Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA MAFUTA YA PANONE YAWAKUMBUKA WATOTO WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA GABRIELA CHA MJINI MOSHI

$
0
0
Wafanyakazi wa kampuni ya Mafuta ya Panone wakiwa katika picha ya Pamoja na watoto wanao lelewa katika kituo cha Gabriela cha mjini Moshi.
Afisa uhusiano wa timu ya soka ya Panone fc Kassmi Mwinyi akitoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Panone Frank Mwaikatale akigawa zawadi ya mikate kwa watoto wanaolelewa katika  kituo cha Gabriela cha mjini Moshi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

PAUL MAKONDA AUNDA KAMATI YA KUSHUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI KINONDONI

$
0
0

Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Wilaya la Kinondoni
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema kuwa wilaya ya Kinondoni inakabiliwa na changamoto migogoro ya ardhi ambayo inatakiwa kila mtu ambaye amenyimwa haki ya ardhi watapata kutokana na utaratibu uliopo.

Makonda aliyasema hayo hivi karibuni wakati ziara ya kutembelea wilaya hiyo, Makonda alisema asili ya migogoro hii inatokana hasa na mgongano wa uhalali wa umiliki pamoja na uvamizi wa maeneo ya wazi yaliyotengwa maalumu kwa shughuli za jamii ni changamoto ya muda mrefu na natambua juhudi nyingi zilizofanyika katika kutatua.

Makonda alisema moja ya mkakati wangu ni kufanya utatuzi unaohusisha taasisi zote muhimu ili kufupisha mlolongo unaowapotezea muda walioko kwenye migogoro na kuhakikisha mwenye haki anapewa haki yake bila kuyumbishwa.

Alisema anatenga siku moja ambayo ni ya Ijumaa kuwa siku maalumu ya kukutana na wananchi na kusikiliza matatizo yanayohusiana na Ardhi na utaratibu huu utaanza machi 6 mwaka huu na zoezi la uandikishaji kwa wale wanaohitaji kusikilizwa matatizo yao utaanza majira ya saa 3.

Makonda alisema Ili kupata ufumbuzi usio na shaka kamati ndogo itakayohusika katika kushughulikia matatizo hayo itaundwa na Katibu tawala wilaya (DAS) akiwa ni katibu, Mwanasheria wa Manispaa, Afisa Mipango miji, Afisa Ardhi.

Aidha alisema ili kufanya zoezi hili liwe na ufanisi na mafanikio ningeomba wananchi wafuate utaratibu kuanzia ngazi za watendaji wa chini kabla ya kufikisha kila muhusika ahakikishe amekuja na vielelezo vyote halali vinavyoweza kutumika katika kufikia uamuzi.

Waziri Membe azungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataiafa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) waliopo hapa nchini kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. Masuala hayo ni pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na mauaji ya Albino, Mkataba wa Makubaliano ya Chama cha SPLM cha Sudan Kusini na  Hali katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu  kama DRC. Kulia  ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa DRC hapa nchini, Mhe. Juma Khalfan Mpango na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam tarehe 03 Machi, 2015
Sehemu ya Mabalozi  na Wajumbe wengine waliohudhuria mkutano kati yao na Waziri Membe (hayupo pichani) wakifuatilia mazungumzo. Mwenye tai nyekundu ni Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Mark Childress.
Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wawakilishi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

INTRODUCING VITAMIN MUSIC - BELLE 9 FT JOH MAKINI OFFICIAL VIDEO

OLOLOSOKWAN WAFURAHIA UJIO WA KIJIJI CHA DIGITALI ENEO LAO

$
0
0
DSC_0003
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya Tehama, Al Amin Yusuph akiwasilisha mrejesho wa kazi ya kikundi chake wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.(Picha na zote Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi Wetu

WAKAZI wa kijiji cha Ololosokwan wamesema kwamba ujio wa kijiji cha digitali katika kijiji chao ni neema kwao kwani kitawasaidia kukabiliana na changamoto kubwa za maisha zinazowakabili.

