Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

mtuhumiwa sugu ujambazi katika mikoa ya mwanza,shinyanga na simiyu atiwa mbaroni

0
0
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP Valentino Mlowola akiwa na makamanda wenzake SACP Charles Mkumbo (Shinyanga) na  SACP Justus Kamugisha (Simiyu) wakati wakizungumza na waandishi wa habari kufuatia kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa wa ujambazi ambaye pia ni mfanyabiashara aitwaye Njile Samweli (46) marufu kwa “John” wa mjini Bariadi mkoani Simiyu, aliyekuwa akifanya matukio ya uhalifu katika Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida na Tabora.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,SACP Charles Mkumbo akionesha silaha iliyokuwa ikitumiwa katika harakati za matukio ya ujambazi katika kijiji cha Idukilo Kata ya Luhumbo Mwadui wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga.Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP Valentino Mlowola na kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,SACP Justus Kamugisha.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SCP Charles Mkumbo akionesha nguo ambazo zilikutwa kwa Mtuhumiwa kiongozi huyo wa genge la uhalifu ambazo zinasemekana ni za baadhi ya watu waliouawa wakiwemo majambazi aliokuwa akishirikiana nao ambao aliwauwa kwa maslahi yake.
Sehemu ya vitu vilivyokutwa kwa mtuhumiwa huyo.


Vijana jiwekeeni malengo kabla ya kukimbilia mikopo: Kongoye

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Christopher Ryoba Kangoye akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini kwake kabla ya kukutana na vijana wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za maisha na ujuzi jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa Dodoma.
Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada ya Uongozi kwa vijana wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Stadi za masiha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.
Vijana kutoka Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa wakifuatilia mada zilizokua zikitolewa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Stadi za masiha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA ASKOFU MKUU JIMBO LA DODOMA LEO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Sherehe ya Kumsimika Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya iliyofanyika leo Januari 18, 2015 katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya baada ya kusimikwa rasmi kwenye Sherehe iliyofanika leo Januari 18, 2015 katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu mbalimbali waliohudhuria sherehe ya kusimikwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya kwenye Sherehe iliyofanika leo Januari 18, 2015 katika Kanisa la Mt. Paulo wa Msalaba Dodoma. (Picha na OMR)

MKUTANO MKUU WA SABA WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA), WAFANYIKA JIJINI DAR

0
0
 Jaji Fredrick Wambali akitoa mada katika Mkutano wa saba wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA),uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.
 Wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

introducing new kid on the block Rossie Mpangala's hit single "Wivu" produced by Mujwahuki

MBUNGE FILIKUNJOMBE ATOA MSAADA WA ZAIDI YA TSH MILIONI 15 UKARABATI WA KANISA LA RC MADUNDA

0
0
Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akizungumza na  waumini wa kanisa la RC Madunda mara  baada ya  kusaidia kanisa  hilo kiasi cha Tsh milioni 15  za ukarabati wa kanisa na vinanda  viwili  vya kwaya kanisani  hapo
Viongozi  wa kanisa hilo wakimshangilia mbunge  huyo kwa  msaada wake
Waumini  wa kanisa   hilo  wakifurahia  misaada  ya mbunge  wao.bofya hapa kuona picha zaidi

WIMBI LA KUTEKWA EMAIL ADDRESS

0
0
Ndugu Wananchi,
Kuna matukio mengi ya kuteka anuani za watu na kuzitumia kwa maovu hasa kuombea misaada n.k.
Endapo janga hili litakukuta wasiliana nasi ili tuokoe anuani na jumbe zako pamoja na kuzuia maafa yatokanayo na uhalifu huu.Tujulishe mara moja kwa kutuma SMS kwenye simu ifuatayo:
+81-90-8498-9270
Huduma hii ni ya majaribio itatolewa
bure hadi tarehe 30/6/2015.

sent by T.J.Martin.

