Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 708 | 709 | (Page 710) | 711 | 712 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Kununua au Kuangalia Filamu Hii unaweza fuata kiunganishi hiki http://www.proinpromotions.co.tz
  To watch online or to buy this movie just click the cover photo or follow this link http://www.proinpromotions.co.tz

  0 0

  Ndugu Elly David Akitoa Mada Kuhusu Vijana kujituma na kufanya kazi kwa Bidii Kwa maendeleo ya taifa.Mtoa Mada huyo amesema kutokana na Ukosefu wa ajira hususani kwa vijana ni vyeme vijana kujituma na kuwa wabunifu na waweze kujiajiri kwa lengo la Kupambana katika Maisha.Katika Kongamano hilo la Vijana lililofanyika Jijini dar es salaam Liliwapa Fursa vijana kueleza Changamoto zinazowakabili na namna ya Kuzikabili.Kongamano hilo lililoandaliwa na Elly David mara baada ya ya kuona changamoto zinazowakabili vijana wa kitazania ili kuwapa fursa vijana kukutana kubadilishana mawazo Pamoja na Kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana wa Kitanzania/


  0 0
 • 01/16/15--10:58: bora liende


 • 0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhavile (kushoto) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), Dk Kitila Mkumbo wakikabidhiana nyaraka za makubaliano ya kuandaa midahalo kwa wagombea wa urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Katikati ni Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano, Dk Ayoub Rioba.
  Picha na Venance Nestory.    1. Katika nchi za kidemokrasia, midahalo ya wagombea imekuwa ni sehemu muhimu katika kufanikisha uchaguzi ulio huru, haki, wazi na amani. Midahalo hutoa fursa muhimu kwa wagombea kueleza falsafa, sera na mikakati yao ya kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi na nchi zao. Aidha, midahalo huwapa fursa ya kipekee wapiga kura na wananchi kwa ujumla katika kuwajua na kupima umahiri na weledi wagombea na vyama vyao. 
  Kwa sababu hii, midahalo imekuwa ni sehemu muhimu ya uchaguzi katika nchi zinazoamini na kuzingatia misingi ya demokrasia. Tafiti zinaonyesha kuwa midahalo ya wagombea urais ina nafasi ya kipekee katika kuwawezesha wapiga kura kuamua mgombea gani wamchague na kwamba midahalo imekuwa ni chombo muhimu katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura kwa wingi. 

  2. Kwa kuzingatia msingi ulioelezwa hapo juu, Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) na ITV/Radio One wamekubaliana kuandaa midahalo ya wagombea urais kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Tunaamini kwamba kwa kuandaa midahalo hii taasisi zetu hizi mbili zitakuwa zimetoa mchango muhimu wa kijamii katika kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka 20152 

  3. Utaratibu wa jumla wa midahalo hii utakuwa kama ifuatavyo: 

  a. Vyama vyote vitakavyoshiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na ambavyo vitasimamisha wagombea wa urais vitaalikwa kushiriki katika midahalo hii. 

  b. Wagombea wote watakaojitokeza kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wataalikwa kushiriki katika midahalo hii. 

  c. Midahalo itaanza kwa kushirikisha wagombea ndani ya vyama vyao pale ambapo chama kitakuwa na wagombea zaidi ya moja, na baadaye kati ya wagombea watakaokuwa wameteuliwa na vyama vyao. 

  4. Utaratibu kamili wa midahalo hii utatolewa baadaye. 

  5. Tunatoa wito na ombi maalumu kwa vyama vya siasa na wagombea wote watakaojitokeza kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kushiriki katika midahalo hii ili kuwapa wananchi fursa ya kuwajua; na wao kueleza falsafa, sera na mikakati yao na ya vyama vyao katika kukabiliana na matatizo yanayoikabili nchi yetu sasa na baadaye. 

  Prof. Kitila Mkumbo

  Mwenyekiti wa UDASA 

  Joyce Mhavile 
  Mkurugenzi Mtendaji ITV na RadioOne

  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana aliwasili Arusha kwa lengo la kufanya mazungumzo na makundi matatu ya chama cha SPLM ya Sudani ya Kusini, mashauriano hayo yalilenga kukamilisha makubaliano baina ya makundi hasimu. 

