Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

POSTPONEMENT OF THE 1ST EAST AFRICA CONGRESS OF ACCOUNTANTS IN ARUSHA-TANZANIA

$
0
0
POSTPONMENT OF THE 1ST EAST AFRICA CONGRESS OF ACCOUNTANTS IN ARUSHA -TANZANIA
Due to unavoidable circumstance the 1st East Africa Congress of Accountants which was scheduled to take place in Arusha from    5th to 7th  March 2015 has been postponed till further notice.
                                                                   
We are very sorry for any inconvenience caused.


Issued by:
Executive Director
NBAA,  Mhasibu House,
P.O. Box 5128,
Dar es Salaam.
23rd February 2015


TAMASHA LA MICHEZO LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI NA TAASISI ZAKE LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa (kushoto) akimsalimia mtumishi wa Wizara hiyo, Said Ngovi ambaye ni mvuta kamba wa timu ya Utawala wakati Mkurugenzi huyo alipokuwa anazikagua timu mbalimbali za wizara hiyo katika Tamasha la Michezo la kwanza lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kapteni wa timu ya wanaume (Utawala) ya kuvuta kamba, Ally Lubuva.
 
 Kapteni wa Timu ya Utawala ya kuvuta kamba wanaume, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Neema Chilipweli (kushoto) akiimasisha timu yake kuivuta timu ya Uhamiaji (haipo pichani) wakati timu hizo zilipokuwa zikishindana katika Tamasha kubwa la Michezo lililoandaliwa na wizara hiyo kwa lengo la kuwakutanisha watumishi wake na kuwawezesha kufanya mazoezi ya viungo. Tamasha hilo ambalo la kwanza kufanywa na wizara hiyo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
 
 Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mary Nyegazeni akiishangilia timu yake ya Utawala ya kuvuta kamba wanaume baada ya kunyakua pointi mbili kwa kuivuta timu ya Uhamiaji katika mashindano maalumu ya Tamasha la Michezo la wizara hiyo ambalo lilishirikisha Wizara pamoja na taasisi zake ambazo ni timu ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Tamasha hilo lilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MHE. JAJI MKUU AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI TABORA

$
0
0
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili Mahakama ya Wilaya Sikonge mkoani Tabora, katika Mahakama hiyo Mje. Jaji Mkuu alipata fursa ya kuongea na Watumishi ambapo aliwasisitiza kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi na taratibu za Kimahakama ili kutimiza wajibu wa utoaji haki sawa kwa wananchi. Kulia ni Mhe. Amir Mruma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, kushoto ni Mhe. Sam Rumanyika, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora.
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akipanda mti wa kumbukumbu katika Mahakama ya Wilaya ya Sikonge iliyopo mkoani Tabora, Mhe. Jaji Mkuu alitembelea Mahakama hiyo akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama mkoani humo.
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania pamoja na Wahe. Majaji wengine wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama wa Wilaya ya Sikonge iliyopo Mkoani Tabora alipotembelea Mahakama hiyo wikiendi.
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Mkoa wa Shinyanga alipowasili mkoani humo kwa ziara ya Siku mbili.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania,akiongozana na Mtaalam kutoka TBA alipokuwa akikagua jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga lililopo katika hatua za mwisho za ujenzi, ukamilishwaji wa jengo la Mahakama Kuu Shinyanga utawezesha Mkoa huo ambao hutegemea Mahakama Kuu Tabora, kuwa na Mahakama yake na hatimaye kupunguza mlundikano wa kesi uliopo Mahakama Kuu Kanda ya Tabora. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania.)

TRAINING THE CHEETAH

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MHESHIMIWA CAPTAIN JOHN DAMIANO KOMBA (MB) TOKA BASATA

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Captain John Damian Komba kilichotokea jioni ya Jumamosi ya tarehe 28/02/2015.

Captain John Damian Komba ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa ni taa na nuru ambayo katika kipindi chote cha uhai wake imeangaza na kutoa mwanga angavu kwenye sekta ya Sanaa.

Mchango wake katika muziki wa dansi, kwaya na ule wa kiweledi katika kuandaa na kukuza wasanii mbalimbali nchini hautasahaulika kamwe. Ni mdau aliyeacha alama kuu katika muziki wa bendi, kwaya na taarabu na amejitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa dansi na kwaya mahali ulipo leo.

Aidha, pamoja na kujiunga na siasa na hatimaye kuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi, Mheshimiwa Komba hakukoma kuendelea kuipigania sekta ya Sanaa kwani alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambayo kwa mujibu wa kanuni za Bunge ndiyo inayoisimamia na kuishauri Serikali katika masuala yote yahusuyo sekta ya Sanaa na Utamaduni.

Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu John Komba hasa katika kutunga nyimbo za hamasa na ujumbe makini na wenye mashiko kwa jamii yote ya Watanzania.

Hakika pengo lililoachwa na Marehemu haliwezi kuzibika, kwani imekuwa ni kama mshumaa uliyozimika ghafla wakati tukiingia kwenye giza.

