Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

mwili wa hayati kepteni John Damiano Komba wawasili Songea

0
0
Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM marehemu John Damiano Kumba ukipokelewa katika uwanja wa ndege wa Songe na umati mkubwa wa waombolezaji wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mhe.Mwambungu,Mhe.John Nchimbi,Mbunge wa Songea Mjini,na Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais(Kazi Maalum)Mark Mwandosya,kulia. Marehemu anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Kesho.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiongoza maelfu ya wakazi wa Songea kwa kutoa salaam za rambirambi za Mkoa.Wa pili kulia ni Mama Shumbusi,Katibu wa CCM Mkoa,wa tatuu kulia ni Waziri Mwandosya,w nne kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma

Benki ya Exim yakarabati kituo cha watoto wenye ulemavu Morogoro

0
0
Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Morogoro, Bi Anna Wesiwasi (wapili kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Kituo cha Amani cha watoto wenye ulemavu, Padri Beatus Sewando (watatu kulia) mara tu baada ya kuzindua jengo la kituo hicho kilichokarabatiwa na benki hiyo jana mkoani Morogoro. Akishuhudia ni Afisa Mauzo wa Benki hiyo Vick Haji (Kulia).

Na Mwandishi wetu, Morogoro

BENKI ya Exim Tanzania imefanya ukarabati wa majengo ya kituo cha watoto wenye ulemavu cha Amani kilichopo eneo la Chamwino mkoani Morogoro ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuboresha maisha ya jamii.

Kupitia sera yake ya kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii, benki hiyo pia imejipanga kutoa misaada zaidi ikilenga mipango yenye kuleta maendeleo kwa jamii hapa nchini hususani katika maeneo ambayo benki hiyo tayari imefungua matawi yake.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya ukarabati wa majengo ya kituo hicho iliyofanyika mkoani humo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa tawi la benki hiyo mkoani Morogoro, Bi Anna Wesiwasi alisema msaada huo pia unalenga uboreshaji wa maisha ya watoto wanaoishi kwenye kituo hicho kwa kuwa wataishi kwenye makazi salama, safi na bora kwa afya zao.

“Benki ya Exim siku zote tunaamini kuwa watoto wenye ulemavu wanahitaji kupewa matumaini zaidi na kwa kushiriki kwetu kwenye mipango ya maendeleo kama huu ndio tunatekeleza hiyo imani yetu kwa vitendo na zaidi tunazidi kuwa karibu na jamii inayotuzunguka jambo ambalo ni muhimu katika ulimwengu wa kibiashara kwa sasa kuona kwamba benki inarudisha sehemu ya faida yake kwa watu inao wahudumia,'' alisema Bi Wesiwasi

Kwa mujibu wa Bi Wesiwasi, benki hiyo inaamini kuwa watoto ndio wateja wao wa kesho kama sio wa sasa na hivyo basi benki hiyo itajitoa kwa hali na mali kuhakikisha kwamba wanapata maisha bora kwa sasa .

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo,  Mkurugenzi wa kituo hicho, Padri Beatus Sewando alisema uamuzi wa benki hiyo kusaidia kituo cha watoto wenye ulemavu ni kitendo kinachotakiwa kuigwa na taasisisi, mashirika na watu mbalimbali hapa nchini.

“Tunashukuru sana kuona wenzetu wa benki ya Exim wameonyesha mfano kwa kuitikia kilio chetu.Msaada huu utawahakikishia  watoto wetu hapa kituoni kuwa na makazi bora na salama kwaa afya zao…naomba wengione waige mfano huu,’’ alitoa wito

MAKALA YA SHERIA: USIFANYE MAKOSA, HUU NDIO UTARATIBU WA KUNUNUA NYUMBA ILIYOWEKWA REHANI/DHAMANA BENKI

0
0
Na   Bashir  Yakub

Nimewahi kuandika  mara  kwa  mara  kuhusu  utaratibu  mzuri  wa  kumwezesha  mtu kununua nyumba  huku  akiwa ameepuka  mgogoro. Nilitahadharisha  sana  kuhusu  migogoro  ya  ardhi  ambayo  sasa  imekuwa  janga  la  kitaifa  hapa  kwetu. Nakumbuka  moja  kati  ya  mambo  niliyoeleza   ni  kuwa utaratibu  wa  manunuzi  ya  nyumba/viwanja unatofautiana.Nikasema kwamba  tofauti  zake  zinatokana  na  ukweli  kuwa   kila  nyumba  ina mazingira  yake. Hata  hivyo sikusema  utofauti  wa  mazingira  hayo ila  sasa  naweza  kueleza  kwa ufupi  utofauti  wa  mazingira  ya  kila  nyumba  unapokuwa  katika  taratibu  za ununuzi. 

