Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

DC MUFINDI ATEMBELEA MRADI WA YA KUZALISHA UMEME -KIHANSI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi,Mhe. Mboni Mhita (Kushoto) akiwa ameambatana na watendaji wengine amefanya ziara ya kutembelea mradi wa Kihansi unaotoa huduma ya kuzalisha Umeme,Kushoto ni Mhandisi wa Kihansi akitoa maelezo juu ya shughuli za uzalishaji wa Umeme.

Spika Makinda, Wenyeviti wa Bunge Watembelea Miradi ya NSSF Dar

$
0
0
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakitembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (MB) juu ya mradi. Wengine ni Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni. Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (MB) juu ya mradi. Wengine ni Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea miradi mbalimbali ya NSSF ya jijini Dar es Salaam ukiwemo mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.


SERIKALI KUENDELEA KUTOA VIPAUMBELE KWA WANAWAKE KIUCHUMI, KIELIMU NA KIUONGOZI

$
0
0




Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake kitafa akibonyeza kitufe katika kompyuta mpakato kwa ajili ya kupinga king'ora ili kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho hayo jana ( Machi 6) ambayo kilele chake ni machi 8, mwaka huu ,katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro ( anayepiga makofi) ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana ( kulia) ni Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa , upande wa Serikali za Mitaa, Noel Kazimoto.

Meneja wa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF , Anjela Mziray akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, alipolitembelea banda hilo.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Rajab Rutengwe ( kushoto) akitoa shukrani zake baada ya kusoma hotuba ya uzinduzi wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya wanawake duniani.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

EALA SPEAKER CALLS ON PRESIDENT OF RWANDA SENATE

$
0
0
Rt Hon Daniel Kidega shakes hands with the Deputy Speaker of the Chamber of Deputies, Hon Uwimanampaye Jean d' Arc as the Speaker, Rt. Hon Donatile Mukabalisa and Deputy Speaker, Hon Abbas Mukama look on.
The Speaker of the Chamber of Deputies, Rt. Hon Donatile Mukabalisa shares a light moment with the Speaker of EALA Rt. Hon Daniel Kidega.
President of the Senate, Rt. Hon Bernard Makuza (right) exchanges notes with the EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Kidega (centre) as Hon Christophe Bazivamo looks on.

RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI STUDIO MPYA ZA AZAM TV JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa.

JK AHUDHURIA KIKAO CHA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI KIGALI, RWANDA, LEO

$
0
0
Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wakuu wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Kigali, Rwanda, mchana huu. Wengine toka kulia ni Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, mwenyeji wao Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Salva Kiir wa Sudani ya Kusini ambaye amehudhuria kama mwalikwa. Picha na Fred Maro

NJIA 8 ZA KUTENGENEZA FEDHA KUPITIA BIDHAA YA TREVO

$
0
0

KUJUA NAMNA YA KUJIUNGA
TUMA EMAIL: kemi@trevo.co.tz

Boko Beach Veterans wamkabidhi zawadi Mchezaji bora wa Mwezi

$
0
0
Mwenyekiti wa Boko Beach Veterans (BBV),Danny Ole a.k.a Aguero (kushoto) akimkabidhi zawadi Mchezaji bora wa Mwezi,Richard Mwandya,baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwa kipindi chote cha mwezi Februari 2015.Zawadi hutolewa na mdau mkubwa wa soka nchini na mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashion, Othman Tippo Shabani (picha ya chini mwenye jezi nyeupe kati).


USHUHUDA WA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA KATA YA MTAKUJA, KUNDUCHI, DAR ES SALAAM

JK ahudhuria mkutano wa kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini jijini Kigali, Rwanda

