Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 737 | 738 | (Page 739) | 740 | 741 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju akisisitiza jambo mbele ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. Mkutano wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wahariri wa vyombo vya habari ulikuwa na lengo la kuwapa fursa pana wahariri kuuliza maswali mbalimbali kuhusu ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda(katikati) na Mhariri wa gazeti la Jamhuri Manyerere Jackton.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju akifurahia jambo na viongozi wa Jukwaa la Wahariri. Neville Meena(katikati) ni Katibu na Absalom Kibanda ni Mwenyekiti. (Picha na Abuu M. Kimario)
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju(tai nyekundu) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu n Utawala Bora Bw. Bahame Tom Mukiria Nyanduga wakati alipofanya ziara fupi kwenye ofisi hiyo leo jijini Dar-es- salaam. Wengine kwenye picha ni Makamishna wa tume hiyo na Katibu Mtendaji Bi. Mary Massay(kwanza kulia)

  0 0  0 0


  0 0

  Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez alisema kwamga upo umuhimu mkubwa wa kuwa na mabadiliko ya mafungamano ya uhusiano wa Kiuchumi na kisiasa kati ya Taifa lake na Marekani. Alisema mafungamano hayo ambayo hayakuwepo kati ya Mataifa hayo ya Bara la America ya Kusini kwa takriban miaka 50 iliyopita endapo yataimarishwa vyema yanaweza kusaidia ustawisha kizazi cha sasa na hatma ya kizazi kijacho.

  Balozi huyo wa Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

  Akitoa ufafanuzi kufuatia Kikao cha hivi karibuni cha mafungamano kati ya Rais Raul Castro wa Jamuhuri ya Cuba na Rais Barak Obama wa Marekani Balozi Lopez alisema yapo mambo mengi ya msingi ambayo pande hizo mbili zitalazimika kuyakalia pamoja kwa lengo la kuyashughulikia kwa kina.

  Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema kwamba mafungamano hayo ya Marekani na Cuba ni Habari njema inayotoa matumaini mapya ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili ambayo haukuwepo kwa nusu Karne iliyopita.

  Balozi Seif alisema iwapo nia ya Rais Raul Castro wa Jamuhuri ya Cuba na Rais Barak Obama wa Marekani itakuwa sahihi kuna fursa pana ya kujenga na kuimarisha uchumi baina ya Mataifa hayo Mawili ambapo pia Cuba inaweza kuitumia nafasi hiyo kwa kujitangaza na hatimaye kujitanua kiuchumi katika pembe zote za Dunia.
  Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwa Mhe. Makamu Vuga Mjini Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa pili kutoka kulia akizaungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez aliyepo kulia yake hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Wake Bwana Abdulla Ali Abdulla { Kitole } na kulia ya Balozi Lopezi ni Ofisa wa Idara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Zanzibar Bwana Iddi Seif Bakari.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo wa Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez aliyefika Ofisini kwake Vuga kusalimiana naye. Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0

  NA  BASHIR  YAKUB-

  Upo wakati kwenye  ndoa ambapo mmoja  wanandoa  anaweza akawa anataka  kuuza au kubadili jina la nyumba/kiwanja  bila ridhaa ya mwenzake ilihali  nyumba  hiyo  ni ya  familia. Lakini  pia  nje ya  hilo kuna  mazingira  ambayo  mtu anaweza  kuwa  si  mwanandoa lakini ana maslahi  katika  nyumba au  kiwanja cha mtu fulani  na anataka  kuzuia  nyumba/ kiwanja  hicho  kisibadilishwe  jina au kisiuzwe.  Kisheria jambo hilo linaruhusiwa  na huitwa zuio( Caveat).

  Hili sio zuio la kwenda mahakamani  kama  mazuio tuliyoyazoea.Hili  ni zuio jingine  kama  nitakavyolieleza. Aidha  kuzuia hati  isibadilishwe  kimsingi ni sawa na  kuzuia nyumba isiuzwe.  Hii ni kwakuwa  hakuna namna ambavyo  mnunuzi anaweza kununua  kitu ambacho  hakiwezi  kubadilika  na kuingia  katika  jina  lake. Ikiwa  mke ana wasiwasi kuwa mume  anaweza kumzunguka  na kuuza mali ya familia  au mume ana wasi wasi juu ya uwezekano  wa mke kuuza basi wanayo  ruhusa  ya kuweka zuio ili hati  ya  nyumba  isibadilishwe.  Yapo mambo mengi kuhusu hili nitaeleza baadhi.
        
