Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live

Wateja StarTimes kununua king’amuzi kwa shilingi 4000

$
0
0
Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania, David Kisaka (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bei mpya ya king’amuzi kitakakochouzwa kwa shilingi 4000 sambamba na kifurushi kipya cha NYOTA cha malipo ya 4000 kwa mwezi, kulia pamoja naye ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Jacky Yu. Bei hiyo mpya ya king’amuzi na kifurushi itamfanya mteja afurahie chaneli zisizopungua 16 ikiwa 9 ni za kimataifa na 7 za nyumbani kwa muda wa miezi saba na nusu.
Baadhi ya wateja waliokuwepo kwenye uzinduzi wa bei mpya ya king’amuzi kitakakochouzwa kwa shilingi 4000 sambamba na kifurushi kipya cha NYOTA cha malipo ya 4000 kwa mwezi. Bei hiyo mpya ya king’amuzi na kifurushi itamfanya mteja afurahie chaneli zisizopungua 16 ikiwa 9 ni za kimataifa na 7 za nyumbani kwa muda wa miezi saba na nusu. Uzinduzi huo ulifanyika katika duka la kampuni hiyo lililopo ofisi za TBC1, Mikocheni-Bamaga jijini Dar es Salaam.

Kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora na nafuu za matangazo ya dijitali, StarTimes imekuja na kifurushi kipya na bei mpya ya king’amuzi kwa shilingi 4000/- tu gharama ambayo ni ya chini kabisa kutowahi kutokea nchini.

Akizungumzia juu ya huduma hii mpya Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Star Media Tanzania ambao ni wauzaji wa ving’amuzi vya StarTimes nchini, Bw. Jacky Yu amebainisha kuwa uzinduzi huu ni sehemu ya kutimiza ahadi kwa watanzania kwamba watakuwa wakitoa huduma bora na kwa bei nafuu ambayo kila mtu ataweza kuimudu.


SHIRIKA LA MISAADA LA MAREKANI USAID LAKABIDHI PIKIPIKI 10 BOHARI KUU YA DAWA ZANZIBAR

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum na Mshauri Muandamizi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bi. Kelly Hamblin wakisaini makabidhiano ya pikipiki 10 kwa ajili ya ufuatiliaji uwepo wa dawa katika vituoni vya afya Wilaya. Hafla hiyo imefanyaka Bohari Kuu la Dawa Maruhubi Mjini Zanzibar. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima na Mshauri Muandamizi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bi. Kelly wakibadilishana hati ya makabidhiano.
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akikabidhiwa funguo ya pikipiki na Bi. Kelly Hamblin (kusho) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Halima Maulid.
Baadhi ya Pikipiki zilizo kabidhiwa. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

PROIN PROMOTION YAZINDUA MPANGO WA KUUZA FILAMU ZAKE KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0
Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akizungumza jambo kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Proin Promotion kwa ajili ya kuzindua mpango wa kuuza filamu kupitia njia ya mtandao. 


Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akizindua rasmi mpango wa kuuza filamu zake kwa njia ya mtadao wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza(wa kwanza kushoto)

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

GADO LEO

MH. PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA BENKI YA BADEA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Fedha Saada Mkuya (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya Arab Bank for Economic Development in Africa (BADEA) baada ya mazungumzo kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 16, 2015.Kutoka kushoto ni Abdulrahm Hassan Naq,Abdulrahman Bin Saleh Al-Otaishan na Abdelaziz Khelef.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa Benki ya Arab Bank for Economic Development in Africa (BADEA) baada ya kukutana nao kwenye Ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 16, 2015.Kutoka kushoto ni Abdulrahman Bin Saleh Al-Otaishan na Abdelaziz Khelef.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya (kushoto) akiteta na Kiongozi wa Benki ya Arab Bank for Economic Development in Africa (BADEA) , Abdulrahm Hassan Naq baada ya mazungumzo kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wa Benki hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 16, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye atema cheche Unguja kisiwani Zanzibar

Naibu waziri wa maliasili na utalii awataka vijana kujituma kufanya kazi

$
0
0
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mahmoud Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini (katikati) akiwa katika moja ya ziara zake za Wizara ya Maliasili na utalii
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mahmoud Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa katika moja ya ziara zake za wizara ya maliasili na utalii na wengine ni viongozi wa TANAPA
Naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa ziarani.

