Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

WAZIRI MUKANGARA MGENI RASMI FAINALI YA WANAWAKE

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara atakuwa mgeni rasmi kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Taifa Wanawake kati ya Pwani na Temeke itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni itachezeshwa na mwamuzi wa FIFA, Jonesia Rukyaa, na itaonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam. Waamuzi wasaidizi ni Hellen Mduma, Agnes Alphonce, na Mwanahamisi Matiku wakati Kamishna ni Ingridy Kimario.

Timu za Ilala na Kigoma zitacheza mechi ya utangulizi kutafuta mshindi wa tatu kuanzia saa 8.00 mchana. Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin na kufanyika kwa mara ya kwanza nchini atapata kombe na sh. milioni tatu.

Makamu bingwa atapata sh. milioni mbili wakati mshindi wa tatu atapata sh. milioni moja. Kiingilio kwenye mechi hizo ni bure.
  
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

warsha ya siku moja kujadili mpango mkakati wa Maendeleo wa miaka 25 ya benki ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania yafanyika jijini Dar

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Thomas Samkyi akizungumza katika warsha juu ya kujadili mpango wa maendeleo wa taasisi hiyo kwa miaka 25 ijayo. Warsha hiyo ilifanyika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam.
Mkuu wa Mipango, Sera na Ushirikiano wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Francis Assenga akizungumza na wadau katika mkutano huo.
Wadau wa sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji wakifuatilia warsha ya mpango wa maendeleo wa miaka 25 wa benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) uliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Prof. Muhongo akabidhi Ofisi kwa Simbachawene jijini dar leo

$
0
0
Waziri  mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati makabidhiano ya ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo,leo jijini Dar es Salaam.
Waziri  mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene (kulia) akikabidhiwa rasmi nyaraka za ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo,leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amesema uadilifu unahitajika katika sekta ya Nishati na Madini pasiwepo na rushwa kwani hiyo ni kuweza kusaidia watanzania masikini wanaongalia sekta hiyo kwa maendeleo ya uchumi wao.

Muhongo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akikakabidhi ofisi kwa Waziri  mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene,amesema lazima kuwepo na uzinagatiaji wa mikataba ili watanzania waweze kunufaika na rasilimali zao.

Muhongo amesema Simbachawene sio mtu wa tamaa siku zote alipokuwa Naibu wa Waziri wa Nishati na Madini walikuwa wakiambiana juu ya kuwatumikia watanzania wengi na sio mtu binafsi.

Amesema lazima tujenge uchumi imara kutokana na sekta hii ili watanzania waweze kukua kiuchumi kutokana na sekta ya madini inavyokua kwa kasi.

Muhongo amewataka waandishi kuelimisha watanzania kwa ajili ya ustawi wa taifa na sio mtu mmoja au ubinafis wa mtu.

Kwa upande wa Simbachawene amesema ataendeleza mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake kwa  kuweka uwazi kwa kila kitu kinachofanyika,kwani ofisi ya umma sio mali ya mtu.

Wateja wa Benki ya CRDB kushindania Magari 12

TAARIFA KUTOKA DAWASCO JUU KUENDELEA KWA MATENGENEZO KWENYE MTAMBO WA MAJI RUVU CHINI

$
0
0
MNAMO TAREHE 23, 24 NA 25 JANUARI 2015, SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO) ILIZIMA MTAMBO WA RUVU CHINI ILI KURUHUSU MKANDARASI KUUNGANISHA BOMBA JIPYA NA LA ZAMANI (CROSS –SECTION). HATA HIVYO BAADA YA KAZI KUKAMILIKA NGUVU YA MAJI ILISABABISHA KUYUMBISHA SEHEMU ILIYOUNGANISHWA AWALI.

HALI HII IMESABABISHA HUDUMA YA MAJI KUKOSEKANA KWENYE BAADHI YA MAENEO YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA ALHAMISI 29/01/2015  
 KWASABABU HIYO MAENEO YAFUATAYO YAMEKOSA MAJI:

MJI WA BAGAMOYO, VIJIJI VYA MAPINGA, KEREGE NA MAPUNGA. BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.