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame amesema kuwa hatua ya Mwenyekiti wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Tisa wa Nchi Zilizoungana Kutekeleza Miradi ya Miundombinu Ukanda wa Kaskazini za Northern Corridor Projects ni hatua muhimu katika kufungua utekelezaji wa miradi ya miundomninu katika kanda nyingine za EAC. 
Aidha, Rais Kagame amemshukuru Rais Kikwete kwa uamuzi wake kuhudhuria Mkutano huo uliofanyika leo, Jumamosi, Machi 7, 2015, katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena mjini Kigali, Rwanda. 
Rais Kikwete amefanya ziara hiyo ya siku moja kuhudhuria Mkutano huo kwa mwaliko wa Rais Kagame. 
Naye Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa ni jambo la kufurahisha kwamba Rais Kikwete ameweza kuhudhuria Mkutano wa leo, kwa sababu sasa njia imefunguka kuanza kazi ya utekelezaji wa miradi kwenye Ukanda wa Kati wa Central Corridor unaokatisha katikati ya Tanzania. 
Marais Kagame na Kenyatta walikuwa wanazungumza wakati wa hotuba za ufunguzi za Mkutano huo uliofanyika kwa kiasi cha saa mbili unusu mara baada ya Rais Kikwete kuwasili Kigali akitokea Dar es Salaam kiasi cha saa sita mchana. 
Akifungua Mkutano huo, Rais Kagame alisema: “Nawashukuru waheshimiwa marais wote kwa kuja. Lakini hasa hasa, namshukuru sana mwenyekiti wetu wa EAC Rais Kikwete kwa kupata muda wa kuja kujiunga nasi katika mkutano huu.” Aliongeza Rais Kagame huku makofi yakiendelea kumkaribisha na kumshangilia Rais Kikwete: 
“Kuwepo kwake hapa leo, kunaongeza matumaini kuwa miradi mbali mbali na mingi zaidi katika kanda mbali mbali za nchi zetu wanachama wa EAC, sasa inaweza kutekelezwa kwa haraka zaidi. Nakushukuru sana Mheshimiwa Rais.” Mbali na Marais Kikwete, Kagame na Kenyatta, Mkutano wa leo pia umehudhuriwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Makamu wa Rais wa Pili wa Burundi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia. 
Nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Sudan Kusini ndizo wanachama wa Northern Corridor na kwenye mkutano wa leo, Burundi pia imetangaza kuwa imeamua kuwa mshiriki kamili wa mikutano ya Ukanda huo badala ya kuwa msikilizaji kwa muda mrefu. 
Akizungumza katika Mkutano huo, Rais Kenyatta amesema: “Tunafurahi sana kwamba Mwenyekiti wetu wa EAC yuko nasi leo kwa sababu uwepo wake utaongeza msukumo wa kutuwezesha kuanza utekelezaji wa miradi mingine hasa katika Ukanda wa Kati. Tanzania ina mengi kuchangia katika jambo hilo. Kwa mfano, umeme mwingi ambao utaanza kuzalishwa na Tanzania mwaka huu, unahitajika kwa nchi zote za EAC na Northern Corridor.” 
Rais Kikwete ambaye alikuwa msikilizaji tu kwa sababu Tanzania inaendelea kuwa mwanachama wa EAC bila kuwa mshirika wa Northern Corridor amezugumza kwa ufupi tu akisema kuwa kwa sababu yeye ni mwalikwa na msikilizaji asingeweza kusema mengi. 
Amewaambia viongozi wenzake: “Nakushukuru Rais Kagame kwa kunialika. Kama unavyojua, mimi ni msikilizaji tu na hivyo siwezi kusema sana. Lakini napenda kuwapongezeni nyote kwa kazi mnayoifanya. Sote tunajua kuwa hakuna utengamano bila kuendeleza miundombinu.” Ameongeza Rais Kikwete: “Kinachoendelea kule Northern Corridor kitasaidia sana katika mawazo na utekelezaji wa kazi ambayo tunajiandaa kuianza kwenye Ukanda wa Kati. Nawatakieni mafanikio zaidi na kasi ya Mwenyeji Mungu katika utekelezaji wa miradi yenu.” 
Chini ya Northern Corridor nchi hizo zimebuni miradi 14, ambayo baadhi yao imeanza kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha visa moja ya kusafiria ya watalii. 
Nchi hizo ziliunda kundi hilo mwaka mmoja na miezi tisa iliyopita na wakuu wa nchi wanachama hukutana kila baada ya miezi miwili kwa mashauriano na maamuzi. Rais kikwete amerejea nyumbani usiku wa leo baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kwa furaha  sahada la maua baada ya kuwasili Kigali, Rwanda, tayari kwa mkutano  na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
Mkutano wa leo pia umehudhuriwa na wakuu wa nchi za Kenya, Uganda na wenyeji Rwanda. Mbali na nchi hizo na mbali na Tanzania, nchi za Burundi na Sudan Kusini pia zilialikwa kuhudhuria mkutano huo. Mkutano huo ni ulijadili hatua za utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyokubaliwa kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa nane wa namna hiyo uliofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 11, mwaka jana, 2014.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda kabla ya kuanza kwa mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni leo Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kati ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema. PICHA NA IKULU

KINANA ATOA USHAURI KWA KATIBU MKUU KIONGOZI KUWASIMAMISHA MARA MOJA VIONGOZI WALIOTAJWA KWENYE SAKATA LA ESCROW .