    1.         NINI  MAANA  YA  ZUIO.

  Zuio ni usitishwaji wa muda ambao huwekwa ili kuzuia mabadiliko yoyote katika hati. Kama maana  yenyewe inavyojieleza  huu unakuwa ni usitishwaji wa muda  ambao unalenga  kulinda  maslahi ya  mtu aliyeomba  zuio.Kuitwa  zuio  la  muda haimaanishi  kuwa  mtu akizuia   itakuwa  ni mwezi mmoja  au  miwili basi, hapana. Ni  zuio  la  muda  kwakuwa  haliwezi kukaa milele  lakini  mtu akishaliweka  linaweza  kukaa  hata  miaka  mingi  kutegemea  na  sababu  za  zuio  hilo.


  0 0
 • 02/12/15--02:07: EAC-EU POLITICAL DIALOGUE
 • The Secretary-General of the East African Community (EAC) and European Union Ambassadors accredited to the United Republic of Tanzania held a Political Dialogue meeting on 11 February 2015 in Arusha, the United Republic of Tanzania.

  The political dialogue takes place within the framework of the Cotonou Partnership Agreement between the EU and the African, Caribbean and Pacific states, to which the Regional Organisations are associated. The meeting was co-chaired by Ambassador Dr. Richard Sezibera, Secretary General of the East African Community and Ambassador Filiberto Ceriani Sebregondi, Head of the EU Delegation to Tanzania and the EAC.

  The Ambassadors and representatives from the Embassies of Belgium, Denmark, Germany, Finland, France, Ireland, Italy, Spain, Sweden, and the United Kingdom and senior officials from the EAC Secretariat participated in the dialogue.

  The parties reviewed the political situation in the countries of the sub-region, discussed EAC interventions towards the promotion of good governance, and deliberated on the preparations for observation of forthcoming elections in the Partner States.

  The parties exchanged views on ways to promote peace and security in the region, including the programs for countering terrorism, armed groups, piracy and drugs and human trafficking; the implementation of programs under the African Peace and Security Architecture (APSA) and the way forward for the period ahead.

  They also discussed the challenges facing the eastern Africa region, including sub-regional conflicts with a focus on the Great Lakes. The EAC and EU also exchanged views on global issues, including the EU economic/financial situation, the fight against extremism as well as instability in Ukraine and Syria.

  The EAC and EU reaffirmed their resolve to work together to advance peace and stability and to promote equitable growth and development in the region. They reiterated their commitment to cooperation and dialogue to further strengthen and deepen the regional integration agenda of the EAC.   

  In concluding the dialogue, Ambassador Sebregondi expressed his satisfaction for the level of cooperation between the EU and the EAC. He said: "I am pleased by the increasing cooperation between the EU and the EAC and we are keen to support democratic processes in the EAC Partners States through EAC Electoral Observation Missions.

  The European Union will continue to support the East African Community, building on the achievements of a long-lasting engagement to foster the EAC Custom Union and Common Market, as well as to promote democratic governance and peace”

  On his part the EAC Secretary General, Amb. Dr Richard Sezibera expressed the Community’s appreciation for the continued support from the European Union. He reiterated that the support is integral to EAC’s efforts towards attaining its objective of an economically, socially and politically integrated East Africa

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mominah, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika wakati Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2015 wakati Balozi huyo alipofika kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya na Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha. Katika hafla hiyo iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwapisha Bwana John Haule kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya na Dkt.Hamisi Mwinyimvua ameapishwa kuwa naibu katibu mkuu wa Wizara ya Fedha.
  Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Bwana John Haule akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Bwana John Haule akipeana mkono na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mara baara ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Naibu Katibu mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiirekebisha tai ya mtoto Amani Mwinyimvua(11) muda mfupi baada ya kumwapisha Baba yake Hamis Mwinyimvua kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

  0 0

   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi,Prof. Amon Challigha
  Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akichangia mada katika mkutano huo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.

