Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 764 | 765 | (Page 766) | 767 | 768 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Akina mama wa Kikundi cha Citizen cha Tabata jijini Dar es Salaam, jana kilitoa magodoro 50 na katoni 25 za maji na 25 za soda aina ya Cocacola ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Akina mama Duniani.

  Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Lilian Wasira alisema wameguswa sana na tatizo la akina mama kujifungulia sakafuni ndiyo maana wakaona watoe msaada huo.

  Lilian alisema, wameamua kufanya hivyo badala ya kusherehea siku hiyo kwenye kumbi za burudani huku wenzao wakijifungulia sakafuni.

  Mwenyekiti huyo alisema hawataishia Temeke tu bali wanatarajia kufanya harambee nchi nzima kuwahamasisha wadau mbalimbali kuhakikisha huduma ya afya inaboreshwa.
  Magodoro hayo yana thamani shilingi milioni 2,740,000
   Wakina mama wa Citizen Foundation wakiwa nje ya Hospitali ya Wilaya ya Temeke na walikokwenda kukabidhi magodoro.
   Mwenyekiti wa Citezen Foundation, Lilian Wasira akimkabidhi moja ya magodoro, Amosi Kabelege ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Hospitali ya Temeke.
   Mwenyekiti wa Citizen Foundation, Lilian Wasira akimkabidhi maji ya kunywa, Bi. Ashura aliyelazwa hospitalini hapo.
  Mganga mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Amani Malima alimshukuru Mwenyeti wa Citezen Foundation kwa masaada wa magodoro waliotoa hospitalini kwake jana.

  0 0

  The EAC Secretariat celebrated International Women’s Day as part of its strategy to increase the participation of women in the EAC’s regional integration process. 

  Under this year’s theme ‘Make it Happen,’ the Deputy Secretary General, together with the Arusha City Council, Women Organisations, Staff members of the EAC and other invited guests, took part in a ‘Walk for Gender Equality’ around designated areas in Arusha town, visited the Maternity Unit of Mt. Meru Regional Hospital, launched the EAC International Women’s website, and benefitted from various presentations and key note addresses on women’s rights and gender equality.

  “International Women’s Day is a time to reflect on the achievements that women in the EAC have attained in the last 20 years, as well as to identify the challenges that still impede their full potential,” said Hon. Jesca Eriyo, EAC’s Deputy Secretary General, Productive and Social Sectors.

  “We recognise that women make a significant contribution towards the process of economic transformation and sustainable growth, and that is why we want to emphasise the importance of their effective participation, empowerment and development in EAC’s integration process,” she said.  

  ‘Make it Happen’ stands as a global call for women and men to concretize Gender Equality, which is a follow up to the prepositions from the 20th Anniversary of the Fourth World Conference on Women held in Beijing in 1995.

  Gender equality can only be attained when women and men enjoy the same rights and opportunities across all sectors of society, including economic participation and decision-making, and when the different behaviours, aspirations and needs of women and men are equally valued and favoured.

  On average women are paid lower salaries than men for the same work. Women also continue to be victims of violence, with rape and domestic violence listed as significant causes of disability and death among women worldwide.

  As a way of fulfilling their commitment to an East African Community where women are able to participate as equal partners, decision makers, and beneficiaries of the sustainable development of their societies, the EAC has created a Sectoral Council on Gender to handle gender issues by proposing legal and policy frameworks accordingly.

  To this end, this would make meaningful and sustainable changes for women and girls.
  The Arusha City Council, Women Organisations, Staff members of the EAC and other invited guests partaking in a ‘Walk for Gender Equality’ around designated areas in Arusha town during EAC’s International Women’s Day celebrations.
  EAC’s Deputy Secretary General, Productive and Social Sectors, Hon. Jesca Eriyo (second right) and Mr. Bernd Malthup Head of EAC/GIZ Programme, Arusha (far left), donating hospital equipments to the Maternity Unit of Mt. Meru Regional Hospital in Arusha.
  EAC’s Deputy Secretary General, Productive and Social Sectors, Hon. Jesca Eriyo (first left) and Head of EAC/GIZ Programme, Arusha (second left), held a special tree planting event at the EAC Headquarters in Arusha to mark International Women’s Day.
  EAC’s Deputy Secretary General, Productive and Social Sectors, Hon. Jesca Eriyo (centre right) and Mr. Bernd Malthup Head of EAC/GIZ Programme, Arusha (centre left) sitting in for a group photo with designated guests and EAC Staff members who are attending EAC International Women’s Day celebrations.