MWIGULU NCHEMBA ATIKISA MKOA WA MOROGORO

0
0
Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita Ndugu.Josephat Msukuma akizungumza na wananchi wa Morogoro Mjini wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu.
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara akiwasalimia wananchi wa Morogoro Mjini hii leo.
Comrade Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Morogoro Mjini,Mwigulu amesisitiza wananchi kusimamia Vizuri Mali za Umma hasa kwa Viongozi waliopewa dhamana,Pia amesisitiza wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la kupiga kura.
Mkutano Ukiendelea Morogoro Mjini.

Mwigulu Nchemba amehitimisha ziara yake ya Kutembelea Mkoa wa Morogoro wote hii leo kwa Kufanya Mkutano Mkubwa Morogoro Mjini.
Katika ziara yake Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu katibu Mkuu CCM Bara amesisitiza Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura,Amesisitiza Viongozi waliochaguliwa serikali za Mitaa kutumia dhamana waliyopewa kwa Maslahi ya Watanzania wote,Pia amesisitiza kuwa hakuna nafasi ya Kulea wezi wa Mali ya Umma,CCM hainamkataba na wezi wa mali ya Umma.Mtu anayeiba Fedha za umma,Mtu anayeiba Madawa Hospitalini,Mtu anayetumia madaraka yake Ovyo ni Mtu asiyevumilika,hastahili kujiuzuru tu,Ni lazima hatua za Kimahakama zifuatwe na afilisiwe.

Mwisho,Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa CCM imetekeleza Ilani yake vizuri sana na bado wanaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo,hivyo Watanzania waendelee kuwa na Imani na chama cha Mapinduzi.

Filamu: Pata Filamu ya Jenipher Kyaka FIGO kupitia Mtandao.

0
0
Filamu ya Figo
Kumsikiliza mzazi ni jambo la kawaida kwa kila mtoto, Lakini wakati mwengine lazima mtoto achague lipi jema, Lipi baya. Kijana Sila alijikuta kwenye pigo kubwa sana katika maisha yake nakujiuliza swali " Nani ni mzazi wangu kati yako na yule"Fuatilia kisa hiki....
Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo FIGO au nunua na iwe yako kupitia mtandao.
Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii
Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

introducing Dj Mix Version "Gere Rudmixx"

0
0
Shukrani kwa mapokezi mazito ya "East African Gere Remix" Salute kwa support yenu Upakuzi mkito na Requests Redioni. Kama Tulivyoahidi kuwapa Deejay Version aka "Rudmixx" Tarehe 19 Januari Bofya HAPA https://mkito.com/song/gere-rudmixx/12262 powered by @weusikampuni @vmgafrica @mkitodotcom www.vmgafrica.com @defxtro #supportafricanartists

INTRODUCING BRAND NEW SINGLE FROM BARAKAH DA PRINCE "SIACHANI NAWE"

TBL YAFADHILI UCHIMBAJI VISIMA BAGAMOYO

0
0
 Mhandisi wa Kampuni ya Al Water Well Drillers, Mohamed Aboud (katikati), akielekeza jambo kwa mmoja ya wafanyakazi wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi ya miradi ya uchimbaji wa visima vya maji unaofafadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B, wilayani Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa wiki. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia) akielekeza jambo kwa fundi alipokuwa akikagua ujenzi wa mradi wa uchimbaj wa visima vya maji katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B, wilayani Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa wiki.Miradi hiyo itagharimu sh. mil.51.7.

 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu, akijadiliana jambo na  na mkandarasi wa  ujenzi wa visima vya maji katika vijiji vya Nianjema C na Mianzini B,Mohamed Aboud, mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo, Pwani. TBL inafadhili miradi hiyo kwa gharama ya sh. mil. 51.7.

Mhandisi wa Kampuni ya Al Water Well Drillers, Mohamed Aboud (katikati), akielekeza jambo kwa mmoja ya wafanyakazi wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi ya miradi ya uchimbaji wa visima.

ngoma azipendazo ankal

0
0

Pepe Kalle "Roger Milla" original video

SERIKALI YA KENYA YAKUBALI KUYARUHUSU MAGARI YA ABIRIA NA WATALII KUTOKA TANZANIA.

