Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WAZIRI NAGU ATEMBELEA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO

$
0
0
Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu akizungumza na watumishi na viongozi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (Hawapo pichani) wakati alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kulia) wakati alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.


ECOBANK TANZANIA YATOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE SIKU YA WAPENDANAO

$
0
0
Mkuu wa Teller wa Benki ya Ecobank, Tawi la Mwenge, Tusekile Mwakyembe (kulia) akikabidhi zawadi Lucas Mosha siku ya wapendanao akiwa ni mmoja wa wateja wa mwanzo wa tawi hilo alipofika kupatiwa huduma jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilitoa zawadi kwa wateja wake wa mwanzo ikiwa ni jinsi ya kuwashukuru na kuonesha wanawajali wateja wake kwa zawadi maalum.
Meneja wa Benki ya Ecobank, Tawi la Mwenge, Patrick Njole (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Brandoni Kimoi ya siku ya wapendanao mmoja wa wateja wa mwanzo wa tawi hilo alipofika kupatiwa huduma jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilitoa zawadi kwa wateja wake wa mwanzo ikiwa ni jinsi ya kuwashukuru na kuonesha wanawajali wateja wake kwa zawadi maalum. Kulia ni Baba yake, Dkt. Ekandumi Brandoni.
Mfanyakazi wa Benki ya Ecobank, Tawi la Mwenge, Sperancia Tarimo (kulia) akikabidhi zawadi Emmanuel Kalolo siku ya wapendanao akiwa ni mmoja wa wateja wa mwanzo wa tawi hilo alipofika kupatiwa huduma jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilitoa zawadi kwa wateja wake wa mwanzo ikiwa ni jinsi ya kuwashukuru na kuonesha wanawajali wateja wake kwa zawadi maalum.
Wafanyakazi wa Benki ya Ecobank, Tawi la Mwenge, (kushoto) wakiwahudumia wateja wake baada ya kukabidhiwa zawadi siku ya wapendanao walipofika kwenye tawi hilo alipofika kupatiwa huduma jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilitoa zawadi kwa wateja wake wa mwanzo ikiwa ni jinsi ya kuwashukuru na kuonesha wanawajali wateja wake kwa zawadi maalum.  

MHE. CHIKU GALLAWA AKAGUA UJENZI WA MAABARA MANISPAA YA DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (mwenye kilemba kichwani) akimsikiliza Afisa Mtendaji wa Kata ya Msalato Dodoma Ndg. Herman Malindira (kulia) akiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi maabara kwenye sekondari ya Chikole Feb. 16, 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akitoa maagizo kwa viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Msalato baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa maabara wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akionesha kutokuridhishwa na hatua ya ujezi wa maabara kwenye sekondari ya Miyuji inayojengwa na Kata za Miyuji na Mnadani ikiwa hatua ya msingi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015, Amemuagiza Mkurugenzi Manispaa ya Dodoma kuwachukulia hatua watendaji wote walioshindwa kusimamia ujenzi wa maabara.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (katikati) akiwaagiza viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Chamwino kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maabara sekondari ya Chinangali ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, Mhe. Gallawa ameonesha kutokuridhika na ujenzi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Mjini Dodoma Feb. 16, 2015 na kukuta maabara ik kwenye hatua ya ujenzi wa msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akiwaagiza viongozi wa Manispaa ya Dodoma na kata ya Chang’ombe kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maabara sekondari ya Lukundo ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, Mhe. Gallawa ameonesha kutokuridhika na ujenzi wa Maabara Manispaa ya Dodoma wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa Maabara Feb. 16, 2015.

Mhe. Janeth Mbene atembelea Ubalozi Mdogo wa Tanzania Dubai

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Janeth Mbene yupo ziarani Dubai. Katika ziara hiyo, Mhe. Mbene ameutembelea Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai na kufanya mazungumzo na Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania. Aidha, Mhe. Mbene amepata maelezo ya kina kuhusu shughuli za Ubalozi Mdogo na Kituo cha Biashara.

Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara Ndugu Ruhumbika, amemueleza Mhe. Mbene ni kwa jinsi gani Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana na Kituo hicho wameweza kuvutia wawekezaji wengi kwenda Tanzania.

