Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

TBA wapewa wiki mbili kukarabati majengo mawili

$
0
0
WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ametoa siku 14, kwa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), kuanza ukarabati wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Siha na Moshi baada ya kubainika majengo hayo kujengwa chini ya kiwango.

Dkt. Magufuli pia ameagiza aliyekuwa meneja wa TBA Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Ndossa kusimamishwa kazi mahali alipo ili arejee kujibu tuhuma na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Waziri huyo alitoa agizo hilo wakati akikagua jengo la mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro baada ya kupewa taarifa za jengo hilo kujengwa chini ya kiwango hali iliyosababisha shughuli za mkuu wa Wilaya ya Siha kuhamishiwa kwenye ofisi za maji za halamashauri hiyo.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji mkuu wa TBA Elius Mwakalinga alisema wakala hao wanasikitishwa na kasoro za kiufundi zilizojitokeza katika jengo hilo na watawachukulia hatua wote waliohusika katika kuchangia majengo hayo kuwa chini ya kiwango.

Mwakalinga amesema tayari TBA imefanya tathmini ya gharama za ukarabati wa jengo la Wilaya ya Siha ambao utafanyika katika kipindi cha wiki 18 na kugharimu shilingi milioni 50.

Majengo ya ofisi za wakuu wa Wilaya za Siha na Moshi yalijengwa kwa usimamizi wa TBA ambapo wahusika walishindwa kuyatumia wakihofia usalama wao baada ya kuona dosari.

EY Tanzania team donated US$ 3,500 and TZS 712,000 to fight brutality against people with albinism in Tanzania

$
0
0
On 2nd March 2015 staff and Partners of EY Tanzania hosted Ms. Maria Stanford a representative from the society of people with albinism in Tanzania at EY offices in Oysterbay.

 The representative, herself a victim of brutality against people with albinism lost both of her arms to wicked people who broke into her house located near Lake Victoria in North-western Tanzania and managed to overcome her as she slept, cut-off and vanished with both her hands. 

Although she later identified the perpetrators who were amongst her fellow villagers, they were never brought to justice. On behalf of the Partners and staff, Joseph Sheffu the Country Managing Partner of EY Tanzania called upon the entire community to work together with the Government organs at all levels of the community in - protecting our sisters and brothers born with albinism, identify and bring the perpetrators to justice and ultimately eradicate this barbaric act against fellow human beings. 
At the event, which was prevailed with sadness and also joyfulness for Maria’s courage, forgiveness and positivity about life, the team raised a total of US$3,500 to support the cause for the people with albinism in Tanzania. The team also raised TZS 712,000 specifically to assist Maria meet her basic needs. In addition, Partners and staff have committed to raise additional funds to enable Ms Maria obtain limited functioning Prosthetic hands and a new embroidery machine to enable her to continue with her embroidery business at the local village. Maria thanked EY community for the support and appealed to the Government of Tanzania to do more in protecting people with albinism in Tanzania.

TTCL yatoa Msaada wa Madawati kwa Shule ya Msingi Bunena,Bukoba

$
0
0
Uongozi wa TTCL ukitoa Msaada wa Madawati katika Shule ya Msingi  Bunena leo Ijumaa.TTCL inaamini kutoa msaada huo wa Madawati utasaidia kuboresha Ufanisi wa Shule na hatimaye kupata Matokeo Makubwa sasa katika Sekta ya Elimu. Pia ni Mategemeo ya TTCL kuwa utaleta chachu kwa wadau wengine katika Sekta kuweza kuchangia katika sekta hiyo pana ya Elimu. Hatimae kuondoa Changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu hapa Mkoani Kagera na Nchi nzima kiujumla. TTCL pia imeweza kuwahakikishia wadau mbalimbali waliohudhuria hafra hiyo kuwa wataendelea kuwa bega kwa bega katika kuleta maendeleo kadri hali ya kifedha itakavyoruhusu.
Wanafunzi wakikalia dawati moja wapo ambapo dawati moja litakaliwa na Wanafunzi 3 hivyo madawati hayo yatawatosha wanafunzi 150 wa Shule hiyo ya Bunena.













MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE KUWA MGENI RASMI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Na Happy Shirima - Habari Maelezo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo [WAMA] anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam .

Akizungumzia maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam , Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar se salaam Mhe. Raymond Mushi amesema kuwa maadhimisho hayo mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Uwezeshaji Wanawake Tekeleza, Wakati ni Sasa “.

Amesema ujumbe huo unaikumbusha jamii kujenga mazingira  wezeshi kwa kutambua mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla .

Ameeleza  kuwa wadau kote nchini wanatakiwa kuelimishwa ili kuangali upya wajibu wao kwa kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa wanawake haki sawa katika nafasi za elimu , uchumi na uongozi ili waweze kuwa chachu ya maendeleo yao binafsi, familia na taifa zima.

“Lengo la maadhimisho haya ni kukumbuka wajibu wa kila mmoja  kushiriki katika mikakati  ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za wanawake kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa” Amesema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho hayo amesema kuwa yanaambatana na maonyesho ya kazi na bidhaa mbalimbali za vikundi vya ujasiriamali na kuzishirikisha Asasi za Kiraia  zinazojishughulisha na masuala ya utoaji wa Elimu ya Uraia na sheria ya utunzaji fedha.

Ameongeza kuwa siku ya kilele  kutakuwa na maandamano yatakayoanzia Barabara ya Lumumba na kuishiaviwanja vya mnazi mmoja ambayo yatapokewa na mgeni rasmi  na wananchi  wa mkoa wa Dare s salaam.

INTRODUCING New Music: Snura Feat Nay wa Mitego - Hawashi

SERIKALI YA JAPAN YAIPATIA MSAADA WA DOLA LAKI 1.4 HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI

$
0
0
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha wakisaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Monduli.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.Wengine pichani ni Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine (katikati),Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli,Edward Sapunyu pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje na Mkuu wa Idara ya Miradi wa Ubalozi wa Japan nchini,Takashi Higuchi.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha wakibadilishana mikataba mara baada ya kuisaini,wakati wa hafla ya fupi iliyofanyika leo nyumbani kwa Balozi huyo,Masaki jijini Dar.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri ya Monduli dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi miwili ya wilaya hiyo.Wengine pichani ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) Mbunge wa Viti Maalum - Monduli,Mh. Namelock Sokoine pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli,Edward Sapunyu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

In Loving Memory

$
0
0
Though your death left an unbearable heartache that no one can heal, we know that your love left us a memory that no one can steal.

You are deeply missed.

Lawrence L. Rutahakana

Wizara ya Mambo ya Nje yajipanga kutekeleza Sera ya Elimu n Mafunzo ya Mwaka 2014

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof.Sifuni Mchome akiwasilisha mada kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika warsha fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa  Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Machi, 2015.

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Idara ya Asia na Austaralasia, Balozi Mbelwa Kairuki (katikati) na Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Sera na Mipango  Bw. Joachim Otaro wakifuatilia kwa makini warsha hiyo

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Prof. Mchome ambaye hayupo pichani wakati akiwasilisha mada kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014.


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,sheria na Utawala yaridhishwa na miradi ya TASAF Mbarali

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala wamefanya ziara katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuona utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) na kukutana na walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini unaotekelezwa na mfuko huo.

Wakizungumza na walengwa hao katika kijiji cha Madabaga wabunge hao wameonyesha kuridhishwa na mafanikio makubwa yaliyoanza kupatikana baada ya walengwa kupata fedha chini ya utaratibu wa uhawilishaji fedha unaotekelezwa na Tasaf.

Wakizungumza katika ziara hiyo baadhi ya walengwa wameeleza namna walivyonufaika na fedha zilizokwishatolewa ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto,kuboresha makazi yao na kuwa na uhakika wa huduma ya afya na lishe.

