Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 741 | 742 | (Page 743) | 744 | 745 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Chifu Abdu Adam Mkwawa, ambaye aliaga dunia jana, Jumamosi, Februari 14, 2015 hospitalini mjini Iringa.

  Katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza leo, Jumapili, Februari 15, 2015, Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na kushtushwa na kifo cha Chifu Mkwawa ambaye amemwelezea kama “Chifu mzuri, kiongozi na mtu wa watu, ambaye katika maisha yake yote alihangaika kuenzi na kudumisha kumbukumbu za utamaduni wa Mkoa wa Iringa, za machifu wa mkoa huo na utalii wa Iringa.”
  Rais Kikwete amemweleza Mheshimiwa Masenza: Nawapeni pole sana na naungana nawe, familia ya marehemu na wananchi wote wa Mkoa wa Iringa katika kuomboleza maisha ya Chifu na kiongozi ambaye tutaendelea kumkumbuka kwa mchango wake katika kujenga na kuendeleza mahusiano mazuri ndani ya jamii. Aidha, naungana na familia katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Abdu Adam Mkwawa. Amen.”

  Wakati huo huo, kesho, Jumatatu, Februari 16, 2015, Rais Kikwete ataungana na wananchi wa Mkoa wa Iringa katika mazishi ya Marehemu Mkwawa.

  0 0

   Dkt. Aziz Ponary Mlima Balozi wa Tanzania nchini Malaysia akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Laos Mheshimiwa Choummaly Sayasone. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Vientiane nchini Laos.
  Dkt Aziz Mlima akifanya mazungumzo na Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Laos ambaye aliwahi kuwa Balozi wa Laos kwenye Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu Mheshimiwa Alounkeo Kittikhoun.Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia unawakilisha nchi nyingine 6 katika ukanda wa Kusini Mashariki mwa Asia.

  0 0
 • 02/15/15--13:17: S.U.A "Stand Up Arusha"
 • S.U.A "Stand Up Arusha" is a Street Art Celebration of Peace,Love,Unity and Happiness under the Okoa Mtaa Foundation since 2012 that include Audio and Visual Artists. 
   From 4th-6th April at AICC ground (Impala Round About). The whole Africa and The whole World will "Stand Up for Arusha" Arusha has its Unique Strong Youth Culture that can Create a Generation with Intelligent,Wisdom and Understanding. 
  Come and  Celebrate and Experience How we Talk,Walk and Wear,The way we Dance,What we eat and you will know and See How Unique and Blessed Arusha is. Come Meet with Arusha Positive Arts and People who works to Make you FALL IN LOVE with ARUSHA.
  Apart from Street Arts Exhibition, Artist Live Performance,The Street Fashion,Workshops and Seminars 
  SUA is now having a lot of Surprises that has been Stored safely waiting for April 4th-6th. Addition: Kids Corner,Food and Beverages,Pool Table,Sheesha,Local and Many More. NOW YOU HAVE REASON TO BE IN ARUSHA IN APRIL 2015 
   The Doors are Still Open for Partners,Sponsors,Donors,and Arts Exhibitions. https://www.facebook.com/SuaTanzania +255 783 853 853/+255 719 300 204 #Back2Sua


  0 0
  0 0

  Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limewakamata majambazi wanne (4) waliomuua ASHELI S/O MAGINA mwenye miaka 40, Msukuma, Mfanyabiashara/Mkulima wa Kijiji cha Bubutole kwa kumkata na mapanga kichwani na mikononi na kufariki papo hapo tukio lililotokea tarehe 11/02/2015 majira ya saa 02:00hrs usiku katika Kijiji cha Bubutole Kata ya Farkwa, Tarafa ya Farkwa Wilaya ya Chemba Mkoani humo.

  Amewataja majambazi hao waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kuwa ni:

  1.    HASSAN S/O MAULIDI @ SALAMA, mwenye miaka 32, kabila Msandawe, Mkulima.
  2.    HAMADI S/O HUSSEIN mwenye miaka 25, kabila Msandawe, Mkulima.
  3.    RASHID S/O YUSUPH, mwenye miaka 21, kabila Msandewe, Mkulima.
  4.    ABDALAH S/O SWALEHE @MUNA, mwenye miaka 25, kabila Msandawe, Mkulima, wote wakazi wa Kijiji cha Porobanguma Wilayani Chemba Dodoma.

