Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 74 | 75 | (Page 76) | 77 | 78 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Prof Japhet Killewo, a medical doctor and Epidemiologist from Muhimbili University, speaks to experts who convened on Monday to share research findings and discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania. The meeting was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Jhpiego. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday. 
   Assistant director, Reproductive and Child Division in the ministry of Health and Social Welfare, Dr Neema Rusibamayila specks during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences and the Johns Hopkins University in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare, whose target is to reduce maternal and infant mortality. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday.
   Mainen Moshi, Director of research and publications at Muhimbili University of Health and Allied Sciences specks during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences and the Johns Hopkins University in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare, whose target is to reduce maternal and infant mortality. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday.
   Jackie Gayle, USAID/Tanzania Community Care Advisor, giving a keynote address on behalf of USAID, during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences and the Johns Hopkins University in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare, whose target is to reduce maternal and infant mortality. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday.
  A section of experts who convened on Monday and Tuesday to share research findings and discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania, follows the proceedings keenly. The meeting was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Jhpiego. The workshop was held in Dar es Salaam from Monday.

  0 0


  Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-DSM
  Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, AZAM FC, wamerejea jijini Dar es Salaam leo asubuhi  na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki na wapenzi wa timu hiyo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

  Azam waliwasili kwa mafungu kwa ndege ya Kenya Airways ambapo baadhi ya wachezaji wakiwapo wanaoichezea Taifa Stars kubaki Naorobi ispokuwa Mcha.

  Azam ambao msimu huu wapo nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara walikuwa Nchini Liberia kuchuana na timu ya Barrack Young Controllers (BYC) ambapo Azam walishinda 2-1 katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya michuano hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Antonette Tubman Monrovia, Liberia.

  Azam sasa itahitaji hata sare tu ili kusonga mbele, raundi ya Tatu na ya mwisho ya mchujo kabla ya hatua ya makundi.

  Pichani ni baadhi ya wachezaji hao walipowasili uwanjani hapo.
  Baadhi ya mashabiki na wapenzi wa timu ya Azam FC wakicheza ngoma kwa furaha wakati wa mapokezi ya timu hiyo leo asubuhi.

  SIMBA, YANGA ZILILIPENDWA... hivi ndivyo shabiki huyu wa Azam FC alivyoandika jezi yake na akitoa salamu kwa Watani hao wa jadi katika soka nchini.

  Wachezaji wa Azam FC wakipanda basi lao


  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Bukoba 

   SHIRIKISHO la Wasafirishaji Bidhaa nje ya nchi (TANEXA) wamelalamikia kukithiri kwa vituo vya ukaguzi wa magari (beria) na mizigo vilivyopo barabarani, unapoingia na kutoka Tanzania kupitia mpaka wa Tanzania na Uganda (Mtukula). 

  Eneo lilalolalamikiwa zaidi ni kutokea Mtukula hadi Bukoba mjini ambapo kuna wingi wa vituo njiani. Akizungumza katika semina ya wadau wa biashara juzi mjini Bukoba, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wasafirishaji Bidhaa Nje ya nchini (TANEXA), Mtemi Naluyaga alisema wingi wa beria umekuwa kikwazo cha wafanyabiashara huku baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wanaohudumia katika vituo hivyo wakijenga mazingira ya rushwa kwa wanachama wao. 

   Akifafanua zaidi alisema baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wanaohudumu katika vituo hivyo nao wamekuwa wakivitumia vituo hivyo vibaya kwa kutoza faini za juu pale wasafirishaji wa bidhaa na abiria wanapobainika kuwa na makosa, jambo ambalo humlazimu mtozwa faini kutafuta mbadala wa kukwepa faini hivyo kujengeka mazingira ya rushwa kirahisi.

   Aliishauri Serikali kuifanya Mtukula kuwa kituo Kikuu cha Ukaguzi wa Bidhaa zinapoingia na kutoka nchini na kukifuta kile cha Kyaka ambacho kwa sasa kinafanya kazi moja na inayofanywa na kile cha Mtukula mpakani, jambo ambalo alisema ni usumbufu kwa wafanyabiashara wanaotumia mpaka huo. 

