Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110125 articles
Browse latest View live

NGO's YA APEC KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI DODOMA YAFUNGA MAFUZO KWA WAENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) MKOANI HUMO

$
0
0
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,SACP David Misime akiongea katika kufunga mafuzo kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Muwakilishi wa Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Dodoma, Bw. Erasto Kasugu akisoma risala kwa mgeni rasmi,wakati wa kufunga mafuzo kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi..
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la APEC  Bw. Respicius Timanywa akiongea jambo kwenye ufungaji wa mafunzo hayo

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Viongozi wa Chama cha Skauti wakutana na Wadhamini wa Chama

$
0
0
Viongozi wa chama cha skauti wakiwa pamoja na wadhamini wa chama hicho ambao ni Rais Mstaafu Mhe Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu,Mhe. Salim Ahmed Salim. Wengine pichani ni mbele ni Kamishina Mkuu Ndg Abdulkarim Shah, Mwenyekiti wa kamati ya Utendaji Balozi Kuhanga na Naibu Kamishina Mkuu Rashid K Mchatta.

CCM KUWACHUKULIA HATUA KALI WANAOSAMBAZA HABARI ZA UZUSHI HASA WANAOWANIA NAFASI YA URAIS.

back by popular demand: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

ZAIDI YA BILIONI 29 ZINAWASUBIRI WATEJA WA VODACOM KUPITIA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kualia)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya sita ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika leo,ambapo jumla ya wateja 947 wamejishindia muda wa maongezi na wateja watano wamejishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja kutoka kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika droo ya droo ya sita ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika leo, ambapo jumla ya wateja 947 wamejishindia muda wa maongezi na wateja watano wamejishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

MKUTANO MKUU WA BARAZA LA WATOTO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAANZA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
Watoto kutoka mikoa Mbalimbali ya Tanzania katika picha ya pamoja na Paul Ngusa (katikati)Msaidizi wa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ummy Jamaly (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rauhiya Ameir (wa kwanza kulia) Makamu Mwenyekiti, Jaqueline Namfua (wa pili kushoto) Afisa Habari UNICEF, Christopher Mushi (wa kwanza kushoto) Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Wizara Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika Mkutano huo.

SOMA HABARI KAMILI HAPA

MTOTO ZAINABU 'IKOTA' MHAMILA ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA

$
0
0
Mtoto Zainabu 'IKOTA' Mhamila (kulia) akimlisha keki mama yake mzazi Bi. Asha Kamnyanga wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika juzi nyumbani kwao Buguruni Rozana.
Zainabu 'Ikota' Mhamila 'Super D' akiwa katika pozi huku akiwa na keki yake.
Zainabu 'Ikota' Mhamila 'Super D' akiwa katika picha ya pamoja na rafiki zake siku ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa.

KAMPUNI ZINAZOWAJIBIKA KWA JAMII KUTAMBULIWA MACHI, 2015

$
0
0
Katibu wa Kamati ya Tathmini wa Taasisi ya Ushauri wa Biashara, Ernest Mwamwaja (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni zinazowajibika kwa jamii kutambuliwa Machi mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Shughuli za Maendeleo ya Jamii, Abraham Shempemba na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ushauri wa Biashara, Dickson Hyera.

NJIA ZA "PANYA" ZA SUKARI ZINAUA VIWANDA VYA NDANI - ZITTO KABWE

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC),Mh. Zitto Kabwe (wa tatu kulia) akizungumza wakati akiongoza kikao cha Kamati yake na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Bunge,Jijini Dar es salaam leo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) na  Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Bunge,Jijini Dar es salaam leo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC),imeitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya uchunguzi wa sukari kutoka nje inayoingizwa nchini kwa njia ya panya,kwani inaua viwanda vya sukari vilivyopo nchini.