Kauli hiyo wameitoa mwishoni mwa wiki wakati wa kuhitimisha warsha ya siku saba ya kuangalia fursa na changamoto zitakazoambatana na mradi huo wa miaka mitatu unaodhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake waliohudhuria warsha hiyo ambapo wataalamu mbalimbali wanaohusika na mradi huo walikutana kujadili changamoto na namna ya kukabiliana nazo, Salangat Mako, alisema kwamba tatizo la miundombinu, Afya na Elimu wanaamini litakabiliwa na mradi huo.

Alisema kuna shida kubwa ya elimu kutokana na mazingira yaliyopo ambapo wanafunzi wanalazimika kutembea kilomita 14 kwenda na kurudi shule hali inayodhoofisha ari ya kujifunza.
DSC_0044
Mwenyekiti wa kikundi kazi cha sekta ya elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akitoa mrejesho wa kilichojadiliwa na kikundi chake.

make your house a beautiful home

EDWARD MBUGI WA MBOZI AKABIDHIWA SHILINGI MILIONI 1/- ALIZOJISHINDIA KUPITIA PROMOSHENI YA JAY MILLIONS

$
0
0
Mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya Edward Mbugi,amekabidhiwa fedha zake kiasi cha shilingi Milioni 1/-na Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyandaya Kusini,Macfadyne Minja,alizojishindia kupitia promosheni ya Jay Millions inayoendeshwa na kampuni hiyo. 
Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa Shilingi Milioni 1 wa Promosheni hiyo, Edward Mbugi, amesema kwanza kabisa hakuamini kama ameshinda kwani kumekuwa na kasumba ya washindi wengi wanaoshinda kupitia promosheni kama hizi zinazoendeshwa na kampuni za simu lazima ni wakazi wa Jijini Dar es Salaam tu. 
Ila nimefurahishwa sana na promosheni hii ya Jay Millions ni yakipekee inatoa washindi kila kona ya nchi.
Napenda kuwaomba Watanzania kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Vodacom Tanzania nchini katika kujenga na kuimarisha maisha ya Watanzania na kuwa murua zaidi. 
"Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa kimaisha watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, ambapo kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa aina hii wanahitaji msaada ili kujiendeleza kiuchumi. 
Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha," alisema Mbugi.
 Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Nyasa, Macfadyne Minja (kushoto) akipokea pesa kiasi cha shilingi Milioni 1/- toka kwa wakala wa M-PESA jijini Mbeya kwa ajili ya kumkabidhi rasmi mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya, Edward Mbugi (kulia) alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini humo hivi karibuni. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au AUTOkwenda 15544.
 Mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya, Edward Mbugi (kushoto) akipokea pesa kiasi cha shilingi Milioni 1/-kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Nyasa, Macfadyne Minja, alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini humo hivi karibuni. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au AUTO kwenda 15544.
 Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Nyasa, Macfadyne Minja (kulia) na Meneja wa Vodashop Baraka Musabila (kushoto) wakimshuhudia Edward Mbugi, ambaye ni Mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya akionesha kitita chake cha shilingi Milioni 1/- alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayondeshwa na Vodacom Tanzania,wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini humo hivi karibuni. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au AUTO kwenda 15544.
Mshindi wa shilingi Milioni 1/- mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya, Edward Mbugi, kupitia promosheni ya JayMillions inayondeshwa na Vodacom Tanzania, akizihebu pesa zake baada ya kukabidhiwa rasmi  na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Nyasa, Macfadyne Minja (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Mbeya hivi karibuni. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au AUTO kwenda15544.

WAZIRI WA UJENZI DKT JOHN MAGUFULI AZUNGUMZA NA WATENDAJI WA KAMPUNI YA UKANDARASI WA BARABARA YA DOT SERVICES YA NCHINI UGANDA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi ,Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mkuu wa wilaya ya Same  Mhe. Herman Kapufi wakati akifanya ukaguzi wa barabara kutoka Korogwe/Mkumbara hadi Same yenye urefu wa  Kilomita 172, inayojengwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB).
Waziri wa Ujenzi Dkt ,John Magufuli akizungumza na wakandarasi kutoka kampuni ya Dot Services ya nchini Uganda inayo jenga barabara ya Korogwe/Mkumbara hadi Same.
Waziri wa Ujenzi Dkt Magufuli akizungumza jambo wakati alipokutana na watenadji wakuu wa kampuni ya Dot Services wanaojenga barabara ya Korogwe/Mkumbara hadi Same.

