Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 761 | 762 | (Page 763) | 764 | 765 | .... | 3348 | newer

  0 0

  JUMLA dola za Kimarekani Milioni 31 (zaidi ya Sh. Bilioni 56 za Tanzania) zimetumika kutengeneza studio mpya za kisasa za Azam TV, zilizopo eneo la Tabata Relini, Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando wamiliki wa Azam TV leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Tabata, Dar es Salaam. 

  Mhando mwenye uzoefu wa kuongoza kampuni kubwa za vyombo vya habari zikiwemo Idhaa ya Kiswahili BBC, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na Mwananchi Communication Limited (MCL), amesema studio hizo zina ubora kuliko nyingine zote nchini.

  “Ni studio ambazo labda unaweza ukazifananisha na studio za kampuni kubwa kama CNN, Aljazeera BBC, na kwa kuwa za kwetu ni mpya, zinaweza kuwa na ubora kuliko hizo,”amesema.

  Tido amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa studio hizo, zoezi la uzinduzi wake rasmi litafanyika kesho, asubuhi mjini Dar es Salaam.

  Mhando ambaye alikuwa mtangazaji maarufu wa mpira wa miguu enzi zake nchini kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

  “Azam TV imeanza kufanya shughuli zake kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini tumekuwa tukiboresha mambo kadha wa kadha kuelekea siku ya kesho, ambayo tunaweza tukasema ndiyo mwanzo rasmi wa Azam TV,”alisema Tido.

  0 0

  Kaimu Mkurugeniz wa Shirika la Bima la Taifa (NIC),Sam Kamanga akuzungumza katika Mkutano na Menejimenti ya Shirika hilo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmont,Golden Jubilee,jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo,Dkt. Edmund Mndolwa.
  Sehemu ya Menejimenti ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakifatilia kwa makini Mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Shirika la Bima la Taifa (NIC),Dkt. Edmund Mndolwa (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika hilo.

  0 0

  Na Chalila Kibuda 

  Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu amewataka watu wajitokeze katika  harakati za kupambana na watu wenye imani  potofu za kuwaua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

  Mdimu amesema uchunguzi umebaini ukosefu wa elimu kwa watu wenye imani hizo ndiyo hupelekea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo silaha ya elimu ni sehemu kubwa ya harakati hapa nchini.

  Hayo ameyasema leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kusema kuwa ana mpango wa kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha  jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

  Aidha,Mdimu ameahidi kutoa elimu hiyo kwa njia ya sanaa kwa kuwatumia baadhi ya wasanii kama Jhikoman,Kassim Mganga,Profesa J,Ray C,Fid Q,Roma Mkatoliki pamoja na Dami Msimamo.

  Pia amevitaka Vyombo vya Habari kutoa ushirikiano katika harakati hizo za  kuhakikisha wanatokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
   Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu (kati) azungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati azungumzia harakati zake za kutaka kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha  jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mwenyekiti wa Imetosha Movment,Masoud Ali "Kipanya" na kushoto ni Monica Joseph mjumbe wa Imetosha.
   Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni Wajumbe wa Imetosha,Joachim Mushi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
  Baadhi ya Wajumbe wa Imetosha wakiwa kwenye picha ya pamoja.

  0 0

  Kufuatia mvua kubwa zilizonyesha usiku wa tarehe 04 Machi, 2015 Wilayani Kahama mafuriko makubwa yalitokea na kuathiri wakazi wa kata ya Mwakata katika vijiji vya Mwakata, Numbi na Mwaguguma.

  Kutokana na mafuriko yaliyotokea tathmini ya awali inaonesha kuwa watu 42 wamepoteza maisha, watu 82 wamejeruhiwa na watu wanaokadiriwa kufikia 574 wameathirika. Jumla ya nyumba 137 zimeathirika kwa viwango mbalimbali.

