Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

MAMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA LINDI KUIPIGIA KURA YA NDIYO KATIBA PENDEKEZWA

$
0
0
Mama Salma Kikwete
Na Anna Nkinda – aliyekuwa Lindi

 Wananchi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuipigia kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa kwani ni bora na imegusa maeneo yote kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

Rai hiyo imetolewa na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wananchi waliohudhuria sherehe ya kushangilia ushindi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mtaa wa Ruaha kata ya Mingoyo wilayani humo.

Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wananchi wa mtaa wa Ruaha waliwachagua Mwenyekiti na wajumbe wote watano kutoka Chama Cha Mapinduzi.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema katiba inayopendekezwa imeangalia maeneo yote yanayomgusa binadamu ikiwa ni pamoja na haki za wanawake na watoto, watu wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu na wazee.

“Katiba iliyopo sasa ilitungwa na baadhi ya watu waliokuwa madarakani kwa wakati ule na haikuwahusisha wananchi, lakini hii inayopendekezwa  wananchi wameshiriki kuitunga kwa kutoa maoni yao”, alisema Mama Kikwete.


PAZI BASKETBALL REUNION COMING IN HOUSTON

$
0
0

 Huu ndio uwanja utakaochezewa Bonanza
Emmanuel akianza kuuzoea uwanja.

PAZI BASKETBALL AND ITS FAMILY MEMBERS HAS ORGANIZED A BASKETBALL BONANZA THAT IS SCHEDULED TO TAKE PLACE ON MARCH 13TH -15TH, 2015 IN HOUSTON, TEXAS.
EVENTS:
      ON FRIDAY 13TH OF MARCH, 2015 NETWORKING

      LUNCH, DINNER, AND DRINKS WILL BE AVAILABLE AT MADIKODIKO LOCATION

BASKETBALL BONANZA LOCATION
      ON SATURDAY 14TH, FROM 10:00A.M TO 5:00 PMAT 8601 CHIMNEY ROCK ROAD, HOUSTON TEXAS, US.

MUSIC VIJIMAMBO-DJ LUKE
       NEW, OLD SCHOOL MUSICS, AND THE EVENT WILL BE STREAMING LIVE

      ONLY SOFT DRINKS AND NYAMA CHOMA WILL BE AVAILABLE

      DURING  BONANZA EVENT

PAZI FAMILY WILL HAVE A MEETING UNDER THE THEME “BRINGING BASKETBALL FAMILY TOGETHER”; VITALIS GUNDA-CHAIR
      TEAM BUILDING

      BASKETBALL DEVELOPMENT IN TANZANIA

      NEW IDEAS ARE WELCOME

      EVERYONE IS WELCOME TO ATTEND THE MEETING

BASKTBAL TEAMS ARE FORMING NOW FOR MORE INFORMATION; PLEASE CALL THE FOLLOWING NUMBERS TO REGISTER:
      PETER BATEGEKI: (713) 550-0468

      EMMANUEL NHIGULA: (713) 870-0547

      FLORA MOCHIWA: (832) 893-5034

      WILLY KURRUSA: (281) 661-0034

      VITALIS GUNDA: (240) 383-6950

      EMIL LWAKATARE: (832) 967-4339

CLOSING WITH NITE OF OLD SCHOOL MUSIC ,BONGO FLAVA  AND YOUNG GUYS  HIP HOP AT SAFARI CLUB
             GUEST DJ LUKE  WILL JOIN THE HOST DJS TO COMMEMORATE OUR OCCASION.
               ADDRESS TO SAFARI CLUB IS 7601 DE MOSS DRIVE,HOUSTO N TEXAS 77036



BRING YOUR SNEAKERS AND DANCING SHOES  

NHIF YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WASIO KATIKA SEKTA RASMI

$
0
0
1
Meneja wa Bima ya Afya NHIF Wilaya ya Temeke, Bi Ellentruder Mbogoro (kushoto), akifafanua machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasimi Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Bw. Rehani Athumani kufungua mafunzo ya siku moja ya viongozi wa SACCOS Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Februari 17,2015 lengo la mafunzo hayo ni kuwapa elimu kuhusiana na mpango wa NHIF wa KIKOA unaotolewa Bima ya Afya waweze kujiunga na Mfuko huo ili wapate uhakika wa matibabu kupitia mfuko wa bima ya afya (katikati), Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Bw. Rehani Athumani (kulia) ni Kaimu Meneja wa CHF, Bw. Salvatory Okumu.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON,
2
Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Bw. Rehani Athumani akifungua mafunzo ya siku moja ya viongozi wa SACCOS Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam lengo la mafunzo hayo ni kuwapa elimu kuhusiana mpango wa kujiunga na NHIF kupitia vikundi (KIKOA) ili wapate uhakika wa matibabu kupitia mfuko wa bima ya afya (kulia) baadhi ya viongozi kutoka NHIF.

