Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Rage na kamati yake ya utendaji wang'olewa?

$
0
0
MKUTANO mkuu wa dharura wa wanachama wa klabu ya Simba umemwondoa madarakani mwenyekiti wao Ismail Rage na kuivunja kamati ya utendaji ya klabu hiyo kwa madai ya kukiuka katiba ya klabu yao.
Mkutano huo ambao kabla ya kufanyika kwake ulikuwa umepigwa marufuku na uongozi wa Simba kwa madai kwamba haukuwa halali ulifanyika kwenye Hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na  kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 600.
Mbali ya kumtimua Rage,mkutano huo pia ulimpendekeza  aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope na Rahma AL kharoos kuongoza kamati maalumu hadi pale uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakapofanyika.
Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Mohamed Wandi na katibu wake Maulid Said ulikuwa na  agenda kuu moja iliyojadili mwendendo mbovu  wa klabu ya Simba kwenye Ligi Kuu inayoendelea na kutokuwa na imani  viongozi.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliokuwa na utulivu mkubwa huku ukilindwa na askari polisi wachache,Wandi alimlaumu  Rage kwa madai kwamba amekuwa akiiendesha  klabu yao pasipo kufuata katiba.
"Ibara ya 16 kipengele G inasema kutakuwa  na mkutano kila baada ya miezi minne kujadili maendeleo ya klabu lakini haujafanyika mpaka leo.
"Vilevile ibara ya 18 kipengele cha sita inasema kamati ya utendaji itaunda baraza la wazee na kifungu cha 28  C,kutakuwa na nafasi ya mwanamke katika kamati ya utendaji lakini imekiukwa,huku ni kusigina katiba,".alisema Wandi na kuongeza kuwa:
"Ibara ya 22 ya katiba ya  klabu ya Simba itupanawapata wanachama haki ya kuitisha mkutano endapo mwenyekiti na makamu mwenyekiti hawatakuwapo na ibara ya 19 kifungu cha tatu inatupa mamlaka ya kumwandikisha na kumfukuza mwanachama,".
Baada ya kumaliza kusoma sehemu ya katiba ya klabu ya Simba aliyodai imekiukwa,Wandi aliwataka wanachama wenzake kuamua kama Rage na kamati yake ya utendaji ipewe muda zaidi au iondolewe ndipo wot waliponyoosha mikono juu wakitaka watimuliwe.
Juhudi za Mwananchi kuwasaka  viongozi wa Simba akiwemo Katibu Mkuu Evodius Mtawala na Msemaji wake Ezekiel Kamwaga ziligonga mwamba huku simu zao zikiiita pasipo kupokelewa.

Mwenyekiti wa mkutano huo, Mohammed Wandwi, akiongea na wanachama.
Wanachama wakinyoosha mikono kupinga uongozi uliopo madarakani.
Mwanachama Salum Simba, akiushutumu uongozi wa sasa.
Bi Hindu, mwanachama maarufu wa Simba, naye alitoa lake la moyoni kwenye mkutano huo.




KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHOUMANA NA BYC II LEO HUKO LIBERIA

$
0
0
Azam FC leo jioni majira ya saa 10 kamili za hapa Liberia ambayo ni sawa na saa 1 kamili usiku za Tanzania, itateremka dimbani katika kiwanja cha ATS hapa Monrovia kupambana na BYC II ya hapa. Kocha Mkuu wa Azam ametangaza kikosi kitachoshuka dimbani leo.
1.Mwadini Ali
2.Himidi Mao
3.Waziri Salum
4.David Mwantika
5.Jockins Atudo
6.Michael Bolou
7.Kipre Tchetche
8.Ibrahim Mwaipopo
9.John Bocco
10.Humphrey Mieno
11.Mcha Khamisi

Article 22

KUOKOTWA LESENI YA UDEREVA

$
0
0

Leseni ya udereva class A,B,D yenye namba 4000966587
 imeokotwa eneo la Boko, barabara ya Ununio-DSM TZ
Mmiliki wa leseni hii anipigie kupitia  0762676661