  Kamanda MISIME amefafanu kuwa majambazi hao walimvamia ASHELI s/o MAGINA nyumbani kwake akiwa amelala dukani na kumshambulia kwa mapanga na kufariki dunia kisha kupora mali mbalimbali ikiwemo pikipiki, mifuko miwili ya sukari ya kilo 25, mifuko miwili ya unga wa ngano ya kilo 25 na soda kreti tatu(3) mali ambayo thamani yake haijafahamika.

  Ameendelea kusema kwamba majambazi hao walikamatwa wakiwa na pikipiki yenye namba T. 449 CQP aina ya SUNLG mali ya marehemu waliyopora eneo la tukio na baadhi ya mali walizopora kama sukari na maharage. Pia waliweza kuonyesha mapanga waliyotumia kumkatakata nayo ASHELI s/o MAGINA. 

  Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa HASSAN s/o MAULIDI @ SALAMA alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la mauaji ya IJUMAA S/O SAID mwenye miaka 30, Msandawe Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Monjore Banguma kwa kumchoma na kisu tukio lililotokea tarehe 19/01/2015 majira ya saa 18:30hrs katika kijiji cha Porobanguma kwa kile kilichodaiwa kua ni ugomvi uliyotokea baina yao. Uchunguzi zaidi unaendelea na ukikamilika watafikishwa mahakamani.

  Kamanda MISIME ametoa wito kwa Wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, kwani wahalifu wanaishi katika jamii na kufanya uhalifu ndani ya jamii. Wahalifu wasifumbiwe macho.

  0 0

  Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) imeandaa  mkutano  wa kikanda  utakaokutanisha viongozi na watunga sera  kutoka  nchi  za Afrika mashariki kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadaye ya miji ya Afrika.

  Mkutano huu uliopewa jina la, ‘Maisha ya baadae ya nchi za Afrika Mashariki: Jinsi gani tunataka kuishi mwaka 2050’, utafanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, Kilimanjaro Hotel tarehe 19 na 20 Februari ambapo Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda (Mb), atakuwa mgeni rasmi.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute, Prof. Joseph Semboja alisema kwamba jukwaa hilo linalenga kuangalia na kujadili changamoto na fursa mbalimbali zinazoletwa na ukuaji wa miji  Afrika Mashariki na jinsi gani viongozi wa Afrika wanaweza kukabiliana nazo kwa pamoja. 

  “Kuna uwiano mkubwa wa ongezeko la watu Afrika (na duniani kwa ujumla) wanaoishi mijini na kupelekea msongamano na shinikizo la nyumba, ajira na huduma za kijamii. Ni kwa matokeo haya jukwaa hili limelenga kujadili namna ya kutatua changamoto hizo na kufikiria miji ambayo itatimiza matakwa yetu,” alisema Prof. Semboja. 

  Kwa mujibu wa chapisho la UN-Habitat  ‘Hali ya miji ya Afrika 2014’ , “Afrika Mashariki inashika nafasi ya chini katika miji inayokua duniani lakini ndiyo kanda inayoongoza katika kasi ya ukuaji wa miji yake hivi sasa.  Ifikapo mwishoni mwa muongo huu wa sasa idadi ya wakazi waishio mijini itaongezeka kwa asilimia 50 na jumla ya idadi ya wakazi wa mijini ifikapo mwaka 2040 inatarajiwa kuwa mara tano ya 2010.
  Hivyo basi, ukanda wa Afrika Mashariki utakumbwa na changamoto zitakazotokana na ongezeko kubwa la  idadi ya watu mijini; ongezeko kubwa la madai mapya na ya ziada kwa ajili ya utoaji wa nyumba za kutosha na kwa gharama nafuu na huduma mijini, na pengine muhimu zaidi, fursa ya kuzalisha kipato mijini.”

  “Ni dhahiri kwamba ukuaji wa miji na maendeleo mijini ni matokeo chanya ya maendeleo ya binadamu na ukuaji wa kiuchumi kama tunaweza kuyakabili kiusahihi. Na hii ndiyo maana nzima ya mkutano huu…Kutuweka katika njia sahihi kwa kutambua vipaumbele vya juu na vitu  muhimu kwa ajili ya maendeleo," aliongeza Prof. Semboja. 
  Washiriki wa kongamano hili watatoka: Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan ya Kusini, Tanzania na  Uganda. Waalikwa watakuwa wawakilishi wa ngazi za juu kutoka serikalini, mashirika ya kikanda na kimataifa, miji mikubwa, wasomi, sekta binafsi na asasi za kiraia.


