Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

Chat live Today (18/03/2013) at 2PM with Vodacom Tanzania Manager of Extenal Affairs Mr. Salum Mwalimu!

$
0
0
Tafadhali bofya link hii http://ow.ly/fLqjx ili uwe nasi Live ifikapo Saa Nane kamili (2pm) katika mahojiano ya moja kwa moja (Live Chat) na Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalimu. Kama una swali lolote kuhusu Ligi Kuu ya Vodacom tafadhali usikose kuwa nasi.

DUCE yazindua Diploma ya Juu ya Elimu

$
0
0
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kimeanzisha program mpya ya Diploma ya Juu ya Elimu iliyoanza chuoni hapo hivi karibuni. Programu hiyo inatolewa massa ya jioni na ina lenga kuwapa fursa watu ambao wangependa kujiendeleza katika taaluma ya ualimu lakini hawana muda wa kujiunga na masomo katika muda wa kawaida. 

Programu hii inatolewa kwa watu ambao wana shahada au stashahada katika fani nyingine nje ya ualimu lakini wangependa kujiunga na taaluma ya ualimu au tayari wanafundisha lakini hawakusomea ualimu. Progranu hii pia inawafaa watu wanaoendesha shule kama wamiliki au viongozi wa shule.
Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Dkt Kitila Mkumbo akitoa maelezo yanayohusiana na program mpya ya Diploma ya Juu ya Elimu inayosimamiwa na kitivo cha Elimu, kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Profesa Godliving Mtui.
Naibu Mkuu wa chuo (Taaluma), Profesa Godliving Mtui akikabidhi makabrasha mbalimbali kwa wanafunzi wapya wa Diploma ya Juu ya Elimu ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa program hiyo.
Wanafunzi wapya wa Diploma ya Juu ya Elimu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa program hiyo.

HAPPY BIRTHDAY MAMA wa FATHER KIDEVU

$
0
0
TAREHE ya leo ni ndio aliyo zaliwa Mama mzazi wa Blogger na Mpigapicha nguli Tanzania, Mroki Mroki, Bi. Mary O.Nathan  (pichani) wa Kinyenze, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambaye leo anatimiza miaka 60 tangu kuzaliwa kwake tarehe kama ya leo. 



Kipekee anamshukuru Mungu kwa kumjalia umri huo alionao hivi sasa. Anawashukuru wote ambao wamechangia yeye kuishi vyema. Anaishukuru sana Familia yake yote kwa umoja na upendo walio nao jambo mabalo anasema linamfanya aishi kwa furaha na amani. 



Aidha watoto wake wote wanampa Pongezi za dhati na Kumuombea Mungu amjalie zaidi Afya njema, akimpa zawadi ya Hekima na Busara katika kipindi hiki cha maisha yake ya utu uzima ambao Busara yake na Hekima vinahitajika sana ndani ya Familia yake na Jamii kwa ujumla.



Wajukuu zako na Vitukuu wako pia wanakusalimia sana na wanakuimbia kale kawimbo ka Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!!

Happy Birthday Bibi!!! Dear Bibi Happy birthday to youuuuuuuu!!!!



Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kipera , Kitongoji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakutakia heri na fanaka.



HAPPY BIRTHDAY MAMA TUNAKUPENDA SANA NA TUNAJIVUNIA KUWA NA MAMA WA NAMNA YAKO, MUNGU AKUJALIE HEKIMA NA BUSARA ZAIDI KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.



BY: FAMILIA YAKO.

HON CHIKAWE OFFICIATES EXPERT MEETING ON GENOCIDE PREVENTION

$
0
0
HON. CHIKAWE OFFICIATES EXPERT MEETING ON GENOCIDE PREVENTION AND THE RESPONSIBILITY TO PROTECT IN DAR ES SALAAM ON 18TH MARCH 2013
 
Hon Mathias Chikawe (MP), Minister for Constitutional and Legal Affairs has on 18th March 2013 opened an Expert Meeting on Genocide Prevention and Responsibility to Protect with a theme “Towards a Community of Commitment”.


The meeting is scheduled to take place for three days with the aim of exploring learning and practical approaches to prevention of Atrocities, learning best practices in prevention and protecting and building national strategies and structures in the field of prevention of genocide and mass atrocities. Several experts from Argentina, Australia, Denmark, Tanzania, Switzerland and Several Civil Societies Organizations working on Prevention of genocide and mass atrocities have attended the meeting.