Kwa upande wake, Mhe. Mjenga amemuomba Mhe. Mbene kuwa Serikali iangalie uwezekano wa kujenga ofisi zake za Ubalozi Mdogo ambazo zitakuwa na nafasi kubwa kwa ajili ya maonyesho ya bidhaa za Tanzania kwa muda wa mwaka mzima. Nchi nyingi zilizo na Ubalozi Mdogo na Kituo cha Biashara hapa Dubai, wameweza kuvutia uwekezaji na uuzaji wa bidhaa za biashara zinazotoka kwenye nchi zao kwa utaratibu huu.
Pichani ni Mhe. Mjenga akimkaribisha Mhe. Janeth Mbene ofisini kwake kwa mazungumzo.

Vijana Manispaa ya Kigoma Ujiji wahamasishwa kuchangamkia fursa za mfuko wa Maendeleo ya Vijana

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Maendleo ya Jamii Bw. Xavier Keebwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa vijana kuhusu Sera ya maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha,Ujuzi, Mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambapo jumla ya zaidi ya Vijana 60 kutoka katika halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijini mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbvi wa manispaa hiyo. Kutoka Kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga na katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mwezeshaji mkuu wa mafunzo hayo kutoka wizara hiyo Bibi. Esther Riwa.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akitoa mada mbele ya Vijana kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini katika warsha iliyofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada mbele ya Vijana kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini katika warsha iliyofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada wakati wa warsha biliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kuhamasisha vijana kuhusu Mfuko wa maendeleo y Vijana nchini. Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo jumla ya zaidi ya vijana 60 kutoka katika halmashauri za Manispaa hiyo, Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini.

MAKALA YA SHERIA: KISHERIA MAMA WA NYUMBANI ANASTAHILI MGAO WA MALI NDOA INAPOVUNJIKA

$
0
0
Na Bashir Yakub

Ndoa inapovunjika kuna kuna mambo makuu matatu ambayo hutokea yakiwa kama matokeo ya ndoa hiyo kuvunjika. Kwanza ni kugawana mali walizochuma wanandoa , pili hifadhi ya watoto na tatu matunzo ya watoto. Haya ni matokeo ya kuvunjika kwa ndoa, mengine zaidi kuhusu kuvunjika kwa ndoa tutayaona hapa wakati nikieleza mgawanyo wa mali za wanandoa.

1.MALI ZIPI HUTAKIWA HUGAWANYWA NDOA INAPOVUNJIKA.

Ndoa inapotangazwa kuvunjika mali ambazo hupaswa kugawanywa ni mali za wanandoa wenyewe. Swali mbele yetu ni kuwa ni zipi mali za wanandoa. Mali za wanandoa ni zile mali zote zilizochumwa na wanandoa hao kwa jitihada au juhudi za pamoja wakati wa ndoa yao. Mali hizo zaweza kuwa zinahamishika au hazihamishiki.

Mali zisozo hamishika ni kama nyumba, viwanja, mashamba n.k. Mali zinazohamishika ni kama magari, baiskeli, pikipiki,vifaa vya ndani kama fenicha, fedha benki,  na mali nyingine ambazo hazionekani kwa macho au hazigusiki kama hisa  n.k. Zingatia sana usije kudhulumiwa kwa kuwa hata hisa pamoja na akiba ya fedha benki nayo ni mali inayostahili kugawanywa.

2. JE MALI ILIYOPATIKANA KABLA YA NDOA HUGAWANYWA.

Mali zilizopatikana kabla ya ndoa haziwezi kugawanywa ndoa inapovunjika isipokuwa tu kama zilibadilishwa kuwa za wanandoa wakati wa ndoa. Swali ni zinawezaje kubadilishwa kuwa za wanandoa. Zinabadilshwa kuwa za wanandoa iwapo wanandoa walikubaliana kwa makubaliano maalum kuwa mali kadha wa kadha zitakuwa zetu wote.

Na hii inaweza kuwa kwa maandishi au kwa kubadili majina ya nyaraka za umiliki na kuzifanya kuwa na majina yote mawili ya wanandoa kutoka la mmoja la awali. Lakini pia zaweza kuwa za kwao wote kimatendo, kwa mfano kabla ya ndoa mmoja wa wanandoa alikuwa na nyumba lakini haijamaliziwa.

NAIROBI TO HOST 16TH ORDINARY SUMMIT OF EAC HEADS OF STATE

$
0
0
The Sixteen Ordinary Summit of the East African Community Heads of State will be held on 20 February 2015 at the Kenyatta International Conference Centre in Nairobi, Kenya. The 16th Summit will be preceded by 30th Extraordinary Meeting of the EAC Council of Minister also in Nairobi, Kenya.

