Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 711 | 712 | (Page 713) | 714 | 715 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Dereva aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.910 CYF aina ya Toyota Noah aliyetambulika kwa jina la Stanford Luenje (30) mkazi wa mbozi alifariki dunia baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka huko eneo la Mlowo Wilayani Mbozi.

  Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 01:30 huko eneo la mlowo, kata ya mlowo, tarafa ya vwawa, wilaya ya mbozi, mkoa wa mbeya katika barabara kuu ya mbeya/tunduma.

  Aidha katika ajali hiyo watu wawili waliofahamika kwa majina ya  1. Ndimyake Mwakisu (33) na 2. Elisha Mwashuya (30) wote wakazi wa mbozi walijeruhiwa na wamelazwa hospitali ya wilaya ya mbozi kwa matibabu. Chanzo cha ajali ni mwendo kasi. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya mbozi.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Barakael N. Masaki anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

  Imesainiwa na:
  [Barakael N. Masaki – ACP]
  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.


  0 0


  0 0

  Balozi wa Wahadzabe na Miss Singida Kanda ya Kati 2014/1,Doris Mollel (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati alipohudhuria kwenye hafla ya ufunguzi wa bweni jipya maalum kwa watoto wa jamiii ya hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilaya ya Mkarama mkoani Singida. Uzinduzi wa bweni hili ni matunda ya jitihada za Serikali ya wilaya hiyo na mkoa wa Singida kuwahamasisha watoto hao kuhudhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya Ndg Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk. Paseko Kone (Wa kwanza kushto).
  Mlezi wa watoto wa jamii ya Hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilayani Mkarama mkoani Singida akimpongeza Miss Singida Kanda ya Kati 2014/1,Doris Mollel baada ya kumteua kuwa ‘balozi wa elimu’ wa watoto wa jamii ya Hadzabe kwenye shule hiyo. Doris ambaye ni Miss Singida na Kanda ya Kati 2014/15 alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na mkuu wa Wilaya Ndg. Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk. Paseko Kone (mwenye suti nyeusi).
  Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel akikabidhi Blanketi kwa watoto wa jamii ya Hadzabe waliojengewa Bweni na Serikali ya Wilaya na Mkoa wa singida katika shule ya msingi Munguli Wilayani Mkarama ikiwa ni jitihada za Serikali kuwahamasisha kuduhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Akishuhudia tukio hilo ni Dk. Paseko Kone, Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.

  0 0

   Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, George Shumbusho, akikata utepe kutambulisha kadi ya “Faida EMV Debit Card” itakayochukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki ya Exim, David Lusala (kulia) na Afisa masoko wa benki hiyo, Noel Tuga.  Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
   Mkuu wa kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki ya Exim, David Lusala (kulia),akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutambulisha kadi ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Kushoto ni Mkuu wa Hazina wa benki hiyo, George Shumbusho. Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
  Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, George Shumbusho (kushoto), akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutambulisha kadi ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” iliyokua ikitumika hapo awali. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha kudhibiti majanga wa Benki hiyo, David Lusala. Kadi hiyo hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja kwa kutumia mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika.
   
  Katika jitihada za kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa wateja wake katika mazingira salama zaidia Benki ya Exim imetambulisha kadi mpya ya kimataifa ijulikanayo kama “Faida EMV Debit Card” kuchukua nafasi ya “Magnetic Stripe Faida Debit Card” zilizokua zikitumika hapo awali.

  Kadi hiyo mpya hutoa usalama wa hali ya juu kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ inayodadavua taarifa za mteja ikiwa na mfumo madhubuti wa kiusalama hivyo kutoruhusu unakili wa taarifa za mteja husika. Hii itasaidia wateja wa benki hiyo kutekeleza miamala yao katika mfumo ulio salama zaidi.  

  Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana,  Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho alisema kadi hiyo mpya ina usalama ulioimarishwa zaidi kutokana na uwepo wa ‘embedded chip’ na kufanyika kwa ukaguzi wa ziada wa namba ya siri.

