Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 752 | 753 | (Page 754) | 755 | 756 | .... | 3286 | newer

  0 0

  KAIMU MENEJA WA SIDO MKOA WA IRINGA, MR NIKO MAHINYA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFINI KWAKE

  NA FRANK KIBIKI, IRINGA
  SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa limewataka watanzania kujenga utamaduni wa kupenda bidhaa zinazotengenezwa ndani, badala ya zile zinazoingizwa kutoka nje ili kukuza uchumi wan chi.


  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, Kaimu meneja wa SIDO mkoani Iringa, Niko Mahinya alisema ikiwa watanzania wataenzi bidhaa zinazotengenezwa ndani itakuwa rahisi kuinua uchumi wa nchi, na mtu mmoja mmoja.


  Alisema shirika hilo limekuwa likitengeneza bidhaa nyingi, zikiwemo mashine na pembejeo za kilimo lakini, kutokana na dhana ya kununua bidhaa za nje wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la soko.


  “Tunazalisha mashine mbalimbali, zikiwemo zana za kilimo kama vile, mashine za kusagia nafaka, kuchujia mafuta ya alizeti, kukamulia asali na nyingine nyingi lakini changamoto kubwa ni soko la bidhaa za ndani,”alisema.


  Aidha alisema itakuwa vyema kama serikali itaweka utaratibu au sera itakayofanya watu wajenge tabia ya kuheshimu, kupenda na  kutumia bidhaa za ndani.


  Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali na wakulima walisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakinunua mashine za kichina kutokana na bei yake kuwa chini ingawa hazina ubora.


  “Bidhaa za nje ni bei ndogo kuliko zile zinazotengenezwa ndani, hii ndiyo sababu inayofanya wengi tutumie bidhaa za kichina ambazo hata hivyo hazidumu kwa muda mrefu,”alisema LeoniKA Sanga, mmilikiwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, mjini Iringa.


  Aliiomba serikali kutoa ruzuku kwa SIDO ili bidhaa zinazotengenezwa zishushwe bei yake na kuweza kuwahudumia wajasiriamali na wakulima wadogo.
  MSIMAMIZI WA KARAKANA YA KUTENGENEZEA MASHINE MBALIMBALI YA SIDO MKOANI IRINGA, LEONARD LUMATO AKIENDELEA NA KAZI KATIKA KARAKANA HIYO

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (katikati) akiwa katika kikao kilichojumuisha watendaji wa TANESCO, REA, na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Kulia kwa Waziri ni, Mhandisi Nishati Mwandamizi, kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Salum Inegeja na kushoto ni Mhandisi Thomas Visi, Meneja wa kampuni ya Naomis Corporate Ltd inayotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini katika mkoa wa Mtwara.
  Mhandisi Mkuu Usambazaji Umeme katika mikoa ya Dar es Salaam, Benedict Lyaruu (wa kwanza kulia), Kaimu Meneja wa TANESCO, mkoa wa Pwani, Eng. Rehema Mashinji (katikati) na Mhandisi Miradi ya Umeme katika mkoa wa Pwani, Leo Mwakatobe (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (haonekani pichani) wakati wa kikao chake na watendaji wa TANESCO, REA, na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini katika miko ya Lindi na Mtwara.


  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora,ACP Suzan S. Kaganda akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) silaha zilizokamatwa na Jeshi la Polisi mkoani humo katika Opereshen kali iliyokuwa ikifanyika. ambapo walikamatwa watuhumiwa watano wakiwa na silaha hizo aina ya SMG mbili No AB-018-0414 na EE 125419 zikiwa na risasi 25 na Gobore tatu,baruti na goroli pamoja na vipande vya nondo.Watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo ya Igunga,Kaliua na Sikonge mkoani Tabora.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora,ACP Suzan S. Kaganda akiongea na waandishi wa habari waandishi wa habari (hawapo pichani).
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora,ACP Suzan S. Kaganda akionyesha sare za JWTZ zilizokamatwa kwa watuhumiwa hao.


  0 0

  Shule tatu za msingi katika mkoa wa Singida,zitapokea vitabu 200 wiki hii kusaidia katika mchakato wa kuboresha elimu ya shule ya msingi. Vitabu hivi vimetolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Children’s Book Project for Tanzania na italenga maelfu ya watoto nchini kote katika kuwakomboa kielimu.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo,Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali alisema kuwa Watoto wanaotakiwa kupata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu.