CHINA YAIPIGA JEKI WIZARA YA AFYA ZANZIBAR,YAIPATIA VIFAA KWA AJILI YA KITENGO CHA MATIBABU YA MACHO KATIKA HOSPITALI KUU YA MNAZIMMOJA

$
0
0
Balozi Mdogo wa China aliopo Zanzibar,Mh. Xie Yuanliang (kulia) akimkabidhi Waziri wa Afya Zanzibar,Mh. Rashid Seif Suleima msaada wa vifaa vya matibabu ya macho uliotolewa na Serikali ya nchi yake. Hafla hiyo ilifanyika Makao Mkuu ya wizara ya Afya Mnazimmoja mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar,Dkt. Saleh Mohamed Jidawi akitoa maelezo wakati wa Hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya uchunguzi na upasuaji wa macho kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Wa kwanza (kushoto) ni Waziri wa Afya Zanzibar,Mh. Rashid Seif Suleiman na (wakatikati) ni Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar,Mh. Xie Yuanliang.
Waziri wa Afya Zanzibar,Mh. Rashid Seif Suleiman akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa dawa za matibabu ya macho uliuotolewa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China katika Hafla iliyofanyika Wizarani Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga Habari Maelezo Zanzibar.

Watanzania waendelea kunufaika na gharama nafuu za mawasiliano

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji waVodacom Tanzania Rene Meza, akiongea na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (hayupo pichani) juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wao Rene Meza (hayupo pichani) kwa waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI ZAIDI

EAC –COMESA YOUTH DIALOGUE FOR CONSOLIDATING REGIONAL STABILITY THROUGH PEACEFUL ELECTIONS IN BURUNDI

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI NA UJUMBE WAKE ZIARANI NCHINI SINGAPORE

$
0
0
luk1
Ujumbe wa Tanzania chini ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukionyesha namna Serikali ya Singapore inavyoratibu upatikanaji wa nyumba kwa wananchi wake ulipotembelea Bodi ya Maendeleo ya Nyumba ya Singapore jana.Jumla ya nyumba 900,000 zimeshajengwa na Bodi hii na kupatiwa wananchi kupitia ruzuku ya serikali na nyumba 50,000 zinapangishwa kwa wananchi kwa kodi isiyozidi asilimia 5. Taifa la Singapore lina watu milioni 5.4 na asilimia 99 ya watu wan chi hiyo wamewezeshwa kumiliki nyumba.
luk2
Ujumbe wa Tanzania ukitembelea vyumba vya mfano vya ukubwa tofauti vinavyojengwa na Bodi ya nyumba ya Singapore kwa ajili ya kuuzia au kupangisha wananchi kulingana na uwezo, mahitaji na ukubwa wa familia. Vyumba hivi vipo Makao Makuu ya Bodi ya Nyumba ya Singapore ambavyo ni kivutio kwa wageni wanaotembelea jengo hilo kujifunza namna ya kuhudumia watu wa kada mbalimbali wanaohitaji nyumba.
luk3
Ujumbe wa Tanzania ukielezwa historia ya hatua mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nyumba nchini Singapore walipotembelea Bodi ya Maendeleo ya nyumba nchini humo jana.

Makamu wa Rais akagua mzani wa Kisasa wa Vigwaza na kufungua barabara ya Msoga - Msolwa km 10

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa km 10 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akihutubia wananchi katika Mzani wa Vigwaza mara baada ya kuukagua.
Mzani wa Kisasa wa Vigwaza kama unavyoonekana. Mzani huu utapima magari kwa haraka zaidi kwa muda wa sekunde 30 kwa kila gari tofauti na mizani ya sasa inayotumia dakika moja na nusu mpaka mbili.


Mhe. Pinda kufungua Mkutano wa Wadau wa PSPF

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda anatarajiwa kufungua mkutano wa Nne wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF utakaofanyika tarehe  18 na 19 Februari 2015 katika Manispaa ya Dodoma. Kauli mbiu ya mkutano huo ni, ‘PSPF- chaguo lako sahihi’.

