Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

UN TANZANIA YAZINDUA RIPOTI YA MAENDELEO DUNIANI 2013 IKIONYESHA NCHI ZINAZOENDELEA 40 ZIMEPIGA HATUA KUBWA SANA YA MAENDELEO YA BINADAMU

$
0
0

Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 - Kuchomoza kwa Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akisema kwa mujibu wa ripoti hii mwaka huu iaonekana kuwa Tanzania tumefanya vizuri na kiwango chetu kimeongezeka kama ngazi mbili ikilinganishwa na ripoti iliyopita.
Hata hivyo amesema kwa bado kuna mikoa mingi ambayo unapopima maendeleo kwa ujumla wake mikoa mingi ipo asilimia 20 hadi 30 ambapo hii inapima ujumla wa maendeleo katika Jamii.
Bw. Lyimo amesema kwa sasa serikali ina mipangp mizuri ya kuisaidia mikoa hiyo, akitolea mfano kilimo kuwa kuanzia miaka ya 80 hatukuiangalia vizuri tulikuwa na taasisi za kilimo, mashirika ya maendeleo ya viwanda lakini katika kipindi hiki cha mageuzi tumepata matokeo mazuri.
Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha Kuchomoza kwa Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai ambapo amesema sera kabambe, zilizotengenezwa vizuri zinaweza kufanya mafanikio ya kimaendeleo ya binadamu kuwa endelevu katika miongo ijayo na kupanuka kufikia nchi nyingi zaidi zinazoendela.
Lakini pia Dkt. Kacou ameonya hatua za kubana matumizi zisizo na mtazamo wa mbali, zaweza kushindwa kushughulikia hali ya kukosekana usawa, na kukosekana kwa ushiriki wa maana wa jamii na kutishia maendeleo haya kama viongozi hawatachukua hatua za kurekebisha.
Aidha amesema baadhi ya mataifa yanayoongoza kwenye nchi za Kusini yanajenga mwelekeo mpya wa kukuza maendeleo ya binadamu na kupunguza tofauti za kimaisha kwa kuweka sera bunifu ambazo zinasomwa na kuigwa sehemu nyingine duniani.
Baadhi ya Wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini wakimsikiliza Dkt. Alberic Kacou (hayupo pichani) alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 iliyofanyika jijini Dar leo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

SATURDAY GROOVE PARTY AT POLAZ PUB, DAR

KAIRUKI AZINDUA KIJITABU CHA MAMBO 101 UNAYOHITAJI KUYAFAHAMU KUHUSU POLISI LAKINI UNAOGOPA KUYAULIZA

$
0
0
Mheshimiwa Angellah Kairuki (MB), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria katika picha ya pamoja na wadau mmbalimbali na wageni waalikwa baada ya kuzindua kijitabu cha “Mambo 101 Unayohitaji Kuyafahamu Kuhusu Polisi Lakini Unaogopa Kuyauliza. ” Waliokaa kulia kwa Naibu Waziri ni Bi. Benardetha Gambishi, Kamishna wa Haki za Binadamu na kusho ni kwa Naibu Waziri ni Bw. Julian Chandler mwakilishi wa Balozi wa Uingereza nchini.
Mheshimiwa Angellah Kairuki (MB), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akiinua juu kijitabu cha “Mambo 101 Unayohitaji Kuyafahamu Kuhusu Polisi Lakini Unaogopa Kuyauliza ” kuashhiria kuwa kijitabu hicho kimezinduliwa rasmi. Wanaopiga makofi waliosimama ni Bi. Mary Massey, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na kulia kwake ni Mhe. Jaji Kiongozi (Mst.) Amir Manento ambaye ni Mwenyekiti wa Tume hiyo. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Bw. Julian Chandler mwakilishi wa Balozi wa Uingereza nchini.
Mheshimiwa Angellah Kairuki (MB), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akikata utepe katika kuzindua kijitabu cha “Mambo 101 Unayohitaji Kuyafahamu Kuhusu Polisi Lakini Unaogopa Kuyauliza.” Aliyeshika kijitabu hicho ni Bi. Mary Massey, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na kulia kwake ni Mhe. Jaji Kiongozi (Mst.) Amir Manento ambaye ni Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Wananchi wametakiwa kutowaogopa na kuwachukia polisi pale wanapokuwa na matatizo yao. Hayo yalisemwa leo na Mhe. Angellah Jasmini Kairuki (Mb) wakati alipokuwa akizindua kijitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu polisi lakini unaogopa kuyauliza katika Makao Makuu ya Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu (THBUB) jijini Dar-es-salaam.