Baraza linatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda, wabunge na wadau wote wa Sanaa hususan wasanii kwa msiba huu. Ni matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu, hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu ya Sanaa na taifa kwa ujumla.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen

Godfrey Mngereza


KATIBU MTENDAJI

MAKALA YA SHERIA: MKE ASIYE WA NDOA NA MTOTO WA NJE YA NDOA HAWARITHI KISHERIA

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Kumekuwepo  na utata  mkubwa  kuhusu  urithi  wa  mali  za  marehemu  hasa  inapotokea  kuwa  marehemu  alikuwa  na  mke   zaidi  ya mmoja  na  hapohapo  watoto  wanaotokana  na  mama  tofauti.  
Tumeshashuhudia  magomvi  makubwa  misibani   lakini  pia  tumeshuhudia  na  tunaendelea kushuhudia  utitiri  wa mashauri  kuhusu  mkanganyiko  wa  mali za marehemu ambaye  familia  yake  ni  ya watoto  wanatokana  na  mama  tofauti. 
Kutokana  na  hayo  kuna umuhimu  mkubwa  wa kueleza sheria  inasemaje  kuhusu  mazingira  ya  namna  hiyo ili  anayemua kuchukua  hatua  au  kulalamika  alalamikie  kitu  ambacho  ni  haki  yake  kweli na  anayeamua  kuacha  aache  akiwa  ameridhika  kuwa  hajaonewa  isipokuwa  hicho  alichopata  ndiyo  haki   yake  kisheria. 

1.NINI  MAANA YA MKE  WA  NJE  YA  NDOA.

Mke  wa  nje  ya  ndoa  ni  mke  ambaye  ameishi  na  mume  kama  mke  na  mume  lakini  akiwa  hajafunga  ndoa  yoyote  ya  kiislamu, ya  kanisani, ya  serikali au  ya kimila. Ndoa  ya kiislamu hufungwa  kwa taratibu  za kiislamu  ambazo huhusisha  masheikh, makadhi n.k. Ndoa  ya  kikiristo  hufungiwa  kanisani  na  yaweza  kufungishwa  na  mchungaji, askofu, padre n.k. Ndoa ya  serikali  hufungwa  katika  mamlaka  za serikali  kama  kwa mkuu wa wilaya  ubalozini n.k. Na  ndoa  za kimila  ni  ndoa  ambazo  hufungwa  kutokana  na mila  na  desturi  za jamii  fulani kwa mfano  ndoa  za kihaya, ndoa  za kichaga n.k. Kwa hiyo  kama  mwanamke  hana  ndoa  yoyote  katika  hizi  basi  yeye  ni  mke  wa  nje  ya ndoa.

2. NINI  MAANA YA  MTOTO  WA  NJE  YA NDOA.

Mtoto  wa  nje  ya  ndoa ni mtoto aliyetokana  na  ndoa  isiyohalali au  mahusiano  yasiyo  halali. Hapo juu  nimetaja  aina  za ndoa halali. Hii ina  maana  kuwa  iwapo  mtoto  amepatikana  nje  ya  ndoa  hizo  basi  huyo  ndiye  anayeitwa  mtoto   wa nje  ya  ndoa. 

3.  MKE    ASIYE  NA  NDOA  HARITHI.

Kwa  mujibu  wa sheria  zetu  hapa  Tanzania  zikiwemo   tafsiri  mbalimbali  za  sheria  hizo  ambazo  hutolewa  na  mahakama  kuu pamoja  na  mahakama  ya  rufaa  mke wa  wa  nje  ya  ndoa  hutambulika  kama  kimada. Neno  kimada  sio  tusi  isipokuwa  ni  neno  la  kitaalam  linalomwakilisha  mwanamke  anayeishi  na  mwanaume  bila  ndoa  na  ndio  maana  neno  hilihili  limetumiwa  na  mahakama  katika  hukumu  zake  mbalimbali. 

BOFYA HAPA Kusoma zaidi...

Mkazi wa Kondoa akabithiwa Toyota IST na Washindi saba wa Airtel yatosha watangazwa

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imemkabidhi gari aina ya Toyata IST kwa Bwana Juma Said Alli mkazi wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma mara baada ya kuiba mshindi katika droo ya wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha zaidi. 
Zawadi hiyo yenye thamani ya Shilingi Milioni 15 ilikabidhiwa kwa Alli mwishoni mwa wiki na Meneja wa Airtel Kanda ya Kati, Stephen Akyoo. Akizungumza mbele ya vyombo vya habari wakati akikabidhiwa gari hiyo aina ya IST, yenye namba za usajili T778 DCZ, Alli alisema shughuli zake ni ukulima wa mazao mbalimbali katika Kijiji cha Ololimo na ana mke mmoja na watoto wawili. 
“Sikutegemea kushinda ingawa nimekuwa nikijiunga mara kwa mara na kifurushi cha Yatosha, kila ninaponunua vocha za Airtel na ninamshukuru Mungu nimeshinda kutokana na Yatosha ya Shilingi 500 tu. Hivyo nawahimiza watanzania wenzangu wasikate tamaa kwani na wao wanaweza kubahatika kama mimi na kujishindia gari hili zuri,”alieleza Alli.
 Kwa upande wake Meneja wa kanda ya kati bwana Stephen Akyoo alisema "tunao washindi wengi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam, Kagera, Mtwara, Mbeya, Tanga,Mwanza,katavi na sasa Dodoma. 
 Promosheni hii bado inandelea ni rahisi sana kwa kutumia vifurushi vya Airtel yatosha vya siku, wiki au mwenzi moja kwa moja unaunganishwa kwenye droo ya Airtel yatosha na kupata nafasi ya kujishindia Toyota IST kila siku. 
Vifurushi vya Airtel yatosha vinapatikana kwa kupiga *149*99# , au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha au kununua kupitia Airtel Money kwa matumizi yako ya kawaida kabisa unapata nafasi ya kujishindia gari " 
 Wakati huo huo Airtel imetangaza washindi saba wa wiki ya nne ya promosheni ya Airtel yatosha waliopatikana kupitia droo iliyofanyika siku ya ijumaa katika makao makuu ya Airtel Moroco, washindi hao ni pamoja na Juma Mapande (30) mkazi wa Pwani, Eusedio Onesmo Kipalile(48) mkazi wa Njombe, Suleiman Daudi Onesmo (20) Mkazi wa Mwanza, Seleman Kikondi Kimu (29) Mkazi wa Morogoro, Hassan Saidi Kimbe(28) Mkazi wa Dar es Saalam, Mohamed Ahmed Hamis (47) mkazi wa Manyara pamoja na Aivan Mbogambi Saigwa (35) Mkazi wa Dodoma 
 Washindi hawa watakabithiwa magari yao wiki hii pindi taratibu zote za makabithiano zikikamilika
  Meneja wa Airtel Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo (kushoto)  akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Saidi Juma Alli (Kulia) mkazi wa kondoa baada ya kuibuka mmoja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani katikati akishuhudiaAfisa Uhusiano na matukio wa Airtel bi Dangio Kaniki .
 Meneja wa Airtel Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo (kushoto)  akimkabithi mshindi wa gari aina ya Toyota IST bwana Saidi Juma Alli (Kulia) mkazi wa kondoa baada ya kuibuka mmoja kati ya washindi wa wiki ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. pichani katikati akishuhudiaAfisa Uhusiano na matukio wa Airtel bi Dangio Kaniki .
 Mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli akilijaribu gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 778 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.
 Wafanyakazi wa Airtel wakisherehekea kwa pamoja na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli (mwenye shati jekundu), baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Airtel wakisherehekea kwa pamoja na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Saidi Juma Alli (mwenye shati jekundu), baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dodoma.