Taarifa iliyotolewa na Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF Bi.  Costantina Martin, inasema mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano ya wadau inayofanyika kila mwaka kwa lengo la kupata fursa ya kukutana na wadau wa Mfuko, kutoa taarifa ya mwaka ya Mfuko na kupokea maoni na ushauri kwa ajili ya maendeleo ya Mfuko.

Katika mkutano huo PSPF itapata fursa ya kutambulisha kwa wanachama na wadau Mkopo wa elimu na mkopo wa kuanza maisha, Bi. Martin alisema; “mikopo hii hutolewa kwa wanachama wa PSPF wakiwa bado kazini ili kutimiza malengo yao mbalimbali.

Meneja huyo alisema mafao mengine yanayotolewa na PSPF ni pamoja na; mafao ya uzeeni, malipo ulemavu, malipo ya mirathi, rambirambi ya mazishi, pensheni ya wategemezi, mafao ya kuachiswa kazi na fao la kujitoa.

Pia alisema pamoja na kutoa mikopo ya elimu na mkopo wa kuanza maisha, PSPF inatoa mikopo ya nyumba na mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu.

PSPF ni Taasisi ya Hifadhi ya  Jamii iliyoanzishwa na sheria ya Mafao ya Hitimisho la kazi kwa watumishi wa Umma namba 2 ya 1999 sura ya 371.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MIKOA YA LINDI, MTWARA

$
0
0
Na Veronica Simba

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo aliahidi huduma za umeme na maji kwa wananchi mbalimbali.

Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene alimwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

“Kutokana na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha hapa. Pamoja na matumizi yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya maji kwa wananchi wanaozunguka mtambo,” alisema Waziri. Vilevile, Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji cha Luvula kilichoko Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na Kiwanda cha kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.

“Tunaendelea na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu ni kuhakikisha idadi ya watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na zaidi ili kuwezesha lengo la nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama dira ya maendeleo inavyoonesha,” alisema.

Ziara hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara tangu aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na Madini, Januari mwaka huu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda (aliyesimama), akiwasilisha taarifa fupi ya hali ya mmomonyoko wa ardhi uliosababisha mazingira ya hatari kwa Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom Tanzania (M&P), kilichopo Mnazi Bay – Mtwara. Wanaosikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kutoka Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (katikati), na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini walioongozana na Waziri.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akikagua sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia) akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (Kulia kwa Waziri.

WAKAZI KIGAMBONI WACHANGAMKIA BIMA YA MATIBABU YA SH. 1000/= KWA SIKU

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja akimfungulia akaunti ya Bima ya Matibabu, Bi. Saada Ramadhani Mkazi wa Yale Yale Puna – Kigamboni, Dar es Salaam, Katika hafla ya kuwahamasisha wakazi hao kujiunga na Bima ya Matibabu inayotolewa kwa Shilingi 1000 kwa siku kwa ushirikiano na AAR, Inayowezesha familia nzima kupata matibabu katika hospitali zote na kununua madawa katika maduka yaliyopendekezwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, Akimsomea kipeperushi cha Bima ya Matibabu, Saada Ramadhani Mkazi wa Yale Yale Puna – Kigamboni, Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kuwahamasisha wakazi wa eneo hilo kujiunga na Bima ya Matibabu inayotolewa kwa Shilingi 1000 kwa siku kwa ushirikiano na AAR, Inayowezesha familia nzima kupata matibabu katika hospitali zote na kununua madawa katika maduka yaliyopendekezwa.
Afisa Masoko wa Covenant Bank, Kheri Tuwa(Wa kwanza kushoto) akimfungulia Akaunti ya Bima ya Matibabu, Mohammed Mkimo, Mkazi wa Yale Yale Puna – Kigamboni, Dar es Salaam, Katika hafla ya kuwahamasisha wakazi hao kujiunga na Bima ya Matibabu inayotolewa kwa Shilingi 1000 kwa siku kwa ushirikiano na AAR, Inayowezesha familia nzima kupata matibabu katika hospitali zote na kununua madawa katika maduka yaliyopendekezwa. Wengine ni wakazi wa eneo hilo wkipata huduma kutoka kwa maofisa wa benki hiyo.
Mkazi wa Yale Yale Puna – Kigamboni, Dar es Salaam, Juakali Masanja akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja (Hayupo pichani) watika hafla ya kuwahamasisha wakazi hao kujiunga na Bima ya Matibabu inayotolewa kwa Shilingi 1000 kwa siku kwa ushirikiano na AAR, Inayowezesha familia nzima kupata matibabu katika hospitali zote na kununua madawa katika maduka yaliyopendekezwa. Wengine ni wakazi wa eneo hilo wkipata huduma kutoka kwa maofisa wa benki hiyo.

