Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

Grace Matata's debut album Nyakati is out


Ziara ya Rais wa Zanzibar Wilaya ya WETE, Pemba

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba,akiwa katika  ziara ya kikazi katika Mikoa ya huko Pemba,akianzia Mkoa wa Kaskazni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi mbali mbali na wana CCM,alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba,akiwa katika ziara ya kikazi katika Mikoa ya Pemba,akianzia Mkoa wa Kaskazni .
 ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein,akipokea  Ripoti ya utendaji kazi ya Mkoa wa Kaskazini Pemba,kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo Dadi Faki Dadi, katika ukumbi wa mikutano wa Jamhuri Hall,akiwa katika  ziara ya kikazi katika Mkoa huo iliyoanza jana kwa kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo
 Baadhi ya Viongozi  na Watendaji wa Ofisi za Mkoa wa kaskazini Pemba wakisikiliza Ripoti ya Utendaji kazi za Mkoa huo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa wa mikutano wa Jamhuri Hall, akiwa
katika  ziara ya kikazi katika Mkoa huo.
 Wajumbe  wakisikiliza Ripoti ya Utendaji kazi za Mkoa huo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein
Baadhi ya Viongozi  na Watendaji wa Ofisi za Mkoa wa kaskazini Pemba wakisikiliza Ripoti ya Utendaji kazi za Mkoa huo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa wa mikutano wa Jamhuri Hall, akiwa katika  ziara ya kikazi katika Mkoa huo

Basi la wanafunzi chupu chupu lilete janga leo jijini Dar kwa kufeli breki

0
0
 Basi la Kubeba wanafunzi la Shule ya Sekondari ya St. Anthony ya Mbagala jijini Dar es Salaam lenye nambari za usajili T 631 AZY (pichani kulia) leo majira ya saa kumi jioni,limenusurika kupiga mweleka kama si kuparamia magari ya watu wengine mara baada ya kufeli breki likiwa kwenye mteremko wa eneo la Mtongani kuelekea Africana,Mbezi Beach.

Basi hilo ambalo lilionekana kuwa kwenye mwendo kasi kiasi,lilishindwa kusimama wakati wa foleni iliyokuwepo kwenye barabara hiyo,hali iliyompelekea dereva wa Basi hilo kuchukua uamuzi wa kuikwepa foleni hiyo na kupita upande wa kushoto wa barabara kwa mwendo ambao hauzungumziki huku wanafunzi waliokuwemo ndani ya basi hilo wakisikika wakipiga mayoe ya kuhitaji msaada,hali iliyowafanya watu wengi waliokuwepo katika eneo hilo kulifuata basi hilo kwa kukimbia huku wazee wa boda boda wakiwasha vyombo vyao na kulifukuzia basi hilo huku wakiwa tayari tayari kwa kutoa msaada wowote utakao hitajika.

Ila kwa kuwa Mungu ni muweza wa kila jambo,Basi hilo lililweza kusimama baada ya kuligonga basi lingine (daladala lenye nambari za usajili T 254 BCR) kwa nyuma ambalo nalo inaonekana lilikuwa limesikaka barabarani hapo (haikufahamika mara moja sababu ya kusimama kwa basi hilo) na hapo ndipo walionekana wanafunzi hao wakishuka kwenye basi hilo huku wakiwa hawaamini kile kilichotokea.

Hakuna aliejeruhiwa kwenye tukio hilo.
 Wanafunzi hao wakiwa nje ya Basi hilo huku wakihadithiana jinsi hali ilivyokuwa wakati basi lao limefeli breki.
 Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa.
 Wengine walipoona mambo yameharibika kule mbele wakaona wachukue uamuzi mbadala wa kuvuka ng'ambo ya pili ya barabara.
 Jamaa wakilikimbilia basi hilo ili kwenda kuona litakapoishia.
 Wengine wakaona isiwe shinda,ngoja wapite pembeni kule ili wawahi waendako.
Bodaboda zikiwa tayari tayari stand by...

shule ya sekondari Tusiime yasaida watoto msimbazi centre

0
0
 Sista wa kituo cha msimbazi center katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya sekondari Tusiime iliyopo Tabata jijini Dar es salaam waliofika kituoni kwa ajili ya kuwatembelea watoto yatima kituoni hapo na kutoa michango yao ambayo imetolewa na wanafunzi wenyewe wakishirikiana na walimu wao pamoja na uongozi wa shule wanafunzi hao  ni wawakilishi kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha tano.
 Walimu na viongozi wa wanafunzi toka shule ya sekondari Tusiime wakitoa mchango wao wa vitu mbali mbali kwa sista mlezi wa kituo cha msimbazi center.
  Baadhi ya wanafunzi wakiwa na walimu wao Mwalimu Daniel Nanyalo na Mwalimu Venant Faustine Tusiime sekondari kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda msimbazi center kuwatembelea watoto wasio jiweza
Gilbert Mtei na Balbina Lwena waki onyesha upendo wao kwa watoto wa kituo cha msimbazi center.

Susan G. Komen Global Race for the Cure 2013

0
0


Hello Everyone,

First, I want to thank everyone for participating in last years Global Race for the Cure. Last year we had about 30 registered team members and we raised $1500 in donations. This year the race is on May 11, 2013. Our goal for this years race is to have at least 30 team members and to raise at least $1500 in donations. 

If you want to join Team Tanzania for this years race, you can register online on our team website. The registration fee is $40 for walkers. you can access our team website by clicking or copying and pasting the link below and clicking "Join Team Tanzania":


Even if you are not able to join us for this years race, you can help us reach our fundraising goal by giving a tax-deductible donation to the team. You can donate by going to the team website and clicking "Donate to this Team."