Elimu ya kidigitali ya Vodafone Foundation kuwanufaisha watoto 15,000 katika kambi za wakimbizi: kutekelezwa Tanzania,Kenya na DRC

$
0
0
  Taasisi ya Vodafone Foundation leo imetangaza kuwa mpango wake wa kutoa elimu kidigitali umewezesha jamii zinazoishi kwenye mazingira magumu yanayosababishwa na majanga mbalimbali na  kujikuta zikiishi kwenye kambi za wakimbizi kuweza  kupata elimu.

Mpango huu wa   unatekelezwa katika  maeneo yenye mazingira magumu ambako kuna matatizo ya kutokuwepo nishati ya umeme na  upatikanaji wa mawasiliano hususani ya mtandao wa interneti na umeweza kutekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR). 
Ufunguzi wa madarasa chini ya mpango huu unafanyika kwa kutumia masanduku maalum yanayobeba vifaa vya kufundishia ,kuzalisha nishati ya umeme,kuchaji vifaa vya kufundishia na modemu maalumu za interneti ambazo hazihitaji kuunganishwa papo kwa papo .Vifaa vyote hivi vilivyoandaliwa kwa ajili ya mpango huu  unaoendeshwa kwenye maeneo yenye mazingira magumu vikiunganishwa kwa muda mfupi vinawezesha walimu maalumu walioandaliwa kuvitumia kuweza kuwapatia elimu wanafunzi bila matatizo yoyote.

Masanduku  maalumu ya kubeba vifaa vinavyotumika kutolea elimu hili yameandaliwa kutumika kuchaji vifaa vyote na vikishawekwa kwenye chaji kwa muda wa kati ya masaa 6-8 sanduku linaweza kutumika siku nzima kufundishia bila kuhitaji nishati ya umeme.

Mpaka mwaka ujao mpango huu utakuwa umetekelezwa katika shule 12 kwenye makambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya,Nyarugusu nchini Tanzania na Demokrasia ya Congo na utatoa elimu bora kwa watoto wapatao 15,000 wenye umri kati ya miaka 7 -20 .

Mpango huu tayari umeonyesha mafanikio makubwa ambapo mnamo mwaka 2014 taasisi ya Vodafone Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi la UNHCR limeweza kutoa elimu kwa watoto wapatao 18,000 kwenye kambi ya Dadaab nchini Kenya na walimu waliokuwa wanaendesha mafunzo chini ya mpango huu  wanakiri kwamba umeonyesha kuwa na  mafanikio na wanafunzi wameupenda na wameweza kupata elimu bora.

Katika kipindi cha miaka miwili ijayo mpango huu utatekelezwa katika makambi mbalimbali ya wakimbizi nchini Kenya,Tanzania na Demokrasia ya watu wa Congo lengo kubwa likiwa ni kuwafikia watoto 40,000 wanaoishi kwenye makambi ya wakimbizi.

Akiongea juu ya mradi huu Mkurugenzi wa taasisi ya Vodafone Foundation anasema: “Hadi mwaka 2013,UNHCR ilitoa takwimu  kuwa inakadiriwa kuwa kuna wakimbizi kwenye kambi mbalimbali duniani wapatao milioni 50 na kati yao nusu yao ni watoto wenye umri chini ya miaka 18 na hali hiyo inasababisha wapoteze ndoto ya kupata elimu.Mpango wa madarasa ya fasta wa Vodafone ni tumaini jipya na utawezesha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kama haya kupata elimu”.