TAARIFA YA RIDHIWANI KIKWETE KUKANUSHA YALIYOANDIKWA DHIDI YAKE KATIKA MITANDAO YA JAMII

$
0
0

Ndugu zangu habari za wikiendi. Yapo mambo machache ningependa kuwashirikisha ili kuweka kumbukumbu sawa na pia kuzuia upotoshaji ambao unaweza kujitokeza siku za usoni iwe kwangu, kwako au kwa mtu mwingine.
Mojawapo ya mambo makubwa ambayo yamejitokeza siku za karibuni hasa katika suala la Teknolojia na habari ni jambo la sheria za faragha (privacy and privacy lawas). Tumeshuhudia kufungwa kwa gazeti za News of The World, mali ya bilionea Rupert Murdoch wa Kimarekani baada ya kudhihirika alitumia wataalam wa teknolojia (hackers) kutafuta siri za watu mashuhuri kwa kuingia katika simu zao za mkononi kinyume cha utaratibu na sheria za faragha (Privacy Laws). Tumeshuhudia pia wahalifu hao hao wa mtandao wakifanya mengi kama kuvamia kwa mitandao ya makampuni makubwa kama Sony na mengineyo na hata katika mitandao hii ya kijamii upo wakati marafiki zako wanakwambia mbona umenitumia kitu kisichoeleweka, na baadaye kuja kugundua kwamba si wewe uliyefanya hivyo.

Tarehe 1, 8 na 9 mwezi huu wa Machi nilikuwa Dar es Salaam kwa shughuli zangu za kawaida kimaisha lakini ziko updates 5 zilifanyika hapa moja ikimhusu ndugu Absalom Kibanda. Ni ajabu kwamba baadhi ya waandishi tena waliojivika taji la usahihi katika uandishi waliiandika habari hiyo bila hata kuniuliza kwamba ni nini kinatokea. Tunajitahitahidi na kutamani kuwa na Taifa la waandishi makini na wenye kufuata maadili lakini wapo wanaoturudisha nyuma. Ni ajabu gazeti kuandika jambo lisilo la kweli huku wahusika wakiwa na kila uwezo wa kumfikia yule wanayedhani kwamba ameandika na kumhoji ili kuhakiki habari. Kazi ya uhariri ni kuhakiki. Ikiwa mtu atakimbilia kuandika jambo likuhusulo ambalo hana hakika nalo na alikuwa na kila uwezo wa kuwasiliana na wewe na kukuuliza lazima utajiuliza maswali mengi. Kwanza: Nini hasa lengo lake na pili ufahamu wake wa kile anachokifanya kwa maana ya taaluma yake katika kazi anayoifanya.

Napenda kuwaambia kwamba katika tarehe tarehe hizo mwezi huu wa Machi, wahalifu wa mtandao wakiwa eneo la Njiro na baadaye Kijenge mjini Arusha (Kila post ilionyesha eneo ilipotoka), (wakati huo mimi nikiwa Dar es Salaam) waliingia bila idhini kwa njia haramu (Hacking) katika anuani yangu ya Facebook na ku-post habari hizo tano. Sasa nimeliacha jambo hilo katika vyombo stahiki vya ulinzi na usalama ili kufuatiliwa kadiri ya taratibu zao.

Natoa wito kwa ndugu zangu waandishi kujitahidi kuhakiki habari kabla ya kuzipeleka katika vyombo vyao. Hii itasaidia 1. Wao kujenga heshima mbele ya jamii 2. Kufikisha kile hasa ambacho ni habari 3. Kuzuia mikanganganyiko isiyo ya lazima. Haya yakizingatiwa nadhani hata sintofahamu hizi za uandishi wa habari unaotokana na hisia na  vyanzo vumbi na  ufahamu mdogo wa jambo utaondoka na tutakuwa na jamii ambayo haki na uwajibikikaji wa wanahabari kwa jamii utaonekana kutendeka

Niombe radhi kwa ndugu yangu, rafiki yangu na pia mwalimu wangu, Ndugu Absalom Kibanda kwa usumbufu wowote uliojitokeza ambao naamini watu wasio na nia njema walitaka kuutumia kuleta hisia tofauti katika jamii na pia kumpa pole kwa mara nyingine tena kwa maumivu yaliyosababishwa na ujangili huo. Namuombea kwa Mungu ampe unafuu mapema zaidi ili arudi katika meza yake kuendeleze harakati za kupambana na mchango wake katika kuleta maendeleo ya kweli kwa nchi yetu. Pili, pole pia kwa wote ambao kwa namna moja au nyengine walikwazwa na uzushi huo, kwa kuwa sina tatizo lolote na Bwana Kibanda na wala nisingependa lililomtokea limtokee yeye wala mtu mwengine yeyote.

