Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 68 | 69 | (Page 70) | 71 | 72 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael(katikati)pamoja na Meneja wa Mahusiano wa kampuni hiyo,Bw. Matina Nkurlu, wakimpigia mmoja wa washindi wa promosheni ya Mahela aliejishindia shilingi Milioni moja, kushoto ni ofisa wa Bodi ya Kubahatisha nchini Bw.Humudi Hussein, bado shilingi Milioni 251 zinaendelea kushindaniwa katika promosheni hiyo.
  Ofisa wa Bodi ya Kubahatisha nchini Bw.Humudi Hussein kushoto akiandika jina la mmoja wa washindi waliojinyakulia shilingi milioni mojamoja kati ya washindi tisa kupitia promosheni ya MAHELA inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,katikati ni Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael,pamoja na Meneja wa Mahusiano wa kampuni hiyo,Bw. Matina Nkurlu.
  Meneja wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)juu ya Promosheni ya MAHELA wakati wa kuchezesha droo ya kuwapata washindi wa shilingi milioni moja moja ambapo washindi tisa walipatikana hivi leo,kupitia promosheni hiyo,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Ofisa wa Bodi ya Kubahatisha nchini Bw.Humudi Hussein na Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael.

  0 0

   
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika sherehe za uzinduzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu mjini Morogoro leo
   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro Mama Mwantumu Malale akiongea machache na kumkaribisha Rais Kikwete
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu mjini Morogoro leo
   Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la kitivo cha TEKNOHAMA katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) hapa nchini, Mhe. Abdulla Ibrahim Al Suwaidi. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofisi kwa Mhe. Waziri Membe leo tarehe 14 Machi, 2013.
  Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Balozi Al Suwaidi  masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na UAE mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi huyo.
  Mhe. Balozi Al Suwaidi akichangia hoja wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Membe. Mwingine katika picha ni Bw. Hangi Mgaka, Afisa Mambo ya Nje katika Idara ya Mashariki ya Kati.

  0 0

  Kwa Mamlaka aliyopewa Spika na kanuni ya 113 ya Kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007, uteuzi wa wajumbe wa kamati kwa kipindi kilichobaki cha uhai wa Bunge hili sasa umekamilika kama ilivyo kwenye orodha.

  Madhumuni ya kuwapanga upya waheshimiwa Wabunge kwenye kamati mbalimbali ni kuwapatia fursa wabunge kadri inavyowezekana kujipatia ujuziu na uzoefu wa shughuli za Kamati tofauti na pia kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na kanuni za 113 (5)

  Uteuzi huu unaanza leo tarehe 14 Machi, 2013, na kesho saa sita mchana tarehe 15 Machi, 2003 ni uchaguzi wa Wenyeviti wa kamati hizo katika kumbi mbalimbali zinavyoonyesha .

  Imetolewa na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
  Ofisi ya Bunge 
  DAR ES SALAAM
  14 MACHI, 2013


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujeruman, Prof. Harald Draun, aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 14, 2013 kwa ajili ya mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujeruman, Prof. Harald Draun, aliyeongozana na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 14, 2013. Picha na OMR.

  0 0


  0 0


   Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (katikati) akigonganisha glass na Mkurugeni wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni Wadhamini wakuu wa Shindano la Miss Tanzania,Kushilla Thomas (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania,Anko Hashim Lundenga ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013/14 wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party),iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam
   Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania,Anko Hashim Lundenga akizungumza machache wakati wa wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party) ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013/14,iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam
   Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (katikati) akiwa katika picha pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro (kushoto) na Meneja wa vilaji vha Castle Lite na Ndovu,Pamella Kikuli wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party) ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013/14,iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam
   Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mamiss Tanzania waliopita,Toke Kushoto ni Faraja Kotta,Salha Israel pamoja na Nancy Sumary.


  0 0

  Na Johary Kachwamba na Eleuteri Mangi _MAELEZO-Dar es salaam

  WANACHUO Shule za biashara kutoka vyuo vikuu nane (8) mbalimbali vya Afrika Mashariki wanatarajia kukutana ili kujadili fursa za ajira katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Kauli hiyo ilitolewa jana (leo) jijini Dar es salaam na Rais wa Wanachuo wanasoma masomo ya Biashara (Dar es salaam University Finance Association -DUFA) Maximillian Msuya wakati wanaongea na waandishi wa habari.

  Alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuzungumzia maswala ya sekta ya mafuta na gesi na vilevile watazungumzia mitaala ya elimu katika eneo la Afrika mashariki.

  Msuya aliongeza kuwa mkutano huo utaangalia namna gani nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaandaa wataalamu katika soko la ushindani la ajira za kuajiriwa na zile kujiajiri wenyewe.

  Mkutano huo unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 16 mwezi huu, katika Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.

  Rais huyo ametaja vyuo vitakavyoshiriki kuwa ni Chuo Kikuu cha Nairobi (UON), Chuo Kikuu cha Kisii na United States International University (USIU) kutoka Kenya.

  Vingine ni Chuo Kikuu Ndejje kutoka Uganda na kwa upande wa Tanzania kutakuwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na wenyeji Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.

  Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stegomena Tax.

  0 0

  Sehemu ya Tatu ya WanaDMV wafanya mjadala wa kushuka kwa kiwango cha Elimu na matokeoa mabaya ya kidato cha Nne wakianza kuelezea Elimu zamani ilivyokuwa na nini kimesababbisha kuporomoka kwa Elimu Je nani alaumiwe na nini kifanyike kuokoa janga hili WASIKILIZE

  0 0

   Mgombea nafasi ya Uwenyekiti wa ya Miundombinu  Mhe. Peter Serukamba ane akinadi sera zake mbele ya wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi leo
   Mgombea nafasi ya Uwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akinadi sera zake mbele ya wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi leo
   Mgombea wa Nafasi ya Uenyekiti katika kamati ya LAAC Mchungaji Israel Natse nae akinadi sera zake
   Wajumbe wa Kamati ya PAC wakiteta na Mhe. John Cheyo anaye tetea kiti chake cha uenyekiti wa kamati 
   Mhe. David Kafulila akimpongeza Mhe. James Lembeli mara baada ya kupita bila kupingwa kwa nafasi ya uenyekiti wa kamati ya Ardhi  Maliasili na Mazingira 
   Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza na wajumbe wa kamati ya Bajeti ambapo tofauti na kamati nyingine amefanya uteuzi wa mwenyekiti wa kamati hiyo kuwa Mhe. Andrew Chenge.
   Katibu wa Bunge Ndg. John Joel akitangaza Matokeo ya wenyeviti na Makamu wa Wenyeviti mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi hao katika kamati zote za Bunge leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa kamati za Bunge Ndg. Theonist Luhirabake na kulia ni Afisa Habari wa Bunge Ndg. Owen Mwandumbya 
   Msimamizi wa Uchaguzi katika kamati ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa Bi. Justina Shauri akiwapa maelezo ya awali wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuchagua viongozi wao.
   Msimamizi wa Uchaguzi katika kamati ya Ulinzi na Usalama Ndg. Peter Magati akiwapa maelezo ya awali wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuchagua viongozi wao. 
   Katibu wa Kamati ya PAC Bi. Lina Kitosi ambaye pia ndiye msimamizi wa uchaguzi akiteta jambo na mwenyekiti wa mda wa kamati hiyo kabla ya uchaguzi kufanyika.


  0 0

   KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akiwa katika mazungumzo na  Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada , Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China  na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
   KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akipewa zawadi ya picha na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China
   KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimpa zawadi ya kinyago cha 'Ujamaa', Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China  na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
   Baadhi ya viongozi wa CCM waliopo katika ujumbe wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakiwa ukumbini wakati wa mazungumzo ya Kinana alipokuwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada , Machi 14, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China  na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
   KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akitoka ukumbini na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana yupo nchini China  na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo
   . Katibu wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi (kulia) akicheza muziki na mmoja wa wasanii wa kundi linalotumbuiza kwa kupewa fedha yoyote na anayevutiwa, kwenye eneo la Mji wa Kihitoria ya zaidi ya miaka 100 wa Jin Sha, jijini Chengdu, China.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi wa wajumbe walioko katika msafara wake, wakitazama baadhi ya bidhaa zinazouzwa, kwenye eneo la mji wa Kihistoria ya zaidi ya miaka 100 wa Jin Sha, mjini Chengdu, Machi 15, 2013. Kinana yupo nchini China  na ujumbe huo kwa ajili ya ziara ya mafunzo.
   Hu Qingzhong akichora katuni kwa ajili ya kuingizw kwenye simu ya mkononi, katika Kituo Cha Vijana wajasriamali wasomi cha Chengdu
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (aliyefunfa mikono kifuani), na baadhi ya wajumbe katika msafara wake, wakimtazama kwa makini kijana, Hu Qingzhong, aliyekuwa akichora katuni kwenye kompyuta kwa ajili ya kuwekwa kwenye simu za mkononi. Kinana na ujumbe wake walipotembelea kituo cha Wajasriamali wasomi cha Chengdu-High-Tech zone, jijini Chengdu, China, Machi 15, 2013.  Kinana yupo nchini China  na ujumbe huo kwa ajili ya ziara ya mafunzo. Picha zote  na Bashir Nkoromo