  0 0

  Benki ya NMB ndio benki pekee yenye matawi katika kila wilaya hapa nchini.Hivyo basi ndio benki pekee inayowajali wateja wake kwa kua karibu zaidi wakati wote.NMB imekua ikiandaa semina elekezi kwa wateja wake .Sasa ilikua zamu ya wakulima na wadau wote wa kilimo cha kahawa wameweza kupata fursa ya kujua huduma mbali mbali zitolewazo na NMB kwa ajili ya wakulima na wadau wote wa hudiuma za kibenki Hivi karibuni NMB iliandaa semina kwa ajili ya wadau wa biashara za Kilimo ambayo imeendeshwa katika mikoa mbali mbali ikiwmo Tabora na Mbeya
  Wadau wa Kilimo cha Kahawa  Mkoa wa Mbeya wakifuatilia jambo wakati wa semina ya kilimo cha kahawa iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya wateja wake ambao ni wadau wa Kilimo Tanzania

  Wadau wa Kilimo cha Kahawa  mkoani Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na na Uongozi wa Benki ya  NMB Kanda ya Nyanda za juu  baada ya kumaliza semina ya kilimo cha kahawa iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya wateja wake ambao ni wadau wa Kilimo Tanzania
  0 0

  Na Bashir Yakub.

  Kuongezeka kwa makampuni na taasisi mbalimbali kumetengeneza wingi wa ajira maeneo mbambali ya nchi. Mbali na kuongezeka kwa ajira hizi kumekuwepo na tatizo kubwa la waajiriwa kutojua haki zao mbalimbali wawapo maeneo ya kazi.

  Niseme jambo moja tu kuwa hakuna suala la msingi kama muajiriwa kujua haki zake. Hii ni kwasababu kupitia kujua haki zake ndipo anapoweza kupata ujira stahiki, posho stahiki, masurufu stahiki, mafao stahiki, malipo stahiki ya kuachishwa kazi ikiwa ni pamoja na ujumla wa kufanya kazi kwa misingi ya kazi.

  Ni muhimu kila mfanyakazi kupitia pitia haki zake mara kwa mara ili kujua nini anapata na nini hapati. Uwe kazini au umeachishwa bado ipo nafasi ya kudai haki hizi ili upate kilicho chako.

  Ukitegemea mwajiri ndio akwambie haki zako utakuwa unajidanganya kwasababu yawezekana kabisa faida kubwa ya mwajiri ipo katika wewe kutokujua haki zako. Ni hasara kubwa kufanya kazi bila kujua haki zako . Kutokana na hilo leo nitaeleza baadhi ya haki za mfanyakazi.

  1. HAKI YA KUJUA SEHEMU YA KUFANYIA KAZI.

  Isiwe uliambiwa eneo la kazi ni Dar es salaam halafu ujikute kila siku una safari za mikoani halafu uambiwe eti hiyo ndiyo kazi yenyewe, hapana. Lazima eneo la kufanyia kazi lijulikane kwa mfanyakazi. Ijulikane kuwa umeajiriwa na eneo lako la kazi ni Dar es salam , au Mwanza au Kagera.

  Hii ina maana kubwa kwakuwa mfanyakazi asipojua eneo lake la kazi hataweza kudai malipo yatokanayo na kufanya kazi nje ya ofisi . Lakini iwapo unajua eneo lako la kazi basi utakapokuwa nje ya eneo la kazi yakupasa kudai malipo ya ziada. Kwa hiyo hakikisha mwajiri wako unakuainishia kwa uwazi kabisa eneo lako la kazi na ulijue. Nje ya hilo eneo ni malipo mengine ambayo ni nje ya mshahara wa kawaida.