  0 0

  Mbio za Kilimanjaro Marathon 2015 zitafanyika kwenye njia ile ile iliyotumika mwaka jana baada ya kupimwa na kuidhinishwa na shirikisho la riadha duniani. Njia hiyo ni mzunguko na imelenga kuwafanya wanariadha wakimie kwa raha na usalama zaidi bila tatizo la msongamano barabarani.

  Akizungumzia njia hiyo Mkurugenzi wa Kilimanjaro Marathon, John Bayo amesema “Ni njia nzuri sana. Mbio za Full marathon zitaanzia uwanja wa Ushirika na kwenda kilomita kumi njia ya kuelekea Dar es salaam na kurudia njia hiyo kupitia geti la Chuo cha Ushirika. Wakati wanariadha wa kilomita 42 wanapita mbele ya geti, wale wa kilomita 21 (Tigo Kili Half Marathon) watakuwa mbele yao kwa takribani dakika 30 maana mbio yao inaanzia kwenye geti la Ushirika na kupandisha kuelekea Mweka kwa umbali wa kiomita 8”.

  Baada ya kilomita 8, njia wataacha barabara ya lami kukimbia kwenye barabara ya vumbi kwa kilomita mbili kupitia mashamba ya kahawa ili kuipata Barabara ya Lema ambapo wataendelea kukimbia na kupita Shule ya Kimataifa ya Moshi na kutelemka kuelekea uwanjani. Bayo alisema kwamba njia nzima ina viburudisho vya kutosha pamoja na vituo vya maji na vile vile magari ya huduma ya kwanza.

  Mbio za walemavu zitaanzia uwanja wa Ushirika na kuifata Barabara ya Kilimanjaro ambayo ni tambarare tupu na ina kivuli hadi Barabara ya Lema ambapo watageuza na kurudi Uwanjani wakiwa wamekamilisha kilomita 10.  

  John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema njia hiyo mpya itapendwa na wanariadha kwakuwa inapita maeneo yenye mandhari nzuri ya miti na mashamba na  njia hiyo haina msongamano na anaamini kwamba washiriki watakimbia kwa raha katika mbio hizo zitakazofanyika tarehe 1 Machi, 2015.

  Aliongeza kuwa mbio ndefu la Kilimanjaro Premium Lager Marathon za kilomita 42 zitaanza saa 12.30 asubuhi kutokea uwanja wa Ushirika wakati mbio za Tigo Kili Half Marathon zitaanzia nje ya geti la Chuo cha Ushirika saa moja kamili asubuhi na kukimbia wakielekea Mweka na mbio yao itaishia hapo hapo uwanjani. Wakati huo huo mbio za walemavu za Gapco zitaanza saa 12.45 (saa moja kasorobo) kutokea uwanja wa Ushirika na huku mbio za kujifurahisha za 5 km Fun Run zikianza saa 1.45 asubuhi kwenye mzunguko wa YMCA na kumalizikia uwanjani.

  Mbio za Kilimanjaro Marathon 2015 zinaratibiwa na Executive Solutions kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Riadha Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Tigo, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,  CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, Kibo Palace Hotel, UNFPA na Kilimanjaro Water.

  0 0

  Bwana Harusi Maneno Abdallah na Mkewe Bi Nusrat Tahwa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga ndoa hapo jana
   Bwana harusi akielekea kuchukua jiko lake Kimara huku akisindikizwa na wapambe na Mshenga wake.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Mke wa Msanii mkongwe wa muziki wa dansi na Mjumbe wa Bodi ya BASATA Bw. John Kitime kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa kuamkia Ijumaa ya Tarehe 13/02/2014.

  Aidha, BASATA linatoa salamu rambirambi kwa kifo cha Baba Mzazi wa Msanii Dully Sykes, Mzee Abby Sykes kilichotokea jana Jumapili ya Tarehe 15/02/2015.

  Pamoja na vifo hivi kuacha majonzi na huzuni kwa wanafamilia, ni pigo pia kwenye tasnia ya Sanaa kutokana na ukweli kwamba wote wawili kwa njia moja ama nyingine wamekuwa na mchango katika kuhakikisha tasnia hii inasonga mbele kwa kuwa karibu na wasanii John Kitime na Dully Sykes sawia.

