Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Programu Maalumu kwa Wasichana inayoendeshwa na Chuo Kikuu huria na Nafasi Opportunity Society(NOS) yazinduliwa

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa tatu kutoka Kulia) akifurahi jambo katika uzinduzi wa mafunzo ya wasichana yaliyojikita katika mafunzo ya ufundi,mawasiliano na ujuzi wa kibiashara.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa mafunzo kutoka VETA Bi.Leah Lukindo,anaefuata ni makamu mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Tolly Mbwette.
Makamu Mkuu wa chuo kikuu Huria cha Tanzania Prof Tolly Mbwette akifungua mafunzo kwa ajili ya wasichana yanayoendeshwa na chuo kikuu huria na shirika kutoka Canada linaloitwa Nafasi Opportunity Society (NOS).Ushirikiano huo umebobea kwenye kusaidia wasichana ambao hawajapata nafasi ya kupata mafunzo ya ufundi,mawasiliano na ujuzi wa biashara ili kuboresha nafasi zaidi za kujiajiri na kujenga uwezo wa kujiamini.Programu iyo itashirikisha pia VETA na Golden Touch Beauty College katika kutoa mafunzo ya utengenezaji wa nywele kwa kutumia utaalamu wa ndani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiwahutubia wasichana waliokatika programu ya mafunzo inayoendeshwa kwa ubia kati ya Chuo Kikuu Huria na shirika kutoka Canada,Nafasi Opportunity Society(NOS).Prof Elisante alikazia zaidi kwa wasichana hao kuuza thamani na sio hujuzi walionao na kuzitumia changamoto walizonazo kuwa fursa.


kamati ya bunge kilimo,maji na mifugo yafanya ziara mkoani morogoro

$
0
0
Kamati ya Bunge ya kilimo, maji na mifugo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Peter Msola imefanya ziara katika mkoa wa Morogoro kwa kutembelea kijiji cha Fulwe,mradi wa maji wa Mambogo manispaa Morogoro na mradi maji mikumi.

Aidha tarehe 22 Januari ,2015 kamati hiyo itatembelea wilaya ya Kilolo na manispaa ya Iringa na tarehe 23 kamati itatembelea wilaya ya Rungwe.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kilimo, maji na mifugo,Prof. Peter Msola (shati nyeupe) akiongoza kamati yake kukagaua mradi maji wa Mambogo manispaa ya morogoro.Katikati ni Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla (kushoto) akiongea na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kilimo, maji na mifugo,Prof. Peter Msola walipotembelea mradi maji Mikumi.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akitoa maelekezo kwa mkandarasi mradi maji Mikumi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje akutana na Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (mwenye tai) akisalimiana na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Luigi Scotto alipotembelea Wizarani leo.
Balozi Gamaha akisalimiana na Kansela Raffaele De Benedictis kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia ambaye alifuatana na Balozi Scotto walipotembelea Wizara ya Mambo ya Nje leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KLABU ZA SOKA KUJIGHARAMIA HOTELI MICHUANO YA CAF

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefanyia marekebisho kanuni zake za michuano ya ngazi ya klabu kwa upande wa malazi ambapo sasa timu zitachagua na kujilipia zenyewe hoteli zinapokuwa kwenye mechi za ugenini.

Kabla ya marekebisho ya kanuni hiyo, timu ngeni ilikuwa ikilipiwa hoteli na timu mwenyeji kwa msafara usiozidi watu 25. CAF ilikuwa imepitisha hoteli maalumu katika kila nchi ambapo mwenyeji alitakiwa kuziweka timu ngeni.

Kwa marekebisho hayo, Chama cha Mpira wa Miguu cha nchi mwenyeji kitakuwa na wajibu wa kuitafutia hoteli timu ngeni iwapo tu kitaombwa kufanya hivyo, lakini jukumu la kulipia malazi litakuwa la timu yenyewe.

Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na timu mbili za Azam na Yanga katika michuano ya CAF. Azam inacheza Ligi ya Mabingwa (CL) ambapo itaanzia nyumbani Februari 15 mwaka huu kwa kuikaribisha El Merreikh ya Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Nayo Yanga itacheza michuano ya Kombe la Shirikisho (CC), na imepangiwa kucheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya BDF IX ya Botswana. Mechi hiyo itafanyika Februari 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

BRN yatekeleza mengi katika mwaka mmoja

$
0
0
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao Serikali ya Tanzania imeanza kuutekeleza tangu Julai, 2013 umeleta matokeo makubwa yatakayosaidia kukuza uchumi wa nchi na huduma kwa wananchi.

Hayo yalisemwa juzi visiwani Zanzibar na Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekeleaji wa Miradi (PDB) inayosimamia utelezaji wa BRN kwa Tanzania Bara, Omari Issa alipokuwa akitoa mada kwa watendaji waandamizi wa Serikali.


Katika semina hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein, Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi wengine waandamizi wa Serikali, Bw. Issa alieleza uzoefu wa mwaka mmoja wa utekelezaji wa BRN Tanzania Bara.

Bw. Issa alisema mafanikio ya BRN kwa Tanzania Baya yametokana na nidhamu ya utendaji ambayo mfumo huo umeileta ikiwemo kuweka vipaumbele vichache vinavyogusa sekta muhimu kwa Taifa, kuweka muda na mfumo wa utekelezaji ili kupata matokeo ya haraka.

WAFANYAKAZI WA VODACOM TANZANIA WAPEWA ELIMU JUU YA HAKI ZA JINSIA

$
0
0
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba akisikilizwa kwa makini na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati alipokuwa akitoa mafunzo ya jinsia kwenye semina iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi wake iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Esther Mattle akimuuliza swali Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba, wakati wa semina ya masuala ya jinsia iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.

NBC YAMWAGA MILIONI 62 KUSAIDIA MRADI WA USIMAMIZI WA TAKA

$
0
0
Meneja Miradi wa Envirocare, Bw Isreal Richard (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja ya mradi wa majaribio wa usimamizi wa taka kwa utunzaji mazingira na ustawi wa jamii jijini Dar es Salaam leo. Mradi unaendeshwa na Envirocare kwa ufadhili wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Ofisa Afya Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni, Kawa Kafuru (kulia) akizungumza na washiriki wa semina hiyo.

Filamu: Pata Filamu ya FEDHEHA kupitia Mtandao

$
0
0
Katika maisha tunayoishi duniani sio vizuri kufanyiana mabaya, Kwani hujui kesho itakuaje. Malipo ni hapahapa Duniani . Fuatilia hii kupitia mtandao .......

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo Fedheha au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii


Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

OFISI YA BUNGE YAKABIDHIWA NA SERIKALI YA CHINA MSAADA WA VIFAA VYA TEHEMA VYENYE TAHAMNI YA DOLA ZA KIMAREKANI LAKI MOJA

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokea kutoka kwa Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Dkt. LU Youquing baadhi ya Vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa serikali ya China kwa ajili ya kusaidia shughuli za Bunge. Vifaa hivyo vyenye thamani ya Dola za Kimarekani laki moja vimekabidhiwia leo katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Spika jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza kutoa neno la shukrani mara baara ya kupokea vifaa hivyo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Dkt. LU Youquing mara baada ya hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA.

Mh. Ummy Mwalimu ziarani jijini Arusha

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Bw. Fidelis Lumato mara baada ya kutembelea kiwanda cha A –Z cha Jijini hapo kukagua masuala ya Mazingira.

Dk. Shein aufungua Mkutano wa Madaktari kutoka Uingereza

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein akifungua mkutano maalum wa wataalamu wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo kutoka Uingereza mkutano huo uliowashirikisha Madakatari Kutoka nchini Tanzania katika ukumbi wa Hoteli ya Breezes Hotel Bwejuu Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja jana
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa madaktari kutoka nchini Uingereza wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein alipokuwa akifungua mkutano maalum wa wataalamu wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo kutoka Uingereza uliofanyika jana katika ukumbi wa Breezes Hotel Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja.Picha na Ikulu.

