Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 709 | 710 | (Page 711) | 712 | 713 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Bw. Ibrahim Nassib (kulia) akifungua warsha ya mafunzo ya utumiaji wa teknolojia ya mfumo wa kidigital wa ukusanyaji, uandaaji na utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (DIGITAL METEOROLOGICAL OBSERVATORY (DMO)) na mfumo wa usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga (METEOROLOGICAL AVIATION INFORMATION SYSTEM (MAIS), kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Dkt. Hamza Kabelwa
  Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo ya utumiaji wa teknolojia ya mfumo wa kidigital wa ukusanyaji, uandaaji na utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (DIGITAL METEOROLOGICAL OBSERVATORY (DMO)) na mfumo wa usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga (METEOROLOGICAL AVIATION INFORMATION SYSTEM (MAIS) kutoka katika vituo 28 vya Mamlaka ya Hali ya Hewa vya uangazi wa hali ya hewa vinavyo pima hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

  Madhumuni ya warsha hii ya mafunzo ni kujifunza kuongeza ubora wa uangazi wa hali ya hewa kwa njia za teknolojia ya kisasa kabisa. Aidha, mafunzo haya yanalenga katika maandalizi ya kuanza kutumika kwa teknolojia hii katika vituo vyote nchini.

  Mifumo hii imetengenezwa na wataalamu wetu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa.

  Mifumo hiyo ni:

  1. Mfumo wa kidigitali wa Ukusanyaji, Uandaaji na Utumaji wa taarifa za uangazi wa hali ya hewa (Digital Meteorological Observatory (DMO)) na

  2. Mfumo wa Usambazaji wa huduma za hali ya hewa kwa Usafiri wa Anga (Meteorological Aviation Information System (MAIS)).


  Mifumo hii itapunguza  gharama za uendeshaji zinazotokana  na utumiaji wa karatasi na kuweka kumbu kumbu, kuboresha mfumo wa mawasiliano ndani na nje ya nchi kwa maana ya ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kutokana na mahitaji na viwango vya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization).


  Hali kadhalika, teknolojia hii inarahisisha ufuatiliaji wa utendaji kazi kwa watoa huduma na kuwawezesha wadau kutoa maoni ya huduma za hali ya hewa kwa urahisi na haraka zaidi kupitia mifumo hiyo.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Mbunge wa Namtumbo, MheshimiwaVita Kawawa ambaye amelazwa katika hospitali ya AMI jijini Dar es salaam kwa matibabu. Kushoto ni mke wa mbunge huyo, Siwa Kawawa.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Mbunge wa Namtumbo, MheshimiwaVita Kawawa ambaye amelazwa katika hospitali ya AMI jijini Dar es salaam kwa matibabu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

   Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Jenista Mhagama akitoa hotuba yake wakati wa Sherehe ya mahafali ya Sita katika Fani mbalimbali leo.
   Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Jenista Mhagama akiwa na Bodi ya Chuo pamoja Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha katika picha ya pamoja na wanafunzi 10 waliojinyakulia kitita cha Sh. milioni 1 kila mmoja kutoka kwa Waziri Mkuu,Mizengo Pinda kwa kufanya vizuri katika masomo yao
   Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Jenista Mhagama akimkabidhi kitita cha Sh milioni 1 mhitimu wa fani ya Utengenezaji Vifaa Tiba(Electrical and Biomedical Engineering),Magreth Michael kwa kufanya vizuri katika masomo yake.
   Baadhi ya wahitimu wakifatilia sherehe za mahafali ya Sita katika Chuo cha Ufundi Arusha leo.
  Wahitimu wa Fani ya Uhandisi Mitambo wakitunukiwa Stashahada kwenye Mahafali ya Sita.

