Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

MADIWANI MANISPAA YA MOSHI WASUSIA KIKAO CHA BAJETI

0
0

Msathiki Meya akizungumzia msimamo wake juu ya hatua ya wajumbe wa baraza hilo kutoka nje ya ukumbi wa mikutano wakimtuhumu mkurugenzi wa manispaa hiyo ,Shabani Ntarambe kujihusisha katika uporaji wa Viwanja.
Diwani wa kata ya Kaloleni ,Michael Mwita (CCM) akizungumza juu ya kitendo cha madiwani wenzake kutoka nje huku wakituhumu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhusika katika uporaji wa viwanja vya halmashauri hiyo.


Diwani wa kata ya Kiusa ,Stephen Ngasa akiongozana na mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo kutoka nje ya ukumbi huo.


Wananchi wa maeneo ya miradi ya maji watakiwa kutozembea kujadili maendeleo ya miradi

0
0
Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi, akieleza jambo wakati alipowasili kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Lindi tayari kukagua miradi ya maji.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Nassor Himid na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi Mathei Makwinya.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mwantumu Mahiza akiwakaribisha wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji waliotembelea mkoa huo kukagua baadhi ya miradi ya Maji iliyopo mkoani humo.
Ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiwasili kwenye mtambo wa kusukuma maji wa Chikombe.

MAREKANI NA UJERUMANI WAIPA TANZANIA VIFAA VYA KISASA KUKABILIANA NA UJANGILI MBUGA YA SELOUS LEO

0
0
Meneja wa Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo kuhusu masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokeavifaa vya kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous leo
Maelezo kuhusu masalia hayo ya  injini hiyo ya moshi iliyoachwa na wajerumani Benson Kibonge.
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress akizungumza kabla ya kutiliana saini na Nyalandu mkataba ya kukabidhiana vifaa hivyo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani  Egon Kochanke.

BALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN AKUTANA NA WATANZANIA WANAOSHIRIKI MAONESHO YA SANAA NA UTAMADUNI MJINI MASCUT

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akisalimiana na Mwandishi wa Chanel Ten Said Makala Ofisini kwake alipowaita kwa lengo la kuwapa nasaha Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman.
Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima kushoto akimkaribisha Balozi wa Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia kutoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman. Katikati ni Mkuu wa Msafara wa Watanzania hao Bi Khadija Batashy.
Baadhi ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.

WAZIRI CHIKAWE AWAAPISHA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA TUME YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA JIJINI DAR LEO

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimuapisha Afisa wa Jeshi la Magereza, Elmas Linus Mgimwa kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Waziri Chikawe ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimpa hati ya kiapo Afisa Utumishi wa wizara hiyo, Ernest Maalugu kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia-meza kuu) akiongoza kikao cha Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya kiutumishi na kiutendaji wa askari katika Majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Meza Kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MKOA WA MBEYA WAIOMBA IDARA YA MAMBO YA KALE KUWAKABIDHI MAKUMBUSHO YA MAMBO YA KALE YA KIMONDO

0
0
Wanahabari wakitoka katika  Kimondo  kulia na Slvanus  Kigomba  (ITV) na kulia ni Iren Mwakalinga (TBC),nyuma yao ni ofisi ya makumbusho  hayo.
Mwanahabari  wa Star Tv Iringa  Mawazo Marembeka  kushoto akiwa na Francis Godwin mzee  wa matukiodaima katika Kimondo
Wanahabari  wakimhoji mhifadhi msaidizi  wa makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo Mbeya  Bw Mussa Nsojo

SOMA HABARI KAMILI HAPA

NAIBU WAZIRI WA UJENZI AKAGUA KIVUKO CHA MV UTETE WILAYANI RUFIJI MKOANI PWANI

0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge(wa kwanza) akishuka ngazi mara baada ya kukagua kivuko cha MV-Utete ambacho hakitoi huduma ya usafirishaji kutokana na kupungua kwa kina cha maji cha mto Rufiji.
Muonekano wa kivuko cha MV-Utete ambacho kimeegeshwa na kusitisha huduma zake kutokana na kupungua kwa kina cha maji cha mto rufiji.

Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Yatembelea Miradi ya Maji Tanzania Bara

0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz Prof. Peter Msolla na Naibu Waziri wa Maji Mh. Amosi Makalla wakifungua koki za maji kando kidogo ya manispaa ya Iringa.
Kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz wakiongozwa na Prof. Peter Msolla na Naibu Waziri wa Maji Mh. Amosi Makalla wakikagua miundombinu ya maji katika Halmashauri ya Ilola.
Mhandisi wa maji Manispaa ya Iringa akisoma taarifa ya miradi ya halmashauri ya manispaa hiyo mbele ya kamati, Naibu Waziri na Mkuu wa Mkoa wa Iringa.


Graca Machel, Waziri Kairuki walia na ndoa za utotoni

0
0
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki akisalimiana na Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini na mwanaharakai wa haki za wanawake na watoto Bi. Graca Machel jijini Dar es Salaam jana (Jumatano, Januari 21, 2014). Wengine ni wadau kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (kushoto) akiongea akiwa na Mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini na mwanaharakai wa haki za wanawake na watoto Bi. Graca Machel (katikati) jijini Dar es Salaam jana (Jumatano, Januari 21, 2014). Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) hapa nchini Dkt. Natalia Kanem. Bi. Machel yupo nchini kuunga mkono jitihada za wadau mbalimbali katika kupambana na vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni.
-----------------
aibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Jasmine Kairuki and Mke wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Graca Machel wametoa wito kwa wadau kutoka taasisi za umma na binafsi kuunganisha nguvu ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu na kuondokana na ndoa za utotoni.

Bi. Machel, kupitia asasi yake inayojulikana na Mfuko wa Graca Machel (Graca Machel Trust), yupo nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya kikazi kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi mbalimbali zilizopo nchini kupiga vita ukeketaji na ndoa za utotoni.

Tangu mwezi Agosti 2014, Mfuko wa Graca Machel kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali ya ‘Children’s Dignity Forum (CDF)’ na Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), wamekuwa wakianzisha na kuendesha miradi mbalimbali inayolenga kumaliza ndoa za utotoni katika mkoa wa Mara ambao matukio ya ndoa za utotoni yanaelekwa kuwa mengi.

Miradi hiyo ni pamoja na mafunzo kuhusu athari za ndoa za utotoni na ukeketaji kwa maofisa wa Mahakama, Polisi, viongozi wa kidini na kimila pamoja na walimu na wanafunzi.

Akiongea jijini Dar es Salaam jana (Jumatano, Januari 21, 2015), Bi. Machel amesema ingawa serikali na wadau wengine wamefanya jitihada kubwa ili kumaliza ukeketaji na ndoa za utotoni, lakini vitendo hivyo bado vinaendelea na hivyo kuhitajika mkakati unaojumuisha wadau wote ili kuondokana na matatizo hayo yanayotokana na tamaduni potofu.

“Baadhi ya tamaduni zinaweza kubadilishwa, hususan pale zinapodhuru watu, jamii na taifa,” alisema Bi. Machel na kuongeza kuwa nguvu za pamoja zinahitajika kutoka ngazi za chini kabisa.

“Hebu tujaribu kuunda umoja wenye nguvu ili kumaliza ndoa za utotoni. Umoja ambao unajumuisha wadau wa sekta ya umma na binafsi, viongozi wa kimila na kidini, shirikisho la walimu na asasi za kiraia…hili jambo lisiwe la mtu mmoja, liwe letu sote!’ alisema Bi. Machel anayetambulika kama mwanaharakaiti wa kimataifa wa haki za watoto.

Bi. Machel, ambaye taasisi yake inajihusisha na haki za wanawake; haki za watoto; na demokrasia na utawala bora, alisisitiza kuwa umoja huo unapaswa kuwa na mipango mathubuti inayotekelezeka wakati wote hata pale kunapokuwa na mabadiliko ya uongozi wa katika wilaya au vijiji.

Akiongea katika mkutano huo, Naibu Waziri Kairuki alimshukuru Bi. Machel kwa jitihada zake na kumhakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa watoto wote, hususan wa kike wanapata elimu na ndoa za utotoni na vitendo vya ukeketaji vinamalizika mkoani Mara na nchini kote.

Naibu Waziri alimweleza Bi. Machel, ambaye aliambatana na Mwakilishi wa UNFPA hapa nchini Dkt. Natalia Kanem na Mkurugenzi Mtendaji waCDF Bw. Koshuma Mtengeti kuwa haki za watoto zimejumuishwa katika Katiba Inayopendekezwa. Aidha, Naibu Waziri Kairuki aliongeza kuwa serikali imeongeza jitihada za kutoa elimu kwa watoto wa kike  na jamii kwa ujumla kuhusu madhara ya ndoa za utotoni na vitendo vya ukeketaji.