  "Watoto wanaopata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu. vitabu hivi vinatolewa kwa watoto ili waweze kutumia katika masoma yao ya kila siku shuleni.” alisema Ramadhani

  Msaada huu wa vitabu umejikita katika kukomboa hali ya elimu Tanzania, huku serikali ikijitahidi kuwekaza katika elimu nchini kwa kipindi kirefu. Inakadiriwa kuwa asilimia kubwa ya watoto wa shule ya msingi Tanzania hawajui kusoma na kuandika,Ukosefu wa vitabu unachangia wanafunzi wa shule ya msingi kushindwa kusoma na kuandika.

  Tafiti mbalimbali kutoka za serikali na sekta binafsi zinaonyesha wazi kuwa kujifunza kusoma mapema ni uwekezaji katika siku zijazo kwa mtoto,kwani elimu katika ngazi ya chini kwa mwanafunzi inachangia kuboresha maisha yake ya baadae.

  Kwa upande wake Doris Mollel ambaye ni Balozi wa Elimu mkoani Singida anatambua umuhimu wa elimu katika ngazi ya chini na anatumia muda wake mwingi katika harakati za kukomboa elimu ya shule ya msingi. Ziara zake nyingi hujikita katika mikoa ya ukanda wa kati hususani Singida na Tanzania kwa ujumla,Vile vile ni mshauri wa wanafunzi wa shule za msingi.

  "Msingi wa kujifunza kusoma hufungua uwezo wa kufikiri kwa mwanafunzi akiwa na umri mdogo bila kiini hiki cha msingi maendeleo na mafanikio ya mwanafunzi ni magumu.” alisema Doris

  Doris Mollel ni Miss Singida kanda ya kati 2014/15 na analenga katika kuboresha maisha ya jamii kwa kupitia elimu na masuala mengine ya kitamaduni.
  Miss Singida kanda ya kati 2014/15,Doris Mollel akisikiliza jambo kutoka kwa Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali wakati akipokea vitabu kutoka Children’s Book Project for Tanzania. 

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA NISHATI NA MADINI


  TANGAZO.


  MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI.

  Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika. Halmashauri zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014. 

  Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement - MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali.  Mha. Ngosi C.X. Mwihava

  KAIMU KATIBU MKUU


  25Februari, 2015


  0 0

    Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akishangiliwa na wafanyabiashara wenzake sokoni hapo, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota
  IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana.
   Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akikabidhi mfano wa ufunguo wa  gari kwa mshindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi, Grace Pascal Kalengela  wakati wa  kumkabidhi  gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni mume wa mshindi huyo, Daudi Mayunga na (kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
    Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akiwa mwenye furaha, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783
  DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.

  0 0

  Kocha Msaidizi wa Timu ya Coastal Union,Jamhuri Kiwelu "Julio" (wa pili kulia waliosimama) akisisitiza jambo kwa wachezaji wa timu hiyo wakati wa mazoezi mara baada ya kuwasilia mkoani Tanga kuifundisha timu hiyo akisaidiana na Kocha Mkuu James Nandwa ( wa nne kushoto).wengine pichani ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Coastal Union,Albert Peter,Katibu Mkuu Coastal Union,Kassim El Siagi na Meneja wa Coastal Union Akida Machai.
  Kocha Msaidizi wa Coastal Union ,Jamhuri Kiwelu "Julio"akizungumza na viongozi wa Coastal Union mara baada ya kuwasili mazoezini jana ,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.

  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akiongea na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam jana (Jumanne, Feb 24, 2015). Kulia kwake ni Naibu Waziri Ummy Mwalimu na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Wakili Bahame Tom Nyanduga na Katibu Mtendaji Bi. Mary Massay. Waziri alifanya ziara katika ofisi za Tume hiyo kubadilishana mawazo na uzoefu.
  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu wake Ummy Mwalimu wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam jana (Jumanne, Feb 24, 2015). Waziri alifanya ziara katika ofisi za Tume hiyo kubadilishana mawazo na uzoefu. Picha na Farida Khalfan, Wizara ya Katiba na Sheria.

  Na Martha Komba
  Serikali imeiagiza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRGG) kuibua masuala yanayoathiri uzingatiaji wa haki za binadamu ili hatua stahiki zichukuliwe na hivyo kuboresha misingi ya haki na utawala bora nchini.