YOUTH CAMPAIGNERS MEET VICE PRESIDENT DR. MUHAMMAD BILAL IN DAR-ES-SALAAM

$
0
0
  Vice President of Tanzania, Dr Gharib Bilal answering youth questions.
       
 Deputy Minister of Culture, Information, Sports and Youth, Juma Nkamia welcoming Vice President Dr Bilal. 
   Dr Sipho Moyo, ONE Afrika Executive Director giving opening remarks at action/2015 launch
   Margaret Mliwa, Restless Development Country Director speaking at the event.
 Some of the youth telling the Vice President their priorities    .
 According to new research, almost a billion extra people face a life of extreme poverty if leaders do not make key decisions on poverty, inequality and climate change at two crucial summits in New York and Paris later this year.

That's the warning by more than a thousand organisations around the world which are launching a new campaign called action/2015, calling on local and world leaders to take urgent action to halt man-made climate change, eradicate poverty and address inequality.


The new calculation released by the action/2015 coalition shows that the number of people living in extreme poverty – on less than $1.25 a day – could be reduced dramatically from over a billion to 360 million by 2030.


However, if leaders fail to deliver and build on the growing momentum for ambitious deals at the UN Special Summit on Sustainable Development in September and the UN Climate talks in Paris in December, and scale back their efforts, the number of people living in extreme poverty could actually increase to 1.2 billion by 2030. This increase would be the first in a generation (since 1993) and almost a billion higher (886million) than if resolute action is taken. Under this scenario, 1 in 3 of the world’s population would live under $2 a day.


Malala Yousafzai, Nobel Prize winner who put her life on the line for the right to education said; 


2015 must be the year the world wakes up and delivers a safer, more just future for children and young people. We all must play our part in ensuring this is the case. Do not let this opportunity go to waste.”

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA KAMPENI YA CHUKUA HATUA MWAKA 2015

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni ya chukua hatua 2015 yenye lengo la kutathmini matokeo ya Milenia ambayo yanafikia ukomo wake Septemba mwaka huu na hivyo kuwa mwanzo wa kupanga malengo mapya baada ya hayo. Uzinduzi huo uliambatana na Vijana wa Kitanzania waliozaliwa mwaka 2000 ambao hivi sasa wana miaka 15 wakielezea nini wangetaka kuona kiafanyika Tanzania kwa miaka 15 ijayo.
Mmoja kati ya Vijana wenye umri wa miaka 15 walioshiriki kwenye uzinduzi wa kampeni ya chukua hatua 2015 akimkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal zawadi kwenye uzinduzi wa Kampeni ya chukua hatua 2015 yenye lengo la kutathmini matokeo ya Milenia ambayo yanafikia ukomo wake Septemba mwaka huu na hivyo kuwa mwanzo wa kupanga malengo mapya baada ya hayo. Uzinduzi huo uliambatana na Vijana wa Kitanzania waliozaliwa mwaka 2000 ambao hivi sasa wana miaka 15 wakielezea nini wangetaka kuona kiafanyika Tanzania kwa miaka 15 ijayo.

Waziri Mukangara apokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Serikali ya China

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabibidhiwa msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Balozi wa China hapo nchini Lu Youqing na Mwakilishi Mkuu wa Wafanyabiashara kutoka China waishio nchini Lin Zhiyong. Jumla ya vifaa kumi na nne vimetolewa ambavyo ni Roboti ya kujifunzia mpira wa Meza, Kifaa cha kupimia upepo kwa ajili ya Riadha,Nyavu ya mpira wa Meza, Mashine ya kupimia Uzito,Ulingo wa Ngumi,Kompyuta,Printa, Radio Call, mashine ya kutafsirina kuhesabu matokeo katika riadha na nyaya za umeme vyenye thamani zaidi ya 200.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akicheza Mpira wa Meza na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiwa msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

CCM ZANZIBAR YAOMBOLEZA KIFO CHA MWASISI WA ASP MAREHEMU MAKAME MZEE SULEIMAN

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamepokea kwa mshituko, huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha aliyewakuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Zanzibar marehemu Makame Mzee Suleiman, kilichotokea usiku wa tarehe  16 Januari, 2015, nyumbani kwake Amani, Unguja.

