Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110115 articles
Browse latest View live

MWIJAGE AZITAKA KAMPUNI ZA MAFUTA KUBORESHA MAHUSIANO

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (Kulia) akielekeza jambo kwa baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya Mafuta ya TIPPER alipotembelea Kampuni hiyo hivi karibuni wakati wa ziara yake kwa Kampuni mbalimbali zinazojishughulisha na biashara ya mafuta nchini.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (Wa pili kutoka Kushoto) akifuatana na baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO kukagua miundombinu ya kuhifadhia mafuta iliyoko eneo la Kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri alitembelea Kampuni mbalimbali zinazojishughulisha na biashara ya mafuta nchini kufanya mazungumzo na kukagua miundombinu inayotumiwa na Kampuni husika.
Meneja wa Kampuni ya Mafuta ya HASS nchini Tanzania, Ali Hassan Ahmed (Kushoto), akisikiliza maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (aliyeinua mkono) kuhusu utekelezaji wa mambo mbalimbali unaotakiwa kufanywa na Kampuni hiyo, hususan kujenga mahusiano mema na jamii. Wa kwanza Kulia ni Mbunge wa Temeke (Viti Maalum – CCM), Mariam Kisaka.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

Mh. Al Shaimar Kweigyir amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino)

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir, amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino,Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.

Katika ziaraa hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, Crencencia Joseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Bayport Financial Services mkoani Mwanza.

Wakiwa Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana nao alipata fursa ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Ersther ambaye ni wa Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha yake pamoja na kulia msiba wa mwanae.

Tukio la utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi limezidi kushika kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau, hususan wale wenye ulemavu wa ngozi wakiamini kuwa serikali imeshindwa kuwapatia ulinzi wa kutosha.

Akiwa jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba kwa ajili ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili kati ya watano waliobaki wakiwa ni albino.
Mbunge wa kuteuliwa Mh. Shaimar Kweigyir katikati akiwa na bibi wa Yohana Bahati (Tabu Maganiko) kulia ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyeuawa hivi karibuni mkoani Mwanza, huku mama yake akiachwa na majeraha makubwa wakati wanagombania mtoto katika tukio hilo la kusikitisha. Kushoto kwake ni Mweka Hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdullah Omari.
Katibu wa Mheshimiwa mbunge, Semeni Kingalu, kulia akipiga picha wakati walipomtembelea majeruhi Ester Maganiko, ambaye mtoto wake Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi aliuliwa katika tukio hilo la kusikitisha. Anayefuata ni Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Bugando na Clencencia Joseph, Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

COCA-COLA YAZINDUA UPYA MAJI YA DASANI

$
0
0

Kutoka kushoto ni Meneja wa Coca- Cola, Yebeital Getachew, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Basil Gadzios, Meneja Masoko wa Coca-Cola Kwanza, Hettiarachchi na Msimamizi wa Masoko Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa wakionyesha muonekano mpya wa chupa ya maji ya Dasani baada wakati wa uzinduzi. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Basil Gadzios akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuzindua upya maji ya Dasani.
Chupa ya Dasani inavyoonekana baada ya kuzindua upya maji ya Dasani.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Mh. Makalla aendelea na ziara jimboni kwake kwa usafiri wa bodaboda

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla ameendelea na ziara Jimboni kwake kwa kutumia usafiri wa pikpiki,na safari hii ameweza kufika kijiji cha Sewe ambacho kipo kilomita 35 toka kijiji cha Maharaka.

Kutokana na kutokuwepo kwa barabara nzuri za kuelekea kwenye kijiji hicho,Mh. Makalla aliamua kutumia zaidi ya saa moja kufika kijiji cha Sewe kwa kutumia usafiri wa pikipiki ili mradi awafikie wananchi wake.

Mara baada ya kuwasili kijiji hicho,wananchi walifurahi na bila kujizua walimpomgeza kwa kuwajali kufika kijiji na kujionea changamoto zinazowakabili.

Amewahaidi kuendelea kushirikiana nao katika kukabiliana na changamoto zilizopo kijijini hapo na amechangia mifuko 50 kwa ajili ya ujenzi shule ya msingi kijiji kipya cha Sewe.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa safarini kwenda kijiji cha Sewe, kwa kutumia usafiri wa pikipiki. 

Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa njiani kuelekea kwenye kijiji cha Sawe kilichopo kilometa 35 kutokea kijiji cha Maharaka,katika safari hiyo kuna baadhi ya maeneo alilazimika kushuka na kutembea kwa miguu kitokana na ubovu wa njia.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Sawe.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana waendesha bodaboda waliofanikisha ziara yake hiyo.

WANANCHI WA MKOA WA NJOMBE NI MFANO WA KUIGWA KATIKA ZOEZI LA BVR

$
0
0
Kazi ya kuandikisha wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kupitia mfumo wa Biometrick Voters Registration (BVR), ambao huhusisha uchukuaji wa alama za vidole na picha, jana iliingia siku ya tatu, huku baadhi yao wakipongeza utendaji wake.
Kwa mujibu wa ripoti iliyokusanywa na mwandishi wetu inasema kuwa tokea siku ya kwanza lilipoanza zoezi hilo lilionyesha matumaini maana wananchi wetu walijitokeza kwa wingi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi katika vituo vya uandikishaji, wananchi hao walisema kuna mabadiliko ukilinganisha na siku zilizopita, hivi sasa kazi zinafanywa haraka.
“Watu wanaokwenda kwenye vituo kujiandikisha idadi yao ni kubwa kuliko hata makadirio ya tume, kama hawataongeza muda au vifaa, siku saba walizopanga, hazitatosha na wengi wataachwa bila ya kujiandikisha,” alisema.
Baadhi ya waandikishaji na wasimamizi wa mashine wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuongeza muda ili kazi hiyo ifanyike kwa ufanisi zaidi.

RITA wazindua mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Wilaya ya Kinondoni

$
0
0
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni,Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkakati huo,akishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Iddi Azzan,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yussuf Mwenda,Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Phillip Saliboko pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty. Uzinduzi huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani,Magomeni jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni,Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani,Magomeni jijini Dar es salaam.Wengine pichani toka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Iddi Azzan,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yussuf Mwenda pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Phillip Saliboko.
 Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati) akimsikiliza Msajili wa Vizazi na Vifo (RITA) Manispaa ya Kinondoni,Mariam Ling'ande (kushoto) wakati akielezea juu ya namna RITA inavyotunza kumbukumbu,wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.Uzinduzi huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani,Magomeni.

Embrace e-commerce: Kaymu advises

$
0
0
Today technology is changing Tanzania - the way we work, communicate with each other, educate ourselves, buy goods and services and transfer money are done increasingly through the Internet, bringing convenience to our day-to-day routine How do we ensure Tanzania keeps pace with the global shifts toward e-commerce? What do we need to do to avoid being left far behind in this development? 

First, we should not only accept that technology is changing our way of life, but embrace that an increasing amount of our time in the near future will be spent conducting more business online. E-commerce commonly refers to any business conducted online, using any of a variety of websites and applications that rely on the Internet (such as e-mail, instant web messaging, social media, websites etc. This kind of trading can be between two businesses transmitting funds, goods, services or between a business and a customer.

For example, the online shopping space has become a source for buyers to do product comparisons and find out all the information they would ever want without setting foot in a store – offering buyers the complete satisfaction of a shopping experience without the hassle of visiting a market and window browsing store-by-store. People can now browse virtual marketplaces and online adverts on their favorite websites or even social media pages. 

AMBASSADOR TUVAKO MANONGI REMARKS AT THE THEMATIC DEBATE ON INTEGRATING CRIME PREVENTION AND CRIMINAL JUSTICE IN THE POST 2015 DEVELOPMENT AGENDA

$
0
0
The PR of the United Republic of Tanzania to the United Nations, Ambassador Tuvako Manongi speaking during a thematic debate on integrating crime prevention and the criminal Justice in the Post 1015 Development Agenda, the debate which was convened by the President of the General Assembly H.E. Sam Kutesa attended also by Depute Secretary General, H. E. Jean Eliason and other dignitaries was held on February 25h at the United Nations.
A Cross section of Member States, Observes and Stakeholders at the Thematic Debate on Integrating Crime prevention and Crime Justice in the Post 2015 Development Agenda. The debate was held on 25th February.

