Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 725 | 726 | (Page 727) | 728 | 729 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Rais wa Ujerumani, Mhe. Joachim Gauck anatarajiwa kuwasili nchini usiku wa tarehe 02 Februari, 2015 kwa ziara ya kitaifa ya siku tano kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

  Mhe. Rais Gauck atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Februari, 2015 na atakagua Gwaride la Heshima na kupigiwa mizinga 21. Wananchi wanaombwa kuwa watulivu wakati mizinga hii ikipigwa kwani ni salama.

  Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Gauck atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete yakifuatiwa na mazungumzo rasmi. Aidha Marais hao watakutana na Waandishi wa Habari.

  Baadaye siku hiyo ya Februari 03, Mhe. Rais Gauck atakutana na Wafanyabiashara, atatembelea Kanisa la Kilutheri la Azania Front, atakutana na Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia na kushiriki Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete, Ikulu.

  Mhe. Rais Gauck ambaye ameongozana na Mke wake Bibi Schadt, Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Ujerumani na Ujumbe wa Wafanyabiashara tisa, ataondoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar tarehe 04 Februari, 2015 ambapo atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabla ya kushiriki kwenye Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Viongozi wa Dini kuhusu Amani. Rais Gauck pia atakutana na Vijana kutoka Ujerumani wanaojitolea katika Programu ya Weltwarts Visiwani humo.

  Jioni ya Februari 04, Mhe. Gauck ataondoka Zanzibar kuelekea Mkoani Arusha. Akiwa Mkoani humo siku ya tarehe 05 Februari, 2015 atatembelea Taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na kuhutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA). Mhe. Gauck na ujumbe wake watatembelea pia Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti ambapo atazindua Kituo kipya cha kudhibiti Ujangili.

  Mhe. Rais Gauck anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 06 Februari, 2015 na kuondokea  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kurejea Ujerumani.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  01 Februari, 2015

  0 0

  Mtaalam wa TEHAMA kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Rajab Sollo akiwaonesha watendaji wa Baraza hilo (Hawako pichani) kuhusu namna mfumo wa kanzidata ya kuhifadhi kumbi za Starehe na Burudani unavyofanya kazi kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii makao ya BASATA yaliyo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
  Mtaalam wa IT kutoka BASATA Bwana Sollo (anayeonekana kwa mbele) akitoa mafunzo kwa watendaji wa BASATA kuhusu kanzidata ya kuhifadhi kumbi za Starehe na urudani nchini.
  Sehemu ya watendaji waliohudhuria mafunzo hayo wakimfuatilia kwa makini Mkufunzi wa TEHAMA kutoka BASATA Bw. Rajab Sollo.


  0 0

  Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga klabu ya Simba faini ya sh. milioni tatu kutokana na timu yake kuvaa jezi ambazo hazikuwa na nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom wakati wa mechi yao dhidi ya Kagera Sugar.

  Mechi hiyo namba 50 ya Ligi Kuu ya Vodacom ilichezwa Desemba 26 mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 13(7) ya Ligi Kuu inayotaka klabu kuheshimu masharti ya udhamini wa Ligi Kuu kwenye mechi zake.

  Nayo Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 28(4) kwa kusababisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati yake na Toto Africans iliyochezwa Januari 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuvurugika.

  Kutokana na mchezo huo kuvurugika, Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu. Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 28(1) inayotawala ligi hiyo.
    
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

   Mshambuliaji Machachari wa timu ya Ndanda,Masoud Ally akitoa pasi maridadi kabisa mbele ya beki wa timu ya Yanga,Juma Abdul wakati wa mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
   Mshambuliaji wa timu ya Ndanda,Omega Seme akiangalia namna ya kumtoka Beki wa Yanga,Oscar Joshua mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
   Beki Hasifiwi: Beki wa timu ya Yanga,Rajab Zahir akiruka juu kuondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwao katika mtanange wa ligi kuu Tanzania Bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imemalizika kwa suluhu ya 0-0.
   Hapiti mtu hapa: ni kama anaonekana kusema  beki wa timu ya Ndanda,Paul Ngalema wakati akimdhibiti Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva.