1.UTOFAUTI  WA KITAALAM  KATIKA  UNUNUZI  NYUMBA.

Usikurupuke   unapohitaji  kununua ardhi.  Unapaswa  kujua  kuwa   nyumba  na  viwanja  zina  taratibu  tofauti unapohitaji  kununua. Ukikurupuka utalipia  gharama  ya kukurupuka  kwako. Kutokana  na  hilo ni muhimu tujue  kuwa kuna  nyumba  inayouzwa  kwa  utaratibu  wa kawaida  wa mmiliki  mwenyewe    kumuuzia  mnunuzi. Hii  mara  nyingi  huwa  haina  shida sana kwakuwa  unahitaji  tu  kujiridhisha  na baadhi  ya  mambo  ya  msingi   kama  kufanya  upekuzi  rasmi  ( official  search) katika  mamlaka  za ardhi n.k.  

Pili kuna  nyumba  inayouzwa  na  wasimamizi  wa  mirathi. Hii  uuzwaji  wake  hauko  sawa  na   ile  inayouzwa  na  mmiliki halisi.  Hawa  ni wasimamizi  wa  mirathi  hivyo  hata  uuzaji  wao  si  uuzaji  kama  wa mmliki  halisi. Utofauti  wao  upo  katika  namna  ya  kuandika  mkataba( sale agreement) na  nyaraka  ambazo  wanapaswa  kukuonesha  wewe  mnunuzi .  Pia  kuna  ununuzi  wa  nyumba  ya  mkopo  ambao  sasa  ndio  mada  ya leo. Ununuzi wa  nyumba  ya  mkopo  nao  si  ununuzi  kama  wa nyumba  ya  kawaida. Haufanani  na  nyumba  ya  kawaida  na haufanani  na wa  nyumba  ya  mirathi. Unazo  tarati  bu zake  tofauti  kabisa  na ununuzi  mwingine.

2.UMUHIMU WA  KUZINGATIA  UTARATIBU  UNAPONUNUA  NYUMBA YA DHAMANA.

Tatizo kubwa  linakuja  kuwa  unaponunua  bila  kuzingatia  utaratibu  pia  uwe  tayari  kupoteza.  Ieleweke  kuwa nyumba  au  ardhi   yoyote ni kitu  ambacho  hudumu  milele. Hivyo  kama  utakosea  utaratibu  hata   kwa  kiwango  kidogo basi  ya kutosha  kuishi  bila  amani  maisha  yako  yote. Kama  si  wewe  watakuwa  watoto  wako  na  kama  si  watoto  wako  watakuwa  wajukuu  wako.  Kati  ya  hawa   kuna mmoja   mgogoro  utamkuta kwa  makosa  uliyoyafanya  wewe. Na ubaya  wa  mgogoro  unapotokea  mahakama  kikubwa  inachokifanya  ni  kuangalia  nani  alikosea  taratibu.  Inaangalia  hilo  kwasababu  yenyewe  inakuwa  haipo   wakati  mnauziana  na hivyo  nyote  haiwajui  na  haijui  kati  yenu  nani  mkweli  na  nani  muongo.

 Kwahiyo kama ni wewe  mnunuzi  uliyekosea taratibu  wakati  wa kununua  basi   hakuna  kingine  ila  kupoteza  bila   kujali  gharama   ulizotumia  katika  manunuzi. Lakini  ikiwa  ulifuata  taratibu   kwa  umakini  kwanza  ni  vigumu kuingia  katika  mgogoro  lakini   hata  bahati  mbaya uingie katika mgogoro  basi  ushindi  utakuwa  ni  wa  kwako. Huu  ndio umuhimu  wa  kuhakikisha  unafuata  taratibu.  Zingatia  maeneo  mawili  kwanza  uandaaji  wa  mkataba  na  pili ukaguzi  na uhakiki  wa  nyaraka. 