  Akizungumza na viongozi wa Tume hiyo jana (Jumanne, Feb. 24, 2015) jijini Dar es Salaam, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Asha–Rose Migiro alisema Serikali ina wajibu wa kuzingatia haki za binadamu katika utekelezaji wa majukumu yake na hivyo na hivyo ni muhimu kwa Tume kuibua na kutoa taarifa juu ya masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto, aliyekaa) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia, aliyekaa), wakitia saini mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia huduma ya M-Pesa na Tigopesa. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (wa pili toka kushoto) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, wakibadilishana nakala za mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia huduma ya M-Pesa na Tigopesa, wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga.


  0 0

  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akisalimiana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Simba alipowasili MKOANI Tabora leo kwa ajili ya ziara ya kutembelea Mahakama mkoani humo.
  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akisalimiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Bi. Suzan Kaganda alipowasili mapema Leo mkoani Tabora kwa ajili ya ziara.
  Baadhi ya Watumishi wa Mahakama mkoani Tabora wakisubiri kumpokea Mhe. Jaji Mkuu .
  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akipata Maelezo mafupi kutoka kwa Mhe. Amir Mruma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu (aliyesimama) Kanda ya Tabora alipowasili katika jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kuanza rasmi ziara yake ya kikazi. Wengine walioketi ni Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora. (Picha na Mary Gwera, Mahakama).

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Zambia Michael Sata aliyefariki mwaka jana katika eneo la maziko ya viongozi wa kitaifa jijini Lusaka Zambia leo.Rais Kikwete alitumia  wasaa huo pia kuweka shada la maua katika marais wa Zambia waliofariki Marehemu Frederick Chiluba na Levy Mwanawasa. Picha na Freddy Maro

  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kutangaza kusitishwa kwa muda huduma ya treni ya Jiji  kuanzia leo  Jumatano jioni Februari 25 hadi  Jumatatu  Machi 02, 2015 itakapoanza tena.

  Kwa mujibu  wa taarifa ya Uongozi wa TRL iliotolewa jioni  leo Februari 25,  2015 uamuzi wa kusitisha huduma hiyo umesababishwa  na vichwa  viwili vya treni hiyo kuharibika na kuhitaji matengenezo makubwa katika Karakana Kuu ya Morogoro .
  Taarifa imefafanua kuwa kwa vile kimebaki  kichwa kimoja huduma hiyo haiwezi kuendelea hadi vichwa hivyo viwili vitakapo maliza kukarabatiwa siku ya Jumamosi huko Morogoro.
  Kwa kawaida treni ya Jiji hutumia vichwa  viwili wakati inapotoa huduma kati ya stesheni za Ubungo Maziwa na Stesheni kuu ya Dar, wakati kile  cha tatu huwa cha akiba endapo dharura itakipata kichwa kimoja wapo  wakati huduma inaendelea.
  Aidha Uongozi wa TRL unawaomba  radhi wateja wake na wananchi  kwa jumla hasa wa eneo la Jiji waliokuwa wamezoeya kupata huduma hiyo kila siku kwa  usumbufu  utakajiotekeza .
  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
  Mkurugenzi Mtendaji ,
  Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
  Dar es Salaam,
  Februari  25, 2015

  0 0
  0 0

  Na Mwene Said wa Blog ya Jamii, Dar es Salaam

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeambiwa na Naibu Kamishna wa Polisi, Kamanda Simon Siro (54), ambaye amedai mahakamani kwamba alitoa zuio la kuandamana kwenda Ikulu kwa Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha) kwa sababu maandamano hayo yangesababisha uvunjifu wa amani.

  Alitoa madai hayo, wakati akitoa ushahidi dhidi ya Mbunge Halima Mdee na wenzake, kwamba baada ya kupitia vigezo vya kiusalama, njia waliyotaka kuitumia kufanya maandamano hayo inatumika na watu wengi hivyo nilishughulikia mara moja kuzuia maandamano hayo.

  Kamanda Siro ambaye pia ni Mkuu wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  alitoa madai hayo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda.

  Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka akisaidiana na Salum Mohamed Inspekta wa Polisi Jackson Chidunda.

  Akiongozwa na Kweka, shahidi huyo alidai kuwa Oktoba 2, mwaka huu alipokea barua iliyopitia kwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kutoka Bawacha wakiomba kufanya maandamani ya amani kwenda Ikulu.

  “Katika barua hiyo Bawacha waliomba kufanya maandamano kwenda Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kumtaka asipokee katiba inayopendekezwa… maandamano hayo yalipangwa kufanyika Oktoba 4, mwaka 2014 saa 3:00 asubuhi”alidai Kamanda Siro.