  “Tunatambua hitaji la wateja wetu kuweza kufanya miamala yao kwa usalama zaidi. Kwa kutumia kadi hii mpya ya kimataifa kutoka Benki ya Exim, mteja anaweza kuwa na uhakika kwamba miamala yake inafanyika katika mazingira salama kabisa,” alisema Bw. Shumbusho.

  Aliongeza kuwa, Kadi hiyo mpya ya kimataifa inamuwezesha mteja kufanya miamala duniani kote katika mashine za ATM na POS zilizothibitishwa na MasterCard.

  “Kama Benki ya Exim, tunaamini kuwa ugunduzi ni maisha. Hivyo basi, tutaendelea kugundua teknolojia mpya zitakazoendana na kasi ya ukuaji wa utandawazi katika dunia hii ya sasa ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika usalama wa kimtandao.

  “Ni matumaini yetu kuwa wateja wetu watazifurahia zaidi kadi zao mpya za “Faida EMV Debit card,” alisema. 

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayoshuhulikia utafiti katika ufumbuzi wa matekeo makubwa na ya haraka Bw.Omari Issa kutoka Tanzania Bara wakati alipokuwa akitoa mada yake wakati wa semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akiwa Mwenyekiti wa Semina hiyo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifungua semina ya siku moja kuhusu matokeo makubwa na ya haraka katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuleta maendeleo nchini,ufunguzi huo ulifanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kuwashirikisha Viongzi wa ngazi za juu wa serikali ya Mapinduzi wakiwemo Mawaziri,Naibu Mawaziri,Makatibu Wakuu,Naibu Makatibu Wakuu na Watendaji wengine.


  0 0


  0 0

   Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

  Uongozi  wa Timu ya Soka ya Arsenal kutoka nchini Uingereza umezuru Tanzania kwa ajili kuhamasisha na kuendeleza soka hapa nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Uhusiano na Maendeleo wa timu  hiyo ,Sam Stone amesema kuwa Tanzania ni  nchi ya sita kwa ukubwa katika bara la Afrika hivyo watasaidia katika kukuza soka nchini.

  Amesema kesho watakuwa na mazungumzo na Rais wa Shirikisho la  Mpira wa Miguu nchini (TFF),Jamal Malizi juu ya uendeleza soka nchini.

  Amesema katika ziara hiyo wanatarajia kukutana na makampuni 20 kwa ajili ya masuala ya biashara katika kuongeza uwigo zaidi kati timu na wadau wengine katika nchi ya Tanzania .

  Kwa upande wa Meneja wa Uhusiano na Maendeleo wa timu ya Arsenal Daniel Willey amesema wataendelea kutafuta wadau zaidi na kuendeleza soka nchini kwani Tanzania ni nchi ambayo ni kubwa inaweza kwenda mbele katika mafanikio ya soka.
  Afisa Mtendani Mkuu wa Kampuni ya EAG Group,Iman Kajura (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akiutambulisha Uongozi  wa Timu ya Soka ya Arsenal kutoka nchini Uingereza,ulikuja Tanzania kwa ajili kuhamasisha na kuendeleza soka hapa nchini.Mkutnao huo umefanyika kwenye hoteli ya Southansun jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Maendeleo wa Timu ya Soka ya Arsenal,Sam Stone na katikati ni Meneja Mahusiano na Maendeleo wa timu hiyo,Daniel Willey.

  0 0

  Vikosi vya Jeshi la Ulinzi, Magereza, Polisi na wataalamu wengine wanaendelea na kazi ya kuthibiti mmomonyoko wa ardhi uliotokea hivi karibuni katika kijiji cha Msimbati, Mkoani Mtwara kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga alipotembelea eneo ambalo limeathirika na mmomonyoko wa ardhi uliotokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali
  Eneo la ardhi ambalo limemomonyoka na kuzama baharini.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (anayeelekeza) akishauriana na Meja Jenerali R. S. Laswai (wa pili kutoka kulia).
  Baadhi ya Wanajeshi wakiendelea na zoezi la kuthibiti mmomonyoko.