  Baraza linatoa pole kwa wadau wote wa Sanaa hususan wasanii na Umoja wa mabloga nchini kwa misiba hii. Ni matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu hawa hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu.

  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen

  Godfrey Mngereza
  KATIBU MTENDAJI

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu Dr Kamugisha Kazaura atembelea mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Mbeya ikiwa na lengo la kukagua miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TTCL wa mikoa hiyo.

  Dr Kazaura ailijionea juhudi mbalimbali zinazofanywa na wafanyakazi wa TTCL katika kuhakikisha miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inakuwa salama muda.

  Hivi sasa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imekuwa kampuni pekee ya mawasiliano ambayo imefanikiwa kuunganisha wateja mbalimbali kupitia mtandao wake.

  Wateja hao ni pamoja na TAMISEMI, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mabenki, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG),Wizara ya Fedha, watoa huduma za mtandao/intaneti (ISPs) pamoja Makampuni ya Simu

  Pia TTCL imefanikiwa kuunganisha nchi jirani katika ukanda huu wa afrika Mashariki (Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda) pamoja na nchi za kusini wa Jangwa la Sahara (SADC) ambazo ni Malawi na Zambia.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua mitambo ya TTCL mkoani Lindi.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akipokea maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa TTCL Mtwara kuhusu juhudi zinazofanyika kulinda na kusimamia mitambo yake.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua Mtambo wa Mkongo wa Taifa, pembeni yake ni Mkuu wa Idara ya Ufundi wa TTCL,Senzige Kisenge.


  0 0

   Umati wa waombolezaji ulioshiriki kwenye mazishi ya Mke wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,Bw. John Kitime,Marehemu Janeth Joan Chidosa Kitime alizikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
  Taratibu za mazishi zikiendelea kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam leo.
   Mume wa  Marehemu Janeth Joan Chidosa Kitime,Bw. John Kitime akitoka kuweka shada la maua kwenye kaburi la mkewe wakati wa mazishi yaliyofanyika jioni hii kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.
  Watoto wa Marehemu wakielekea kuweka shada la maua kwenye kaburi la Mama yao.
   Mfiwa Bw. John Kitime katikati akiwa na Watoto zake mara baada ya Mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni,jijini Dar es salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mh, Wilman Kapenjama akikabidi funguo ya gari kwa Mshindi wa Promosheni Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara bw, Sefu Namtapika (60) ambae ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi inayoendesha na Airtel. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni toka kushoto nyuma ni Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu, Afisa Masoko wa Airtel Bi Aminata Keita, na Meneja Biashara wa kanda ya Pwani Bw Albert Majuva.

  Meneja Biashara wa kanda ya Pwani Bw Albert Majuva (wakwanza kulia) akimpongeza Mshindi wa Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara bw, Sefu Namtapika ambae ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi inayoendesha na Airtel. Anaefuata ni Afisa Masoko wa Airtel Bi Aminata Keita na Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mkoani humo kwenye viwanja vya mashujaa mwishoni mwa wiki.

  Meneja uhusiano wa Airtel bw, Jackson Mmbando akiongoza umati wa wakazi wa mkoani mtwara waliojitokeza katika viwanja vya Mashujaa kushudia hafla ya makabidhiano ya gari Toyota IST kwa mshindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel yatosha Mzee Sefu Namtapika mwishoni mwa wiki hii.

  Mshindi wa gari aina ya Toyota IST mzee Sefu Namtapika akipongezwa na mke wake Bi… mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya gari alilojishindia kupitia promosheni ya Airtel Yatosha zaidi. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani mtwara mwishoni na wiki na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini mh, Wilman Kapenjama.