   "Kutokea Mtukula hadi Bukoba Mjini kuna beria 9 upande wa Tanzania, lakini ukiingia Uganda hadi mjini kuna beria moja...na kibaya zaidi ukiangalia beria hizi nyingine zinafanya kazi sawa na beria zingine huu ni usumbufu kwa wafanyabiashara" alimaka. 

  Alishauri Serikali kupitia mamlaka husika kujipanga na kuweka beria moja eneo la Mtukula na kuimarisha uteandaji ili kituo hicho kifanye kazi ya beria zote. 

   Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake Mpakani mwa Tanzania na Uganda (IWCBTA), Mtukula, Jane Charles alisema akinamama wamekuwa wakinyanyaswa na kutishiwa na baadhi ya watendaji katika beria hizo jambo ambalo limekuwa vikwazo katika ufanyaji biashara zao. 

   Akizungumza katika semina hiyo, Mjumbe wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi ya mikoani (TABOA), Wilaya ya Bukoba, Eliud Rumanyika alipinga kitendo cha wafanyakazi wa TRA kuyashikilia baadhi ya magari ya wanachama wao kwa makosa ya abiria pindi inapotokea abiria kaingia na mzigo ambao umekuwa na tatizo mpakani.

   "...Sisi tunaona si haki kwa baadhi ya watendaji wa TRA kwenye vituo vya ukaguzi kuamua kuyashikilia magari yetu kwa kosa la abiria, abiria anapokutwa na kosa mpakani atozwe faini mwenyewe na si kushikilia gari la abiria hii ni usumbufu kwa wengine na wamiliki," alisema Mjumbe Rumanyika.

   Akijibu baadhi ya hoja katika semina hiyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Nassoro Mnambila alisema Serikali ya Mkoa wa Kagera haiungi mkono hoja ya baadhi ya wafanyabiashara wanaotaka kuhamishwa kwa beria ya Kyaka kwenda Mtukula kwani uamuzi wa awali ulizingatia masuala mengi ya muhimu katika nyanja anuai. 

   "Serikali ya Mkoa wa Kagera haishauri kabisha kuvunjwa kwa kituo cha Kyaka...sisi tunaona ipo haja ya kuangalia namna ya kufanya marekebisho kimaboresho zaidi. Watu wachache wasituharibie maana ya kuweka kituo kile (Kyaka) eneo lile," alisema Mnambila.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wasafirishaji Bidhaa Nje ya nchini (TANEXA), Mtemi Naluyaga (kulia) akiwa kwenye semina ya wadau wa biashara Bukoba
  Moja ya gari la mizigo likifanyiwa ukaguzi wa nyaraka kwenye beria kabla ya kuingia Tanzania
  Mkurugenzi wa Programu na Miradi toka TANEXA, Nyandallo Mboyi akiwa katika semina hiyo
  Moja ya beria zilizopo eneo la Kyaka.

  0 0
 • 03/20/13--01:01: HARUSI TRADE FAIR EXHIBITORS


 • 0 0

   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) Steve Kilindo akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 60, Diwani wa Kata ya Sasilo wilayani Manyoni, mkoani Singida, Robert Mussa kwa ajili ya uchimbaji wa visima vya maji 20 ili kupunguza tatizo la maji. Wanaoshuhudia tukio hilo lililofanyika juzi katika kata hiyo ni Meneja wa TBL Kanda ya Kusini, James Bokela (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Fortunata Malya.
   Wananchi wa kata ya Sasilo wilayani Manyoni Mkoa wa Singida wakifurahia baada ya kata hiyo Kukabidhiwa hundi ya Tsh 60 Mil iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania [TBL] kwa ajili ya uchimbaji wa visima 20 vya maji ambapo waliomba kupiga nayo picha
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida, Fortunata Malya akitoa shukrani kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa kutoa msaada wa sh. mil 60 katika Kata ya Sasilo kwa ajili ya uchimbaji wa visima 20 vya maji. Hafla ya makabidhiano ilifanyika hivi karibuni katika kata hiyo.