Na Dixon Busagaga wa

Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


SERIKALI imetaka wakandarasi wa barabara nchini, kutekeleza miradi ya barabara kwa wakati na ubora unaokubalika  ili kuwaonesha wahisani namna ambavyo fedha  wanazotoa zinafanya kazi iliyokusudiwa kwa kuonesha thamani halisi ya mradi husika.

 Hayo yalielezwa juzi na waziri wa Ujenzi, Dkt John Magufuli wakati akifanya ukaguzi wa barabara kutoka Korogwe/Mkumbara hadi Same yenyeurefu wa  Kilomita 172,inayojengwa kwa fedha za mkopo kutoka benki ya 
dunia (WB).

Dkt Magufuli  alisema changamoto mbalimbali  zinazojitokeza katika ujenzi wa barabara hazina budi kutafutiwa ufumbuzi wa mapema, ili kutoa nafasi kwa rais Jakaya Kikwete kuifungua na kuruhusu wananchi kuendeleza shughuli za uzalishaji mali.

Alisema katika kuhakikisha barabara hizo zinadumu ni vyema kwa Tanroad  kutafuta mizani inayohamishika (Mkeka) ili kuwadhibiti wasafirishaji wasio waaminifu ambao wamekuwa wakibeba mizigo mikubwa kwa tamaa ya fedha.

" Kukamilika kwa barabara hizi kutarahisisha shughuli za kiuchumi kwa mikoa hii inayopitika ,Nikuombe katibu mkuu kwa kushirikiana na wahandisi, kuhakikisha hizi Bil 200 ambazo ni mkopo hazipotei, nataka mdhibiti magari yanayobeba mizigo mikubwa....wakati fulani tulishika magari yenye uzito wa Tani 96 hadi 102, uzito unaokubalika kisheria ni

Tani 56 tu"alisema Magufuli..


Naye mtendaji mkuu wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mhandisi Partick Mfugale alimweleza Wazri Magufuli kuwa barabara ya kutoka Korogwe/Mkumbara hadi  Same yenye urefu wa  Kilomita 172 inajengwa kwa

awamu mbili tofauti.

Alisema barabara hiyo ambayo  sehemu ya barabara inatoka Dar es salaam ,Chalinze,Arusha  hadi Nairobi, imegawanywa mara mbili, Korogwe/Mkumbara  Km  76 kinachojengwa na kampuni ya Strabag  ya Ujerumani na Mkumbara/Same  Km 96 inajengwa na kampuni ya Dott services ya Uganda.


Mfugale alisema   ujenzi  wa kipande cha Korogwe/Mkumbara ulianza Mei,2012 na kumaliza Desemba 3,2014 na uligharimu Bil sh 87.805 kwa mkandarasi na kiasi cha Sh Bil 6.787 kwa mhandisi msimamizi kampuni ya Nicholas O'Dwyer Ltd ya nchini Ireland kwa miradi yote miwili. 
Alisema Kazi alizofanya katika mradi huo ni kubandua na kusaga lami iliyokuwepo na kuweka lami nyingine mpya kwa mfumo imara zaidi,kuimarisha daraja la Mombo, kujenga makalvati  makubwa 18 na madogo 175 na sasa kazi imekamilika na yupo katika muda wa uangalizi.

Mradi wa pili ni Mkumbara/Same Km 96 wenye gharama ya Bil 103.8kupitia mkandarasi wa Dott services ya Uganda ambao walikubwa na changamoto kadhaa ambazo sasa zimerekebishwa na sasa ameanza ujenzi kwa kasi.

Alisema makubaliano ni kujenga angalau Km 4 kwa kila mwezi ambapo sasa amekamilisha asilimia 67 ya mradi husika na matarajio ni kukamilishamradi wote hadi kufikia muda wa mkataba ambao ni Disemba mwaka huu.

