Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

YANGA YAIADHIBU TIMU BDF XI FC YA BOTSWANA KWA BAO 2-0

$
0
0
 Mchezaji wa timu ya Yanga,Mrisho Khalfan Ngassa akiwania mpira na Mchezaji wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0 zilizotiwa kimiani na Mshambuliaji Hamis Tambwe dakika ya kwanza ya mchezo na 55. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
 Golikipa wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana akiondosha hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni mwake wakati wa Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0.
 Winga machachari wa Yanga,Saimon Msuva akiangalia namna ya kumtoka beki wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana,Othusitse Mpharitlhe wakati wa Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo.Yanga imeshinda bao 2 - 0.
Beki wa Yanga,Mbuyu Twite akirusha mpira kwa ustadi mkubwa.


MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKABIDHI KATIBA PENDEKEZWA KWA WILAYA ZOTE MKOANI RUKWA LEO

$
0
0
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akimkabidhi Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian Katiba pendekezwa leo tarehe 14 Februari 2015 kwa niaba ya wananchi wa Wilaya hiyo ambao watapata fursa ya kuiona na kuisoma kwa ajili ya kuipigia kura ya maoni mwezi Aprili mwaka huu. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha muimbaji wa kikundi cha ngoma za asili ya Kanondo Katiba pendekezwa katika hafla fupi ya kukabidhi Katiba hiyo iliyofanyika katika Wilaya ya Kalambo. \Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha Ndugu Mulele Mulenda Mwanaukawa aliyeshiriki hafla hiyo fupi ya kukabidhi Katiba pendekezwa kwa niaba ya Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Kalambo sehemu ya vifungu vya katiba pendekezwa ambavyo vipo na vilikuwepo kwenye rasimu ya Katiba ya Jaji J. Warioba ambpo ni kinyume na inavyodaiwa na UKAWA kuwa vimechakachuliwa.
 Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo, Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kalambo muda mfupi baada ya kukabidhi Katiba pendekezwa. Aliwataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi mwezi April kwa ajili ya kuipigia kura  katiba hiyo na kutopotoshwa kwa namna yeyote ile na watu wasioitakia mema nchi yao. Alisema kuwa katiba hiyo ni nzuri kwani imegusa maslahi ya watanzania wote na ustawi wa taifa kwa ujumla. 

Baadhi ya wananchi wakionekana kujifunika na mwanvuli kufuatia mvua iliyokua ikinyesha mwishoni mwa hafla hiyo.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)

BARNABA BOY NA AMINI WATINGA RADIO KASIBANTE 88.5 FM RADIO BUKOBA, TAYARI KWA KUTOA BURUDANI LEO VALENTINE DAY LINA'S NIGHT CLUB

$
0
0
Mwanamuziki anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini Elias Barnabas ‘Barnaba’ akiimba moja ya wimbo wake Ndani ya Studio Radio Kasibante 88.5 FM huku akipiga Gitaa lake..
Mzee wa Robo saa Amini akitokelezea leo wakati anazungumza na Wananchi wa Bukoba Kupitia Radio Kasibante 88.5 FM leo ambapo usiku huu watakuwa pamoja na Barnaba kwenye Ukumbi wa Lina's Night Club kutoa Burudani ya Nguvu na Special kwa Siku ya Wapendanao "Valentine Day" Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Msanii Elias Barnabas ‘Barnaba’ akifanya yake..
Mc Jerry kutoka Shemeji Investment ambaye ni mmoja wa Waandaji wa Show ya leo akitoa ufafanuzi wa Tiketi kupitia Radio Kasibante Fm.Mc Jerry na Barnaba
Msanii wa bongo flava aliyefanya Vyema kwenye Jumba la (THT) Tanzania House of Talent, Amini Mwinyimkuu na (kulia) ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Zachwa Investment ambaye ndie Mwandaaji akishirikiana na Shemeji Investment kuandaa Show bab kubwa ambayo itapambwa na Wasanii hao kutoka Jijini Dar es salaam leo siku ya Valentine Day kwenye Ukumbi wa Lina's Night Club. Hapa walikuwa kwenye Chumba cha Radio kasibante wakifanya mahojiano na Mtangezaji Nicolaus Ngaiza (hayupo pichani). Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Faustine Ruta wa bukobasports.com(kushoto) akiwa na Msanii wa Bongo Flava Amini nje ya Jengo la Kasibante FM Radio leo hii jioni.