  0 0

  24/1/2015 ndani ya leaderz club. kutakuwa na bonge la show. wasanii 18 stage moja.
  instagram @tigomusictz


  Diamond
  ali kiba
  linah
  vannesa mdee
  shaa
  shilole
  khadija kopa
  isha mashauzi
  joh makini
  niki wa pili
  gnako
  fid q 
  mwana fa
  Ay
  prof jay


  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd mara baada ya kumaliza kikao cha halmashauri kuu ya wilaya ya Dimani. 
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyeka majani mbele ya Chuo cha Sayansi ya Bahari (IMS), alipotembelea chuo hicho kilicho chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Buyu, Unguja Zanzibar leo wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi ili zipatiwe ufumbuzi. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

  Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
   Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukielekea katika jimbo la Fuoni kushiriki upandaji wa mikoko katika hifadhi ya Baahari,kaa na ufugaji nyuki  katika eneo la Fuoni Bondeni. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Dimani mkoa wa Magharibi Zanzibara na kuataka wana CCM kushikamana huku akiwaambia vijana kuwa wasiwewanyonge katika kukitetea chama chao.
    Mamia ya watu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja vya Magereza ,Tomondo wilaya ya Dimani mkoa wa Magharibi Zanzibar.
     Katibu wa NEC Itikadi Na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Dimani mkoa wa Magharibi ambapo aliwaeleza hesabu na sayansi ya kisiasa imewamaliza wapinzani hivyo CCM itashinda uchaguzi ujao.
   Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini .
   katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake wakielekea kukagua na kupata maelezo juu ya ujenzi wa Chuo cha sayansi ya Bahari na kutoa nasaha kwa chuo hicho.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikata utepe kuzindua rasmi gari la wagonjwa lililotolewa na Mbunge wa jimbo la Fuoni kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa katika jimbo hilo.
   Mamia ya watu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja vya Magereza ,Tomondo wilaya ya Dimani mkoa wa Magharibi Zanzibar.

  PICHA NA MICHUZI JR-WILAYA YA DIMANI-UNGUJA

  0 0

  Picha na habari na Faustine Rutta
  Ligi Kuu ya Vodacom imeendelea Jumamosi  kwa Mechi kadhaa na Mabingwa Watetezi Azam FC kushinda huko Shinyanga na kutwaa uongozi wa Ligi toka kwa Mtibwa Sugar ambao wanacheza leo, huku Yanga wakiteleza kutwaa uongozi huo baada ya kubanwa na Ruvu Shooting kwa Sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

  Yanga walistahili ushindi lakini walishindwa kufunga wakati walipata nafasi za wazi kibao.

  Huko Kambarage, Shinyanga, Azam FC wameifunga Stand United Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 43 la Frank Domayo na kukaa kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 1 mbele ya Mtibwa Sugar ambao wanacheza Jumapili Ugenini na JKT Ruvu.

  Huko CCM Kirumba, Mwanza, Mbeya City wameifunga Kagera Sugar, wanaotumia Uwanja huo kwa Mechi za Nyumbani baada Kaitaba kufungwa kwa ukarabati, Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 84 la Peter Mapunda.

  Nao Simba wameichapa Ndanda FC waliokuwa kwao Uwanja Nangwanda Bao 2-0 kwa Bao za Dan Sserunkuma na Elias Maguri.
  Mchezaji wa Mbeya City akiondosha mpira kenye eneo la hatari walipokipiga na Kagera Sugar Uwanja wa CCM kirumba na kushinda bao 1-0.
  Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia bao baada ya Timu yao kupata bao katika dakika za Mwishoni dakika ya 84 dhidi ya Kagera Sugar.
  Langoni mwa Timu ya Mbeya City wakiusubiri mpira wa kona.
  Kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi akihojiwa na Baadhi ya Waandishi wa Habari kwenye Uwanja wa Kaitaba jioni ya leo baada ya Timu yake kuibuka na Ushindi wa bao 1-0 Dhidi ya Kagera Suagar ya mjini Bukoba. Picha na Faustine Ruta wa Bukobasports.com
  Raha ya Ushindi wa Mbeya City jijini Mwanza jana.


