Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 739 | 740 | (Page 741) | 742 | 743 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. James Lembeli, imefanikiwa kuitembelea Manispaa ya Dubai na Mji wa Michezo wa Dubai (Dubai Sports City). 
   Aidha, Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongozana na Kamati. 
  Ziara hii fupi imekuwa ya mafanikio makubwa, kwani kamati pamoja wajumbe wengine wamekubaliana masuala muhimu ambayo wameona yanafaa kuishairi Serikali kuyafanyia kazi ili kuwa na Mipango Miji ya kisasa. 
   Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai aliongozana na ujumbe huu wa Kamati wakati wote wa ziara.
  Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, (wa pili kushoto) akiwa  na ujumbe huu wa Kamati hiyo
  Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai (kushoto) akiwa na Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. James Lembeli (katikati)
  Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai (kushoto) akiwa na Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na mjumbe wa kamati Mhe Esther Bulaya
  Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai (kushoto) akiwa na  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. James Lembeli


  0 0

  Na Faki Mjaka, Muscat, Oman 
  Serikali na Wadau binafsi wameshauriwa kuwasaidia Wajasiriamali wa Kitanzania ili waweze kuziweka bidhaa zao katika Vifungashio (Package) vyenye mvuto na kiwango cha ubora wa kimataifa. Kufanya hivyo kutawawezesha Wajasiriamali hao kupata soko la Bidhaa zao kwa Wateja wadogo na wakubwa katika nchi mbalimbali duniani.
   Ushauri huo umetolewa na Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh alipowatembelea Wajasiriamali wanaoshiriki katika Maeonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Muscat nchini Oman. 
   Amesema licha ya Tanzania kufanya vyema katika Maonesho hayo kuna baadhi ya changamoto ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi ili Tanzania izidi kupata sifa ya bidhaa zake kimataifa. Changamoto hizo ni pamoja na uwezo mdogo wa kuziweka bidhaa wanazozitengeneza katika Vifungashio (Package) ambavyo ubora wake haujafikia kiwango kinachotakiwa cha kimataifa. Balozi Saleh amefahamisha kuwa mbali na bidhaa hizo ikiwemo zile za Viungo kupata Soko kutoka kwa Wakaazi wa Oman lakini inakuwa ngumu kupata Soko kwa Wateja wa Maduka Makubwa (Supermarkets) ambao wangenunua bidhaa hizo kwa ujumla. 
   Ameongeza kuwa Wateja wa Maduka Makubwa wanahitaji bidhaa zilizowekwa katika Package ambazo zinaonesha kuwa zimepitia katika maabara ya kisayansi na kupata vigezo vyote vinavyohitajika kimatumizi. 
   “Naamini tukiwa na Package zenye ubora wa kimataifa zinazoonesha Warrant, muda wa matumizi basi hata Order za Wateja wa Supermarkets tungepata za kutosha ” Alisema Balozi Saleh Aidha Balozi Saleh amewashauri Wajasiriamali hao kuziweka bidhaa zao katika Vifungashio (Package) hata zile ambazo bado hawajafikiria kuziweka ikiwemo zile za Vinyago na Viatu ili kuvutia zaidi Wateja. 
  “Tumezoea kwetu kuwa Vinyago haviwekwi kwenye Package ila navyo vinatakiwa viwekwe pamoja na vitu vingine ili wateja wahamasike na Ubora wa Bidhaa zetu” Alishauri Balozi Saleh Hata hivyo Balozi Saleh ameishukuru Serikali ya Oman kwa mashirikiao yake makubwa na Tanzania na kwamba fursa hiyo iliyopatikana itakuwa na Matunda mazuri kwa Tanzania kutokana na kujitangaza vyema kwa Wageni na Wenyeji wa Oman. 
   Kwa upande wao Wajasiriamali hao Walimshukuru Balozi Saleh na Ofisi yake kwa kuwa karibu nao na kushauriana nao kila muda jambo ambalo linawapa faraja kubwa.
  Balozi wa Tanzania nchini Oman Ali Ahmed Saleh kushoto Aliyekaa kwenye kiti akipata burudani ya Msewe iliyoandaliwa kwa ajili yake na Kikundi cha Sanaa cha Zanzibar mara baada ya Balozi huyo kumaliza ziara yake ya kuwatembelea Watanzania na kushauriana nao mambo mbalimbali ya kukuza soko katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mjini Mascut nchini humo
   Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Zanzibar wakicheza Ngoma aina ya Uringe kwa Balozi wa Tanzania nchini Oman (hayupo pichani) mara baada ya Balozi huyo kuwatembelea Watanzania na kushauriana nao mambo mbalimbali ya kukuza soko katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mjini Mascut nchini humo. 
  Mjasiriamali wa Mavazi mbalimbali ikiwemo ya Kimasai Bi Anna Matinde akitoa ufafanuzi wa bidhaa zake kwa Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia.Balozi Saleh alifanya ziara ya kuwatembelea Watanzania hao na kushauriana mambo mbalimbali ya kukuza soko katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mjini Mascut nchini humo. Picha zote na Faki Mjaka-Mascut Oman.