  Baada ya Mazungumzo Ndugu Kinana alisema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kukiunganisha chama cha SPLM katika siku chache zijazo 
  Kutoka kushoto ni Balozi David Kapya,Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa Mazungumzo Dk.John Samuel Malecela na Makamu Mwenyekiti wa mazungumzo Dk. Hassan Kibelloh mazungumzo hayo yalifanyika Ngurdoto Arusha. 
  Viongozi wa Makundi matatu kutoka chama cha SPLM kutoka Sudani ya Kusini wakiwa kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuunganisha chama chao cha SPLM. Hapa wakiwa  na viongozi wa Tanzania wanaosaidia kumaliza tofauti na yakiwa yanasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.

  ======  ======  ===== =======
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kuwa Tanzania imekubali kuwa msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa ndani ya chama tawala cha Sudan Kusini cha Sudanese People’s Liberation  Movement (SPLM), mgogoro ambao ulisababisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

  Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kuwa usuluhishi huo utakuwa wa kichama na Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kitaongoza usuluhishi huo katika mazungumzo yatakayofanyika Arusha na kuwa jitihada hizo za Tanzania hazitaingilia mazungumzo ya kujaribu kusimamisha mapigano nchini humo yanayoendelea huko Addis Ababa, Ethiopia.

  Rais Kikwete alisema kuwa ulikuwa uongozi wa SPLM na hasa Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Salva Kiir ambao wameiomba Tanzania kusaidia jitihada za kisiasa za kupatanisha pande ambazo zinavutana na kutofautiana ndani ya SPLM wakiamini kuwa mapatano ndani ya chama yatafanikisha kumaliza mgogoro wa kisiasa katika Serikali ya nchi hiyo ambayo  imegawanyika na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

  Rais Kikwete alitangaza jitihada hizo za upatanishi za Tanzania wakati alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi na kupitia kwao Taifa kwenye Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kilele cha Wiki ya Vijana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

  “Ni fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika Kusini nao wako huru na tumetoa mchango wetu.  Ni jambo la faraja kubwa kwamba nchi yetu imeweza kupatia hifadhi ndugu zetu wa nchi jirani na hata mbali wakati maisha yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya kukosekana kwa amani ama kukimbia mateso ya uongozi wa kidikteta. Ndugu zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Comoro wanaujua ukweli huo. Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa Dikteta Idd Amin na Comoro tulisaidia kuunganisha nchi yao tena.”.

  0 0

  Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Faundation, Sitti Mtemvu (wa tatu kulia) akimkabidhi vifaa vya kuhifadhia taka Mbunge wa Jimbo la Ilala  Mhe.  Mussa Azzan Zungu (kushoto), kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Ilala Dar es Salam.  kuanzia kushoto  nyuma ya mbunge ni Diwani wa kata ya Kinyerezi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Leah Mgitu katikati ni mama mzazi wa Sitt Mariam Mtemvu, wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala kupitia Chama cha Mapinduzi  Edson Fungo na anae fatia ni  Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Mkoa Ilala
  Mbunge wa Jimbo la Ilala  Mhe Mussa Azzan Zungu akiongea na Waandishi wa Habari ( pichani hawapo)  mara baada ya kupokea  vifaa mbalimbali  vya kuhifadhia taka na Sabuni.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The  Sun Tanzania  Bi. Vicky Ntetema (kulia) , akifafanua jambo wakati Mwenyekiti huyo alipotembelea kituo hicho
   Afisa utetezi  Bw. Kondo Seif (wa kwanza kushoto)  akitolea malezo ya ukosefu wa rangi asili mwilini ambayo huathiri ngozi, macho na nywele na kukosekana kwa  melani mwilini, akiseme miongoni mwa athari zake ni wepesi wa kuungua na jua unapotembea juani na ufanyapo kazi juani.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The  Sun Tanzania  Vicky Ntetema (kulia) akimuonyesha   Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation,  Sitti Mtemvu (kushoto)  Picha ya mtoto  alie tekwa akiwa mgongoni mwa mama yake. Wa pili  kushoto ni Mama mzazi  wa Sitti.