The 16th Ordinary EAC Heads of State Summit will among others consider; Annual Report of the Council of Ministers for the period December 2013 to November 2014; Progress report in the implementation of key outstanding decisions of strategic importance to the East African Community; Appointment of new Judges of the East African Court of Justice; Designation of a new Principal Judge of the East African Court of Justice; Appointment of a new Deputy Secretary General from the Republic of Burundi to replace Mr Jean Claude Nsengiyumva, whose tenure of office will end in April this year; Renewal of contract of Hon. Jesca Eriyo, Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sector and Consideration of a report on selected priority matter.

The change of Chairmanship is also expected at the 16th Ordinary Summit. The Republic of Kenya is the current Chair of the regional bloc.

The 16th Ordinary Summit is expected to be attended by their Excellencies President Jakaya Kikwete of United Republic of Tanzania, Pierre Nkurunziza of Republic of Burundi, Yoweri Kaguta Museveni of the Republic of Uganda, Paul Kagame of Republic of Rwanda and the host, Uhuru Kenyatta of the Republic of Kenya.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA CHIFU MKWAWA,MKOANI IRINGA

$
0
0

3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na   Chifu mpya wa Wahehe, Chifu Adam Abdu Mkwawa, Mtwa Adam wa Pili (14), wakati wa mazishi ya baba yake aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa leo  katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015.

56

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa leo  Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015.

8

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa leo  katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015

………………………………………

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Februari 16, 2015, ameungana na mamia ya waombolezaji kumlaza katika nyumba yake ya milele, Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa.

Aidha, Rais Kikwete ameshuhudia kutawazwa kwa Chifu mpya, Chifu Adam Abdu Mkwawa, Mtwa Adam wa Pili, kijana wa miaka 14, ambaye yuko darasa la saba na ambaye anachukua nafasi ya baba yake ambaye aliaga dunia juzi, Jumamosi, Februari 14, 2015. twa Adam wa Pili ni mtoto pekee wa kiume na pia ni mtoto sita na wa mwisho wa Chifu Abdu Adam Mkwawa ambaye ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 65.

Rais Kikwete amewasili katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kijiji cha Karenga, kiasi cha saa saba kujiunga na mamia ya waombolezaji na kushuhudia kutawazwa kwa Mtwa Adam wa Pili, ambaye amekuwa chifu kwa kupewa mkuki na ngao, ambavyo vilitumiwa na Chifu Mkwawa mwenyewe, na baadaye kukalishwa kwenye kiti cha uchifu.
 Kwa vile hajafikisha umri wa miaka 20 ambao ndio umri rasmi wa kuwa Chifu wa Wahehe, ameapishwa pia chifu wa muda, Chifu Hassan Adam Sapi (Mahinya), ambaye atashikilia kiti cha uchifu kwa niaba ya Mtwa Adam wa Pili, mpaka hapo atakapofikisha umri wa miaka 20, miaka sita kutoka sasa.

Wakati mmoja wakati wa sherehe ya kutawazwa, Rais Kikwete amelazimika kumbembeleza na kumtuliza Mtwa Adam Abdu Mkwawa, ambaye alizidiwa na hisia na kuanza kubujikwa na machozi.

Baada ya kutawazwa kwa chifu mpya, yameanza mazishi ya chifu aliyeaga dunia ambaye amezikwa kwa heshima na taratibu zote za dini ya Kiislam lakini pia akapigiwa risasi tatu kwa kutumia gobole kwa mujibu wa mila na tamaduni za Kabila la Wahehe.

Baada ya kumalizika kwa mazishi ya Marehemu Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa, Rais Kikwete amekwenda nyumbani kwa marehemu kutoa pole kwa wafiwa akiwemo mama mjane.
 Rais Kikwete amewasili Mkoani Iringa asubuhi ya leo, akitokea Dar es Salaam, ambako anafanya ziara ya kikazi ya siku mbili. Rais Kikwete ataondoka Iringa kesho, Jumanne, Februari 17, kurejea Dar es Salaam.

ngoma azipendazo ankal - Kimulimuli "Tumerudi kishujaa"

BANGO SANGHO YAWEZESHA WANAFUNZI 150 SHULE YA MSINGI KIBUGUMO KUKETI

$
0
0
DSC_0003
Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akisalimiana na Daktari bingwa wa Afya ya jamii na familia, Dkt. Ali Mzige kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati 50 pamoja majengo mawili ya shule ya msingi Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO. Katikati ni Mbunge wa Kigamboni Dk Faustine Ndungulile. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu

WANAFUNZI 150 waliokuwa katika dhiki ya elimu shule ya msingi Kibugumo kutokana na kulazimika kusoma wakiwa wameketi sakafuni wamekabidhiwa madawati yatakayowawezesha kusoma kwa raha.

