Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

MISS UNIVERSE NALE BONIFACE ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) CHA SALVATION ARMY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akikata  keki na wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha  Salvation Army jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya  siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi  watoto hao.
 Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akiwalisha  Keki na wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakati  alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha  Salvation Army jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya  siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi  watoto hao.

 Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akitoa zawadi kwa mmoja wa  wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha  Salvation Army jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya  siku yake ya kuzaliwa
 Sehemu ya wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) katika  kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha  Salvation Army jijini Dar es Salaam
Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akigawa  madaftari kwa wanafunzi wenye mahitaji wakati alipotembelea  kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvation Army  jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya  kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi watoto hao.


TPB yaunganisha matawi yake na Mkongo wa Taifa

$
0
0
Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) akipokea hati ya mradi wa mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) toka kwa Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge (kulia). Mradi huo umeunganisha matawi ya benki ya TPB kimawasiliano ya kisasa. Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) akipokea hati ya mradi wa mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) toka kwa Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge (kulia). Mradi huo umeunganisha matawi ya benki ya TPB kimawasiliano ya kisasa.Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini. Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KUMBUKUMBU

$
0
0
MZEE RAPHAEL LEKAIKO TINGO
30 – 12- 1919 - 26 – 02 – 2007 

 Leo umetimiza miaka minane (8) tangu ulipoitwa mbinguni kwa Baba, baada ya kuugua kwa muda mfupi. Tunakukumbuka  kwa mengi sana hasa Upendo na Uchapakazi wako uliokuwa nao.

Baba, tupo kama ulivyotuacha – Imani yetu ni  kuwa ipo siku, wote tutakutana  tena Paradiso.

Unakumbukwa sana na mimi Mkweo JANE, Mume wangu OTTO na Familia yake Mkeo Mpendwa ROSALIA, wanao PANTALEO, FERDINAND, ESTOMII, MODEST, ERNEST NA ROSE, Wakwezo wote, Wajomba,Mashemeji, Wajukuu,Ndugu, Jamaa na Marafiki na wote wa Ukoo wa TINGO popote pale walipo Misa ya Kumuombea itafanyika Mkolani – Mwanza

KARIBU WOTE

“RAHA YA MILELE UMPE Eee BWANA…………………..”

Tume ya Kurekebisha Sheria nchini Uganda Yaitembelea Tume ya Tanzania

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akimkaribisha Kaimu Mwenyekiti wa Tume ya Uganda Bi. Vastina Nsanze na ujumbe wake.
Mwenyekiti wa Tume Mhe. Aloysius Mujulizi akiwa na ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria ya Uganda ofisini kwake.
Ujumbe wa Tume ukiongozwa na mwenyekiti Mhe. Aloysius Mujulizi ukiwa katika mkutano na wenzao wa Uganda unaoongozwa na Bi. Vastina Nsanze.
Ujumbe wa Tume ukiwa katika picha ya pamoja na wenzao wa Uganda (Picha zote na Munir Shemweta LRCT)

Washindi wa Promesheni ya Airtel yatosha Zaidi wakabithiwa magari yao

$
0
0
Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kulia), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa mshindi huyo, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 464 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Wakala wa Mtandao huo, John Fred Kiwale katika hafla iliyofanyika, Mtaa wa Togo, eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando na (kulia) ni Mke wa mshindi huyo, Anna Kiwale na motto wake, Sylvia John.
Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (katikati) akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Kondakta wa Malori, Jastini William Dodoo katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde.

Tamthilia ya "A Boys Mission" yahitaji Milioni 800 ili ikamilike

$
0
0
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana katikati akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye vituo vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Brian daniel, Neema Mung'anya, Samuel katabazi, Jesca haule, Aisha bakari na Victor Casmir.
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Forward Formidable Enterprises (FFE) inayoandaa tamthilia mpya na ya kisasa ya “A boys mission” Johnson Lujwangana akifafanua jambo kuhusiana na tamthilia hiyo itakayoanza kurushwa kwenye vituo vya televisheni kuanzia mwezi septemba. Wengine katika picha kutoka kulia ni Jesca haule na Aisha bakari.
Waigizaji wa tamthilia ya “A boys mission” inayoandaliwa na kampuni ya Forward Formidable Enterprises katika picha ya pamoja.

