Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 73 | 74 | (Page 75) | 76 | 77 | .... | 3348 | newer

  0 0

  KIINGILIO MECHI YA STARS, MOROCCO 5,000/-
  Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani.


  Viti vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000 viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 ni sh. 10,000.


  Viingilio vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.


  Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku mbili ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni na Dar Live Mbagala.


  Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Vilevile tunapenda kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi hiyo.


  SAMATA, ULIMWENGU WARIPOTI STARS.
  Washambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili nchini jana usiku na kwenda moja kwa moja kambini.


  Ujio wa washambuliaji hao unafanya idadi ya wachezaji walioripoti kambini kufikia 20 kati ya 23 walioitwaa baada ya mshambuliaji Khamis Mcha aliyekuwa na kikosi cha timu yake ya Azam nchini Liberia naye kuripoti kambini leo asubuhi.


  Wachezaji John Bocco na makipa Mwadini Ally na Aishi Manula ambao pia nao walikuwa Liberia na timu yao ya Azam wataripoti kambini leo alasiri. Wachezaji hao ni sehemu ya msafara wa timu ya Azam ambao utakuja na ndege ya mchana kutokea Nairobi kwa vile ile ya asubuhi waliyotangulia nayo wenzao kuwa imejaa.


  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha Kim Poulsen leo inaendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa. Mazoezi hayo yataanza saa 9 alasiri.


  TIMU TATU ZASHUKA DARAJA FDL
  Timu tatu zimeshuka daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kurudi Ligi ya Mkoa msimu ujao wa 2013/2014 baada ya kushika nafasi za mwisho katika ligi hiyo msimu huu 2012/2013 iliyomalizika wikiendi iliyopita.


  Small Kids ya Rukwa imeporomoka kutoka kundi A baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo mapema kwa kushindwa kufika uwanjani kwenye moja ya mechi zake. Kwa mujibu wa kanuni matokeo yote ya mechi ilizocheza yalifutwa.


  Moro United ya Dar es Salaam ndiyo iliyoaga FDL kutoka kundi B baada ya kumaliza mechi zake ikiwa na pointi tatu. Wakati kutoka kundi C timu iliyoshuka ni Morani ya Manyara iliyomaliza ligi ikiwa na pointi kumi na moja.


  Timu zilizopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2013/2014 ni Mbeya City ya Mbeya iliyoongoza kundi A ikiwa na pointi 31, vinara wa kundi B timu ya Ashanti United ya Dar es Salaam yenye pointi 29 wakati Rhino Rangers ya Tabora imepanda kutoka kundi C ikiwa na pointi 32.


  LIUNDA KUTATHIMINI WAAMUZI KOMBE LA DUNIA.
  Mwamuzi Msaidizi wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Leslie Liunda ameteuliwa kuwa mtathimini wa waamuzi (referee assessor) kwenye moja ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia.


  Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Liunda kutathimini waamuzi kwenye mechi kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Libya itakayochezwa Jumapili (Machi 24 mwaka huu).


  Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Martyrs jijini Kinshasa kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika ya Kati (CAT).

  Waamuzi watakaochezea mechi hiyo William Selorm Agbovi atakayekuwa mwamuzi wa kati, Malik Alidu Salifu (mwamuzi msaidizi namba moja), David Laryea (mwamuzi msaidizi namba mbili) na mwamuzi wa mezani (fourth official) Cecil Amatey Fleischer. Waamuzi wote hao wanatoka Ghana.


  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Bara la Afrika, Bw. Carlos Lopes,  Ofisini kwake leo tarehe 19 Machi, 2013 ambapo walizungumzia masuala mbalimbali ya ukuzaji uchumi hapa nchini ikiwemo maendeleo ya viwanda.
  Mhe. Maalim akiwa katika mazungumzo na Bw. Lopes.
  Mhe. Maalim akimsikiliza kwa makini Bw. Lopes wakati wa mazungumzo yao.
  Mhe. Maaalim akifafanua jambo kwa Bw. Lopes wakati wa mazungumzo yao. Mwingine katika picha ni Bw. Antonio Pedro, Mkurugenzi wa Kamisheni hiyo kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.
  Mhe. Maalim akimweleza jambo Bw. Lopes (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bw. Nathaniel Kaaya (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Ali Mwadini (mwenye tai nyekundu), Msaidizi wa Naibu Waziri na Bw. Macocha Tembele (kulia), Afisa Mambo ya Nje katika Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa.
  Mhe. Maalim na wajumbe wengine wakimsikiliza Bw. Lopes.