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amebeba maji kwenye madumu aliposhiriki umwagiliaji maji katika shamba la nyanya la vijana wajasiriamali wa CCM katika Kijiji cha Nkulabi, Kata ya Mpunguzi, Jimbo la Dodoma Mjini leo wakati wa ziara yake,Kinana yupo mkoani Dodoma kwa ziara ya siku tisa ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimwagilia maji zao la nyanya la vijana wajasiriamali wa CCM katika Kijiji cha Nkulabi, Mpunguzi, Dodoma. Kinana aliwapongeza vijana hao wanne kwa kuamua kuanzisha shamba hilo ambalo mazao yake yanawasaidia kujikimu kimaisha.Kinana aliwataka vijana wengine kuiga mfano huo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Dodoma, ambapo ametoa ushauri kwa Katibu Mkuu Kiongozi, kuwasimamisha mara moja watumishi wanaotajwa kwenye sakata la Escrow kama CCM ilivyowasimamisha viongozi watatu waliotajwa kwenye sakata hilo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Dodoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya  Barafu,Nape aliwaambia wakazi hao kuwa makini na wapinzani kwani wamekuwa wakihangahika na fedha za wafadhili ambazo hawaitakii mema nchi yetu.
 Pichani ni baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo. 

PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA

REMEMBRANCE OF 3RD YEAR SINCE PROMOTION TO GLORY

$
0
0
JUDICA STEPHANO TERI
22.06.1946  to  08.03.2012

Passed away peacefully after a short illness. 
It is 3 years today since you departed from this life and promoted to glory. Your dear wife Jane, children Joan, Linda, Davis and Hillary Teri, sister Mony and their families together with the entire TERI family and friends deeply miss you daily.
Each day we are filled with fresh memories of your love, wisdom and care. 
However,
WE THANK GOD FOR HIS PROTECTION AND BLESSINGS TO ALL OF US.
"John 11:25.. whoever believes in me (Jesus), though he die, 
yet shall he live!" 

KIPINDI CHA MASKANI YA TIMES FM WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA KATIKA HOSPITALI YA MWANAYAMALA, DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Times Radio Fm, Mr. Rehure Nyaulawa (kushoto) akimkabidhi msaada wa mashuka Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk, Sophinias Ngonyani (kulia) mara baada ya Timu nzima ya Kipindi cha Maskani kilipopiga hodi hospitalini hapo kutoa misaada ya mashuka yapatayo 200 kwa ajili wodi ya akina mama na watoto. Msaada huo ilikuwa ni kuunga mkono maadhimisho ya wanawake duniani inayoadhimishwa leo Machi 8, duniani kote. Wanaoshuhudia ni Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan na Mkurugenzi wa Mazinat Bridal Maza Sinare. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ni 'Uwezeshaji Wanawake, Tekeleza Wakati ni Sasa'.
Wakifurahia msaada.
Mtangazaji wa Kipindi cha Maskani ya Times Fm, Stanslaus Lambat (wa kwanza kulia) akiendelea kurusha matangazo live toka eneo la tukio.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NYUMBA INAPANGISHWA! KIJITONYAMA

$
0
0
Nyumba ipo KIJITONYAMA, Barabara ya kwenda kwa kopa, ina vyumba 12, inafaa kwa huduma za Ofisi, Biashara pia inaeneo kubwa la kuegesha magari na ipo jirani na Barabara ya lami kama inavyoonekana katika picha. Kwa mawasiliano zaidi tumia 0754 285529 au 0787285529 au Barua pepe florenyambo@gmail.com
Muonekano wa ndani wa nyumba hiyo.
Muonekano wa nje wa nyumba hiyo.

VETA YAKUTANA NA WADAU WA VIWANDA VYA UMEME NA MAGARI KUJADILI KUHUSU MRADI WA MAFUNZO YANAYOTOLEWA NA VETA KWA KUSHIRIKIANA NA VIWANDA

$
0
0
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) imekutana na wadau wa viwanda vya umeme na magari jijini Dar es Salaam kujadili utekelezaji wa mradi wa mafunzo yanayotolewa na VETA kwa kushirikiana na viwanda ujulikanao kama Dual Apprenticeship Training Project.

Mradi huo uliopo kwenye majaribio tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 kwa ushirikiano kati ya Hamburg Chamber of Skills Craft ya Ujerumani na VETA,unalenga kuandaa idadi kubwa ya mafundi stadi wenye ujuzi zaidi kwa vitendo kwa kuwa sehemu kubwa ya mafunzo hayo inafanyika viwandani.

Akifungua rasmi warsha hiyo mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi-VETA Leah Lukindo alisema kwamba ni muhimu kwa vyuo vya ufundi stadi kutoa stadi zinazohitajika na viwanda kwa kuwa viwanda vinategemea nguvu kazi hiyo ili kufanikisha malengo yake.