  0 0


  Na Bashir Yakub
  Wiki  iliyopita  niliandika  kuhusu  Asilimia kumi ambayo  serikali  za mitaa huwa  wanaidai  hasa  maeneo  ya  mijini baada  ya  wahusika  kuwa wameuziana nyumba au  kiwanja. Nikasema  wazi  kabisa  bila  kungata  meno  kuwa  hiyo  pesa iitwayo asilimia kumi au pesa nyingine yoyote   mtu  atakayolipa  serikali  za  mitaa eti  kwakuwa amenunua  au  ameuza   eneo  lake   ni rushwa. 
  Na  leo  nakumbusha na  kusisitiza  tena   kuwa  Watanzana wajue   ukitoa   pesa  ile   umetoa  rushwa  na huyo  kiongozi  wa  serikali   za   mitaa uliyempa amepokea rushwa  kwakuwa  malipo  hayo  hayatambuliwi  na hayaainishwi  na sheria  yoyote. 
  Lazima ifike   hatua  haya  mambo yaeleweke.   Pia  nimetahadharisha mara nyingi kuhusu  umakini unaponunua  kiwanja/nyumba  na kueleza baadhi ya mambo  ambayo  ukiyafanya utakuwa umefanya manunuzi salama na utakuwa umeepuka migogoro na hata mgogoro ukitokea wewe hautapoteza. Anayetaka kusoma  haya  yaliyopita aandike neno  MAKALA  SHERIA  kwenye google ataona makala  hizo. 
  Leo tena  naeleza uhalali kisheria wa serikali za mitaa kusimamia mikataba. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya

  Vijana wa Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Mbeya Vijijini wametakiwa kutokuwa na tafsiri hasi kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kuwa ni takrima inayotolewa na serikali kwa vijana hivyo kuchezea fedha hizo na kushindwa kurejesha mkopo watakaouomba kupitia mfuko huo.

  Hayo yamesemwa na Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wakati wa semina iliyotolewa kwa Vijana wa Mbeya Vijijini kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha, Ujuzi na Ujasiriamali jana Mkoani Mbeya.

  Bibi Riwa amesema kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unahudumia vijana wote nchini bila kuangalia itikadi za kisiasa ukiwa na lengo la kuwakomboa vijana na kuinua vipaji vya vijana nchi nzima.

  “Vijana ni taifa la leo na kesho likiwezeshwa taifa zima limewezeshwa, Wizara yenye dhamana na Vijana inalenga kuwafikia vijana wote nchini bila kuangalia itikadi za kisiasa kwani vijana wote ni wetu na tunatamani kuona vijana wanajiendeleza kufikia ndoto walizonazo” amesema Bibi Riwa.

  Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya Vijijini Bibi Upendo Sanga amesema kuwa ni bahati ya pekee kutembelewa na ugeni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivyo kuwaomba vijana wa Wilaya yake kuzingatia elimu watakayoipata na kusambaza elimu hiyo kwa vijana wengine wa Wilaya yake ambao hawakuweza kufika katika semina hiyo.

  Bibi Sanga ameiomba Wizara yenye dhamana na Vijana kuendeleza programu ya kuwaelimisha vijana mara kwa mara na kuwahamasisha vijana kujiunga katika vikundi kwani ni raisi kusaidia vijana wakiwa katika vikundi kuliko kumsaidia kijana mmojammoja.

  Akichangia wakati wa semina hiyo kijana Evans Bembeja kutoka Shirika la Efao linalojishughulisha na kilimo cha mbogamboga amesema kuwa vijana wengi hawaangalii mbele wamekua kwenye mwamko wa kisiasa wakiamini kuwa siasa ndio sehemu ya kupata pesa za haraka hivyo kuachana na fursa nyingine kama vile kilimo na ufugaji.
  Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini Bibi Upendo Sanga akifungu semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana katika Mkoa wa Mbeya. Waliokaa katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
  Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiwaelimisha vijana wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kuhusu mwongozo unaosimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Mkoa wa Mbeya.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Leo wananchi wa Zambia wanafanya Uchaguzi mdogo kumchagua Rais wa sita tangu wa nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1964. Uchaguzi huu unafanyika kufuatia kifo cha Rais Michael Chilufya Sata, kilichotokea tarehe 28 Oktoba 2014, mjini London Uingereza alikokwenda kwenye matibabu. Rais Sata aliingia madarakani Septemba 2011.