Mfugale alisema mkandarasi huyo tayari amelipwa kiasi cha Sh Bil 44.5na kazi inaendelea vizuri ingawa alitaka mkandarasi huyo kuhakikisha kasi ya ujenzi anayofanya sasa  ilingane na ubora wa barabara inayojengwa.





BONDIA OMARI KIMWERI AMPIGA TAFU YA VIFAA KOCHA SUPER D

$
0
0

Mwanasoka wa kike, Melanie Gines (kushoto) ambaye ni raia wa Hispania na  bondia Omari Kimweri na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakiwa tayari kupanda ndege na kurudi kwao 
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto)  akimkabidhi glove kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati ni  bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchiniAustralia. Omari Kimweri ambaye aliongozana nchini na mwanasoka huyo muda mfupi kabla awajapanda ndege kurudi kwao.

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Mtanzania Omari Kimweri anaefanya shughuli zake za mchezo wa masumbwi nchini Australia amempiga tafu ya vifaa vya kufundishia kocha wa kimataifa wa mchechezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' 

wakati wa zihara yake ya wiki mbili ya kutembelea nyumbani kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu zitumiwazo na mabondia wa nje

kabla ya hapo bondia huyo aliongea na wadau mbalimbali wa masumbwi wakati wa mchezo wa ngumi za kulipwa kati ya Iddi Bonge na Alphonce Mchumiatumbo mpambano uliofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na kumvalisha mkata wa ubingwa bondia wa uzito wa juu Mchumiatumbo baada ya kuibuka na ushindi wa K,O ya raundi ya kwanza

siku hiyo pia alimpiga tafu kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kwa kumkabidhi vifaa vipya vya kufundishia mchezo wa masumbwiakizungumza baada ya kumkabidhi vifaa kocha Super D alisema amekumbuka nyumbani kwa kuwa ndio alipo zaliwa na kitovu chake kimezikiwa hapa nchini hivyo ataendelea kuwakumbuka zaidi kwa kuwawezesha mabondia kucheza mara kwa mara pindi atakapoanzisha Kimweri Promotioon itakayoshilikiana na Super D Boxing Coach And Promotion kwa kushilikiana kuwapatia mabondia kupigana ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujiongezea kipato pamoja na kupandishe rekodi zao kwa mabondia chipukizi
nae kocha Super D alishukulu kwa kukabidhiwa vifaa hivyo ambavyo vitamsaidia kuendelea kuinua mabondia mbalimbali chipkizi



FURAHA YA KUNUNUA KOCHI MPYA

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE AWASILI MKOANI DODOMA KUANZA ZIARA YA SIKU TISA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa uwanja wa ndege mjini Dodoma mapema leo asubuhi na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Mh. Adam Kimbisa,tayari kwa kuanza ziara ya siku tisa, yenye lengo la kukagua, kuhimiza miradi ya maendeleo ya wananchi pamoja na kuangalia uhai wa chama, ambapo mara baada ya kuwasili amefanya mkutano wa ndani na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mpwapwa yenye majimbo mawili ya Uchaguzi.Kinana ametokea Mkoani Ruvuma mara baada ya kushiriki mazishi ya aliekuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi,Marehemu Kapteni John Komba aliyezikwa kijijini kwao Lituhi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akilakiwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma,Mh.Chiku Galawa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Dodoma mapema leo asubuhi,kulia kwake ni  Katibu wa CCM Mkoa,Albert Mgumba
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.Chiku Galawa mapema leo asubuhi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege,tayari kwa kuanza ziara ya siku 9 mkoani humo,
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa,Mh.Addam Kimbisa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake pamoja na baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM Wilaya ya Mpwapa mapema leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Wanachama wa CCM waliofika mapema leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mpwapwa kumpokea Ndugu Kinana na Ujumbe wake,ambapo anaanza rasmi ziara yake wilayani humu na vitongoji vyake.

PICHA NA MICHUZIJR-MPWAPWA.