Alisema kukosekana kwa ushirikiano kati ya vyuo vya ufundi stadi na viwanda kunasababisha malalamiko mara kwa mara kutoka viwandani ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi nchini.

Alisisitiza kuwa mfumo wa Dual Apprenticeship Training unamwezesha kijana kupata ujuzi wa fani husika wakati anafanya kazi kwenye kiwanda hivyo kumuwezesha kwa kiasi kikubwa kujifunza zaidi kwa vitendo na kuendana na mahitaji ya soko la ajira pmaoja na kupata uzoefu na uelewa wa mazingira halisi ya kufanyia kazi.

Aliwataka wenye viwanda kuonyesha ushirikiano kwa kujiunga na mradi huu ambao una faida kubwa kwao kwani unawasaidia kupata mfanyakazi mwenye ujuzi unaotakiwa pamoja na uzoefu wa kazi kwa kuwa muda mmwingi wa masomo anakuwa kwenye kiwanda husika.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi-VETA Leah Lukindo akizungumza wakati akifungua rasmi warsha hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Giraffe-Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha hiyo ambao ni wadau wa viwanda vya umeme na magari wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
Mratibu wa mradi huo Francis Komba akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akiwasilisha mada inayohusu wajibu wa wadau wa viwanda katika utekelezaji wa mradi. 


Afande Prisca Komba atwaa Tuzo ya Mwanamke mwenye Mafanikio Tanzania 2014

$
0
0
 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni anayesimamia Dawati la Jinsia, Inspekta Prisca Komba (pichani), ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mwanamke mwenye Mafanikio Tanzania kwa mwaka 2014.
 
Inspekta Komba, alishinda pia Tuzo ya Mwanamke wa Mwenye Mafanikio katika Sekta ya Umma.

Wengine waliopata tuzo mbalimbali ni pamoja na Debora Mwenda, aliyepata tuzo ya Mwanamke mwenye mafanikio ya maisha, Penina Mlama, alipata tuzo ya Utamaduni na Sanaa, Mary Gitanho, Tuzo ya Ustawi wa Jamii.

Sharmillah Bhatt, tuzo ya Sayansi na Teknolojia, Jennifer Shigoli, tuzo ya Mwanamke mdogo mwenye Mafanikio, Blandina Sembu, tuzo ya Habari na Mawasiliano.

Pia Dk. Wineaster Anderson, tuzo ya Taaluma, Nahida Esmail, tuzo ya Elimu, Devotha Likokola, Biashara  na Ujasiriamali, Jacqueline Mkindi, tuzo ya Kilimo, Mpendwa Chihimba,tuzo ya Afya na Angel Eaton, tuzo ya Michezo.

Tuzo hizo, zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Tuzo za Wanawake Wenye Mafanikio Tanzania (TWAA) inayoandaa tuzo hizo zilizokutanisha wanawake zaidi ya 700.

 Rais na Mwandaaji wa tuzo hizo, Irene Kiwia, akikabidhi tuzo hizo alisema  jumla ya Wanawake 36 waliingia tatu bora katika vipengele 12 vilivyokuwa vinashindaniwa na kati ya hizo jumla ya tuzo 14 zimetolewa.

“Katika kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo inafanyika kitaifa  kesho (leo) tumeona ni vyema tukawapatia tuzo wanawake ambao wameleta mabadiliko chanya ndani ya jamii,kwani mafanikio yao yanaleta hamasa kwa wanawake wengine wenye malengo,”alisema Kiwia.

Alivitaja vipaumbele vya mwanamke ambaye anataka kuleta mabadiliko ndani ya jamii kuwa ni ndoto,uthubutu,kufuatilia ndoto,uvumilivu na ustahimilivu.

Akizungumzia tuzo hiyo, Ispekta Komba, ameishukuru jamii kwa kutambua umuhimu na kazi ambazo amekuwa akizifanya ndani ya jamii na kwamba amepata nguvu ya kuendelea kufanya kazi hiyo kwa ufanisi zaidi.

“Sikutegemea kupata tuzo hii na nimelia kwa chozi la furaha,namuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Ernest Mangu, pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, kutoa vyeo kwa wakati ili kuongeza motisha wa kufanya kazi,”alisema Komba

Aliitaka serikali na mahakama kuhakikisha inasimamia kesi za udhalilishaji na ukatili wa kijinsia zinatolewa hukumu mapema ili kumaliza vitendo hivyo ndani ya jamii na pia kupunguza kasi ya udhalilishaji ambayo inatokana na watuhumiwa kutochukuliwa hatua kwa wakati.
 