Akizungumza na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Zitto Kabwe amesema TRA inatakiwa kufanya kazi katika kudhibiti mianya inayoisababishia mamlaka kukosa mapato.Amesema  katika agizo la kamati wameiagiza TRA katika ripoti za forodha kuweka misamaha ya kodi ili kuweza kujua ni misamaha mingapi inaingizwa katika ushuru wa forodha.

Kamati hiyo iliipongeza TRA kwa kurasimisha kazi za wasanii ambayo imeweza kulingizia Taifa Sh.Milioni 348 kwa mwaka jana hivyo wanawajibu wa kuendeleza ili kuweza kuondoa wizi wa kazi zao pamoja na kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ili wananchi waweze kupata tiketi kwa mfumo wa eletroniki kwa kuweza kuweka zawadi za kuwavutia na huduma hiyo.

Hata hivyo kamati imeiagiza wizara ya fedha ianze kutekeleza sheria mpya ya ongezeko la thamani (VAT) na TRA inawajibu wa kufatilia agizo hilo kwa waziri na kanuni zake za sheria hiyo inatakiwa kuwa tayari.

Zitto amesema makusanyo ya TRA yaendane na bajeti na ni lazima wakusanye zaidi ili kuweza kuweka malengo yao  ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto na kuweza kufikia malengo ya 2025.

YALE YALEEEEE.......

$
0
0

Kama ilivyo kawaida ya watu wa maeneo mengi hapa nchini,kwamba likitokea la kutoka basi huwa ni faida kwa watu wengine.Mchana wa leo katika Makutano ya barabara ya Nyerere rodi na Kawawa rodi,gari ndogo aina ya Toyota Hilux iliyokuwa imebeba Vioo ilipatwa na mkasa na kupelekea mzigo wa vioo hivyo kuanguka katikati ya barabara na kupasuka,hali iliyowapelekea vijana wanaofanya biashara za mikononi (maarufu wa machinga) katika eneo hilo kuingia barabarani na kuanza kujibebea mabaki ya vioo hivyo kama ionekanavyo pichani hapa.hali iliyopelekea magari mengine yaliyokuwa yakiitumia njia hiyo kuwakwepa vijana hao ili waendelee na kazi yao ya kujisevia vioo. 

Hali hiyo ilidumu kwa muda kidogo na kupelekea Askari wa usalama barabarani kuyaongoza magari kupita pembezoni mwa barabara hiyo ili kuwaacha vijana hao ambao hawakutana kusikia la muadhini wala la mnadi swala.
 Kazi ikiendelea.

Filamu: Pata Filamu ya Never Give Up kupitia Mtandao

$
0
0
" And in her smile I see something more beautiful than the stars " Fuatilia hii kupitia mtandao .......

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo NEVER GIVE UP au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii


Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

ETI HII IMEKAAJE??

$
0
0
Salaam Ankal na Timu nzima ya Globu ya Jamii

Nawasilisha picha mbili zilizopigwa kutoka Mazengo Street, Upanga (Chibuku, Faya),maana naona hawa Jamaa wa RAPID wanatupotosha na tukikosea trafiki wanatupiga faini. Tufanyeje?
kwa mfano,picha hii inaonyesha hakuna kuingia Morogoro Road Kuelekea Ubungo.Alama ya Barabarani inaelekeza magari yote yanayotoka Mazengo kwanza lazima yanyooshe kwenda Barabara ya Msimbazi na baadae kuingia Morogoro Road kufuata mshale inavyo onyesha hapo pichani,wakati ukielekea Msimbazi hakuna sehemu ya kuingia kushoto ili uje kutokea Morogoro Road.

Na kuna alama nyingine mbele kidogo na hapo inayoelekeza namna ya kuingia Mazengo Street kwenye barabara kuu ya Morogoro Road ambayo haieleweki vilevile (Sikuweza kuipiga picha).

Picha hii ya pili inaonyesha Alama ya kwenda Swahili Street huku mshale unaelekeza kwenda Mazengo Road, Sasa hiyo Swahili Street iko wapi huko Upanga? Na kama Mazengo Street imebadilishwa jina,imebadilishwa Lini?