  0 0

  Benki ya NMB imemkaribisha Mkurugenzi Mtendaji mpya – Ineke Bussemaker anayechukua nafasi ya Mark Wiessing aliyemaliza muda wake. Mark Wiessing amepangiwa kituo kingine cha Kazi ndani ya Benki Mama ya NMB – ‘Rabobank’ na sasa ataenda kuwa Meneja Mkuu nchini Brazil.
  Bwana Wiessing ataanza rasmi wadhifa mpya mwezi wa tano mwaka huu. 
  Ineke Bussemaker anakuja NMB akitokea ndani ya shirika mama la NMB – ‘Rabobank’ la nchini Uholanzi ambako alikuwa Mtendaji Mkuu katika Kitengo cha Malipo.
  Ineke ana uzoefu wa juu wa masuala ya kibenki na biashara ya kimtandao, utaalamu ambao unaelezwa kuwa utaisaidia benki ya NMB kukua zaidi. 
  Kabla ya RaboBank, Ineke alishika nyadhifa mbalimbali za juu katika banki za Citibank, ABN Amro Bank ya uholanzi, Uingereza na Denmark.
  Mark Wiessing anaiacha NMB ikiwa imekuwa kwa kasi kwa miaka minne ya uongozi wake, ameiacha NMB ikiwa na matawi zaidi ya170 na ATM zaidi ya 600 nchi nzima, huku ikiwa na hazina ya wateja zaidi ya milioni mbili, ambapo faida imekuwa kwa kasi kutoka Shilingi Bilioni 54 (Baada ya Kodi) mwaka 2010 mpaka faida ya Shilingi Bilioni 155 baada ya kodi mwaka 2014.
  Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NMB – Ineke Bussemaker akisalimiana na naibu gavana wa benki kuu ya Tanzania (BOT) – Juma Reli katika hafla iliyofanyika na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
  Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NMB – Ineke Bussemaker akitoa hotuba fupi kwa wageni waalikwa, uongozi wa juu wa benki na bodi ya wakurugenzi wa NMB katika hafla iliyofanyika na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
  Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NMB – Ineke Bussemaker katika mazungumzo na meya wa Ilala – Jery Silaa na Mwenyekiti wa Bodi ya NMB – Prof Joseph Semboja katika hafla iliyofanyika na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
  Mwenyekiti wa Bodi ya NMB – Prof Joseph Semboja akiongea wakati wa  katika hafla iliyofanyika na NMB  kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.
   Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Bw.  Mark Wiessing (kushoto) akiongea na waalikwa  katika hafla ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.

  0 0

  Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete katika picha hii ya maktaba anaonekana akimpa hongera mama ambaye amejifungua salama yeye na mtoto wake. Afya ya mama na mtoto ni moja ya ajenda ambayo inapewa umuhimu wa pekee katika duru ya Jumuiya ya Kimataifa. Tanzania na Canada kupitia wakilishi zao za Kudumu katika Umoja wa Mataifa zimeanzisha kundi la Nchi Marafiki kuhusu ajenda hiyo ya Afya ya Mama na Mtoto lengo kuu kuhakikisha kuwa mama na mtoto ni ajenda ambayo haifi.
  Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Canada katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Balozi Gillermo Rishechynski (pichani) mapema wiki iliyopita waliitisha kikao cha kwanza cha Nchi Marafiki kuhusu afya ya Mama na Mtoto, kikao hicho cha kwanza na ambacho kilifanyika katika uwakilishi wa Kudumu wa Canada, kilijadili pamoja na mambo mengine dhumuni la kuundwa kwa kundi hilo ambalo lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba afya ya mama na mtoto inaendelea kupewa umuhimu katika malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015, pamoja na kushawishi uwajibikaji na uwekezaji katika eneo hilo. kundi hilo linaundwa na nchi 40 kutoka mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea.

  Na Mwandishi Maalum, New York

  Kundi la Nchi Marafiki kuhusu afya ya mama na mtoto limekutana na kufanya kikao chake cha kwanza na kukubaliana kwa kauli moja kwamba mama anapokuwa na afya njema anakuwa na uhakika wa maisha yake na maisha ya mtoto wake.

  Kama hiyo haitoshi kundi hilo la nchi marafiki na ambalo limekutana nchi ya uenyekiti- wenza wa Wakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Canada katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Balozi Gillermo Rishchynski, limekubaliana haja na umuhimu wa kuhakikisha kuwa ajenda kuhusu afya ya mama na mtoto inaendelea na kubaki kuwa moja ya vipaumbele vya malengo mapya ya maendeleo baada ya 2015.


