Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 765 | 766 | (Page 767) | 768 | 769 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Ukuaji wa Sekta ya TEHAMA umekuwa wa mafanikio na msaada mkubwa katika kuharakisha, kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia  kikamilifu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa letu. Kwa mfano, wananchi walio wengi sasa wanapata huduma mbalimbali za mtandao kwa kutuma na kupokea pesa; kulipia ankara za maji, umeme na tozo mbalimbali kama vile ada na leseni; na mawasiliano ya simu na intaneti pamoja na elimu mtandao na tiba mtandao.

  Palipo na mafanikio hapakosi changamoto. Pamoja na kwamba tumeshuhudia manufaa na umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, biashara, miundombinu ya mawasiliano, pia kumekuwepo na changamoto ya matumizi mabaya ya mtandao katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, baina ya makundi ya watu na hata kutoka Taifa moja kwenda Taifa lingine kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni.

  Baadhi ya mifano ni pamoja na  suala la wizi wa fedha kwa njia ya mtandao, matukio ya uhalifu kwa kutumia mtandao, uvujaji wa taarifa za siri, upotevu wa haki miliki na matumizi ya saini na ushahidi, mmomonyoko wa maadili, athari za makundi maalumu kama vile watoto na usalama wa miundombinu mbalimbali ya TEHAMA ambapo Serikali imeingia gharama kubwa kuiweka.


  Wakati hayo yakijiri, Kwa sasa kumekua na wimbi kubwa la kurubuni watu kupitia mitandao ambapo majina ya wanasiasa, wanamuziki na wenye majina makubwa yameendelea kutumiaka vibaya katika mitandao ili kufanikisha urubuni wa kuwaibia watu pesa kwa kutumia jina la “VIKOBA” – Chakushangaza zaidi kurasa hizo zinazo onekana zaidi kupitia mitandao yakijamii zinaonekana zimedhaminiwa ili kuweza kusomwa na wengi kitu ambacho  kinapelekea kuonyesha jinsi gani wimbi hili na wahalifu hawa mtandao wamejipanga.


  Watanzania hawanabudi kuwa makini sana na kuwa waangalifu sana wanapo takiwa kuingiza taarifa zao binafsi na wanapo takiwa kufata maelekezo wa kutekeleza miamala kupitia mitandao kwenye vyanzo vyenye utata.


  0 0


  0 0


  Total Contrast - Takes a little time

  0 0
 • 03/11/15--20:30: TANGAZO KWA UMMA


 • 0 0


  0 0  0 0

  Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Jijini London na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Peter Kallaghe na Naibu Mkuu Mkuu wa Ubalozi Msafiri Marwa (wa pili kushoto) na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy.

  Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe na ujumbe wake kwenye mazungumzo ya kikazi na Mhe. James Duddridge, Waziri wa Masuala ya Afrika wa Uingereza mara baada ya kuwasili London Jumatano tarehe 11/03/2015.
  Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe na ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha kazi na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola Mhe. Kamalesh Sharma Jumatano tarehe 11/03/2015.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Dear Friends

  Napenda kutoa taarifa kwamba kumekuwa na tapeli mmoja ambae amekuwa akitumia picha zangu kwa kufungua facebook accounts kwa majina mbali mbali kama Justin Stan,James Brown,Onesmo,Felister Julius, Anthony Yohana au Yohana Anthony na mengineyo mengi.

  Mtu huyu amekuwa akijenga urafiki na watu wasiotambua kuwa ni TAPELI katika mtandao wa kijamii wa Facebook

  Urafiki ukiwa umekamilika kwa maana ya friends request kutoka kwake and acceptance kutoka kwa victim amekuwa akiwaambia marafiki zake hawa wa Facebook kuwa yeye ni muajiriwa sehemu mbali mbali tofauti katika kila account hizi za facebook kama kwa mfano  kwingine akidai anafanya Vodacom Mlimani City, kwingine akidai anafanya Tanesco Makao Makuu,PPF na sehemu nyingine kadhaa na amekuwa akiwaahidi kwamba ana watu wenye uwezo wa kuwaunganishia kazi sehemu hizo kwa sharti la wanaotaka kazi kujikusanya na kufikia idadi ya watu watano na wakilipa kiasi cha shilingi 50,000 kila mmoja basi watapata nafasi za kazi hizo.