In his opening remarks Hon Chikawe said, the world has witnessed profound acts of atrocities in the past decade even in areas that were least expected, therefore it does not come as a surprise that prevention is attracting a common cause.

He said Tanzania remain committed to UN Convention on the Prevention of Crime of Genocide and continues to adopt domestic and international policies geared towards building a hate free society and contribute to the attainment of a world free from Genocide. 

That Tanzania has always been in the forefront to global and regional initiatives on peace and prevention of genocide, mass atrocities and war crimes. He underscored the importance of partnering with others to share best practices, technical assistance and find solutions to address the potential threat of Genocide.
Hon Mathias Chikawe (MP)(2ND left) giving his opening remarks during the meeting of Experts on Genocide Prevention and the Responsibility to Protect. Left is H.E Oliver Chave, Ambassador of Switzerland to Tanzania, Right is Mr. Patience Ntwina, Acting Director, Directorate of Public Legal Services in the Ministry of Constitutional and Legal Affairs and Mrs Felistas Mushi, Chairperson of the National Committee on Genocide Prevention in Tanzania.
Expert of Genocide Prevention and The Responsibility to Protect from different countries listening to Hon Chikawe’s opening remarks.
Hon Chikawe (right) shares a moment with H.E Oliver Chave (Middle) Ambassador of Switzerland in Tanzania and Ambassador Liberata Mulamula(left) Senior Advisor in Diplomatic Affairs to President Kikwete.

Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje afungua mkutano kuhusu ushirikiano wa India na Afrika

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (katikati) (Mb.) akifungua mkutano wa siku mbili ulioaandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa masuala  ya Kiuchumi na Kijamiii (ESRF) ya hapa nchini kuhusu mahusiano kati ya India na Afrika. Mkutano huo ambao uliwahusisha wasomi kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali duniani ulifanyika katika Hoteli ya Protea Courtyard Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Maalim (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano kuhusu ushirikiano kati ya India na Afrika.

HATMA YA RAGE MIKONONI MWA KAMATI YA MGONGOLWA

$
0
0

Kuwepo ama kutokuwepo madarakani kwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage kutaamuliwa na Kamati ya  Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji inayoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa.
Afisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania TFF Boniface Wambura amesema leo kuwa wamepokea barua kutoka uongozi wa Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa wanachama wake uliofanyika jana kwenye  ukumbi wa Starlight, jijini Dar es salaam  huku wakimwondoa madarakani mwenyekiti wao.

Wambura alisema katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake na Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.

"Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo na ndio utatoa maamuzi yake kama chombo cha mwisho"alisema Wambura.

Hata hivyo Mwenyekiti wa muda wa mkutano uliomwondoa madarakani Rage Mohamed Wandi amesisitiza kuwa wameandaa muhtasari kwa ajili ya kuupeleka kwa msajili wa  vyama ili kuthibitisha uhalali wa katiba iliyotumika kumwengua Mwenyekiti huyo.

Jana wanachama wasiopungua700 kwa pamoja walifanya mkutano katika hotel ya Starlight na waliafiki kumwengua madarakani Mwenyekiti wao Rage kutokana na mwenendo mbaya wa timu.
Akizungumza jijini jana Wandi ambae aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa muda wa mkutano ulioitishwa na wanachama alisisistiza  pamoja na kauli ya Rage ya kugomea kujiondoa madarakani lakini msimamo wao upo pale pale wa kutomtambua kama Mwenyekiti na badala yake asiendeshe klabu kwa matakwa yake bali ni kwa maslahi ya Simba.

"Amesema tunajifurahisha lakini ukweli sisi tunafahamu  vyema Katiba ambayo inaruhusu wanachama wasipopungua 500  ibara ya 22( 2) wanauwezo wa kufanya mkutano ndani ya siku30 kama ambavyo tumefanya sisi,kwanza asiendeshe klabu kama sultani atambue sisi ni wanachama hai ambao tumekamilika na ndio maana kwa azimio moja tumeafikiana hivyo,"alisema Wandi.
Alisema wameandaa muhtasari ambao watauwasilisha kwa msajili wa vyama lengo ni kutaka kupata ukweli juu ya matumizi ya katiba iliyotumika katika mkutano huo na watauwasilisha wakati wowote kuanzia sasa.