  Akifafanua zaidi alidai kuwa "niwaagiza wafuasi wangu kwenda kukagua njia waliyotaka kuitumia lakini kwa bahati mbaya haikuwa salama kwa sababu ingeweza kusababisha  uvunjifu wa amani".

  Alidai kuwa kwa nafasi yake anasimamia vikosi vyote vya kupambana na uhalifu kwa Kanda Maalum, kwa hiyo nilishughulikia mara moja kwa kuwajibu Bawacha kwamba maandamano hayo yasifanyike kwa sababu za vigezo vya kiusalama.

  Aidha, Kamanda Siro aliomba mahakama ipokee nakala ya barua hiyo kama kielelezo lakini yalitokea mabishano ya kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 3, mwaka huu ushahidi utakapoendelea kusikilizwa.

  Mbali na Mdee, washtakiwa wengine ni,Rose Moshi , Renina Peter maarufu kama Lufyagila, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fangel,  Edward Julius, Martha Mtiko na Beatu Mmari.

  Katika kesi ya msingi, washitakiwa hao wanadaiwa  Oktoba 4,mwaka 2014, katika mtaa wa Ufipa, bila kuwa na uhalali walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi Emmanuel Tille kwa niaba ya Jeshi la Polisi.

  Pia wanadaiwa siku hiyo walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo moja la kutembea kwenda ofisi ya Rais Kikwete.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Busega na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (mwenye shati la kijani) akitoa mchango wa saruji mifuko 70 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa shule ya msingi Nyamajashi iliyopo mjini Lamadi katika Jimbo la Busega.
  Mbunge wa Jimbo la Busega na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akiwahutubia Wananchi waliohudhuria kwenye hafla hiyo.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(suti nyeusi) akijiandaa kukata utepe kwenye hafla ya Ufunguzi wa Jengo la "Rest House" ya Magereza leo februari 25, 2015 Mkoani Morogoro ambapo ukarabati wa Jengo hilo umefanyika chini ya Kikosi cha ujenzi cha Jeshi la Magereza(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akisoma jiwe la msingi mara baada ya ufunguzi wa Jengo la "Rest House" ya Magereza leo februari 25, 2015 Mkoani Morogoro.


  0 0


  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na vingozi wa serikali wakati alipowasili katika soko la mwanjelwa Februari 25,2015 tayari kwa uzinduzi wa soko hilo ambalo linaloendelea kujengwa jijini Mbeya.Picha na Fadhil Atick,Globu ya Jamii.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wakazi wa mji wa Mbeya mjini mara baada ya uzinduzi wa Soko la Mwanjelwa.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akipewa maelezo mafupi ya maendeleo ya soko hilo kutoka kwa mkandalasi wa ujenzi wa Soko hilo.
  Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya,Mh. Mary Mwanjelwa akizungumza machache.
   

  0 0

  Na   Bashir   Yakub.

  Hapa kwetu Tanzania  habari ya kubambakiziana kesi ni kama mtindo. Mara nyingi matendo haya yamekuwa yakifanywa na watu wenye uwezo  kifedha dhidi ya wasio na fedha  pia kati ya  maofisa wa polisi na raia. Mtu kwasababu ana pesa au cheo anaweza kuamua  kumfungulia yeyote mashtaka.  Watu wengi wako magerezani kwa kubambikizwa kesi, hili wala sio siri tena. Siseme walio mahabusu, hao nao hawana idadi. Inasikitisha mno. Ni wazi kuwa wengi wao wamefikia huko aidha kwa kusingiziwa kosa na askari au mtu mwenye cheo au  fedha. Lakini zaidi wametoka mikononi mwa askari kwakuwa hata huyo mwenye cheo au fedha hawezi kumbambikizia  mtu kesi  bila kupitia kwa askari. Kwahiyo askari  ndio  tatizo  kubwa  katika  hili.

   1.NINI  MAANA  YA   KUBAMBIKIZWA   KESI.

  Kubambikizwa kesi au kumshtaki mtu kwa  hila  maana yake ni kumfungulia mtu kesi ya jinai  bila  mafanikio , na bila sababu za msingi za kufanya hivyo  na mtu huyo  akapata  athari zozote kutokana na kumfungulia kesi hiyo. Athari ni pamoja  na kupotezewa muda, gharama, usumbufu, kudhalilishwa, kupata hasara kibiashara au kikazi kutokana na kushikiliwa na kila kitu ambacho kimekuwa kama  matokeo ya kusingiziwa kesi  ni athari kwa maana hii.