0
0
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema serikali ya Kenya imekubali kuyaruhusu magari ya abiria na watalii kutoka Tanzania, kuingia ndani ya Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Awali, Serikali ya Kenya iliyazuia magari hayo kuingia uwanjani hapo huku ukiyatoza ushuru kwa yale yanayoingia, jambo ambalo lililalamikiwa na wafanyabiashara wa Tanzania.
Marufuku hiyo ya Kenya kwa magari ya Tanzania, ilidumu kwa zaidi ya wiki mbili, ambapo katika kusaka suluhu hiyo Nyalandu alikutana na wafanyabiashara hao jijini Arusha kisha kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya, Phyllis Kandie.
Katika mazungumzo yake na Kandie, Nyalandu alisema kwa sasa magari ya Tanzania yataendelea kuingia uwanjani hapo wakati ufumbuzi wa kudumu ukitafutwa.
Alisema kutakuwa na vikao vya kazi baaina ya Wizara ya Utalii ya Kenya na wizara yake, ambapo vitaanzia ngazi ya watandaji, watalaamu, makatibu wakuu na mawaziri.Alisema katika mikutano hiyo masuala mbalimbali kuhusiana na biashara ya utalii yatazungumzwa baina ya nchi hizo mbili.
Hata hivyo, alisema katika vikao hivyo suala la mpaka wa Bolongoja halitajaliwa wala kuwepo kwenye ajenda.
“Kwa sasa wafanyabiashara wetu wataingia Jomo Kenyatta kama ilivyokuwa awali. Tumezungumza na kupanga kuwa na vikao kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto zote kuhusiana na sekta ya utalii.“Niwahakikishie tu katika vikao hivyo maslahi ya pande zote yatazingatiwa, lakini suala la mpaka wa Bolongoja halitajadiliwa wala kuwemo kwenye ajenda za vikao vyetu.“Wataalamu na watendaji wa wizara yangu watakutana na wenzao jijini Arusha na maofisa wa Jumuia ya Afrika Mashariki watashiriki ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu,” alisema Nyalandu.
Kupatiwa ufumbuzi kwa tatizo hilo kumekuwa faraja kubwa kwa wafanyabiashara na wadau wa utalii katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, ambapo walipongeza jitihada za haraka zilizofanywa na Nyalandu.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wadau hao wa utalii walisema Nyalandu ameonyesha utendaji kazi kwa vitendo na kwamba, hilo linapaswa kuwa mfano kwa viongozi wengine.
Walisema waziri huyo baada ya kupata taarifa za wafanyabiashara wa Tanzania kuzuiwa kuingiza magari Jomo Kenyatta, aliwafuata kwenye maeneo yao na kuwasikiliza kero zinazowakabili kisha kufunga safari kukutana na waziri Kandie jijini Nairobi.
“Hawa ndio aina ya viongozi ambao Tanzania ya sasa na inayokuja inawahitaji, wanaposikia wananchi wana kero na wananyimwa haki ama kunyanyaswa wanakwenda kuwasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa haraka. “Kwa hili Waziri Nyalandu anastahili pongezi na viongozi wengine waige mfano huu, wangekuwa wengine wangeanza kuleta siasa na tatizo kuchukua muda mrefu kupata ufumbuzi,” alisema John Mlay, ambaye ni mmoja wa wafanyakazi kwenye kampuni za usafirishaji watalii.

Obi sets sights on Africa smartphone market; brand by former Apple CEO to launch in Tanzania in Q1 2015.

0
0
·         New venture led by former Apple CEO, former president of PepsiCo, and renowned tech investor John Sculley aims for rapid global expansion
·         Following its successful launch in India and the Middle East, Obi Mobiles plans substantial investments in to the Tanzania smartphone market

·         Signs on renowned regional IT distributor DESPEC as exclusive channel partner in Tanzania and other African countries


Dar es Salaam, Tanzania: 19 January, 2015 Obi Mobiles, the new smartphone brand co-founded by veteran marketer and former Apple CEO John Sculley, is preparing an ambitious launch in Tanzania and other countries in East Africa, and has signed on DESPEC, the leading IT distributor as its exclusive channel partner in the region. The firm is set to roll out a superior line-up of Obi devices suited to consumers in the region in Q1 2015, with an aim to capture 5% market share by the end of this year.