  Wakati mwingine amekuwa akiwa wadanganya baadhi ya watu kuwa yupo mkoani kikazi au akihudhuria semina na kwamba mdogo wake anashida ya dharura ya pesa kama shilingi 25,000 au 30,000 na kuomba marafiki wamtumie na kuwaahidi atawarudishia mara atakapokua free, amekuwa akitoa namba mbali mbali za simu mojawapo zikiwa hizi 0785412653 na 0688081032. Wale walioshtuka amekuwa akiwatukana matusi makubwa ya nguoni bila uoga.

  Natoa tahadhari kwa watu wote kujihadhari na kufanya urafiki na watu msio wajua, kuzingatia umakini haswa katika mambo ya pesa, pia kujua watu wa namna hii ni wengi sana online haswa kwenye social media. Nashauri uki suspect mtu wa design hii basi wasiliana na polisi na ikibidi kumtengenezea mtego wa kumnasa.

  Vijana tunatakiwa tuchape kazi kwa nguvu na sio kutafuta njia za mikato. Hakuna hadithi yeyote niliyowahi kuisikia ya aliyefanikiwa katika maisha kwa njia ya mkato. Mwana fundi ni kusoma kwa bidii ili elimu yako ikupatie ajira.

   Mwisho naomba marafiki zangu wooote mnisaidie kurepost message hii kwani naamini itawaokoa wengi (vulnerable) ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kuwa hawajui utapeli huu wa online.

  Picha hiyo hapo juu ni yangu na ndio amekuwa akiitumia kwenye account nyingi za facebook.

  Mimi ninaamini Mungu na hivyo huyu bwana Siku zake 40 zipo karibu. Napenda pia kwa namna ya kipekee nawashukuru wale wote (zaidi ya 10) waliotumia muda wao kunitafuta na kunipa taarifa hizi muhimu walipomshtukia Tapeli huyu.

  Mwenyezi Mungu awabariki saana.

  0 0


  0 0

  Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais.

  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na Wataalam wa Mazingira wameagizwa kutoa elimu ya mazingira kwa wawekezaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Sunshine uliyopo Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya .Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Injinia Binilith Mahenge jana alipotembelea machimbo ya Mgodi huo nakubaini kuwa unaendeshwa bila kuzingatia Kanuni za Mazingira.

  Katika ziara hiyo Mh. Mahenge alibaini kuwa mgodi huo hauna mtambo wa kutibu maji-taka yake kabla ya kuyatiririsha katika mazingira pia bwawa linalotumika kuhifadhi maji-taka hayo halikidhi viwango vya Kanuni za Mazingira pamoja na kuzibwa kwa mfereji wa asili hivyo kuzuia mkondo wa mvua.  Kutokana na hali hiyo, Waziri Mahenge alitoa siku 30 kwa wataalam wake kuwapatia elimu ya Kanuni za Mazingira wawekezaji wa Mgodi wa Sunshine ikiwa ni pamoja na kuwataka wawekezaji hao kutekeleza kanuni hizo ndani ya siku 30 kuanzia jana.

  Wakati huo huo Mh. Mahenge alitembelea Machimbo ya Dhaabu ya Mek na Mgodi wa Shanta Wilayani Chunya ambapo Wataalam wake Mazingira walibainisha kuwa wawekezaji wa migodi hiyo wametiza kanuni za mazingira.

  Sanjari na hayo Injiania Mahenge alikutana na Watendaji wa Halmashauri ya Chunya na kukabidhiwa Mapendekezo ya Mradi Maalumu wa kulinusuru Ziwa Rukwa ili lisitoweke kutokana na kilimo holela, uchimbaji wa madini na utirirshwaji wa maji- taka kwenye vyanzo vya Ziwa hilo.