Miss Rahima Jackson na Jae Star, watoa kibao kipya cha ''MALAIKA FT!"

$
0
0
Sikiliza kibao kipya cha ''MALAIKA FT''kutoka kwa Miss Rahima Jackson akishirikiana na Jae Star, waTanzania ndani ya Wasahington Seattle, Nchini MAREKANI..!

SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

Mwandani wa: Mapango ya Amboni mkoani Tanga

$
0
0
Na Sultani Kipingo 
Mapango maarufu ya Amboni mkoani Tanga ni eneo kubwa kuliko yote lenye majabali ya chokaa katika Afrika Mshariki. Yapo takriban kilomita nane hivi Kaskazini mwa mji wa Tanga, njia ya kuelekea huko ikichepuka huko toka barabara kuu ya Tanga-Mombasa. 
Kumbukumbu zilizopo zinaonesha mapango hayo yalizuka kiasi cha miaka milioni 150 iliyopita, katika zama za mijusi wakubwa ijulikanayo kama Jurassic age. 
Eneo lake lina kilomita za mraba 234, na kwa mujibu wa watafiti, eneo hilo lilikuwa chini ya maji yapata miaka milioni 20 iliyopita. 
Ndani ya eneo hilo kuna jumla ya mapango 10, ila hadi sasa ni mawili tu yatumikayo kwa watalii wa ndani na nje, watafiti na wanafunzi wa somo la jiografia wanapofanya ziara za kimasomo. 
Mnamo mwaka 1892, kampuni ya Amboni iliyokuwa inalima katani mkoani Tanga, ililichukua eneo hilo, na baadaye ikaiarifu serikali ya mkoloni ya Uingereza wakati huo kuhusu mapango hayo, na mara moja ikaamuliwa mapango ya Amboni ni eneo la hifadhi tokea mwaka 1922. 
Haijulikani ni lini hasa mapango ya Amboni yaligunduliwa lakini ripoti zinaonesha kuwa wenyeji wa mkoa wa Tanga walikuwa wakiyatumia kama sehemu ya matambiko, jambo ambalo inasemekana hadi hii leo linaendelea. 
Mnamo mwaka 1963, Serikali ya Tanganyika wakati huo, kwa kuona umuhimu wa mapango hayo kihistoria na kihifadhi, ikaamua kuyakabidhi kwa Idara ya Mambo ya Kale kwa usimamizi. Hadi leo mapango ya Amboni yapo chini ya Idara hiyo. 
Pamoja na mambo mengine, mapango ya Amani huvutia watalii, watafiti na wanafunzi kwa vivutio vya kusisimua, ikiwa ni pamoja na jinsi mamilioni ya popo hutoka mapangoni na kwenda kutafuta riziki nje kila jua linapotua. Wingu kubwa jeusi la popo huziba lango kuu kwa muda wakati wanyama hao wanapotoka kwenye mapango hayo ya giza.
Vile vile katika mapango hayo kuna miamba yenye maumbo kama ya sofa, meli, mamba, tembo, kichwa cha simba dume, ramani ya Afrika na hata kile kinachoonekana kama mnara wa Uhuru wa Marekani “Statue of Liberty”
Sehemu ya mapango ya Amboni mkoani Tanga

Utalii wa ndani
Bango la Idara ya Mambo ya Kale

JUST IN: TAARIFA RASMI YA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA MAPAMBANO NA MAJAMBAZI TANGA

JIPATIE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA QT YA MWAKA 2014 YOTE HAPA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa  kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini  (NECTA),Dk.Charles Msonde amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu umeongezeka  kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab ,Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia wavulana.