  0 0

  Majimaji
  Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imethibitisha ushindi wa pointi na mabao matatu kwa timu za Majimaji na Toto Africans baada ya mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuvurugika kutokana na sababu mbalimbali.

  Toto Africans imepewa ushindi huo kwa mujibu wa Kanuni ya 41(3) ya FDL baada ya vurugu za washabiki wa Geita Gold kusababisha mechi hiyo iliyochezwa Februari 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita kuvunjika dakika ya 12.

  Pia Kamati hiyo iliyokutana Dar es Salaam jana (Februari 12 mwaka huu) imezuia mechi za FDL kuchezwa kwenye uwanja huo ambao hauna uzio wa kutenganisha wachezaji na washabiki kwa sababu za kiusalama.

  Toto Africans
  Naye mchezaji Venance Joseph wa Geita Gold ambaye alimpiga kichwa refa akipinga adhabu ya penalti iliyotolewa dhidi ya timu yake kwenye mechi hiyo amesimamishwa wakati akisubiri kosa lake kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

  Malalamiko ya Friends Rangers kwenye mechi dhidi ya Majimaji yametupwa na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kusababisha mchezo huo uliochezwa Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Majimaji mjini Songea kuvunjika dakika ya 39. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(4) ya FDL.

  Friends Rangers imepoteza mechi hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 28(1) ya FDL, Majimaji kama ilivyo Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu.


  Naye Kocha wa Friends Rangers, Herry Chibakasa (Mzozo) suala lake limepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF ili aweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni ya 39(8) ya FDL kwa kuhamamisha vurugu kwenye mechi dhidi ya Majimaji.

  Mwamuzi John Mafuru wa Mbeya aliyechezesha mechi ya Majimaji na Friends Rangers amefungiwa miezi 12 (kumi na mbili) kwa kutozingatia sheria kiasi cha kuvuruga mchezo. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 37(1) ya FDL.

  Pia Kamishna wa mechi hiyo Kim Rajab wa Dodoma amefungiwa miezi 12 (kumi na mbili) kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) ya FDL kwa kutoa taarifa zisizo sahihi.

  Lipuli ya Iringa imepewa ushindi wa mabao matatu na pointi tatu baada ya timu ya KMC (Tessema) kumchezesha mchezaji Morris Paulo Katumbo aliyekuwa na kadi tatu za njano kinyume na Kanuni ya 41(12) ya FDL. Katumbo ambaye alipata kadi hizo kwenye mechi namba 85, 100 na 112 alicheza mchezo huo uliomalizika kwa timu ya KMC kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
    

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


  0 0


  0 0

  Na  Bashir  Yakub

  Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, zipo aina nyingi za ndoa. Pamoja na kuwa na aina nyingi za ndoa, ndoa hizi tunaweza kuzigawa katika makundi makuu mawili. Kwanza, ndoa za serikali(civil marriage) na Pili ni ndoa za kimila(customary marriage).

  Ndoa za serikali ni zile ndoa zinazofungwa kwa mkuu wa Wilaya, Msajili wa ndoa pamoja na katika Ofisi nyingine za serikali kama Ubalozini n.k.

  Ndoa za kimila ni zile ndoa zinazofungwa kulingana na taratibu za kabila la wahusika; kwa mfano ndoa za wahaya, wachaga, ndoa za wazaramo na ndoa nyingine zitokanazo na makabila mbalimbali. 