DKT. TITUS KAMANI ATEMBELEA MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO NCHINI UFARANSA

0
0
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Mhe. Dkt. Titus Kamani akitembelea mabanda ya maonesho ya kimataifa ya kilimo yanayofanyika katika Jiji la Paris nchini Ufaransa,na kujionea aina ya mifugo inayoshindanishwa. Hapa anaangalia ng'ombe wa nyama aina ya Charolaise.
Mhe. Dkt. Kamani akiangalia kondoo wa sufi waliopo kwenye mabanda ya maonesho.
Umati wa watu kutoka mataifa mbalimbali duniani waliohudhuria maonesho hayo. Takriban watu milioni moja wametembelea maonesho hayo kwa mwaka huu 2015 ambayo hufanyika kwa muda wa siku tisa.
Mhe. Dkt. Kamani pamoja na ujumbe wa watanzania wakisikiliza kwa makini maelezo ya maendeleo ya sekta ya mifugo nchini Ufaransa na mfumo wa uendeshaji wa maonesho ya kimataifa ya kilimo kabla ya kupata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali.

USIKOSE KUFATILIA MICHEZO YA LIGI KUU YA UINGEREZA KUPIA SUPERSPORT NDANI YA DSTV

RAIS KIKWETE AAGANA NA BALOZI WA JAPAN

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa Japan Mhe.Masaki Okada ikulu jijini Dar es Salaam wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini.(picha na Freddy Maro)

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI MKOANI RUVUMA KUSHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU KAPTENI KOMBA

0
0


Msanii wa TOT Khadija Omary Kopa akiwasili uwanjani hapo.

MESSAGE ON WORLD WILDLIFE DAY

0
0
The United Nations General Assembly has proclaimed 3 March – the anniversary of the adoption of the Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Fauna and Flora (CITES) – as World Wildlife Day.  On this second observance of the Day, the UN system, its Member States and a wide range of partners from around the world are highlighting the simple yet firm message that “It’s time to get serious about wildlife crime”.

Illegal trade in wildlife has become a sophisticated transnational form of crime, comparable to other pernicious examples, such as trafficking of drugs, humans, counterfeit items and oil.  It is driven by rising demand, and is often facilitated by corruption and weak governance.  There is strong evidence of the increased involvement of organized crime networks and non-State armed groups. 

Illegal wildlife trade undermines the rule of law and threatens national security; it degrades ecosystems and is a major obstacle to the efforts of rural communities and indigenous peoples striving to sustainably manage their natural resources.  Combatting this crime is not only essential for conservation efforts and sustainable development, it will contribute to achieving peace and security in troubled regions where conflicts are fuelled by these illegal activities. 

Getting serious about wildlife crime means enrolling the support of all sections of society involved in the production and consumption of wildlife products, which are widely used as medicines, food, building materials, furniture, cosmetics, clothing and accessories.  Law enforcement efforts must be supported by the wider community.  Businesses and the general public in all countries can play a major role by, for example, refusing to buy or auction illegal ivory and rhinoceros horn, and insisting that products from the world’s oceans and tropical forests have been legally obtained and sustainably sourced.  

On this World Wildlife Day, I urge all consumers, suppliers and governments to treat crimes against wildlife as a threat to our sustainable future.  It’s time to get serious about wildlife crime. 

MAONYESHO YA SIKU YA WANAWAKE YA MKOA WA MOROGORO YAINGIA DOSARI BAADA YA MVUA KUBWA KUNYESHA

0
0
  Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Bi. Theresia Muhongo akisikiliza maelezo kutoka kwa Haji Sajilo ambaye ni Kiongozi msimamizi wa Mipango wa NGO,s ya MOYODEI wakati alipotembelea kwenye mabanda yaliyoharibwa vibaya na mvua iliyonyesha jana jioni. Haya mabanda yalikuwa ni kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyotakiwa kuanza leo jumanne lakini kutokana na maafa hayo maonyesho hayo yamesogezwa mpaka tarehe 5/03/2014 kwa ajili ya ukarabati wa mabanda hayo.(Picha na Pamoja Blog)
 Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Bi. Theresia Muhongo akipata maelezo kutoka kwa mama kuhusu mabanda yaliyoezuliwa na mvua iliyokuwa na upepo mkali
 