  Mshindi katika uchaguzi huu atatawala hadi 2016 ambapo utafanyika Uchaguzi Mkuu.

  Katika uchaguzi huu wagombea kutoka vyama vya siasa vipatavyo kumi na moja (11) wamejitokeza kushiriki kama ifuatavyo:

  Mhe. Edgar C. Lungu – Chama cha Patriotic Front (PF) –mpaka anapoingia kwenye kinyangányiro hiki ni Waziri wa Sheria na Waziri wa Ulinzi. Yeye anajaribu kutetea chama hiki tawala ili kimalizie kipindi kilichobaki.

  Bw. Hakainde Hichilema - Chama cha United Party for National Development (UPND) - ambaye anajaribu tena kwa mara ya nne, anachuana vikali na mgombea wa chama cha PF. 

  Dkt. Nevers S. Mumba - Chama cha Movement for Multi Party Democracy (MMD)- mgombea wa  chama hiki ana changamoto kubwa hasa baada ya wengi wa Wabunge wa chama chake kuamua kumuunga mkono mgombea wa chama cha UPND.

  Bw. Elias Chipimo (jnr) - National Restoration Party (NAREP) - ambaye anashiriki kwenye uchaguzi kwa mara ya pili sasa. 

  Dkt. Ludwig S. Sondashi - Forum for Democratic Alternatives (FDA) - anashiriki kwa mara ya kwanza. Mgombea ni Daktari ambae anasema anatengeneza dawa za ukimwi na ameahidi wapiga kura kutoa dawa yake hiyo bure endapo atachaguliwa.                         

  Bibi  Edith Z. Nawakwi - Forum For Democracy and Development (FDD) -  ni mgombea pekee mwanamke na mara yake ya tatu kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais.

  Bw. Tilyenji Kaunda - United National Independence Party (UNIP)- ni mtoto wa muasisi wa Chama hiki kilichoipatia Jamhuri ya Zambia uhuru wake kutoka kwa mkoloni, Mhe. Dkt Keneth David Kaunda. Tangu kiondolewe madarakani 1991, kimeendelea kushiriki kwenye chaguzi hizi bila ya mafanikio ya kurudi tena madarakani.

  Brig. Jen. (Rtd) Godfrey Miyanda - Heritage Party (HP) - anaingia kwenye kinyang’anyiro kwa mara ya  tatu.

  Bw. Daniel M. Pule - Christian Democratic Party (CDP)--- anagombea kwa mara ya kwanza. 

  Bw. Peter C. Sinkamba - Green Party- ni mgombea machachari  ambaye anasema akipewa madaraka haya ya juu atafanya bangi kuwa zao halali la biashara. Ana uhakika kuwa serikali itapata mapato makubwa kutoka kwenye bangi hivyo kuondoa tegemezi kwenye zao moja tu la shaba.

  Bw. Eric M. Chanda – Chama cha 4th Revolution - Chama hiki kinaingia kwenye uchaguzi wa Rais kwa mara ya kwanza.

  Ujumbe wa Waangalizi kutoka nchi wanachama wa SADC uliopo Lusaka, Zambia akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace J. Mujuma umetembelea vituo vya uchaguzi asubuhi hii na kukuta watu wamejipanga kwenye vituo hivyo tangu majira ya saa kumi na moja asubuhi. 

  Kituo cha kwanza ambacho kilitembelewa na ujumbe huu kilifunguliwa rasmi saa 12 asubuhi kukiwa na wahusika wote na kulingana na taratibu zilivyopangwa na Tume ya Uchaguzi wa Zambia na uchaguzi kuendelea kwa hali ya shwari.