Naye Afisa Mwandamizi wa UNHCR Olivier Delarue anasema:Kutokana na  majanga yanayojitokeza  na kusababisha kundi kubwa kuishi nje ya utaratibu wa maisha yao ya kawaida,UNHCR inakabiliwa na changamoto mbalimbali kuwapatia mahitaji mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo elimu.Tunakaribisha ubunifu huu wa taasisi ya Vodafone katika kutoa elimu kwa wakimbizi na tuko tayari kufanya kazi na taasisi hii katika kukabiliana na changamoto nyingine tunazokabiliana nazo.”

 masanduku maalum yanayobeba vifaa vya kufundishia ,kuzalisha nishati ya umeme,kuchaji vifaa vya kufundishia na modemu maalumu za interneti ambazo hazihitaji kuunganishwa papo kwa papo .Vifaa vyote hivi vilivyoandaliwa kwa ajili ya mpango huu  unaoendeshwa kwenye maeneo yenye mazingira magumu vikiunganishwa kwa muda mfupi vinawezesha walimu maalumu walioandaliwa kuvitumia kuweza kuwapatia elimu wanafunzi bila matatizo yoyote.



Record 9 EPL games live on DStv’s SuperSport

$
0
0

SuperSport will be the only broadcaster in the world to air 9 English Premiership matches on Tuesday and Wednesday, with some tantalising clashes that include a fierce local derby and a tough away trip for leaders Chelsea.
The Blues must make the journey across London to West Ham United on Wednesday.
The Hammers have hit a wobble since manager Sam Allardyce claimed he was the most sophisticated boss in the Premiership, a comment that will not have gone unnoticed by the most successful – Jose Mourinho.
West Ham have the ability to surprise at Upton Park and will be able to unleash new Brazilian winger Nene.
Manchester United visit Newcastle United on Wednesday with their top four hopes under a spotlight.
With only three league wins all season on the road, the Red Devils have not been happy travellers and St James’ Park is no place for the faint-hearted under lights and with the home faithful in full voice.
This will be another test of Louis van Gaal’s ability to fire up his troops.
The night before there is a West Midlands derby that is about a lot more than bragging rights when Aston Villa entertain West Bromwich Albion.
Villa have slipped into the relegation zone in recent weeks, but are hopeful that new boss Tim Sherwood will help spark a revival to pull them to safety.
West Brom have enjoyed better times under their new manager Tony Pulis, but will be wary of being sucked back into the relegation mix.
On Wednesday, Manchester City host bottom side Leicester City, while Arsenal head across London to Queen’s Park Rangers and Tottenham Hotspur entertain Swansea City.
Burnley will seek to ease their relegation woes when they travel to Anfield to face Liverpool.       


BROADCAST DETAILS

TUESDAY
Aston Villa v West Brom, SS3 & SSMaximo,  Kickoff at 21:45 (CAT)
Southampton v Crystal Palace, SS5, Kickoff at 21:45 (CAT)
Hull v Sunderland, SS7, Kickoff at 21:45 (CAT)


WEDNESDAY
West Ham v Chelsea, SS3, Kickoff at 21:45 (CAT)

Liverpool v Burnley, SS4, Kickoff at 22:00 (CAT)
Newcastle United v Manchester United, SS5 & SSMaximo, Kickoff at 21:45 (CAT)
QPR v Arsenal, SS6, Kickoff at 21:45 (CAT)
Manchester City v Leicester, SS7, Kickoff at 21:45 (CAT)
Spurs v Swansea, SS9, Kickoff at 21:45 (CAT)

Rais Kikwete aongoza maelfu ya waombolezaji kuaga mwili wa Kapteni John Komba

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa marehemu Salome Komba katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro)
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa salamu za Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete (katikati) akijadiliana jango na Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Wengine pichani toka kushoto ni Rais Mstaafu,Mh. Ali Hassan Mwinyi,Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete pamoja na Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee leo.

PICHA ZAIDI ZITAWAJIA HIVI PUNDE

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' ANYAKUWA UBINGWA WA U.B.O AFRICA KWA KUMTWANGA COSMAS CHEKA

$
0
0

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa kugombea ubingwa wa U.B.O Africa mpambano uliofanyika jumamosi ya jana Class alinyakuwa ubingwa huo kwa kushinda kwa Point na sasa Class anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Africa W.P.B.F na U.B.O Africa 

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' askiwa na mikanda yake ya ubingwa wa Africa wa U.B.O na WPBF

Bondia Cosmas Cheka akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O AFRICA
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akishangilia ushindi na mashabiki wake baada ya mpambano wake na Cosmas Cheka na kufanikiwa kumdunda kwa point
------------------------------
BONDIA machachali wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ametwaa ubingwa wa U.B.O Africa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kumtwanga bondia Cosmas Cheka wa Morogoro kwa point mpambano wa raundi kumi lililofanyika katika uwanja wa ndani wa taifa Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
katika mpambano uho ulioanza kwa mashambilizi kwa kila bondia kumtupia makonde mwenzie kwa ufundi wa  ali ya juu na ulikuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande baada kila mmoja kujiandaa kwa mda mrefu ata hivyo class alibuka mbabe baada ya raundi kumi kwisha.
katika mipambano mingine iliyopigwa siku hiyo bondia Fadhili Majiha alimsambalatisha Fransic Miyeyusho kwa point mpambano mwingine uliowakutanisha bondia chipkizi Vicent Mbilinyi aliyepambana na Epson John wa Morogoro mpambano uliomalizika kwa sare.
wakati bondia Shedrack Ignas alimpiga bila ya huruma bondia Husein Mbonde kwa K,O ya raundi ya nne ya mpambano wao nae Saidi Mundi akimpiga kwa point bondia Ramadhani Shauri.
aidha wadau wa mchezo wa ngumi waliofulika kuona mpambano huo wa kistoria wameomba kuwa mapambano hayo yanatakiwa kuanza mapema kuondoa hadha ya usumbufu wa usafili wakati wa kutoka na kwenda majumbani kwao kwani wapenzi wa mchezo wengi wa masumbwi wanategemea daladala kwa usafiri wa kurudi makwao ambapo ikifika zaidi ya saa sita daladala zinatoweka barabarani