 
Baadhi ya Mabanda yakiwa yameharibika vibaya 

Hayati John Komba enzi za uhai wake akihojiwa na Salama Jabir katika kipindi cha mkasi pale pale amaya beauty spa jijini Dar es salaam

HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE YA MWISHO WA MWEZI WA FEBRUARI,2015

WATU WANNE MBARONI AKIWEMO M/KITI WA KIJIJI CHA IHANDA WILAYANI KONGWA DODOMA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YAKIHUSISHA IMANI ZA KISHIRIKINA

0
0
Na. Sylvester Onesmo/Dorice Kigombe wa Jeshi la Polisi Dodoma.


Watu watatu wameuawa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti yanayohusisha imani za kishirikina.

Akizungumzia matukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema tukio la kwanza limetokea tarehe 01/03/2015 majira ya saa 01:00hrs katika kitongoji cha Golani, kijiji cha Masinyeti, kata ya Iduo, tarafa ya Mlali Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la SAIDIA S/O CHAKUTWANGA mwenye miaka 80, kabila Mkaguru, Mkulima Mganga wa kienyeji aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kutobolewa macho.

Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina wakimtuhumu marehemu kuwa anazuia mvua kunyesha katika eneo hilo.

Pia Kamanda MISIME amesema katika tukio lingine limetokea tarehe 01/03/2015 majira ya saa 02:00hrs katika kitongoji cha Majengo, kijiji cha Ihanda, Kata na Tarafa ya Mlali Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la PETER S/O KALULI mwenye miaka 85, kabila Mkaguru akiwa na mkewe aitwaye KAILA W/O KALULI mwenye miaka 80, Mkaguru wote wakulima na wakazi wa Kitongoji cha Majengo wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao ya tembe, waliuawa na watu wasiofahamika kwa kuangushiwa ukuta wa nyumba yao kisha kuchoma moto na kubomoa nyumba mbili za tembe.

Watu hao walifanya uharibifu mwingine kwa kuwaua nguruwe mmoja na ng’ombe mmoja kumkata miguu.

Aidha Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji na uharibifu huo ni imani za kishirikina wakiwatuhumu marehemu kuwa wanazuia mvua kunyesha. Watuhumiwa wanne akiwemo M/Kiti wa Kijiji cha Ihanda na wazee wawili wa kimila wa kijiji wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hili kwani taarifa zinaonyesha waliandaa vikao vya kutekeleza mauaji haya. Upelelezi wa matukio yote mawili unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika na matukio haya.

Kamanda MISIME ametoa wito kwa wananchi kutochukua sheria mkononi  na kujiepusha na imani za  kishirikina zinazopelekea kuleta hofu na mashaka kwa jamii. Alisema ni jambo la aibu kwa jamii hadi karne hii watu kuamini kuwa kuna watu wanaoweza kuzuia mvua isinyeshe. Pia amewataka viongozi wa maeneo mbalimbali kutoa taarifa mapema polisi pale wanapoona mipango ya kihalifu kama hiyo ikipangwa.

WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU JIJINI ARUSHA KUJENGEWA HOSTEL

0
0
Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Arusha wanatarajiwa kujengewa Hostel zitakazowasaidia kuondokana na adha ya kupata sehemu za malazi hivyo kulazimika kulala maeneo ya stendi za mabasi na masoko.

Mkurugenzi wa shirika la Gola linalojihusisha na masuala ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Arusha,Sawale Maghema  amesema kuwa mpango huo utasaidia watoto hao kuondokana na mazingira magumu yanayowapelekea kujiingiza katika vitendo vya uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya.

Sawale alisema kuwa iwapo watoto hao watatelekezwa na jamii bila kusaidiwa wanaweza kugeuka na kuwa mwiba kwa jamii ya Watanzania hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuwasaidia watoto hao .

"Watoto hawa tuna mpango maalumu wa kuwakusanya na kuwakutanisha pamoja kujua mahitaji yao ,malengo na matarajio waliyonayo ili kuwasaidia kwa kushirikiana na jamii hata kwa hili la ujenzi wa Hostel litasaidia kuwaweka pamoja tukiwaacha waendelee kukaa mitaani hawatabadilika wataendelea kuwa na maisha mabaya" Alisema Sawale

Mdau wa Masuala ya utalii Mustafa  Panju  alijitolea kuwasaidia watoto hao kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 20 ili waweze kupata mahitaji muhimu  ,Ameeleza kuwa jamii inapaswa kuamka na kuwasaidia watoto hao badala ya kuwaacha waendelee kukaa kwenye mazingira hatarishi.

Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Arusha ,Hassan Omari akizungumza kwa niaba ya watoto wa mitaani anaeleza kuwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wana ndoto nyingi,vipaji na uwezo wa hali ya juu hivyo wakisaidia wanaweza kufika mbali na kulisaidia taifa .
 Kikundi cha ngoma cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakitumbuiza katika shughuli ya kuwakusanya watoto wa mitaani iliyofanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto hao kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao
Baadhi ya Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Arusha waliokusanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto hao kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao

Chanzo:libeneke la kaskazini blog

MKUU MPYA WA WILAYA YA NGORONGORO AAPISHWA

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Hashimu Shaibu akila kiapo cha utumishi mbele ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda  jana katika hafla iliyofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huyo
chanzo libeneke la kaskazini blog

Halmashauri ya mji wa Kahama yapokea ushuru wa asilimia 0.3 kutoka mgodi wa Buzwagi

0
0
Kampuni ya ACACIA kupitia mgodi wake wa Buzwagi uliopo kwenye halmashauri ya mji wa Kahama,imeipatia ushuru wa asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi halmashauri hiyo,ikiwa ni ushuru kwa kipindi cha miezi sita (Julai - Disemba,2014) ambayo ni zaidi ya shilingi za kitanzania millioni 800,uliokabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Kaimu Meneja Mkuu wa mgodi wa Buzwagi  ulio chini ya Kampuni ya ACACIA,Ing. Mutereko Muganda (wa pili kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania millioni 800 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Bw. Felix Kimaryo (kulia) nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya (wenye tai).



TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services yazindua tawi lake jipya wilayani Kwimba jijini Mwanza

0
0
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo imepongezwa na serikali kwa hatua yake ya kufungua tawi wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Meneja Mauzo wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, akimuelekeza jambo Katibu Tawala wa Wilaya Kwimba, Vicent Emmanuel, katika uzinduzi wa tawi jipya wilayani humo, uliofanyika Machi 2 mwaka huu. Wengine ni maofisa wa taasisi hiyo, Ramadhan Hanafi na Monica Mwangoka. Picha na Mpigapicha Wetu.

Shughuli za uzinduzi huo zilifanyika Machi 2 mwaka huu, huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, akiongozana na viongozi mbalimbali wa serikali wilayani humo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, kushoto akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi tawi jipya la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Kulia ni Meneja Mauzo wa taasisi hiyo Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Picha na Mpigapicha Wetu.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Tawala huyo wa wilaya Kwimba, Emmanuel alisema kwamba kufunguliwa kwa tawi hilo kutatoa huduma karibu na wananchi, kama njia ya kukuza uchumi wao kwa ujumla, zikiwapo fursa za kukopeshwa bidhaa mbalimbali, vikiwamo vyombo vya usafiri.

Alisema kwamba awali watu wa Kwimba walilazimika kusafiri umbali mrefu kupata huduma za mikopo, lakini sasa wamesogezewa huduma karibu, hivyo ni jukumu lao kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujinufaisha kwa ajili ya maisha yao.

WAFANYAKAZI WA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR WAPEWA MAFUNZO JINSI YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA

0
0
Mshauri wa mambo ya Afya kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) Dk. Andemichael Ghirmay akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort na yamezaminiwa na WHO.
Mgeni rasmin Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed Jidawi akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.

MAKALA YA SHERIA: JE UMENYANYASWA NA MWAJIRI, HII NI NAMNA YA KUMFUNGULIA MASHTAKA

0
0
NA  BASHIR  YAKUB

Makuzi ya biashara hasa biashara za kimataifa yameleteza utitiri wa makampuni. Karibia kila biashara kubwa au ya kati  kwa sasa  hufanywa na makampuni. Baadhi ya ndani na mengine  ya nje. 

 Hatua hii njema kwa kiasi  fulani imeongeza  ajira  japo ajira zenyewe hazina vigezo vya kuitwa ajira. Yatosha ziitwe kazi tu. Ajira hizi ambazo nyingi  ni za umanamba zimekuwa  zikifanywa na wazawa.  Upande mmoja zimekuwa neema na upande mwingine zimekuwa laana. 