  Hatua zilizochukuliwa

  Serikali imechukua hatua za haraka kwa kushirikiana na wananchi kuwafikia na kuwanusuru waathirika wa mafuriko hayo waliokuwa wamezingirwa na mafuriko. Aidha vimeanzishwa vituo vya muda kuwahifadhi wananchi hao  kwenye Shule.

  Serikali imepeleka misaada ya kibinadamu kama ifuatavyo;

                       i.        Chakula tani 20. Maharage tani 5, Mafuta ya kupikia lita 1,126 na  Sukari tani 1.3

                      ii.        Vifaa vya matumizi ya ndani ambayo vinajumuisha blanketi 650,  ndoo 82 za lita 20, ndoo 82 za lita 10 ; Vifaa vya kupikia seti 82 na madumu 82 
  Kwa kuwa bado Serikali inalo jukumu kubwa la kuwawezesha waathirika kurejea katika maisha      yao ya kawaida; inapenda kuwatangazia wale wote wanaoguswa na         maafa haya kuwa Serikali inaendelea kupokea misaada mbalimbali ambayo inahitajika kwa waathirika.

  Mahitaji haya ni pamoja na sare za shule; daftari za wanafunzi; mavazi ya kike na kiume; na chakula. Aidha kwa kuzingatia kuwa waathirika hawa wamepoteza mali na fedha katika maafa haya; misaada ya vifaa vya ujenzi (sementi, mabati, mbao, n.k.) inahitajika sana.

  Utaratibu wa kupokea misaada hiyo kwa walio Dar es Salaam wanaweza kuiwasilisha misaada hiyo Idara ya Kuratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu au kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga_ Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


  Serikali itaendelea kuwasaidia Waathirika dhidi ya Changamoto zinazoweza kujitokeza hususani za kiafya zinazosababishwa na uchafuzi wa vyanzo vya maji na mazingira. Elimu juu ya ujenzi wa nyumba bora na makazi maeneo salama itaendelea kutolewa.


  IMETOLEWA NA

  Dkt. Florens Turuka

            KATIBU MKUU

  OFISI YA WAZIRI MKUU


  6 MACHI, 2015.


  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Mzee  Donald Lubunda ambaye  amepoteza watoto wane katika maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha  katika  eneo la Mwakata wilayani Kahama Machi 3 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kuwapa pole waathirka leo
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa pole wanafamilia wa MzeeZakaria  Limbe ambao wamepoteza wototo wane katika mafa ya mvua kubwa yenye upepo na  mawe iliyonyesha katika eneo la Mwakata Machi  3 usiku. Alikwenda katika maeneo yaliyoathirika leo  kuwapa pole wananchi. 
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipa pole Shoma Petro  ambaye ni mmoja wa majeruhi wa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa yenye upepo na mawe iliyonyesha kwenye  eneo la  Mwakata wilayani Kahama Machi 3, 2015 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kwenye hospitali a wilaya ya Kahama kuwapa pole  majeruhi waliolazwa hospitalini hapo
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu, Jenista Mhagama  (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa ShinyangaDr Rufunga kukagua maeneo yalyoathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana  na upepo mkali na mawe katika eneo  Mwakata wilayani Kahama usiku Machi 3, 2015. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Pichani Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Abdulrahman Kinana ukielekea jimbo la Kimbakwe  Wilayani Mpwapwa mapema leo asubuhi kuendelea na ziara yake ya siku 9 mkoani Dodoma ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 pamoja na kusikiliza kero za Wananchi ikiwemo na kuzitafutia ufumbuzi.
  Mwenyekiti wa kikundi cha Mkombozi,Bwa.Athanas Kigosi akitoa maelezo mafupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,kuhusiana na shamba la mfano ambalo limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha Kibakwe,Wilayani Mpwapwa.Bwa.Athanas alieleza changamoto wazipatazo katika maandalizi yao ya kilimo kuwa suala la pembejeo limekuwa tatizo kubwa kwao,kwani zimekuwa zikiletwa kinyume na wakati,hali inayowapelekea ugumu wa kuendelea na kilimo kwa wakati,mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo sambamba na mazao yao kutopandishwa bei,Hivyo Bwana Athanas ameiomba serikali kuwasaidia wakulima kupelekewa pembejeo kwa wakati ili kuhakikisha maandalizi ya kilimo yanakwenda kwa wakati.
  Katibu Mkuu wa  CCM,Ndugu Kinana akifafanua jambo kwa Wanahabari katika shamba la mfano ambalo limepandwa mahindi,lililopo katika kijiji cha Kibakwe,Wilayani Mpwapwa.Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Kibakwe,jimbo la Kibakwe wilaya ya Mpwapwa,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoa wa Dodoma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe wilayani Mpwapwa.
   Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo husika.