Jana Rage alikaririwa akizungumza kwa njia ya simu akitokea India ambapo alipinga maamuzi yaliyofikiwa na wanachama hao huku akifananisha mkutano huo kama kikao cha harusi na kudai bado anajitambua kama Mwenyekiti na atakaporejea ndipo atatoa maamuzi yake mwenyewe kwa kuitisha mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi haujafanyika.

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII WAKUTANA NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII NA WIZARA YA HABARI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,Mhe.Jenister Mhagama akiongea wakati wa kikao na Watendaji Wakuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kilichofanyika leo kwenye Ukumbi wa Bunge Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Waziri Ummy Mwalimu na Kulia kwake ni Waziri wa Habari Dr.Fenella Mukangara.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mhe. Dr. Fenella Mukangara akiwasilisha taarifa ya Majukumu ya Wizara yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya Wizara kwa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda akiwasilisha taarifa ya Wizara yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.
Kaimu Katibu Mkuu, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bibi. Anna Maembe akiwaeleza Wajumbe wa Kamati Majukumu ya Wizara.
Baadhi ya Watendaji Wakuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Wakifuatilia kikao kati yao na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.

Zigua - Game on Lock (Official Video)


SHAIRI: MASIKINI NCHI YANGU WAPI TUNAELEKEA?

$
0
0
Niwazapo nchi yangu, roho yangu husinyaa

Tokea enzi za tangu, mali za kugaa gaa
Lakini kuna ukungu, mnene ulozagaa
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?

Tumejaliwa na Mungu, kila chenye manufaa
Watu, ardhi na mbingu, kote vimetapakaa
Bado tuko kwenye pingu, pakutokea hadaa
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?

Tulianza wanguwangu, uhuru kupigania
Tukawan’goa wazungu, ili tubaki huria
Tukayapita machungu, nchi tukashikilia
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?

Tukalikamata rungu, dola kuishikilia
Wakatupisha vipungu, nchi wakatuachia
Na ndipo kizunguzungu, kikaanza kutitia
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?
  
Sera za kinyungunyungu zikaanza kutokea
Tukataifisha vyungu, kupika hatujajua
Uchumi ukawa gungu, ngoma ya kizazaa
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?
  
Tukaanzisha ukungu, elimu kuihadaa
Tukakiacha kizungu, kama lugha fundishia
Kiswahili kawa dungu, bila ya kukiandaa
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?
  
Elimu kawa Kurungu, aliyepotea njia
Tukaunda Kiswazungu, lugha ya kupotezea
Elimu mwogo mchungu, usomapo Tanzania
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?

Na Shafi Kaluta Abedi

Kiota cha maraha kwa kujipumzisha Easter Hii

UFAFANUZI WA TUME KUHUSU MKAZI WA KUDUMU NA MABADILIKO YA TAREHE ZA UCHAGUZI WA WAJUMBE NGAZI YA KIJIJI NA MITAA

$
0
0

 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba na Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.

Na Mwandishi Wetu
 Tume ya Mabadiliko ya Katiba imewakumbusha wananchi wanaopenda kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kutumia siku mbili zilizobaki kuwasilisha maombi yao kwa Maofisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa na kusisitiza kuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi hayo ni  siku ya Jumatano, tarehe 20 Machi mwaka huu (2013).
Wananchi wanaopenda kuwa Wajumbe wa Mabaraza hayo wawasilishe maombi yao yakiwa na taarifa zifuatazo: Majina Kamili; Jinsi; Umri; Eneo analoishi kwenye Kijiji/Mtaa; Kiwango cha Elimu; na Kazi yake.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume leo (Jumatatu, Machi 18, 2013), wananchi wamekumbushwa kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo: Awe ni Raia wa Tanzania na awe na umri wa miaka 18 au zaidi na awe na uwezo wa kusoma na kuandika. Sifa nyingine ni pamoja na kuwa mkazi wa kudumu wa kijiji, mtaa au shehia husika na awe ni mtu mwenye hekima, busara na uadilifu na pia awe mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kupambanua mambo.
 