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika kijijini Madabaga,mwenyekiti wa kamati hiyo Vedastus Rweyikiza amewahimiza wananchi hao kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu ikiwa ni pamoja na kubuni miradi itakayowafanya wawe katika mazingira mazuri hata baada ya mpango huo kumalizika.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Tasaf Ladslaus Mananga,mkurugenzi wa ukaguzi wa mfuko huo,Christopher Sanga alibainisha kuwa jitihada za kuwafikia walengwa wote wa mpango huo zinaendelea ambapo ifikapo katikati ya mwaka huu zaidi ya kaya milioni moja zitanufaika na utaratibu wa uhawilishaji fedha nchini kote.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro(wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabala ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.Kulia ni mkurugenzi wa ukaguzi wa Tasaf Christopher Sanga.
 MKuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhussein Kifu(wa nne kulia) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabla ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na UtawalaVedastus Rweyikiza akizungumza jambo baada ya kamati hiyo kukutana na wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani mkoani Mbeya.
 Wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani mkoani Mbeya wakimsikiliza mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Vedastus Rweyikiza kabla ya kuanza kugawiwa fedha kwenye mkutano uliofanyika kijijini hapo jana.
 Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani Hellena Bamba akikabidhiwa fedha kutoka kwa kamati ya mradi ya wilaya(CMC).
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala wakiangalia namna wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani wanavyokabidhiwa fedha.Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Vedastus Rweyikiza kushoto kwake akifuatiwa na Felix Mkosamali na Willium Ngeleja.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE AENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBO LA KONGWA MKOANI DODOMA.

$
0
0
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Mkoka wakitazama Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ukikatiza kwenye moja ya daraja wakati wakielekea katika kijiji hicho cha Mkoka,Wilayani Kongwa mkoani Dodoma,Ndugu kinana aliweka jiwe la msingi la kitega uchumi cha tawi la CCM pamoja na kufungua Ofisi ya CCM Tawi la Mkoka.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Mamia ya wakazi wa kijiji cha Mkoka wakishangilia jambo wakati
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara Wilayani Kongwa mkoani Dododoma.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkoka,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.



 sehemu ya umati wa watu wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mkoka,Wilayani Kongwa.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa wamefuatana na wananchi walipokuwa wakiwasili katika uwanja wa Mkoka kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara,mbali ya Uongozi huo wa juu wa CCM,pia waliambatana Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Chiku Galawa,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma,Mh.Addam Kimbisa pamoja na viongozi wengine wa wilaya.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani juu ya jengo akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai wakishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Njoge,Kata ya Njoge pamoja na kusalimia Wananchi wa eneo hilo.
Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kushiriki ujenzi wa darasa la shule ya msingi Mlali,katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa,mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni mia sita ulianza kujengwa mnamo mwaka 2013 na kutarajiwa kumalizika mei 2014,lakini kwa bahati mbaya mradi huo haukukamilika kwa wakati kutokana na ukosefu wa fedha.Mbunge wa jimbo hilo la Kongwa,Mh.Ndugai alieleza kuwa mradi huo kwa sasa umekwishakamilika kwa asilimia tisini na kwamba mradi huo wa maji safi na salama utawanufaisha wanakijiji wapatao mia saba na zaidi.

PICHA NA MICHUZI JR-WILAYANI KONGWA.

KITWANGA AHIMIZA UBUNIFU, UZALENDO KWA SEKTA YA MADINI

$
0
0
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini, Sehemu ya Uchumi na Biashara ya Madini, Aloyce Tesha (Kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (Kushoto) kuhusu utendaji kazi katika sekta hiyo. Naibu Waziri Kitwanga aliwatembelea Watumishi wa Idara ya Madini kuzungumza nao na kukagua utendaji kazi wao.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (wa kwanza Kulia), akifafanua jambo kwa Viongozi wa Idara ya Madini alipokutana nao kujadili utendaji kazi katika sekta hiyo. Naibu Waziri Kitwanga aliwatembelea Watumishi wa Idara ya Madini kuzungumza nao na kukagua utendaji kazi wao.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (Katikati) akizungumza na baadhi ya Wafanyakazi wa Idara ya Madini alipowatembelea kujionea utendaji kazi katika Idara hiyo.

MKURUGENZI MKUU MPYA WA TBL AKAGUA MAJENGO WALIYOYAKABIDHI KWA CHUO KIKUU CHA STEPHANO MOSHI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin akiongozwa na mkufunzi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,Gasper Mpehongwa kutembelea vyumba vya madarasa ambavyo vinatumika kwa ajili ya masomo pamoja na mitihanikatika eneo la TBL mjini Moshi.Eneo hilo limetolewa na TBL kwa chuo hicho ikiwa ni kurudisha sehemu ya faida inayopatikana kwa wananchi.