BMTL –COPY CAT TANZANIA LIMITED YAZINDUA MFUMO WA MITANDAO.

$
0
0
Mkuu wa Biashara za Kimtandao wa Copy Cat Tanzania Limited,Jonnavithola Prasad akizungumza na waandishi wa habari juu uzinduzi wa kifaa cha kuzuia wizi wa mtandao na jinsi walivyojipanga katika kutoa ushauri wa kifaa hicho katika hafla  hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam jana.
Mshauri wa Teknolojia na Biashara wa Copy Cate Tanzania Limited, Nathalie Ayonga akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya uzinduzi wa kifaa cha kuzuia wizi wa mtandao, hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam jana.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.


Kampuni ya Copy Cate Tanzania Limited wamezindua mfumo wa kuzuia wizi katika mtandao ambao una uwezo mkubwa wa kuzuia kwa mtu mmoja mmoja au kundi lililo katika mtandao mmoja.


Akizungumza na waandishi wa habari jana  katika ukumbi wa  Hoteli Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam,Mshauri wa Masuala ya Teknolojia ,Biashara,Naththalie Ayonga ,alisema  mfumo huo katika mitandao utasaidia taasisi za serikali  sekta binafsi  na mtu mmoja moja kuweza kudhibiti  wizi wa taarifa katika mitandao.


Ayonga alisema kampuni imekuwa ikifanya kazi za mafanikio katika mfumo wa mabadiliko wa teknolojia kwa kuweza kufanya ingiaji wakati uzinduzi wa kimfumo katika karne ya 21 ya sayansi na Teknolojia.


Alisema kifaa hicho cha kuzuia wizi wa taarifa katika mitandao  wa mfumo huo kimekuja kwa wakati mwafaka kwa Tanzania kutokana na kuwepo watu wengi kuingia katika teknolojia za mitandao bila kuwa na ulinzi.


Kifaa cha mfumo kinajulikana kama Cisco ambacho kimekuwa na chachu kudhibiti wizi katika mitandao hivyo ni fursa ya watazania kupokea katika kulinda taarifa zao zisiingiliwe na mtu mwingine.



Kampuni ya Copy Cat Tanzania Limited  ndio itakuwa inafanya masuala ya kifumo katika mitandao na uingizaji wa bidhaa mpya  na ambayo ilikuwa ikifanyw na BMTL.

WAKUTANA KUJADILI MKAKATI WA MRADI WA KIJIJI CHA DIGITALI

$
0
0
DSC_0113
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada ya mchanganuo wa ufumbi wa changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali.

Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
WADAU mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi ambao wamo katika mradi wa kijiji cha dijiti cha Ololosokwan kilichopo wilayani Monduli Arusha wanakutana kwa warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji hicho nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Al Amin Yusuph warsha hiyo imelenga kuangalia changamoto na namna ya kuzitatua ili mradi kuwa na tija kwa wananchi wake.
Yusuph alisema kwamba wadau hao wanapanga mkakati kuangalia vipaumbele na changamoto katika utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitatu.
DSC_0141
Mwenyekiti wa kikundi cha elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta akishiriki kutoa maoni wakati wa warsha hiyo inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani. Aliyesimama ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.

Vacancies for Employment at Muhimbili National Hospital

MAANDALIZI YA KILIMANJARO MARATHONI YAPAMBA MOTO,KLABU YA RIADHA YA HOLILI YAPELEKA WANARIADHA WAKE MAZOEZINI KENYA

$
0
0
Mkurugenzi wa klabu ya riadha ya Holili (HYAC) Domician Genand akizungumza juu ya maandalizi ya mbio za kimataifa za Kilimanjaro Maratahoni kwa wanariadha wake ambao baadhi yao amewapeleka nchini Kenya kwa ajili ya mazoezi.
Baadhi ya wanariadha walioko katika kambi ya klabu ya riadha ya Holili wakicheza Draft ambapo miongoni mwao yumo mkimbiaji wa Kimataifa ,Osward Levelian ambaye anajiandaa na Mbio za Marathoni kilometa 42 zitakazofanyika nchini Nchina hivi karibuni.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MKURANGA WAPATA MSAADA WA MADAWATI

$
0
0
 Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Mkuranga,Benjamini Majoya akipokea msaada  uliotolewa na Kampuni ya Upendo Media Group,Benki ya Maendeleo na Fifa Flow Limited kwa  Mteule Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani,Chediel Luiza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya Azania Front Jijini Dar es Salaam. 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.