  PICHA NA MICHUZI JR-KIBAKWE MPWAPWA


  0 0

  Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya jhabari. Kampeni hiyo inajulikana kwa jina la Imetosha. Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam. Kampeni hiyo inajulikana kwa jina la Imetosha.Mchoraji maarufu na mmoja wa wanakamati wa kampeni za imetosha Masoud Kipanya (kulia) akizungumza na DW. Mchoraji maarufu na mmoja wa wanakamati wa kampeni za imetosha Masoud Kipanya (kulia) akizungumza na DW.Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kulia) akihojiwa na DW mara baada ya mkutano wao. TBN imeunga mkono kampeni hizo zinazoongozwa na balozi wa kujitolea wa mapambano hayo, Henry Mdimu. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akihojiwa na DW mara baada ya mkutano wao. TBN imeunga mkono kampeni hizo zinazoongozwa na balozi wa kujitolea wa mapambano hayo, Henry Mdimu.Baadhi ya wajumbe wa kampeni za imetosha wakipata picha za ukumbusho mara baada ya kuzungumza na wanahabari. Baadhi ya wajumbe wa kampeni za imetosha wakipata picha za ukumbusho mara baada ya kuzungumza na wanahabari.Mkutano na wanahabari ukiendelea. Mkutano na wanahabari ukiendelea wakati Henry Mdimu akifafanua jambo kushoto kwake ni Masoud Kipanya

