Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA WADAU WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda (Kushoto) akizindua huduma mpya itolewayo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ya Fao la Uzazi, mwanzoni mwa mkutano mkuu wa wadau na wanachama wa Mfuko huo mjini Dodoma jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia, ni naibu waziri wa fedha, Adam Malima, Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko huo, GHeorge Yambesi, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Nne wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulioanza leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ,Adam Mayingu kihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Nne wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulioanza leo mjini Dodoma.


DAWASCO YATOA TAARIFA YA KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU JUU

$
0
0
SHIRIKA LA MAJISAFI NA MAJITAKA DAR ES SALAAM (DAWASCO) INAWATANGAZIA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM NA KIBAHA MKOANI PWANI KUWA MTAMBO WA KUZALISHA MAJI WA RUVU JUU UTAZIMWA KWA WASTANI WA SAA 12 KUANZIA SAA 12:00 ASUBUHI HADI SAA 12:00 JIONI KWA SIKU YA IJUMAA 20/02/2015.

MTAMBO YA RUVU JUU UTAZIMWA ILI KUMRUHUSU MKANDARASI KUFANYA SHUGHULI ZA UPANUZI WA MTAMBO.

KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU JUU KUTASABABISHA MAENEO YAFUATAYO KUKOSA MAJI;

MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, KILUVYA, KONGOWE, MISUGUSUGU, VISIGA, TONDORONI,KIMARA BARUTI, BAHAMA MAMA, UBUNGO, MSEWE, CHUO KIKUU, KOROGWE, GOLANI, KIBO, MAVURUNZA, UBUNGO MAJI, TANESCO, KIBANGU JUU, TABATA (MAWENZI, KISUKURU, CHANG’OMBE, KIMANGA, SEGEREA.

MAENEO MENGINE NI BONYOKWA, MAKOKA, KILUNGULE, 770, MANDELA ROAD, MABIBO HOSTEL, KIBANGU CHINI, MAKUBURI, TABATA (KISIWANI, MATUMBI, BIMA NA DARAJANI).
DAWASCO INAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA

KWA TAARIFA ZAIDI PIGA SIMU KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022-2194800 /
 0658-198889
.IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

DAWASCO- MAKAO MAKUU

Wasanii wa Filamu Nchini watakiwa kutokuwa makontena ya biashara haramu

$
0
0
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo akizungumza na wasanii wa bongo movie wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment iliyopo nchini Uingereza. Kulia ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa  
 Kutoka kulia Msanii Yusuph Mllela, Afisa kutoka Bodi ya Filamu Bibi Beatrice Msumari, Msanii Esha Buhet na Msanii Husna Athumani wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuwaaga wasanii hao wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kulia akimpa mkono msanii Yusuph Mllela baada ya neno la kuwaaga wasanii watatu (Yusuph Mllela, Esha Buhet na Husna Athumani) wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment.
 Msanii wa Bongo Movie Bi. Esha Buhet kushoto akifurahi wakati wa kuagana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment. Katikati ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa.



Msanii Husna Athumani akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo (kulia) wakati wa kuwaaga wasania wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na Kampuni ya Didas Entertainment. Katikati ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa.          (Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)         

MAANDALIZI YA MIAKA 15 YA TAMASHA LA PASAKA YAENDELEA KUNOGA,BAISKELI 100 KUTOLEWA KWA WALEMAVU MIKOA KUMI

$
0
0

 
Msama ameongeza kuwa hivi sasa wako katika mazungumzo na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje ya nchi hasa kule Afrika Kusini na Uingereza, waimbaji ambao wako katika mazungumza na kampuni ya Msama Promotion ni Solomon Mahlangu, Rebecca Malope, Keke Pofolo na wengine wote kutoka nchini Afrika Kusini.

Msama alisema kuwa idadi ya mikoa ambayo imeomba iandae onesho la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka sasa imefikia 17,amesema Tamasha la Pasaka kwa mwaka huu litakuwa la aina yake tangu walipoanzisha tamasha lao mwaka 2000.
 