  0 0  0 0

  (OfficialMusiCVideo : Mrefu A Feat Mdoti - Never Give Up  Directed by o-key Ghetto Child

  0 0

  Bofya HAPA https://mkito.com/song/sihanyi-ft-defxtro/12082 kupakua ngoma ya RikyVato ft Defxtro ngoma kwa jina "Sihanyi" na kwa mawasilano/mahojiano zaidi check na Riky Vato kwa nambari +255 718 229 154 powered by www.vmgafrica.com @vmgafrica @defxtro #supportafricanartists

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na chuo hicho kusaidia wagonjwa katika hospitali hiyo.Makabidhiano hayo yalifanyika jana wilayani Mkuranga kama sehemu ya Chuo hicho kuadhimisha miaka 50 toka kianzishwe mwaka 1965.
  Baadhi ya Wauguzi na wahudumu wa afya wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga wakiangalia moja ya shuka kati ya mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kukamilika kwa barabara ya Ndundu- Somanga (Km 60) na kuwataka wakazi wa mikoa ya kusini kuitumia vizuri barabara hiyo kuibua fursa za kiuchumi na hivyo kujiletea maendeleo. 
  Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa barabara hiyo uliofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe. 
  “ Wito wangu kwenu wakazi wa mikoa ya kusini ni kuitunza barabara hii ili idumu kwa muda mrefu na kuibua fursa za kiuchumi zitakazo wawezesha kupata maendeleo na kupunguza umaskini” alisisitiza Waziri Magufuli. 
  Kufatia kukamilika kwa barabara hiyo, Dkt. Magufuli ameishukuru Wizara ya Ujenzi pamoja na Wakala wa Barabara Nchini, (TANROADS), kwa kazi kubwa ya kusimamia kazi hiyo iliyodumu kwa muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbali. 
  “Nampongeza Katibu Mkuu wa Wizara pamoja na Mtendaji Mkuu wa TANROADS kwa usimamizi makini uliosababisha kukamilika kwa mradi huu muhimu utakaoleta ukombozi kwa wakazi wa mikoa ya kusini” alisema Waziri Dkt.Magufuli 
  Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe ameelezea kuridhishwa kwake na ujenzi wa barabara hiyo na kuwaomba wananchi kuitunza ili idumu kwa muda mrefu. “Barabara hii imekamilika kwa kuchelewa lakini imezingatia viwango vilivyowekwa kimkataba hivyo nawasihi madereva na wananchi kuitumia kwa uangalifu ili kuepuka ajali na kuibua fursa za maendeleo” alifafanua Eng. Iyombe
   Barabara ya Ndundu-Somanga ni sehemu ya barabara kuu ya Dar-Es-salaam -Lindi-Mtwara ambayo imekuwa kwenye matengenezo kwa muda mrefu na Ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 60. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe akiteremka kukagua tuta la barabara ya Ndundu –Somanga(KM 60) iliyokamilika kwa kiwango cha lami.
  Sehemu ya barabara ya Ndundu –Somanga(KM 60) iliyokamilika kwa kiwango cha lami
  Mhandisi wa Mkoa wa Lindi Eng. Isack Mwanawima akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe akikagua sehemu ya barabara ya Ndundu –Somanga(KM 60) iliyokamilika kwa kiwango cha lami.
  Wanahabari wakimhoji Dereva wa basi la abiria kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam kuhusiana na kukamilika kwa sehemu ya barabara hiyo. 
  Habari na picha na 

  kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi


  0 0

  Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa Swissport, Stella Kitali, akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, karatasi inayotumika kuonyesha aina za mizigo inayopakiwa kwenye ndege wakati wataalam hao walipotembelea Kampuni hiyo, mwishoni mwa wiki kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
  Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa Swissport, Stella Kitali, akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, ngazi mbalimbali zinazotumika wakati abiria wanaposhuka kutoka kwenye ndege, wakati wataalam hao waliotembelea Kampuni hiyo.