Marehemu Makame Mzee Suleiman, alizaliwa tarehe 14 Aprili, 1926, katika Kijiji cha Mitakawani, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini, Unguja.

Alipata Elimu ya Msingi katika Skuli ya  Uzini mwaka 1936. Aidha, alijiendeleza na Masomo ya Qur’an katika Kijiji hicho cha Mitakawani. Mwaka 1945, marehemu alijiendeleza na Elimu ya Sekondari.

Mbali ya Elimu ya Sekondari aliyoipata marehemu, pia alipata mafunzo mbali mbali ndani na nje ya nchi yetu.

Marehemu Makame Mzee, alijiunga na Chama Cha Afro Shirazi (ASP) mwaka 1957 na ni miongoni mwa Waasisi wa Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977, katika Tawi la Mitakawani.

Katika uhai wake, marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya Chama na Serikalini. Kwa upande wa Chama na kutokana na uhodari, uwezo na weledi mkubwa wa masuala ya kisiasa, Chama Cha ASP kilimteua kushika nafasi za uongozi zifuatazo :-

·         Mwaka 1957 - 1961, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ASP Tawi la Mitakawani.

·         Mwaka 1961 - 1977, aliteuliwa kuwa Katibu wa ASP wa Wilaya ya Kati. Pia alikuwa :

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa ASP Taifa.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya
Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Wilaya
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM wa Wilaya na Mkoa wa Kusini, Unguja.
  

Kwa upande wa Serikali, marehemu alibahatika kushika nyadhifa mbali mbali ikiwa ni pamoja na :

Katibu wa Baraza la Mapinduzi (1964 - 1972).
Mkuu wa Wilaya ya Kati, Unguja mwaka 1972 - 1974.
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Pemba mwaka 1974 - 1978.
Mshauri wa Rais wa Mambo ya Siasa - 1978.

Kwa kutambua mchango wake mkubwa katika Uongozi na Utumishi wa Umma, mwaka 2014, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, alimtunuku marehemu Nishani ya Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake kinaungana na wanafamilia, ndugu na marafiki wa marehemu na kuwaomba wawe na moyo wa subra katika wakati huu mgumu wa maombolezi ya mpendwa wetu huyo.

Bila ya shaka kifo cha marehemu kimeacha pengo kubwa kwa Taifa letu.

Hadi kufariki kwake, marehemu Mzee Makame Mzee Suleiman, alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Zanzibar.

Marehemu ameacha vizuka wawili na watoto ishirini (20).

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema Peponi. AMIN.  

BREAKING NYUZZZZZ.....: Transfoma la kituo kikuu cha umeme cha Mgololo Mkoani Iringa lateketea kwa moto

$
0
0
Transfoma la kituo kikuu cha umeme cha Mgololo Mkoani Iringa likiteketea kwa moto mchana baada ya kulipuka ghafla,chanzo kilichepekea kulipuka kwa Transfoma hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa na hali hiyo itapelekea baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya na Njombe kuwa gizani kwa muda.Taarifa zaidi zitawajia baadae kidogo.

Washuhuda wakiangalia Mtambo huo unavyoendelea kuteketea kwa moto mchana huu.

Mkutano Mkuu wa Nne wa wadau wa PSPF Kufanyika Februari 18 - 19, 2015 mjini Dodoma

TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA SANAA,UBUNIFU NA UTAMADUNI NCHINI OMAN

$
0
0
Shamra shamra za ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.
Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Oman Dkt. Fuad bin Jaafar al Sajwan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maonesho ya Mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman. 
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othman kulia akibadilishana mawazo na mmmoja ya Wajasiriamali kutoka Tanzania anayeshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut nchini Oman.