“Tumepokea maombi ya wadau kutoka mikoa 17 wakitaka tupeleke Tamasha la Pasaka mikoani kwao. Tunachofanya kwenye kamati yangu ni kupokea maoni kwa njia mbalimbali kwa wadau wetu wa huko.
 
 “Lakini si kupendekezwa au kuombwa tu na wadau ndiyo kigezo cha kupewa nafasi, lazima tuangalie na mazingira ya mkoa husika katika mambo ya matamasha,” alisema Msama.Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Morogoro, Rukwa,  Mara, Singida, Arusha, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Dar s Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Kilimanjaro na Zanzibar.

  Alisema kamati yake inatarajia kukutana Jumatano wiki hii na kufanya tathmini ya maombi kwa wadau wao wa maeneo hayo ili kupata mikoa sahihi ambayo tamasha hilo litafanyika mwaka huu.
 
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Krismas kila mwaka, lakini wanataka Tamasha la Pasaka mwaka huu liwe bora zaidi kwa sababu wanasherehekea miaka 15 tangu waanzishe tamasha hilo. 

WAJASIRIMALI TUMIENI FURSA YA KUJIUNGA NA NHIF KWA KUCHANGIA SH.78,600 KWA MWAKA

$
0
0
 Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Kinondoni ,Grace Temba akizungumza leo na wajasirimali wa Mkoa wa Kinondoni (hawapo pichani) juu ya faida ya kujiunga na mfuko huo kupitia Mtandao wa ASEE iliyofanyika katika ukumbi Pricess ,Sinza Jijini Dar es Salaam.

 Afisa Matekelezo na Uratibu wa NHIF,Catherine Masingisa akitoa maada kwa wajasirimali wa Mkoa wa Kinondoni (hawapo pichani) namna ya kujiunga  na mfuko wa Bima ya Afya  kupitia vikundi vya ujasiriamali iliyofanyika Katika Ukumbi wa Princes ,Sinza jijini Dar es Salaam.

 Sehemu ya wajasiriamli wakisikiliza maada kutoka kwa maafisa wa NHIF katika ukumbi wa Princess ,Sinza jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
=======  ========  ======  =========
 Na Chalila Kibuda.


Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF)umewataka wajasiriamali wajiunge katika Mtandao wa Jamii wa Huduma ya Afya (ASEE)ili waweze kupata huduma ya afya kwa kuchangia Sh.78,600 kwa mwaka mzima.


Akizungumza na wajasiriamali wa Mkoa wa Kinondoni,Afisa Matekelezo na Uratibu ,Catherine Masingisa amesema si wakati wote mjasiriamali hawezi akawa fedha ya matibabu kujiunga na mfuko kunamfanya aweze kupata matibu katika vituo vyote vilivyosajiliwa na mfuko huo.


Masingisa amesema mpango huo wa kurasimisha wajasirimali kupitia mtandao unatambulika kama Kikoa kutokana na michango yao inakusanywa sehemu moja na kupelekwa katika mfuko wa NHIF.


Amesema watanzania wote wanatakiwa kuwa kadi ya mfuko wa bima ya afya ili kumuwezesha kila mtu kupata matibabu sehemu yeyote kutokana na hali ya uchumi,kwa sababu mtu hawezi kuwa na fedha wakati wote.



Kwa upande wa Afisa Mtekelezo na Uratibu,Tumaini Geofray amesema mfuko umejipanga kufikia wananchi wote juu ya kuwaelimisha faida ya kujiiunga na mfuko huo  kupitia vikundi ili kupata urahisi wa kuratibu zoezi hilo

MAMILIONI YA DOLA YAIBIWA KATIKA MABENKI KUPITIA WIZI MTANDAO

$
0
0
Baada ya kikao kilichofanyika wiki iliyopita chuo kikuu cha Stafford ambapo Rais Obama wa marekani alikutana na wafanya biashara, Wanasheria na wasimamizi washeria kujadili hali ya mtikisiko wa maswala ya usalama mitandao, Inadhihirisha wazi bado kuna safari ndefu kukabiliana na wimbi hili la uhalifu mtandao duniani kote.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tishio la uhalifu mtandao na utayari wa kukabiliana nao bado kuna kutowiana ipasavyo ingawa jitihada bado ni kubwa kuweza kukabiliana na uhalifu huu unaokua kwa kasi ya pekee duniani kote.

