Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 738 | 739 | (Page 740) | 741 | 742 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza kikao cha Wizara ya Mifigo na Uvuvi kilichozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi


  0 0
 • 02/12/15--12:30: 5 YEARS ANNIVERSARY
 •  


  0 0

  Naibu Waziri wa Maji,Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi wilaya ya Longido mkoani Arusha ikiwa ni muendelezo wa ziara za kukagua miradi mbali mbali ya maji hapa nchini. 

  Katika ziara yake hiyo,alikutana na viongozi wa wilaya hiyo ya Longido na kuiagiza kampuni ya Haward Humfrey iliyofanya usanifu mradi wa maji wa Kisima cha Tembo ichukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kutopewa kazi zozote za miradi ya maji nchini kwa kusanifu mradi wa maji wa thamani ya shilingi milioni 253, mradi ambao baada ya kujengwa hautoi maji.

  Pia ameagiza taarifa ya tume iliyoundwa iwekwe wazi na watumishi wa halamashauri ya Longido waliohusika kusimamia mradi huu wachukuliwe hatua kali za kinidhamu na kusheria.

  Naibu Waziri  Makalla ameweka jiwe la msingi la mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya bilioni 1.8 katika kijiji cha Meirugoi.
  Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akizindua mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya bilioni 1.8 katika kijiji cha Meirugoi.
  Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akifurahia vazi la kimasai alilovalishwa na wenyeji wa kijiji cha Meirugoi,wilaya ya Longido.
  Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa katika picha ya pamojna na wananchi wa wenyeji wa kijiji cha Meirugoi,wilaya ya Longido.

  0 0

  Sikiliza kwa makini Mahojiano na Omar Ally, Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Association, akiongelea njia nzuri kuhusu  maendeleo ya kuinua wana ZADIA pamoja na Zanzibar kwa ujumla.

  0 0  0 0
 • 02/13/15--05:13: TAARIFA YA MSIBA
 • Marehemu Andrew Michael Kumalilwa enzi za uhai wake

  Familia ya Bwana Andrew Michael Kumalilwa inasikitika kutangaza kifo cha wa baba yao mpendwa Bwana Andrew Michael Kumalilwa  kilichotokea tarehe 09 Februari 2015 Jijini Dar Es Salaam.

  Marehemu Andrew Michael Kumalilwa alizaliwa mnamo tarehe 10 Machi 1938 na aliwahi kushika nyazifa mbalimbali ikiwepo ya Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania (DCP) na msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea na Mazishi yatafanyika Kesho Nyumbani Kwake Segerea.

  Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi - Amina
  Timu nzima ya Lukaza Blog inapenda kutoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa kuondokewa na Mpendwa wao. Mungu awatie nguvu katika Kipindi hiki Kigumu

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa Dodoma na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa hotuba ya kufungua mkutano wa baraza hilo Mjini Dodoma Feb. 13,2015.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) Ndg. Raymond Mbilinyi akiwasilisha majukumu ya Baraza hilo katika kusaidia mabaraza ya biasara ya Mkoa na jinsi ya kukuza ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi wakati wa mkutao wa baraza la biashara la Dodoma Feb. 13, 2015.
  Wajumbe wa baraza la biashara Mkoa wa Dodoma wakifuailia mada juu ya ushirikiano wa serikali na sekta binafsi na kuzalisha fursa za uwekezaji Mkoani Dodoma wakati wa Mkutano wa Baraza hilo Feb. 13, 2015.
  Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) Manispaa ya Dodoma Ndg. Nobert Donald akiwasilisha changamoto zinazowakabili wamachinga wakati wa mkutano wa baraza la biashara Mkoa wa Dodoma Feb. 13, 2015.
  Mwenyekiti wa wafanyabiashara, wakulima na wenyeviwanda Mkoa wa Dodoma (TCCIA) Ndg. Faustine Mwakalinga akiwasilisha mada juu ya fursa za kipekee za uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma na Changamoto zilizopo wakati wa Mkutano wa Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma Feb. 13, 2015

  0 0

  Meneja Masoko na Bidhaa wa Benki ya Biashara ya Dar es Salaam (DCB), Boyd Mwaisame, akitoa maelezo kwa wateja waliohudhuria Kongamano la Wajasiriamali Wanawake, kwenye viwanja vya Makumbusho Dar es Salaam, namna benki hiyo inavyoendesha huduma zake kadhaa, ikiwemo huduma za akiba, DCB Mobile, DCB jirani na utaratibu wa jinsi ya kukopa na masharti ya huduma za mikopo hasa SGL na Super SGL.