Katika hatua nyingine, Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Jospeh Warioba imefafanua kuhusu sifa ya ukazi wa kudumu kwa waombaji na kusema kuwa sifa hiyo haina maana kuwa mwananchi anapaswa kumiliki nyumba katika mtaa au kijiji husika.
  "Tume inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa mkazi wa kudumu ni mwananchi yeyote anayeishi katika mtaa au kijiji husika na sio lazima awe anamiliki nyumba katika mtaa au kijiji hicho," imesema sehemu ya taarifa hiyo iliyosambazwa kwa vyombo vya habari.
  
Kuhusu wananchi kuhakiki majina ya waombaji, Tume hiyo imewataka wananchi walioomba kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kuhakiki majina katika orodha ya majina ya waombaji wote itakayobandikwa katika eneo la wazi au mbao za matangazo katika Mtaa, Kijiji au Shehia husika kwa siku saba kuanzia tarehe 22 hadi tarehe 28 mwezi machi mwaka huu.
  Katika taarifa hiyo, Tume pia imesema imefanya mabadiliko madogo katika mwongozo wake (uliotolewa hivi karibuni) katika tarehe za vikao vya mitaa na vijiji vitakavyowachagua Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba. Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Tume mwezi uliopita, vikao hivi vilipaswa kufanyika kati ya tarehe 30 mwezi Machi mwaka huu (2013) na tarehe 3 Aprili mwaka huu (2013).
"Kwa mujibu wa mabadiliko mapya, vikao hivyo sasa vitafanyika kati ya tarehe 30 Machi mwaka huu (2013) hadi tarehe 5 Aprili mwaka huu (2013). Kwa msingi huu kila kijiji au mtaa kitachagua tarehe atika vikao hivyo, wananchi watapiga kura za siri kuwachagua wananchi wanne kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya," imeongeza sehemu ya taarifa hiyo.
Kufuatia mabadiliko haya, Tume imeongeza, Vikao Maalum vya Kamati za Maendeleo za Kata vya kuwachagua wajumbe wanne kutoka miongoni mwa wananchi waliochaguliwa na vijiji na mitaa navyo vimesogezwa mbele na sasa vitafanyika kati ya tarehe 7 Aprili mwaka huu (2013) na tarehe 10 Aprili mwaka huu (2013). Awali, vikao hivi vilipangwa kufanyika kati ya tarehe 5 Aprili mwaka huu (2013) na tarehe 9 Aprili mwaka huu (2013).
Tume inawaomba wananchi kushiriki na kuendesha mchakato wa kuwapata Wajumbe kwa amani na utulivu na kuzingatia mwongozo uliotolewa na Tume.

TAARIFA KWA UMMA toka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

$
0
0

Ni vyema wananchi wote wakafahamu kuwa ni kosa kwa mtu au taasisi yeyote ile kuchukua Matangazo ya Sekretarieti ya Ajira na kuyafanyia marekebisho au kuandaa matangazo mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kupotosha umma ilihali wakijua wazi kuwa taarifa hizo wanazozichapisha au wanazoziandika katika mitandao ya kijamii hazijatolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.


Tumefikia hatua ya kusema haya kutokana na baadhi ya taarifa zinazohusu mchakato wa ajira hususani uwepo wa nafasi za kazi zilizopo katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira ametoa matangazo hayo.


Moja ya tangazo hilo  la kughushi na lenye nia ya kupotosha umma ni lile lililoko katika anwani hii www.eastafricajobscareer.com lenye kichwa cha habari kinachosomeka “Tangazo la Kazi Utumishi Tanzania June 2013”ambalo linaonyesha “Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Juni, 2013”.

T.C.R.A YATAHADHARISHA UKIUKWAJI WAMAUDHUI KATIKA VYOMBO VYA HABARI

VICTORIA PRINCESS BAR MABINGWA SAFARI NYAMA CHOMA MWANZA

$
0
0
Mpishi Mkuu wa Bar ya Victoria Princes, Joseph Swai akishangilia mara baada ya kutangazwa mshindi wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika viwanja vya furahisha mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Amina Masenza (kulia) akimkabidhi kitita cha shilingi milioni moja Joseph Swai wa Bar ya Victoria Princes mara baada ya kuibuka mabingwa wa fainali za mashindano ya Safariri Nyama Choma yaliyofanuika katika Viwanja vya furahisha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mpishi Mkuu wa Victora Princes, Joseph Swai akishangilia na kitita cha shilingi milioni moja mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Amina Masenza (kushoto kwake) ikiwa ni Mabingwa wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma 2013 Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika viwanja vya furahisha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja mauzo na usambazaji wa kanda ya ziwa , Malaki Sitaki na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mchina ambaye hakutambulika jina lake akicheza wakati Bendi ya Africana inatumbuiza wakati wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma yaliyofanyika katika Viwanja vya Furahisha mwishoni mwa wiki.