  0 0

  Mwili wa baba wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes,Marehemu Ebby Sykes ukiswaliwa nyumbani  kwa kaka wa marehemu maeneo ya Kawe jijini Dar leo mchana.Marehemu Ebby Sykes amezikwa jioni hii kwenye makabiri ya Kisutu.
   Mwili wa Marehemu Ebby Sykes ukipandishwa kwenye gari kwa safari ya kwenda kwenye mazishi,makaburi ya Kisutu jijini Dar jioni hii.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes akiwa amepanda gari lililobeba mwili wa Marehemu baba yake kwa safari ya kwenda kupumzishwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar leo
  Baadhi ya wasanii pamoja na ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba wa marehemu Ebby Sykse.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu warsha maalumu iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 7, 2015 ukumbi wa Mlimani City. Wengine kutoka kushoto ni maofisa wa Trumark,  Antu Mandoza na Nuru Lyau.
   Mratibu wa Warsha hiyo Antu Mandoza (kulia), akisisitiza 
  jambo wakati akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa warsha hiyo, Nuru Lyau.
   Ofisa wa Kampuni ya Trumark, Zulekha Samwix (kulia), akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  …………………………………………..
  Na Dotto Mwaibale
   
  KAMPUNI ya TruMark ya jijini Dar es Salaam imeandaa warsha yenye lengo la kumjengea mwanamke uwezo wa kutambua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa.
   
  Hayo yamemwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Agness Mgongo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
  Mgongo alisema warsha hiyo itafanyika Machi 7, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa  Mlimani City ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
   
  ‘Tunataka tumjengee mwanamke uwezo wa kujiamini, kujithamini na kutambua kuwa changamoto anazozipata ni fursa zitakazomfanya aweze kupambana na makali ya maisha na kisha kujiendeleza bila kumtegemea mwanaume’ alisema Mgongo.
   
  Aidha Mgongo alisema kuwa warsha hiyo itajumuisha shuhuda na maonesho ya bidhaa na kazi za mikono kutoka kwa wanawake waliofanikiwa kupitia changamoto mbalimbali walizozipitia.‘Siwezi kuwataja ila watakuwepo wanawake ambao walikumbwa na changamoto mbalimbali lakini hawakukata tamaa na mwisho wa siku wakafanikiwa,’ alisema Mgongo.
   
  Naye kwa upande wake Mratibu Mkuu wa warsha hiyo, Antu Mandoza alisema kuwa kutakuwa na kiingilio cha sh. 50,000 ambayo asilimia 10 ya fedha zitazopatikana zitaelekezwa katika kuwaandaa wasichana kujitambua mapema kabla ya kuingia katika soko la ajira.
   

  ‘Tutaenda katika shule mbalimbali za wasichana kuwafundisha mbinu nbalimbali za kuwa wajasiriamali na kujiajiri punde wanapohitimu masomo yao’ alisema Mandoza.

  0 0

  DSC_0358
  Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 40 na meza za walimu wenye thamani ya sh. milioni 5 katika shule za msingi  Mwaramu,iliyomo wilayani humo,huku msaada huo ukiwa umetokana na faida inayopata benki hiyo.

  Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo,meneja wa benki  hiyo kanda ya kaskazini, Vicky Bishubo alisema benki hiyo imeamua kutoa msaada wa madawati hayo baada ya kuona shule nyingi zikikosa madawati na wanafunzi wake wakikaa chini kwenye sakafu.

  Alisema kutokana na hali hiyo wanafunzi wengi wamekuwa hawazingatii masomo pindi wawapo darasani kwa sababu ya ukosefu wa vitendea kazi vya madarasani hususani madawati.

  ‘’leo benki ya NMB imeamua kutoa msaada wa madawati 40 , meza za walimu na viti wenye thamani ya shilingi milioni 5 ,tumeamua kufanya hivyo kutokana na uhitaji wa shule husika napenda niwahakikishie kuwa benki yenu imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuirudishia jamii faida kidogo inayopata’’alisema Bishubo

  Bishubo aliongeza kuwa,benki hiyo iliamua kutoa msaada wa madawati hayo ya wanafunzi ili kuweza kutoa motisha kwa wanafunzi hao kuweza kusoma kwa bidii kwa madai kuwa kutokuwepo kwa vitendea kazi mashuleni ni moja ya sababu zinazopelekea wanafunzi wengi kufeli.

  "Msaada huu wa madawati  umetokana na faida kidogo ambazo benki inapata hivyo tumeona katika faida hizo ni jambo jema kutoa msaada wa aina hii kwa ajili ya kuweza kuendeleza watoto kielimu kwani wao ndiyo Taifa la kesho," alisema Bishubo.


  Naye Meneja wa NMB tawi la Hai Merdadi Malisa alisema benki hiyo imejipanga kusaidia jamii  katika wilaya hiyo kwa kutoa msaada pindi inapohitajika na kuwataka wananchi kufungua akanti katika benki hilo ili kuiwezesha benki hiyo kupata faida zaidi.
  Kwa upande wake Mkuu wa Hai , Novatus Makunga aliipongeza benki ya NMB kwa kutoa msaada huo na kuwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki hiyo kwa kutoa mchango kama huo ili kupunguza ya madawati wilayani huo.