Taarifa ya upimaji na uuzaji wa viwanja katika mji wa Chalinze (New Chalinze City)

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini Wizara ya Fedha anautangazia Umma juu ya upimaji na uuzaji wa viwanja katika mji wa Chalinze (New Chalinze City). 

Fomu za Maombi zinapatikana katika matawi ya Benki ya Posta ya Azikiwe, Metropolitan na Mkwepu kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa Pwani zinapatikana katika tawi dogo la Benki ya Posta Bagamoyo na ofisi za Posta Chalinze. Pia maombi yanaweza kufanyika kupitia tovuti yetu ya : 

Au
                       http://www.utt-pid.org/application.php

Na kulipia katika tawi lolote la Benki ya Posta nchini.

Wajasiriamali, Wasanii na Wanahabari walioshiriki kwenye maonyesho ya Utamaduni nchini Oman,warejea nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar,Bi. Hindi Hamadi Khamis (katikati) akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Zanzibar wa Abeid Karume akisubiri kuwasili kwa Wajasiriamali, Wasanii na Waandishi wa Habari waliokuwa nchini Oman kwa ajili ya maonyesho ya Tamasha la Utamaduni yaliyofanyika nchini humo.
Wajasiriamali, Wasanii na Waandishi wa Habari waliopata nafasi yakwenda Oman kwa ajili ya kuutangaza Utamaduni wao wakipokelewa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bi Hindi Hamadi wa mwanzo kulia akiwasalimia wasanii hao baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimuhoji mmoja kati ya Wasanii waliyopata bahati ya kwenda nchini Oman kwa ajili ya maonyesho hayo. (Picha na Miza Othman Maelezo, Zanzibar)

REVISED STATEMENT: UN CONDEMNS ABDUCTION & MURDER OF ONE YEAR OLD CHILD WITH ALBINISM

UFAFANUZI KUHUSIANA NA TUHUMA ZA VITENDO VYA UNYAMA MGODINI.

$
0
0
KAMPUNI YA STAMIGOLD
MGODI WA BIHARAMULO

TAARIFA KWA UMMA
17 Februari, 2015.

Kampuni ya STAMIGOLD Biharamulo ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) inakanusha vikali taarifa zilizotolewa na mtandao wa kijamii unaojulikana kama Jamii Forums mnamo tarehe 15 Februari, 2015 kuwa kuna unyama wa kutisha uliofanyika Mgodi wa Dhahabu Biharamulo tarehe 26 Octoba, 2014.

Mgodi wa Stamigold Biharamulo unakanusha tuhuma zote za mauaji zilizotolewa na Jamii Forums kwani taarifa hizi ni za kutunga na zinalenga kupotosha umma kwa kuuchafua mgodi huu pekee wa Serikali unaoendeshwa na wazawa pamoja na kumchafua mtu mmoja ambaye ni Meneja Mkuu wa Mgodi Mhandisi Dennis Sebugwao.

Maisha ya Binadamu ni kitu chenye thamani kubwa kiasi ambacho kifo cha mtu mmoja ni masikitiko kwa kila mtu. Hakuna mtu yeyote aliyewahi kuuwawa ndani ya Mgodi na Kuzikwa Kinyemela na baadae kufukuliwa na kuzikwa sehemu tofauti kama mtandao wa Jamii Forums ulivyopotosha. Wafanyakazi na Wananchi wanaoishi karibu na Mgodi hawajawahi kuona mwili wa marehemu yeyote aliyeuawa au kukutwa amekufa ndani ya eneo la mgodi.

Vilevile, si kweli kuwa Polisi waliokuwa wanasaidia kulinda eneo la mgodi waliondolewa ili kuficha tuhuma za mauaji zilizotolewa bali, waliondolewa kwa lengo la kupunguza matumizi kutokana na ufinyu wa mtaji uliopo kuendesha mgodi kwani kampuni ilikuwa ikiilipa polisi takribani shilingi milioni kumi na sita (16M TSH) kila mwezi kwa ajili ya kusaidia ulinzi eneo la mgodi.