  0 0

  Dear Salseros, we are back with full force and great news;


  Tuesdays @ Samaki Samaki Masaki! Starting from next week welcome to our new addition:
  Kizomba class at 7pm
  Social dance from 8pm (We will mix it up but we will emphasize Kizomba music) 

  Thursdays @The Terrace Slipway. From today, the restaurant will pay your salsa class if dining between 6 and 8. Book in advance  by calling Michelis on 0659608507
  Salsa class at 8:30pm
  Social dance from 9:30pm 

  30th-31st January Salsa-Tango Weekender @ Melia Zanzibar!!!
  We have put a very special package with parties, classes, sun, beach and international teacher for you!
  Have a look...

  Friday:  Tapas, Salsa class, Party and Show at Taperias in Stone Town from 8pm to 1am (Drinks not included) We have invited our friends from Cuba and the salsa community that live in Zanzibar. Transport to Melia and Room included. (Double occupancy) 

  Saturday: Lunch time wine tasting and show. All workshops by the swimming pool from 4:30 Tango, Kizomba, Bachata. We have International teachers to get you the best and we will cater for different levels to make sure you advance in your learning. 
  At night a Latino Party at this beautiful hotel,salsa  class, show and drinks. (Yes that is right all drinks included!)  Room full board included.

  Sunday: swimming pool chill out (Breakfast and lunch included)
  Price: 450$

  Dar-Zanzi Boat/flight is not included but we are waiting to hear for a group discount so book asap to know numbers. 

  This is going to be epic! Are you going to miss?

  0 0

   Mkurugenzi wa Mradi wa Jengo la Tatu la Abiria(Terminal III), Mhandisi Mohammed Milanga(mwenye suti), akiwaeleza wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, namna ya mradi unavyoendelea, waliotembelea Mradi huo leo asubuhi kuona maendeleo ya Ujenzi wake. Wa kwanza kushoto ni  Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi,Bw. Biseko Chiganga na kushoto kwa Chiganga ni Afisa Usafirishaji,Bw. Said Marusu.

   Mkurugenzi wa Mradi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III), Mhandisi Mohammed Milanga, akiwaeleza wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, utekelezaji wa ujenzi wa jengo hilo, waliotembelea sehemu unapotekelezwa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria leo asubuhi.
   Kaimu Meneja wa Kituo cha Hali ya Hewa Tanzania katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA),  John Mayunga, akiwapa maelezo wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi juu ya namna Kompyuta maalum inayotoa taarifa za hali ya inavyofanya kazi leo asubuhi, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho kuona namna ambavyo Kituo hicho kinavyotoa taarifa kwa marubani na kwa sekta ya usafiri wa Anga.
   Kaimu Meneja wa Kituo cha Hali ya Hewa Tanzania katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA),  John Mayunga, akiwapa maelezo wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi juu ya namna Kompyuta zinazotumika kwa ajili ya utabiri wa hali ya hewa zinavyofanya kazi leo asubuhi, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho. Wa kwanza kutoka kushoto ni  Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Said Marusu na wa kutoka kulia ni Afisa Usafirishaji, Bw. Biseko Chiganga.
  Kaimu Meneja wa Kituo cha Hali ya Hewa Tanzania katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA),  John Mayunga, akiwapa maelezo wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi juu ya namna Mtambo wa kisasa wa kuchambua data za hali ya hewa(computer cluster) inavyofanya kazi leo asubuhi, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho kuona namna ambavyo Kituo hicho kinavyotoa taarifa kwa marubani. 
  Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi

  0 0

  Hii ndio video mpya ya Lady Jaydee aliyomshirikisha Dabo inayoitwa "Forever". Video ya wimbo huo imefanywa na muongozaji mkongwe Adam Juma wa Next Level, na imeshootiwa on location ndani ya jiji la Johannesburg, South Africa. Wimbo umetayarishwa na producer mahiri Man Water wa Combination Sounds.
   Instagram: @jidejaydee @dabomtanzania
  Twitter: @jidejaydee @dabomtanzania
  Facebook: @ladyjaydee

  0 0

  Kilio cha watanzania hususani wakazi wa jiji la Dar ni kero ya upatikaji Majisafi na Salama kwa matumizi mbalimbali. Kumekuwa na sababu nyingi zinazochangia wananchi kutopata Maji hayo ikiwemo sababu ya uharibifu wa Miundombinu kwa wananchi wasiokuwa waaminifu kwa kukata mabomba na kujiunganishia Maji kiholela.