Kairuki pia alimweleza Bi. Machel namna katiba mpya inatakavyoisadia serikali katika kusimamia sekta muhimu kama elimu ili kuwawezesha watoto wote, wakiwemo wa kike, kupata haki zao ikiwemo haki ya kupata elimu.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Kairuki, ili mafanikio makubwa yapatikane, ni muhimu kuwa na mikakati inayojumuisha watunga sera, viongozi wa kidini na jamii zinazojihusisha na vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni.

Bi. Machel alitarajiwa kuondoka leo (Alhamisi, Januari 22, 2015) kwenda mkoani Mara kukagua utekelezaji wa miradi ambayo inatekelezwa kwa pamoja kati ya serikali, CDF na UNFPA.


shukurani

Filamu: Pata Filamu ya Mdundiko kupitia Mtandao

0
0
Katika maisha tunayoishi duniani sio vizuri kufanyiana mabaya, Kwani hujui kesho itakuaje. Malipo ni hapahapa Duniani . Fuatilia hii kupitia mtandao .......

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo Fedheha au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii


Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

Dk. Hussein ateuliwa kuwa mwenyekiti wa muda wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC

0
0
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imemteua Dk Kassim Hussein kuwa mwenyekiti wa muda wa bodi ya wakurugenzi.

Hatua hiyo imetokana na kuteuliwa kwa aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Profesa Mussa Assad, kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa NBC, Bwana Pius Tibazarwa alisema Dk Hussein atashika wadhifa wa uenyekiti wa bodi ya benki hiyo mpaka pale atakapoteuliwa mwenyekiti wa kudumu wa bodi hiyo.

Dk Hussein ni mhadhiri mwandamizi katika masomo ya kibenki na ya fedha katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (Institute of Finance Management – IFM) cha Dar es Salaam. Dk Hussein ni msomi mwenye Digrii ya Uzamivu katika masomo ya kibenki na Digrii ya Uzamili katika masomo ya fedha. Aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya Wakaurugenzi wa NBC tangu mwaka 2010.

“Kwa mara nyingine tena, tunampongeza Profesa Assad kwa kuteuliwa kwake na kumtakia kila la kheri katika kazi hiyo. Tunamshukuru pia kwa utumishi wake uliotukuka katika kipindi chake kama mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya NBC. 

NBC itaendelea kushirikiana nae kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta ya fedha hapa nchini. Wakati huo huo, tunamtakia kila la kheri Dk Hussein katika nafasi yake mpya ya uenyekiti wa bodi ya NBC,” alisema Tibazarwa.

Profesa Assad aliteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mnamo mwezi Novemba 2014 baada ya kuitumikia NBC kama mwenyekiti wa bodi tangu mwaka 2006.

Harakati za kuhamasisha vijana zawafikia Vijana wa Mbozi

0
0
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mbozi Bw. Elisey Ngowi akifungu semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya. Kushoto ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
Vijana wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya wakisikiliza kwa makini mafunzo yaliyokua yakitolewa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa kulia akifafanua jambo walipotembelea mradi wa kikundi cha vijana cha Miranaco wanaomiliki duka la madawa muhimu katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya. Kushoto ni Afisa Utamaduni Wilaya ya Mbozi Bw. Godfrey Msokwa, wapili kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na wapili kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha Miranaco Bw. John Maige. (Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo)

MAMA MKULIMA ASHINDA MIL. 10/- ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM

0
0
Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao(kulia)akiandika namba ya Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa aliyeibuka mshindi wa Shilingi Milioni 10/- katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,wengine katika picha kutoka kushoto Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu na Meneja uhakiki wa mapato Vodacom Zakaria Kamweru.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na mshindi wa shilingi Milioni 10/- Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa,aliyeibuka na ushindi huo katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

BALOZI WA VIETNAM AMTEMBELEA WAZIRI MIGIRO OFISINI KWAKE JIJINI DAR LEO

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akiongea na Balozi wa Vietnam nchini Bw. Vothanh Nam wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Januari 22, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro na Balozi wa Vietnam nchini Bw. Vothanh Nam wakiwa ofisini kwa Waziri jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Januari 22, 2015). Balozi Nam alimtembelea Waziri Migiro ili kubadilishana mawazo.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati) na Balozi wa Vietnam nchini Bw. Vothanh Nam (kushoto) wakiwa ofisini kwa Waziri jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Januari 22, 2015). Kulia ni Ofisa Balozi wa Vietnam Bw. Mai Anh Thai ambaye aliongozana na Balozi Nam aliyemtembelea Waziri Migiro ili kubadilishana mawazo. Picha na Said Benjamin.