UDSM KUIWAKILISHA NCHI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA UENDESHAJI KESI BANDIA(MOOT COURT)WASHINGTON,MAREKANI

$
0
0
 Msajili wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Dk Eno Robert akizungumza kabla ya kutangaza matokeo ya mashindano ya uendeshaji wa Mahakama kwa wanafunzi wa Vyuo(Moot Court)yaliyofanyika katika Mahakama hiyo jijini Arusha.
 Wanafunzi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Saalam(Udsm)kutoka kushoto,Emmanuel Bakilana,Jacob Muheesi,Alicia Atukunda na Adela Msofe wakiwa hawaamini ushindi wao dhidi ya Chuo Kikuu cha Saint Augustine(Saut)Mwanza.
Wanafunzi wa Chuo cha Udsm wakipongezana na Sauti baada ya kutangazwa matokeo ambayo yanawawezesha wanafunzi wa Udsm kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa Washington,Marekani.
 Msajili wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Dk Eno Robert(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na waandaji wa mashindano hayo pamoja na washiriki. 

ankal na selfie,,,,

KUMBUKUMBU NA MISA

$
0
0
Maria G. Mapango (IA) leo umetimiza miaka miwili tangu ulipoteuliwa na Baba wa Mbingumi. Daima tunakukumbuka mwanetu, mdogo wetu, 

Tunakuombea upunguziwe adhabu za kaburi na upatiwe mwanga wa milele.

Misa itafanyika leo tarehe 4 Machi, 2015 katika kanisa Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam, Saa 11.00 jioni

kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) ytembelea miradi ya miundombinu dar es salaam, yataka mradi mabasi yaendayo kasi uanze

$
0
0
Kamati ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetoa muda wa wiki mbili kwa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Wakala wa Barabara (TANROAD) kutoa taarifa ya inayoeleza muda halisi wa kuanza kwa mabasi ya mradi huo katika kipindi cha mpito. 
 Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Bw. Hamis Kigwangala alitoa maelekezo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati kamati yake ilipokuwa ikipokea taarifa ya utekelezaji wa maradi huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia DART na TANROADS. “Kipindi cha mpito cha mradi huu kilikuwa kianze mwezi April mwaka huu lakini hadi sasa maandalizi yake bado hayakamilika,”alisema. 
Alisema kutokana na hali hiyo kamati imetoa siku 14 kuanzia sasa waandae taarifa inayoonyesha kukamilika kwa mandalizi hayo ikiwemo kusaini kwa mikataba na mtoa huduma na kuikabidhi taarifa hiyo. 
“Tunahitaji kuona mabasi ya kipindi cha mpito yanaanza kufanya kazi katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa,” alisema. Alifafanua kwamba mradi huo ni muhimu kwa vile utaokoa Tshs 4.5 bilioni kwa siku zinazopotea katika jiji la Dar es Salaam kutokana na msongamano wa magari. 
Pia aliitaka TAMISEMI kwa kushirikiana na mamlaka nyingine kuhakikisha inawaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika miundombinu ya mradi huo. 
“Miundombinu hii imejengwa kwa gharama kubwa hivyo inapaswa kutunzwa na pia wananchi wanapaswa kuithamini” alisema. 
Alisisitiza kuwa Wakala uhakikishe mtoa huduma kipindi cha mpito anakuwa mzalendo na pia asizuiwe kuomba zabuni ya kuwa mtoa huduma mkuu muda utakapofika. 
Waziri, wa TAMISEMI, Mhe. Hawa Ghasia alisema serikali kwa upande wake itaendelea kutoa kipaumbe kwa wafanyabiashara wazawa kuendesha mradi huo. “Jambo zuri ni kwamba hata kamati ya bunge nayo inasisitiza kuwa wazawa wapewe kiupaumbele katika jambo hili,”alisema. 
Alisema serikali imepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kamati ya bunge na wataenda kuyafanyia kazi dhamira ikiwa ni kuhakikisha mradi unaanza mara moja. 
Mtendaji Mkuu wa DART, Bi, Asteria Mlambo alisema mradi huo hadi sasa umetumia Tshs bilioni 413,836 na kusema kuwa kumekuwa na ongezeko la Tshs bilioni 122,841. 
“Benki ya Dunia inajiandaa kutoa mkopo wa pili wa fedha za ziada ambapo itatoa nusu na nusu nyingine inaombwa itolewe na serikali,” alisema. Alisema ongezeko hilo limetokana na mahitaji ya kujengwa kwa barabara za juu katika makutano ya Ubungo na kuongezeka kwa kima cha chini cha mishahara ya wafanyakazi wa ujenzi.
 Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) Mh. Hamis Kigwangala (kushoto) akisikiliza maelezo ya Meneja Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kutoka TANROADS Mhandisi Elibariki Mmari wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka, (kulia) ni Mtendaji Mkuu wa DART Asteria Mlambo (wa pili) ni Mhandisi Athuman Mfutakamba mbunge wa jimbo la Igalua na mjumbe wa kamati hiyo.

 Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) Mh. Hamis Kigwangala (wa pili kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Hawa Ghasia wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, (kulia) ni Mjumbe wa kamati hiyo Moses Machali (wa pili kushoto)  ni Naibu waziri TAMISEMI Kasim Majaliwa.

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ( DART) Asteria Mlambo (kulia) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (Tamisemi) Mh. Hamis Kigwangala (wa pili kulia)  wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, (wa pili kulia) ni Waziri wa nchi – TAMISEMI, Mh. Hawa Ghasia, (kulia) ni Mhandisi Athuman Mfutakamba mbunge wa jimbo la Igalua na mjumbe wa kamati hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ( DART) Asteria Mlambo (kushoto) akimweleza jambo Waziri wa nchi – TAMISEMI, Mh. Hawa Ghasia (katikati)   wakati kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa ( TAMISEMI) ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hamis Kigwangala.


Dar es Salaam Conference Centre is Now Open for Business!

KATIBU MKUU KIONGOZI AFURAHISHWA NA UWEPO WA SACCOS MAKAZINI

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akimsikiliza Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga (wa pili kulia) akimuelezea mikakati ya ushirika huo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio, akifuatiwa na Katibu wake Bw. Benedicto Damiano na kulia ni Mtunza Hazina Bi. Judith Medson.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu chake cha uanachama toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio (wa tatu toka kulia). Wengine ni Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto Damiano (wa pili kulia), Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) na Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha kitabu chake cha uanachama baadas ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio wakishuhudiwa na Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto Damiano, Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.

MAGEREZA WAJIFUA TAYARI KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Sehemu ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali katika mitaa ya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6,2015. Katikati (mwenye vazi jeupe) ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy kutoka Makao Makuu ya Magereza, wa kwanza kulia ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Mbezi Ramadhani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga na wa kwanza kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Jamhuri Yassin kutoka Makao Makuu ya Magereza, Dar es salaam.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya kutembea katika viunga vya Manispaa ya Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6, 2015. Kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Vicent Magessa kutoka Gereza Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Mkaguzi wa Magereza Tumaini Kihampa na Mkaguzi wa Magereza Jamhuri Yassin wote kutoka Makao Makuu ya Magereza.
Maafisa na Askari na baadhi wa watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali ya kupita katika njia ngumu ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6, 2015. Wa sita kutoka mbele ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Estomiah Hamis na wa mwisho ni Mkaguzi wa Magereza Abas Mikidadi.

UFAFANUZI JUU YA HALI YA AFYA YA NAIBU SPIKA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai.

Rais Kikwete amtembelea Rubani wa ndegevita Hospitali ya Jeshi Lugalo

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakimjulia hali Meja Peter Lyamuya aliyelazwa katika hospitali kuu ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam akiuguza jeraha la mguu alilopata baada ya ndege ya kivita aliyokuwa akiiendesha kuanguka na kulipuka wiki iliyopita.Askari huyo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) alinusurika kifo baada ya kufanikiwa kujiokoa katika ajali hiyo iliyosababishwa na ndege mnyama kuingia kwenye injini na kusababisha hitilafu iliyopelekea kushika moto, kuanguka na kulipuka.Ndege hiyo ilikuwa katika mazoezi ya kawaida kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza.(picha na Freddy Maro).

Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images