  Kiwango cha Maji kinachopotea kwa mujibu wa DAWASCO ni kwa asilimia 54 ambapo kiwango hicho ni kikubwa zaidi kutoka kile cha kimataifa cha asilimia 16 kinachotakiwa.

  Ofisa uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro (pichani) akiongea na waandishi mapema wiki hii alibainisha kuwa shirika limejipanga kwamba ifikapo 2020 kiwango cha Maji kinachopotea kiwe hakitozidi asilimia 25 ili kuwawezesha wananchi wengine kupata huduma hiyo.


  “ipo mikakati mingi na mizuri ya kuhakikisha maji hayapotei ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa viongozi wa wananchi tukianzia kwenye ngazi ya Madiwani na watendaji wa serikali za mitaa ili waweze kuwaelimisha wananchi juu ya udhibiti upotevu wa Maji” alisema Lyaro.


  Alisema 2015/2016 imeweka mikakati madhubuti na pia imejipanga kuhakikisha wizi wa maji unapungua ili kurudisha huduma hiyo kwa wananchi ambao wameikosa kutokana na hujuma ya wananchi wachache.

  “Hivyo basi kutokana na kwamba tayari tumewabaini watu wanaofanya vitendo hivyo mwaka huu tumejipanga kuingia mtaani zaidi na kuhakikisha tunazungukia maeneo yote na tunapogundua kuwepo kwa tatizo hilo tunawachukulia hatua za kisheria” aliongeza Lyaro.

  Wito kwa wananchi ni kushirikiana na DAWASCO katika kutoa taarifa za mara kwa mara pindi uhujumu wa miundo mbinu ya Maji na wizi wa Maji unapofanyika ili kujenga jamii yenye upatikanaji wa huduma hii kwa usawa na haki kwani maji ni Uhai.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) akijumuika na Waislamu na Viongozi katika Kumswalia aliyekuwa Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman katika Msikiti wa Ijumaa Mgenihaji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Marehemu alifariki jana Nyumbani kwake Amani Mjini Unguja .
  Wananchi na Waislamu wakilibeba Jeneeza la Marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman aliyekuwa Mwenyekitiwa Wazee wa CCM na kuzikwa lao kijijini kwako Mgenihaji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katika) akijumuika na Waislamu na Viongozi katika Maziko ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman aliyezikwa leo kijijini kwao Mgenihaji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitia udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman aliyezikwa leo kijijini kwao Mgenihaji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Ikulu,Zanzibar]

  0 0

   Mwenyekiti wa Chuo cha Karate nchini Tanzania,Willy Ringo ameyataka mashirika na makampuni nchini kuunga mkono mchezo wa Karate ili kufika mbali zaidi ulimweguni.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam,Rwezaula ameitaka Serikali pamoja na Makampuni yeyote  kuusaidia mchezo huo wa Karate,pia ameitaka Serikali kuacha kudhamini michezo mingine kama mpira wa miguu na mashindano ya urembo.

  Kwa upande wake, Bingwa wa Dunia katika mchezo wa Karate, Rutashobya Ringo amewataka Watanzania kuwa na nidhamu pamoja na kumuamini Mungu katika mchezo wowote ili kujihakikishia ushindi.
   Mwenyekiti Chuo cha Karate Tanzania Willy Ringo Rwezaula akionesha mmoja cheti alichokipata baada ya kushinda moja ya mashindano nje ya nchi ndugu Rutashobya Ringo.
   Rutashobya Ringo akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuonesha vyeti vyake pamoja na kombebaada ya kushinda nchini Urusi. Pia ameeleza kuwa anakwenda kushiriki olympic nchini Brazil kwenye mshindano ya Karate.
   Bwana Dormidontov Vadim ambaye ni mwalimu wa mchezo wa Karate nchini Urusi akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani).

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Tunasikitika kutangaza kifo cha ghafla cha  dada yetu mpendwa Leticia Mattei Rwechungura kilichotokea hapa Ujerumani tarehe 06.01.2015.Mazishi yatafanyika hapa Ujerumani Königswinter, karibu na mji wa Bonn tarehe 24.01.2015. Misa itaanza saa tano asubuhi (11:00 a.m.), katika Kanisa la St. Michael Niederdollendorf, Petersbergerstr. 14, 53639 Königswinter.