Nategemewa kuwasilisha mada itakayoangazia jitihada za mataifa makubwa 8 dhidi ya uhalifu mtandao na athari za jitihada hizo kwa mataifa mengine katika mkutano wa mwaka utakaofanyika Nchini Croatia unaounganisha wataalam wa maswala ya usalama mitandao kutoka mataifa kadhaa ambapo patajadiliwa mambo kadhaa ya kiusalama mitandao – Taarifa Zaidi za mkutano zinaweza kupatikana kwa "KUBOFYA HAPA"

Wakati haya yakijiri na mikakati Zaidi ikiendelea ya kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu mtandao hivi sasa makampuni yanayojihusisha maswala ya fedha yameonekana yakiathirika Zaidi na uhalifu mtandao – Hii ni kwamujibu ya ripoti maalum iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky Lab.

NEWS ALERT: RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27,WAPYA WAKIWEMO SHABANI KISU,PAUL MAKONDA,FREDRICK MWAKALEBELA

$
0
0

*Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani.

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais  Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.

Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.

Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).

Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).

Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).

Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.

JUMATANO, FEBRUARI 18, 2015.

HII HAPA ORODHA KAMILI YA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA WALIOTEULIWA LEO NA RAIS KIKWETE


WAZIRI MEMBE AMUAGA RASMI BALOZI WA SAUDI ARABIA ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba wakati wa hafla ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje kwa ajili ya kumuaga   Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini, Mhe. Hani Abdullah Mominah  ambaye amemaliza muda wake wa kazi. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro tarehe 18 Februari, 2015
Balozi Hani naye akitoa hotuba mbele ya wageni waalikwa
Mhe. Waziri Membe akimkabidhi zawadi ya picha ya kuchora Balozi Hani
Picha ya pamoja Picha na Reuben Mchome 

MH. WASIRA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 38 WA WADAU IFAD,ROMA ITALY

$
0
0
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,Mhe. Stephen Wasira akihutubia katika Mkutano wa 38 wa wadau wa mfuko wa Maendeleo wa Kilimo Duniani (IFAD) uliofanyika mjini Roma Nchini Italy.

BODI YA BARABARA MKOA WA DODOMA YAZITAKA HALMASHAURI ZA WILAYA DODOMA KUCHAGUA WAKANDARASI WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI WANAPOTOA KANDARASI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akifugua Mkutano wa bodi hiyo Feb. 17,2015 Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bodi ya barabara ya Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza mwenyekiti wa Bodi Mhe. Chiku Gallawa wakati akifungua Mkutano wa kwanza wa Bodi hiyo kwa mwaka 2015 mjini Dodoma Feb. 17.

ABIRIA WA TRENI MKOANI DODOMA KUTUMIKA KITUO KIDOGO CHA KATOSHO BADALA YA STESHENI YA TRENI YA KIGOMA KWA TRENI ZA ABIRIA KUANZIA FEBRUARI 18, 2015

$
0
0
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitka kutangaza kuwa treni za abiria za kwenda Kigoma hazitofika katika stesheni ya Kigoma badala yake zitatumia kituo kidogo cha Katosho.

Kwa mujibu wa wa taarifa ya Uongozi wa TRL lilitolewa Februari 16, 2015 uamuzi wa treni  kutofika katika stesheni ya Kigoma  unatokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mjini  Kigoma na hivyo kuzoa mchanga ambao umefunika tuta la reli katika eneo la  stesheni ya Kigoma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo abiria wote wanaowasili na wale wanaondoka Kigoma itawalazimu kujitegemea usafiri  kwenda makwao  na pia wale watakaosafiri  kuja Tabora na Dar es Salaam kwa kutumia kituo kidogo cha Katosho.

Mara baada ya hali kutengemaa na kurekebishwa miundo mbinu ya reli katika stesheni ya Kigoma huduma zitarejeshwa kama kawaida.

Aidha Uongozi wa TRL unawaomba  radhi wateja wake na wananchi  kwa jumla hasa wa mkoa wa Kigoma kwa usUmbufu utakajiotekeza .