Shule za Sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine.

Msonde amasema matokeo hayo  yanatokana na mfumo mpya  wa GPA kwa kuangalia masomo saba  hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini dar leo.



ngoma azipendazo ankal - "Laiti moyo"

MH. MAKALAA ZIARANI WILAYA YA MWANGA,MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla ameendelea na ziara zake za kukagua maendeleo ya miradi mbali mbali ya maji,ambapo safari hii ilikuwa ni mkoani Kilimanjaro na alianzia wilaya ya Mwanga.

 Katika ziara hiyo amekutana na kuongea na uongozi wa wilaya ya Mwanga na baadae kuongozana nao katika ukaguzi wa miradi ya maji iliopo kwenye vijiji vya Kisanjini,Msangeni na Lomwe na pia alikagua maandalizi ya vifaa na eneo patakapojengwa mradi mkubwa wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe utakaogharimu dola za kimarekani milioni 41.5.

Akiongea na wananchi kijiji cha njiapanda unapojengwa mradi huo,Mh. Makalla amesema amefurahishwa na mkandarasi kuanza kazi na amewataka waanchi kutoa ushirikiano na wawe waaminifu kwa wale watakaopata ajira.Mradi huo utachukua miezi 31 na utanufaisha vijiji 17 vya wilaya ya Same, vijiji 16 vya wilaya ya Mwanga na vijiji 5 vya wilaya ya Korogwe
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akilakiwa na viongozi wa Wilaya Mwanga,wakati akiwasili.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akipata maelezo ya mradi wa maji wa Same,Mwanga mpaka Korogwe toka kwa Mhandisi Mshauri wa mradi huo,Bw. Sharif Salah.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiongea na wananchi wa kijijji cha Msangeni,Wilayani Mwanga.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiongea na Mhandisi Mshauri wa mradi Same-Mwanga-Korogwe,Bw. Sharif Salah.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiongozana na Mhandisi Mshauri wa mradi Same-Mwanga-Korogwe,Bw. Sharif Salah pamoja na ujumbe wake wakati wa kukagua mradi huo.

INAFRIKA BAND KUTOKA DAR WATINGISHA JIJI LA BREMEN,UJERUMANI, TANZANIAN FOLK MUSIC MADE IN BONGO TO THE WORLD YAKUBALIKA KIMATAIFA!

$
0
0
Bendi ya muziki INAFRIKA BAND aka "Wazee wa Indege" kutoka jiji Dar es salaam, imelitingisha jiji la Bremen, nchini Ujerumani katika onyesho liliofanyika usiku wa 13 Februari 2015 katika ukumbi mkubwa wa Musik-Theater mjini humo. 
Bendi hiyo kutoka Chang'ombe ilisimama jukwaani na kuziteka nyoyo za maelfu ya wapenzi wa muziki kiasi cha kutajwa kuwa bendi bora ya muziki wa Folk na radio Funkhaus-Europe kutokana na vionjo vya mitindo ya muziki wa asili wa makabila ya Kitanzania vilivyotumiwa na Inafrika Band katika kuteka yonyo za washabiki kila kuona duniani.
 Inafrika Band, ambayo  imefanikiwa kuliweka jina la Tanzania katika tufe la dunia kwa kutumia mitindo yake ya vionjo vya kiasilia, inaongoza katika  kufanya tour ndefu duniani,
Hadi sasa  wameshafanya ziara katika mabara yote duniani kuanzia Afrika, Austalia, Amerika, Asia Ulaya na visiwa vya Karebiki. 
Wakali hawa wa mdundo inayokubalika kimataifa wanatisha na kuzoa washabiki kwa dhoruba kali la mtindo wao wa muziki. 
Inafrika band inatuwakilisha na hivi sasa bado wapo katika ziara ndefu ughaibuni kuhakikisha  kuwa muzikiwa wao unasikika kila kona nje ya mipaka ya Tanzania.
Usikose kuwasikiliza Inafrika Band "Wazee wa Indege" kupitia  http://www.inafrikaband.co.tz
Pia unaweza kuwapa  hi kupitia info@inafrikaband.co.tz ii
 INAFRIKA BAND aka "Wazee wa Indege" kutoka jiji Dar es salaam wakifanya onesho kubwa katika jiji la Bremen, nchini Ujerumani, usiku wa 13 Februari 2015 katika ukumbi mkubwa wa Musik-Theater jijini humo. 
Ngoma ya "Indege" ikivurumishwa
Kazi mbele kwa mbele
Nyomi ya mashabiki wa jiji la Bremen