   Mkazi wa Kijiji Cha Sasilo Wilayani Manyoni Mkoa wa Singida Selebia Robert 51 mfugaji  akiwa Nyumbani kwake pamoja na Familia yake kwenye pozi la picha huku wakiwa na vibuyu vya kuchotea maji na matumaini ya kupata maji Baada ya Kata yao kukabidhiwa Milion 60 na TBL kwa ajili ya Uchimbaji wa visima 20 vya maji vitakavyopunguza tatizo Hilo.
   Meneja wa kampuni ya Bia Tanzania [TBL] Kanda ya Kusini, James Bokela akizungumza na wananchi wa Kata ya Sasilo, wilayani Manyoni, baada ya hivi karibuni kampuni hiyo kukabidhi msaada wa sh. mil 60 za kusaidia kuchimba visima vya maji.
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania [TBL] Steve Kilindo akifafanua jambo mbele ya wananchi wa kata hiyo wakati alipoenda kukabidhi msaada wa 60 milion kwa ajili ya Uchimbaji wa Visima 20 vya maji.
   Wananchi wa kata ya Sasilo wakifuatilia jambo wakati walipokuwa wakishuhudia upokeaji wa Msaada wa Tsh 60 mil zilizotolewa na TBL kwa ajili ya uchimbaji wa visima vya maji 20 makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Selakari ya mtaa na Mtendaji


  0 0

  Licha ya kwamba mji wa Moshi unatajwa kuwepo kwa ujenzi holela katika maeneo mbalimbali,hivi sasa majengo makubwa ya ghorofa yameanza kujengwa katikati ya mji na pembezoni mwa mji hali ambayo itapendezesha zaidi mandhari ya mji huo.Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

  0 0


  Kikosi cha Morocco

  Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.

  Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili alasiri.

  Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha Rachid Taoussi ni Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar, Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal, Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.

  Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.

  Wakati huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa keshokutwa katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa na Dar Live Mbagala.

  Milango siku ya mechi kwa ajili ya watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili mchana.

  0 0

  Miss World Africa mwaka 2005 na Miss Tanzania mwaka huo huo,Nancy Sumari (pichani) jana alizindua Kitabu chake kiitwacho "Nyota Yako",ambacho ni Kitabu cha simulizi inayohadithia mafanikio na uwezo wa wanawake tofauti wa Kitanzania wanaoonyesha jitihada na upekee unaolenga kumhamasisha mtoto wa kike kwenye jamii kutaka kuota ndoto kubwa na kudhubutu kuyafanikisha yale ayawazayo.

  Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kitabu hiki cha Nyota Yako alikua Profesa Esther Mwaikambo, ambaye alikua mwanamke wa Tanzania kuwa daktari, muanzilishi wa MEWATA na rais wa chama cha wanasayanzi Tanzania. Prof Mwaikambo pia ni daktari wa watoto katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es salaam, na ni moja kati ya hadithi ya wanawake ambao hadithi zao zimesimuliwa kwenye kitabu.

  Hafla hiyo ya Uzinduzi wa Kitabu hicho imefanyika jana jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na baadhi ya wageni maalum waliofanikiwa kufika katika hafla hiyo ya uzinduzi ambao ni pamoja na Faraja Kotta Nyalandu, Fina Mango, Jacqueline Ntuyabaliwe,Sophia Byanaku, Jokate Mwegelo, Shamim Mwasha, Khadija Mwanamboka, na wadau wa habari pamoja na marafiki.
  Nancy Sumari (kushoto) akiwa na Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Profesa Esther Mwaikambo wakionyesha kitabu hicho mara baada yakukizindua.Kati kati ni Mtoto wa Nancy Sumari.
  Nancy Sumari akisaini moja ya kitabu kabla ya kumpatia Mwanafunzi.
  Nancy Sumari akiwa na Jacqueline Ntuyebaliwe (shoto) pamoja na Faraja Kotta wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.

  Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamepewa vitabu hivyo.
  Nancy Sumari na Jokate Mwegelo.