    Na TBN
    MMOJA wa watu wenye ulemavu wa ngozi  na mwanahabari shupavu kutoka kampuni ya Mwananchi Communication, Henry Mdimu amejitolea kuwa balozi wa hiyari kupinga mauaji ya kikatili ya watu wenye albino yanaoendelea nchini. 
   Bw. Mdimu ambaye ameungwa mkono na baadhi ya marafiki na watu wanaokerwa na vitendo hivyo, ikiwemo Chama cha Bloggers nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kushuhudia ndugu zake wakiteseka kwa muda mrefu dhidi ya mauaji hayo. 
   Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Balozi Mdimu amesema lengo lake kuu ni kuhakikisha anazunguka pamoja na marafiki watakao muunga mkono na kutoa elimu kwa kuanzia Kanda ya Ziwa ili tatizo hilo lisiendelee kuenea nchi nzima. 
   Akifafanua zaidi alisema mauaji ya watu wenye albino yanaichafua Tanzania hivyo atahakikisha anaisaidia Serikali kupambana na watu wenye imani hizo za kipuuzi ili kuondoa doa linaloichafua nchi yetu ambayo imekuwa na sifa ya amani dunia nzima. 
   "...Nimeamua kufanya hivi baada ya kushuhudia ndugu zangu wakiteseka kwa muda mrefu. Awali nilishindwa kuanzisha harakati hizi nikiamini kuna vyombo vinavyohusika na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi.""...Hivyo nimeamua niweke jitihada zangu binafsi niisaidie Serikali yangu katika kuondoa doa hili linaloichafua Nchi yetu yenye sifa ya Amani duninia nzima. Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu mniunge mkono tukishirikiana na Serikali ili mauaji haya yakome," alisema Mdimu. 
   "Kutokana na ushawishi nilionao kama Mwandishi, Mtangazaji wa redio na Blogger naamini nitaleta mabadiliko makubwa katika kuhakikisha haki ya kusihi kwa ndugu zangu inaheshimiwa na kubaki historia. 
  "Salamu zangu ziwafikie wanyanyasaji, wauaji na wenye kufanya dhihaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuwa IMETOSHA." 
   Akifafanua zaidi alisema kwa uchunguzi wake wa awali umebaini ukosefu wa elimu juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi ndio chanzo cha tatizo hilo kukua na hatimaye kuuana kwa imani za kishirikina. 
  "...Hivyo basi, silaha ya Elimu ni sehemu kubwa ya haraki hizi," alisisitiza Balozi huyo wa kujitolea. Aidha alisema kuendesha harakati hizo alizozipa jina la 'IMETOSHA' elimu itatolewa kwa njia ya sanaa, na washauri nasaha pamoja na kundi la wanamuziki ambao pia wataandaa nyimbo mbalimbali za kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili huu. Alisema wasanii ambao hadi sasa wamejitokeza kuunga mkono kampeni hizo ni paoma na Jhikoman, Kassim Mganga, Profesa J, Ray C, Fid Q, Roma Mkatoliki na Dami Msimamo. Hata hivyo alisema bado pia anaamini nguvu ya vyombo vya habari ikiungana na kampeni hizo wanaweza kufanikiwa zaidi hivyo kuomba ushirikiano katika kuhakikisha vinapaza sauti kutokomeza mauaji hayo ya kikatili. 
  *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo. Walioketi kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo wakati akiongea na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi Wa Chama Cha Albino Tanzania baad ya kukutana nao pamoja na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabirika Mushi na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw. Emmanuel Achayo Ikulu jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

  0 0

  Mkutano wa 46 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja ya Mataifa umeingia katika siku ya pili ambapo wajumbe wa Kamisheni hiyo wanajadiliana na kupitisha maazimio mbalimbali yanayohusiana na masula ya kitakwimu katika maeneo mbalimbali.

  Mkutano huu ambao ni wa siku nne unafanyika katika kipindi ambacho Jumuiya ya Kimataifa inaendelea na jukumu kubwa la kuaanda na kukamilisha rasimu ya malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs) mchakato ambao umekwisha ainisha jumla ya malengo 17 yamekwisha ainishwa.

  Pamoja na wajumbe wa Kamisheni hiyo ambayo inaundwa na nchi 24, ikiwamo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni kati ya nchi tano za Afrika zikiliwakilisha Bara la Afrika, kujadiliana masuala mtambuka yahusuyo Takwimu pia wanajaliana na kubadilishana mawazo kuhusu umuhimu wa nafasi ya Taasisi za Takwimu katika kuandaaa viashiria ( Indicators)vya malengo hayo 17.
  Taswira ya washiriki wa Mkutano wa 46 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo wa siku nne, unaongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Dr. Albina Chuwa ( mwenye suti ya damu ya mzee).