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania, David Mgwassa akizungumza na baadhi ya waombolezaji waliofika kumfariji kwa kufiwa mamake mzazi Suzan  Mgwassa, Kijitonyama, Dar es Salaam. Mwili utasafishwa leo kwenda kwao Manda, Ludewa kwa mazishi.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
  Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, wakitoa heshima kwa mwili wa mamake, David Mgwassa. Benny Kisaka (kulia), Juma Pinto (kushoto) na Juma Mabakila.
  Mjukuu wa marehemu Suzan Mgwassa, Isaack Mgwassa 9kulia0 akijadiliana jambo na maaskofu wa Kanisa la Pentekoste wakati wa msiba huo.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
                                                            Sehemu ya waombolezaji  Kwaya ya Kanisa la Pentekoste ikomboleza kwa nyimbo za injili wakati wa kuaga mwili wa marehemu Suzan
  David Mgwassa (wa pili kulia) akijadiliana jambo na maaskofu wa Kanisa la Pentekoste waliokwenda kuuombea mwili kabla kusafirishwa.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

  David Mgwassa akifarijiwa na mmoja wa waombolezaji
  Mgwassa akifarijiwa na mmoja wa waombolezaji
  Waombolezaji wakipata mlo
  Mgwassa akizungumza na Abdul Sisco (kushoto)
  Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Teddy Mapunda (aliyevaa miwani) akishiriki kwenye msiba huo (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa timu ya SADC inayosimamia kura ya maoni ya Katiba ya Zimbabwe akiwa kwenye mazungumzo na Rais Robert Mugabe kwenye Ikulu ya Harare, akitoa salamu za Mwenyekiti wa Troika ya SADC, Rais Jakaya Kikwete leo tarehe 15 Machi, 2013. Wananchi wa Zimbabwe wanapiga kura ya kukubali au kukataa Katiba mpya iliyoandaliwa na utatu wa vyama vya siasa nchini mwao kesho tarehe 16 Machi, 2013.

  0 0

  Kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo eneo Nane Nane mjini Morogoro kimekamatwa leo kwa wizi wa umeme baada ya kuharibu mita ya umeme kwa kuweka rezista kwa lengo la kupunguza upimaji wa mita ya umeme. Kituo hiki ni cha pili kukamtwa na kikosi cha ukaguzi toka makao makuu, ndani ya masaa mawili yaliyopita na kituo kingine ni cha Oil Com kilichopo eneo Kihonda
   Mafundi wa Tanesco wakitoa waya zote za umeme zilizokuwa zinapeleka umeme Oil Com baada ya kukamatwa kwa wizi wa umeme
   Kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo katika eneo  Kihonda Mkoani Morogoro kimekamatwa kwa wizi wa umeme na kikosi cha ukaguzi toka makao. Ni hujuma na ambazo kama zikiendelea ni hatari kwa uhai wa Shirika hili la umma.

   Meneja wa Kituo (kushoto) akipewa maelekezo baada ya kushuhudia mita ilivyoharibiwa
   Mita ya umeme iliyoharibiwa toka Kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo eneo Nane Nane.

   Mita iliyoharibiwa kwa kuwekewa rezista kupunguza upimaji wa mita
  Meneja wa kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo eneo Nane Nane ambaye ndiye meneja wa kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo eneo la Kihonda (kulia)akishuhudia mita ya umeme iliyoharibiwa ikijaribiwa.