BEI YA MADAFU LEO

MAGOMENI MAPIPA YA LEO

$
0
0
Mambo yanazidi kuwa mswano jijini Dar,kwani kila kukicha mabadiliko yanaonekana.pichani ni Kituo cha Basi cha Magomeni Mapipa leo.
Inavyoonekana Magomeni Mapipa sasa.

Magomeni Mapipa kuelekea Kariakoo.
Vikwangua acha vya nguvu upande wa Kariakoo kutokea Magomeni Mapipa.

ZAIDI YA WAKUFUNZI (30) MKOANI MBEYA WASHIRIKI KATIKA SEMINA YA M-PAWA

$
0
0
Zaidi ya wakufunzi (30) wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya washiriki katika semina ya elimu ya kifedha na huduma ya M-Pawa inayolenga kuwanufaisha zaidi ya wakulima 140,000 Tanzania. Semina hiyo iliandaliwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) na Shirika lisilo la kiserikali la TechnoServe chini ya udhamini wa (USAID).
Mshauri wa biashara wa shirika lisilo la kiserikali la TechnoServe, Reginald Mpolo akitoa elimu kwa wakufunzi wa Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya (hawapo pichani) wakati wa semina iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania na Benki ya Afrika (CBA) hapo jana juu ya huduma ya M-Pawa inayolenga kuwanufaisha wakulima 140,000 Tanzania kupata Elimu ya M-Pawa na elimu ya kifedha. Semina hiyo ilidhaminiwa na (USAID).
Baadhi ya wakufunzi wa Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya wakimsikiliza Mshauri wa Biashara wa shirika lisilo la kiserikali la TechnoServe, Reginald Mpolo akitoa elimu wakati wa semina hiyo hapo jana iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) juu ya huduma ya M-Pawa inayolenga kuwanufaisha wakulima 140,000 Tanzania kupata Elimu ya M-Pawa na elimu ya kifedha. Semina hiyo ilidhaminiwa na (USAID).

NHIF KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOA YA PEMBEZI WA NCHI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kitabibu na Kitaalam wa NHIF,Dkt. Aifena Mramba (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akizungumzia juu ya huduma ya madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni.Kushoto ni Meneja Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF,Angela Mziray.

Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatarajia kupeleka madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni kwa ajili ya kutoa huduma za kitaalam kwa wakazi wa maeneo hayo.

Kupeleka kwa madaktari hao kunatokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali zikiwemo za uchache wa madaktari hao,umbali wa hospitali kubwa zenye huduma hiyo au changamoto za Kijiografia zinazozuia kufika kirahisi pamoja na za kimiundombinu.

PATO LA TAIFA LAONGEZEKA, LAFIKIA SHILINGI TRILIONI 21.2.

$
0
0
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Morrice Oyuke (Kulia)akitoa taarifa ya Pato la Taifa kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2014 leo jiji Dar es salaam. Pato hilo kwa mwaka 2014 limefikia kiasi shilingi trilioni 21.2 kutoka trilioni 19.8 za mwaka 2013, Kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Gregory Milinga, Picha na Aron Msigwa-MAELEZO.

Aron Msigwa –MAELEZO.

Pato la Taifa (GDP)  katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2014 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 21.2  kutoka shilingi trilioni 19.8  za kipindi kama hicho kwa mwaka 2013.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jiji Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Morrice Oyuke, amesema kuwa katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2014 sekta nyingi za uchumi zimefanya vizuri katika uzalishaji ikilinganishwa na mwaka 2013.

