali wa NMB - Richard Makungwa(pili kulia) pamoja na Given Ngajilo wa kampuni ta Tunhimbaghe Traders Ltd (mteja).Wakifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB Executive Network jijini mbeya huku wakishuhudia ni Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa NMB - Filbert Mponzi (kulia) na menejaa wa NMB Nyanda za juu- Lucrecia Mkarie

  Maafisa wa NMB wakifurahi pamoja na mteja wao baada ya uzinduzi rassmi wa mtandao wa ‘NMB Executive Network’

  Sehemu ya wateja wakubwa wa NMB walioalikwa katika uzinduzi huo.
  Mmoja wa wateja wakubwa wa NMB akiomba ufafanuzi juu ya huduma zitolewazo na benki hiyo  wakati wa hafla iliyowakutanisha wateja wakubwa wa benki ya NMB.
  Meneja Maendeleo ya Biashara wa NMB, Masato Wasira(kushoto) na Mtaalam Mwandamizi wa bidhaa za hazina kwa wateja wakubwa ,Ronald Kato  wakiwa pamoja na wateja wa NMB kutoka kampuni ya Sunshine Mining ya Chunya.


older | 1 | .... | 769 | 770 | (Page 771) | 772 | 773 | .... | 3286 | newer