  0 0

  Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
  Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa viongozi mbali mbali wa CCM wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.
  Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na UVCCM katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.


  0 0

   Mshindi wa pikipiki aina ya Bajaj kupitia promosheni  ya 'Weka Upewe' ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Judith Gwimile (wa nne kushoto), akikabidhiwa kadi ya Bajaj na kibao cha namba na Meneja wa Tawi la benki ya NBC Mwanza, Godhard Hunja, jijini humo. Wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo tawini hapo.
   Mshindi wa pikipiki aina ya Bajaj kupitia promosheni  ya 'Weka Upewe' ya  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Judith Gwimile akiwa ndani ya bajaji hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Tawi la benki ya NBC Mwanza, Godhard Hunja (katikati),  jijini humo. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa benki  hiyo tawi la Mwanza, Margareth Touwa.
  Mshindi wa pikipiki aina ya Bajaj kupitia promosheni  ya 'Weka Upewe' ya  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Judith Gwimile (katikati), akibadilishana  mawazo na Meneja wa Tawi la benki ya NBC Mwanza, Godhard Hunja (kulia)huku wafanyakazi wengine wa benki hiyo wakimsikiliza katka hafla hiyo.


  0 0

  Mgeni rasmi Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akizunguza na wanafunzi walioudhuria kwenye siku ya Career Day iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam
  Rais wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara,(CBE),Ramadhani S Kirungi akiwakaribisha wageni mbalimbali katika siku ya "CAREER DAY" iliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Jijini Dar es salaam
  Afisa wa PSPF Hadji Jamadary akiwa anafafanua na kuelezea  kuhusu na uchangiaji wa hiari wa PSS kwa wanafunzi wa Chuo Cha Biashara (CBE) jijini Dar es salaam
  Maseko Kodalo Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF akiwa anatoa maelekezo ya kujiunga na mfuko huo kwa mpango wa lazima, Mikopo ya Elimu na mikopo ya kuanzia maisha.
  Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akitolewa ufafanuzi kufusu kazi za mfuko wa PSPF na Afisa wa PSPF Hadji Jamadary (wa pili kutoka Kushoto).

  0 0

   Kituo cha radio cha E FM 93.7 leo kimezindua kipindi kipya kabisa cha Sports Headquarter (Makao Makuu ya habari) kikiwa cha kwanza katika historia kuruka kwa masaa matatu kuzungumzia michezo tena asubuhi saa tatu mpaka saa sita mchana.  
  Pichani juu ni Watangazaji nguli wa Michezo nchini Maulid Baraka Kitenge na  Ibrahim Masoud Maestro wakikiendesha kipindi hicho cha masaa matatu leo.
  Kitakuwa kinaruka Jumatatu mpaka Ijumaa saa tatu Asubuhi mpaka saa sita mchana. Hii no katika historia kabisa katika radio za Tanzania kipindi cha michezo kuwa cha masaa matatu tena kuanzia asubuhi mpaka mchana.


  0 0

  Paroko wa Kanisa Katoliki,Parokia ya Enduimet,Jimbo Kuu la Arusha,Padri Pius Shao(katikati)akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuzalisha Umeme kwa nguvu za Jua ,kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kusambaza Teknolojia(KAKUTE),Livinus Manyanga na Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Longido,Gerson Mtera.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Kusambaza Teknolojia(KAKUTE),Livinus Manyanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuzalisha Umeme kwa nguvu za Jua katika hospitali ya Kanisa Katoliki,Parokia ya Enduimet wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,mtambo huo umegharamiwa na Wakala wa nishati Vijijini(REA)na wadau wengine.
  Paroko wa Kanisa Katoliki,Parokia ya Enduimet,wilaya ya Longido Jimbo Kuu la Arusha,Padri Pius Shao akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtambo wa kuzalisha Umeme kwa nguvu za Jua uliogharamiwa na Wakala wa nishati Vijijini(REA)na wadau wengine.