MAENEO MENGINE NI MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, MANZESE, MABIBO, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.

MKANDARASI ANAENDELEA NA MATENGENEZO NA HUDUMA YA MAJI ITAREJEA TENA BAADA YA SAA 12 KUANZIA LEO.       
         
WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA”

Taswa FC yatinga nusu fainali Asas Dairies bonanza

$
0
0
Iringa. Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imetinga kwa vishindo michuano ya soka ya Asas Dairies Limited inayoendelea mkoani Iringa baada ya kushinda mechi zake zote za hatua ya makundi. 
Taswa FC ilichezo mechi yake ya kwanza dhidi ya Mkwawa Senior na kuicharaza kwa mabao 5-0 katika mchezo wa kundi A. Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Samora, ulikuwa mkali na wa kusisimua na Taswa FC ilifunga mabao yake kupitia kwa Zahoro Mlanzi aliyefunga mabao matatu kutokana na pasi safi kutoka kwa Muhidin Sufiani, Ibrahim “Maestro”Masoud na Edo Kumwembe. 
Mabao mengine ya Taswa yalifungwa na Ali Mkongwe baada ya pasi safi ya Mohamed Akida na Nico Ndifwa baada ya pasi ndefu ya Elius Kambili. Mkwawa Senior ilishinda kuipita ngome ya Taswa FC chini ya Wilbert Molandi, Athuman Jabir na Mbozi Katala. 
Katika mchezo wa pili, Taswa FC iliifunga Pawaga mabao 3-0 yaliyofungwa na Saidi Seif, Nico Ndifwa na Athuman Jabir. Katika mchezo wa kundi B, Iringa Veteran ilifunga Mkwawa Junior mabao 6-1 yaliyofungwa na Lisa Mwalupindi aliyefunga mabao matatu, Mzee Mbata na Haji Mambo. 
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary aliipongeza timu yake kwa ushindi huo ten bila kufungwa na kuahidi kutwaa ubingwa huo. Kutokana na matokeo hayo, Taswa itacheza na Mkwawa Junior katika nusu fainali ya kwanza iliyopangwa kuanza saa 2.00 asubuhi kwenye uwanja huo huo.

CHIPUKIZI WA UVCCM WAJIFUA VIKALI TAYARI KWA KILELE CHA MIAKA 38 YA CCM KESHO

$
0
0
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa  UVCCM Sixtus Mapunda wakitazama mazoezi ya mwisho ya Chipukizi hao
 Mshika bendera ya CCM kwenye kikosi cha Bendera cha Gwaride la Umoja wa Vijana wa CCM, Sharif Mohammed na wenzake wakipita kwa ukakamavu mbele ya jukwaa kuu wakati wa mazoezi ya mwisho ya gwaride na halaiki kwa ajili ya Kilala cha Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yanayofanyika kesho Kitaifa kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma 
 Vijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
 Vijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
 Vijana wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wakati wa mazoezi yao ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.

Bunge laridhishwa na utendaji wa serikali, lapitisha taarifa za za Kamati ya Bajeti, Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Hesabu za Serikali (PAC), Miundombinu na Nishati na Madini.

$
0
0
 Na Hussein Makame, MAELEZO, Dodoma
KAMATI za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na ile ya Hesabu za Serikali (PAC), zimeridhishwa na mafanikio na hatua zilizochukuliwa na Serikali kwa kuongeza mapato yake na kushughulikia changamoto zinazoikabili katika kutekelza majukumu yake.

Kufuatia hali hiyo, Bunge limepitisha taarifa za kamati hizo na nyingine tatu, huku Serikali ikiahidi kufanyia kazi yale yote yaliyopendekezwa kwenye taarifa hizo ili kulipeleka Taifa kule kunakotakiwa.

Taarifa za Kamati ambazo Bunge limezipitishwa jana na juzi usiku ni za Kamati ya Bajeti, Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Hesabu za Serikali (PAC), Miundombinu na Nishati na Madini.