  Dada Leticia Mattei alikuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko South Sudan (UNMIS) - United Nations Mission in Südan, Eastern Equatoria State of Torit-Sudan. Aliugua muda mfupi na kufariki dunia katika hospitali iliyoko mjini Bonn hapa Ujerumani. 

  Watanzania wote walioko hapa Ujerumani, nyumbani Tanzania na ulimwenguni kote wameshtushwa na kifo hiki cha ghafla cha kuondokewa na mama yetu na dada yetu mpenzi Leticia Mattei. Tutamkumbuka daima kwa kazi kubwa alizoifanyia nchi yetu ya Tanzania, bara la Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Mungu amlaze mahali pema Peponi - Amin!
  Kwa yeyote atakayependa kutoa sanda yake, tunaomba michango itumwe moja kwa moja kwa mtoto wa marehemu:

  Diana Kajuna
  IBAN: DE76 3806 0186 5501 3030 13
  BIC: GENODED1BRS
  Kreditinstitut: Volksbank Bonn Rhein-Sieg eG

  Tunaomba sana ili tuweze kutekeleza mipango hii vizuri ya kumsindikiza dada yetu kwa heshima zote, wale wanaopenda kuhudhuria mazishi haya wawasiliane na mratibu wa shughuli hizi Nd. Majura, ili tupate orodha kamili ya wale wanaokuja ili itusaidie kuandaa mambo mengi ya muhimu. Kwa wale watakaopenda kupata malazi (ya hoteli), kadhalika tunaomba wawasiliane na Dr. Isack Majura kuanzia sasa kupitia:

  Tel. +49 173 7089513
  e-Mail: IMajura@aol.com
  Germany

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini Sudan jana amtembelea moja ya miradi mikubwa ya kuzalisha umeme kwa kutumia mabwawa ambao unaendeshwa na Kampuni ya Merowe Dam Electricity Company. 
  Mradi huu ambao uko Kaskazini mwa Nchi ya Sudan umejengwa kwa gharama ya USD 2.0 milioni ambapo Serikali ya Sudan imechangia 30% na zilizobaki ilikuwa misaada na mikopo kutoka kwa wafadhili
  Mradi umejengwa kando kando ya Mto Nile na una uwezo wa kuzalisha 1,250 megawati unachangia 60% hadi 70% ya mahitaji ya nishati ya umeme nchini Sudan. Mkurugenzi Mkuu wa Merowe Dam Electricity Company, Bw. Mahgoub Eisa Khalil amemtembeza Waziri na Ujumbe wake sehemu mbalimbali za mradi kama inavyoonekana katika picha zifuatazo:

   Prof. Mwandosya, (wa pili mbele) ,na ujumbe wake, wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Ashraf Mustafa,kuhusu usimamizi,udhibiti,na uendeshaji wa mitambo ya kuzalisha umeme.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya ( wa sita toka kushoto) na ujumbe wake wakiwa na Uongozi wa Bwawa la Umeme la Merowe wakiwa mbele ya Kitoleo cha Maji(Spillway) Wengine kutoka kushoto ni: Ngusa Izengo,Katibu wa Waziri;David Mziray kutoka Sumatra;Grace Nsanya;kutoka Wizara ya Maji;Wallace Chiwawa,TCAA;Hassan Amin Mohammed Ahmed Omer,Mkurugenzi wa Usalama wa Bwawa;Ashraf Mustafa,Meneja wa Uendeshaji;Mahgoub Eisa Khalil,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Umeme,Merowe;Felix Ngamlagosi,Mkurugenzi Mkuu,EWURA;Mhandisi Mustafa Hussein,Afisa Mwandamizi,Wizara ya Maji na Umeme,Sudan;Meneja wa Kituo; na Clemence Kichao kutoka TCRA.
  Prof.Mwandosya alipata nafasi ya kuongea na Waandishi wa Habari wa Sudan walioongozana na ujumbe wake huko Merowe,Sudan,akiwa mbele ya moja ya Piramidi za Merowe.Piramidi za Merowe zilijengwa zaidi ya miaka 7000 Kabla ya Ukristo,na ni zamani zaidi kuliko zile za Misri.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Januari 16, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea Iliyofanya Tathmini ya Utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam
  Rais Kikwete amewashukuru wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea iliyofanya tathmini ya utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
  Rais Kikwete amewashukuru kwa kazi nzuri wajumbe hao saba wa Kamati hiyo ya BRN Independent Review Panel ikiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana, Mheshimiwa Festus Mogae. Wajumbe 
  Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. James Adams, aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Bwana Tony Blair ya Uingereza Lord Mandelson, Gavana wa Benki Kuu ya Botswana Bi. Linah Mohohlo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya ONE Bi. Sipho Moyo. 
  Wengine ni Bwana Knut Kjaer kutoka Norway na Bwana Nkosana Moyo. 