  0 0

  Naibu Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa BRN, Bw. Peniel Lyimo akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi na maafisa kilimo kilichoanza Dar es Salaam leo Jumatatu ambapo aliwataka kuwa wabunifu, kutatua changamoto za kisekta na kushirikishana na wataalamu wengine ili malengo ya BRN katika kilimo yafanikiwe.
  Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika Wizara ya Kilimo, Bw. January Kayumbe akitoa mada kuhusu malengo na utekelezaji wa BRN katika sekta ya kilimo kwa washiriki kutoka mikoa inayotekeleza BRN katika kilimo (hawapo pichani).
  Sehemu ya mada ikiainisha eneo mojawapo ambapo BRN iliweka mikakati katika sekta ya kilimo ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa maghala 275 kwa ajili ya kuhifadhi mazao nchi nzima. Taarifa ya utekelezaji wa mwaka mmoja tu ikionesha kuwa maghala yote yameshafanyiwa tathmini na ujenzi na ukarabati wa baadhi ukianza.

  Sehemu ya maafisa wa ngazi mbalimbali katika sekta ya kilimo kutoka mikoa inayoshughulika na kilimo chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) wakifuatilia hotuba ya Naibu Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango huo, Bw. Peniel Lyimo (hayuko pichani) wakati wa kikao kazi kilichoanza Dar es Salaam jana.
  Washiriki wa kikao kazi kilichoanza leo Dar es Salaam wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa kujadili namna ya kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi ya BRN katika sekta ya kilimo. (Picha na Idara ya Mawasiliano PDB)

  0 0

  Benki ya NMB imewafagilia jeshi la polisi kwa kuikubali benki yao kuwa benki chaguo la kwanza na kusema kitendo hicho kinadhihirisha kuridhishwa kwao na huduma bora za kibenki zinazotolewa na NMB kupitia Makundi mbalimbali katika jamii ya Tanzania. 
   Hayo yalisemwa jana mjini Dodoma na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Tom Borghols alipokuwa akitoa Maneno ya utangulizi.
  Aliyasema hayo kabla ya Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi wa benki ya NMB - Abdulmajid Nsekela kuwasilisha  maada juu ya mchango wa taasisi za kifedha katika shughuli za polisi. 
   NMB ndiyo benki pekee ambayo imekuwa ikidhamini Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Polisi unaofanyika kila mwaka
  Jeshi la polisilimeipongeza benki ya NMB kwa udhamamini huo na kuiomba iendelee  kuwasaidia pale wanapokwama kwani kufanya hivyo ni kuunga juhudi za jeshi la polisi kusimamia sheria za nchi na kuzuia uhalifu katika jamii ambayo ndani yake kuna wateja wa NMB. 
   NMB imedhamini kiasi cha shilingi Milioni 75 kwaajili ya maandalizi na shughuli za mkutano pamoja na kutoa pikipiki 5 zenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwaajili ya kurahisisha kazi za operation za polisi za kila siku. 
   NMB ndiyo benki yenye mtandao mkubwa Zaidi nchini ukiwa na matawi Zaidi ya 75 na ATM Zaidi ya 600 nchi nzima pamoja na Zaidi ya wateja Milioni 2, hazina ambayo hakuna benki nyingine nchini yenye nayo
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bw.  Tom Borghols  akitoa Maneno ya utangulizi kwenye mkutano wake na  maafisa waandamizi wa jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam
  Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi wa benki ya NMB  Bw. Abdulmajid Nsekela kuwasilisha  mada juu ya mchango wa taasisi za kifedha katika shughuli za polisi kwenye mkutano huo. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathia Chikawe (mwenye suti katikati mbele) akiwa na maafisa wa polisi waandamizi katika picha ya pamoja na maafisa wa Benki ya NMB

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu , Bw Abbass Talimba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi leseni ya kuendesha bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa.
  Bodi ya Michezo ya bahati nasibu ya Taifa leo imetoa leseni ya kuendesha Bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa ambayo itakuwa ikiendesha bahati nasibu hiyo hapa nchini ambapo Bahati nasibu hiyo itaanza mnamo tarehe 4 Julai 2015.
  Bei ya tiketi zitakazouzwa itagharimu shilingi za Kitanzania shilingi 500 kwa kila tiketi.
   Baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Murhandziwa pamoja na viongozi wa Bodi ya Michezo ya Bahati nasibu ya Taifa wakitazama video ya Mwenyekiti wa kampuni ya Kampuni ya Murhandziwa amaye hakuweza kufika kwenye hafla hiyo
   Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, Abbass Talimba (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, William Mdundo  wakikabidhi leseni kwa viongozi wa Kampuni ya Murhandziwa ambao ndio wamepewa kibali cha kuendesha bahati nasibu ya Taifa nchini Tanzania. Aliyeshika Leseni hiyo ni Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Murhandziwa, Lucien D Avece( wa tatu kutoka kulia).
   
   Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Murhandziwa, Lucien D Avece akiyatolea ufafanuzi maswali yaliyoulizwa na waandiahi wa habari (hawapo pichani)
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton - Masaki

  0 0

  Mgeni Rasmi katika Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Waziri wa Uchukuzi,Mh. Samuel Sitta akiwasilisha mada katika semina hiyo iliyofanyika leo mjini Dodoma.
  Waziri wa Fedha Saada Mkuya akitoa ufafanuzi juu ya maswali ya wabunge. 
  Kamishna wa Sensa Tanzania, Hajjat Amina Mrisho akiwasilisha mada.


  0 0

  Na Mwandishi wetu, 
  Morogoro 
  Bondia mashuhuri wa kulipwa nchini, Francis Cheka, ambaye maarufu kwa jina la SMG (pichani), amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh, milioni moja kwa kosa la kumpiga meneja  wa baa yake, Bahati Kibanda. 
  Cheka alitiwa hatiani Julai 2 mwaka jana kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali Kibanda ambaye alikwenda hapo kudai fedha zake katika baa aliyokuwa anaifanyia kazi  ijulikanayo kwa jina la Vijana Social Hall. 
  Hakimu Mwanamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Mhe. Said Msuya alikubaliana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuthibitisha shitaka hilo. 
  Hakimu Msuya alisema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao kwa watu wengine na anatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni moja. 
  Pamoja na Cheka kupewa nafasi ya kujitetea, bondia huyo hakutoa maelezo yoyote na kuiachia mahakama hiyo kutoa adhabu inayostahili kwa bondia huyo aliyejizolea sifa kemkem katika ngumi za kulipwa nchini. 
  Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni, familia ya Cheka inasemekana ina mpango wa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

  0 0

  The International Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR) is primed to finally close down during this year, 2015, after over twenty years of prosecuting persons who played leading roles in the Rwandan genocide in 1994 that claimed the lives of more than half a million innocent civilians of mainly Tutsi and some moderate Hutus who sympathized with them.
  In preparation for its closure, the Tribunal separated 117 out of 414 staff members between October and December 2014 that were on board at the beginning of 2014. The number consists of 91 international and 26 local staff members. Although this is part of an ongoing process of implementing the ICTR Completion Strategy, in accordance with the UN Security Council Resolution 1966 of 22 December 2010, it represents the largest number of staff who have been downsized by the Tribunal and signifies the near completion of its mandate.
  It is expected that about an additional 159 international staff members will be separated during 2015. Should everything proceed according to schedule, the ICTR will shut down on 30 September 2015. This date has been given to both the UN General Assembly and the Security Council.
  Only one major case remains for the Tribunal to complete after which it will release the remaining staff members and close permanently. The Butare appeal case, involving 6 accused persons among whom is Pauline Nyiramasuhuko, the only woman that the ICTR has tried for genocide, is expected to hold its oral arguments in Arusha during April 2015 and judgement is expected to be delivered in August 2015.
  Regarding what will happen to the functions and activities that will outlive the ICTR, the UN Security Council established a Residual Mechanism for International Criminal Tribunals (the Mechanism), in its Resolution 1966 (2010), to take over the remaining functions of the Tribunal and that of its sister Tribunal, the International Criminal Tribunal for the former Yugoslavia (ICTY). The Mechanism has already taken over some of the ongoing functions of the ICTR, including the enforcement of sentences of those convicted and sentenced by the Tribunal, the tracking, arrest and prosecution of the three top priority fugitives who remain at large as well as the care and protection of witnesses.