  0 0

  Karibu katika sehemu hii ya pili ya mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.
  Aliketi nasi kuzungumzia kuhusu kazi zake kama Waziri wa Uchukuzi na pia nia yake ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2015)
  Karibu


  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi uliofanyika Mkuranga mkoani Pwani. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,  Abdallah Kihato na Mkurugenzi wa Mwang'amba Communication, James Mwang'amba. (Picha na John Dande)
  Mkuu wa  Wilaya ya Mkuranga,  Abdallah Kihato akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi lililofanyika Mkuranga mkoani Pwani.
   Mkurugenzi wa Mwang'amba Communication, James Mwang'amba akitoa mada kwa wanawake wajasiriamali.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua bei ya mahindi katika soko la Miembeni mjini Dodoma Machi 8, 2015. Alipita sokoni hapo kukagua upatikanaji wa vyakula.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa maelezo kuhusu kilimo cha zabibu Walimu wa Shule za Kata ya Zuzu, Dodoma waliokwenda shambani kwake Machi 8, 2015 kwa ziara ya kujifunza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Naibu waziri wa Maji Amos Makalla ameendelea na ziara katika mkoa wa Lindi na leo amefanya ziara katika jimbo la Mchinga kwa kutembelea vijiji vya Kitohavi na LIHIMILO ambavyo vina shida ya maji kwa muda mrefu huku serikali ikiwa ameviweka vijiji hivyo katika mpango wa Matokeo ya haraka 
  Akiongea katika mikutano ya hadhara ameagiza uongozi wa halmashauri ya Lindi kuchimba visima virefu ndani ya wiki mbili kwa kuwa wizara yake ilishatuma fedha za kuchimbia visima hivyo na haoni sabababu za viongozi wa halmashauri hiyo kuendelea kuchelewa kuchimba visima hivyo huku utafiti na usanifu ulishafanyika muda mrefu na bei za kuchimba visima inaeleweka
   Mbunge wa jimbo la Mchinga Mhe. Said Mtanda ameishukuru serikali kwa hatua hii muhimu ambavyo itapunguza kero ya Maji katika vijiji vya Kitohavi na LIHIMILO.
  Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akisisitiza Jambo wakati wa mkutano wa hadhara kijiji cha Lihimilo jimbo la Mchinga mkoani Lindi
  Mbunge wa jimbo la Mchinga Mhe Said Mtanda akimkaribisha naibu Waziri wa Maji. 
  Naibu Waziri akizungumza na wananchi wa kijiji cha LIHIMILO ambapo walikuwa na hamu kubwa ya kusikiliza Kauli yake juju ya suala la kuchimbiwa Kisima.   0 0

  Kituo kinacho jihusisha na tiba asilia na huduma ya vyakula-lishe kwa wenye kusumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya, inatangaza nafasi za kazi ya usambazaji dawa kwa wateja wake waliopo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es salaam. 
  SIFA ZA MWOMBAJI : 
  1. Awe wa jinsia ya kike 
  2. Elimu isiyopungua darasa la saba na isiyo zidi kidato cha nne.
  3. Awe msafi, maridadi, mwaminifu na anayejituma. 
  4. Awe anaishi jijini Dar Es salaam. 
   MAJUKUMU YA KAZI : 
  Kusambaza dawa zetu kwa wateja wetu waliopo katika kata mbalimbali za jiji la Dar Es salaam.
   IDADI YA NAFASI : NAFASI HAMSINI ( 50 ). 
  MALIPO : Shilingi ELFU KUMI KWA SIKU. 
  Andika maombi yako ya kazi kupitia barua pepe yetu ambayo ni : neemarecruitmentagency@gmail.com Maombi yako yaelekezwe kwa MKURUGENZI MTENDAJI, NEEMA RECRUITMENT AGENCY. 
  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 21 MACHI 2015. 
  Kazi kuanza tarehe 30 MARCH 2015

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Raymond Mushi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar esb Salaam terehe 8.3.2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na mamia ya akina mama kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar es Salaam tarehe 8.3.2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi iliyotolewa na akina mama kutoka moja ya wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.