  Ndoa za kidini pia zinaingia katika kundi hili la ndoa za kimila. Ndoa za kidini ni zile zinazofungwa kutokana  na imani ya dini za wahusika. Katika ndoa za dini kuna ndoa za kiislamu, kuna ndoa za kikiristo, ndoa za kibudha na dini nyingine nyingi wanazo ndoa zao. Mbali na aina hizo za ndoa nilizotaja hapo juu ipo aina nyingine ya ndoa ambayo kwa masikio ya wengi yaweza kuwa ngeni kwa wasomaji wetu  hapa.

  Aina hii ya ndoa inapatikana katika kifungu cha 160 kifungu kidogo cha kwanza katika Sheria ya Ndoa. Kifungu hiki kinasema kuwa “Itakapothibitika kuwa mwanaume au mwanamke wameishi wote kwa miaka miwili au zaidi  katika hali ambayo maisha yao yamekuwa kama mume na mke, litajengwa wazo au dhana (presumption) kuwa watu hao wameoana.” 

  Maana yake ni kuwa  mwanaume na mwanamke wakiishi wote kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi bila kufunga ndoa, kwa mujibu wa sheria watu hao watahesabika kama watu waliooana  hata kama watu hao hawakufunga ndoa kanisani, msikitini au  serikalini.

  Ni kwa ufupi sana tunaweza kusema kuwa wachumba au wapenzi wanaoishi kama mke na mume kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi, hao wanahesabika kuwa wameoana na sheria inawalinda sawa kabisa na inavyomlinda mke na mume waliofunga ndoa ya kawaida.  0 0


   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto) akimsimika kwa kumkabidhi fimbo ya ulezi baada ya kumvalisha joho, kofia na skafu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias Chikawe, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Regina Chonjo, na wapili kushoto ni mwanachama wa UWT wilayani humo, ambaye pia ni Mke wa Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lyamba
   Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo (kushoto), Mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, Profesa Amandina Lyamba (kulia) wakilisakata rumba na wanachama wenzao wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilayani humo baada ya Mbunge wao kusimikwa rasmi na Mwenyekiti wa UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo.
   
   Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Nachingwea, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa UWT wilayani humo baada ya Waziri huyo kusimikwa na rasmi na Mwenyekiti UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto kwa Chikawe), kuwa mlezi wa UWT wilayani humo. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo
   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba akizungumza kwa furaha wakati akitoa hotuba yake kwa wananchama wa UWT Wilaya ya Nachingwea baada ya kumsimika Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) kuwa mlezi wa UWT wilayani humo. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Katika hotuba yake hiyo, Waziri Simba alimuomba Waziri Chikawe aendelee kuisaidia UWT wilayani humo kama alivyokuwa anafanya awali. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Lindi, Faudhia Chiwangu.
   
   Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Nachingwea, ambaye pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akiwashukuru wanachama wa UWT wilayani humo kwa kumchagua kuwa mlezi wa umoja wao katika sherehe ya kusimikwa kwake iliyofanyika mjini Nachingwea leo. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, aliwaomba wanachama hao kuwa na ushirikiano kwa kuijenga CCM, pamoja na kuhakikisha wanawahamasisha wananchi jimboni humo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili kujiandaa kwa kuipigia kura Katiba iliyopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao. Kulia ni Mwenyekiti UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ambaye alimsimika mlezi huyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto) akimsimika kwa kumvalisha joho la ulezi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias Chikawe, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Picha zote na Felix Mwagara.


  0 0

   Kiwanja kina ukubwa wa 7,720 sqm ( Zaidi ya acre moja na nusu), Kipo Kiharaka, Bagamoyo umbali wa kama 5km kutoka baharini. Kina ardhi nzuri yenye rutuba, kipo tambalale. 
  Kipo karibu na mradi mpya wa kumbi za mikutano na pia karibu na kivuko kipya cha Bagamoyo kwenda Posta. Nguzo za umeme  na maji ya dawasco yako karibu. Bei ya kiwanja ni Tshs 395,000,000/=. Hati miliki itashughulikiwa kwa makubaliano maalum kati ya muuzaji na mnunuzi. kwa mawasiliano zaidi piga number 0766 333 700
   Tambalale