  Wajumbe hao wamekutana kwa siku mbili kuanzisha  Alhamisi, Januari 15, 2015 mjini Dar es Salaam ambako wametathmini mwaka wa kwanza wa utendaji wa BRN baada ya kuwa wamepokea maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Presidential Delivery Bureau (PDB), mawaziri sita ambao wanaongoza sekta ambazo ziko katika BRN kwa sasa na timu maalum ya Kampuni ya PWC ambayo ilifanya ukaguzi matokeo ya utendaji ya mwaka wa kwanza wa BRN. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 16 Januari,2015
   Rais Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu  ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN Independent Review Panel) linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Mheshimiwa Dkt. Festus Mogae ( aliyekaa wa kwanza kulia kwa Rais Kikwete) huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
   Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Results Now kwa Rais Mstaafu wa Botswana Mheshimiwa Dkt. Festus Mogae aliyeongoza jopo maalum la kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
    Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Result Now kwa Dkt. Sipho Moyo, Mkurugenzi Mtendaji wa ONE wa Kanda ya Afrika aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa jopo la kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa. Rais Kikwete aliwakabidhi tuzo hizo huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
   Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi Tuzo Maalum ya Vision 2025 Big Results Now kwa Bwana James Adams, Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
  Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN Independent Review Panel). Kulia kwa Mheshimiwa Rais Kikwete ni Rais Mstaafu wa Botswana Dkt. Festus Mogae akifuatiwa na Bwana James Adams (Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia), aliyesimama wa kwanza kushoto ni Bibi Linah Mohohlo (Gavana wa Benki Kuu ya Botswana) na wa kwanza kulia ni Dkt. Sipho Moyo (Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika, ONE. Waliosimama mstari wa nyuma (kulia kwenda kushoto) Dkt. Nkosana Moyo (Mwanzilishi wa Mandela Institute for Development Studies) akifuatiwa na Lord Peter Mandelson (Mwenyekiti, Global Counsel ‘Uingereza’), anayefuata ni Bwana Knut Kjaer, (Mwenyekiti, Trident Asset Management, ‘Norway’) PICHA NA JOHN  LUKUWI 