  0 0


  Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI’s) kutoka Umoja wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) wanatarajia kuanza mkutano wa siku mbili jijini Dar Es Salaam kuanzia tarehe 18-19 mwezi machi mwaka huu chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Tanzania.
  Mkutano huo wa siku mbili utafunguliwa tarehe 18/03/2013 na Mwenyekiti wa sasa wa SARPCCO ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema na kufungwa tarehe 19/03/2013 na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Tanzania.
  Katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya operesheni za pamoja na ushirikiano baina ya SARPCCO na umoja wa Wakuu wa Polisi wa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO).
  Vilevile, mkutano huo utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na wakuu wa Polisi wa SARPCCO katika mkutano uliofanyika Zanzibar mwezi Septemba mwaka 2012.
  Mkutano huo pia utaambatana na vikao vya Kamati Tendaji za SARPCCO ambazo zinajumuisha wajumbe kutoka nchi wanachama katika nyanja za Sheria, Mafunzo na kamati tendaji inayoshugulikia mambo ya wanawake na jinsia ambazo zitajadiliana ili kutoka na maazimio ambayo yatapelekwa katika mkutano wa Wakuu wa Polisi wa SARPCCO mwezi Mei mwaka huu.
  Aidha, suala la michezo baina ya majeshi ya Polisi kwa umoja wa SARPCCO nalo litajadiliwa katika mkutano huo.

  Imetolewa na.
  Advera Senso-ASP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi (TZ).

  0 0
 • 03/15/13--12:01: Article 18
 • SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD 
  WAZEE WA KAZI
  GOOD NEWS FOR KENYA
  AIR CARGO TO NAIROBI 
  £2.80 per KILO! INCLUSIVE CLEARANCE
  ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN KENYA
  THIS PRICE IS INCLUSIVE OF 
  CUSTOMS CLEARANCE IN KENYA
  MZIGO UKIFIKA NAIROBI HAULIPI TENA PESA NYINGINE
  kama unataka kuagiza kitu au kufanya booking yoyote ingia kwenye website yetu au tupigie kwenye namba zifuatazo;
  CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
  SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
  HASSAN (RICHARD) +44 07405159255
  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

  0 0  Assalam akaykum
  Nimeona nichukue nafasi hii nitoe mapendekezo maana sijaona mwananchi kuchangia mawazo kutokana na matatizo yaliyopita ya mitihani Tanzania sasa kwa upande wangu nina haya naomba sana tena sana niwekee japokuwa ni marefu kidogo lakini nahisi ni jambo muhimu:

  Mfumo wa Elimu Ningependekeza ungekuwa hivi:

  Kuwepo na Tuition Resources (iwepo Online au hata maktaba zetu) ambayo itakuwa na mgawanyiko wa mambo makuu matatu (3) nayo ni haya:
   
  1.      1. Syllabuses (Silabas)
  2.      2. Lecture Guides (Muongozo wa Kusoma na kusomesha)
  3.   3.    (a) Specimen question papers. (Sampuli ya Maswali) (b) Past Question papers and Answers.(Maswali na Majibu ya Mitihani iliyopita)
  Mambo ya Nyongeza :
  ·         Kama kutakuwa na mabadiliko yoyote kwa mtihani ujao uelezwe hapa.(MFANO Masuala mangapi yanatakiwa yajibiwe yameongezeka au kupungua)
  ·         Kama kutakuwa na Mabadiliko au nyongeza  ya Syllabus vile vile ioneshwe hapa.
  ·         Ripoti ya Mtihani ambayo ieleze wapi wanafunzi walifanya uzuri na wapi bidii iongezwe na wapi walifanya vibaya.
  ·         Vidokezo vya kusoma (Reading Tips)
  ·         Listi ya Vitabu au website za kutafuta material zaidi (Reading lists)
  ·         Kuwepo na Manual au Mkusanyiko wote wa masomo  ambayo kama kutakuwa na mabadiliko yaelezwe kama nilivoorodhesha hapo juu wapatiwe wanafunzi kwa either bure au pesa kidogo walipie
  ·         Kuwepo na reward kwa wanafunzi waliofanya vizuri na utambulisho mfano watolewe kwenye majarida maalum ya elimu ambayo yatasambazwa bure au hata kwa fee ndogo.

  Ufafanuzi kidogo
   
  1.       Sylubuses : Zioneshe mgawanyiko wa masomo ambao mwanafunzi akitoka atatoka na ujuzi mfano somo la Biologia
  1.       Agriculture iwepo na core unit (masomo ya lazima) na optional zake asipandikizwe mwanafunzi mambo ya Anatomy au Biochemistry au biomechanics pamoja na masomo yanayohusu Agriculture, (information overload).
   