Ni imani yangu ya dhati kwamba vyombo husika katika nchi yetu havitasita kulitalifanyia kazi jambo hili na ukweli juu ya nini kimemtokea Bwana Absalom Kibanda utajulikana na kuwekwa bayana.

Mwisho, shukrani kwa wote mlionipigia simu kuhusu hili, tuko pamoja na nawatakia kila la kheri katika shughuli za ujenzi wa Taifa letu hili la Tanzania ambalo msingi wake umejengwa katika haki, umoja, amani na kujali hali za watu wake.

Asanteni sana.

Ndugu yenu,
Ridhiwani Kikwete,
Jumapili Machi 17, 2013.

Elimu ya Sheria za Usalama barabarani inahitajika sana hapa nchini

$
0
0
 kwa uendeshaji wa namna hii,ajali zitaisha kweli nchi hii??

Habari za Tanzania kwa kina toka TBC

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Boyz II Men walitoka na ngoma ya 'End Of The Road'

Twanga Pepeta kusindikiza utambulisho Miss Tabata 2013 Pasaka

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tabata 2013, watatambulishwa  siku ya sikukuu Pasaka katika ukumbi wa Dar Wes Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga amesema jana kuwa utambulisho huo utasindikizwa na burudani kababembe kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”.
Kalinga alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya fainali itakayofanyika Mei.
Utambulisho wa Miss Tabata 2013 imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti 5 na Kitwe General Traders na kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.
Mratibu huyo alisema warembo 25 wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.

Tamasha la Coke Zero lafana

$
0
0
 Mwanamuziki Madee akiimba sambamba na umati wa wapenzi wa muziki wakati wa uzinduzi wa kinywaji baridi cha Coca-Cola Zero uliofanyika Coco Beach  Oysterbay jijini Dar es Salaam.

 Mwanamuziki nyota wa THT Linah (kulia), akicheza na mmoja wa mashabiki wake aliyepanda jukwaani wakati wa uzinduzi wa kinywaji cha Coca-Cola Zero uliofanyika Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Ommy Dimples akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa kinywaji cha Coca-Cola Zero katika ufukwe wa Coco

Mh. Lowassa akutana na vijana wa Boda Boda jijini Arusha

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana waliojiajiri kwa kufanya biashara ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Boda Boda wa Jijini Arusha wakati alipokutana nao na kuzungumza nao jijini humo hivi karibuni,Mh. Lowassa amesema kuwa Bodaboda ni sera ya CCM ambayo Ina nia ya kusaidia  na kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana.
Waendesha Bodaboda Jijini Arusha wakimsikiliza kwa makini,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Vijana wa Boda Boda wa Jijini Arusha wakati alipokutana nao hivi karibuni.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkoni Vijana wa Boda Boda waliofika kumsikiliza.
Waziri Mkuu Mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa amesema kuwa bodaboda ni sera ya CCM ambayo Ina nia ya kusaidia,kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana hapa nchini.

Akizungumza katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda mkoani Arusha,Lowassa amesema hiyo Ni sera ya CCM kuwakomboa Vijana na kuongeza Kuwa kitendo Cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda Ni Cha mfano KWA wafanyabisharaa wengine nchini

"CCM Ni Chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji kunyanyuliwa kimaisha,kitendo hiki Cha wafanyabishara wa Arusha Ni kuunga mkono sera ya Chama.

Huku akishangiliwaa kila Mara na waendesha bodabodaa hao, Lowassa alirejelea tahadhari yake kuwa tatizo la ajira Ni bomu linalosubiri kulipuka.