BALOZI WA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM'JAY'AWALIPIA ABIRIA WOTE NAULI WA KITUO CHA MAWASILIANO JIJINI

$
0
0
Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(kushoto)akimkabidhi fedha mmoja wa abiria wa basi linalofanya safari zake kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano cha ubungo kwenda Mwananyamala jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwalipia abiria wenzake nauli ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda.
Mkazi wa jijini Dar es Salaam Mudy Seleman(kushoto)akikabidhiwa fedha kwa ajili ya nauli na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela” wakati wa kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda iliyofanyika katika kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakisubiria usafiri katika kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(kushoto)baada ya kuwalipia nauli wakati wa kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda iliyofanyika katika kituo hicho.

NHIF shikamaneni kwenye kazi - Humba

$
0
0
WATUMISHI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF) wametakiwa kushikamana kwa pamoja na kufanya kazi bila kujali muda wa kazi ili kuhakikisha shirika hilo linabaki na heshima yake huku wanachama wakihudumiwa kwa heshima.

Rai hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bw. Emanuel Humba katika hafla ya kuaagwa wastaafu wa Mfuko huo.

Bw. Humba ambaye naye alikuwa ni miongoni mwa waagwa, alisema kuwa mbinu kubwa ya kushinda katika utenda kazi kushikamana na kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali hali ya aina yoyote.

“Nawaombeni wafanyeni kazi kwa ushirikiano, Menejimenti wajalini watumishi na ninyi kwa ninyi kuweni kitu kimoja, sisi tumeacha heshima kwa shirika kwa kuwa tulifanya kazi bila ubaguzi na tulishirikiana sana,”

 “Nitahudhunika sana nikiona au kusikia shirika hili likifa au kudorola, sisi wenzenu nikiwemo mimi ambaye ni mwanzilishi sitakubali kuona hali hii kwa kuwa nimewekeza nguvu kubwa sana ndani ya Mfuko huu, watumikieni Watanzania kwa heshima ili lengo la kuanzishwa kwa Mfuko huu lisipungue,” alisema Bw. Humba.

WAPENDA SOKA ZAIDI YA ELFU MOJA WASHINDWA KUANGALIA MECHI YA AZAM NA EL MELEKH YA SUDAN KWENYE UWANJA WA CHAMAZI LEO

$
0
0
Hali ya kustaajabisha imejitokeza jioni ya leo katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi,kwa washabiki na wadau wa soka zaidi ya elfu moja (1000) kushindwa kuingia uwanjani wakati wa mtanange uliozikutanisha timu za Azam Fc ya Tanzania na El Merreikh ya Sudan ikiwa ni mchezo wa awali wa michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Hali hiyo imekuja baada ya watu hao waliokuwa na tiketi zao mkononi kuambiwa uwanja umejaa,hivyo hakuna sehemu ya kuwaweka.

Taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa,uwingi huo wa watu wenye tiketi zao mikononi,umetokana na ujanja ujanja uliofanywa na baadhi ya wakaguzi wa tiketi waliokuwepo milangoni kwa kucheza michezo michafu ya kutozichana tiketi wakati wa ukaguni na kuja kuziuza tena kwa bei ya juu kwa wale waliokuwa wamekosa tiketi,hali iliyopelekea kutokea hamaki kubwa baada ya kushindwa kuingia uwanjani kutokana na uwanja huo wenye uwezo wa kubeba watazamaji 7,000, kuonekana kujaa kupita uwezo wake.

Katika mazingira hayo, baadhi ya mashabiki walianza kufoka kwa hasira wakihoji mantiki ya wao kuuziwa tiketi wakati uwanja huo ukiwa hauna uwezo wa kubeba mashabiki wengi, jambo ambalo kwa kiasi fulani liliondoa hali ya utulivu katika milango yote ya kuingilia uwanjani hapo.

Miongoni mwa walioonja joto ya jiwe kwa kushindwa kuingia katika mechi hiyo, ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni na Kocha wa timu ya soka ya Wanawake, Twiga Stars, Rogasian Kaijage.

Wengine ni Mwakilishi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Henry Tandau maofisa wengine wa Programu ya kuvumbua vipaji ya NSSF-Real Madrid Sports Academy, walioambatana na Kayuni,pamoja na baadhi ya waandishi wa habari.

Wakati wanafika tayari mageti yote ya uwanja huo yalikuwa yamefungwa kwani isingewezekana tena watu kuendelea kuingia kutokana na watu waliokuwa wameingia kutosha idadi inayotakiwa kwa mujibu wa uwezo wa uwanja huo,na wakati huo mchezo ulikuwa bado haujaanza.

Kwa mujibu wa waliokuwepo ndani ya uwanja,wametudokeza kuwa Timu ya Azam FC imeibuka kidedea kwa kuwachapa El Merreikh ya Sudani kwa mabao 2-0, yaliyowekwa kimiani na washambuliaji Didier Kavumbagu dakika ya 8 na John Bocco 'Adebayor' dakika ya 77.

Baadhi ya viongozi mbali mbali wa soka nchini akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni (wa pili kushoto) wakiwa nje ya Uwanja wa Azam Complex,Chamanzi baada ya kushindwa kuingia uwanjani hapo kutokana na kufungwa kwa mageti baada ya kuonekana kujaa kwa uwanja huo.

JUST IN: BABA WA MSANII DULLY SYKES AFARIKI DUNI

$
0
0
BABA mzazi wa msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Dully Sykes, mzee Ebby Sykes amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Presha.

Ebby Sykes alikuwa muimbaji na mpiga gitaa mashuhuri na ndiye anayedaiwa kumfundisha mambo mengi ya muziki mwanae Dully Sykes.

Sykes alizaliwa February 24, 1952 ambapo tarehe hiyo mwaka huu alikuwa anatimiza miaka 63.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