  0 0

   Ule usemi wa za mwizi ni arobani,umetimia leo baada ya vijana wawili wanaotumia pikipiki (majina yao hayakupatikana mara moja) wenye utaalamu wa hali ya juu wa kukwapua simu za mikonini za watu wawapo kwenye magari au hata watembea kwa miguu kushindwa kufurukuta mbele ya wananchi wenye hasira.
  Tukio hilo limetokea jioni hii mbele ya bustani ya Botanical kwa upande unaotazamana na geti kuu la kuingia Hospitali ya Ocean Road, baada ya kumkwapulia simu mwanadada mmoja (jina kapuni) aliekuwa akitembea kwa miguu na kwa bahati nzuri kulitokea msamalia aliekuwa na gari yake akaliona tukio zima na hapo ndipo alianza kuwafukuzia na mwisho wa mbio hizo ndio ukafika hapa baada ya kuzidiwa maarifa na pikipiki yao, hali iliyowapelekea kuanguka eneo hilo.Vijana hao walikamatwa na pikipiki yao ikachomwa moto.
   Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo,akiwasimulia watu waliofika kwenye tukio hilo namna mambo yalivyokuwa mpaka kufikia kuchomwa moto kwa pikipiki hiyo yenye nambari za usajili T 636 CXX.
   Taswira za kuwaka moto kwa pikipiki hiyo zikiendelea kuchukuliwa.
   Mdau akijipatia Selfie mbele ya pikipiki iliyokuwa ikiteketea kwa moto wakati huo.


  0 0

   Mandhari ya kiota kipya cha kisasa cha kilaji kiitwacho Break Point Carnivore jijini Dar es salaam  kilichofunguliwa rasmi jana Ijumaa na kuvutia wadau wengi wa mighawa ya Break Point za mjini na Kijitonyama ambapo mambo yote yanayopatikana huko kama vile "jirambe", "mchemsho", "foil meat" na kadhalika. Msemaji wa kiota hicho Kaka Daudi anasema Break Point imeamua kuondokana na staili ya "Msonge" na kuja na kiota chenye mandhari tofauti kabisa lakini huduma zile zile na zaidi kama vile Cappuccino, Ice Cream, Fresh Juice na mambo kama hayo... 
   Mandhari kwa ndani ambako kila pembe kuna big screen 
   Jiko la kisasa
   Msimamizi na mtaalamu wa makulaji Kaka Gadi kutoka Reading, Uingereza, yupo kuweka mambo sawa
   Kaka Gadi anasema "Nguvu ya Mamba, kumayi", yaani nguvu ya mamba ni majini. Na Break Point wanasema nguvu yao iko katika jiko maalumu la nyama choma inayoonekana pichani. Picha zaidi BOFYA HAPA
  video bofya mshale hapo kati chini....

  0 0


  0 0

  Wala hakosei kusema ‘kujua kazi ni raha’. Isha Mashauzi anakushuka tena kivingine na wimbo mpya kabisa “Nimpe Nani” unaodhihirisha kuwa anaijua vema kazi yake.

  Hii ni ‘single’ yake ya pili nje ya taarab ukiacha ule wa kwanza “Nimlaumu Nani” uliopigwa katika miondoko ya rhumba.

  “Nimpe Nani” ni wimbo unaoelea kwenye miondoko ya zouk rhumba lakini ukikolezwa kwa mbali na vionjo vya mduara.

  Wimbo huo wa dakika tatu na nusu ambao umerekodiwa katika studio za C9 Records chini ya producer C9 Kanjenje.

  Kinanda kimepigwa na Kali Kitimoto na C9, magitaa ya bass na solo yamepigwa na Babu Bomba wa Malaika Band.

  Sauti zote tamu unazozisikia humo ni za Isha Mashauzi kasoro sehemu ndogo sana isiyozidi sekunde 5 iliyotikiwa na Easy Man.
  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Francis Nanai, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo na kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bakari Machumu.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Teddy Mapunda Mshauri wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa juu wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Mkurugenzi Mtendaji Francis Nanai (katikati) na Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bakari Machumu, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo na kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuelezea kazi zinazofanywa na kampuni hiyo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Francis Nanai wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo na kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuelezea kazi zinazofanywa na kampuni hiyo.