  TUTAENDELEA KUPATA MAONI KATIKA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA-JAJI LUBUVA


  Na Chalila Kibuda.


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema itaendelea kupata maoni kwa wadau juu ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya  wa uchukuaji wa alama za vidole kwa kutumia BVR ili kurahisisha wapiga kura.


  Hayo ameyasema leo  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine jijini Dar es Salaam ,Lubuva amesema mfumo wa uandikishaji wa daftari la wapiga kura ni mpya hivyo ni lazima Tume itoe  taarifa mara kwa mara na kupata mawazo mengine katika uboreshaji wa daftari hilo.


  Lubuva amesema daftari la wapiga kura limekuwa na malalamiko mengi kwa vyama vya siasa na kuona haja ya kubadili mfumo wa uandikishaji kwa kuchukua alama za vidole kwa kutumia kifaa cha BVR ili kuondokana na malalamiko hayo.


  “Tume inafanya kazi kwa kujitegemea hakuna mtu yeyote anaweza kuipangia majukumu na hata mkutano wetu wa leo sio shinikizo la Mbunge wa chama chochote kwani hii ni tume huru”amesma Jaji Lubuva.


  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi -CCM (Taifa) ,Nape Nnauye amesema Tume imekuwa ikikaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa taarifa na kuwa na shaka kutokana na masuala yaliyopo katika tume ni mazito ikiwemo uboreshaji wa daftari la wapiga kura ambalo linatakiwa litumike katika kura ya maoni pamoja na uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.  Amesema kama chama tawala wanataka kuona masuala haya yanawekwa wazi na tume mara kwa mara ili wananchi wawe tayari katika kuandikishwa katika daftari hilo.  0 0

   Balozi wa Iran nchini Tanzania,Mh.Mehdi Aghajafari akimpokea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) alipowasili katika hafla ya kusherehekea siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi huyo Jijini Dar es Salaam jana usiku.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) akizungumza mbele ya wageni mbalimbali walioalikwa katika hafla ya siku ya Taifa la Iran iliyofanyika kwenye makazi ya balozi wa Iran Jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Syria nchini, Mhe.Abdulmonem Annan (kushoto) Jaji mkuu wa Tanzania,  Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) na Balozi wa Yemen nchini, Mhe.Abdulla Hassan Alamri wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Siku ya Iran, Naibu waziri Dkt. Mahadhi.
   Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahaya (kulia) akiwa na Maafisa kutoka Wizara hiyo Bw. Mkumbwa Ally (kushoto) na Bw. Leonce Bilauri (katikati) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri (hayupo pichani) katika hafla hiyo.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Syria nchini Mhe. Abdulmonem Annan kwenye sherehe hizo.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  DSC_0333
   
  “NILIAMUA kuanzisha Msama Promotions baada ya kuona muziki wa Injili umesahaulika na unashuka thamani yake.“Hivyo kwa kushirikiana na wenzangu nikaona ni busara kuuinua ili tuwe kama wenzetu Afrika Kusini ambao wana waimbaji wa nyimbo za Injili wanaotamba kama Rebecca Malope, Itani Madima, Steve Kekane, Vuyo Mokoena na wengine wengi,” hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama.
   
  Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, anasema alitaka watu wajue na kutambua kuwa muziki wa Injili unaweza kupigwa kama burudani katika kumbi mbalimbali za starehe na kuondoa dhana potofu kwamba muziki huo wa Injili haufai kupigwa katika kumbi hizo.
   
  “Kupeleka muziki wa Injili kwenye kumbi ambazo hupigwa muziki wa miondoko mingine ya kidunia si dhambi kama baadhi ya watu wanavyofikiri,” anasema.Anasema ni zaidi ya miaka 15 tangu walipoanzisha Tamasha la Pasaka wakati wa sikukuu hiyo kila mwaka na sasa jamii imelikubali na limekuwa gumzo kubwa kwa jamii.
   
  Anasema pia dhamira yao nyingine ya kuanzisha tamasha hilo ilikuwa kusaidia jamii kwa namna mbalimbali kutokana na fedha za viingilio, lakini pia kuwapa ajira vijana kutokana na tamasha hilo.“Ninachoweza kusema ni kwamba mwaka huu tumedhamiria kwa dhati kusaidia jamii kwa namna mbalimbali kutokana na fedha zitakazopatikana kwenye viingilio vya tamasha.
   