TAARIFA TOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO


BAADHI YA MAOFISA WA JESHI LA POLISI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO MAALUM NA VODACOM TANZANIA

$
0
0
Meneja huduma Vodacom Tanzania,Simon Martin,akitoa mafunzo kwa baadhi ya jeshi la polisi makao Makuu ya Trafiki Dar es Salaam juzi,jinsi ya matumizi ya simu za mkononi kwa kutumia Intaneti na kumiliki simu bila ya kuazimana.
 Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani nchini Kamanda Mohamed Mpinga(kushoto)akimuuliza swali Meneja huduma wa Vodacom Tanzania, Simon Martin(kulia) wakati alipokuwa akitoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya Maofisa wa jeshi la polisi makao Makuu ya Trafiki Dar es Salaam jinsi ya matumizi ya simu za mkononi kwa kutumia Intaneti na kumiliki simu bila ya kuazima.
Baadhi ya Maofisa wa jeshi la polisi makao Makuu ya Trafiki Dar es Salaam wakifatilia mafunzo maalumu ya jinsi ya matumizi ya simu za mkononi kwa kutumia Intaneti na kumiliki simu bila ya kuazima yaliyotolewa na Ofisa wa Vodacom Tanzania juzi.

MAKAMU WA RAIS DKT BILALA AKUTANA UJUMBE WA BRN IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe unaofanya tathmini ya mpango wa matokeo makubwa sasa Nchini (BRN) unaoongozwa na Rais mstaafu wa Botswana Mhe. Festus mogae, wakati ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es salaam leo Januari 16,2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe unaofanya tathmini ya mpango wa matokeo makubwa sasa Nchini (BRN) unaoongozwa na Rais mstaafu wa Botswana Mhe. Festus mogae, wakati ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es salaam leo Januari 16,2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na baadhi ya Mawaziri na wajumbe wanaofanya tathmini ya mpango wa matokeo makubwa sasa Nchini (BRN) wakati ujumbe huo ulipofika Ikulu Dar es salaam leo Januari 16,2015. (Picha na OMR)

NHIF WAJA NA BIMA YA AFYA YA VIKUNDI VYA WAJASILIAMALI

$
0
0
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii 

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeanzisha huduma ya bima ya afya kwa vikundi vya ujasiriamali,Shirika katika sekta binafsi ili kuweza kila mtanzania anapata huduma ya afya kupitia mfuko huo.

Akizungumza leo na wanavikundi vya ujasiriamali (ASSE),Meneja wa CHF- Makao Makuu ya NHIF,Costantine Makala amesema mfumo huo ni kikoa ambapo kila mmoja atachangia Sh.76,800 kwa mwaka.

Amesema kila mwana kikoa ambaye atalipa malipo hayo atatibiwa na bima ya afya mwaka mzima katika hospitali zote za serikali pamoja na baadhi ya hospitali binafsi.

Makala  amesema gharama za matibabu ni kubwa hivyo kila mjasiriamali anaweza kutumia fursa hiyo kwa kuchangia pamoja na wategemezi wake wasiozidi watano.

“Gharama za afya ni kubwa hivyo kila mmoja kutokana na gharama za uchangiaji anaweza kumudu katika mfumo wa kikundi na kupata matibabu yetote yanayolingana na mwanachama yeyote”alisema Makala.
Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Costantine Makala akizungumzia umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kwa vikundi vya wajasiliamali,katika mkutano uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Msimbazi Center,Ilala jijini Dar es salaam.wengine pichani toka kulia ni Mratibu wa Mtandao wa Mfuko wa Afya ya Jamii (TNCHF), Camillius Haul,Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) - Kanda ya Ilala,Christopher Mapunda pamoja na Afisa Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutoka Makao Makuu,Catherine Masingisa.
Mratibu wa Mtandao wa Afya ya Jamii,Kidani Magwira akitoa maelekezo ya namna ya kujaza fomu za ya kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya,katika mkutano uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Msimbazi Center,Ilala jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.

VANESSA MDEE AULA UBALOZI WA SAMSUNG TANZANIA

$
0
0
Kampuni ya kielektroniki ya Samsung imemtangaza Mwanamziki ,Mtangazaji wa Televisheni na Radio Vanessa Mdee kuwa balozi wa Samsung nchini Tanzania.

 Akizungumza leo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli Hayyat Regency Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung,Mike Seo amesema kuwa, "kwa kutambua  ongezeko la uhitaji wa simu za kisasa kwa soko la kati nchini Tanzania ni bora kuwasiliana na wateja wetu kupitia  mtu ambaye amebeba sifa zinazoendana na vifaa vyetu na soko letu. 