  2.       Lecture guides: ambayo itagawika kwa:
  (a) Learning outcomes (Mwanafunzi aelezwe umuhimu wa hicho unachomsomesha       
              kwanza kabla hata ya kwenda kwenye mada.
               (b)Indicative contents ( Ambazo zipo kwa number mfano  Somo la Human Resources  
               1.1Definition, 1.2.Work related stress ,1.3 Equality) Hii itamsaidia mtu kukumbuka   
                ambapo akijibu suala la mtihani kuwa topic hii ni topic ya 1.3. au 2.4.au hata  
               akitafuta material online yatamuonesha kuwa soma topic no.1.3 au 3.4 n.k
               (c)Examination tips (Muhimu sana unamueleza mwanafunzi atarajie swali la aina
                  gani katika topic hii na jibu la aina gani ajibu)
   
  3.        (a) Specimen Question papers ambazo zinakuwepo mwanzo wa mwaka kuonesha mwanafunzi atarajie masuala ya aina gani yatakuja katika mtihani sasa anajifanyia mara kwa mara kujibu maswali haya  kwa kutumia resources mbali mbali na pia zioneshe marks ambazo atapata kwa kila suala atakalojibu .
              (b)Maswali na majibu ya mtihani iliyopita,ni muhimu kwa kuwa unamjengea  
              mwanafunzi jinsi gani ya kujibu masuala au atarajie nini ,
   
  Hitimisho
  Wengi watasema mfumo wa maswali na majibu wanafunzi watakuwa hawasomi wata solve maswali tu,lakini sio kweli mfano yakiwepo maswali ya somo la Biologia tokea ya mwaka 2005 naamini kujibu mara kwa mara haya maswali yanakujengea confidence na ufahamu vile vile na mara nyingi elimu ni ile ile mambo madogo madogo tu yanaongezeka ambayo hata kwenye mitihani ya ulaya huwekwa kijiswali kidogo tu kimoja cha mark ndogo kutokana ni jambo jipya.
  Mfumo huu pia unatumika U.K mfano maswali ya interview unatakiwa uyasome na sio uwende interview kichwa kichwa,
  masuala ya driving lesson unakuwa na CD na vitabu ambayo kwenye mtihani wenyewe yanakuwa hayohayo
  Masuala ya uraia unapewa kitabu unasomeshwa hivo hivo hata masuala ya shule .
  Sasa tuchukue mfano wa Driving lesson unajiona unajibu tu maswali lakini utakapoanza kuendesha je halikujii swali ulosolve ukaona aha nilisolve hili swali kuwa round about nikae upande gani sasa je si ujuzi huu?
   
  Haya ndio nionayo mimi ila kila mtu ana mawazo yake
  Ahsanteni.

  Dr.Abdul AE 
  University of Huddersfield 


  0 0

  Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Mh. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa pamoja na ujumbe wa wafanya biashara kutoka Ujerumani walioongozwa Balozi wa Ujerumani nchini Klaus –Peter Brandes katika hafla ya kuzindua Showroom ya magari ya kampuni ya Alliance Autos inayouza magari aina ya Volkswagon ambapo pamoja na mambo mengine amepongeza hatua hiyo na kusema serikali iko bega kwa bega na wafanya biashara wabunifu na pia kuuhakikishia ujumbe kutoka Ujerumani kuwa serikali imeweka mazingira bora ya kuwekeza hivyo wasisite kujitokeza.
  Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp(kulia) wakifurahia hotuba ya Dkt. Mwakyembe.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo amesema kufuatia kupanuka kwa kampuni ya Alliance Autos na kuongezeka kwa wateja tumeonelea ni vizuri kufungua showroom mpya ya magari ya Volkswagon ambapo wateja wanaweza kuitembelea wakati wowote.
  Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akifurahia jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp (hayupo pichani) akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD. Kulia ni Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia wa Ujerumani. Kushoto ni Tender Manager wa CFAO Motors Bw. Marco Kahabi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun (wa pili kushoto).

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Wapiga picha za habari wa vyombo mbalimbali vya mkoa wa Morogoro wakiwa kazini wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la kitivo cha sayansi cha Chuo Kikuu cha Kiisalmu kilichopo katika mji huo uliokosa bahari tu. 

  Mkoa wa Morogoro ni mmoja kati ya mikoa iliyo na vyombo lukuki vya habari ikiwa ni pamoja na TV pamoja na redio,  na vinavyotoa ushindani mkubwa dhidi ya vyombo vya habari vya Dar es salaam. Wa pili kulia mwenye kibandiko ndiye mdau John Nditi wa Globu ya Jamii.

older | 1 | .... | 68 | 69 | (Page 70) | 71 | 72 | .... | 3284 | newer