  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabia nchi kwa Njia ya Asili kwenye ukumbi wa Mkutano Ofisini Mtaa wa Luthuli Mjijini Dar es Salaam, Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula kushoto Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Bw Richard Muyungi
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Kuhimili  Mabadiliko ya Tabianchi kwa Njia ya Asili Mkutano huo Umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisini Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam, Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula.[Picha na Ali Meja]

  0 0


  TAMASHA la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Machi 31, mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, linatarajia kuwanufaisha zaidi watu wenye ulemavu, imeelezwa.
  Akizungumza jijini leo, Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama, alisema kuwa malengo yake kwa mwaka huu ni kuhakikisha tamasha hilo linawasaidia walemavu wengi tofauti na miaka iliyopita.

  Msama alisema kuwa nia kuu ya tamasha la mwaka huu ambalo pia litahudhuriwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ni kuhubiri amani na upendo, lakini nchi haiwezi kuwa na amani na upendo kama kuna baadhi ya watu wanataabika.
  “Kauli mbiu ya tamasha la mwaka huu ni amani na upendo, lakini wote tunajua ni ngumu kumuhubiria amani na upendo mtu ambaye anataabika, sasa katika kuhakikisha watanzania wote wanaifurahia amani yao na kuongeza mapendo baina yao, nimepanga kuwasaidia kwa namna yeyote walemavu ili kuwapa nguvu za kuifurahia nchi yao yenye amani,”alisema Msama. Aidha aliongeza kuwa wigo wa kuwasaidia walemavu utaongezeka kulingana na kiasi cha fedha kitakachopatikana.

  Tamasha la mwaka huu limeonekana kukubalika na jamii kubwa ya watanzania kutokana na kauli mbiu yake, lakini pia utaratibu wa kuwapa nafasi watanzania kuchagua mikoa na wasanii watakaopamba tamasha umekubalika na wengi hali iliyolifanya tamasha hilo kuwa la watu wote bila kujali dini, rangi ama kabila.

  Wanamuziki wa Injili wanaotarajiwa kupamba tamasha hilo ni  Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa ambaye raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi nchini  Kenya, pamoja na kwaya ya Ambassadors of Christ yenye makazi yake Kigali nchini Rwanda.

  Kwa upande wa wasanii wa hapa nchini watakaotumbuiza ni Upendo Kilahiro,  Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

  Tamasha la Pasaka hilo pia litafanyika katika mikoa ya Mbeya ambapo litaendelea Aprili Mosi kwenye Uwanja wa Sokoine, Aprili 3 litafanyika katika Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 litakuwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. 

  0 0


  Ofisa wa polisi jamii Tarafa ya Moipo Mkoani Manyara,Amiri Mlemba akikabidhi mpira kwa mabingwa wa soka wa Wilaya ya Simanjiro,timu ya Middle Age ya Mji mdogo wa Mirerani kwenye uwanja wa Barafu.(picha na woinde shizza,manyara.

  0 0

   Na Ripota Wetu , Mwanza
   
  Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imepongezwa kwa jitihada inazochukua hivi sasa kuhakikisha kuwa sekta hiyo inakua imara, sauti moja na hivyo kuchangia zaidi katika ujenzi wa uchumi.
   
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Mwanza hivi karibuni Bi. Jovita Bubere na Bw. Moses Nyaronga walisema TPSF imesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza biashara zao na kuongeza mitaji.
   
  “Tunaomba taasisi hii iendelee na jitihada zake za kuwasaidia wanachama wake mikoani ili kuendelea kutujenga katika kukuza biashara hasa kwa mikutano kama hii ya kikanda kwa nchi nzima” alisema Mama Bubere wakati wa mkutano ulioshirikisha wanachama wa TPSF kanda ya Ziwa.
   
  Mama Bubere ambae ni Mwenyekiti wa Asasi ya akina Mama Wajasiriamali Tanzania, yenye makao yake makuu jijini Mwanza wanajishughulisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama ususi, ushonaji na utengenezaji wa vifaa vya majumbani.
   
  “Tunahitaji msaada mkubwa ilikuweza kufikia malengo yetu,” alisema Mwenyekiti huyo. Akizungumzia soko la Afrika Mashariki, Mwenyekiti huyo alisema wamejipanga vizuri kuingia katika ushindani na tayari wameshaanza kutoa mafunzo kwa baadhi ya akina mama kuhusiana na mbinu za kutumia ushindani unaokuja wa kibiahsra.
   