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya 
Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam,
Februari 18, 2015

MAREKANI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUDHIBITI UINGIZAJI WA BIDHAA HARAMU NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akiwafafanulia jambo maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani katika mkutano wao uliofanyika jijini Washington DC katika Ukumbi wa Mkutano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Katika mazungumzo yao maafisa hao wa Marekani wanatarajia kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (watatu kushoto), na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani. Waziri Chikawe alikutana na Maafisa hao wa Marekani, jijini Washington DC kujadiliana masuala mbalimbali likiwemo la Maafisa hao wakitarajia kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani. Waziri Chikawe yupo jijini Washington DC katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsalimia Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakati Waziri huyo alipowasili ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo katika Jiji la Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (kushoto) na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini humo, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumpokea Waziri huyo aliyewasili jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho.Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Vijana wilayani Kasulu wapewa somo kuhusu fursa za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Dani Makanga akizungumza na wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliofika ofsini kwake kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuendelea na ratiba yao ya mafunzo kwa Vijana wa Halmashauri za Kasulu na Bihigwe leo mjini Kasulu. Katikati ni Mkuu wa msafara huo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa na wa kwanza kushoto ni Afisa Vijana wa wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Bw. Bernard Ntikabuze (kushoto) akiagana na akipeana mkono na Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga wakati walipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi huyo leo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Bw. Muguha Titus Muguha akizungumza na Vijana wanaoshiriki mafunzo kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (hawapo pichani) yanayotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kutoka kulia ni Afisa Vijana wa Wizara hiyo Bi. Amina Sanga, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bibi. Esther Riwa, Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mbeya Bw. Laurian Massele na Afisa Vijana wa Mkoa wa Kigoma Bw. Edward Manase.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUFANYIKA MACHI 8, 2015

$
0
0

Tarehe 8 Machi, 2015 Tanzania itaungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Kwa mwaka huu, tunaadhimisha siku hii adhimu katika ngazi ya kitaifa ambapo mkoa wa Morogoro utakuwa mwenyeji wa Maadhimisho haya. Mikoa mingine itakuwa na fursa ya kuandaa maadhimisho haya katika maeneo yao kwa kuzingatia mazingira yao. 


Maadhimisho haya hutoa fursa kwa Taifa, mikoa, wilaya na wadau wengine kupima mafanikio yaliyopatikana katika kuwendeleza wanawake na kubainisha changamoto zilizojitokea katika kuwawezesha  wanawake na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto  hizo. 

Maadhimisho ya mwaka 2015 ni ya kipekee kutokana na kuwepo kwa matukio muhimu ambayo yote yatagusa masuala ya haki za wanawake na usawa wa jinsia. Matukio hayo ni: Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge, na madiwani; tathmini ya mafanikio ya utekelezaji wa Azimio la Ulingo wa Beijing baada ya miaka 20 (1995 – 2015); tathmini ya Malengo ya Millenia (2005-2015) na mwelekeo wa Agenda 2063; kuhusu kuwa na ‘Afrika Tunayohitaji’ ifikapo mwaka 2063.

Kufuatia umuhimu huu Wizara imeandaa Kongamano la Kitaifa litakalofanyika tarehe 6 Machi, 2015  na maonesho ya shughuli mbalimbali  sanjari na utoaji wa tuzo kwa waliochangia uwezeshaji wa wanawake nchini. 

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2015 ni: ‘Uwezeshaji Wanawake; Tekeleza Wakati ni Sasa’. Kaulimbiu hii inalenga kuhamasisha jamii kutambua mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo yao; na kuelimisha wadau kuangalia upya wajibu wao wa kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa wanawake haki sawa katika nafasi za elimu, uchumi na uongozi ili waweze kuwa chachu katika maendeleo yao. 

Natoa wito kwa wananchi katika mikoa yote nchini kushiriki kikamilifu kuienzi siku hii adhimu. Ni matumaini yangu kwamba kupitia maadhimisho haya wadau wote na serikali watakumbushwa wajibu na mchango wao katika kutekeleza ujumbe wa kaulimbiu na kubaini mbinu za kukabiliana na changamoto za ushiriki wa wanawake katika maendeleo. 