Mhe. Kairuki alisema kuwa raia wema wenye kuwajibika hawapaswi kuwaogopa na kuwachukia polisi au kuogopa kwenda kituo cha polisi pale wanapokuwa na matatizo au kutoa taarifa kuhusu matukio ya uhalifu. “Wananchi na polisi wanatakiwa wafanye kazi pamoja na kuleta amani na utulivu kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.” Alisema.

Mhe. Kairuki katika uzinduzi huo alisema kuwa ni muhimu kwa wananchi kuzielewa kazi za polisi, jinsi wanavyozifanya na kujua changamoto wanazokumbana nazo katika kutekeleza majukumu yao. “Ni ukweli usiopingika kuwa Jeshi la polisi bado linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi,” alisema.

Naibu Waziri alisema ana amini kuwa kijitabu hiki pamoja na mambo mengine kitasaidia si tu kwa wananchi kujua haki zao bali pia kitakuwa msaada mkubwa kwa askari wa Jeshi hilo katika kujiongezea uelewa na majukumu na mipaka ya kazi zao.

Wakati huohuo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu Bi. Mary Massay alisema kuwa kijitabu hiki kitasaidia kuongeza uelewa wa wananchi watakapokisoma na pia uelewa wa polisi kuhusu wajibu, kusudi, muundo, na haki za wananchi wanapokutana na polisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aliongeza kuwa kijitabu hiki kimeandaliwa chini ya mradi wa kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao na kazi kazi kwa kushirikiana na Commonwealth Human Rights Initiative yenye makao yake New Delhi nchini India.

Bi. Massay amesema kwa awamu ya kwanza wamechapisha jumla ya nakala 4838, kati ya hizo, nakala 4,500 zimeandaliwa kwa lugha ya Kiswahili, nakala 300 kwa lugha ya kiingereza na nakala 38 zimeandaliwa kwa nukta nundu kwa ajili ya watu wasioona.

Aidha, Katibu huyo wa Tume ya Haki za Binadamu alisema kuwa nakala hizi zitasambazwa bure kwa wananchi na taasisi mbalimbali katika miji ya Dar-es-salaam, Zanzibar, Mwanza na Lindi

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Kuna mdau kaleta mzigo na  special request ya ngoma hii ya 'Ikati' ya Condry Ziqubu. Asante mdau kwa kututoa machozi sie wa enzi hizo

hospitali ya lindi yanusurika kuungua

$
0
0
 Na Abdulaziz,Lindi
Hospital ya mkoa wa Lindi(Sokoine hospital) imenusurika kuungua usiku wa kuamkia leo kutokana na kilichotajwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Muuguzi wa Zamu ,Bi Rehema Mbinga alieleza kuwa Moto huo ulioanzia katika swichi ya Umeme uliweza kudhibitiwa vyema kufuatia huduma ya haraka ya kuzima moto iliyokuwepo hospitalini  hapo.
 Hata hivyo alieleza masikitiko yake kufuatia simu walizopiga katika kikosi cha kuzima moto cha Manispaa ya Lindi na mpokeaji kujibu majibu rahisi ya Acheni kutania nyie na kukata simu kila ikipigwa.
 "Mwandishi tunashukuru kwa msaada wa wauguzi wenzangu tumefanikiwa kuzima moto huo ulioanzia katika dirisha la kutolea dawa
"Ila fikisha ujumbe Kikosi cha zimamoto waache dharau na majibu rahisi wanapopigiwa simu vinginevyo watasababisha maafa. leo sijui ingekuwaje kama tusingewahi kuuzima huo moto"limalizia Bi Rehema

Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa yapokea Msaada wa Mashuka kutoka NHIF

$
0
0
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Lindi,Bi. Fortunata Raymond (kushoto) akikabidhi msaada wa mashuka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Bi. Agness Hokororo kwa ajili ya Hospital ya wilaya hiyo,Kulia Mkugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa,Bw. Mfune akishuhudia tukio hilo.
Mkuu wa wilaya pamoja na Meneja wa Nhif Lindi wakitandika moja ya shuka zilizokabidhiwa.
Wadau mbalimbali wakishiriki semina Kuhusiana na mfuko wa afya ya jamii CHF Wilayani RUANGWA.