  Katika makabidhiano ya Mapendekezo hayo Mh. Mahenge aliwaahidi Watendaji wa Halmashauri ya Chunya kuwa atayafanyia kazi Mapendekezo yao lakini pia aliwaomba na wao kuishauri Wilaya waingize Mazingira katika bajeti zao .
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mheshimiwa Binilith Mahenge akisiliza jambo kutoka kwa Mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Abas Kandoro kabla ya kuanza Ziara yake ya siku mbili Mkoani humo jana.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mh. Binilith Mahenge (katikati), wakijadili jambo na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mh. Deodatus Kinawito (kushoto) pamoja na Diwani wa Kata ya Mkugani ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mh. Bosco Mwanginde (kulia) wakati wa Ziara ya Waziri Mahenge Wilayani humo jana.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Binilith Mahenge (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa Machimbo ya Dhahabu katika Mgodi wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya, Bwana Andy Wu (kulia), katika ziara ya Mazingira Mgodini humo jana na wakati katika picha ni Diwani wa Kata ya Mkugani ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya, Mh. Bosco Mwanginde.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mh. Binilith Mahenge, akionesha Bwawa linalotumika kuhifadhi Maji-taka yenye Sumu kutoka kwenye Mgodi wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya jana, huku akiwataka Wawekezaji wa Mgodi huo kuboresha Bwawa hilo ili kukidhi Kanuni za Mazingira za Tanzania . (Picha na OMR) 

  0 0

  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa,(LAAC) ikitembelea kukagua mradi wa umwagiliaji wa Skimu ya Mang'ora wilayani Karatu.
  Baadhi ya Mashamba ya Vitunguu katika skimu ya umwagiliaji ya Mang'ora.
  Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa,Azza Hamad akitizama mfereji wa maji katika skimu ya Maji ya Mang'ora iliyojengwa kwa fedha za serikali ambao hata hivyo hautumiki.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Baadhi ya Maafisa, Askari na Mtumishi raia ambaye pia Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Estomih Hamis (Mzee wa Magereza Kileleni) wa saba kutoka kushoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika kilele cha Mlima Kilimanjaro asubuhi ya Machi 9, 2015 na kutundika bendera ya Jeshi hilo kileleni.
  Kiongozi wa Msafara wa Maafisa, Askari na baadhi ya watumishi raia wa Jeshi la Magereza waliopanda mlima Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy akiwa katika uso wa furaha mara alipowasili katika kituo cha Gilman’s kabla ya kuanza safari ya kuelekea kilele cha Mlima huo cha Uhuru. Kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Bakari Boi akiwa katika sura ya uchovu baada ya safari ndefu ya usiku kucha kutoka Kituo cha Kibo kuelekea Gilman’s.
  Kundi la Maafisa, askari na watumishi raia wa Jeshi la Magereza pamoja wa waongoza njia (guiders) kwa pamoja likiwa katika mwendo wa kilometa tisa kutoka Horombo kwenda kituo cha Kibo ambapo liliwasili majira ya saa tisa alasiri na kupumzika kabla ya kuanza safari ya kwenda Gilman’s saa tano usiku.


  0 0


  0 0

  WAKATI zimebaki siku chache kwa timu za waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuanza kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa Kombe la NSSF, timu kongwe ya TBC imepokea vifaa vya michezo kutoka Kampuni ya Isere Sports kwa ajili ya michuano hiyo.

  Katibu wa timu ya TBC, Jesse John alisema vikosi vyake vinajifua usiku na mchana kuhakikisha ukongwe wao katika fani ya habari unaonekana kwa ushindi wa uwanjani.

  "Tunaishukuru Kampuni ya Isere kwa kutusaidia vifaa vya michezo vitakavyokuwa chachu ya kujituma kwetu kuhakikisha tunachukua ubingwa mwaka huu" alisema Jesse John ambaye ni kipa namba moja wa timu hiyo.

  Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Soprts, Abbas Isere alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wa michezo  na kuwa mstari wa mbele kutoa vifaa vya michezo kwa wanamichezo na pia iko mbioni kuanzisha bonanza maalum kwa wapenda michezo hapo baadaye.

  Alisema Isere Sports ambayo ni familia ya wanamichezo inaonelea kuwa ikisaidia kuinua michezo nchini tkaokoa maisha ya vijana watanzania ambao badala ya kukaa vijiweni na kujiingiza kwenye biashara haramu wanaingia viwanjani kufanya mazoezi ili kuiweka mili yao fiti.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akitoa maelezo ya hali ya migogoro ya Ardhi iliyopo Mkoani Mwanza kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi alipokutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa katika ziara yake Mkoani Mwanza.Picha na Muungano Saguya- Mwanza
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mh. Jaji Mfawidhi Makalamba alipokutana naye ofisini kwa Jaji huyo Jijini Mwanza ili kupata namna bora ambayo mhimili wa mahakama unaweza kusaidia kutatua migogoro ya ardhi nchini. Waziri Lukuvi yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Mwanza yenye nia ya kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.