Baada ya kusitisha mkataba na Polisi mwezi Disemba, 2014; (uzushi huu umetungwa kuwa tukio lilifanyika tarehe 26 Oktoba, 2014 wakati huo huo Polisi wasiopungua 17 walikuwa wakifanya doria kwenye eneo la mgodi); mgodi uliendelea kutumia askari wa SUMA JKT ambao tayari walikuwa na mkataba na mgodi wa kufanya shughuli za ulinzi katika eneo la mgodi kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Kitengo cha Ulinzi hapa mgodini. 

Shughuli zote za ulinzi zimekuwa zikifanywa kwa kuzingatia sheria za nchi na zile za kimataifa hasa za haki za binadamu na Meneja Mkuu wa mgodi hakuwahi kutoa amri ya kuruhusu au kuagiza mtu yeyote kupigwa kama taarifa hiyo ilivyopotosha umma.

Tunaomba umma utambue kuwa mgodi wa Stamigold Biharamulo unaendeshwa na kufanya shughuli zake kwa kuzingatia Sheria zote za nchi, Kanuni na Matakwa mengine yanayowezesha utendaji uliotukuka kwa shughuli kama za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu. 

Tangu kuanza kwa mgodi kumekuwepo mahusiano mazuri na Jamii inayotuzunguka. Tunashirikiana na kushirikishana mambo mengi ikiwa ni pamoja na kusaidiana wakati kuna majanga au dharura.ya aina yo yote kijijini au katika maeneo ya mgodi.

Meneja Mkuu wa Mgodi Mhandisi Sebugwao anayetuhumiwa na mtungaji wa taarifa hiyo tayari amekwisha toa taarifa kwenye vyombo vya dola ili sheria iweze kuchukua mkondo wake hivyo ni vizuri Polisi wakapewa nafasi ya kufanya upelelezi wao. 

Kupitia taarifa hii Kampuni ya Stamigold Biharamulo inamtaka Mhariri wa Jamii Forums kuomba radhi kwa wasomaji wa mtandao huo pamoja na kuondoa taarifa hiyo potofu kwenye mzunguko wa mtandao wake. Kampuni ya STAMIGOLD Biharamulo inasisitiza vyombo vya habari kuzingatia weledi wa taaluma ya habari na kuandika habari zenye ukweli bila kupotosha umma, ili kwa kufanya hivyo vyombo hivyo visaidie uwepo wa utengemano na uadilifu .

Imetolewa na:
Idara ya Mawasiliano.
STAMIGOLD Biharamulo
S.L.P 78508 Dar es Salaam. 
Barua pepe: info@stamigold.co.tz 
Tovuti: www.stamigold.co.tz

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAJULIA HALI WANANCHI WALIOANGUKIWA NA NYUMBA ZAO KWA UPEPO NA MVUA KUBWA MSOGA.

$
0
0

LIB4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji Bi.Fatuma Janga na baadhi ya majeruhi wakati alipowatembelea jana Feb 17, 2014 baada ya kuangukiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi kijijini  hapo. 
LIB1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na baadhi ya Viongozi, wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao  kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. Picha na OMR
LIB2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia), wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli (kulia) wakiongozwa na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto),  baadhi ya Viongozi, wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. Picha na OMR .

DAWASCO YALIA NA WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA MAJI JIJINI

$
0
0
Licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa kuzuia uhujumu miundombinu ya Majisafi na wizi wa Maji, hujuma nyingine kubwa ya chuma chakavu za MAJITAKA imebainika baada ya DAWASCO kukamata mifuniko ya Majitaka katika kiwanda cha nondo cha IRON&STEEL cha jijini Dar es salaam.

 Vyuma Chakavu hivyo ambavyo ni mifuniko ya chemba za Majitaka za DAWASCO zimebainika baada ya uchunguzi wa kina na taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu upatikanaji wa mifuniko hiyo kiwandani hapo.

Afisa Uhusiano wa DAWASCO Bi Everlasting Lyaro alisema ilibidi watumie mbinu mbadala ili kubaini biashara hiyo iliyokuwa ikiendelea kiwandani hapo, ambapo kwa kushirikiana na Polisi kutoka kituo cha kijitonyama na Afisa Mtendaji wa kata ya Mikocheni waliweza kuvamia kiwanda hicho na kukuta mifuniko mingi ya chemba za Majitaka ambazo ni mali ya DAWASCO.