   UBALOZI WA TANZANIA
  LUSAKA, ZAMBIA

  0 0

  Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Marekani na wizara.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) pamoja na wasaidizi wa balozi huyo, kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini. Balozi Childress alimtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

   Mfuasi wa CHADEMA,Bi.Fatma Hassan akikabidhi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na kujiunga na chama hicho,ambapo wanachama watano wa CHADEMA walirudisha kadi na kujiunga na CCM.
   Baadhi ya Wanachama wapya wakila kiapo
   Sehemu ya Umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Tunduni,Jimbo la Uzini,Mkoa wa Kusini Unguja
   Sehemu ya Umati wa watu waliofika kwenye mkutano wea hadhara uliofanyika katika kijiji cha  Tunduni,Jimbo la Uzini,Mkoa wa Kusini Unguja.PICHA NA MICHUZI JR-KUSINI UNGUJA-ZANZIBAR

  0 0

   Mkurugenzi wa Mahusiano ya kimaendeleo wa Klabu ya Arsenal Bw. Sam Stone (Kulia) akimkabidhi jezi ya timu hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu. Kushoto ni Bw. Daniel Willey, Meneja wa Mahusiano ya Kimaendeleo ya Arsenal. Maafisa hao wapo nchini kwa lengo la kukutana na wadau mbalimbali ili kufungua mahusiano ya kibiashara, katika mpango huo makocha wa timu hiyo na baadhi ya nyota waliowahi kuchezea timu hiyo watapata fursa kutembelea Tanzania. Klabu ya Arsenal ni kati ya klabu maarufu ulimwenguni ambayo inashiriki ligi maarufu duniani ya Barclyas.



  Mkurgenzu Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu (kushoto) akimkabidhi zawadi Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Bw Imani Kajura ambaye ni mwenyeji wa maafisa kutoka klabu ya Arsenal ambao wapo nchini kwa ajili ya kukutana na wadau mbalimbali kwa lengo kufungua mahusiano ya kibiashara.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Urusi Nchini Tanzania Alexander A.Ranikh aliyefika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiongea na Balozi wa Urusi Nchini Tanzania Mhe Alexander A.Ranikh aliyefika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi wa Urusi Nchini Tanzania Alexander A.Ranikh  baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa amemaliza muda wake wa kazi nchini, Picha na Ikulu Zanzibar

  0 0


  0 0

   Mmoja wa wakazi wa Unguja Ukuu-Kae Pwani akimuweka vizuri samaki aina ya Taachui baada ya kuandaliwa kwa ajili ya kuuzwa katika soko la samaki,ambapo kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo samaki huyo huuzwa jumla kati ya shilingi 40,000/= mpaka 50,000/=,na kwa kipande kipande huuzwa kati ya 25000/= mpaka 3000/=
   Mdau wa ITV,Jonh Chacha akishangaa samaki huyo aina ya Taachui,ambaye mkia wake wakati mwingine hutumika kama mjeredi wa kuchapia punda ama vinginevyo



  0 0

  Msururu wa wapiga kura katika kitongoji cha 
  Kanyama nje ya jiji la Lusaka leo asubuhi
                                             

   Leo wananchi wa Zambia wanafanya Uchaguzi mdogo kumchagua Rais wa sita tangu wa nchi hiyo tangu ipate uhuru mwaka 1964. Uchaguzi huu unafanyika kufuatia kifo cha Rais Michael Chilufya Sata, kilichotokea tarehe 28 Oktoba 2014, mjini London Uingereza alikokwenda kwenye matibabu. Rais Sata aliingia madarakani Septemba 2011.

  Mshindi katika uchaguzi huu atatawala hadi 2016 ambapo utafanyika Uchaguzi Mkuu. Katika uchaguzi huu wagombea kutoka vyama vya siasa vipatavyo kumi na moja (11) wamejitokeza kushiriki kama ifuatavyo:

  ·         Mhe. Edgar C. Lungu – Chama cha Patriotic Front (PF) –mpaka anapoingia kwenye kinyangányiro hiki ni Waziri wa Sheria na Waziri wa Ulinzi. Yeye anajaribu kutetea chama hiki tawala ili kimalizie kipindi kilichobaki.


  ·         Bw. Hakainde Hichilema - Chama cha United Party for National Development (UPND) - ambaye anajaribu tena kwa mara ya nne, anachuana vikali na mgombea wa chama cha PF.