  0 0


  Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu,Lazaro Titus akiongozana na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Bunge ya Hesabu za serikali za Mitaa kwenda kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.
  Mwenyekiti akikagua jengo la Chuo cha Ualimu cha Ayalabee ambacho kinatajwa majengo yake kujengwa chini ya kiwango.
  Hili ndio jengo la Chuo cha Ualimu cha Ayalabee kama linavyoonekana sehemu ya Paa lake likiwa tayari limebinyea.
  Baadhi ya wananchi walipata fursa ya kutoa madukuduku yao kwa kamati juu ya ujenzi wa Chuo hicho.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya mnuso wa wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi,Tumsifu Swai akitoa neno la ukaribiho kwa wageni waliofika katika mnuso huo uliofanyika katika Hotel ya Sal Salnero mjini Moshi.
  Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungumza na watoto pamoja na kuwakaribisha wanafamilia wa benki hiyo katika mnuso wa usiku ulioandaliwa mahususi kwa ajili ya wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia zao.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Henry Mdimu
  Tangu asubuhi leo nilikuwa busy na awareness za uwanja wa Taifa katika mechi ya watani wa Jadi Yanga na Simba (picha ya pili). Ila jioni hii nilipoangalia simu yangu nikakuta watu wakinilaumu kutokana na tukio la mtoto Baraka Cosmas (picha ya kwanza) ambaye usiku wa kuamkia leo amekatwa mikono yake. 
  Wanasema nilikuwa nakula Bata Uwanja wa Taifa huku watu wanateketea. Hasa alikuwa akiongea mtu anaitwa @hmgeleka. 
  Kwanza nalaani kitendo hicho cha kikatili  na kuzidi kumuomba Rais wangu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete aongee na vyombo vyake vya usalama, wasiliache hili lipite hivi hivi. 
  Lakini jingine jamani suala hili sio la mmoja. Kwa sababu nimejitwika ubalozi ndio nilaumiwe kwa hata lililo mbali na mimi? Vita hii ni ya wote, mimi nina wiki mbili tu tangu nianze kazi hii na bado natafuta mtaji wa kuendesha zoezi langu. Tafadhali tutende wote tusinyoosheane vidole, huku tukiwa vijiweni, mmenielewa? #IMETOSHA
   Bango la harakati za "Imetosha!" likiingizwa uwanjani sambamba na ya FIFA ma FIFA Fair Play wakati wa mchezo wa ligi kuu wa watani wa jadi Simba na Yanga Uwanja wa Taifa leo. Chini ni Balozi wa Harakati za Imetosha Henry Mdimu akiongea machache kuhusu harakati hizo zenye lengo la kuhamasisha wadau wote kukomesha vitendo vya mauaji na vya kikatili dhidi ya ndugu zete Albino. 
  Wachezaji wa Yanga na Simba wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakiwa wamevaa fulana maalumu za harakati za "Imetosha!"
   Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani
  Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani. Marafiki hao ni mchanganyiko wa wana habari, bloggers, wasanii na wanaharakati wengine 
  Rafiki wa harakati za "Imetosha!" na balozi wa Jay Millions ya VODACOM Zembwela akihamasisha akiwa na marafiki wenzie. Kulia ni mchora katuni maarufu Masoud Kipanya ambaye pia ndiye mwenyekiti wa harakati hizo

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (kushoto) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed Albawardy
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (katikati) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed Albawardy
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana naSheikh Ali Sayeed Albawardy mmiliki wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar alipotembelea sehemu mbali mbali za Hoteli hiyo iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya kuifungua rasmi leo,
  Wasoma utenzi Amina Mohamed na Khadija Ridhiwani (kulia) walipokuwa wakitoa burudani hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi mbali mbali wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini akiwa Kaimu waziri wa Fedha alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi waHotel ya Park Hyatt Zanzibar kwa wananchi pamoja na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein azungumze na Wananachi baada ya kuifungua Hoteli hiyo iliyopo mtaa waMambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati alipokuwa akizungumza na wananchi na Viongozi mbali mbali na wawekezaji walioalikwa katika ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar yenye hadhi ya juu katikamtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo
  Baadhi ya waalikwa mbali mbali wakiwemo wawekezaji na wafanyabiashara wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi na Viongozi mbali mbali na wawekezaji walioalikwa katika ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar yenye hadhi ya juu katika mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiagana na Sheikh Ali Sayeed Albawardy baada ya kumalizika kwa sherehe za ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (katikati) Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bi Mercela Heeendoerfer.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard  Membe (kulia) akiwa nyumbani kwa chief Edward Wanzagi, kaka mkubwa wa Mwalimu Nyerere kijijini Butiama kabla ya kuanza kwa sherehe za kumkumbuka Chief Wanzagi. Chini Mhe Membe akihutubia.
  Chief Japhet Wanzagi  akiongea mbele ya mgeni rasmi Mhe Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kuhutubia  familia ya ukoo wa Nyerere mchana huu kijiini Butiama. Wengine ni Bw. Jesse Kwayu anayemwakilisha Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt Reginald Mengi na Mbunge wa Musoma vijijini Mhe Nimrod Mkono