"Tusipowasaidia vijana kuondokana na tatizo hili, amani itatoweka, na ndiyo maana CCM katika Ilani yake ya Uchaguzi imeliweka hilo na pia kulisisitiza katika vikao vyake vya juu mkutano mkuu pamoja na halmashauri Kuu"alisema.

Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa halmashauri Kuu na Diwani wa Mererani Mathias Manga ndiyo waliobuni wazo Hilo la kuwaanzishia Mfuko Vijana wa bodaboda.

"Hii Ni Changamoto kubwa KWA wafanyabiashara wengine Nchini wenye mapenzi na nchi yetu,kuiga mfano huu wa kuwasaidia vijana kujiajiri na kuwarejeshea matumaini, kwa kufanya hivi kutaepusha hatari ya kupotea kwa amani"alisema Lowassa ambaye amekuwa akilipigia kelele tatizo la ajira kwa Vijana.

"Kuna msemo usemao, kichwa kikiwa kitupu ni rahisi shetani kuingia,vijana wakiwa hawana ajira ni rahisi kushawishiwa kuingia kwenye vurugu na maandamano yasiyo na maana"alionya na kuingia kuwa Serikali isiachiwe pekee yake jukumu hilo.

KWA upande wake mwenyekiti wa Chama Cha waendesha bodaboda mkoani Arusha Fabian Shayo alimpongeza Mh Lowassa kwa kuwa msemaji mkuu wa tatizo la ajira kwa vijana na kumuomba asikatishwe tamaa na yanayosemwa.

Katika Harambee hilo zaidi ya shillingi millions 84 zilipatikana, huku mh Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia mil 10 na pikipiki 10.

FEEDBACK ya Mdau aliekuwa amepotelewa na leseni

$
0
0
Salaam Ankal,


Naomba kukufahamisha kwamba ile Leseni ya udereva iliyookotwa jana maeneo ya Boko barabara ya Ununio DSM Tz,mwenyewe tayari amepatikana na amekabidhiwa.
Wadau bado wanaendelea kunipigia simu nadhani ni vizuri wakifahamishwa hili.

Ahsante sana na Lidumu Libeneke la Globu ya Jamii.

Mkutano wa Baraza la Watumishi wa Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi-Idara ya Mipango (OR MUU) Bi. Alberta Kinabo akiwasilisha mada wakati wa Mkutano wa Baraza la Watumishi wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR MUU) uliofanyika hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu wa OR MUU Bw. Aloyce Msigwa akifafanua kuhusu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR MUU).
Wajumbe wa Sekretarieti wakichukua taarifa wakati mkutano wa Baraza la Watumishi wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR MUU).
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakichukua taarifa mbalimbali wakati wa mkutano.

wakazi wa jiji la arusha wakipokea vyema kinywaji cha Tusker lite

$
0
0
Meneja wa bia ya Tusker Lite Bi. Anitha Msangi kielezea wadau jinsi bia ya Tusker Lite ilivyotengenezwa kwa vimelea asili na yenye wanga kidogo sana katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.

Wadau wa bia ya Tusker Lite na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakionyesha furaha na kuipokea bia ya Tusker Lite jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.

Msanii wa Hip Hop kutoka jijini Arusha aitwaye JCB akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuleta bia nzuri ya Tusker Lite katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.

Mwanamuziki wa Bendi ya Vibration ya jijini Arusha akiwaongoza mabalozi wa bia ya Tusker Lite kucheza pamoja na wadau wa jijini Arusha katika hafla hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.


1.       Meneja wa bia ya Tusker Lite Bi. Anitha Msangi (mwenye gauni nyeusi) akiwa amepozi pamoja na wasanii wa jijini Arusha Nakaaya Sumari kushoto kwake na Peter kutoka Arusha na kushoto kwake ni Peter Ngassa mdau kutoka Dar Es Salaam katika hafla ya ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.