  0 0  0 0  0 0

  Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Mrisho Millao aliyesimama(kushoto)akionyeshwa namba ya mmoja wa washindi na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)wakati wa kuchezesha droo ya nne ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki,wengine katika picha(kulia) ni mtaalamu wa mifumo ya kompyuta Michael Kanakakis,waliokaa (kutoka kulia) ni Dimitrios Lintis na Zakaria Kanyi.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
  Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Mrisho Millao(kulia)akihakiki namba ya mmoja ya washindi toka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto) wakati wa kuchezesha droo ya nne ya Jaymillions ambapo Jumla ya wateja watano wamejishindi shilingi Milioni moja kila mmoja.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Hali Hatarishi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Nicholaus Paul (wa nne kushoto) akikata utepe kuashiria makabidhiano ya msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 3 yaliyotolewa na wafanyakazi wa kitengo cha mikopo ya makampuni cha benki hiyo kwa Shule ya Msingi Maweni. Hafla ya makabidhiano ilifanyika shuleni hapo, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Maweni, Sylvester Roche, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Martha Silavwe, Mwalimu Mkuu, Zuhura Mwaliko na baadhi ya wafanyakazi wa NBC.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maweni, Zuhura Mwaliko (wa pili kulia) akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Hali Hatarishi wa Benki ya NBC, Nicholaus Paul baada ya kupokea msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 3 yalitolewa na wafanyakazi wa kitengo cha mikopo ya makampuni cha NBC. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Kigamboni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Mikopo ya Makampuni, Beatrice Musira na mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo, Martha Silavwe.
  Meneja wa Kitengo cha Mikopo ya Makampuni wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC, Beatrice Musira (kulia) akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Maweni, Msafiri Habakuki, wakati wa hafla hiyo shuleni hapo jana.


  0 0


  0 0

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
  Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) Mwezi Novemba 2015 kwamba usajili umeanza rasmi tarehe 01 Januari 2015. 

  Watahiniwa watakaojisajili katika kipindi cha kawaida yaani tarehe 01 Januari 2015 hadi 28 Februari 2015 watalipa ada ya Shilingi 50,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT). 

  Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015 watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini). 

   Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani: www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number). 
  Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo. 
  Aidha waombaji watapaswa pia kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa kabla ya kujisajili kwani hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kulipa ada ya mtihani. 
  Waombaji wote wazingatie kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015