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin akiwa ameambatana na mkuu wa chuo Kikuu Kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,Profesa Anord Temu,wakati akitembelea majengo ya jengo hilo mjini Moshi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrinakizungumza wakati wa mkutano wake na waaandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea kiwanda cha kimea cha Moshi nachuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,

WAZIRI NYALANDU AKUTANA NA WAZIRI MWENZAKE WA UTALII WA KENYA KWENYE MAONESHO YA ITB BERLIN

$
0
0
Na Geofrey Tengeneza – Berlin Ujerumani 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu amekutana na waziri mwenzake wa Biashara na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie katika banda la Kenya na kuwa na mazungumzo yanayohusu ushirikiano wa nchi mbili katika sekta ya Utalii. 
Mazungumzo hayo hayakuwa rasmi hivyo hayakuhudhuriwa na wandishi wa habari Aidha Wiziri Nyalandu alitembelea banda la Tanzania na kuzungumza na washiriki wa maonesho ya ITB kutoka makampuni mbalimbali washiriki hao kwa ambapo amewapongeza kwa kuitangaza vema Tanzania katika maonesho hayo.
Mh. Waziri  Nyalandu akihojiwa katika banda la Tanzania na mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Check inn cha Qatar Bw. Tajamul Hussain kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.

MKurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Zara tours kutoka Moshi Tanzania bibi Zainabu akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalndu alipotembelea banda la Tanzania kujionea namna waoneshaji wa Tanzania wanavyoitangaza Tanzania katika maonesho ya ITB berlin.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie mara baada ya mazungumzo yao.

Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Mh. Phylis Kandie akisakata rhumba na Waziri wa Maliasili na utalii wa Tanzania Mh. Nyalandu katika banda la Tanzania.

USIKU WA MWANAMKE DUNIANI NDANI YA SAFARI CARNIVAL MIKOCHENI JUMAPILI

$
0
0
Gusa Gusa Band, Sabaha Muchacho, Afua Suleiman  na Shakila kutoa burudani
Na Mwandishi Wetu
Asia Idarous Khamsin (Fabak Fashions) inakuletea Usiku wa Mwanamke Duniani (Woman Celebration), utakaofanyika Jumapili ya Machi 8  ndani ya ukumbi wa Safari Carnival uliopo Mikocheni B, Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Fabak Fashins, Asia Idarous Khamsin aliwaomba Wanawake kujitokeza kwa wingi usiku huo maalum kwani ni usiku wao na utakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo burudani ya taarab kutoka kwa bendi ya Gusa Gusa
huki waimbaji nguli wa taarab, Sabaha Muchacho,  Afua Suleiman  na Shakila wakitarajiwa kutoa burudani.
“ Karibuni wanawake wote ndani ya Safari Carniva, Kwa kiingilio cha sh 10,000/=. Ni  usiku wa Jumapili wa Machi 8, Nyoote munakaribishwa” alibainisha Asia Idarous Khamsin.
Asia Idarous Khamsin alisema vazi maalum la usiku huo ni ‘African print’, Ambapo pia kutakuwa na zuria jekundu ‘Red carpet’  kwa ajili ya picha za kumbukumbu litakalopambwa na wabunifu na wanamitindo mbalimbali usiku huo.
Aidha, usiku huo pia  Wanaume wanakaribishwa kujumuika pamoja na kufurahia pamoja.
Kwa upande wa Tikiketi zinapatikana Fabak fashions na Safari Carnival Mikocheni.
WAHI TIKET YAKO MAPEMAAA TUPIGIE 0713263363 or 0784263363.
Wadhamini wa usiku huo wa Mwanamke duniani ni pamoja na Fabak fashions, Mashughuli Blog, Vijimambo blog, Michuzi Media Group, Magic Fm, 8020fashion blog, Mo dewji  blog,Clouds fm, Eventlight na wengine wengi.

Muhimbili University of Health and Allied Sciences gets state-of-the-art pharmacy laboratory from PEPFAR

$
0
0
Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) Professor Eligious Lyamuya (left) observes as USAID Health Office Director Miriam Lutz (right) receives scissors from Ruth Ng'wananogu, Quality Assurance Officer at MUHAS Pharmacy School (center) for a ribbon cutting ceremony to hand over a new state-of-the-art pharmacy laboratory to MUHAS on Thursday, March 5, 2015. 
USAID supported renovation of the laboratory and the provision of new equipment as part of the President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR). 
The kitted and renovated research and development laboratory, valued at approximately $400,000, will ensure that quality drugs reach the people of Tanzania.