introducing new track "Vidundurusi" by Mtafya from Mbeya's green records

MHE. JANET MBENE AKAMILISHA ZIARA YAKE UINGEREZA KWA KUKUTANISHWA NA WAFANYABIASHARA WA KITANZANIA JIJINI LONDON

$
0
0

Na Ally Rashid Dilunga, London
Katika kukamilisha mojawapo ya malengo ya ziara yake ya kikazi hapa Uingereza, Naibu waziri wa viwanda na biashara Mheshimiwa Janet mbene, amemalizia ziara yake ya wiki moja nchini Uingereza kwa kukutanishwa na baadhi ya wafanyabiashara wa Kitanzania hapa Ubalozini jijini London.

Ametumia fursa hiyo kuwafahamisha hatua zinazochukuliwa na Serikali kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na pia kuwataarifu juu ya fursa za kibiashara zilizoko katika sekta mbalimbali nchini Tanzania na kuwahamasisha kuzichangamkia fursa hizo na wasiwe ni wenye kuwaachia tu wanufaike nazo wageni.

Amewaambia kuwa kuna njia nyingi za kujishughulisha kibiashara, kuanzia kwao wenyewe kuwa ni sehemu ya masoko kwa kuwa waagizaji na wasambazaji wa bidhaa za Kitanzania, au kwa kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini au kuingia nao ubia.

Hata hivyo nao walimlalamikia Mheshimiwa Naibu Waziri juu ya ukosefu wa taarifa za biashara juu ya miradi ya uwekezaji nchini, ambapo naye amekiri upungufu huo na kwamba ushauri wao ameuzingatia.

Tangu alipowasili nchini Uingereza, Mheshimiwa Mbene alikutanishwa na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali kupitia Vyama vyao vya kibiashara na pia alikutana na baadhi ya wafanyabiashara na wawekezaji binafsi na kufanya nao mazungumzo yenye lengo la kuwekeza kwenye uongezaji thamani wa mazao au kufanya biashara hasa kwa kuvipatia masoko bidhaa kutoka nchini Tanzania.

Viongozi wa vyama vya kibiashara na baadhi ya wanachama wao aliokutanishwa nao ni wa Eastern Africa Association (EAA), Business Council for Africa (BCA) na UK-Tanzania Business Group.

Mheshimiwa Janet Mbene pia alikutanishwa na mshauri wa Serikali ya Uingereza juu ya masuala ya biashara kwa Tanzania, Lord Clive Hollick na watendaji wengine wa Idara ya uhamasishaji uwekezaji na Biashara (UKTI), ambapo alielezwa baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo wawekezaji nchini Tanzania. Mheshimiwa Mbene alitumia fursa hiyo kuwapa ushauri anaoamini utasaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa changamoto hizo na hasa baada ya mifumo ya utendaji kazi serikalini kurekebishwa kupitia Mpango maalum wa Matokeo Makubwa sasa (BRN).

Katika siku ya tatu ya ziara yake, mheshimiwa Mbene alitembelea Ofisi za Ubalozi na kukutana na watumishi wa Ubalozi na baadaye kukitembelea Kituo cha Biashara na kupata maelezo juu ya shughuli zake na changamoto zake.

Pia kutokana na ziara yake na kuongea na wafanyabiashara mbalimbali, Mheshimiwa Mbene amegundua kuwa Kituo kinafanya kazi kwa karibu sana na wafanyabiashara wa Ulaya, hivyo Serikali inatakiwa kukiongezea Kituo nguvu zaidi ili kiweze kutekeleza majukumu yake mengi kwa ufanisi zaidi na kuendelea kutoa mchango wake mkubwa katika kufanikisha malengo ya kiuchumi ya Taifa, kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Mbene baada ya kugundua kuwa ziko fursa nyingi za biashara na uwekezaji na kwamba wafanyabiashara wengi wana imani na Tanzania, ameahidi kupeleka mapendekezo yake Serikalini ya jinsi ya kuimarisha shughuli za Vituo vyetu vya Biashara ambavyo viko nje ya Tanzania.

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Tanzania, Mheshimiwa Janeth Mbene(kulia), akiongea na Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika masuala ya Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Lord Clive Hollick, walipokutana kuzungumzia masuala ya Biashara ya kati ya nchi mbili ya Tanzania na Uingereza na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Uingereza kusaidia wawekezaji wa Kiingereza kuwekeza Tanzania.
 Mheshimiwa Janeth Mbene, akiongeza na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Kiingereza alipokutana nao kwa mwaliko wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa East African Association. Mheshimiwa Naibu Waziri alikutana na Wafanyabiashara hao kwa lengo la kuwashawishi kuja kuwekeza nchini Tanzania
 Mheshimiwa Waziri Janeth Mbene(kulia), alipokutana na Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza na Chama cha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa nchini Uingereza (UKTI) (kati mwa picha), kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania nchini Uingereza, Bwana Yusuf Kashangwa.
 Wawakilishi wa Jumuiya za Wafanyabiashara na Wanachama wa chama cha Wafanyabiashara wa Tanzania nchini Uingereza (Tanzania Business Group) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda, Mheshimiwa Janeth Mbene, alipokutana na kuzungumza nao siku ya Ijumaa tarehe 28 Februari 2015, mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London. Mheshimiwa Waziri alikutana nao kuzungumzia hali ya Siasa na Uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Mheshimiwa Waziri aliwakumbusha Wafanyabiashara hao kutumia fursa zilizopo na kuwekeza nyumbani Tanzania, kwa lengo la kuongeza ajira na kuinua uchumi wa nchi.