Aidha, nawaomba wanahabari kushirikiana na Serikali kuelimisha jamii kuhusu shuhuda bora zinazoonyesha jinsi gani wanawake walivyoweza kuaminiwa na hivyo kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa kwa ujumla. 
Nawatakia maadhimisho mema.

Anna T. Maembe
KATIBU MKUU
19/03/2015

WADAU WA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI (HPV) WAKUTANA KILIMANJARO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa Wadau wa Chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV) katika ukumbi wa Uhuru Hostel mjini Moshi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa karibu hotuba ya mkuu wa mkoa Gama.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TAARIFA YA MSIBA: MKE WA PROF MLEKWA WA UDSM AFARIKI DUNIA

$
0
0
Familia ya Prof Victor Mlekwa wa  Savery Mlalakuwa, Dar Es Salaam


Inasikitika kutangaza kifo cha mama yao Febronia Mshomba Mlekwa kilichotokea tarehe 16/02/2015 Katika Hospitali ya Kairuki, Dar Es Salaam.
Mazishi yatafanyika tarehe19/02/2015 Alhamisi, Goba Dar Es Salaam.

Wale wote watakao kuungana penda na wafiwa, wanakaribishwa nyumbani kwa Mrehemu Savery mapema. Wote tunawatakia pole ya msiba.

MHE. NYALANDU AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MALIASILI, ARDHI NA MAZINGIRA KUTOKA NCHINI NORWAY

$
0
0
Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu ( katika kati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola Elvestuen (kushoto) wakiwa na Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) Kabla ya Mkutano wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola Elvestuen ( kushoto) akimakabidhi zawadi Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu baada ya Mkutano wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.
Waziri waWizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway kwenye Mkutano uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam.

The African Development Bank Group Supports Power Trade between Kenya and Tanzania ADF USD 144.9 million Loan to Kenya – Tanzania Power Interconnection Project

$
0
0
The Board of Directors of the African Development Bank Group (AfDB) approved an African Development Fund (ADF) Loan of USD 144.9 million1, to Kenya - Tanzania Power Interconnection Project.

The project will allow the two countries to exchange power. In addition, the Kenya-Tanzania Interconnection Project plays an important role in promoting regional integration through power trade.

The project is expected to improve the supply, reliability and affordability of electricity in the Eastern Africa region through cross-border exchanges of cheap and cleaner surplus power The project involves the construction of approximately 508 km of transmission line between Kenya and Tanzania (about 93 km in Kenya and 415 km in Tanzania) and associated substations in Arusha and Singida (Tanzania).

The line will have a transfer capacity of up to 2,000 MW in either direction. It will allow to interconnect Eastern Africa Power Pool to the Southern African Power Pool and further in the future to Northern Africa through East Africa Electricity highway project, the Ethiopia – Kenya interconnection line. At initial stage, the project will allow the two countries to exchange power and followed by import and export energy from the interconnected countries.

Following the Board’s approval, the Director of the AfDB’s Energy, Environment and Climate Change Department, Alex Rugamba, explained that, the project aligns with the pillars of the regional integration strategy papers (RISPs) for Eastern Africa which focus on regional infrastructure and capacity building and fulfills the objectives of the New Partnership for Africa'sDevelopment (NEPAD), in terms of regional integration and promotion of infrastructure development through regional co-operation in key productive sectors such as energy.

He also added that the interconnection line will create competitiveness in the energy sector and encourage the private sector investing in generation of electricity by facilitating power transfer through the interconnector.

BREAKING NYUZZZ...: MWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI ZANZIBAR AFARIKI DUNI GHAFLA MCHANA HUU

$
0
0

Habari iliyotufikia hivi punde toka Visiwani Zanzibar,inaeleza kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni,Mhe. Salmin Awadh amefariki dunia mchana huu baada kuanguka ghafla akiwa kikaoni katika Afisi kuu ya CCM kisiwandui,mjini Unguja Zanzibar.

Pichani ni Mwili wa Mwakilishi huyo ukipakiwa kwenye gari ukitolewa kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja kwenda nyumbani kwake kwa matayarisho ya mazishi.

taarifa kamili tutapeana hapo baadae.
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live




Latest Images