  “Haitakuwa mara ya kwanza kwetu kusaidia, tumefanya hivyo miaka ya nyuma na tutaendelea na juhudi hizo kila tutakapopata nafasi ya kufanya hivyo, “ anasema.Anatolea mfano kuwa miaka ya nyuma wamesaidia watu mbalimbali ikiwemo  waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto, Dar es Salaam. Pia anasema wamepata kutoa fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane.
  Msama anabainisha kwamba kutokana na dhamira hiyo, ndiyo maana wamekuwa mstari wa mbele kuandaa matamasha ya muziki wa Injili, lengo likiwa ni kusaidia masuala mbalimbali.Anasema mwanzoni wakati wanaanza tamasha hilo mwaka 2000, wamewahi kuandaa matamasha kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuchangia watoto yatima wa mikoa ya Morogoro na Pwani, ambao wazazi wao walifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi, ambapo yote waliyopanga yalifanikiwa.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) wakiongozwa na mwenyekiti wake ambae pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi  Dr. Servaciaus Likwelile (kulia)  ofisini kwake leo tarehe 12 Februari 2015. Katika salam zake ameishukuru Serikali na mfuko huo kwa kazi nzuri inayofanyika Mkoani Rukwa na taifa kwa ujumla hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami, Pamoja na hayo ameiomba Serikali na wafadhili wa MCC kusaidia pia katika ujenzi wa barabara muhim za Wampembe iliyopo Wilaya ya Nkasi, barabara ya bondeni kwa ajili ya kuunganisha ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa unaoongoza kwa uzalishaji wa mpunga na Mikoa ya Katavi na Mbeya, barabara ya Kasesha kwa ajili ya kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Zambia na barabara ya kuelekea Kalambo Falls yalipo maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akiendesha kikao ofisini kwake mapema leo tarehe 12 Februari 2015 kati yake na viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) .
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa zawadi ya kanga kwa Katibu Mkuu Wizara ya fedha na uchumi Dr. Servaciaus Likwelile pamoja na viongozi wengine na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T), Kanga hiyo ni ishara ya mafanikio ya miaka 40 ya Mkoa wa Rukwa 1974-2014.    
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (kulia) alipata fursa ya kuwaalika viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) kwa ajili ya chakula cha usiku walipowasili Mkoani Rukwa tarehe 11 Februari 2015. Anaechukua chakula ni Mwenyekiti wa mfuko huo ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Uchumi Dr. Servaciaus Likwelile.
  Picha ya pamoja.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Jaji Kakusulo Sambo akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo mapema leo tarehe 12 Februari 2015. Mafunzo hayo ya siku mbili yanayoshirikisha Mikoa ya Rukwa na Katavi yanafanyika Mkoani Rukwa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi. 
  Jaji wa Mhakama Kuu ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto Jaji Ferdinand Wambali akiendesha mafunzo hayo ambayo yameanza leo tarehe 12 Februari na yatamalizika kesho tarehe 13 Februari 2015 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (RDC).
  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi akitoa shukurani za Mikoa ya Rukwa na Katavi kwa kuletewa mafunzo hayo ambayo ni muhimu kwa Kamati za maadili za Mikoa hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake ya siku.

  0 0

  Na Chalila Kibuda.


  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezuia maandamano ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF) na kusema watakaoandamana

  kesho  nguvu ya dola itatumika


  Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema wamewashauri vijana hao na kusema wataandamana hivyo ni lazima nguvu itumike kuzima maandamano hayo kutokana na kuzuia kufanyika kwa shughuli zingine.


  Kova amesema kusudi la maandamano hayo ni ukiukaji wa haki za binadamu kwa jeshi la polisi pamoja na Tume ya Uchaguzi kuongeza siku za kuandikisha kutoka siku  saba hadi 14, ambapo waliwashauri kwenda huko kwa viongozi lakini wameshindwa kufanya hivyo na kuwataka wakate rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ili wafanye maandamano, nalo wamekataa.