Ni neema kwakuwa baadhi  wanaweza kuishi japo  kwa pato la mlo tu na kusiwe na akiba yoyote  lakini  pia zimekuwa laana kwakuwa  ukihadithiwa baadhi ya mambo yanayoendelea huko waweza toa chozi.

Sio pote ila yapo maeneo yaliyoshindikana kama viwandani, migodini, miradi ya barabara na kwingineko waliko wawekezaji hasa wa kigeni. Hili ndilo limenituma kuandaa makala haya ili basi wenye  fursa wasome na waelewe na wenye kutaka msaada waweza kuwasiliana nami na kuona la kufanya.

Nianze hivi, kampuni kwa mujibu wa sheria ni mtu( legal person). Kuna tofauti kubwa kati ya kampuni na mmiliki wake. Kisheria kampuni  ikifanya kosa  yatakiwa ishitakiwe kampuni na sio  wamiliki au mfanyakazi kama mameneja, mkurugenzi n.k. 

Nimewaona wengi  hasa vijana ambao  huyadai makampuni haki zao hufungua kesi wakiwashitaki  wamiliki au mabosi wao. Hili ni kosa kubwa na wengi wao huwa wanashindwa zile kesi  na badala yake  kuanza kulalamikia mfumo wa nchi , mahakama au viongozi na hata chama tawala.

Ndugu hili halikusaidii. Hili sio  la serikali wala rais wala nani ni suala ka kisheria. Kampuni yako imekukosea unataka kudai fidia umemshtaki mmilki au viongozi badala ya kampuni, ni lazima utashindwa kesi  usimtafute mchawi wala kulalama kwa tuhuma za rushwa. Unapokosea taratibu  sheria haina huruma inakata. Upo msemo usemao (  A law is a merciless sword) yaani sheria ni upanga usio na huruma unamkata yeyote anayeuchezea. Kampuni  kama kampuni inao uwezo wa kushtaki kwa jina lake na kushtakiwa kwa jina  lake,namna gani tutaona hapo chini.

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA LIVE MJINI STUTTGART,GERMANY

0
0
Bendi ya maarufu barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni aka Anunaki aliens bendi hiyo inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho maalumu la AFRICA UNITE PARTY litakalofanyika katika ukumbi wa VTS uliopo mtaa wa Augusburger Str.442 D-70327 mjini Stuttgart,nchini Ujerumani.Onyesho hilo limeandaliwa na shirika la Afrikaktiv e.V wakishirikiana na shirika la Cabaret du Monde, Ngoma Africa band iliyozoeleka kwa kuwatia kiwewe washabiki wake kila kona duniani wataporomosha muziki moto moto na mdundo wao maarafu kama " Extraordinary Bongo Dansi" mdundo unaotingisha bila ya kuwa na mpinzani huko ughaibuni, bendi hiyo inadumu katika medani ya muziki kwa muda wa miaka 23 na kufanikiwa kujizolea washabiki kila kona. Ticket za onyesho hilo zinapatikana kwa simu ( booking): Call9+49 0)152 12091242 au +49(0)152 106106137 Mnakaribishwa wote,pia usikose kuwasikiliza FFU-Ughaibuni at www.ngoma-africa.com

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAFANYA ZIARA KATIKA MITAMBO YA KUFUA UMEME YA KINYEREZI 1

0
0
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wanja Mtawazo ( kulia) akisalimiana na Mbunge wa Lulindi- Masasi, Jerome  Bwanausi ( kushoto) ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini mara baada ya kamati hiyo kuwasili katika eneo la mtambo wa kufua umeme wa Kinyerezi I. Kamati hiyo inafanya ziara katika miradi ya umeme katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa madini ya tanzanite katika mkoa wa Manyara ili kujionea maendeleo ya sekta hizo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (kulia) akimsikiliza kwa makini Meneja Mradi Mkazi wa Kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway inayojenga mtambo wa Kinyerezi I Markkli Repo ( wa pili kutoka kushoto) mara baada ya kuwasili katika eneo la mtambo huo ili aweze kuwaongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwenye ziara katika mitambo hiyo.

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images