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Ulinzi na Usalama Mh. Anna Abdalah akipata maelezo kuhusu ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo hilo unaoendelea jijini Dar Es Salaam.Kamati hiyo pia ilitembelea eneo la mradi wa Polisi Ostarbay.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Ulinzi na Usalama Mh. Anna Abdalah akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema pamoja na wajumbe wa kamati hiyo  wakikagua ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi jijini Dar Es Salaam. Kamati hiyo pia ilitembelea eneo la mradi wa Polisi Ostarbay (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh.Pereila Silima (kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Ulinzi na Usalama Mh.Anna Abdalah (katikati) na Mkuu wa kitengo cha Miradi ya Maendeleo na Miradi ya Polisi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Sostenes Kondela pamoja na wajumbe wengine wakikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Idara ya upelelezi jijini Dar Es Salaam Jana.

  0 0

    KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri anayeshughulikia mambo ya chama katika Chama Cha Kikomunisti cha China, Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing, China na kuwa na mazungumzo naye. Nyuma ya Kinana ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai.
    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waziri anayeshughulikia masuala ya chama wa Chama cha Kikomnisti cha China, Wang Jiarui, alipokutana naye leo Machi 20, 2013, kwenye Ofisi za CPC, mjini Beijing, China. (Picha na Bashir Nkoromo).
    Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) akitazama baadhi ya malighafi, alipotembelea kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO), alipotembelea kiwanda hicho mjini Beijing,  Machi 20, 2013. Wapili kulia ni Rais wa Kampuni hiyo Xiong Weiping
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na uongozi wa CHINALCO, Kinana na ujumbe huo walipotembelea kampuni hiyo wakiwa katika ziara ya mafunzo Beijing, China.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa zwadi ya kinyagoo cha Kimakonde cha aina ya 'Ujamaa', Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo nchini China.
    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitia saini kweneye kitabu maalum cha wageni, katika kampuni ya Aluminum ya China ((CHINALCO). Kushoto ni Rais wa Kampuni hiyo, Xiong Weiping na wapili kushoto ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Khamis Suleiman Dadi.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zawadi ya pambo la Kichina, na  Rais wa kampuni ya Aluminum ya China (CHINALCO) kilichopo mjini Beijing, Xiong Weiping, Kinana alipotembelea kampuni hiyo na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM ambao yupo nao katika ziara ya mafunzo nchini China. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0


  Na Ripota wetu.
    
  TUME ya kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012, imesema Serikali inaandaa mkakati wa kuboresha matokeo unaojulikana kama Mkakati wa Kuboresha Matokeo (Better Results Now -BRN).

  Mwenyekiti wa Tume hiyo Profesa Sifuni Mchome amesema lengo la mkakati huo ni kuleta maendeleo ya elimu nchini na tayari wataalamu wa ndani na nje ya nchi wanashiriki kikamilifu katika kufanikishwa zoezi hilo

  Profesa Mchome amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizugumza na waandishi wa habari juu ya hatua iliyofikiwa mpaka sasa na Tume hiyo katika kutekeleza majukumu yake ya uchunguzi na kupata majibu kutoka kwa wadau wa elimu nchini.

  Mwenyekiti huyo aliwaomba wananchi, taasisi mbalimbali na hata vyama vya siasa nchini bila kujali itikadi zao, kushiriki na kuhamasishana katika utoaji wa maoni kwa tume ili kufanikisha utatuzi wa changamoto zinazokwaza maendeleo ya elimu nchini.

  “Pamoja na changamoto za muda mrefu zinazoikabili sekta ya elimu nchini, taifa bado linaendelea kupiga hatua na kujiwekea dhamira na mikakati ya kuleta maendeleo kupitia sekta mbalimbali” alisema Profesa Mchome.

  Alifafanua kuwa changamoto hizo zinahitaji kuwekewa nguvu za pamoja na kutoa maoni endelevu ili kupata mustakabali wa jinsi ya kuinua elimu nchini katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

  Profesa Mchome alisema hadi sasa wamefanya mahojiano na taasisi, mamlaka na wadau mbalimbali wa elimu nchini ambao wameainisha sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika mtihani huo.

  Alitaja baadhi ya taasisi na mamlaka hizo kuwa ni Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi nchini (TAMONGSCO),Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) kanda ya Dar es Salaam, Chama cha Walimu Tanzania, viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Taasisi ya Elimu Tanzania na Baraza la Mitihani Tanzania.