Siku ya warembo ndani ya kiota cha Samaki Samaki katikati ya Jiji

Mfuko wa Pensheni wa PPF watembelewa na uongozi wa club ya Arsenal kwa lengo la kujitangaza

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF ndugu William Erio (katikati) akipokea jezi ya timu ya Arsenal kutoka kwa Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimaendeleo ya Arsenal Bwana Sam Stone (kulia). Kushoto ni Meneja wa Mahusiano ya Kimaendeleo ya Arsenal Bwana Daniel Willey.Lengo la ziara hiyo ni kuanzisha mahusiano kati ya PPF na Club ya Arsernal kwa kuendelea kujenga imani kwa wateja wao na kuendelea kujitangaza.
Uongozi wa club ya Arsenal ukipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF ndugu William Erio (Kushoto).

kamera ya mtaa kwa mtaa ndani ya Michuzi TV leo

MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAPEWA MAFUNZO KUHUSU TAKWIMU RASMI

$
0
0
Meneja Tawala wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madembwe (katikati) akiwahutubia Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi yaliyofanyika leo mkoani Morogoro. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Bw. Edward Kaluvya.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua habari wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo akiwa katika mahojiano na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.


Mchezaji Hamis Tambwe alia na TFF,atawaka wanaoleta vurugu wachukuliwe hatua

$
0
0

Mshambuliaji Hamis Tambwe amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuchukua hatua stahiki dhidi ya wachezaji wa Ruvu Shooting kwa kitendo cha kumshambulia na kumtolea lugha chafu uwanjani ikiwemo kumbagua kwa kumuita mkimbizi.


Akizungumza Makao Makuu ya klabu ya Yanga iliyopo mtaa wa Twiga na Jangwani leo, Tambwe alisema kuwa kitendo alichofanyiwa ni cha kinyama na anakilaani kwa nguvu zote, na anataka aelezwe wazi iwapo wachezaji kutoka mataifa mengine hawatakiwi kucheza Tanzania.

"Uwanja wa Taifa kuna kamera, matendo mengi sana mabaya tumekuwa tukifanyiwa wachezaji wa kigeni, naamini baada ya mchezo TFF wanakaa kupitia mikanda ya mchezo wanaona kila kitu lakini hakuna adhabu zinazochukuliwa tunavyodhalilishwa na kubaguliwa.

"Nimetukanwa, nimeitwa Mkimbizi, nipo nchini kihalali na nafanya kazi kwa kufuata sheria zote kwa nini waniite mkimbizi, nipo tayari kusema matusi waliyonitukana kwa mabosi wangu na kwa TFF ili hatua stahiki zichukuliwe, mpira sio vita, mpira ni burudani, mpira ni 'fair play', lakini hapa imekuwa ni tofauti.

"Kitendo walichonifanyia ni sawa na kunishikia bastola, ni unyama wa hali ya juu walitaka kuniua, yani wamenikaba nilikuwa naona roho yataka toka, hatukuwa vitani walitakiwa wacheze mpira wa 'profesional' hivi tutaogopa kucheza Tanzania."alisema kwa masikitiko.

"Hawakuja kucheza soka, walikuja kupigana, walinipiga kiwiko, wakanipiga ngumi na mwisho walinikaba shingoni nikaona pumzi zinataka niishia.


Hii ni hatari, kuna mtu anaweza kuanguka akapoteza maisha siku moja. Wale wanajeshi hawaingii uwanjani kucheza soka, wanakwenda kucheza na mwili wa wachezaji wenzao.

Ngoma Africa band na Jinamizi lao la Bongo Dansi barani ulaya lazidi kuwanasa washabiki

$
0
0
Imebainika kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni almaarufu viumbe wa ajabu Anunnaki Alien,inayoongoza na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja, imejikuta ipo katika hali ya kukosa usingizi tena baada ya kutakiwa kutumbuiza maomyesho zaidi katika msimu ujao wa joto.

Watayarishaji wa maonyesho makubwa ya nje barani ulaya wanashinikizwa na washabiki wao kuwa ni lazima waipandishe jukwaani Ngoma Africa Band kutokana na mdundo wao wa Bongo dansi.