  2. SABABU   ZA   KUWABAMBIKIZA  WATU   KESI.

  Sababu  za kumuuzia mtu kesi  huwa ni nyingi. Ni  nyingi  kutokana  na kuwa kila aliyebambikizwa  kesi huwa kuna mgogoro nyuma uliosababisha  jambo hilo  na migogoro  kawaida inatofautiana. Pamoja  na hayo sababu  kuu  za kubambikizia  mtu kesi huwa ni kwa ajili ya kumkomoa  au kulipiza kisasi kutokana na chuki zilizotokana na mgogoro  kama  nilivyosema.

  3. WELEDI  WA ASKARI WETU  NA KUWABAMBIKIZIA  RAIA KESI. 

  Wakati  mwingine  askari  wetu  huwabambikizia  watu kesi  katika  mazingira  ya  kushangaza kabisa. Askari  anaweza  kumbambikizia  raia  kesi  kwasababu  tu  raia  amehoji  jambo  fulani. Kwa mfano mtu anaweza kumuuliza askari nioneshe  kitambulisho  chako kabla  hujanikamata. Utasikia  askari akimwambia  mtu unajifanya  mjuaji tutaona, mara unanifundisha  kazi utanitambua n.k. Eti mazimgira kama hayo kwa askari wetu utakuwa tayari  ni mgogoro  na  mtu atapofikishwa  kituoni  basi ni rahisi  kupewa  kesi ambayo si  yake  ilimradi tu askari  aoneshe  kuwa aliposema  utanitambua, utaona  alikuwa  na uwezo  wa kufanya  hivyo  kweli.


  0 0

  Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali, akipata picha ya pamoja na Bw. Erastus Mwencha, Naibu Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, baada ya mapokezi kwa ziara yake maalum, siku ya Jumatano Feb 25, 2015 ndani ya  Washington Dulles International Airport.( Picha na swahilivilla.blogspot.com
  Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali. akiwa na Bw. Erastus Mwencha, pamoja na Shamis Alkhatry baada ya mapokezi.
  Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali, akiwa na Bw. Erastus Mwencha, pamoja na Cheif wa swahilivilla blog  Abou Shatry, siku ya Jumatano Feb 25, 2015 ndani ya  Washington Dulles International Airport 

  0 0

  Mkutano uliowakutanisha Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki wakiwemo Mabalozi wa nchini zao nchini Marekani ulifanyika Februari 25, 2015 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, mkutano huo  uliohusiana na maandalizi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi ya Marekani na nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.

  Mkutano huo uliongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  Balozi   Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

  Washiriki wengine kwenye mkutano huo kutoka Tanzania walikua ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Usafirishaji Mhe. Samwel Sitta, Maria Bilia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Amantius Msole, Naibu Katibu Mkuu  MEAC Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

  Washiriki kwenye mkutano huo kutoka Burudi walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Burundi Mhe.Mzigiyimana Marie Rose, Balozi wa Burundi nchini Marekani Mhe. Ndabashinze Ernest, Ntibarutaye Glorioje ambaye ni mshauri ofisi ya Wizara ya Biashara ya Burundi, 

  Wawakilishi kutoka Kenya walikuwa ni James  Kiiru amabaye ni Mkurugenzi masaidizi MFA & IT Kenya, Balozi  Nelson Ndirangu ambaye ni mkurugenzi  MFA & IT Kenya, Bi.  Phylus Kandie Cabinet Secretary MEACT Kenya, Ronnie Gitonga Naibu Katibu Ubalozi wa Kenya nchini Marekani na Esther Chemirmir  PA to CS MEACT Kenya.

  Wawakilishi kutoka Uganda walikua ni Balozi wa Uganda nchini Marekani Mhe. Alfred  Nwam na Stilson  Muhwezi. Rwanda waliwakilishwa na Waziri wa Bisahara na Viwanda Mhe. Robert Opirah na Innocent Kabandana.

  Mkutano huo ni mwendelezo wa ule mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana nchi ya Marekani ilipowaalika Marais wa Afrika katika mkutano kama huo ulioongozwa na Rais Barack Obama.

  Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti wa mkutano wa kujiandaa kutiliana saini makubaliano ya biashara na uwekezaji wa nchi za Afrika Mashariki na Marekani. Utiliano saini huo utafanyika Alhamisi Februari 26, 2015 katika Ofisi za Wizara ya Biashara Marekani, kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

  Ujumbe wa Tanzania.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 752 | 753 | (Page 754) | 755 | 756 | .... | 3286 | newer