Raisi  wa Taasisi ya Tuzo ya Wanawake Wenye Mafanikio Tanzania, Irene Kiwia akizungumza katika hafla ya Utoaji wa tuzo hizo uliofanyika katika  Ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es salaam.

Mrembo Miss Tanzania aongoza wakazi wa dar katika zoezi la uchangiaji damu jijini dar leo

$
0
0
Mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2014,Doris Mollel akishiriki zoezi la uchangiaji damu katika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya wanawake Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Ofisa Muuguzi kutoka Benki ya Damu Salama,Selina Joseph. Zoezi hilo la uchangiaji damu liliandaliwa na Mrembo huyo.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakishiliki zoezi la uchangiaji damu katika kusherehekea Siku ya wanawake Duniani,iliyofanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam leo.
Mpiga Picha wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd,John Dande akipima uzito tayari kwa kushiriki zoezi la uchangiaji damu,ikiwa ni sehemu kuunga mkono sherehe za Siku ya wanawake Duniani.zoezi hilo limefanyika Buguruni Chama jijini Dar es Salaam leo.Picha na John Dande.

Mdau Abdulaziz Ahmed ajitosa kuwania Ubunge Jimbo la Lindi Mjini

$
0
0
Na Ahmaid MMOW-Lindi 

Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu,Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel ten,Abdulaziz Ahmed leo Ametangaza nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Lindi mjini katika uchaguzi mkuu ujao kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,Abdulaziz ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Lindi alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kujitathimini na kugundua kuwa anao uwezo wa kuzikabili na kuzitafutia majibu yakinifu changamoto mbalimbali zilizopo katika jimbo la Lindi ambalo kwa sasa lipo chini ya Mbunge toka CUF,Salum Barwany.

"mwaka 2010 niliomba ridhaa ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi hata hivyo kura hazikutosha kupitia chama changu na Jimbo kuchukuliwa na Upinzani na nimeona changamoto nyingi zimeendelea kuwepo kwa miaka nenda rudi bila kutafutiwa ufumbuzi wa uhakika Nipeni Ridhaa wana lindi niwatumikie kuliko ilivyotokea katika matarajio yenu 2010-2015".

Aidha alibainisha changamoto hizo ni pamoja na miundombinu ya barabara,maji,huduma za afya na umeme usio na uhakika huku Akiainisha kuwa nguvu na uwezo wake kushinda katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi na uchaguzi mkuu zipo mikononi mwa wananchi wa jimbo hilo na ambao wanakiu ya maendeleo na mabadiliko.

" sitegemei kutumia Fedha ili kuwa nunua wapiga kura bali wale wapenda maendeleo na mabadiliko ndiyo mtaji na silaha yangu,rushwa hapana kwani chama chetu hakitaki kabisa kitendo hicho kwa kuwa kinaathiri Maendeleo na kinaua chama cha Mapinduzi kwa Uwepo wa Makundi yanayotaka kupona maisha yao tu si maendeleo.

Aidha alitoa wito kwa Vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha huku wengine wakijiunga na Chama hicho ili kumpigia kura Mgombea ambae anatoka katika kundi la Vijana kwa kuwa Vijana ndio Taifa la leo.

Sambamba na hilo Abdulaziz aliziasa kamati za chama na vikao vya uteuzi kuzingatia matakwa na maamuzi ya wanachama huku akikemea matumizi ya fedha kwa wagombea kuhonga wanachama ili wawapigie Kura. 

"Mpango huu wa kuhonga wanachama una athari kubwa kwa Chama Pia upo uwezekano wa kupata mgombea asiekubalika na kuendelea kutwaliwa na Upinzani ni lazima tuwe makini katika hili,Nina Imani hata Vijana toka vyama vya Upinzani wataniunga mkono na kunichagua kuwawakilisha".Alimalizia Abdulaziz alipokutana na waandishi wa habari wa Vyombo Mbali mbali

RATIBA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA MKOA WA NJOMBE

watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi walivyoadhimisha Siku ya Wanawake duniani

$
0
0
Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali wakishiriki katika matembezi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani ambayo katika mkoa wa Dar es Salaam yamefanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam jana.Kauli mbiu yao kama Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka huu tunapoadhimisha siku ya wanawake duniani ni: Uwajibikaji Katika Rasilimali za Umma: "Tekeleza Wakati ni Sasa". Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii yetu kutambua dhana ya uwajibikaji katika rasilimali za umma ni shirikishi na hivyo ni muhimu kwa kila mtu kutekeleza wajibu wake sasa.

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images