  0 0

  Na Tinah Reuben, Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Dar es salaam (JWT), Philimon Chonde amesema suala la kupandishwa kwa kodi kwa asilimia mia moja limepitishwa kinyemela bila ya wao kuwashirikisha wala kujadiliana na wafanyabiashara hao.
  Akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Lamada Hotel jijini Dar es Salaam ukiwashirikisha wabunge, ameeleza kuwa mfumo wa kodi uliopo umekaa kikoloni kwani unawakandamiza wafanyabiashara ili waendelee kuwa tawala kwani haungalii uwiano uliopo baina ya wafanyabiashara wakubwa na wafanyabishara wadogo.
  Chonde amesema kutokana na kuwepo kwa usumbufu wa kudai leseni ameitaka Serikali kuweka suala la kodi katika mfumo unaoeleweka ili kumsaidia mfanyabiashara kujua ni kiasi gani anatakiwa kulipa kwa mwezi.
  Naye Mbunge wa Temeke Abasi Mtevu amezitaja changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao ni suala la usafi wanalipia lakini mazingira bado ni machafu na wamesema wapo tayari kufanya usafi wenyewe na suala la zima moto kwamba kila mfanyabiashara aweze kuwa na mtungi wa gesi lakini hawapewi mitungi hiyo bali hupewa karatasi ya malipo.
  Pia amesema sheria zinazopitishwa Bungeni baadhi ni kweli na nyingine zimetengenezwa na watu wenye maslahi binafsi na amewasisitiza wafanyabiashara kupambana katika kulinda biashara pamoja na mitaji yao.
   Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Dar es Salaam (JWT), Philimon Chonde akizungumza katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
    Mbunge wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu akisisistiza jambo katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
   Mbunge wa Ubungo, Mhe. John Mnyika akifanya majumuisho katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Titus Kamani (Mb) alipotembelea Bandari ya Uvuvi ya Boulogne (Port de Boulogne Sur Mer) ambayo ni ya tatu kwa ukubwa Barani Ulaya. Bandari ina eneo la Ha.150 ambalo lina huduma zote muhimu kwa sekta ya uvuvi ikiwa ni pamoja na mnada wa samaki, viwanda vya kuchakata samaki, maabara ya kuhakiki ubora wa mazao ya samaki, Taasisi ya utafiti na mafunzo kwa wavuvi na wasindikaji wa samaki.
  Mhe. Dkt. Kamani akiwa katika mnada wa samaki na kupatiwa maelezo ya jinsi mnada wa samaki unavyoendeshwa.
  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Titus Kamani akipata maelezo ya shughuli zinazofanywa na Taasisi inayotoa mafunzo kwa wavuvi na wasindikaji wa samaki alipotembelea Taasisi hiyo ambayo ipo katika eneo la Bandari ya Uvuvi.

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Kumekuwa  na  shida  sana  hasa  kwa  upande  wa  wanaume  kuwatelekeza  watoto. Mara  nyingi  wanaume  ndio   hutelekeza  watoto  kuliko  wanawake. Zipo  baadhi  ya  kesi  zimeripotiwa  zikihusisha  wanawake  kuwatelekeza  watoto   lakini hizi  si  nyingi  kama  ilivyo  kwa  wanaume. Hii  ni kwasababu  uwezekano  wa  mwanaume  kumkimbia  mtoto  ni  mwepesi  kuliko mwanamke  kumkimbia  mtoto/watoto.  Jambo  hili  ni  baya  na  limeshakemewa  na  sheria  mbalimbali.  Nataka   niwaeleza  kuwa  kumtelekeza mtoto   ni  kosa  la  jinai. 

  Nikisema ni  kosa  la  jinai   maana  yake  ni kuwa  kulifanya  kwake  kunahitaji   adhabu  ya  kifungo  jela au adhabu  nyinginezo. Wapo watu  hasa  wanawake  ambao  wamekuwa  wakitupiwa  watoto  na  wanaume  kwa makusudi.  Ni  ushauri  wangu  kwamba  muda  ni huu  sasa kama  ulikuwa  hujui  kuanzia  leo  ujue  na  uchukue  hatua. 

  1.NINI  MAANA  YA  KUTELEKEZA  WATOTO/MTOTO  KISHERIA.

  Kutelekeza mtoto/watoto   ni  pamoja  na  kutotoa  matumizi  kama  chakula, mavazi , matibabu, makazi,  na  mahitaji  ya  msingi( necessity) kama  ada  za shule, vifaa  vya  shule  na  kila  kitu  ambacho  ni mahitaji  ya  msingi  kwa  makuzi  na ustawi  wa  mtoto.  Kwa hiyo  mzazi  asiyejihusisha  kwa  namna  yoyote  na  huduma  hizi  nilizotaja kwa  mujibu  wa sheria  huyu  ndiye  aliyetelekeza  mtoto/watoto.