  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa juu wa Kampuni ya Mwananchi Communication,Mkurugenzi Mtendaji Francis Nanai (wa pili kushoto) Mhariri Mtendaji Bakari Machumu (kulia) na Mshauri wa Kampuni hiyo, Teddy Mapunda (kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Feb 13, 2015. Picha na OMR

  0 0


  Dear friend of Lumumba Theatre Group and Nafasi Art Space

  We hope you are all doing well , and we would like to take this opportunity to invite you in our opening theatre performance on 21/2/2015 at Nafasi Art Space from 7:00 pm entrance 5000/= 

  This performance is a continuation of our project called PROFESSIONALIZING THEATRE PRACTICE IN TANZANIA that we started in 2014 , This project sponsored by EU and Parapanda Theatre lab Trust. The goal to bring back theatre performance in Tanzania and this will be the first time for the Lumumba Theatre to performance at Nafasi Art Space. So please don't miss it and try to share this email with your friends  as you can.


  0 0


  Na Profesa Joseph Mbele


  Kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, kimetimiza miaka kumi tangu nilipokichapisha, tarehe 5 Februari, mwaka 2005. Siku hiyo niliuingiza muswada katika mtandao wa lulu nikalipia namba ya utambulisho wa kitabu, yaani ISBN. Siku hiyo hiyo niliagiza nakala ya kwanza, nikaipata baada ya wiki moja hivi. Wiki hii ni kumbukumbu ya miaka kumi ya kuwepo kwa kitabu hiki.

  Mambo mengi yametokea katika miaka hii kumi kuhusiana na kitabu hiki. Nimepata fursa ya kusikia maoni ya wasomaji wengi. Baadhi wameandika maoni hayo na kuyachapisha, kama vile katika tovuti, blogu, na majarida. Wengine wameniandikia maoni yao katika barua pepe. Wengine wamenieleza maoni yao katika maongezi ya ana kwa ana. 
  Watu waliotoa maoni yao kuhusu kitabu hiki ni wa aina mbali mbali. Baadhi nawakumbuka vizuri, kama vile Mhashamu Askofu Owdenburg Mdegella wa dayosisi ya Iringa ya Kanisa la Kiluteri Tanzania, ambaye alisema kuwa kitabu kimemfurahisha sana na anataka wageni wakisome ili watuelewe wa-Tanzania. Aliniambia hayo siku tulipokutana kwenye chuo cha Peace House, Arusha, na alikuwa anaongea kutokana na uzoefu wake mkubwa wa kuwapokea na kushughulika na wa-Marekani wanaokuja Tanzania katika mpango wa ushirikiano baina ya waumini wa-Marekani na wa-Tanzania uitwao Bega kwa Bega.


  0 0

  Afisa Matekelezo Mwandamizi(SCO) wa mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Matilda A. Nyallu  akitoa elimu ya Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kwa Askari na watumishi raia makao makuu ya Wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es Salaam
   

  Askari na watumishi raia wakifuatilia elimu hiyo iliyokuwa inatolewa na maafisa wa PSPF waliofika makao makuu ya Wizara ya mambo ya ndani kutoa elimu ya  Mpango wa Uchangiaji wa Hiari.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  NOEL PIC
  Katika picha ni Noel Olevaroya akihutubia Maelfu ya wananchi katika moja ya harakati zake katika mkutano wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

  Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa vijana na mjumbe Wilaya ya Arusha kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Noel Olevaroya (37) ametangaza rasmi kupeperusha bendera ya chama hicho kwa kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha mjini

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Noel Olevaroya alisema kuwa nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha ni msukumumo kutoka kwa Mungu baada ya kumaliza nafasi yake ya uwenyekiti wa vijana na mjumbe wilaya ya Arusha mwaka 2014

  Alieleza kuwa msukumo huo ulikuwa ukimsumbua sana na ndipo aliamua kutii sauti ya Mungu kwa kutangaza kuwania nafasi hiyo ya kugombea kiti cha ubunge katika jimbo la Arusha mjini ambapo kwasasa jimbo hilo lipo mikononi mwa Godbless Lema