Mapromota hao baada kuwekwa roho juu na washabiki wao nao wamedhamilia kuwapambanisha washabiki hao na bendi maarufu ya Ngoma Africa band yenye makao yake nchini ujerumani,habari za uhakika zimetonya kuwa bendi hiyo imekubali kuenda kutumbuiza katika nchi za Latvia na Austria na maonyesho mengine katika msimu wa joto.

Hali hiyo ya washabiki kushinikiza katika maonyesho inaifanya bendi ya Ngoma Africa band kuwa katika mzunguko wa maonyesho makubwa na wanamuziki kukosa muda wa kupumzika.
Lakini inasemekana kamanda Ras Makunja na kikosi chake wanauwezo wa aina yake wa kuwamudu washabiki wao waliodata akili na jinamizi la muziki wa dansi wa bongo kule barani ulaya.ffu-ughaibuni pia wanasikika online at www.ngoma-africa.com

NHC yaendesha kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wake katika hoteli ya Naura Springs, Arusha.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akikabidhi zawadi ya simu ya kisasa ya I Phone 6 kwaajili ya kuboresha ufanisi kwa Ofisa Mwandamizi Uendelezaji Biashara Fatima Rajabu ambaye aliibuka mshindi wa jumla wa maigizo ya vitendo kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha. Kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba (NHC), David Shambwe akitoa mada kwenye kongamano hilo. Shambwe alizungumzia hatua muhimu za kuibua miradi kuitekeleza na hatimaye kuiuza kwa ufanisi kwa wateja na kufuatilia malipo baada ya kuuza nyumba zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini. 

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA CBE LEO

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema (wa pili kutoka kulia) akimtambulisha viongozi wa chuo cha CBE ,Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd (katikati) leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akipata maelezo kutoka kwa Bi. Esther Kibua, mwanafunzi wa mwaka wa 3 wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Dar es salaam juu ya namna chuo hicho kinavyowaandaa kuitumia elimu wanayoipata chuoni hapo pindi watakapomaliza masomo yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akifafanua akifafanua jambo alipotembelea banda la maonesho la Idara ya Mizani na Vipimo la Chuo cha CBE leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya chuo hicho.Kushoto ni Mwalimu wa Idara ya Mizani na Vipimo wa Chuo hicho Bw. Faraja Nyoni. 

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

KAGERA WATUPWA NJE YA MASHINDANO YA WANAWAKE TAIFA CUP KWA MATUTA 4-3 NA TIMU YA MWANZA

$
0
0

Na Faustine Ruta, Mwanza
Timu ya Wanawake kutoka Mkoa wa Kagera imetupwa nje ya Mashindano kwa Matuta baada ya kumaliza mtanange wao kwa sare ya Nyumbani ya Ushindi wa 2-1 na  Ugenini,CCM Kirumba Mwanza na Matuta kupigwa na Timu ya Mwanza kuibuka na Ushindi wa bao 4-3. 



Mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Timu ya Mwanza ndio walianza kupata bao mapema dakika ya 2 kupitia kwa mchezaji wao matata Meriam Kimbuya (10) kwa kukatiza katikati ya mabeki na kufunga bao hilo la kwanza. Kipindi cha pili mchezaji huyo huyo Meriam Kimbuya aliwafungia bao tena Mwanza katika dakika ya 64 na kufanya 2-0 dhidi ya timu ya Kagera. Kagera waliongeza Bidii na dakika ya 73 Mchezaji Anna Katunzi aliachia shuti kali lililomzidi nguvu kipa wa Mwanza na kuishilia nyavuni na kufanya 2-1.
Kwenye kasi...... Mchezaji wa Kagera akiambaa na mpira
Kipa wa timu ya Mwana akiwapanga Wachezaji wakati wa kupiga mpira wa adhabu langoni mwake kipindi cha Kwanza. 
Nani zaidi!! Mahesabu ya kumtoka Mtu yanatakiwa hapa!!

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images