John Sculley is an internationally renowned marketing expert, entrepreneur and investor in high-tech startups. He was vice-president (1970–1977) and president of PepsiCo (1977–1983), until he became CEO of Apple in 1983. He held that position till 1993 and, under his management, annual sales at Apple increased from $800 million to $8 billion.


A new entrant in the consumer technology sector, Obi Mobiles is a venture of Sculley’s Toronto-based Investment and Acquisition Company, Inflexionpoint. It marked its global launch in India, followed by the Middle East markets in 2014. The brand, which aims to attract the growing segment of young and trendy smartphone users, confirmed that Tanzania is an important market in Obi’s rapid global expansion strategy.


John Sculley, co-founder and managing partner at Inflexionpoint, says: “Our vision is to use Obi’s success in each new market to create an international brand, especially targeted at the feature-rich and trendy smartphone segment. Having launched in India and the Middle East, with a better-than-anticipated response, has helped us set the pace for the Obi expansion blueprint, and now we are expanding our strategy of effective brand building and marketing for superior mobile devices in other regions.


“The African markets present a huge opportunity for new smartphone devices, with a growing population of technology- and fashion-savvy youth. Consumers today want the best feature-rich smartphone experience at desirable price points, without compromising on quality. There is also a growing trend of feature phone users moving towards smartphones. Our analysis has revealed that consumers today are more likely to switch brands as long as they have sufficient incentive. Obi is uniquely positioned to leverage all these changing market dynamics.”


Designed to capture the minds of the younger demographic, Obi devices are packed with style and superior features. The range includes mobile devices that run on the efficient Android Kit Kat platform, powered by multi-core processors, including an octa-core option, dual-SIM capabilities, large screen sizes and high quality camera options, all packaged in a robust and stylish exterior.


Amit Rupchandani, Managing Director for the Middle East and Africa region at Obi Mobiles, adds: “While the mobile industry is often associated with highly expensive products sold using technical jargon, at Obi Mobiles the belief is that it doesn't have to be this way. Obi is perfect for the growing number of mobile phone users in this region who desire the best smartphone experience without a huge financial investment.


“Added to that is our brand philosophy of ‘Whoever you are’. What it essentially means is that Obi doesn’t judge you, it lets you be you. In keeping with that, we have a broad range of quality products to suit the different personalities and preferences of smartphone users.


“We are charting out our entry in to the East Africa market currently, and aim to rapidly grow in the region by forging synergies with effective channel partners. Obi will continue to expand extensively through 2015, with Latin America and the former CIS region up on the list of priority markets.”


As a value-added reseller to Obi Mobiles for Tanzania, Kenya and other African markets, DESPEC will manage the distribution of Obi devices to all key retailer and independent retailer channels in these countries.


Farouk Jivani, CEO, DESPEC Africa, says: “DESPEC is excited to be appointed as the exclusive channel partner for Obi Mobiles in Tanzania and other East African markets. Obi has paid special attention to creating an image that resounds with the large section of young and aspirational smartphone users in Africa. Their entry in these markets will additionally be buoyed by trends such as increased mobile internet usage and penetration among target consumers. We look forward to working with Obi and establishing the brand as one to reckon with in the region.”



The Obi smartphones for the African markets will be unveiled in March in Tanzania followed by a phased roll-out across other markets in the region.


JAJI MUTUNGI AVIONYA VYAMA VYA SIASA VINAVYOENDEKEZA MIGOGORO

0
0
Hivi Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya Siasa. Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi hiki ukielekea katika uchaguzi Mkuu wa nchi.