Akihitimisha hoja yake, Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC Mhe. Rajabu  Mbarouk aliipongeza Serikali na Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia kwa hatua alichokua kwa watendaji wa Serikali waliobainika kutumia vibaya fedha za umma.

“Mimi ni mpinzani lakini kwa hili, kwa kweli nimpongeza Waziri kwa sababu jana aliniletea list (orodha) karibu ya halmashauri zote nchini ambazo wakurugenzi amewachukulia hatua, kilichobaki ni mimi kuichukua ile taarifa na kumpelekea kwa CAG kwa ajili ya kuihathibitisha” alisema Mbarouk.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Zitto Kabwe aliipongeza Malmalaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuongeza mapato na kwamba wameiomba iongeze mapatao katika miaka ijayo ili kuifanya mamlaka hiyo iwe na tija kwa taifa.

“Ni lazima tuwe wakweli, Mamlaka ya Bandari imeongeza sana sana ufanisi katika kazi zake, mapato yameongezeka kutoka shilingi Bilioni 320 mpaka shilingi Bilioni 537 katika kipindi cha miaka miwili” alisema Zitto.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba aliithibitishia kamati na wabunge waliotoa michango yao kuwa wamepokea michango yao na wataifanyia kazi.

“Kwanza nisema ndugu Mwenyekiti, tumewasikia wabunge, tumepokea waliyoyasema na tutayafanyia kazi, tupo kwa ajili hiyo” alisema Naibu Waziri Nchemba.

Alisema tangu mwaka wa fedha ulipoanza, mkakati wa Wizara chini ya usimamizi wa Waziri wa Fedha ilikuwa ni kuhakikisha kila fedha inapokusanywa inakwenda pale ilipokusudiwa.

Alifafanua kuwa hata hoja za baadhi ya wabunge kuwa kuna miradi imepata mgawo sifuri, inawezekana hiyo sifuri ni ya fedha zile zinazotoka nje.

“Naongea hili kwa uhakika, mwaka wa fedha uliooanza tu tulitoa Bilioni 500 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na mpaka wizara zingine wakashangaa wakauliza hizi fedha mmekosea au ndivyo kweli zinatakiwa zije” alisema na kuongeza:

“Walidhani ni za mishahara, haikuzoeleka kutokea fedha nyingi ndani ya mwezi wa kwanza wa bajeti kwa ajili ya shughuli za maendeleo”

Hivyo aliwaomba wabunge wazingatie mambo mamwili, moja Waziri ameweka utaratibu kwamba kila taasisi inapopokea fedha za maendeleo  ni lazima ipeleke mrejesho imetumia fedha zile kwa shughul gani na mradi ule uonekane kabla fedha zingine hazijakwenda.

Alisema jambo la pili ni nia ya Serikali kuhakikisha kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya mifuko na matumizi maalum ya miradi ya maendeleo na kwamba kuanzia mwezi Februari wanarekebisha utaratibu wa kutengeneza mchanganuo wa fedha kuhakikisha fedha hizo zimekwenda kwenye miradi ya maendeleo.

Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri unatarajiwa umeahirishwa hadi Jumatatu ambapo bunge hilo linataraji kupokea taarifa za Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.


 Spika wa Bunge la Jamhuri, Mhe Anne Makinda akieleza jambo leo Bungeni mjini Dodoma ambapo mkutano wa 18 wa Bunge hilo unaendelea.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji George Masaju akitoa ushauri kwa Bunge la Jamhuri.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Dkt. Festus Limbu, alijibu hoja za wabunge waliochangia kwenye taarifa yake.


 Naibu Waziri wa Fedha, Mhe Mwigulu Nchemba akijibu hoja za kamati zilizoelekezwa katika wizara yake.
Mbunge wa Kawe, Mhe Halima Mdee akitoa mchango wakati wa kujadili taarifa za kamati za Bunge, bungeni mjini Dodoma. Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma

introducing "kifanuni" by email star from arusha

introducing "Sitaki mess" by Wilko from arusha

Under the Same Sun through IZAAS Medical Project provide lotions to albinos at Mugeza Mseto in bukoba

DRFA YATANGAZA TIMU ZILIZOINGIA 18 BORA LIGI YA MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimetangaza timu 18 zilizofanikiwa kutingia katika hatua ya 18 bora (raundi ya pili) ya michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam. 