Balozi Seif Ali Iddi afanya ziara maalum ya kukagua shamba la Mkurunge,Bagamoyo

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Tanzania Bara Mh. Angela Kairuki akimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Wizara hiyo itasimamia kukamilisha taratibu zote zitakazothibitisha uhalali wa umiliki wa SMZ katika shamba la mifugo la Makurunge Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Kulia ya Naibu Waziri wa Ardhi Mh. Angela Kairuki ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
Ujumbe wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar uliotembelea shamba la Mifugo la SMZ la Makurunge waliangalia fukwe ya Bagamoyo iliyomo pembezoni mwa shamba hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kati kati na ujumbne wake wakifurahia fukwe safi iliyomo ndani ya shamba la Serikaliu ya Mapinduzi ya Zanzibar liliopo Makurunge. Kushoto ya Balozi Seif ni Meneja wa Shamba hilo Nd. Abdulrahman Hamid Mahmoud, wakati kulia ya Balozi Seif ni Katibvu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Nd. Afan Othman Maalim, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Waziri wa Kilimo Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwambioya na Naibu Waziri wa ARDHI Bara Mh. Angela Kairuki.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

MHE. CHIKU GALLAWA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WATEULE WA WILAYA ZA MKOA WA DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kulia) akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa Februari 25, 2015, anaeshuhudia katikati ni Katibu Tawala wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kulia) akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe Shabaan Kondo Kissu Februari 25, 2015, anaeshuhudia katikati ni Katibu Tawala wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge.

Tanzania na Zambia zadhamiria kufufua Reli ya TAZARA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Zambia kwa ajili ya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Edgar Lungu ( mwenye suti ya kijivu aliyesimama mbele ya Rais Kikwete)
Rais Lungu akimkaribisha Rais Kikwete (hayupo pichani kuzungumza)
Mhe. Rais Kikwete akizungumza wakati wa mazungumzo rasmi na Rais Lungu na Ujumbe wake katika Ikulu ya Zambia. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe na kulia ni Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YAANGAMIZA UNGA WA NGANO TANI 70 AMBAO HAUFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU

$
0
0
  Magari yakipakia Unga wa ngano mbovu katika godauni lililokuwa la Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) Mnazi mmoja, unga huo haufai kwa matumizi ya binadamu.
 Unga wa ngano mbovu tani 70 uliokamatwa ukiwa sokoni na mafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar ukimwangwa eneo la Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini ''B'' Unguja tayari kawa kuangamizwa.
 Kijiko likichukua mchanga kuchanganya na unga ulioharibika kwa lengo la kuangamiza katika kijiji cha Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini ''B'' Unguja.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Kijiko likichukua mchanga kuchanganya na unga ulioharibika kwa lengo la kuangamiza katika kijiji cha Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini ''B'' Unguja.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

JAHAZI MODERN TAARAB NA MASHAUZI CLASSIC JUKWAA MOJA MACHI 22 …ni Usiku wa Baba na Mwana

$
0
0
Hatimaye makundi mawili yanayoaminika kuwa na mashabiki wengi zaidi katika taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic yatafanya onyesho la pamoja mwezi ujao.
Onyesho hilo litafanyika Travertine Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam, Jumapili ya tarehe 22 mwezi Machi.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa makundi hayo mawili kufanya onyesho la pamoja (bila kushirikishwa makundi mengine).
Onyesho la kwanza lililopewa jina la Usiku wa Baba na Mwana lilifanyika miaka minne iliyopita ndani ya ukumbi huo huo na inaaminika kuwa hadi leo bado rekodi yake ya mahudhurio pale Travertine haijavunjwa.
Mzee Yussuf na Isha Mashauzi ambao ni wamiliki wa makundi hayo, wameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo ni “Usiku wa Baba na Mwana …Season 2”.
Viongozi hao wamesema onyesho hilo ni la kukuza udugu pamoja na kuwakutanisha pamoja mashabiki wao na kamwe halina hata chembe ya wala mpambano.

Dkt. Aziz Ponary Mlima awasilisha Hati za Utambulisho kwa Sultan wa Brunei Darussalam.