  “Mambo haya yote yakutaka kufanya maandamano yanazungumzika lakini wanataka kufanya hivyo ni lazima nguvu itumike kuzima kuacha kila mtu anafanya kitu anachotaka ni kufanya nchi isitawalike na sisi tunafanya nchi itawalike kwa watu kufuata taratibu”amesema Kamishina Kova.


  Amesema kuwa Jeshi la  Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kesho wamejipanga katika kuhakikisha maandamano ya vijana hao hayafanyiki na watakaothubutu nguvu ya polisi itakuwa juu yao.
  0 0

     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimtambulisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Ali Juma Shamuhuna, kwa Waziri Mkuu wa Qatar sheikh Abdallah Bin Nasser Bin Khalifa Al-Thani walipokutana leo mjini Doha, Qatar.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Qatar sheikh Abdallah Bin Nasser Bin Khalifa Al-Thani walipokutana leo mjini Doha, Qatar.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar Dr. Khalid bin Mohammed Al-Attiyah mjini Doha. Kushoto ni Waziri wa Nchi, OMKR Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej na kulia ni msaidizi wa Waziri wa Qatar.
    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na ujumbe wake, wakiongozana na Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar Dr. Khalid bin Mohammed Al-Attiyah mjini Doha.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na  Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar Dr. Khalid bin Mohammed Al-Attiyah mjini Doha. (Picha na Salmin Said, OMKR).

  0 0

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad Bibi Nasra Mohamed Hilal(wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na mlezi wa Taasisi hiyo Rais Mstaafu awamu ya pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi ikului jijini Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Abdulkarim Esmail Hassan Shah (Mafia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki na kuambatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Tumaini Thika wakati walipofika ubalozini hapo. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
  Ujumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira uliofuatana na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukiwa katika picha ya pamoja nje ya Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, jana. Kamati hiyo iko katika ziara ya mafunzo nchini humo.
  Mjumbe wa Kamati ya Maliasili na Mazingira Benedict Ole Nangoro, (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa, Fatuma Chillo.


  0 0

  Klabu ya Red Arrow FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia inatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam-Tanzania jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya kuweka kambi ya mafunzo ya wiki moja kujindaa na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo 2015.

  Uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake Col Nolacso K Chilando ulifika leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF sambamba na Afisa habari wa klabu Lt Col Melody Siisii, Bw Alex Chila ofisa ubalozi wa Zambia nchini Tanzania kujitambulisha uwepo wao nchini.

  Wakiongea na katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF Selestine Mweisgwa, uongozi wa timu hiyo umesema maandalizi ya kambi yameshakamilika na kikubwa walikua wanaliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kutambua uwepo wao na kuwasaidia kupata viwanja vya kufanyia mazoezi.

  Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF Bw.Mwesigwa alisema wameyapokea maombi hayo ya Red Arrow FC na kuwakaribisha nchini kwa ajili ya kambi yao na kusema ujio wao utafungua milango kwa vilabu vingine pia kuja kuweka kambi nchini.

  Timu ya Red Arrow FC inayomilikiwa na jeshi la Anga nchini Zambia ikiwa nchini kwa mafunzo, inatarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na imeliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kuwatafutia timu moja ya kucheza nayo.
  Kutoka kushoto ni Ofisa habari wa Red Arrows Lt Melody Siisii, Mwenyekiti wa Red Arrows Col Nolasco Chilando, Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa na Ofisa Ubalozi wa Zambia nchini Tanzania Alex Chila, wakiwa ofisi za TFF - PPF Tower leo.

  0 0


  0 0

  Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela” (kulia) akisalimiana na Mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 kupitia promosheni hiyo mkazi wa Kilolo mkoani Iringa Uwezo Magedenge (22)mara alipomtembelea hotelini kwake alipofikia jijini Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa kitita chake wiki iliyopita na kurudi mkoani Iringa.
  Mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania ,Uwezo Magedenge (22) ambaye ni mkazi wa Kilolo mkoani Iringa,akiteta jambo na Balozi wa Promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” alipotembewa hotelini kwake na Balozi huyo kabla ya kukabidhiwa kitita chake wiki iliyopita.


older | 1 | .... | 737 | 738 | (Page 739) | 740 | 741 | .... | 3270 | newer