  Wadau wengine waliohojiwa na tume hiyo ni Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala, Mameya, Maafisa Elimu wa miko ya Dar es Salaam na Tanga, Wakaguzi wa Elimu, Wajumbe na Wakuu wa shule mbalimbali za Dar es Salaam, wazazi wanafunzi na wananchi kwa ujumla.

  “Mpaka sasa tumeshapokea ujumbe mfupi wa simu  zaidi ya 300, ujumbe kupitia tume tumepokea zaidi ya 200, baruapepe nyingi sana na watu tuliokutana nao ni zaidi ya 40, pia tumepokea simu nyingi sana ingawa changamoto ni mazungumzo” alisema Profesa Mchome na kuongeza kuwa:

  “Maoni tuliyoyapata mpaka sasa ni shida ya walimu hawatoshi, uchache wa vitabu, hali ya majengo hairidhishi na umbali wa shule, na hizi shida zipo kwenye shule za Serikali na binafsi na kuna baadhi ya shule binafsi ni nzuri  lakini lina shida zaidi”

  Kwa sasa wajumbe wa tume wako katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Manyara, Arusha, Morogoro, Pwani, Simiyu, Shinyanga na Mbeya ambapo wanafanya mahojiano na wakuu wa mikoa na wilaya na shule, walimu, wanafunzi na wajumbe wa bodi za shuke za sekondari zilizoko kwenye mikoa hiyo.

  Mwenyekiti huyo alisema baada ya wajumbe wa tume hiyo kumaliza kazi katika mikoa hiyo, watafanya safari za Zanzibar na Dodoma kuanzia Mchi 24 na kufanya mahojiano na vingoz wa serikali wa visiwa vya Unguja na Pemba na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

  Tume ya kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012, iliundwa na Waziri Mkuu Machi 2 mwaka huu ili kutafua sababu zilizochangia matokeo yasiyoridhisha ya mtihani huo na inatarajiwa kukamilisha kazi yake baada ya majuma manne kuanzia sasa.

  0 0


  0 0  • Baada ya kufanya vizuri sana katika mikoa ya Mbeya, Dar Es Salaam na Mwanza, Safari Lager inakukaribisha kushuhudia fainali za mwisho katika miji ya Arusha na Moshi weekend hii!!.
  • Kwa Arusha fainali zitafanyikaJumamosi hii tarehe 23 March, katika Kiwanja Cha General Tire, kuanzia saa 4.00asbh.Njoo ushuhudie bar za Arusha zilizoingia fainali zikichuana kukupa Nyama Choma Bomba zaidi;
   • QX Pub Kijenge.
   • Blue Line Park Kwa Iddy.
   • VIP Bar Sekei.
   • Royal Stop Over Bar Kwa Mrefu.
   • Rombo Deluxe Bar Tangi La Maji.
  • Kwa Moshi fainali zitafanyikaJumapili hii tarehe 24 March, katika Kiwanja Cha LS Garden CCM Mkoa, kuanzia saa 4.00asbh. Njoo ushuhudie bar za Moshi zilizoingia fainali zikichuana vikali;
   • River Nile Bar Double Road.
   • Makanyaga Bar Soweto.
   • East Africa Pub Double Road.
   • White Star Bar Kiusa Road.
   • Seven ElevenBar Double Road.
  • Njoo uburudike kwa aina tofauti za nyama choma, kuanzia mapande hadi mishkaki, nyama za Kuku, Ngombe na Mbuzi!!.Chachandu, Kachumbari, pilipili, ndimu nk.. vitakuwepo.
  • Matamasha ya Safari Lager Nyama Choma weekend hii Arusha na Moshi ni BURE, hakuna Kiingilio!.
  • Bila Safari Lager, Nyama Choma Haijakamilika!!..

  0 0


  Chama cha wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo (Tanzania chember of commerce Industry and agriculture-TCCIA) mkoa wa Dar es salaam kinapenda kuwataarifu wafanyabiashara wote wa mkoa wa Dar es salaam kwamba kutakuwa na semina elekezi kwa wafanyabiashara wote wa mkoa wa Dar es salaam juu ya utumiaji wa mashine za ukusanyaji kodi na mapungufu yaliyojitokeza kupatiwa ufumbuzi, pia elimu juu ya ulipaji kodi itatolewa. semina hii itaendeshwa na TCCIA kwa kushirikiana na TRA.