Madawati hayo yamekabidhiwa jana na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO mbele ya shuhuda ya balozi wa India nchini, Debnath shaw.
Pamoja na madawati hayo taasisi hiyo ilikabidhiwa madarasa mawili yaliyokarabatiwa.

Akipokea msaada huo Kaimu Ofisa elimu wa Manispaa ya Temeke Angelina Nasazwa, alisema umekuja wakati muafaka hasa kwa kuangalia changamoto nyingi zilizopo katika shule hiyo, ikiwemo miundombinu ya madarasa na ofisi.
DSC_0026
Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw (wa pili kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (kulia) kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati 50 pamoja majengo mawili ya shule ya msingi Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO.

MIVARF yaboresha soko la Vitunguu Saumu Mbulu.

$
0
0
Sehemu ya Ghala la kuhifadhi vitunguu Saumu liliojengwa na MIVARF, lipo Mkoani Manyara Wilayani Mbulu, kijijini Bashay. Ghala hilo lina uwezo wa kuhifadhi tani 50 za vitunguu Saumu.

Na. Ibrahim Hamidu

Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) imeboresha Soko la Vitunguu Saumu kwa kujenga ghala la kuhifadhi vitunguu mkoani Manyara, wilayani Mbulu katika kijiji cha Bashay.

Ghala hilo lenye uwezo wa kuhifadhi tani 50 za vitunguu, limegharimu Jumla ya shilingi milioni 88 ikiwa MIVARF imechangia asilimia 95 ya fedha hizo na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imechangia asilimia 5 ya fedha hizo.

Akiongea na timu ya wataalam kutoka MIVARF ofisini kwake hivi karibuni wakati timu hiyo ilipokuwa ikikagua utekelezaji wa shughuli za Mradi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Nicholaus Haraba, alifafanua kuwa ujenzi wa ghala hilo umeongeza mnyororo wa thamani wa zao la vitunguu Wilayani Mbulu.

2015 MISA’S ‘WOMEN TO WATCH’: NOMINATE HOYCE TEMU, VOTE TANZANIA

$
0
0
HOYCETEMUNAWALEMAVU2
Former Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu on field during the recording of her TV talk show.
She also has her own talk show, Mimi na Tanzania (Me and Tanzania), which focuses on CSRs, fundraising, and supporting women and children through the promotion of human rights, gender equality, and access to healthcare and education.
Please nominate her on this category: “Journalists, reporters, presenters who stand out in their field”
International Women’s Day just around the corner, MISA’s is looking to choose 2015 Women to Watch. So, who better to ask for nominations then motivated, inspirational women such as Hoyce Temu, I hope you will agree with me.
You can nominate as many women as you like, from any of the 11 SADC countries in which MISA operates, that’s: Angola, Botswana, Lesotho, Namibia, Malawi, Mozambique, South Africa, Swaziland, Tanzania, Zambia and Zimbabwe.
To nominate Hoyce Temu, simply email at this address (alexandrapeard@gmail.com) or info@misa.org with the name of your nominations, contact details for them (such as an email address or phone number) and a short explanation of their background and why you are nominating them - a sentence or two is all we need.
HOYCETEMUNAWALEMAVU8
MISA’s is interested in showcasing women across a range of fields whose work / interests and passions touch on the issues of free expression and access to information. Some examples might include:
-Artists and performers who use their art to advocate for human rights / speak out against injustice etc.
-Civil society representatives
-Journalists, reporters, presenters who stand out in their field(GOR FOR THIS ONE AND PLEASE NOMINATE HOYCE TEMU)
-Women in fields or roles traditionally male dominated such as camera operators, news anchors, sound technicians etc.
-Human rights lawyers
-Citizen journalists
-Women in ICT, creating new platforms for expression, improving access to ICT etc.
-Children / youth who are ‘rising stars’ in the media or human rights fields
Untitled1
Picha mbalimbali za Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwa katika kazi za kijamii na kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania kinachorushwa kupitia Runinga ya Channel Ten kila Jumapili.

UNATAFUTA KAZI AU TENDA NA BADO HUJAPATA?? NAFASI NI HII SASA

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini,CGP John Casmir Minja (kulia) akimkaribisha Ofsini kwake Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo februari 17, 2015, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini,CGP John Casmir Minja (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha - Rose Migiro mara baada ya mazungumzo yao alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo februari 17, 2015, Jijini Dar es Salaam.