-Amen

BENKI YA NBC NA ENVIROCARE KUWAKOMBOA VIJANA KUPITIA MRADI WA MAZINGIRA

$
0
0
Naibu Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Envirocare, Catherine Jerome na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kulia) wakionyesha kipande cha mkaa uliotengenezwa na taka za karatasi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati wakizungumzia kampeni ya kuhamasisha utunzaji mazingira katika mtaa wa ubungo kibangu na jinsi takataka zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi. Kampeni hiyo imefadhiliwa na benki ya NBC.
Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kulia), akizungumza kuhusu ufadhili wao kwa asasi isiyo ya kiserikali ya Envirocare jijini Dar es Salaam mwishoni jana, kwa kampeni yao ya kuhamasisha utunzaji mazingira katika mtaa wa ubungo kibangu na jinsi takataka hizo zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi na kusaidia vijana kujiajiri.
Ofisa Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la Envirocare, Israel Richard (kushoto), akimwonyesha Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (wa tatu kulia) jijini Dar es Salaam jana, mashimo ya kutengenezea mbolea kutokana na takataka ikiwa ni sehemu ya kampeni yao ya kuhamasisha utunzaji mazingira na jinsi takataka hizo zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi na kusaidia vijana kujiajiri kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali. Wa pili kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter, Naibu Mkurugenzi wa Envirocare, Catherine Jerome na Meneja Rasilimali Watu wa asasi hiyo, Carolyn Mwanry (kulia)
Meneja Rasilimali Watu wa Shirika lisilo la kiserikali la Envirocare, Carolyn Mwanry (wa pili kulia) akishiriki kufanya usafi na baadhi ya wakazi wa mtaa wa ubungo kibangu, Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha utunzaji mazingira na jinsi takataka hizo pia zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi na kusaidia vijana kujiajiri. Kampeni hiyo imefanyika chini ya ufadhili wa benki ya NBC.
Meneja Rasilimali Watu wa Shirika lisilo la kiserikali la Envirocare, Carolyn Mwanry (kulia), Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kibangu, Desdery Ishengoma (kushoto) na Diwani wa kata ya makuburi, William Mwangwa wakishiriki kufanya usafi na baadhi ya wakazi wa mtaa wa ubungo kibangu, Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha utunzaji mazingira na jinsi takataka hizo pia zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi na kusaidia vijana kujiajiri. Kampeni hiyo inafanyika chini ya ufadhili wa benki ya NBC.

Wafanye watabasamu

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKABIDHI TUNZO YA RAIS YA MZALISHAJI BORA MWAKA 2014

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia maonesho mbalimbali kwenye Ghafla ya utoajio Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wadau mbalimbali kwenye Ghafla ya utoajio Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Ubalozi wa Tanzania nchini Oman unastahili pongezi

$
0
0
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othaman (mwenye Kaunda suti) akipokea Tunzo ya ushiriki iliyotolewa na Mwakilishi kutoka Manispaa ya Mji wa Muscat ambao ni Waandaaji wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni. Tanzania imepeleka zaidi ya Watu 40 kuonesha kazi wanazoifanya za sanaa ikiwemo,Uchongaji,uchoraji na ufumaji wa nguo. Kulia ni Kiongozi wa Msafara huo Khadija Battashy na kushoto ni Msaidizi kiongozi Masha Hussein. Picha na Faki Mjaka, Muscat Oman
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othman (katikati) akiwa kashika Tunzo ya ushiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni nchini Oman waliyopewa kutoka Manispaa ya Mji wa Muscat ambao ndio waandaaji wa Maonesho hayo. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Washiriki kutoka Tanzania Khadija Battashy na kushoto ni Msaidizi kiongozi Masha Hussein na Mkuu wa mambo ya kiufundi wa Msafara Moza Habib.

Na Faki Mjaka, Muscat Oman

Msemo wa Kiswahili usemao ‘aisifiaye Mvua huwa imemnyeshea’ unafanana kwa mbali na ule usemao ‘adhabu ya Kaburi aijuaye Maiti’. Misemo hii huonesha jinsi ambavyo muhusika kwenye tukio husika ndiye mwenye uelewa mpana zaidi wa kufahamu umuhimu au madhara ya jambo fulani.

Hata kunapotokea tatizo la kihalifu na kutakiwa ushahidi mara nyingi Polisi huanzia kuwakamata wale waliokuwa katika tukio hilo ili kusaidia kutoa ushahidi wa awali.

Mantiki ya utangulizo huo ni kusifia namna gani Ofisi ya Balozi wa Tanzania nchini Oman ilivyofanikisha Maonesho ya kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika nchini Omani na namna Maonesho hayo yanavyoweza kuisaidia Tanzania kupiga hatua mbele katika Sekta ya Kiutalii.

COUNTDOWN KUELEKEA SHEREHE ZA MIAKA 10 YA MICHUZI BLOG: ANKAL AKIHOJIWA NA SPORAH JIJINI LONDON, UINGEREZA, MWAKA 2010

$
0
0
MAKALA AINA HII ITAKUJIA KILA JUMAPILI
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images