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Sultani wa Brunei Mheshimiwa Haji Hassanal Bolkiah Mu'izzaddin Waddaulah Ibin Al-Marhum Sultan Haji Omar 'Ali Saifuddien Sa'adul Khairi Waddien ambaye ni Sultan na Mtawala wa Brunei Darussalam, Kwa ufupi hii ni moja ya nchi zenye watu wachache, utajiri mkubwa wa mafuta na kiwango kizuri cha maisha ya wananchi wake wenye kipato cha wastani cha USD 43,000 kwa mwaka. Pato la taifa na uchumi unategemea zaidi mafuta na gesi na sekta zingine.
 Balozi Dkt. Aziz Mlima pia alifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mheshimiwa Paduka Seri Waziri Sahibul Himmah Mohamed Bolkiah na vile vile alionana na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje II Dato Seri Awang Lim Jock Seng na atakuwa na mazungumzo na Waziri wa Elimu Dato Seri Haji Awang Abu Bakar bin Haji Apong.
 Dkt. Aziz Ponary Mlima pamoja na mabalozi kutoka Afghanstan, Korea Kaskazini Palestine, Iraq, Spain na Ghana katika picha ya pamoja leo hii  bada ya kuwawasilisha Hati zao za Utambulisho na kuwa rasmi mabalozi wasio wakazi kwa nchi ya Brunei Darussalam.
 Balozi Dkt. Aziz P. Mlima na Naibu Balozi Bwana Rogatius Shao (kulia)   baada ya kuwasilisha hati za utambulisho leo

JK amtembelea Rais Mstaafu wa Zambia Mzee Kenneth Kaunda jijini Lusaka

$
0
0
 Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda akimkaribisha nyumbani kwake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete huko kijijini kwake Mkango Barracks, State Lodge nje ya jiji la Lusaka leo Dkt. Kaunda ambaye alimwalika Rais Kikwete alifanya naye mazungumzo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la mke wa Rais wa Kwanza wa Zambia Mama Betty Mutinkhe Kaunda huko Mkango Barracks,State lodge, nje ya jiji la Lusaka leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda(aliyesimama akiangalia) leo wakati alipomtembelea mwasisi wa taifa hilo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth David Kaunda nyumbani kwake  Mkango Barracks,State lodge, nje ya jiji la Lusaka leo.
 Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda akimpa zawadi Rais Dkt.Jakaya Kikwete
 Rais Dkt.Jakaya Kikwete akisindikizwa  na Rais wa Kwanza wa Zambia Mzee Kenneth Kaunda mara baada ya kumtembelea na kufanya naye mazungumzo leo
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiagana na Rais wa Kwanza wa Zambia Mzee Kenneth Kaunda mara baada ya kumtembelea na kufanya naye mazungumzo leo Picha na Freddy Maro

UTEUZI KATIKA TUME YA UTUMISHI WA UMMA NA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Katika uteuzi huo, Rais amemteua Mhe. DKT. STEPHEN JAMES BWANA, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma na BWANA EDRISSA R. MAVURA, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw. Mavura ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu.

Sambamba na uteuzi huu, Rais amewateua Makamishna katika Tume hizo, ambapo Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma ni:

(i)
Bwana George D. YAMBESI, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.  
(ii)
Alhaj Y. F. MBILA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.
    
(iii)
Bwana Mgeni Mwalimu ALLY, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma iliyomaliza muda wake.

(iv)
Bibi Adieu H. NYONDO, Mkurugenzi wa Maadili mstaafu.     
(v)
Bibi Salome S. MOLLEL, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu mstaafu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali    

(vi)
Bibi Evelyne ITANISA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.

Aidha Makamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ni:

(i)
Bwana Paul Herbert Kinemela, Kamishna wa Kazi, Wizara ya Kazi na Ajira  
(ii)
Bwana Mathias Bazi Kabunduguru, Mkurugenzi wa Uendeshaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
    
(iii)
Bwana Njaa Ramadhani Kibwana, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU).

(iv)
Bwana Jones Kyaruzi Majura, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Sekta ya Biashara na Viwanda – (TUICO).
(v)
Bwana Jaffari Ally Omari, Mwanasheria Kiwanda cha Sukari – TPC, na Kamishna wa Tume iliyomaliza muda wake.

(vi)
Bibi Suzane Charles Ndomba, Afisa Sheria wa ATE na Wakili wa Mahakama Kuu.

Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Februari, 2015.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

26 Februari, 2015
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images