  0 0

  Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nasary akitoa salamu za Pole kwa wafiwa wote wakati wa mazishi ya Marehemu Emmanuel Pendael Pallangyo aliyefariki Tarehe 7.02.2015 na kuzikwa kijijini kwao Sing'isi Meru tarehe 12.02.2015 .
  Baba wa Marehemu Mzee Pendael T.  Pallangyo akitoa Salam zake za Mwisho kwa Mwanae Mpendwa Emmanuel Pallangyo.


  0 0

  Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imezindua mnara wa mawasiliano katika kata ya Kiegei, wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi hivi karibuni.

  Akiongea na wananchi Kiegei, Mkuu wa Biashara  (TTCL) kanda ya Zanzibar Bw. Hussein Nguvu amesema; kwa kutambua umuhimu wa mawasiliano, TTCL pekee ndiyo ipo katika kijiji cha KIEGEI na ipo mstari wa mbele katika kuchangia kufanikisha malengo ya Serikali katika Sekta hii mtambuka kwa maendeleo ya haraka kwa Taifa letu.

  Amesema Serikali ina imani kubwa na imeridhishwa na utendaji na ufanisi wa TTCL katika kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi hapa nchini na nje ya mipaka kwenda nchi jirani ndio maana imepewa dhamana ya kuendesha na kusimamia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuinua uchumi wa nchi kupita Sekta hii muhimu ya TEHAMA chini ya usimamizi wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  Ameongeza kwa kumshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Bw. Peter Ulanga kwa  juhudi zake katika kusimamia mfuko huu ambo umekuwa ni msaada mkubwa katika kuleta maendeleo kupitia Sekta ya Mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini ambayo bado yapo chini Kiuchumi, Kimaendeleo na Kibiashara.

  Naye mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa mnara huo ambaye ni Mbunge wa Nachingwea na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Mathias amesema kupatikana kwa mawasiliano hayo ya simu katika kata ya  Kiegei, Wananchi wa eneo hilo wataweza kuwasiliana na pande zote za dunia, fursa ambayo wamekuwa wakiikosa kwa muda mrefu.

  Pamoja na hilo vile vile kwa kutumia mawasiliano wataweza  kupata na kutumia taarifa za kibiashara na kiuchumi - katika  masoko  mbalimbali  nchini na duniani, hususani bei za mazao yao na kupata habari za masoko mapya. Hii itawawezesha kupata fursa sawa na watu wa maeneo ya mijini na nchi zingine zinazoendelea ili kuendelea kujenga uwiano sawa wa kupata na kutoa taarifa kwa maendeleo ya nchi na watanzania kwa ujumla.

  Katika hafla hiyo mkuu wa wilaya ya Nachingwea Bi. Regina Chonjo aliwasisitiza wananchi wa Kiegei kulinga miundombinu ya mawasiliano ili iweze kudumu kwa muda mrefu kwa manufaa ya sasa na yajayo.