  ·         Dkt. Nevers S. Mumba - Chama cha Movement for Multi Party Democracy (MMD)- mgombea wa  chama hiki ni  ana changamoto kubwa hasa baada ya wengi wa Wabunge wa chama chake kuamua kumuunga mkono mgombea wa chama cha UPND.


  ·         Bw. Elias Chipimo (jnr) - National Restoration Party (NAREP) - ambaye anashiriki kwenye uchaguzi kwa mara ya pili sasa.


  ·          Dkt. Ludwig S. Sondashi - Forum for Democratic Alternatives (FDA) - anashiriki kwa mara ya kwanza. Mgombea ni Daktari ambae anasema anatengeneza dawa za ukimwi na ameahidi wapiga kura kutoa dawa yake hiyo bure endapo atachaguliwa.                         


  ·         Bibi  Edith Z. Nawakwi - Forum For Democracy and Development (FDD) -  ni mgombea pekee mwanamke na mara yake ya tatu kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais.


  ·         Bw. Tilyenji Kaunda - United National Independence Party (UNIP)- ni mtoto wa muasisi wa Chama hiki kilichoipatia Jamhuri ya Zambia uhuru wake kutoka kwa mkoloni, Mhe. Dkt Keneth David Kaunda. Tangu kiondolewe madarakani 1991, kimeendelea kushiriki kwenye chaguzi hizi bila ya mafanikio ya kurudi tena madarakani.


  ·          Brig. Jen. (Rtd) Godfrey Miyanda - Heritage Party (HP) - anaingia kwenye kinyang’anyiro kwa mara ya  tatu.


  ·         Bw. Daniel M. Pule - Christian Democratic Party (CDP)--- anagombea kwa mara ya kwanza.


  ·         Bw. Peter C. Sinkamba - Green Party- ni mgombea machachari  ambaye anasema akipewa madaraka haya ya juu atafanya bangi kuwa zao halali la biashara. Ana uhakika kuwa serikali itapata mapato makubwa kutoka kwenye bangi hivyo kuondoa tegemezi kwenye zao moja tu la shaba.


  ·         Bw. Eric M. Chanda – Chama cha 4th Revolution - Chama hiki kinaingia kwenye uchaguzi wa Rais kwa mara ya kwanza.

    
  Ujumbe wa Waangalizi kutoka nchi wanachama wa SADC uliopo Lusaka, Zambia akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace J. Mujuma umetembelea vituo vya uchaguzi asubuhi hii na kukuta watu wamejipanga kwenye vituo hivyo tangu majira ya saa kumi na moja asubuhi.


  Kituo cha kwanza ambacho kilitembelewa na ujumbe huu kilifunguliwa rasmi saa 12 asubuhi kukiwa na wahusika wote na kulingana na taratibu zilivyopangwa na Tume ya Uchaguzi wa Zambia na uchaguzi kuendelea kwa hali ya shwari.

    
                               UBALOZI WA TANZANIA


                                  LUSAKA, ZAMBIA


  0 0

  TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA, MUSIC DEPARTMENT would like to invite you to a Cultural Music Concert on the 25th January (this coming Sunday). This is a once in a semister program, a wonderful opportunity to share and experience diversity in Culture. 
  KARIBUNI SANA..!

  0 0

  Mwaka huu 2015 ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya nchi. Ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM kwa nafasi hizo haijatolewa bado.


  Itakumbukwa Kamati Kuu iliyopita ya tarehe 13/01/2015, iliyoketi Kisiwandui Zanzibar ilipitisha ratiba ya shughuli za kawaida za Chama kwa mwaka 2015 na kupanga kushughulikia ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa CCM vikao vijavyo.


  Pamoja na kutotolewa kwa ratiba hiyo, bado zimekuwepo harakati nyingi za wanaotaka kuteuliwa na CCM kugombea nafasi mbalimbali hasa ya urais wa Jamhuri ya Muungano. Harakati hizo baadhi halali, nyingi haramu.



  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

older | 1 | .... | 711 | 712 | (Page 713) | 714 | 715 | .... | 3270 | newer