AFISA Elimu Sekondari,Wilaya ya Mkuranga Benjamini Majoya amekishukuru Kituo cha Radio cha Upendo pamoja na gazeti la Upendo kwa kutoa habari za Wilaya ya Mkuranga na kupata msaada wa madawati pamoja na sare za shule kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.


Majoya ametoa shukrani hizo wakati akikabidhiwa madawati 40 na sare kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu iliyofanyika leo katika viwanja vya Azania Front jijini Dar es Salaam.


Madawati na sare kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu zimetolewa na Benki ya Maendeleo ,Kampuni Fifa Flow Limited pamoja na Kituo cha Radio Upendo pamoja gazeti la upendo.


Msaada huo umetokana na Kituo cha Radio Upendo pamoja gazeti la upendo kwenda katika Wilaya ya Mkuranga kutafuta habari na kuona kuna umuhimu wa kupata msaada wa madawati pamoja sare kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.


Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Maendeleo, Ibrahimu Mwangaraba amesema wanatambua umuhimu kama benki kuwa wanaowasaidia watakuwa ni wateja wa benki yao,wengine ni viongozi mbalimbali ambao watasaidia maendeleo.

NEWS ALERT: NDEGE YA JWTZ YAPATA AJALI JIJINI MWANZA LEO

$
0
0
Ndegevita moja ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiteketea kwa moto huku jitihada za kuuzima zikiendelea katika ajali iliyotokea leo Februari 27, 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,  Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto. 

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda  alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu. 


Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Familia ya Marehemu Mzee Lwanda na Mama wa Nyasa - Ruvuma wanasikitika kutangaza kifo cha kijana wao mpendwa Samwel Lwanda (SAM Macheni) kilichotokea tarehe 25/02/2015 katika hospitali ya Regency jijini Dar es salaam kwa kuugua gafla. Marehemu alikuwa mwajiriwa katika manispaa ya jiji la Mbeya. 

Kwa mujibu wa msemaji wa familia marehemu ataagwa leo nyumbani kwake maeneo ya Boko jijini Dar es lsaam na kwenda kuzikwa Mkoani Tanga (Tanga mjini) siku ya kesho ya tarehe 28/02/2015. 

Kwa mawasiliano zaidi piga namba: 
Arch asahel

Blog yenu inatoa pole kwa wale wote waliofikwa na msiba huu, tunasema tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. 
Amen

RAIS KIKWETE ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Masaki jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea Msaki jijini Dar es salaam leo walipofika heshima zao za mwisho kwa mama yake mzazi Marehemu Esther Gigwa Hosea huko Masaki jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghariv Bilali, Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiwa pamoja na wafiwa wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Masaki jijini Dar es salaam leo.
Sehemu ya wafiwa na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Masaki jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

Waziri wa afya ahudhuria Kongamano la AFRIKA HEALTHCARE SUMMIT 2015 JIJINI LONDON

$
0
0
Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dkt. Seif S.Rashid (MB) mwenye tai nyekundu mstari wa mbele  akiwa katika sherehe ya ufunguzi ya kongamano hilo. Katika  ni msajili wa baraza la wafamasia lililo chini ya wizara ya afya na ustawi wa jamii Bi.Elizabeth Shekelaghe na wa kwanza kushoto ni Dkt.Mariam Ongalla, mratibu wa kitengo cha "Public Private Partinership" kutoka wizara ya Afya na ustawi wa Jamii.