  Kupitia mfuko wa kusimamia utoaji wa huduma ya Mawasiliano kwa wote nchini (UCSAF), TTCL ilipewa jukumu la kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 20 kwa thamani ya  Tshs 3.4 bilioni.  Lengo likiwa ni kupeleka huduma za mawasiliano  katika maeneo ambayo hayana mawasiliano, ni pamoja na kuhakikisha  wananchi waliopo vijijini wanapata fursa ya kuwasialiana na ndugu, kukuza biashara zao na kujenga uwiano sawa kwa wananchi wote nchini.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Mathias Chikawe (mwenye miwani) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya TTCL katika Kata ya Kiegei, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akipiga simu ya Kampuni ya TTCL baada ya kuzindua rasmi mnara mkubwa wa mawasiliano wa Kampuni hiyo katika Kata ya Kiegei, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.Aliyevaa kofia (kulia) ni Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya TTCL, Kanda ya Zanzibar, Hussein Nguvu.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Kuwait hapa nchini, Mhe.Jasem Ibrahim Al-Najem leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Malawi hapa nchini Mhe.Hawa Ndilowe leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
   Balozi mpya wa Afrika Kusini hapa nchini Mhe.Thamsanqa Dennis Msekelu akiwasilisha Nalaka za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Kenya hapa nchini Mhe. Chirau Ali Mwakwere leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARI ya China, Bw. Bao Tianhua, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya NARI ya China mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARI ya China, Bw. Bao Tianhua, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2014. Picha na OMR

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mweenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodriguez akiongoza ujumbe wa Wakuu wa Taasisi za Umoja wa Mataifa wenye Ofisi zao Nchini Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kuonana na Rais.
  Rais wa Zanzibar na Mweenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Ujumbe wa Wakuu wa Taasisi za Umoja wa Mataifa wenye Ofisi zao Nchini Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo mchana ukiongozwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodriguez.
  Rais wa Zanzibar na Mweenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodriguez akiongoza Ujumbe wa Wakuu wa Taasisi za Umoja wa Mataifa wenye Ofisi zao Nchini Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo mchana.Picha na Ikulu.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 katika hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadik.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa elimu na ufundi Kassim Majaliwa wakiangalia jaribio la Sayansi lililokuwa likifanywa na mwanafunzi katika shule ya sekondari ya kata ya Majani ya Chai huko Kipawa jijini Dar es Salaam.Awali Rais Kikwete alizindua maabara za sayansi katika shule hiyo na baadaye alizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.picha na Freddy Maro

  0 0

  TIMU ya Coastal Union ya Tanga imesema kuwa itapambana vilivyo ili kuweza kuhakikisha inachukua pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayochezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani,jijini Tanga.

  Coastal Union itangia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi yao ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa sokoine jijini Mbeya ambapo Mbeya City iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilipatikana kwa njia ya penati.

  Akizungumza maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga alisema kuwa maandalizi ya kuelekea mechi hiyo imekamilika kwa asilimia kubwa kwa kufanya mazoezi asubuhi na jioni.

  Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha wanafuta machungu ya kufungwa na Yanga bao 1-0, kwenye mechi yao ya Ligi kuu iliyochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani jambo ambalo halikuwafurahisha mashabiki na wapenzi wa soka.

  Aidha amesema kutokana na kikosi chake kuendelea kuimarika kila mchezo wanaokuwa wakicheza wana matumaini makubwa ya kupata ushindi ambao utawawezesha kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo.

  Alisema kuwa ligi kuu msimu huu imekuwa ni ngumu sana lakini kubwa ni kujipanga hivyo wamejipanga vizuri kwa umakini mkubwa lengo likiwa kukiwezesha kikosi hicho kinapata matokeo mazuri

  0 0


  Mmoja wa waasisi na viongozi wakongwe wa CCM Hajat Kijakazi Salum Kyerula amefairiki dunia  jijini Dar es salaam jana. Taratibu za mazishi  zinafanyika mikocheni eneo la Victoria karibu na Oil com pamoja na hospitali ya Kairuki,  jijini Dar es salaam. Swala ya maiti itafanyika hapo hapo Mikocheni sambamba na swala ya Ijumaa na baadaye  maziko yatafanyika Mtoni Kijichi, kwenye makaburi ya  njia panda ya Neruka.

  WASIFU WA MAREHEMU

  HAJAT KIJAKAZI SALUM KYELULA NA RATIBA YA MAZISHI


  Hajat  KIJAKAZI SALUM KYELULA alizaliwa tarehe 1/1/1941, katika uhai wake amefanya kazi Radio Tanzania(TBC),  Shirika la Habari la Tanzania (SHIHATA).  PIA  Marehemu kijakazi amewahi kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)  Wilaya ya Ilala. katibu mkuu wa CCM mkoa wa Morogoro na Kilimanjaro kwa vipindi tofauti.