  2.KUTELEKEZA  WATOTO/MTOTO  NI  KOSA  LA  JINAI.

  Sura  ya  16  Sheria  ya Kanuni  ya  Adhabu  kifungu cha  166  kinasema  kuwa  Mtu yeyote ambaye, ni  mzazi  au  mlezi  au mtu  mwingine  mwenye  uangalizi    halali  wa mtoto  yeyote  mwenye  umri  usiozidi  miaka   kumi na nne, hali  ana  uwezo, wakumuhudumia  mtoto, kwa  kuamua  au kinyume  cha sheria, au  bila ya sababu za msingi akakataa  kumhudumia, na akamtelekeza  mtoto  bila  msaada, atakuwa  ametenda kosa. Kwahiyo  kumbe  kutokana  na  sheria  hiyo  kumtelekeza  mtoto   ni  kosa  la  jinai  kama  zilivyo  jinai  nyingine  kama  kuiba, kuua , kubaka n.k.
  Aidha  ni muhimu  walioarhirika  na  matendo  ya  kutupiwa  watoto  wachukue  hatua  za  kufungua  kesi  za  jinai  ili  wahusika  wawajibishwe.  


  0 0

  Kamera ya Globu ya Jamii imewanasa abiria hawa wakipanda daladala kupitia Mlango wa Dereva kutokana na hali ya gombalia goli iliyikuwepo kwenye mlango wa kawaida wa abiria.

  0 0

  Ndege ya shirika la Delta, AlhamisI March 5, 2015 imepata ajali ya kuteleza kwenye theluji ilipokua ikitua kwenye uwanja wa ndege wa LaGuardia wa New York, ndege hiyo iliyokua ikitokea Atlanta iliacha njia na kugonga uzio wa senyenge ya waya kama inavyoonekana kwenye picha na msemaji wa zima moto ameripoti hakuna mtu aliyekufa kwenye ajali hiyo isipokua baadhi ya ya abiria wamepata majeraha ya kawaida na walikimbizwa hospitali kwa matibabu na kwa sasa uwanja huo umefungwa kwa ndege kuruka au kutua mpaka saa 1 usiku kwa saa za Amerika ya mashariki.
  Abiria wakisalimisha maisha yao baada ya ndege ya shirika la ndege la Delta kupata ajali ilipoteleza kutoka kwenye njia yake kutokana na theluji inayoendelea kuanguka mapema leo.
  Abiria wakitoka kwenye ndege kuokoa maisha yao.Chanzo:Vijimambo Blog

  0 0

   
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye sambamba na viongozi mbalimbali wa chama mkoani Dodoma jana wamemaliza ziara ya Kikazi katika jimbo la Mpwapwa na Kibakwe mkoani Dodoma,ambapo leo wanaanza ziara katika jimbo la Kongwa.Kinana anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.

  0 0
 • 03/06/15--03:13: Viwanja vinauzwa


 • 0 0

  DSC_0001
  Mshehereshaji wa kongamano la siku moja lililofanyika jijini Dar kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Mtaalamu wa masuala ya fedha wa UNCDF, Bw. Imanuel Muro akisherehesha kongamano hilo. Katikati ni mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akifuatiwa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika.(Picha zote na Zainul Mzige)

  Na Mwandishi Wetu
  ZAIDI ya watu 10,000 wanaozunguka bwawa la Kalemawe wilayani Same mkoani Kilimanjaro watanufaika na ukarabati wa bwawa hilo na kuwekewa muundo mpya wa kiutawala na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Ukuzaji wa Mitaji (UNCDF).