 Timu hizo ni kutoka katika kundi (A) ambazo ni Red Coast,Yanga U20,Changanyikeni na Ukonga UTD,kundi (B) Simba U20,Stakishari,Zakhem na Beira Hotspurs,kundi (C) FFU,Sifa UTD,Pan Africa na Sinza Stars,huku kundi (D) likitoa timu za Shababi,New Kunduchi,Ugimbi na Azania Ngano.

Timu mbili zilizopata nafasi ya kuongezwa kwenye hatua hiyo ya pili,ni Sifa Politan FC pamoja na Tuamoyo FC,zinazokamilisha idadi ya timu 18. 
 Makatibu wakuu wa timu zote 18,wanatakiwa kufika katika ofisi za DRFA zilizopo kwenye jengo la Machinga Complex Ilala (Ghorofa ya 3),siku ya jumatano 04/02/2015,saa 8 mchana,kukutana na kamati ya mshindano kwaajili ya kupata utaratibu. 

 Baada ya kikao hicho DRFA itapanga makundi na kutoa ratiba ya kuanza kwa patashika hiyo. 

Imetolewa na Omary Katanga
 Afisa habari wa DRFA

PINDA, MANGULA NA KINANA WAWASILI SONGEA KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 38 YA CCM

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akilakiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, jioni ya leo tayari kushiriki maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM yanayofanyika kitaifa kesho Mkoani Ruvuma ambapo mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Pinda akiwapungia mkono wananchi na wana CCM waliofika kumlaki uwanjani hapo
 Vikundi vya sanaa vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Pinda, Kinana na Philip Mangula

SIMBA YAITUNGUA JKT RUVU BAO 2 - 1 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Beki wa timu ya Simba,Hassan Isihaka (26) akiangalia namna ya kumzuia Mshambuliaji wa Timu ya JKT Ruvu,Jabir Aziz katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi pinde kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda Bao 2-1.
 Nyanda wa Timu ya Simba,Ivo Mapunda akiwania mpira wa juu na Mshambuliaji wa timu ya JKT Ruvu,Samuel Kamuntu katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi pinde kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda Bao 2-1.
 Wachezaji wa Timu ya JKT Ruvu wakishangilia goli lao la kusawazisha dhidi ya Simba,katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi pinde kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda Bao 2-1.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

charles hilary ana kwa ana na kipa wa cameroun joseph-antoine bell jijini Malabo, equatorial guinea

$
0
0
 Mtangazaji mashuhuri wa BBC Swahili Charles Hilary (kati) akiwa na kipa wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroun na klabu ya Marseille ya Ufaransa Joseph-Antoine  Bell pamoja na kocha wa Congo Brazaville Claude Le Roy walipokutana jijini Malabo, Equatorial Guinea kwenye michuzo ya kombe la Afrika. Bell ameshacheza katika michuzno ya kombe la dunia mara tatu (198219901994), na pia kwenye michuano ya Olimpiki 1984 Summer Olympics na kwenye kombe la African Cup of Nations
Watangazji wa BBC Swahili, Charles Hilary na Salum Kikeke wakiwa katika uwanja wa Bata nchini Equatorial Guinea kutangaza moja kwa moja michuano ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika hii leo kati ya Congo Brazaville na Congo DRC ambapo hadi mapumziko ni 0-0
 kipa wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroun Joseph- Antoine Bell akiwa langoni pake enzi hizo  kipa wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroun Joseph Anthonie Bell 
Joseph-Antoine Bell akipambana na Bebeto wa Brazil kwenye kombe la dunia 1994

SELLS AND SALE WITH MICHUZI TV: INTRODUCING LAGOS IN DAR ES SALAAM BOUTIQUE

Waziri wa Ujenzi Afanya ziara Mkoani Mbeya

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bi Rosemary Sitaki Sinyamule wakati wa Ukaguzi wa daraja la mto Songwe linalounganisha Wilaya ya Ileje na nchi ya Malawi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Isongole-Itumba km 9 katika Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya. Kulia ni Mbunge wa Ileje Mheshimiwa Aliko Kibona. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bi Rosemary Sitaki Sinyamule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akipewa maelezo kuhusu ukarabati wa Daraja la mto Songwe Wilayani Ileje.