  Kwa upande wake Moses Nyaronga ambae ni Mwenyekiti wa shirika la Lemon Development Foundation lililopo katika wilaya ya Rolya Mkoani Mara, alisema huu ndio wakati wa kuiunga mkono TPSF ili iweze kufanya kazi kwa uhakika zaidi ya ilivyo sasa.
   
  “Mikutano ya namna hii ni mizuri, inatuleta pamoja kama wanachama na inasadia kutoa mawazo kwa taasisi hii ili iweze kufanya vizuri zaidi,” alisema Nyaronga. Akizungumzia vijana kukimbilia ajira serikalini, Bw. Nyaronga alisema vijana wengi wanatakiwa kujiunga katika sekta binafsi ambako kwa sasa ndiko kwenye ajira nyingi hasa za kujiajiri.
   
  “Sekta binafsi imekuwa sana hapa nchini tofauti na miaka ya nyuma, nashauri vijana wasitegemee ajira serikalini, waingie katika sekta binafsi, kinachohitajika ni kuwezeshwa tu na hili linawezekana kama watajiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali” alisisitiza.
   
  “Kuingia katika magenge ya ajabu, kurubuniwa kwenda kwenye maandamano ni ukosefu wa maarifa, na hii inachangiwa na vijana wengi kukosa mwongozo wa nini wachague na nini waache na kwa wakati gani, wakielewa hilo watabadilika,” alisema  Nyaronga.
   
  Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Geofrey Simbeye, alisema taasisi hiyo ina lengo la  kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wanachama wake katika kuongeza kasi ya uanzishwaji wa makampuni na viwanda kwa ajili ya kuongeza ajira na kuinua uchumi wa nchi.
   
  Alisema pia taasisi hiyo inataka kuishawishi serikali kuondoa baadhi ya vikwazo katika ufanyaji biashara ndani na nje ya nchi. Alisema TPSF inataka wanachama wake wafahamiane katika ufanyaji biashara hasa katika mikoa iliyopo katika kanda moja pia kujenga kongano (clusters) imara zitakazoweza kuwaunganisha katika sekta mbalimbali za kiuchumi.
   
  Mkutano huo wa siku moja uliofanyika jijini Mwanza ulikuwa na lengo la kuelimisha na kuhamasisha muundo wa uwakilishi katika kongano (clusters) na kuhusisha mikoa ya Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza, ambayo inaunganisha kanda ya ziwa.

  0 0

  Na Waandishi wetu-MAELEZO_Dar es Salaam.
   
  Kamati ya  Bunge  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano kimataifa imeshauri Serikali kutoa fursa kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kuja kuwekeza  nchini katika sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wetu.
   
  Kauli hiyo imetolewa leo na wajumbe wa Kamati hiyo ilipokutana na viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya bajeti ya mwaka 2013/2014
   
  Walisema wakati umefikwa kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kutowekewa vikwazo katika kupata taarifa muhimu  zinazohusu sekta mbalimbali za uchumi ili waweze kuja kuwekeza badala ya fedha zao kukaa nazo nje ya Tanzania.
   
  Waliongeza kuwa ni vema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikaunda Kitengo maalum cha diplomasia ya uchumi kitakachoshirikisha  wataalamu wa sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utangazaji wa fursa za uwekezaji nchini kwa ili kuboresha nyanja za uchumi kupitia Watanzania waishio nje.
   
  Akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Kamati hiyo Naibu Waziri wa Wizara wa Mambo ya Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Maalim alisema kuwa Serikali hivi sasa inaendelea kutangaza fursa mbalimbali ambazo zipo Tanzania ambapo tayari wawekezaji kutoka Oman wameshaonyesha nia ya kuwekeza nchini.
   
  Alisema kuwa wawekezaji hao wanakusudia kununua nyama ambapo pia watajenga machinjio ya kisasa ambayo yatatumika kuchinjia mifugo kabla ya nyama haijasafirishwa kwenda nje ya Tanzania.

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Anna Abdallah akizungumza na maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Kamati hiyo ilifanya ziara ya ukaguzi wa mipango ya maendeleo ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam jana. Aliyevaa tai ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima. 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama na maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya ukaguzi wa mipango ya maendeleo ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.

   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Anna Abdallah akifurahi jambo wakati alipokuwa anakagua na kamati yake ujenzi wa makao makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linalojengwa Tazara Mchicha, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima. 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kushoto-aliyevaa tai) akiwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama wakati walipokuwa wanakagua ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam. 


  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (aliyevaa tai) akiwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama wakati walipokuwa wanakagua ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam. 

  PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, Kinana alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana ambaye aliwasili kwenye Ofisi hizo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. 
   Katibu wa NEC ya CCM,  Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP), Ai Ping, alipowasili na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mambo ya Nje ya chama cha CPC, mjini Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na ujumbe wake wakiwa kwenye semina kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umasikini  vijijini, semina hiyo iliendeshwa na Mkurugenzi wa  Kituo cha Kimataifa cha kupambana na umasikini, Profesa  Huang Chenwei (kushoto), katika hoteli ya Wanshou, Beijing, China, Machi 19, 2013. Wengine ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia), Kulia kwa Kinana ni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Yusuf na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. 
   MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Ai Ping, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China ( kulia) akiendesha semina kwa kuhusu ujenzi wa vyama vingi katika mazingira ya utandawazi, kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe wake wa viongozi 14 wa CCM, leo Machi 19, 2013. Semina hiyo ilifanyika katika Ofisi za Mambo ya Nje ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). Viongozi wa CCM kutoka kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Mohamed Yusuf, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela na Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.  Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakibadilishana mawazo, baada ya semina kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umasikini, iliendeshwa na Mkurugenzi wa  Kituo cha Kimataifa cha kupambana na umasikini, Profesa  Huang Chenwei, katika hoteli ya Wanshou, Beijing, China, Machi 19, 2013. Kinana na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM, wapo nchini China  kwa ajili ziara ya mafunzo, kwa mwaliko wa Chama Cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto Bolozi wa Korea, Young-Hoon. Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa.
   Rais Jakaya Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kulia ni Balozi wa Korea, Young-Hoon na kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa.
   Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Jengo la Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Veta Kipawa jijini Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Kikwete akimwagilia maji mti baada ya kuzindua Chuo cha Tehama cha VETA Kipawa jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde zinaeleza kuwa  yule dereva aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2493 CPL-Elikiza  Lokisa Nko na kutokomea, amekamatwa jana usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya Bamaga mapema jana mchana.

  Kwa Mujibu wa Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani nchini, Kamanda Mohamed  Mpinga amesema leo kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo aina ya Landlover Discovery rangi nyeusi limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.

  Kupatikana kwa gari hilo kumekuja baada ya Polisi kufuatilia na kujua mmiliki wa gari hilo kuwa ni kanisa la TAG chini ya Mchungaji Wambura, ambaye kwa ushirikiano alioutoa dereva aliyetambuliwa kama Jackson Stephen, alijulikana na hatimaye kupatikana

  Kamanda Mpiga ametoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete jioni hii nyumbani kwa Marehemu hukoUnunio kiasi cha kilomita 25 hivi Kaskazini mwa jiji la Dar. 
  Rais Kikwete pamoja na uongozi wa juuu wa jesgi la polisi walifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha  Mume na watoto watatu. Mume wa marehemu pia ni askari polisi.

  Pichani juu Rais Kikwete akimfariji mume wa marehemu na watoto wake pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema.  0 0
 • 03/19/13--18:10: Article 23


 • Book Now At:

  Holiday Inn Hotel, Dar City Centre
  Mara Foundation at Mayfair Plaza
  Amina Design at Quality Centre
  Tausi Fashions at Mlimani City
  Mpanji Fashions at Jamirex Complex Mwenge
  Or:

  Call 0717 109 362.

  Email: info@mikono.biz

  0 0
 • 03/19/13--19:30: TAPSEA 2013 AT AICC ARUSHA

 • 0 0
 • 03/19/13--20:00: KUMBUKUMBU
 • MAREHEMU THEREZA DANIEL KAPONGO

  Tarehe 20/03/2013 unatimia mwaka mmoja tangu mpendwa wetu mama ulipoiaga dunia hii na kwenda kwa Baba yetu mbinguni. Tunaamini kimwili hauko nasi lakini kiroho tunakukumbuka daima mpendwa wetu. Upendo wako kwa familia hautasahaulika kamwe na hakuna wa kuliziba pengo lako.

  Unakumbukwa daima na watoto wako Juliana, Celestin, Deocal, Renatus, Alex, Agatha na Vicent; wakwe zako; wajukuu zako, vitukuu na wadogo zako.

  Kutakuwa na Misa ya kumwombea marehemu siku ya Jumapili tarehe 24-03-2013 katika kanisa la Parokia ya Mtakatifu Isidori Bakanja, Boko. Wote mnakaribishwa.

  Raha ya Milele Umpe eeeh Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazi Apunzike kwa Amani 

  – Amina

  0 0
 • 03/19/13--20:18: Article 20


 • 0 0

   New Arrivals Easter Collection,It's time we change your wardrobe,come and visit our store J&M Virgo at C&G Plaza,Mikocheni kwa Warioba in Dar es Salaam.Our wide range of body and foot wear for men & women is exclusively imported from USA, UK, Italy & Turkey.    Gowns for kina Dada...
   Mens Shoe's
  Womens High Heels.