  Bwawa hilo ambalo lipo katika kata za Kalemawe na Ndungu lilijengwa na watawala wa Kiingereza mwaka 1952-1959 kwa ajili ya kusaidia shughuli za kilimo na ufugaji baada ya kuanzishwa kwa hifadhi ya Mkomazi na hivyo wakazi kuzuiwa kwenda katika hifadhi hiyo kwa shughuli mbalimbali.

  Taarifa ya kuwepo kwa mradi huo mkubwa, imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) nchini, Bw. Peter Malika wakati akiwakaribisha madiwani wa kata hizo ambao wameitwa katika kongamano la siku moja Dar es salaam kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa hilo.
  DSC_0038
  Pichani juu na chini ni Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi kufungua rasmi kongamano hilo.


  0 0

  Muimbaji wa Nyimbo za Injili Rehema Chawe

  MSANII wa nyimbo za Injili, nyanda za juu kusini Rehema Chawe ambaye ni Mwanachama wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA), anatarajia kuzindua albamu yake ya kwanza, inayoitwa Kusamehe ni afya.


  Uzinduzi huo unatarajia kufanyika Jumapili, March 8, mwaka katika kanisa la EAGT, Frelimo kwa mchungaji Mwenda, ambaye ni Mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste mkoani Iringa.


  Akizungumza na wanahabari, Chawe alisema uzinduzi huo utapambwa na waimbaji wengi toka nje na ndani ya mkoa wa Iringa.


  Alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa, ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Iringa, Enock Ugulumo.


  Mwenyekiti wa CHAMUITA mikoa ya nyanda za juu kusini, Tumaini Msowoya Kibiki aliwataka wanachama wote kuwepo kwenye uzinduzi huo ili kumsindikiza mwenzao.


  “Ni jukumu la waimbaji wote hususani wanachamuita kuhakikisha wanakuwepo siku ya uzinduzi ili kumuunga mkono mwanachama wenzetu,”alisema Kibiki.

  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Bunge Hesabu za serikali za Mitaa(LAAC) Azza Hamad akizungumza wakati wa kikao na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakati kamati hiyo ilipotembelea halmashauri kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Michael Hadu akijibu hoja mbele ya kamati hiyo.
  Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali za mitaa (LAAC) wakiwa katika eneo ilipojengwa shule ya sekondari Singland kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba ya mwalimu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeeleza kuguswa na tukio la mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambayo imesababisha vifo vya watu 42 na wengine mamia kujeruhiwa na kuacha familia nyingi zikiwa hazina makazi na kuanzia leo imeanza kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tukio hilo.

  Akiongea na waandishi wa habari leo,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema anawaomba watanzania wote wanaotaka kuchangia wahanga hao kutuma fedha zao kwenye namba maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya 155990.

  “Tukiwa kama kampuni ya mawasiliano tumeguswa na tukio hili na tunawapa pole waathirika wote na tunaungana na wakazi wa kahama kwa janga hili tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kupitia kitengo chetu cha kusaidia jamii cha Vodacom Foundation na tunawaomba watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao na tutahakikisha tunaifikisha sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu ambao wako katika mazingira magumu na wanahitaji msaada wa haraka”.

  Alisema kupitia njia hii ya namba maalumu ya”Red Alert” 155990 ya kuchangisha fedha imewahi kurahishisha uchangishaji wa fedha kwa waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na kuathiri wananchi moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto jijini Dar es Salaam na aliwahimiza wananchi kuitumia kama njia rahisi ya uchangiaji.

  Jinsi ya kuchangia ni rahisi sana unachotakiwa kufanya unaponyeza *150*00# alafu unachagua namba 4 yaani Lipa kwa M PESA baada ya hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba 155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.
  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akionesha namba ya Red Alert ambayo watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao kwenye hiyo namba.Jinsi ya kutuma ponyeza *150*00# alafu unachagua namba 4 yaani Lipa kwa M PESA baada ya hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba 155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.

older | 1 | .... | 761 | 762 | (Page 763) | 764 | 765 | .... | 3348 | newer