  0 0

  Mfuko wa Pensheni wa GEPF umesaini mkataba wa uwekezaji na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika eneo la Bunju. Uwekezaji huo utakaohusisha kumbi za mikutano (Conference Halls) zenye uwezo wa kuchukua watu Zaidi ya 1,200, migahawa (Restaurants), Hoteli yenye hadhi ya kimataifa yenye vyumba Zaidi ya 102, Maktaba, Bwawa la kuogelea (Swimming Pool) pamoja na sehemu za mazoezi (Gymnasium) Uwekezaji huo utagharimu Zaidi ya shilingi Bilioni 10 za kitanzania na unategemewa kukamilika katikati ya mwaka huu 2015.
  Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi (wa pili kulia) akiongoza majadiliano ya awali kati ya Menejimenti ya GEPF pamoja na Menejimenti ya NBAA kabla ya zoezi la kutiliana saini mkataba wa uwekezaji.
  Mwenyekiti wa Bodi ya GEPF,Bi. Joyce Shaidi (kulia) pamoja na mwenyekiti wa NBAA Profesa Issaya Jairo wakisaini mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji wa pamoja wakiongozwa na mwanasheria wa NBAA Bi Agness Kessy.
  Utiaji saini huo ulishuhudiwa na makamu mwenyekiti wa NBAA Bi Anna Mbughuni ( mwenye suti ya blue), Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Bw Pius Maneno, Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw Daud Msangi pamoja na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GEPF Bw Festo Fute.
  Mwenyekiti wa Bodi ya GEPF Bi Joyce Shaidi akibadilishana nyaraka za mkataba wa uwekezaji wa pamoja na Mwenyekiti wa NBAA Profesa Issaya Jairo.
  Pichani baadhi ya watendaji wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) wakifurahia jambo mara baada ya zoezi hilo kukamilika.

  0 0


  0 0

   Merceds Benz ML 350 ya mwaka 2003 inauzwa.
  Rangi ni Silver, engine capacity ni 3720 cc, petrol, iko kwenye hali nzuri kabisa. Bei milioni 22 Tshs tu
  Kwa mawasiliano zaidi 
   tafadhali tumia namba za simu :
   Ubavuni
   Kwa mbele 
  Ndani

  0 0

   Wananchi wakiwa wamepanga mawe na miti kuziba barabara ya Bagamoyo Road maeneo ya Kawe Bondeni jijini Dar es salaam leo ili kushinikiza kuwekewa matuta ya barabarani ili kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara eneo hilo. Hadi tunaruka hewani Jeshi la Polisi lilikuwa limeshawatawanya wananchi hao na kuondoa vizuizi hivyo baada ya kusababisha foleni ya takriban saa moja hivi.


  0 0


  East African Court of Justice Arusha, 2 February 2015: The East African Court of Justice First Instance Division will resume its sessions this week. The Lower Court sets off immediately after the Appellate Division concluded theirs last week. 
  The First Instance Division headed by the Honorable Principal Judge, Justice Jean Bosco Butasi will sit for the whole month of February and thirteen (13) matters will be handled in this quarter. The 13 matters include four (4) Applications and four (4) References matters coming up for hearing, Four (4) References coming up for scheduling conferences and one (1) Reference coming up for delivery of Judgment. 
  The bench of the Judges of the First Instance Division is composed of Honourable  Justice Jean Bosco Butasi (Principal Judge), Justice Isaac Lenaola (Deputy Principal Judge), Justice Dr. Faustin Ntezilyayo, Lady Justice Monica Mugenyi and Justice Fakihi A. Jundu. 
  All matters will be in open Court 2nd Floor EACJ wing. 
  The East African Court of Justice (EACJ or ‘the Court’), is one of the organs of the East African Community established under Article 9 of the Treaty for the Establishment of the East African Community. Established in November 2001, the Court’s major responsibility is to ensure the adherence to law in the interpretation and application of and compliance with the EAC Treaty.
   Arusha is the temporary seat of the Court until the Summit determines its permanent seat. The Court’s sub-registries are located in the respective National Courts in the Partner States.

older | 1 | .... | 725 | 726 | (Page 727) | 728 | 729 | .... | 3278 | newer