Ni hayo tu Ankal kwa leo,Naomba Msaada tutani.

wanamichezo wakongwe wa dar es salaam wakumbuka wenzao waliotangulia mbele ya haki

ngoma azipendazo ankal

$
0
0

Bokelo Isenge - Tambola na mokili.

DAWASCO YATANGAZA KUKOSEKANA HUDUMA YA MAJI KWA SIKU MBILI JIJINI DAR

$
0
0
Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za Ijumaa na Jumamosi ya tarehe 23 na 24 Januari 2015, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (Cross-connection) ndani ya Mtambo wa Ruvu Chini, Bagamoyo. 

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe. 

Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.       

Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.

Au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja namba 022- 2194800   
Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na ofisi ya uhusiano, Dawasco - Makao Makuu.

BREAKING NYUZZZZ.....: KITUO CHA POLISI IKWIRIRI,RUFIJI CHAVAMIWA NA MAJAMBAZI,ASKARI WAWILI WAUWAWA

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii,inaeleza kuwa majambazi yamevamia kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua Askari wawili na kupora silaha (bunduki) zilizokuwepo kituoni hapo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo,huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar  aliyekatwa mapanga na Wp Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.

 Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika Tukio la uvamizi, kituo cha polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani

Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabom ya machozi na risasi 60 za smg.

tutaendelea kujuzana kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.

WAZIRI WA MAJI ATOA SIKU 90, KWA MKANDARASI ANAESAMBAZA BOMBA LA MAJI MRADI WA MLANDIZI

$
0
0
Waziri wa maji ,Jumanne Maghembe (wa kwanza kulia) akizungumza na wakandarasi wanaojenga bomba la maji la Mlandizi Kimara Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati alipotembelea miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na maji Taka (DAWASA), kwalengo la kupata tathimini ya mradi huo ulipofikia sasa.
Waziri wa maji Jumanne Mghembe (wa pili kulia) akiwa ameongozana na meneja mradi Pintu Dutta (watatu kulia) wakati akikagua maendeleo ya mradi wa kituo cha kusafisha maji cha ruvu juu .

DALADALA WAGOMA KUTOA HUDUMA JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Waendesha Daladala jijini Arusha,leo wamefanya mgomo wa kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo mbali mbali ya mji huo kwa kile kinachodaiwa kugomea kuanzishwa kwa route mpya wanayotakiwa kuianza hivi sasa. 

Wakazi wa maeneo mengi ya jiji hilo wanalazimika kutembea kwa miguu,huku wengine wenye uwezo kidogo wakitumia  usafiri wa bodaboda ili kuwahi katika shughuli zao za kuendelea kujitafutia chochote.Askari Polisi na migambo wamesambaa kona za njia zote jijini Arusha.

Route zenye mgogoro zaidi ni ile ya Kutoka Njiro na Moshono kuelekea mjin.

Ripota wetu ambane nae ni mhanga wa mgomo huo,anasema kuwa angalau hali ya hewa leo inaruhusu kutembea bila kuchoka na Bodaboda hazijazuiwa kufika katikati ya mji wa Arusha,hivyo zinasaidia usafirishaji.

Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji yaridhishwa na miradi ya maji ya Kibiti, Ikwiriri

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu (kushoto) akimuongoza Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi aliyeambatana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kuwasili ofisi za Mradi wa Maji Kibiti ulioko wilayani humo mkoani Pwani kabla ya kuukagua.Ukaguzi wa mradi huo ni sehemu ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara inayofanywa na wajumbe wa Kamati hiyo.
Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati Amina Makilagi akipanda ngazi za tanki la maji la mradi wa maji wa Kibiti wakati akikagua mradi huo, huku Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu na watendaji wengine wakishuhudia.

Viewing all 110125 articles
Browse latest View live




Latest Images