Amesema "Tunafuraha sana kutangaza ushirikiano wetu na Vanessa Mdee akiwa kama Balozi wetu mpya nchini Tanzania. Akiwa kama mwanamziki nyota na mchangiaji chanya kwa wananchi wa Tanzania. Vanessa anawakilishi vijana wa kisasa wa Tanzania na ni  mtu ambaye kampuni ya Samsung inaweza kufanya naye kazi hivyo basi tunafuraha kubwa kuwa na mtu kama huyu kuwakilisha bidhaa zetu. "

Seo amesema  mkataba wa Vanessa na uongozi wa kampuni ya Samsung ni ishara  tosha ya makubaliano rasmi kati ya Kampuni ya Samsung na msanii huyo. Kitendo hicho  kilihashiria  mwanzo wa kazi mpya kama mwakilishi wa kampuni ya  Samsung.

Akiwa kama balozi wa kampuni ya Samsung, Vanessa atakuwa kiungo muhimu katika muonekano na uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo.

Kwa upande Vanessa amesema furaha yake kwa kuwa sehemu ya kampuni ya Samsung kubwa  na yenye hadhi ya juu, ni heshima kubwa sana kwangu kuwa balozi wa kampuni hii inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya kielektroniki ulimwengu, huu ni mwanzo tu wa jinsi mwaka 2015 utakavokuwa wa mafanikio kati yangu na kampuni ya Samsung, binafsi, natumaini juu ya kazi hii na nasubiri kwa hamu siku nitakayoanza kazi rasmi. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania,Mike Sio (kushoto) akibadilishana mkataba na Mwanamuziki Vannesa Mdee kuwa Balozi wa Kampuni hiyo.Kulia ni Meneja wa Mwanamuziki Vannesa Mdee,Michele Baldin.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania,Mike Sio (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Samsung Tanzania,Vannesa Mdee (pili kushoto), Meneja wa Mwanamuziki Vannesa Mdee,Michele Baldin (kushoto) pamoja na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni hiyo,Sylvester Manyara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samsung Tanzania,Mike Sio akimuonyesha kitu kwenye simu ya Samsung Balozi wa Samsung Tanzania,Vannesa Mdee mara baada ya kusaini mkataba.

MOGAE COMMENDS TANZANIAN PROJECT DELIVERING PROGRAMME

$
0
0
By Hassan Abbas, Dar es Salaam

Former President of the Republic of Botswana, HE Festus Mogae
The Independent Review Panel (IRP) led by former President of the Republic of Botswana, Festus Mogae has noted that the Big Results Now! (BRN) programme initiated by the government of Tanzania represents a key effort towards a best practice system for transformational change in the way the government operates. 
Presenting the Panel’s independent report after evaluating the program in Dar es Salaam, Mr. Mogae commended significant strides achieved during Year One. The IRP convened for the first time in Dar es Salaam to review the performance of the BRN Programme. 
Ministers implementing first wave of BRN projects presented their first year achievements and challenges yesterday before the Panel, followed by a rigorous question and answer session with the Independent Review Panel (IRP) members. 
In reviewing progress in the first year, the Panel noted that the NKRAs made commendable progress in the key initiatives outlined in the first year and appreciated the frankness with which some of the weaknesses of the programme were discussed. 
They also recognized that the programme has only been in operation for little more than a year, and start-up issues faced should not be allowed to undermine continued implementation. Recommendations were provided by the Panel in addressing these weaknesses. 
“While we endorse the pragmatism of some of the programme in focusing on “easy wins”, over time the Panel thinks it would be prudent to put an appropriate focus on activities that will secure large and more sustainable gains.” H.E. Mogae said. 
The Panel emphasized that it is critical to sustain the BRN programme and for future Governments to continue its support, in order to realize its full impact. “BRN offers the opportunity over time to bring about fundamental improvements in the development programme in Tanzania,” added H.E. Mogae.
 The Chief Executive Officer of the President’s Delivery Bureau (PDB) that oversees the BRN, Omari Issa said as part of commitment to transparency the annual reviw of the BRN will be part of their culture and that a detailed evaluation report from the Panel will be included in the 2013/14 BRN Annual Report, together with the results recorded in the first year and will be shared to the public in the near future.
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live


Latest Images