A toZ,Mengi wamsaidia Lowassa jimboni kwake,wachangia shule iliyoungua

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli wakati alipotembelea leo.Lowassa ambaye alirejelea kauli yake ya kwamba yeye si tajiri bali ni tajiri wa marafiki, alichangia shilingi milioni tatu kwa ajili ya sare za shule kwa wanafunzi ambao nguo zao ziliteketea.Aidha mwenyekiti mtendaji wa makampuni IPP amechangia shilingi milioni 25 kwa ajili ya vitanda.
Mmiliki wa kiwanda kikubwa cha A to Z cha Arusha,Anoji Shah (aliesimama) akiwaeleza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli umuhimu wa elimu na pia kutangaza msaada wa enzi wa mabweni yote mawili yaliyoteketezwa kwa moto wiki mbili zilizopita.
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli. 

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

BEI YA MADAFU LEO

Chama Cha Kutetea Abiria (CHAKUA) YAITAKA SUMATRA KUSHUSHA NAULI KWA DALADALA NA MABASI YA MIKOANI

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria Taifa(Chakua),Hassan Mhanjama akionyesha barua kwa waandishi wa habari  (hawapo pichani) ambazo wamejibiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka).


Na Chalila Kibuda.

Chama Cha Kutetea Abiria (Chakua) kimesema kuwa kutokana na bei ya mafuta kushuka nchini nauli ya daladala na nauli ya mabasi mikoani inatakiwa kushuka kwa asilimia 25.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Mwenyekiti wa chama hicho,Hassan Mhanjama amesema Mamlaka ya Usafiri wa Maji na Nchi Kavu (Sumatra) ina wajibu wa kuitisha mkutano na wadau kujadili kushuka kwa gharama ya nauli ili mwananchi aweze kunufaika bei ya kushuka kwa mafuta.

Mhanjama amesema kwa nauli ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Kilomita 10 ya sh.400 inatakikwa kushuka na kufikia sh.300 na nauli ya mkoani ya Sh.40,000 inatakiwa kushuka na kufikia sh.30,000.

Amesema kuwa wamiliki wa Daladala na mabasi ya mikoani kusema bei ya vipuli na tairi zimepanda haihusiani na kushuka kwa bei ya mafuta kwani wakati mafuta yanapanda wanalamika na bei kupandisha hivyo sasa wanalazimika kushusha nauli zao.



WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS DKT.MARY NAGU ATEMBELEA OFISI ZA TASAF

$
0
0

Karibu TASAF hivyo ndivyo anavyoelekea kusema mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga  alipomkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Dokta Mary Nagu ambaye amefanya ziara ya kujitambulisha katika taasisi hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga akimtembeza Waziri wan chi Ofisi ya Rais Dokta Mary Nagu katika jingo linalotumiwa kuhifadhi kumbukumbu za walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini.
 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Dokta Mary Nagu akizungumza na menejimenti ya TASAF katika ziara yake katika taasisi hiyo . 
 Waziri wan chi ofisi ya Rais mahusiano na uratibu Dokta Mary Nagu (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya TASAF kushoto kwake ni mkurugenzi mtendaji wa TASAF Ladislau Mwamanga (mwenye suti  nyeusi).

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE FEBRUARI 23.

$
0
0
Na Chalila Kibuda

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya uchukuaji wa alama za vidole (BVR) kwa mji mdogo wa Makambako mkoani Njombe utaanza Februari 23 hadi Machi 1 mwaka huu.

Kwa taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Ruth Masham kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ilisema zoezi hilo litapita katika kata za Kitisi,Kivavi,Lyamkena,Maguvani,Majengo ,Makambako ,Mji Mwema,Mlowa,na Mwembetogwa na zoezi hilo litaanza majira ya saa 2 hadi majira ya saa 12 jioni ,

Ruth katika taarifa yake ilidai kuwa Kata ya Kitandililo zoezi la uboresha la daftari la wapiga kura utafanyika Machi 3 hadi 9 na Kata ya Mahongole Machi 11 hadi 17  pamoja na Kata ya Utengule utafanyika Mach 19 hadi 25 na vituo vya kujiandikisha vitakuwa kwenye Vitongoji ,Vijiji na Mitaa.

Watakaohusika katika zoezi hilo ni wale ambao wametimiza miaka 18 na kuendelea na wale watakaotimiza miaka ifikapo Oktoba mwaka huu,waliojiandikisha kwenye daftari la zamani wanatakiwa kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.

Wananchi wote wanatakiwa kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuwezesha kupiga kura ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa pamoja na Kuchagua Viongozi ambao ni Rais,Mbunge pamoja na Diwani.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images