IGP Mwema aweka Jiwe la Msingi katika kituo kipya cha Polisi Mji mpya wa Mabwepande

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Said Mwema, akiweka jiwe la Msingi katika kituo cha Polisi Mji mpya wa mabwepande, Wilaya ya kinondoni Jijini Dar es salaamu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Said Mwema akiwahutubia wakazi wa mji mpya wa mabwepande mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo kipya cha Polisi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika mji huo mpya.
Maofisa wa Polisi na wakazi wa mabwepande wakishangilia kufunguliwa rasmi kwa kituo cha Polisi katika mji mpya wa mabwepande.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Advera Senso pamoja na maofisa wengine wakiwa nje ya jengo jipya la kituo cha Polisi Mabwepande mara baada ya Mgeni rasmi IGP Said Mwema kuweka jiwe la Msingi

KATIBU MKUU WA CCM NA UJUMBE WAKE WAPATA SEMINA BEIJING LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa nne kulia) na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM anaoongoza nao katika ziara ya mafunzo nchini China kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo (PCP), wakiwa kwenye semina iliyoendeshwa na Profesa Fan Jida (wa nne kushoto) kukua kwa Uchumi wa China na changamoto inazokabiliana nazo kiuchumi. Semina hiyo imefanyika katika hoteli ya Wanshou mjini Baijing Chna, Machi 18, 2013. Baadhi ya washiriki kutoa kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Martine Shigela, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani, Mjumbe wa Kati Kuu ya CCM, Khadija Aboud na Katibu wa NEC, Siasa, Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai. (Picha na Bashir Nkoromo).

Tanzania hosts a three-day Meeting on Prevention of Atrocities

$
0
0

Hon. Mathias Chikawe (MP), Minister for Constitution and Legal Affairs gives his opening remarks during the High Level Working Meeting on Prevention of Atrocities, particularly on genocide prevention and responsibility to protect.  The Meeting is held at Pretoria Courtyard Hotel in Dar es Salaam.  Listening is H.E. Olvier Chave (left), Ambassador of Switzerland in the United Republic of Tanzania. 

During his opening remarks, Hon. Chikawe said it is not by sheer luck that Dar es Salam is the right venue to host such important meeting.  He said that preventing mass atrocities in our countries requires partnering with citizens, civil societies, media, private sector and important countries such as Switzerland who is funding this meeting.

Hon. Chikawe concluded his remarks saying, that the Meeting will produce substantial deliberations which will "contribute to efforts towards collective responsibility on preventing any future genocide tragedy and raise awareness on responsibility to protect hence creating a peaceful world." 

Several experts from different countries that included Costa Rica, Argentina, Tanzania, Australia, Switzerland, Denmark and civil society organizations listening to the opening remarks by Hon. Chikawe. 
A group photo of Hon. Mathias Chikawe (MP) (seated - center), Minister for Constitution and Legal Affairs together with experts on genocide prevention that included countries from Australia, Argentina, Denmark, Costa Rica, Switzerland, Tanzania and Civil Society Organizations.


twiga cement yazindua mradi wa kokoto

$
0
0
 Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (kushoto) akipokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement,Pascal Lesoinne, alipokwenda   kukabidhi cheti cha uwekezaji cha mradi 
wa kokoto za kujengea wa Twiga Cement kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun (hayupo pichani)kwa niaba ya kampuni hiyo kilichotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania

(TIC) katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC,Raymond Mbilinyi.
 Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu akikabidhi  cheti cha uwekezaji cha mradi wa kokoto za kujengea wa Twiga Cement kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun kwa niaba ya kampuni hiyo kilichotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC,Raymond Mbilinyi.
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI toka TFF Machi 18, 2013

$
0
0

HONGERA AZAM KWA USHINDI LIBERIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaipongeza klabu ya Azam kwa ushindi wa mabao 2-1 ilioupata timu yake katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

Mechi hiyo dhidi ya Barrack Young Controllers II ilichezwa jana jijini Monrovia, na timu hizo zitarudiana wikiendi ya Aprili 6 au 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ushindi huo unaiweka Azam chini ya kocha wake Stewart John Hall katika mazingira mazuri ya kusonga mbele baada ya mechi ya marudiano. Bila shaka ushindi wa timu ya Azam pamoja na mambo mengine umechangiwa na klabu hiyo kujipanga vizuri.