  KINONDONI- Semina itafanyika katika hotel ya Rombo green view iliyopo sinza shekilango tarehe 22/03/2013 kuanzia saa tatu na nusu asubuhi mpaka saa saba mchana.


  Mtendaji

  TCCIA Dar es Salaam Regional Chamber
  Tanzania Chamber of Commerce, Industry & Agriculture
  Air Tanzania Building, 3rd fl

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na Mwenyekiti wa kampuni ya Poly Technologies Inc ya China, Bw. Zhang Zhengao (katikati). Mwenyekiti huyo aliongozana na watendaji wakuu wa kampuni hiyo ili kueleza nia yao ya kuwekeza katika ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea kutokana na gesi asilia katika mkoa wa Mtwara au Lindi.
  Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akimuonesha Mwenyekiti wa kampuni ya Poly Technologies Inc ya China, Bw. Zhang Zhengao ramani ya bomba la gesi kutoka Mnazi Bay Mtwara hadi Dar es Salaam na kumfafanulia kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya gesi asilia.
  Wajumbe wakimsikiliza rais wa kampuni ya Poly Technologies Inc ya China, Bw. Wang Lin (aliyenyoosha mkono) wakati wa kikao na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wa wizara.

  0 0

  The KMSC (Kilimanjaro Motor Sports Club ) has organised the Kilimanjaro Vaisakhi rally NRC2 which is set to take place on March 23rd and 24th March 2013 in Moshi. Entries are pouring in from Dar, Arusha, Tanga, Morogoro and Moshi. 
   The rally is expected to be flagged off by the Kilimanjaro Police Commander Mr Peter Boaz at the at the Sikh Club in Moshi.
  The rally shall have two legs with a special stage on Saturday of the opening day which will cover a distance of about 20 kilometres in a competitive section around the TPC areas and the final leg on Sunday will endure 101 kilometres in Boma Ng'ombe/Sanya Juu areas. 
   Entries are still pouring in, and over twenty eight drivers are expected to participate in this year’s Kilimanjaro Vaisakhi rally which among others includes, last year’s winner Shafin Khan (and also 2012’s national rally champion), Dharam Panday, Lali, Gurjit Singh Dhani and  Rajpal Singh Dhani.

  Others are  Salvatory / Akram Hafidh,,Victor Rogart / Sharook Aloo,Kirit Pandya / Awadh Bafadhil, Binesh Haria / Viren Shah, Amarjit Dilon, Tufail Amin, Fayaz Chandu, Eric Cormack / Daudi Charles, Marco Fereira / Ratnaveer Darbar, Gurpal Singh Sandhu / Manmeet Singh Birdi , Gerrard Miller / Peter Fox,Louis Bonzon / Ahmed Hussein, Shiraz Shabay / Ashraphe Ashraph, Jamil Khan, Harshil Bhatt/Victor,, Twalib and Manmohan Aggarwal, 

  The rest are Rizwan Haji / Shabir bandali,Salim Kamal / Raheem Kara,Bob Taylor / Denis Robert, Jamal Nirmal Singh / Ally Al-Salmy, East African Rally Veteran Jayant Shah / Ravi Chana,, Frank Tailor etc. 

   The event has been sponsored by Hari Singh & Sons Ltd along with other associate sponsors backing the rally including Sunvic Express, Keys Hotels Travel & Tours, Maji Poa, Charan Singh & Sons, Yes Automotive Parts, Panone and Company Ltd, Tanzania Volunteers, Authentic Emergency Services Ltd, Snow View Hotel and Nanak Hauliers Ltd.
  0 0

  Mkurugenzi  wa Kampuni ya QS Entertainment, Joseph Mhonda, amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa tamasha lao la ‘Tumaini Jipya’ linalotarajiwa kufanyika Machi 31 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, linagusa hisia za wengi kwa kushirikisha wakali mbalimbali wa muziki wa Injili nchini.

   Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mhonda alisema kuwa alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kwenye jamii ikiwemo watoto yatima na kutarajiwa pia kufanyika katika mikoa mbalimbali baada ya kuzinduliwa mkoani Morogoro. 

   “Tamasha hili limeanzia Morogoeo lakini litaendelea kwenye m ikoa mingine ya Tanzania likiwa na lengo la kutoa tumaini kwa jamii, na mapato yatakayopatikana yatasaidia watu walio katika mazingira magumu” alisema Mhonda.

    Alisema katika tamasha hilo ambalo ni la aina yake kufanyika Tanzania, litapambwa na waimbaji wakubwa wa muziki wa Injili Afrika Mashariki ambao ni Bahati Bukuku, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Joseph Nyuki, Stara Thomas, Matha Mwaipaja, Sifa John, Chamwenyewe na Revina Steven.

   Mbali na waimbaji hao pia kutakuwa na kwaya mbalimali Rafiki Gospel Singers, Haleluya Kwaya, Victoria Kwaya na MTC . Mhonda alisema sambamba na kutoa burudani ya mziki kupitia waimbaji hao pia watakuwa na muda maalum wa kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa watu wote, pamoja na mbinu za kufaulu mtihani kwa wanafunzi. 

   Kwa mujibu wa waandaaji hao, Tamasha la Tumaini Jipya, ni fursa pekee kwa wakazi wa Morogoro kuweza kujumuika na watu wengine duniani katika kusherehekea siku Kuu ya Pasaka.
   Stara Thomas, Martha Mwaipaja, Bahati Bukuku, Masanja Mkandamizaji kukamua Tamasha la Tumaini Jipya Morogoro
   Stara Thomas akiwa na wakali wengine wa muziki wa injili ambao watakuwapo kwenye tamasha la Tumaini Jipya na picha nyinginezo  0 0

  Rais Dkt.Jakaya akikagua nyumba za polisi katika eneo la Mabwepande zinazojengwa kwa msaada wa kampuni ya TSN ya jijini Dar es Salaam.Kushoto ni mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya TSN Bwana Farough Ahmed Baghozah
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua kituo cha polisi Mabwepande huku Kamanda wa Polisi Kanda maalum Suleiman  Kova akiangalia.Kituo hicho cha kisasa kimejengwa kwa msaada wa kampuni ya TSN.
  Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar Es Salaam Suleiman  Kova akimuongoza Rais Dkt. Jakaya  Kikwete kukagua kituo kipya cha Polisi Mabwe Pande wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo

  0 0


  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Zahanati ya Guluka Kwalala iliyopo katika Halmashauri yake baada ya kuwasili kwa ajili ya kumpongeza Mkazi wa eneo hilo kwa kujifungua Salama mtoto wa Kwanza katika Wodi ya Wazazi aliyoijenga kwa nguvu zake kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo ikiwa ni kutekeleza katika moja ya ahadi alizozitoa kwa wapiga kura wake.
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akimsalimia na kumpongeza Bi. Halima Abubakari aliyejifungua mtoto wake katika Zahanati G/Kwalala iliyojengwa na Mstahiki Meya.
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa amepakata mtoto wa Bi. Halima Abubakary mkazi wa Kata ya Gongo la Mboto katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala aliyejifungua salama usiku wa kuamkia Machi 19, 2013 kwenye Zahanati iliyojengwa na Mstahiki Meya ikiwa ni kutekeleza ahadi zake kwa wapiga kura wake.
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akimchekesha mtoto huku akiwa ameshikilia zawadi ya mtoto kwanza kuzaliwa kwenye Zahanati yake.
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika wodi ya wazazi iliyopo kwenye Zahanati ya G/Kwalala.
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kwa kuwasogezea huduma za Afya karibu na makazi yao.

  0 0

  Jioni hii mdau Gerson Msigwa wa TBC (shoto) amegongana na kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars,  Kim Poulsen, katika lift Tansoma Hotel jijini Dar es salaam. Amemweleza Gerson kuwa  kikosi cha Taifa Stars kipo safi kuwakabili Morocco. Kila la kheri Taifa Stars, anasema Gerson Msigwa.

older | 1 | .... | 74 | 75 | (Page 76) | 77 | 78 | .... | 3285 | newer