Athari za migogoro hii ni nyingi, ikiwemo chama cha kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, kupoteza mvuto kwa jamii na wanachama wake, ukosefu wa amani na utulivu ndani ya chama na kupoteza sifa za usajili.
Hivi sasa mfumo wa demokrasi ya vyama vingi vya siasa una takribani miaka 23 tangu urejee tena mwaka 1992. Hivyo jamii inategemea kuwa mwanasiasa na vyama vya siasa kuonyesha ukomavu na busara katika kuokuongoza na kushiriki shughuli za chama.
Mojawapo ya ukomavu na ustarabu huo ni kuweka mifumo, kuongoza na kushiriki shughuli za chama katika namna ambayo itaepusha migogoro. 
Mojawapo ya Mambo ya kuzingatia ni chama kudhibiti tofauti za wanachama na baina ya viongozi kwa njia ya kidemokasia na utawala bora katika kuongoza na kushiriki shughuli za chama na kuheshimu na kufuata sheria, katiba na kanuni za chama.
Hivyo natumia nafasi hii kama ninavyotambulika na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa, kuvisihivyama vyote vya siasa, kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, katiba na kanuni zake. Pia kuwa mfano mzuri kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.

MBUNGE JAMESN MBATIA AWASHUKURU WANANCHI JIMBO LA VUNJO KUKIUNGA MKONO CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

0
0
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ghalani katika mji mdogo wa Himo jimbo a Vunjo alipokuwa akiwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kukipa ushindi chama chake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa ulimalizika hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza na wananchi katika jimbo la Vunjo,wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi kwa lengo la kuwashukuru kwa kuchagua wenyeviti wengi waliotokana na chama cha NCCR-Mageuzi,mkutano uliohutubiwa pia na Mbunge wa kuteuliwa na rais,James Mbatia.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ,Ndolakindo Kessy akizungumza katika  mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ghalani ,mji mdogo wa Himo ,mkutano uliokuwa na lengo la kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Vunjo kukipa chama hicho viti vingi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji.
Mmoja wa wakazi katika jimbo la Vunjo ,Elizabeth Mrema  akimkabidhi Mbunge wa kuteuliwa na rais ,Mh James Mbatia zawadi ya shati la Kitenge kwa niaba ya wakazi wa jimbo la Vunjo ,kuipeleka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu ,Joseph Waryoba.

Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Huyu na Yule...........Mahojiano na Dr na Mama Williams

0
0
Karibu kwenye mahojiano ya Dr na Mama Williams.
Waasisi wa AHEAD Inc. Taasisi ambayo iliasisiwa mwaka 1985 na inajishughulisha kubadili maisha ya wengi nchini Tanzania kupitia Elimu, Stadi za Maisha, Afya ya Mama na Mtoto na pia kuzisaidia jamii mbalimbali..
Wamezungumzia mengi kuhusu namna walivyofika Tanzania kwa mara ya kwanza 1974. Kilichowapeleka, walivyoamua kubaki huko mpaka sasa, shughuli za Taasisi yao na mengine mengi
Karibu
Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production
Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction@ gmail.com

HOJA YA HAJA: MSINGI WA MAKOSA KATIKA MCHAKATO WA KUTAFUTA NA KUPATA VIONGOZI WA KISIASA TANZANIA NA SULUHISHO LAKE

UFAHAMU MTANDAO WA MALEZI MAKUZI NA MAENDELEO YA WATOTO WADOGO TANZANIA (TECDEN)

0
0
unnamed
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi
Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania – TECDEN ni chombo kinachoundwa na mashirikia mbalimbali yanayofanya kazi za kuhudumia watoto wadogo Tanzania. 

Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2000 na kusajiliwa rasmi mwaka 2004. Makao makuu ya Mtandao huu yapo Jijini Dar es salaam. 

Hadi kufikia mwaka 2014 Mtandao huu una jumla ya mashirika wanachama wasiopungua 200 katika mikoa 14 ya Tanzania bara na Visiwani yanayotoa huduma kwa watoto wadogo Tanzania Lengo kuu la Mtandao ni kuboresha huduma za watoto wadogo Tanzania ili waweze kukua na kufikia utimilifu wao Shughuli Kuu za Mtandao ni pamoja na:- • Kufanya ushawishi na utetezi wa masuala yanayohusu uboreshaji wa huduma na kulinda haki za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na kushawishi maboresho ya sera na kufuatilia utekelezaji wa sheria na miongozo mbalimbali inayohusu uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.

Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images