   Marehemu amekuwa Mbunge wa Taifa kwa takribani miaka 15,  Naibu Waziri  Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Pamoja na nafasi hizo Bi. Kijakazi ni mwanzilishi wa umoja wa  kina mama wa Regent (Regent Women Neighbourhood -  REWONE),  umoja wa kina mama wa kiislamu MIKOCHENI(SAFINA), na pia alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa msikiti wa Regent Estate.

  Marehemu ameacha watoto 7 ,wajukuu 14 na vitukuu viwili.

  Innalilah wainailalai Rajiun


                                    RATIBA YA MAZISHI  LEO MTONI KIJICHI, DAR ES SALAAM                                                           
                   TUKIO

                   MUDA   

               MUHUSIKA

  KISOMO(SURAT RAHMAN & SURAT YASSIN)

  SAA 5:00 ASUBUHI

  ABDALLAH KIONGA

  WASIFU WA MAREHEMU

  SAA 5:50 ASUBUHI

  RAMADHANI KITWANA

  SADAKA

  SAA 6:OO MCHANA


  KUELEKEA MSIKITINI KWA SALAT JUMAA NA SALAT JANAIZA

  SAA 6:45 MCHANA

  ABDALLAH KIONGA

  MSAFARA KUELEKEA MTONI KIJICHI

  SAA 7:15 MCHANA

  MJOMBA MSAKUZI

  MSAFARA KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU KIJICHI KWA SALAT JANAIZA NA KISHA KUELEKEA MALALONI

  SAA 8:15 MCHANA

  MJOMBA HAJJI
  0 0

  Mkurugezi wa Kundi hilo Mkubwa Fella kwanza alianza kwa kutoa shukran zake kwa Mwenyezi Mungu, Mashabiki, Wadu na vyombo vyote vya habari kwa kuweza kutoa sapoti kwa vijana hao tangu walipo toa Kazi yao ya kwanza kabisa mpaka kufikia Leo wamepata mualiko mkubwa kabisa wa kwenda kufanya show UK.
  Kwa upande wa Msemaji mkuu na Kiongozi wa Band Aslay Isihaka amesema kuwa wanafuraha sana kwa kupata mualiko huo lakini pia wanashukuru kwa mungu, mashabiki na wale wote wanaonyesha sapoti katika muziki wao. Aslay amesema   kuwa watakwenda kufanya Kazi nzuri huko ili kuleta sifa ya muziki wa hapa nyumbani na hata heshima ya Taifa kwa ujumla.Kwa upande mwingine Vijana hao Wametoa shukrani zao kwa Viongozi wao Mkubwa Fella, Bab Tale, Chambuso, Mh Temba na Shirko kwa usimamizi Mzuri wa Kazi hizo.

  0 0

  Baadhi ya bidhaa zilizoandaliwa kwa ajili ya wapendanao.

  MABINGWA wa kuuza vipodozi vya ukweli, AK Classic Cosmetics wamewaandalia Valentine's Special wale wote wanaowajali na kuwaenzi wapenzi wao.
  OFA: Ukinunua bidhaa zozote zitakazofikia kiasi cha shilingi laki moja, utapata kifurushi cha bure cha zawadi za Valentine's na ofa hii itaendelea mpaka mwishoni mwa mwezi huu.
  Pata package maalum kwa ajili ya mpenzi wako kwa bei ya punguzo kabisa.
  Bidhaa pendwa za Victorias Secrets, Lotion, Showergel, Lipstick, Lipgloss, Deodrant, Perfumes, Body Shaper, tiba za chunusi, bidhaa za kupunguza unene na uzito, bidhaa za kung'arisha ngozi n.k.
  Karibuni dukani mjionee mambo kadha wa kadha. Bidhaa zinaweza kukufikia mpaka ulipo.
  Tupo Mlimani City karibu kabisa na kituo cha mafuta cha Total na Kinondoni Manyanya jijini Dar.
  Tupigie 0753482909 au kupitia WhatsApp +255 753482909

older | 1 | .... | 738 | 739 | (Page 740) | 741 | 742 | .... | 3285 | newer