Rais Kikwete awasilisha Ripoti ya Kamati ya viongozi Juu ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasilisha ripoti ya utendaji wa kamati hiyo katika mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia.Mkutano huo ulimalizika jana
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi(The Committee of African Heads of State and governments on Climate change) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimakabidhi nakala ya Ripoti ya utendaji mwenyekiti mpya wa kamati hiyo Rais wa Misri Abdel Fattah el Sisi wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa Ethiopia.Rais Kikwete alipongezwa kwa kuiwezesha kamati hiyo kupata mafanikio makubwa.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Sweden,Stefan Lofven jijini Addis Ababa Ethiopia jana.Tayari Rais Kikwete amerejea nchini baada ya kumaklizika mkutano wa wakuu wa nchi za umoja wa Afrika AU jijini Addis Ababa Ethiopia uliofanyika kwa siku mbili.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa 23 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ulifanyika katika mji Mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.
(picha na Freddy Maro).

UTT-AMIS YATOA SEMINA KUHUSU UWEKEZAJI WA PAMOJA KWENYE MASOKO YA FEDHA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga akitoa mada kuhusu Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja UTT-AMIS  kuhusu Uwekezaji wa pamoja kwenye Masoko ya Fedha wakati wa semina ya kuwaelimisha watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika uwekezaji.
Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wakimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga (hayupo pichani) wakati akitoa mada kuhusu Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja UTT-AMIS  kuhusu Uwekezaji wa pamoja kwenye Masoko ya Fedha wakati wa semina ya kuwaelimisha watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika uwekezaji.
Baadhi ya wafanyakazi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakiwa katika semina hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT, Hamis Kibola (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina ya iliyoendeshwa na UTT-AMIS kuhusu Uwekezaji wa pamoja kwenye Masoko ya Fedha ikiwa ni kuwaelimisha watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuhusu masuala ya uwekezaji.

Mshindi wa milioni 100 za Jaymillions kukabidhiwa kitita cha fedha alizojishindia

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (kulia) akimsikiliza kwa makini mshindi wa milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo Bi.Uwezo Magedenge (22) akimfafanulia jambo kuhusiana na ushindi wake,wakati alipomtembelea kijijini kwao Pamilini Kilolo mkoa wa Iringa kwa ajili ya kumchukua na kumpeleka jijini Dar es Salaam, kwa makabidhiano rasmi ya kitita chake hivi karibuni.Wengine katika picha kushoto ni Mama yake mzazi Delfine Kisoma(64) na Baba yake Alatanga Magendenge (70).
Baba mzazi wa mshindi wa kwanza wa milioni 100 kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Alatanga Magendenge akimfafanulia jambo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(kulia) kuhusiana na ushindi wa mwanae Uwezo Magendenge(watatu toka kushoto)wakati alipomtembelea mshindi huyo nyumbani kwao kijiji cha Pamilini Kilolo Iringa kwa ajili ya kumchukua na kumpeleka Dar es Salaam kwa ajili ya kumkabidhi rasmi ya kitita chake hivi karibuni,kushoto ni mama mzazi wa mshindi Delfine Kisoma.
Mshindi wa Milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Bi. Uwezo Magedenga (kushoto) akifurahia jambo na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)wakati alipofika kijijini kwao Pamilini Kilolo Iringa ili kujua mazingiara yake na kumpeleka jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kwa ajili ya kumkabidhi rasmi ya kitita chake hivi karibuni. Katikati ni Mkuu wa kampuni hiyo Kanda ya Kusini magharibi Amos Vuhahula.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images