MUONEKANO WA MANDHARI MWANANA KABISA YA WILAYA YA KONGWA MKOANI DODOMA

Eneo linauzwa Mkuranga, Dundani, Mkoa wa Pwani

$
0
0
 Eneo lina ukubwa wa ekari 4 liko Mkuranga,  Dundani, Mkoa wa Pwani. Ni karibu kabisa na barabarani. Linafaa kwa matumizi ya kituo cha mafuta au shughuli yoyote ya kibiashara, bei ni nafuu sana. Kwa maelezo zaidi tuwasiliane kwa number hii 0759085069.


PSPF YASAIDIA KITUO CHA KULEA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU, VINGUNGUTI JIJINI DAR

$
0
0
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akipena mikono na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam, Elvis Bwahama, wakati akikabidhi msaada wa mifuko ya saruji tani 3 na mabati, kwa ajili ya ujenzi kwenye kituo cha kulea watoto walio katika mazingira magumu, cha Lukema. Hafla ya kukabidhin msaada huo kwa kituo hichomnkinacholea watoto 70, ilifanyika Ijumaa Machi 6, 2015. Kushoto ni mwenyekiti wa kituo hicho, Fatuma Ramadhani.
Baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho wakisubiri kukabidhiwa msaada huo
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akiteta jambo na mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha kulea watoto walio katika mazingira magumu cha Lukema, kilichoko Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam Ijumaa Machi 6, 2015. Mfuko huo umetoa msaada wa saruji na mabati kwa ajili ya kupanua ujenzi wa kituo hicho kinacholea watoto 70 kwa sasa.

MMILIKI WA KAMPUNI YA URBAN AND RULAR ENGINEERING PAMOJA NA WAJUMBE WAKE WAMTEMBELEA BALOZI LIBERATA MULAMULA

$
0
0
 Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya urban and rular engineering ndugu Awadh Zuberi pamoja na ujumbe wake pichani wamemtembelea Balozi Liberata Mulamula, Kuanzia kushoto ni  ndugu Paula Mwafongo (Afisa Ubalozi uchumi),Bwa. Joseph Mnzanilla ,Mh.Bbalozi Mulamula,Bwa. Awadh Zuberi,Shemuni Halahala pamoja na ndugu Majid Zuberi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Urban and Rular  Engineering wa kwanza kulia ndugu Awadh  Zuberi na msaidizi wake Shemuni Halahala wakiwasili  Tanzania house ,ubalozini Washington, D.C. 

KINANA AWATAKA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NCHIN KUJITOKEZA KUGOMBEA NAFASI ZA JUU ZA CHAMA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania mapema leo asubuhi katika ukumbi wa White House,mjini Dodoma.Ndugu Kinana amewataka wasomi hasa wanafunzi wa vyuo vukuu nchini kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za juu za chama hicho.

Kinana amesema kuwa chama cha mapinduzi CCM kimejipanga kutumia vijana hasa wasomi kwa kuleta changamoto mpya ndani ya chama hicho,ambapo amewatoa hofu ya kushiriki kwenye siasa hata kama hawana fedha na kuwa kujaribu si kushindwa na watakuwa wamejitambulisha kwenye majukwaa ya siasa na kutoa mifano kwa baadhi ya vijana ambao walijaribu na siku ya mwisho waliibuka washindi kwa kuwabwaga baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho na serikalini wakiwemo madiwani.
 Baadhi ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania wakishangilia jambo ndani ya ukumbi wa wa White House kabla ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuzungumza nao mambo mbalimbali.
 Mkutano ukiendelea ndani ya ukumbi wa White House mjini Mdodoma.
Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh Chiku Galawa akiwa pamoja na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Dodoma mjini,Mh.Bi Fatuma Mwenda pamoja na Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma mjini,Mh.Betty Mkwassa wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana nje ya ukumbi wa White House mapema leo asubuhi.Nduugu Kinana anaendelea na ziara yake wilaya ya Dodoma mjini na vitongoji vyake.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma,Mh.Betty Mkwassa.

PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images