“Bei ya mfuniko mmoja wa Majitaka huwa tunanunua kati ya Tsh laki tano hadi sita (500,000 -600,000) kutegemeana na ukubwa wa mfuniko, lakini hawa wakishaiba huwa wanaenda kuuza sh 500 kwa kilo hivyo unakuta gharama kubwa inabaki kwetu sisi tunaotoa huduma hii” alisema Lyaro

“mifuniko ya chemba za Majitaka ni muhimu kwa uhifadhi wa Majitaka na pia kuzuia uchafu huo kutapakaa ovyo mitaani, hivyo kuendelea kushamiri kwa biashara hiyo kunatupa wasiwasi wa uwezekano wa magonjwa ya mlipuko utakaosababishwa na utiririshwaji wa Majitaka ovyo mitaani” alifafanua Lyaro Aliongeza kwa kusema mapambano ya uhujumu katika miundombinu ya DAWASCO bado ni kubwa na inahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya wananchi, viongozi husika pamoja na DAWASCO katika kulinda na kuhifadhi miundombinu ya Majisafi na Majitaka.

Katika tukio hilo Meneja Mkuu wa kiwanda hicho Raju N. Chita na Meneja utumishi Idrisa Ally wamekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kijitonyama na kufunguliwa Jalada namba KJN/1786/2015 kwa hatua zaidi kisheria.

MAMILIONI YA DOLA YAIBIWA KATIKA MABENKI KUPITIA WIZI MTANDAO

$
0
0
Baada ya kikao kilichofanyika wiki iliyopita chuo kikuu cha Stafford ambapo Rais Obama wa marekani alikutana na wafanya biashara, Wanasheria na wasimamizi washeria kujadili hali ya mtikisiko wa maswala ya usalama mitandao, Inadhihirisha wazi bado kuna safari ndefu kukabiliana na wimbi hili la uhalifu mtandao duniani kote.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tishio la uhalifu mtandao na utayari wa kukabiliana nao bado kuna kutowiana ipasavyo ingawa jitihada bado ni kubwa kuweza kukabiliana na uhalifu huu unaokua kwa kasi ya pekee duniani kote.

Nategemewa kuwasilisha mada itakayoangazia jitihada za mataifa makubwa 8 dhidi ya uhalifu mtandao na athari za jitihada hizo kwa mataifa mengine katika mkutano wa mwaka utakaofanyika Nchini Croatia unaounganisha wataalam wa maswala ya usalama mitandao kutoka mataifa kadhaa ambapo patajadiliwa mambo kadhaa ya kiusalama mitandao – Taarifa Zaidi za mkutano zinaweza kupatikana kwa "KUBOFYA HAPA"
 
Wakati haya yakijiri na mikakati Zaidi ikiendelea ya kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu mtandao hivi sasa makampuni yanayojihusisha maswala ya fedha yameonekana yakiathirika Zaidi na uhalifu mtandao – Hii ni kwamujibu ya ripoti maalum iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky Lab.


KNCU WAINGIZA MTAMBO MPYA WA KUKOBOLEA KAHAWA

$
0
0
Mtambo mpya wa kisasa wa kukobolea Kahawa ulionunuliwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa zao la Kahawa mkoani Kilimanjaro kwa gaharama za dola laki 9.48 ukishushwa katika kiwanda.
Mota ya kuzungusha mashine wakati wa ukoboaji ikishushwa ikiwa ni sehemu ya mtambo mpya wa kukobolea Kahawa utakaofungwa katika kiwanda cha Cofee Curing.

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI

MSANII CHID BENZ AKIRI MASHITAKA YAKE MAHAKAMANI LEO

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi  Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz leo amekiri mahakamani mashitaka matatu yanayomkabili ya kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Chid Benz alikiri mashitaka hayo baada ya kusomewa upya hati yake ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Warialwande Lema.

Hakimu Lema alisema kwa kuwa mshtakiwa amekiri mashitaka yake mahakama yake itasikiliza maelezo ya awali Februari 23, mwaka huu.

Kabla ya kutolewa amri hiyo, Wakili wa Serikali, Diana Lukondo, aliomba kumsomea mshtakiwa mashitaka yake upya.

Hakimu aliridhia ombi hilo.

Lukondo alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.

Ilidaiwa kuwa katika shitaka la pili, siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.

Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvua dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.

Chid Benz alikiri mashitaka yote matatu, atasomewa maelezo ya awali Jumatatu ijayo na dhamana yake inaendelea.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images