  Imetolewa Na: KATIBU MTENDAJI

  0 0


  0 0

  Na Teresia Mhagama 
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amezindua rasmi Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na kuipa vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu vitakavyotekelezwa na Bodi hiyo kabla ya kufikia ukomo wake mnamo mwaka 2017. Uzinduzi wa Bodi hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini 
  Ulihudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini akiwemo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Ngosi Mwihava na Menejimenti ya Tanesco. 
  Waziri Muhongo aliieleza Bodi hiyo kuwa ina jukumu kubwa la kuliongoza Shirika hilo kwa ufanisi na kuhakikisha kuwa Shirika hilo linajitegemea na hivyo kupunguza utegemezi wa fedha kutoka serikalini. 
  "Kwa kipindi kirefu, serikali imekuwa inatoa fedha nyingi kuisaidia Tanesco kutekeleza miradi katika maeneo ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme hivyo Bodi hii ionyeshe jinsi mtakavyolibadilisha Shirika hili ili hii misaada kutoka serikalini ipungue na ifike mahala Shirika hili lijitegemee," alisema Profesa Muhongo. 
  Kuhusu madeni ambayo Tanesco inadai kutoka kwa Taasisi za Umma, binafsi na watu binafsi, Waziri Muhongo aliiagiza Bodi hiyo kulisimamia suala hilo na kuja na mkakati utakaoliwezesha Shirika hilo kukusanya madeni hayo kwani lengo la serikali ni kuona Shirika hilo linakusanya madeni kutoka kwa wadeni wake wakubwa na wadogo ili Shirika hilo nalo liweze kulipa madeni linalodaiwa na wadau wake. 
  Suala la wananchi kufungiwa umeme ndani ya siku 30 mara wanapopeleka maombi hayo Tanesco lilimkera Profesa Muhongo na kuiagiza Bodi hiyo kulishughulikia suala hilo ili siku hizo zipungue. "Bodi simamieni maombi ya kufungiwa umeme ambayo sasa yanaelezwa kushughulikiwa ndani ya siku 30, hii lazima ibadilike, watanzania lazima wapewe umeme ndani ya wiki, zaidi ya hapo haikubaliki. 
  "EWURA waelezwe kuhusu suala hili ili kuona namna ya kupunguza hizi siku sababu wao wanahusika katika suala la upangaji wa siku husika," alisisitiza Profesa Muhongo. 
  Vilevile Profesa Muhongo aliiagiza Bodi mpya ya Tanesco kuhakikisha kuwa Shirika hilo linashirikiana na sekta binafsi katika miradi yake ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme ili kufanikisha lengo la serikali la kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025. Profesa Muhongo alieleza kuwa kulingana na sera zilizopo, uendelezaji wa sekta ya umeme unahitaji ushirikishwaji wa sekta binafsi kwa kuwa uwekezaji katika sekta hiyo unahitaji kiasi kikubwa cha fedha za kigeni, kiwango ambacho kinahitaji ushirikiano na sekta hizo kupitia mitindo ya IPP na PPP. 
  Alisema Tanesco inapaswa kuonesha nia thabiti ya kuunga mkono juhudi za serikali za kukamilisha majadiliano na wawekezaji na waendelezaji wa miradi bila kuwakatisha tamaa. 
  Awali Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele aliieleza Bodi hiyo kwamba serikali ina imani kuwa uzoefu na weledi wa Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi hiyo utasaidia katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya nishati ili sekta hiyo muhimu ichangie katika kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati.
  Aliwaasa Wajumbe hao kuhakikisha kuwa taaluma walizonazo wanazitumia katika kuliboresha Shirika la Umeme nchini. 
  Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Mighanda Manyahi ameeleza kuwa majukumu waliyokabidhiwa ya kuisimamia Tanesco ni makubwa lakini kwa kutumia taaluma zao watahakikisha wanayatimiza ili kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa uhakika kwa kuwa nchi zina rasilimali za kutosha zinazowezesha kutimiza lengo hilo. 
  Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco anaongoza wajumbe Nane ambao ni Bibi. Kissa Vivian Kilindu, Mhandisi Juma Mkobya, Dkt. Haji H. Semboja, Bw. Shaaban Kayungilo, Dkt. Mutesigwa Maingu, Mhandisi Boniface Muhegi, Bw. Felix Kibodya, na Dkt. Nyamajeje Weggoro.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwapongeza Wajumbe wa Bodi mpya ya TANESCO mara baada ya kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu. Wanaoshuhudia ni viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Naibu Waziri, Stephen Masele (kushoto kwa Waziri) na Kaimu Katibu Mkuu, Eng. Ngosi Mwihava (wa nne kulia).

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo mara baada ya kuzindua Bodi mpya ya TANESCO katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa tatu kutoka kushoto), Kaimu Katibu Mkuu, Eng.Ngosi Mwihava (wa nne kutoka  kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba (wa nne kulia). Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi hiyo, Eng. Juma Mkobya,(wa tatu kulia), Bw. Felix G. Kibodya (wa pili kulia), Bibi. Kissa Vivian Kilindu (wa kwanza kulia), pamoja na watendaji mbalimbali wa TANESCO (waliokaa mstari wa nyuma).

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa tatu kutoka kushoto), Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba (wa pili kulia), wakimsikiliza mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO (haonekani pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni mmoja wa wajumbe wa Bodi hiyo, Eng. Juma Mkobya.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Mighanda J. Manyahi (aliyesimama) akizungumza mara baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Waziri, Profesa Muhongo (kulia) na Mjumbe wa Bodi hiyo, Dkt. Haji H. Semboja (kushoto). 

  Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Mighanda J. Manyahi (wa sita kutoka kushoto) wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng.Ngosi Mwihava (wa tano kulia) mara baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Wajumbe wengine wa Bodi hiyo (kutoka kushoto) ni Dkt. Nyamajeje C. Weggoro, Eng. Boniface C. Muhegi, Dkt. Mutesigwa I. Maingu, Bw. Shaaban S. Kayungilo, na Dkt. Haji H. Semboja. Wajumbe wengine (kutoka kulia) ni Bibi. Kissa Vivian Kilindu, Bw. Felix G. Kibodya na Eng. Juma F. Mkobya.


older | 1 | .... | 709 | 710 | (Page 711) | 712 | 713 | .... | 3272 | newer