  0 0

  Dr. Natalius Kapilima wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimpima shinikizo la damu Bw. Exadius Nthono wa Lesotho katika mkutano wa mwaka wa wahasibu waandamizi unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere ambapo NHIF inatoa huduma za upimaji afya bure. 

  Na Catherine Kameka

  WADAU wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wameuomba Mfuko huo kuendeleza programu za upimaji wa afya bure ili kuwasaidia wanachama wake na wananchi kwa ujumla kujua hali za afya zao lakini pia kuepekana na maradhi yasiyoambukiza.

  Hayo wameyasema Dar es Salaam jana katika mkutano wa Wahasibu Waandamizi wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere ambapo NHIF ilishiriki kwa kuwa na banda la elimu kwa umma na upimaji wa afya bure uliokwenda sambamba na utoaji wa elimu ya namna ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza kama moyo na mengine.

  Pamoja na ombi hilo, NHIF imekuwa ikiendesha upimaji katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kuwasaidia wananchi kufahamu afya zao lakini pia kuwapa ushauri wa namna ya kujikinga na maradhi hayo ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na matibabu yake ni ya ghari.


  0 0

  Baadhi ya watalaam kutoka Kampuni ya Elektro Merl ya nchini Austria ambao walileta na kufunga makontena ya umeme wa jua pamoja na mfumo wa usambazaji umeme kwa vijiji 10 vilivyo mbali na gridi ya taifa, pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakikagua moja ya makontena ya umeme wa jua katika Kijiji cha Lobilo, wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma hivi karibuni.
  Baadhi ya nyumba za wananchi katika Vijiji vya Lobilo na Silale, wilayani Kongwa, mkoa wa Dodoma, zilizounganishiwa huduma ya umeme wa jua kupitia makontena maalum.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Familia ya Marehemu Robert Mwang'onda wa Mabibo jijini Dar es Salaam wanapenda kutangaza kupotelewa na ndugu yao Nsajigwa Kennedy Mwang'onda ambaye aliondoka nyumbani Mabibo CCM - Karibu na Chuo Cha Usafirishaji toka tarehe 26-2-2015. Anamatatizo la kupoteleza Kumbukumbu.
  Atakayemuona awafahamishe kwa simu namba 0715 919 168 Frank Mwang'onda, 0682 822 111/ 0754 631 888.
  Au atoe taarifa kituo chochote cha Polisi kwa URP/RB/2331/2015.

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Huawei,Ken Hu akizungumza katika Mkutano wa Dunia wa masuala ya simu (MWC) uliofanyika jijini Barcelona nchini Hispania mwishoni mwa wiki iliyopita,uliokuwa ukijadili teknolojia ya simu za mkononi (5G).
  Kizazi cha tano cha teknolojia ya simu za mkononi (5G) kinategemewa kuwa nguzo muhimu sana ya miundo mbinu katika ulimwengu ujao wa teknolojia. Hayo yamesemwa na Bwana Ken Hu, Makamu mwenyekiti wa Kampuni ya Huawei ambaye kwa kupokezana yeye ndiye Mkurugenzi Mtendaji kwa sasa.

  Akizungumza katika Mkutano wa Dunia wa masuala ya simu (MWC) uliofanyika jijini Barcelona nchini Hispania mwishoni mwa wiki iliyopita, Mr, Hu alisisitiza kwamba maono ya kuwa na teknolojia ya 5G yatafanikiwa kupitia ushirikiano wa sekta mbalimbali, ubunifu makini katika teknolojia na mageuzi katika mikakati ya kibiashara.

  “Msukumo mkubwa wa kuwa na teknolojia ya 5G unahusisha mahitaji ya kumwezesha mtumiaji kupata urahisi kutumia, uwezekano wa vifaa vingi zaidi kutumia Internet katika maisha ya kila siku, na mahitaji ya kuwa na watoa huduma wanaozingatia sekta maalum pekee katika mapinduzi ya viwanda siku zijazo” Alisema Bwana Hu.


older | 1 | .... | 765 | 766 | (Page 767) | 768 | 769 | .... | 3272 | newer