Dar es salaam's PAZI BASKETBALL IN DIASPORA REUNION COMING TO HOUSTON THIS MARCH!

$
0
0
Kikapu kitapigiwa hapa


Wachezaji wakijifua



DAR ES SALAAM'S PAZI BASKETBALL  IN DIASPORA AND ITS FAMILY MEMBERS HAS ORGANIZED A BASKETBALL BONANZA THAT IS SCHEDULED TO TAKE PLACE ON MARCH 13th -15th, 2015 IN HOUSTON, TEXAS.

EVENTS:
      ON FRIDAY 13TH OF MARCH, 2015 NETWORKING
      LUNCH, DINNER, AND DRINKS WILL BE AVAILABLE AT MADIKODIKO LOCATION
BASKETBALL BONANZA LOCATION
      ON SATURDAY 14TH, FROM 10:00A.M TO 5:00 PM, AT 8601 CHIMNEY ROCK ROAD, HOUSTON TEXAS, US.
MUSIC
BY DJ LUKE

       NEW, OLD SCHOOL MUSICS, AND THE EVENT WILL BE STREAMING LIVE
      ONLY SOFT DRINKS AND NYAMA CHOMA WILL BE AVAILABLE
      DURING  BONANZA EVENT
PAZI FAMILY WILL HAVE A MEETING UNDER THE THEME “BRINGING BASKETBALL FAMILY TOGETHER”; VITALIS GUNDA-CHAIR
      TEAM BUILDING
      BASKETBALL DEVELOPMENT IN TANZANIA
      NEW IDEAS ARE WELCOME
      EVERYONE IS WELCOME TO ATTEND THE MEETING
BASKTBAL TEAMS ARE FORMING NOW FOR MORE INFORMATION; PLEASE CALL THE FOLLOWING NUMBERS TO REGISTER:
      PETER BATEGEKI: (713) 550-0468
      EMMANUEL NHIGULA: (713) 870-0547
      FLORA MOCHIWA: (832) 893-5034
      WILLY KURRUSA: (281) 661-0034
      VITALIS GUNDA: (240) 383-6950
      EMIL LWAKATARE: (832) 967-4339

CLOSING WITH NITE OF OLD SCHOOL MUSIC ,BONGO FLAVA  AND YOUNG GUYS  HIP HOP AT SAFARI CLUB
             GUEST DJ LUKE  WILL JOIN THE HOST DJS TO COMMEMORATE OUR OCCASION.
               ADDRESS TO SAFARI CLUB IS 7601 DE MOSS DRIVE,HOUSTO N TEXAS 77036

DON'T  FORGET  YOUR SNEAKERS
 AND DANCING SHOES ................

Msanii Maarufu Rwanda Kiziti Mihigo Afungwa Miaka 10 Jela kwa Kupanga Njama njama za kupindua serikali na kuua viongozi wake

$
0
0


Muimbaji maarufu wa Rwanda Kizito Mihigo amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kushtakiwa kwa njama za kutaka kupindua serikali na kuua viongozi wake na kuonyesha chuki dhidi ya serikali.



Kizito Mihigo awali alisema alikuwa na makosa na kuomba msamaha, akimaanisha hukumu yake ipunguzwe.
Kizito Mihigo amekuhumiwa jela miaka 10 kwa njama za kutaka kupindua serikali na kua viongozi wake.

Mshtakiwa mwenzake, Cassien Ntamuhanga kiongozi wa kituo cha redio ya Kikristo, alifungwa miaka 25 kwa ugaidi na matusi. Ameendelea kukataa mashtaka yote. 

Mihigo alikubali kutumiana ujumbe na kundi la upinzani lenye maskani Afrika Kusini, Rwanda National Congress (RNC). Alifutiwa mashtaka ya ugaidi huku Ntamuhanga alifutiwa kosa la kupanga kumuua Rais Kagame.

Kwa chanzo na habari kamili BOFYA HAPA

UTT YATOA SEMINA YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWENYE MASOKO YA FEDHA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA KUSIKIA

$
0
0
Ofisa Masoko Mwandamizi kutoka Kampuni ya Uwekezaji ya UTT, Martha Mashiku akitoa semina kuhusu uwekezaji wa pamoja kwenye Masoko ya fedha. Akizungumza na washiriki wa semina hiyo Mashiku alisema kuwa kazi kubwa inayofanya na UTT ni kuwawezesha watanzania wote wenye vipato tofauti kushiriki kwenye masoko ya fedha, kwa kujiwekea akiba taratibu huku pesa inawekezwa kwenye masoko ya fedha na mitaji. Ofisa huyo alisema UTT imekusudia kutoa elimu kwa makundi mbali mbali ya jamii ili watambue fursa hii ya kujiwekea akiba huku fedha zao zikikua kwa kiwango shindani kwenye soko.
Mwenyekiti wa Kikundi cha wanawake wajasiriamali wenye Ulemavu (Fuwavita), Mathayo Kawogo akitoa shukrani kwa kampuni ya UTT kwa kutoa mafunzo juu ya uwekezaji wa pamoja kwenye masoko ya fedha. Aliwasisitiza washiriki kutumia fursa zilizopo kujikwamua kwenye dimbwi la umasikini na hasa kutumia fursa ya UTT kuwekeza na ni huduma rahisi kujiunga na pia nafuu.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali wenye Ulemavu (Fuwavita), Mathayo Kawogo (kushoto) akikabidhi pesa taslimu kwa mlezi wa kikundi hicho, Mike Mwita, kwa ajili ya kuanza kuwekeza kwenye Mfuko wa Umoja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. 
Washiriki wa Semina ya Kuwajengea uwezo Wanawake Wajasiriamali wenye ulemavu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa semina iliyoendeshwa na kampuni ya Uwekezaji ya UTT.

Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe (Cuf) Ismail Jussa Ladhu azungumza na watanzania DMV

$
0
0
 Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe. Ismail Jussa Ladhu akiongea na Watanzania wa DMV siku ya Jumamosi Feb 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall uliopo University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.
 
  Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe: Ismail Jussa Ladhu akiongea na waTanzania wa DMV, walioka meza kuu wakanza kushoto Katibu wa Tawi la Chadema DMV Liberatus "Libe" Mwangombe, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Tawi la Chadema DMV Mhe. Kalley Pandukizi, Shamis Alkhatry CUF pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la kina mama CHADEMA DMV Bi Baybe Mgaza.
Watanzania waishio DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) wakimsikiliza Mh Ismail Jussa alipohutubia katika mkutano uliondaliwa na muungano wa vyama vya CUF na CHADEMA Marekani.
---
Taarifa ya Abou Shatry /swahilivilla, Washington DC
Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wananchi, CUF Mhe. Ismail Jussa Ladhu amesema Tanzania inaelekea kusipotarajiwa na maoni ya wananchi waliyotoa maoni.
Aidha amesema matarajio ya Watanzania hayajatimizwa mbali ya kuwepo mijadala mingi juu ya rasimu ya Jaji Warioba ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu katika suala la katiba mpya.
Mhe. Jussa aliyasema hayo wakati akizungumza na Watanzania waishio DMV siku ya Jumamosi Februari 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall 1401 University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.
Pia Mhe. Jussa ambaye pia ni mjumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) amesema uamuzi wa UKAWA kususia na kujitoa katika Bunge Maalum la Katiba ni kwa sababu chama tawala, CCM kimekwenda kutetea sera zake na kupinga mawazo ya wananchi ambayo yamewakilishwa katika rasimu ya Jaji Warioba.
Mkutano huo ulijumuisha agenda kadhaaha ikiwemo mchakato wa Katiba Mpya, ufafanuzi juu ya muundo wa serikali tatu, uamuzi wa UKAWA kususia mchakato dhalimu na sababu ya maoni ya diaspora kuhusu Uraia Pacha kutokutekelezwa kama walivyotarajia.

CHADEMA Red Brigade wala kiapo Mwanza mbele ya Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe

$
0
0
 Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, al maarufu kama RED BRIGADE, wakila kiapo cha utii, mbele ya Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jijini Mwanza siku ya Jumamosi Februari 28, 2015. Kiapo hicho kinafuatia kukamilika kwa mafunzo ya kiulinzi na usalama kwa vijana hao.
 Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), akisoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigade' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) akisikiliza.
Vijana hao wakila kiapo mbele ya Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe (kulia).Picha: K Vis blog

DKT.MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MWANGA-KIKWENI-VUCHAMA/LOMWE KM 40.6 MKOANI KILIMANJARO

$
0
0

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ametangaza kutobomolewa nyumba zilizopo kando kando ya  barabara ya Mwanga-Kikweni/Vuchama-hadi Lomwe km 40.6 na kusema kuwa barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami kwa kutumia upana wake uliopo hivi sasa.
Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo ya faraja kwa wakazi wa Kikweni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro kabla ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mwanga-Kikweni/Vuchama-Usangi hadi Lomwe(km 40) itakayojengwa kwa kiwango cha lami hivi karibuni.

Waziri wa Ujenzi amechukua uamuzi huo kutokana na maeneo mengi ya milimani ambapo barabara hiyo inapita kuwa na mashamba ya watu tofauti na sehemu nyingine.

“Nikiwa kama Waziri wa ujenzi katika maeneo haya ya milima sitatumia sheria ya mita 30 kila upande katika ujenzi wa barabara hii ili nyumba na mashamba ya wakazi wa huku yasiathirike”

Dkt. Magufuli aliongeza kuwa ujenzi wa Barabara una sheria zake ndio maana ameamua kutumia sheria ya barabara  namba 13 ya mwaka 2007 kifungu cha 13 na 20 kinachompa mamlaka kupunguza upana wa barabara

Aidha, Waziri Magufuli aliwatoa hofu wakazi wote waliowekewa alama ya X katika nyumba zao na kuwataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwasababu nyumba hizo hazitabomolewa.

Katika hatua nyingine Dkt. Magufuli aliwataka watu wote waliojenga vibanda karibu na barabara ya zamani waanze kuondoka mapema kabla ya ujenzi wa barabara hiyo kuanza hivi karibuni.

“Nawaomba wote mlioweka vibanda karibu na barabara mtoe kwa hiari yenu ili tutengeneze barabara hii bila vikwazo na kwa haraka tofauti na awali ambapo tulikuwa tunatangaza zabuni kwa kilomita chache” alisisitiza Waziri Magufuli

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amemshukuru Waziri Magufuli kwa hatua yake hiyo na kusema kuwa kufunguka kwa barabara hiyo ni mkombozi mkubwa kwa wilaya ya Mwanga na Mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

“Wilaya yetu hii inapakana na nchi jirani hivyo hata kiusalama ni vizuri barabara hii ikajengwa kwa lami ili irahisishe mawasiliano kwa haraka zaidi katika Wilaya yetu hii” alisema Mkuu wa Mkoa

Naye Mbunge wa Mwanga ambaye pia ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe ameishukuru Serikali na kusema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutawaondolea kero kubwa ya usafiri wananchi wa Usangi na mwanga na kuwasaidia kufanya biashara kwa urahisi zaidi tofauti na awali.