  Aidha alisema kuwa Mbunge anafursa nzuri sana ya kusaidia wananchi hata kwa kupitia mfuko wa jimbo,mshahara hali ambayo itasaidia kuwainua wananchi na kupunguza umaskini

  Alitoa wito kwa vijana wa Arusha kusikiliza sauti ya Mungu kwa kuwachagua viongozi bora wenye hofu ya Mungu kwa maslahi ya Nchi yetu
  (Habari na Pamela Mollel wa jamiiblog)

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  mradi wa msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani Lushoto mkoani Tanga jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita na Katibu Tawala wa wilaya hiyo (DAS), Josephine Kisigila. Mradi huo unaendeshwa na EfG.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akitoa hutuba fupi kwa mgeni rasmi.
    Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo.
   Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliopatiwa mafunzo hayo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliamia na Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa wakati wa Misa maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu wakati wa Misa maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliamia na Mwenyekiti wa Bodi ya Madini Wizara ya Fedha Richard Kasesela, wakati walipokutana katika Misa maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam. Katikati yao ni Mwenyekiti wa Kanisa hilo, Paul Mzuka.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Kanisla la Mtakatifu Joseph, Paul Mzuka, baada ya kuhudhuria Misa maalum ya kumuombea Marehemu Evodius Walingozi, iliyofanyika leo Feb 14 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam. Picha na OMR.

  0 0

   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Klabu ya Real Madrid, Rayco Ghasia (kulia).
   Mzee Augustino Mtauka akisaini fomu za usajili wa kituo kipya cha mchezo wa soka kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania.. Mzee Mtauka alikuwa akisaini fomu hizo kwa niaba ya mjukuu wake Godfrey Oscar (katikati), usajili uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam Jumamosi. Kulia ni Msajili Ally Salehe wa Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  Msajili wa Vijana katika Program ya NSSF-Real Madrid Sports Academy, Rachel Kayuni (kulia), kutoka Idara ya Elimu ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akitoa maelekez kwa baadhi ya wazazi na vijana waliokuwa wakisajiliwa kujiunga na kituo hicho cha soka kilicho chini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na klabu ya Real Madrid ya Hispania. Usajili huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Karume.
  Mtoto Osama Rashid akijaza fomu maalum kwa ajili ya kujiunga na kituo cha michezo cha NSSF-Real Madrid Academy. Kulia ni mama yake Tatu Ali akishuhudia. Taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mwenyekiti wa Chadema Freman Mbowe akiwa anasoma utuba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa  chama hicho wa kanda ya kaskazini unaofanyika leo katika  hotel ya new Arusha jijini hapa
  viongizo wa chadema  akiwemo mwenyekiti wakiwa wanasali kwanza kabla ya mkutano wa viongozi wa kanda ya kaskazini kuanza
   Naibu katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu akiwa anaongea na waandishi wa habari
   Na Woinde Shizza
  MWENYEKITI wa chama cha demokrasi na maendeleo Chadema Freeman Mbowe amesema kuwa  chama chao kimejipanga kuahakikisha kinahamasisha  kwa  nguvu zote wananchi weweze kwenda kujiandikisha katika  daftari la mpiga kura 

  Alisemakuwa hii itaweza kumsaidia kila mwananchi  kuweza kupata haki yakumchagua kiongozi bora  anaemtaka  katika uchaguzi mkuu  ujao  wa kuwachagua viongozi wakuu ambao ni rais ,wabunge na madiwani.
  Alisema kuwa pamoja ya kuwa tume wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi hili , wao wamejipanga kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili litatangazwa  kuanza rasmi watajitaidi kwa njia yoyote kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha
  Alisema kuwa kwa upande wa kupiga kura katiba wanaendelea na msimamo wao ambao walitangaza awali wa kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba  huku akisisitiza kuwa swala la kutoshiriki katika mchakato wakura za maoni auingiliani kabisa na  kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura 

  Alimaliizia kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi  sana pindi pale ambapo watasikia zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu limewadia  ili waweze kupata haki yao ambayo itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao wataka.
   


older | 1 | .... | 739 | 740 | (Page 741) | 742 | 743 | .... | 3270 | newer