  0 0
 • 03/19/13--21:36: TCRA NA DIGITALI NA ANALOGI

 • 0 0


  Siku ya Jumanne, tarehe 19 machi, majira ya saa tatu na nusu asubuhi, Baba Mtakatifu Francis, amezindua rasmi utume na utawala wake kwa Ibada ya Misa, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican. kwenye Ibada hii ya uzinduzi Baba Mtakatifu ameongoza Ibada pamoja na Makardinali na Maaskofu wapatao 180 na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi 31, Viongozi wa Kifalme 6, Wana Wafalme 3, Mawaziri Wakuu 11. Ibada hii iliudhuliwa na umati wa watu, sio tu waumini wa Kikatoriki bali hata waumini wa madhehebu mbalimbali na zaidi watu tokea dini mbalimbali. Umati wa watu unakadiriwa kutokupungua 200.000. 

  Katika Ibada hii, Baba Mtakatifu alivalishwa Pete ya Petro na Kardinali Angelo Sodano , ikiwa kama ishara ya wadhifa wake. 
  Bendera ya Tanzania ilipeperushwa vizuri sana na umati mkubwa wa Watanzania walioudhulia Tukio ili la Kihistoria.

  Kwa picha na video ya Tukio ili la Kihistoria mnakaribishwa kutembelea blog ya Jumuiya ya Watanzania Rome:www.watanzania-roma.blogspot.com

  Picha zote zimeletwa kwenu na ndugu: Andrew Chole Mhella.

    
                                  Baba Mtakatifu akipita kubariki watu 


                Bendera ya Tanzania ikipeperushwa mbele ya Baba Mtakatifu.


                                      endera yetu ikipepea katikati ya Umati wa Watu.

         Kulia ni katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma Ndugu 
  Andrew Chole Mhella pamoja na Ndugu Safari Mwacha wakiipeperusha 
                                   bendera ya Tanzania.

                Masista na ma Padri wa Kitanzania wakiifurahia bendera yetu. 
                      Kwa pembeni ni baadhi ya Watalii wa kiargentina.
       Furaha ziliwajaa baadhi ya Watanzania waliokuwepo mbele ya Kanisa 
                                             Takatifu la Mtakatifu Petro.


  Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma ndugu Andrew Mhella Pamoja na Ndugu Safari Silvanus Mwacha na ndugu Dusten wakipata picha ya Pamoja na askali waliokuwepo kwenye kuhakikisha shughuli nzima inaenda salama.

  0 0


    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akikata utepe kufungua madarasa mapya ya Skuli ya Msingi ya Ole,Jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba jana,akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa huo,(kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna.
   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna,akizungumza na Walimu na wanafunzi wa Skuli ya msimgi Ole,Jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba jana,kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuzungumza na wanafunzi na wananchi baada ya kufungua madarasa mapya skulini hapo. Picha na Ramadhan Othman Ikulu.
    Wanafunzi Jamila Abdalla Swaleh,(kushoto) na Haulat Yussuf Abdi,wakihani utenzi mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa Sherehe ya ufunguzi wa Madarasa mapya.
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipokea risala wakati wa Sherehe ya ufunguzi wa Madarasa mapya.
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wananchi wa Konde wilaya ya Wete, Pemba jana alipotembelea barabara ya Konde-Wete,inayojengwa na kampuni ya LEA Associates South AsiaPvt Ltd, chini ya ufadhili wa shirika la MCC la Marekani,akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Ole,Jimbo la Ole Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipozungumza nao baada ya kufungua madarasa mapya ya kusomea Skulini hapo jana.Picha na Ramadhan Othman Ikulu-Zanzibar

  0 0
 • 03/19/13--22:14: Ngoma azipendazo ankal
 • Ankal, wape vitu Ankal apendazo enzi hizo 'Mabrazameni' a.k.a masharabaro wa enzi hizo wakiwajibika kwa kwenda mbele na vitu vya uhakika iwe studio au live kama ktk clip hii kuanzia utanashati, mistari, uchangamfu, kutumia ala za muziki na kubwa zaidi kundi zima kufanya onyesho kama timu iliyokamilika idara zote na safu zote. Si wengine bali ni Kool & Gang live wakikupa 'Get down on it'

older | 1 | .... | 73 | 74 | (Page 75) | 76 | 77 | .... | 3348 | newer