  0 0

  Kampuni kubwa za mawasiliano Afrika mashariki Vodacom Tanzania na Safaricom ya Kenya leo zimezindua huduma mpya ambapo kuanzia sasa zaidi ya wateja Milioni 7 wa M-Pesa waVodacom Tanzania wanaweza kutuma na kupokea pesa kwa watumiaji zaidi ya milioni 18 wa Safaricom M-Pesa ya Kenya. 
  Huduma hii mpya ambayo imebuniwa na makampuni haya yanayoongoza kutoka huduma za mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki itawawezesha wateja wake kutuma pesa kwa kutozwa viwango sawa na vinavyotumika katika nchi husika. 
  Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hii,Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza alisema kuwa takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa mwaka 2013 zaidi ya shilingi bilioni 200 zilitumwa kutoka Tanzania kwenda Kenya halikadhalika zaidi ya bilioni 1 zilitumwa kutoka Kenya kuja Tanzania. 
  “Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa fedha karibu shilingi bilioni 200 zilizotumwa nchi Kenya kutoka Tanzania zilitumwa kwa njia rasmi za utumaji fedha na inakadiriwa kuwa kiasi cha fedha hizo zaidi ya mara mbili zimetumwa kwa njia zisizo rasmi za utumaji fedha ikiwemo kutumia madereva na makondakta wa mabasi au kutumia ndugu na marafiki wanaosafiri”amesema Meza. 
  “Tumeona ugumu wanaokabiliana nao wateja wetu kutuma fedha katika nchi jirani ya Kenya na tumepata suluhisho kwa kuleta huduma hii ambayo ni ya haraka na uhakika.
  Kuanzia leo hakuna sababu ya kutuma pesa kwa kumtumia dereva au kondakta wa basi au kutozwa gharama kubwa kutoka taasisi za kifedha unapolipa karo za watoto wanaosoma nchini humo,unaweza sasa kufanya malipo na kulipa ankkra mbalimbali kutoka pochi ya M-Pesa ukiwa umetulia nyumbani kwako,”amesema Meza. 
  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Safaricom Bob Collymore alisema “Tunaamini tumefungua ukurasa mpya wa kuendeleza huduma ya M-Pesa kwa kuwezesha wateja wa Kenya na Tanzania kutumia huduma hii katika kutumiana fedha na kufanya malipo katika nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya”.Alisema Alisema katika awamu hii ya kwanza iliyozinduliwa leo inawawezesha wateja kutuma pesa Kenya kama ambavyo wamekuwa wakituma hapa nchini, tofauti itakuwa wakati wa kutuma pesa kwenye simu kutakuwepo na kipengele kinachoonyesha kuwa wanataka kutuma pesa kwa M-Pesa ya Kenya na kuandika namba za mpokeaji kwa kutumia namba za Kenya yaani +254 na katika awamu ya pili ya huduma hii wateja wa Safaricom ya Kenya wataweza kutuma pesa kwa wateja wa Vodacom Tanzania kupitia huduma hii.” 
  Huduma ya M-Pesa inatolewa na makampuni ya Vodacom Tanzania na Safaricom ya Kenya yote yakiwa makampuni makubwa yanayotoa huduma ya mawasiliano katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.Wakati Vodacom inatoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwa asilimia 65 nchini. 
  “Ushirikiano huu wa mtandao wetu wa M-Pesa wenye mawakala zaidi ya 75,000 nchini Tanzania utawarahishia wateja wetu kupata huduma bora ikiwemo kufanya mihamala yao ya fedha kwa urahisi na tumejipanga kutoa huduma bora kwa wateja kwa muda wote wa masaa 24 kila siku.”Alisisitiza Meza. 
   “Kenya ni moja ya nchi inayofanya biashara kwa kiasi kikubwa na Tanzania ndio maana huduma hii imeanzia nchini humo na kuzidi kuunganisha na kuimarisha ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Tunaamini kuwa mawasiliano hayana mipaka kwa kuwa kwa kuwa huwaunganisha watu na jamii na jamii na kusaidia kuharakisha maendeleo na ndio maana Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika sekta hii”.Alisisitiza Meza. 
   Kuna zaidi ya Wakenya 300,000 wanaotuma fedha nchini kwao kwa kutumia njia zisizo rasmi na salama kama vile kuwatumia makondakta na madereva wa mabasi vilevile kuna watanzania wengi wanasomesha watoto wao nchini Kenya ambao nao wamekuwa wakipata shida kutuma fedha nchini humo.
  ”Kwa kuanzia leo huduma kwa wafanyabiashara kulipana zimerahisihwa ikiwemo kulipa karo za shule na vyuo na mihamala mingine,Huduma ya M-Pesa imerahisisha kila kitu na kuzidi kufungua milango ya biashara na ushirikiano”Aliongeza kusema Meza. 
   Alimalizia kusema kuwa huduma hii itafanya maisha ya watumiaji wake kuwa murua kwa kuwa watatuma fedha zao na kuwa na uhakika wa kuwafikia walengwa moja kwa moja na ni njia ya uhakika na yenye usalama inayowapunguza adhabu kubeba kiasi kikubwa cha fedha mifukoni na kwenye mabegi pia walengwa watapokea malipo kwa viwango vya ubadilishanaji sahihi visivyobadilika kila siku.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa kutuma na kupokea pesa nchini Kenya kwa njia ya M-PESA. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kulia) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania, Bernard Dadi (katikati) na Meneja wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu Tanzania, James Masoy, mara baada ya uzinduzi rasmi wa kutuma na kupokea pesa nchini Kenya kwa njia ya M-PESA uliofanyika jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania, Bernard Dadi (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Isack Nchunda wakimsikiliza jambo Meneja wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu Tanzania, James Masoy (katikati) wakati wa uzinduzi wa kutuma na kupokea pesa nchini Kenya kwa njia ya M-PESA. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania, Bernard Dadi (katikati) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto) baada ya uzinduzi rasmi wa kutuma na kupokea pesa nchini Kenya kwa njia ya M-PESA uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu Tanzania, James Masoy.