ngoma mpya ya lady jay dee featuring profesa J

Wengi wajitokeza kuaga Mwili wa Marehemu Mama Susan Mgwasa jijini Dar

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania, David Mgwassa akizungumza na baadhi ya waombolezaji waliofika kumfariji kwa kufiwa na  mama yake mzazi Suzan  Mgwassa, Kijitonyama, Dar es Salaam. Mwili ulisafishwa jana kwenda kwao Manda, Ludewa kwa mazishi.
Mjukuu wa marehemu Suzan Mgwassa, Isaack Mgwassa 9kulia0 akijadiliana jambo na maaskofu wa Kanisa la Pentekoste wakati wa msiba huo.
Kwaya ya Kanisa la Pentekoste ikomboleza kwa nyimbo za injili wakati wa kuaga mwili wa marehemu Suzan
David Mgwassa (wa pili kulia) akijadiliana jambo na maaskofu wa Kanisa la Pentekoste waliokwenda kuuombea mwili kabla kusafirishwa.


REMEMBRANCE

15 - 21 MARCH 2013 - CENTURY CINEMAX - MLIMANI CITY & MWENGE BRANCH (NEW WORLD CINEMAS)

COSTECH YATOA MIL. 10 KUDHAMINI TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI

$
0
0
AFISA UHUSIANO WA TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (COSTECH) BW THEOPHIL LAURIAN PIMA AKIMKABIDHI KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA HABARI TANZANIA BW KAJUBI MKAJANGA MFANO WA HUNDI YA SHILINGI MILIONI KUMI KWA AJILI YA KUDHAMINI TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI ZITAKAZOFANYIKA MWEZI APRIL 2013.TUKIO HILO LILIFANYIKA JANA KWENYE OFISI ZA BARAZA HILO.
KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA HABARI TANZANIA BW KAJUBI MKAJANGA AKITETA JAMBO KABLA YA KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZITAKAZOFANYIKA MWEZI UJAO.
BAADHI YA WAGENI WALIOHUDHURIA TUKIO HILO LA UTOLEWAJI HUNDI KATIKA BARAZA LA HABARI TANZANIA

SAFARI LAGER NYAMA CHOMA KURINDIMA JIJINI MWANZA KESHO

$
0
0
SAFARI LAGER NYAMA CHOMA MWANZA FINALS
Sunday, 17 March 2013 – Kiwanja Cha Furahisha
  • Kwa mara nyingine tena, Safari Lager inakukaribisha kushuhudia mchuano wa mwisho kuona ni Baripi inayochoma nyama Bomba zaidijijini Mwanza!.
  • Ni Jumapili hii tarehe17 March, katika Kiwanja Cha Furahisha jijini Mwanza kuanzia saa 4.00asbh.
  • Njoo ushuhudie bar zilizoingia fainali Mwanza zikichuana kukupa Nyama Choma Bomba zaidi;
    • Victoria Prince Bar Kirumba.
    • Shokeni Bar Mkuyuni.
    • AR Pub Kilimahewa.
    • Lunara Bar Nyakato.
    • Shooters Bar Kirumba.
Washindi watajipatia zawadi zaidi ya shilingi milioni nne!.
  • Njoo uburudike kwa aina tofauti za nyama choma, kuanzia mapande hadi mishkaki, nyama za Kuku, Ngombe na Mbuzi!!.Chachandu, Kachumbari, pilipili, ndimu nk.. vitakuwepo.
  • Kutakuwa na zawadi kibao kutoka Safari Lager, burudani za wasanii mbalimbali, na kufunga kazi jukwaani watakuwepo The Africana Music Band!!..
  • Tamasha la Safari Lager Nyama Choma jumapili hii pale kiwanja cha Furahisha jijini Mwanza ni BURE, hakuna Kiingilio!.
  • Bila Safari Lager, Nyama Choma Haijakamilika!!..

Ujumbe wa CCM waendelea na ziara yao nchini China

$
0
0
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimpa zawadi ya kinyago cha 'Ujamaa', Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada , Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akipewa zawadi ya picha na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China.Kushoto anaeshuhudia ni Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.