rais kikwete azindua maabara ya kisasa ya mamlaka ya chakula na dawa

$
0
0
 Mhe. Rais akikata utepe kuizindua maabara ya kisasa ya TFDA, wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid, Mkuuwa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiki, Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Huduma za Jamii, Margreth Sitta, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabida
Rais Kikwete akiwa ameshika Tuzo ya kutambua mchango wake katika uzinduzi huo mara baada ya kukabidhiwa na TFDA.
Rais Kikwete akihutubia wageni waalikwa na wafanyakazi wa TFDA
Rais Kikwete akitazama dawa bandia ambayo ilikamatwa katika soko na baada ya kuchunguzwa na maabara ya TFDA iligundulika ndani ya kidonge kumewekwa unga wa mahindi badala ya dawa. Anayetoa maelezo ni Meneja mchunguzi wa dawa, Bw. Yonah Hebron 
 Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, akitoa maelezo kuhusu TFDA kwa Mhe. Rais.
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Bibie Anita Ward alipoibuka na "Ring My Bell" mwaka 1979 alikuwa hakai mtu kitini...

utalii halisi wa ndani

$
0
0
Utalii wa wenzetu kwenye zoo moja huko Budapest Hungary ambapo watalii wanawekwa kwenye Canter lenye wavu na kuanza kuzunguka maeneo ya wanyama. Je wadau wanaonaje magari ya utalii nyumbani Tanzania pia yangekua na wavu kama huu?
Chef Issa

Toto day

shilingi bilioni 18 kutumika katika uchimbaji wa visima

$
0
0
Na Frank John-Maelezo. 
 Jumla ya shilingi bilioni 18 zitatumika kwa ajili ya uchimbaji wa visima 20  vya maji vitakavyokuwa na  uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 266 kwa siku katika maeneo ya Kimbiji wilaya ya Temeke na Mpera wilayani Mkuranga kuanza mwezi wa sita mwaka huu na kukamilika mwezi wa sita mwaka 2014.

Hayo yamesemwa leo na afisa mtendaji mkuu  wa mamlaka  ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)  Archard Mutalemwa wakati akiwasilisha ripoti ya utendaji kwa  kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea maeneo ya miradi ya visima hivyo.  

Mutalemwa alisema kwamba utafiti uliofanywa  umeonesha kuwa maji hayo ni safi na salama kwa matumizi ya binadamu na tayari mkandarasi kwa ajili ya kutekeleza wa mradi huo ameshapatikana . Pia mpango huo utahusisha maeneo kadhaa ikiwemo upanuzi wa kituo cha Ruvu juu ambao utaanza  Julai mwaka huu na kukamilika  Machi mwaka 2015.

“Tumeandaa mpango maalum wa kuhakikisha tunatatua  tatizo la maji safi linalowakabili wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kujenga  bwawa la Kidunda kuanzia  Septemba mwaka huu na upanuzi wa mtandao wa mabomba utakaoanza mwakani na miradi yote hii itakamilika  mwaka 2015”, alisema Mutalemwa.
 
Aliitaja miradi mingine katika mpango huo kuwa ni upanuzi wa mfumo wa majitaka unaotarajiwa kuanza mwakani na kukamilika mwaka 2016 na  upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini.
 
Kwa upande wa mradi wa upanuzi wa Ruvu Chini ambao unagharamiwa na Serikali ya Marekani kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 57, Mutalewa alisema kuwa utaongeza uwezo wa upatikanaji wa maji lita milioni 270 kwa siku.
 
Naye Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Dk. Binilith Mahenge alisema kuwa shilingi bilioni 27 zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi watakaotakiwa  kupisha mradi huo na  aliwataka wananachi wa jiji la Dar es Salaam kuipa Serikali muda wa kufanya kazi hasa za kutatua tatizo la maji.
 
Tatizo la upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam limekuwa ni changamoto kubwa ambapo hadi sasa DAWASA ina uwezo wa kuzalisha lita milioni 300 kwa siku huku mahitaji yakiwa ni lita milioni 450.

bei ya madafu leo

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images