  0 0

  The Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Hon, Bernard K. Membe (L) is in the joint press conference with Russian Foreign Minister, Hon. Sergey Lavrov in Moscow today.
  ==================================
  Today the governments of Tanzania and Russia have jointly agreed to speed up the process of establishing Tanzanian - Russian Intergovernmental Commission on Trade, Investment and Economic Cooperation to be signed during the first quarter of 2015.
  This was announced during the meeting between Hon. Bernard Membe, Tanzanian Minister for Foreign Affairs and International Cooperation and his Russian counterpart H.E. Sergey Lavrov in Moscow.
  The commission aiming at expanding trade and investment between the two countries is expected to boost trade which at the moment is at the minimum.
  "Although the volume of trade between our two countries has increased to reach 52 million USD for Tanzania and 60 million USD for Russia, it is not enough. We can do better" said Minister Membe.
  On his part, Minister Lavrov said the last bilateral investment forum between the two countries was held in 2009. The Commission will provide the needed platform for the countries to conduct regular forums which in turn will increase trade and investment opportunities.
  The commission will also assist in promoting the fast-growing energy sector in Tanzania whereby a number of Russian Companies have already expressed their interest investing in it.
  Other areas that will benefit through the establishment of this commission are tourism and education sectors whereby strategies to attract more Russian tourists to Tanzania and to increase number of Tanzanian students in Russia will be implemented respectively.
  The two Ministers also agreed to strengthen the Military Technical Cooperation between their countries due to the crucial role they both play in conflict resolution and peace building in Africa.
  On peace building aspect, Hon. Membe thanked Russian Government for its continued support and assistance in resolution of conflicts in Somali, DRC and now South Sudan.
  In turn, Minister Lavrov commended Tanzania for her unwavering historical role in promoting and sustaining peace in DRC, South Sudan and other areas in Africa.
  In his response, Hon. Membe who is in Moscow following an invitation of his counterpart, urged Russia to stay on course in promoting Africa's development agenda.
  "Time has now come for AU to implement its decision to open an office in Moscow to allow continuous discussions on this agenda. It is our hope that your government will facilitate the process for our mutual benefit" said Minister Membe.
  The two ministers also agreed to take their countries bilateral relations to greater heights by promoting culture of both countries and people to people relations.
  While in Moscow, Hon. Membe also had an opportunity to brief African Ambassadors and diplomats based in Moscow on the on-going peace processes in DRC and South Sudan.
  Minister Membe's two-days official visit in Moscow will conclude with the meeting with Tanzanians students and professionals from Moscow and surrounding areas.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe January Makamba akisaini kitabu cha Mazungumzo na January Makamba kabla ya kumpa nakala Waziri wa Sheria na katiba Dkt Asha-Rose Migiro jijini Dar es salaam
   Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe January Makamba baada ya kumpatia kitabu cha "Mazungumzo na January Makamba" kabla ya kumpa nakala Waziri wa Sheria na katiba Dkt Asha-Rose Migiro jijini Dar es salaam.   0 0


  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Kamani (Mb) (mwenye miwani), akiwa katika zoezi la kuteketeza nyavu haramu alipotembelea mwalo wa Kasanga katika Mkoa wa Rukwa.

  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Kamani (Mb) (mwenye miwani), akwasaidia wavuvi kukarabari mtumbwi wao tayari kwa kazi ya uvuvi alipotembelea mwalo wa Kasanga mkoani Rukwa.

  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Kamani (Mb) mwenye miwani, alipomtembelea mfugaji Ndugu. Kisinza (mwenye koti la bluu) katika Wilaya ya Nkasi ambaye ameanza ufugaji wa kisasa na kufuga mifugo bora yenye tija. Ng’ombe mmoja anafikisha wastani wa kilo 700 katika kipindi cha miaka miwili.(Picha na Mwakipesile)

  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii Dar

  Viongozi wa dini za kiislaam na kikristo wamesema dini ni za unyenyekevu na sio za kufanya maovu,ikitokea mtu mmoja katika imani anafanya maovu ni lazima akemewe ndani ya imani yake kwanza.

  Wameyasema hayo leo katika kongamano la kujadili madhara ya misimamo mikali ya imani za kidini (Tafkiri) katika jamii na taifa lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa kufungua kongamano hilo Katibu wa Taasisi za Kiislaam Wanazuoni,Sheikh Khamis Mataka amesema mambo yanayoendelea Afrika Magharibi na duniani kote wanatumia kufanya maovu kwa kutumia mgongo wa dini wakati maandiko ya mungu hayasemi hayo

  Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Bukhary Islamic Foundation,Sheikh Khalifa Khamis amesema sasa umefika wakati wa kukemea maovu kwa wanaotumia mgongo wa dini kufanya hivyo.

  Kwa upande wa Askofu wa Kanisa la EGS,Dk.Phirbert Mbepela amesema amejifunza kitu kwa dini ya kiislaam kuwa unataka watu wawe wanyenyekevu.
  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Khamis Mataka akizungumza wakati wa kufungua kongamano la viongozi wa dini,lililofanyika kwenye ukumbiwa Hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Imam Bukhary Islamic Foundation,Sheikh Khalifa Khamis akifafanua jambo wakati wa kongamano la viongozi wa dini,lililofanyika kwenye ukumbiwa Hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar es Salaam.

  Askofu wa Kanisa la EGS,Dkt. Philbert Mbepela akichangia mada kwenye kongamano la viongozi wa dini,lililofanyika kwenye ukumbiwa Hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Washiriki wa Kongamanp hilo wakifatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

older | 1 | .... | 708 | 709 | (Page 710) | 711 | 712 | .... | 3272 | newer