ISACA TANZANIA YATOA SEMINA KUHUSU USALAMA WA MITANDAO

0
0
 Makamu wa Rais wa Isaca Tanzania Chapter ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao, Dk. Jabir Bakari akitoa hotuba yake wakati akifungu semina kuhusu usalama wa mifumo ya kompyuta pamoja na ukaguzi wa mifumo hiyo kwa kuwakutanisha wataalumu na kujadiliana kuhusu ukuaji wa teknolojia na usalama.

Aidha Dk. Jabir alisema kuwa semina hiyo inawakutanisha wataalamu wa mifumo ya kompyuta kutoka ndani na nje ya nchi watakaojifunza na kuongeza utaalamu wa kulinda mifumo ya mitandao. 

Naye Mratibu wa Semina hiyo ambaye pia ni Rais wa Isaca Tanzania, alisema kuwa semina hiyo kwa ajili ya kuelezea wadau wa mitandao kuhusu mwelekeo wa teknolojia duniani na ukubwa wa tatizo katika wizi wa mitandao  'miaka ya nyuma kulikuwa na wizi wa kuvunja katika mabenki lakini siku hizi mbinu za wizi zimebadilika na wezi wanaiba kupitia mifumo ua mitandano hasa kompyuta pamoja na simu, kutoa elimu ya ajili ya mifumo ya kompyuta namna ya kuilinda na kuiendeleza.
Katibu wa Tanzania Chapter, Nemayani Kaduma (kulia)akiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina ya ya kimataifa kuhusu usalama wa mitandao wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Taasisi ya Isaca Tanzania Chapter, Dk. Jabiri Bakari (hayupo pichani) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA LEO.

0
0

 Ktibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Wanachama wa kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara mara baada ya kushiriki kupanda Migomba,katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.

 katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda Mgomba katika shamba la Kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga  katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.
 Mbunge wa Jimbo la Chaani,Mh.Ally Juma Haji a.k.a Chepe akizungumza na baadhi ya vijana kuhusiana mambo mbalimbali ikiwemo na kuwahimiza kupiga kura ya ndio kwa katiba inayopendekezwa.
 Baadhi ya Wananchi wanaoshiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mapema leo.Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.7 ina thamani ya shilingi milioni 26
 Katibu mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.7 yenye thamani ya shilingi milioni 26
Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini katika jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80 ukiendelea,Mradi huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini,jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80.Mradi huo huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Banda Maji mara baada ya kupokea taarifa ya kikundi cha ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga,pia kushiriki kazi ya kilimo cha Migomba na Mbogamboga,katika Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.

PICHA NA MICHUZI JR-KASKAZINI UNGUJA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Mh. Lowassa aomboleza kifo cha muasisi wa TANU Monduli

0
0
Waziri mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa mkono wa pole kwa waombolezaji katika Msiba wa aliekuwa muasisi na kiongozi wa kwanza wa Chama Cha TAA na baadaye TANU wilayani Monduli,Marehemu Mzee Lazaro Ole Ngoilenya Laizer aliyefariki juzi na kuzikwa leo Alhamis kijijini kwake Ngarash Monduli.Marehemu Mzee Lazaro Ole Ngoilenya Laizer ambaye ndiye alikuwa chachu kwa Mh. Lowassa na wanasiasa wengine wa Monduli kuingia katika siasa,amefariki akiwa na umri wa miaka 120,alioa wake 9 na kufanikiwa kupata watoto 53.
Waziri mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa mkono wa pole kwa wajane wa Marehemu.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mzee Lazaro ole Ngoilenya Laizer aliyefariki juzi na kuzikwa leo Alhamis kijijini kwake Ngarash Monduli.

BUNGE KUANZA VIKAO VYAKE JUMANNE TAREHE 27 JANUARI 2015

American and German Governments Partner with Tanzanian Government and Frankfurt Zoological Society to Save Elephants in the Selous

0
0
German Ambassador Egon Kochanke (second from left), Minister of Natural Resources & Tourism Lazaro Nyalandu (center), and U.S. Ambassador Mark Childress (right) talk with Tanzanian game scouts from the Selous Game Reserve at an equipment handover event in the Reserve on January 21, 2015.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images