  0 0

  Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia January Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ya na kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
  Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo yenye lengo la kuwakwamua wanamuziki katika umaskini. CMEA pia itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.

  Mwanamuziki Mkongwe nchini, John Kitime akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ya inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za Afrika Mashariki ijulikanayo kwa jina la Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).


  0 0

  Bondia Mohamed Matumla atapanda ulingoni kuzichapa kuwania ubingwa wa dunia wa WBF Machi 27 dhidi ya Wang Xin Hua wa China.

  Pambano hilo la raundi 12 la uzani wa Bantam limepangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa juu, Francois Botha.

  Promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na pambano litasimamiwa na Shirikisho la ngumi la dunia la WBF ambaye rais wake atawasili nchini Machi 21.

  Kwa mujibu wa Msangi, bingwa wa pambano hilo atakata tiketi ya kwenda kuzichapa kwenye pambano la mabondia nguli duniani, Floyd Myweather na Manny Paqiao litakalofanyika Mei 2 jijini Las Vegas.

  "Mbali na pambano hilo pia mabondia Mada Maugo atazichapa na Japhet Kaseba kwenye uzani wa super middle na Thomas Mashali atazichapa na Karama Nyilawila.

  Wakizungumzia maandalizi yao, Matumla Jr, Kaseba na Nyilawila walisema wako fiti na kuwataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi  kushuhudia.

  Wakati bingwa wazamani wa dunia wa WBU, Rashid Matumla ambaye ni baba na kocha wa mwanae, Matumla Jr akitamba kuwa anaamini mwanae hawezi kumwangusha.


older | 1 | .... | 764 | 765 | (Page 766) | 767 | 768 | .... | 3272 | newer