“Kukamilika kwa barabara hii kutasaidia kuinua uchumi mkubwa uliopo huku Usangi tofauti na hali iliyopo sasa” Alisema Profesa Maghembe.

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiweka jiwe na msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40. Kulia kwake ni Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Mwanga.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40.6. Katikati ni Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe.

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakicheza ngoma na kikundi cha ngoma za asili Kikweni kabla ya uzinduzi wa barabara ya Mwanga-Kikweni-Vuchama-Usangi-Lomwe yenye urefu wa kilomita 40.
 . Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na kikundi cha ngoma cha Msanja group kabla ya kuhutubia mamia ya wakazi wa Usangi kuhusu ujenzi wa barabara ya Kikweni-Usangi-Lomwe ambayo itaanza kujengwa hivi karibuni.

Wakazi wa Zanzibar waipongeza kampeni ya usalama barabarani ya “Wait to Send”

$
0
0
Wakazi wa Zanzibar wameipongeza kampeni ya”Wait to Send” inayohamasisha usalama barabarani kwa madereva. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi la usalama barabarani na Vodacom Tanzania imefanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki na kuwavutia wakazi wengi wa kisiwa hicho ambao walisema inaweza kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajali kisiwani humo. 
 Akiongea juu ya kampeni hiyo Kamishna Msaidizi wa Polisi wa Usalama Barabarani wa Zanzibar, ACP Nassor A.Mohamed alisema kuwa ajali za barabarani bado ni tatizo kubwa hapa nchini na ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva hasahasa kutokana na kutozingatia sheria za usalama barabarani. 
 “Unakuta dereva wa gari la abiria anaendesha gari wakati huo huo anatuma ujumbe wa maneno kwenye simu au anaongea na simu wengine pia kuangalia picha kutoka kwenye mitandao ya simu,utakosaje kupata ajali au kuwasababishia ajali watumiaji wengine wa barabara,tena jambo la ajabu hata waendesha pikipiki nao wanatumia simu wakati wanaendesha vyombo hivyo jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao”.Alisema. 
 Aliwataka madereva kuzingatia sheria za barabarani na aliishukuru kampuni ya Vodacom na wadau wengine ambao wako mstari wa mbele kuhamasisha uzingatiaji wa sheria za barabarani. 
 Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Zanzibar, Mohamed Mansour alisema kuwa kampeni ya ‘Wait to Send’ inalenga kupunguza ajali za barabarani na inawataka madereva kuacha kutuma meseji au kuongea na simu zao wanapoendesha vyombo vya moto. 
“Katika kufanikisha kampeni hii Vodacom imetoa pete maalum za kuwakumbusha madereva kuacha kutuma meseji wanapoendesha vyombo vya moto na tumezileta kwa ajili ya madereva wa Zanzibar na tutaendelea kuzigawa kama ambavyo tumekuwa tukifanya katika sehemu mbalimbali za nchi ambako kampeni hii imefanyika”Alisema 
 Baadhi ya madereva walieleza kuwa kampeni hii ni muhimu katika kupunguza ajali “Nashauri kampeni hii zifanyike mara kwa mara ili kuwakumbusha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani “.Alisema Abdul Kassim dereva wa basi la abiria Zanzibar. 
 Naye Mansour Juma alisema ajali nyingi zinazotokea zinasababishwa na kukua kwa teknolojia ikiwemo matumizi ya simu,wengine kuangalia televisheni wakati wakiendesha magari na magari yanayoingizwa nchini ni rahisi kwa kila mtu kuyaendesha bila kuhitaji mafunzo ya ziada hivyo alishauri kampeni za aina hii zifanyike mara kwa mara ili kuwakumbusha madereva kuwa makini ili kuepusha ajali zisizo za lazima.
 Kamishna Msaidizi wa Polisi wa Usalama Barabarani wa Zanzibar, ACP Nassor A.Mohamed (kushoto) akikabidhiwa vitendea kazi, fulana, pete na stika ofisini kwake Malindi mjini Zanzibar na Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Zanzibar, Mohamed Mansour mwishoni mwa wiki kwa ajili ya mwendelezo wa kampeni ya usalama barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Wengine katika picha wa pili toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu na Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Henry Bantu.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Henry Bantu (kulia) na ACP Nassor A. Mohamed wakionyesha pete zenye ujumbe maalumu wa Wait to Send baada ya Kamishna Msaidizi wa Polisi wa Usalama Barabarani wa Zanzibar kukabidhiwa vitendea kazi mbalimbali na Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Zanzibar, Mohamed Mansour (kulia) Malindi mjini Zanzibar kwa ajili ya mwendelezo wa kampeni ya usalama barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Wengine katika picha wa pili toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo ya Baraza la Taifa la  Usalama Barabarani, Henry Bantu na Ofisa wa Jeshi la Polisi kituo cha Malindi mjini Zanzibar, Abdullah Juma kwa pamoja wakimvisha pete maalumu dereva Khamis Sheha Madua anaeendesha daladala iendayo Kizimbani Spice ikiwa na ujumbe wa “Wait to Send” wakati wa zoezi la kutoa elimu kwa madereva mbalimbali lililofanyika mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki. Pete hiyo inamkumbusha dereva asitumie simu wakati akiendesha chombo cha moto. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Zanzibar,  Mohamed Mansour na Frank Maston.

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images