Wafanyakazi wa Airtel wachangia kuboresha mazingara ya shule ya msingi Ushindi

$
0
0
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa “AirtelTunakujali” wakishirikiana na wafanyakazi wa kitengo cha Airtel Biashara za Mashirika wameendeleza dhamira ya kusaidia jamii kwa kukarabati darasa la chekechea katika shule ya msingi Ushindi iliyopo jijini Dar Es Salaam. 
 Airtel imeendelea kushirikiana na wafanya kazi wake kutoa mchango kwa jamii kwa kuhakikisha shule zinakuwa na miundombinu na mazingira bora ya kujifunza hali itakayochochea wanafunzi kupenda shule. Uchakavu wa miundombinu ya shule hasa za msingi nchini ikiwemo vyumba vya madarasa ni moja ya chanzo kikuu kinachodhoofisha mahudhurio ya wanafunzi na hivyo kusababisha matokeo yasiyoridhisha. 
 Mwishoni mwa wiki wafanyakazi wa kitengo hicho walishiriki ukarabati wa darasa hilo la chekechea katika shule ya msingi Ushindi lenye kuhitaji marekebisho makubwa ambayo yanatazamiwa kuongeza hamasa ya watoto kuhudhuria shuleni. 
 Akizungumza katika tukio hilo mwalimu Mkuu wa Shule ya hiyo Bw Iddi Kaminja alisema, "tumekuwa na changamoto kubwa mahudhurio kutokana na wanafunzi kutokufurahia kuja shuleni na hii inasababishwa na shule kuwa na miundombinu chakavu isiyowapa ari ya kusoma.
"Tangu mpango huu wa ukarabati ulipotangazwa wanafunzi wamekuwa na shauku kubwa ya kutaka zoezi hili liweze kuisha na kuanza kutumia darasa hili. Hali hii limekuwa faraja kwetu hivyo ni wazi kwamba itatusaidia kuongeza kiwango cha mahudhurio shuleni na hatimaye kuongeza kiwango cha elimu hapa shuleni."Aliongeza Mwalimu Kaminja 
 Aidha Mwalimu Kaminja ametumia fursa hiyo kuwapongeza wafanayakazi wa Airtel kwa moyo wao wa kujitolea kwa hali na mali kuinua kiwango cha elimu ya awali na kutoa rai kwa makampuni mengine kuona umuhimu wa kuborosha madarasa ya shule za awali na msingi kwani njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu hapa nchini ni kuwapa watoto wetu mazingira mazuri na yenye usalama wawapo hapo shuleni. 
 Nae meneja wa Airtel wa huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema,"madarasa mazuri ni muhimu kwa usalama wa wanafunzi lakini pia huleta hamasa ya mahudhurio hivyo ni lazima wazazi wawe tayari kusaidia hatua za haraka kufanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuepusha hatari na gharama kubwa ya fedha. Kwa njia hiyo madarasa haya yatadumu.
"Leo tumeshiriki zoezi hili katika shule ya msingi ya Ushindi lakini kazi hii imekuwa ikifanyika sehemu mbali mbali nchini kupitia mradi wa “Airtel Tunakujali” ambao unawawezesha wafanyakazi wa Airtel nchi nzima kushiriki katika shughuli za kijamii hususan zinazoinua sekta ya elimu Tunajisikia furaha kuwekeza katika jamii kwa kiwango ambacho kinaleta tofauti kubwa. 
Siku zote tumelenga kufikisha huduma bora na za gharama nafuu kwa watanzania huku tukitambua na kupambana na changamoto mbalimbali za jamii inayotuzunguka.  
"Leo nanyi mnashuhudia utofauti wetu na makampuni mengine, Airtel sio tu inaongoza katika mtandao ulio bora hapa nchini bali pia namna tunavyojali wanaotuzunguka" aliongeza Bayumi.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakiupamba ukuta kwa viganya vya mikono vilivyopakwa rangi nyekundu wakati waliposhiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es
Salaam.
 Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakishiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni
‘B’, jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakishiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni
‘B’, jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, Kitengo cha Biashara za Mashirika, wakigawa zawadi kwa watoto wa chekechea baada ya kushiriki kupaka rangi darasa la Chekechea linalokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’,  jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KUHUSU KUIDHINISHWA KUTUMIKA KWA AINA MPYA ZA MBEGU ZA MAZAO

$
0
0
Naibu Natibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chula na Ushirika Dkt.Yamungu Kayandabila (wa kwanza kushoto)  akiongea na vyombo vya habari wakati wa kuidhinisha aina mpya 65 za mbegu za kilimo katika mkutano uliofanyika hivi  karibuni katika  ukumbi wa New Safari  hotel ya mjini Arusha.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Viewing all 110115 articles
Browse latest View live




Latest Images