Hata hivyo ushindi huo bado ni changamoto kwa wachezaji, benchi la ufundi na uongozi wa Azam kuhakikisha unajipanga vizuri kwa mechi ya marudiano kwa vile mpira wa miguu una matokeo ya aina tatu; kushinda, kutoka sare au kufungwa.

Msafara wa timu ya Azam unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Blassy Kiondo unatarajiwa kurejea nchini kesho alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi.

TAIFA STARS TRAINING PROGRAMME
Taifa Stars itacheza mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka nchini Brazil dhidi ya Morocco. Mechi hiyo itachezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Jumamosi, Machi 16- Wachezaji kuanza kuripoti kambini
Jumapili, Machi 17- Mazoezi Uwanja wa Karume- Saa 2 asubuhi
Jumatatu, Machi 18- Mazoezi Uwanja wa Karume- Saa 9 alasiri
Jumanne, Machi 19- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Jumatano, Machi 20- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 2 asub na saa 9 alasiri
Alhamisi, Machi 21- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Ijumaa, Machi 22- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Jumamosi, Machi 23- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 10.30 jioni

PONGEZI KWA UONGOZI MPYA TAFCA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi (Machi 16 mwaka huu) mjini Dodoma.

Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TAFCA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia taaluma ya ukocha nchini.

TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TAFCA chini ya uenyekiti wa Oscar Don Koroso aliyeibuka mshindi kwa kura zote za ndiyo baada ya kukosa mpinzani.

Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba ya TAFCA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.

Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA chini ya Ramadhan Mambosasa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

Safu nzima ya uongozi wa TAFCA iliyochaguliwa inaundwa na Dk. Oscar Dan Koroso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu Mkuu), Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Dismas Haonga (Mhazini), Wilfred Kidao (mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF).

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Jemedari Saidi, George Komba na Magoma Rugora.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Article 5

$
0
0

CALL FOR PAPERS
The Universities Act 2005, gives the Tanzania Commission for Universities (TCU) mandate to perform three major roles for Higher education Institutions in Tanzania which are: i) Regulatory, ii) Supportive and iii) advisory. Under the supportive roles, TCU has been organizing among other things the Higher Education Science and Technology Exhibitions.  This is one of the effective ways of keeping the general public informed about the growth and application of Higher Education, Science and Technology for human development and improvement in Tanzania.
This year, about 80 institutions from within and outside Tanzania are expected to participate at the Exhibitions. Being an annual event, TCU is once again organizing the eighth exhibitions in higher education, science and technology. Each year the organizing team sets the theme of which it becomes a leading fortitude of the exhibitions, and this year’s theme is: “Building a Knowledgeable, Accountable and Progressive Society through Higher Education, Science and Technology.The Exhibitions will take place at the Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam from 22nd– 24th May 2013.

This event provides an avenue for a number of education stakeholders gather. In recent years, Tanzania has been experiencing some critical issues facing education sector which require immediate address. TCU sees the forthcoming exhibitions as an opportunity to present/share some issues with general public through paper presentation.

There are three major themes in which papers will focus, which are:

1.     Higher Education in Tanzania: Trends, Prospects and challenges

2.     Preparation of students for Higher Education in Tanzania

3.     Steering the culture of academia-industry-governmentlinkage in promoting HE in Tanzania.

This is to call for competent academic practitioners to express their interest in preparing and presenting papers during the exhibitions on the above themes. Interested individuals are welcomed to send maximum of two pages (times New Roman, font 12, 1.5 space)“Concepts” 5th April 2013through the following email address:

The Organizing team will go through the concepts and the successful individuals will be contacted and given TORs for full paper writing. However, successful individuals will be paid an honorarium for preparation and presentation of the papers.


Issued by the:

Executive Secretary

Tanzania Commission for Universities,

P. O Box 6562,

Dar es Salaam

Tel: +255 22 277 2657

Fax: +255 22 77 2891

E-mail: es@tcu.go.tz

Website: www.tcu.go.tz  


March 2013

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images