Kibonzo cha Kijast Bikozz

MABADILIKO SEMINA ELEKEZI COPA COCA-COLA

$
0
0

Semina elekezi kwa ajili ya michuano ya Copa Coca-Cola 2013 iliyokuwa ifanyike Jumanne (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam sasa imesogezwa mbele hadi Machi 26 mwaka huu.

Uamuzi wa kusogeza mbele semina hiyo umetokana na maombi ya wadhamini, Coca-Cola ambao katika tarehe ya awali watakuwa na shughuli nyingine za kampuni hiyo.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi wajumbe kwa usumbufu wowote utakaokuwa umejitokeza kutokana na semina hiyo kusogezwa mbele.

Hivyo, washiriki wa semina hiyo wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam (TFF) siku moja kabla (Machi 25 mwaka huu).

Washiriki hao ni makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia waratibu wa mikoa wa mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).

Barua za mwaliko kwa ajili ya semina hiyo tayari zimetumwa kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

RAIS KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA HOSPITALI YA KAIRUKI, DAR ES SALAAM, LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua rasmi hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Mama Koku Kairuki akimkabidhi tuzo Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NHIF YATOA MAFUNZO KWA WANACHAMA WA UVIMA KUHUSU HAKI NA WAJIBU WAO

$
0
0

Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Rehani Athumani akizungumza katika semina vikundi vya akina mama wa Majohe (UVIMA) vilivyopo chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayosimamiwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete hiyo iliyofanyika Majehe leo.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Eugen Mikongoti akizungumza na washiriki wa semina hiyo iliyofanyika Majohe Pugu jijini Dar es salaam leo
 Philomena  Marijani Meneja Uragibishi kutoka WAMA akizungumza katika semina hiyo.
 Afisa wa Masoko na Elimu kwa Umma NHIF Grace Michael akitoa maelezo kabla ya kuanza kwa semina hiyo leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BALOZI KAMALA AWASIHI WATANZANIA WAISHIO UHOLANZI KUWEKEZA NYUMBANI

$
0
0
Balozi wa Tanzania katika eneo la BENELUX, linalojumuisha nchi za ni Ubelgiji, Uholanzi na Luxemberg Dk Diodorus Kamala amekutana na baadhi ya Watanzania waishio nchini Uholanzi katika safari ya kikazi nchini humo, ambapo kwa pamoja walijadiliana masuala mbalimbali yanoyuhusiana na mustakabali wa uchumi na maendeleo ya Tanzania. 
 Balozi Kamala amewasihi Watanzania hao kuwa wazalendo kwa kutumia utaalamu wao katika kuitumikia nchi katika maeneo mbalimbali yanayohitaji utaalamu hali itakayopelekea kuhakikisha ukuaji wa haraka wa uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. 
Aliongeza kuwa hawana budi kuchangamkia fursa lukuki za uwekezaji kiuchumi zinazopatikana Tanzania. Pia, katika mazungumzo yake na Watanzania hao, Balozi Kamala, amewasihi kuishi kwa umoja na ushirikiano na kuendelea kuipeperusha vyema Tanzania. 
 Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Dorus, uliopo katika Taasisi ya Elimu ya Jamii (ISS), jijini The Hague.
 Mwenyekiti wa TANE, Bw. Kweba Bulemo (aliyesimama Kulia), akisema machache kabla ya kumkaribisha Mhe. Balozi.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio Uholanzi (TANE), Bw. Musuto wa Chirangi  (aliyesimama) akizungumza wakati wa kumkaribisha Balozi Kamala.
 Balozi wa Tanzania katika eneo la BENELUX, Dk Diodorus Kamala akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi.
 Balozi Dk. Kamala akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi.

azim dewji atoa maoni juu ya sakata la TFF na FIFA

$
0
0
Azim Dewji
Na Mwandishi Wetu
MWANAMICHEZO aliyewahi kuifadhili Simba na pia kumiliki timu ya Ligi Kuu ya soka nchini, Azim Dewji ameingilia katika suala la mgogoro wa Katiba ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), akisema ni bora Tanzania ikafungiwa na FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) kuliko kuyumbishwa na Rais wa TFF, Leodegar Chilla Tenga.