  Alisema wilaya ya Hai inakabiiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa madawati hata hivyo alisema taitizo hilo lipo kwa baadhi ya shule za msingi na wilaya ipo kwenye mkakati wa kukabiliana nalo.

  ‘’Changamoto ya madawani ipo sana katika wilaya yetu ya Hai ila tunajitahidi kukabiliana nayo kwa kuwatumia wadau mbalimbali hususani nyie wa NMB ,najua benki itakuwa imepokea maombi mengi lakini tunawapongeza kwa kuona umuhimu wa kutoa katika shule ya msingi Mwaramu iliyopo wilaya yangu,alisema

  Aliwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki ya NMB,kwa kuisaidia serikali kupunguza changamoto zilizopo kwenye shule mbalimbali hapa nchini hasa za msingi ambako ndiko tatizo kubwa lilipo.
  ‘’Kupatikana kwa madawati haya naimani kutaongeza ari ya ufaulu kwa wanafunzi sambamba na walimu kuongeza ari ya ufundishaji katika shule hii’’alisema Makunga

  habari hii kwa hisani ya libeneke lakaskazini blog

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua dawati lenye ubora uliothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lililobuniwa na kutengenezwa na Kampuni ya EDOSAMA HARDWARE ya jijini Dar es salaam. Dawati hilo linalotengenezwa kwa mbao laini ambazo zimebanwa bila kutumia misumari linakadiriwa kugharimu sh. 80,000/=. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Eric Shigogo, Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Benki ya TIB, Masanja Kungu, na Mkurugrnzi Msaidizi wa Kampuni hiyo,Edward Saguda.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua dawati lenye ubora uliothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lililobuniwa na kutengenezwa na Kampuni ya EDOSAMA HARDWARE ya jijini Dar es salaam. Dawati hilo linalotengenezwa kwa mbao laini ambazo zimebanwa bila kutumia misumari linakadiriwa kugharimu sh. 80,000/=. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Eric Shigogo, Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Benki ya TIB, Masanja Kungu, Ofisa Mazingira, Daniel Kapakala na Mkurugrnzi Msaidizi wa Kampuni hiyo,Edward Saguda.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua dawati lenye ubora uliothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania lililouiniwa na kutengenezwa na Kampuni ya EDOSAMA HARDWARE ya jijini Dar es salaam, ofisini kwake Februari 16, 2015. Dawati hilo linalotengenezwa kwa mbao laini ambazo zimebanwa bila kutumia misumari linakadiriwa kugharimu sh. 80,000/=. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Eric Shigogo, Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Benki ya TIB, Masanja Kungu, Ofisa Mazingira, Daniel Kapakala na Mkurugrnzi Msaidizi wa Kampuni hiyo,Edward Saguda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hiki cha HUYU NA YULE
  Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi
  Tumefanya mazungumzo naye ya sehemu nne, kueleza safari yake kimaisha
  Tunaendelea na sehemu ya tatu ya mazungumzo yetu, ambapo Mhe Balozi Nyang'anyi anaanza kuelezea namna
  1: Alivyoingia kwenye siasa (ubunge mwaka 1970)
  2: Alivyopata taarifa za kwanza za uteuzi wake serikalini. Hapa napo pana mvuto wake kusikiliza.
  3: Nafasi alizoshika kama naibu waziri na waziri kamili
  4: Nafasi ya ukuu wa mkoa
  5: Na hata harakati zake na pia alivyopata nafasi ya kuja kusoma Chuo Kikuu Havard
  KARIBU

  0 0

  Kufahamu Vodashop iliyo karibu nawe ili kujipatia simu hii ingia https://www.vodacom.co.tz/productsandservices/devices/vodacom-zte

  0 0
 • 02/16/15--12:00: HII NI MAKUSUDI KABISA
 • Pichani kulia gari yenye namba za usajili T545 DBR ikivunja sheria za barabarani kwa makusudi kabisa katika makutano ya barabara eneo la Manyanya Kinondoni jijini Dar jioni ya leo.


older | 1 | .... | 741 | 742 | (Page 743) | 744 | 745 | .... | 3284 | newer