Dewji aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, huku akimtaka Tenga kuwa na msimamo katika maamuzi yake. Alisema kuwa, Tenga akiwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alikuwa tayari kuona Tanzania inafungiwa na FIFA, kuliko kuacha soka la nchi hii liendeshwe kiholela.


“Sasa kama wakati ule alitaka tufungiwe, kwa sasa anaogopa nini na kuanza kubishana na Serikali?

“Kwa maoni yangu, ni bora tufungiwe lakini tusiendeshwe na FIFA…Tanzania ina Serikali na ndiyo inayosimamia michezo, kwa hili sioni sababu ya TFF kuitunishia msuli serikali. Hii ni nchi, haiwezi kutishwa na taasisi tu ya soka ya kimataifa ambaye Tenga mwenyewe
aliwahi kukaririwa miaka ya nyuma akisema ina genge la wahuni…,” alisema Dewji.


TFF imejikuta ikiingia katika mgogoro na Serikali baada ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kuingilia kati suala la mgogoro wa uchaguzi ndani ya TFF kwa kuagiza kufutwa kwa matumizi ya Katiba ya shirikisho hilo ya mwaka 2012, kwa kuwa imekiuka Kanuni na Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT).


Waziri huyo aliiagiza TFF kufuata utaratibu wa kurekebisha Katiba za vyama vya michezo, kwa mujibu wa Sheria ya BMT iliyotungwa na Bunge pamoja na Kanuni zake ambazo ziko wazi na rahisi kuzifuata.


Hata hivyo uamuzi huo wa Waziri, ulipingwa na Tenga pamoja na Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo, ambapo Tenga ameomba kuonana na Waziri akidai amepotoshwa na wasaidizi wake na uamuzi wake unaweza kulitia soka la Tanzania katika matatizo.


Tenga alidai Serikali na BMT vimeachana na kuingilia masuala ya soka tangu mwaka 2004 na ndani ya Katiba hiyo kuna utaratibu mzima ambao unaonesha namna ambavyo TFF inapaswa kufanya uamuzii wake kama chombo huru. Hata hivyo, kisheria Katiba ya TFF lazima isajiliwe serikalini.


Awali TFF iliomba kukutana na Waziri na ikafanya hivyo, lakini shirikisho hilo limeomba tena kukutana na Waziri Mukangara kwa madai kuwa katika kikao cha awali Tenga hakuwepo badala yake walienda watendaji, hivyo ni vyema kikafanyika kikao hicho ili kumpa ufafanuzi
wa baadhi ya mambo kwa nia ya kulimaliza jambo hilo.


Katika kikao hicho cha awali, Serikali iliitaka TFF kuitisha mkutano wa katiba ndani ya siku 40 na baada ya hapo kuitisha uchaguzi ndani ya siku kama hizo na pia imeitaka kutoa taraifa kwa wanachama wake kuhusu mkutano huo ndani ya siku tano tangu siku walipokutana.


Uamuzi wa Dk  Mukangara ulikuja siku chache kabla ya timu ya maofisa wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuja nchini kufuatilia mgogoro ulioikumba TFF na wadau wake kutokana na masuala mbalimbali ya uchaguzi huo uliokuwa ufanyike Februari 24 mwaka huu. Ujumbe wa FIFA haukuja badala yake shirikisho hilo limetuma barua ya kutishia kuifungia Tanzania kama itathibitika serikali inaingilia masuala ya soka.

MBUNGE NA MWAKILISHI WA MAGOMENI ZANZIBAR WAGAWA SARE KWA WANAFUNZI WALIO FAULU MJINI UNGUJA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Magomeni Muhamad Amour Chombo akitoa nasaha kwa wanafunzi,na pia kuwapongeza kwa kufaulu kwao kabla ya kuwazawadia sare za Skuli kwa kila mwanafunzi,huko katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere Mjini Unguja.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin akimkadhi sare ya Skuli mwanafunzi Shida Muh'd Abdalla aliefaulu kuingia Darasa la 11 katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere Mjini Unguja.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.)
Mbunge wa Jimbo la Nyerere Muhamad Amour Chombo akimkadhi sare ya Skuli mwanafunzi Abdilan Mzee aliefaulu kuingia Darasa la 11 katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere Mjini Unguja.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images