Please feel free to e-mail me at TeamTanzania2013@gmail.com if you need further information about registering for the race or donating to the team.  

Thank you
Nelleta Kassembe
Team Captain

NDUGU KINANA WAKIWA NANCHONG, CHINA

0
0
 KATIBU Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuhusu shughuli za  kilimo alipotembelea mji wa Dantong, Nanchong kwenye miradi ya kilimo kwa ajili ya kupambana na umasikini, Machi 16, 2013. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, akiwasalimia wazee katika kijiji cha mradi wa wakulima wa kupunguza umasikini cha Nanchong, jimbo la Sichuan, China, alipotembelea kijiji hicho, Machi 16, 2013. Anayemsalimia ni Ning Xiu (78). Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China, jimbo la Sichuan, Zhang Ning, wakitazama kazi za watoto, katika shule ya awali katika kijiji cha Dantong, wilaya ya Nanchong, Kinana na ujumbe wake walipotembelea miradi ya kilimo kwa ajili ya kupunguza umasikini, katika kijiji hicho, Machi 16, 2013.Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu Amina Makilagi, akitazama vifaa vya michezo ya watoto katika shule ya  awali ya Kijiji cha Dantong, jimbo la Sichuan, Msafara wa Kinana ambao Amina yumo, ulipotembelea kijiji hicho kuona shughuli za mradi wa kilimo wa kupunguza umasikini, Machi 16, 2013. Kinana yupo China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, na Watatu kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM , Khadija Aboud.
 Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman na akipata maelezo katika duka la kisasa na mazao ya chakula, katika kijiji cha  Dantong, wilaya ya Nanchong, jimbo la  Chengdu China, Machi 16, 2013. Duka hilo ni la mazao ya wakulima katika kijiji hicho kupitia mradi wa kupunguza umasikini Nanchong. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC.
Katibu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama moja ya mashamba makubwa ya wakulima walipo kwenye mradi wa kupunguza umasikini, katika Kijiji cha Dantong, Jimbo la Sichuan, China, Machi 16, 2013. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. Picha zote na Bashir Nkoromo.

Yanga yazidi kujikita kileleni

0
0
Picture
Yanga vs Ruvu Shootings katika Uwanja wa Taifa, Dar leo
Timu ya Yanga leo imeifunga timu ya Ruvu Shooting goli 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya VodaCom uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Goli hilo lilifungwa na Hamisi Kiiza “Diego” kunako dakika ya 48 ya mchezo na hivyo kuipa Yanga jumla ya pointi 48 katika ligi hiyo.


Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa kwenye kiwanja cha Manungu mkoani Morogoro, timu za Mtibwa Sugar na Coastal Union zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana 1-1 na hivyo kufikisha pointi 32 kila moja.



Coastal Union walipata goli lao katika dakika kwanza tu ya kipindi kupitia kwa Ibrahim Twaha “Messi”, goli ambalo lilidumu kipindi kizima cha kwanza. Mtibwa Sugar walisawazisha katika kipindi cha pili.



Hadi kufikia sasa, Azam FC inashikilia nafasi ya pili wakati Simba SC ipo katika nafasi ya tatu.


TAARIFA YA KAIMU MKUU WA MKOA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KITAIFA

0
0

Napenda  kuwafahamisha kuwa Mkoa wetu umepewa heshima na Wizara ya Maji kuwa Mwenyeji wa maadhimisho ya 25 ya Wiki ya Maji Kitaifa yatakayo anza tarehe 16 Machi, 2013 na kufika kilele tarehe 22 Machi, 2013.

1.   Shukrani

Napenda kuishukuru Wizara ya Maji kwa kutupa heshima ya kuwa wenyeji wa maadhimisho ya Kitaifa ya 25 ya Wiki ya Maji.

Aidha, navishukuru sana Vyombo vya Habari kwa kufika katika mkutano huu na kuwa tayari kutangaza mafanikio yaliyowekwa katika Sekta ya Maji.

Naamini maadhimisho haya yatakuwa chachu kwa wadau mbalimbali kuchangia kwa hali na mali katika ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji Mkoani wa Lindi.

2.   Utangulizi;    

Kila mwaka kuanzia mwaka 1988, Tanzania imekuwa ikiadhimisha Wiki ya Maji kuanzia tarehe 16-22 Machi kwa kuwahusisha wananchi na wadau wote wa maji. 

Kilele cha maadhimisho huwa ni tarehe 22 Machi ambayo siku hiyo inafahamika Kimataifa kuwa ni Siku ya Maji Duniani kwa mujibu wa Azimio Na. 193/47 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Uzinduzi utafanyika tarehe 16 Machi 2013 katika Kijiji cha Mtandi Wilaya ya Kilwa na Kilele cha Maadhimisho kitakuwa tarehe 22 Machi 2013 katika Manispaa ya Lindi kwenye Uwanja wa Ilulu.  Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho atakuwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.JAKAYA MRISHO KIKWETE.

Maadhimisho ya Wiki ya Maji ya mwaka  huu yataongozwa na Kauli Mbiu isemayo “MWAKA WA USHIRIKIANO WA MAJI KITAIFA”.

Madhumuni ya Maadhimisho;

Madhumuni ya Maadhimisho ya wiki ya maji ni  pamoja na:-

·        Kuwaelimisha wananchi kuhusu Sera ya Maji na majukumu yao katika kuitekeleza.

·        Kutathmini maendeleo ya Utekelezaji wa Programu ya  Maji, hali ya huduma ya maji na usafi wa mazingira na kuweka mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma na uhifadhi wa rasilimali za Maji.

·        Kuhamasisha wananchi na wadau wengine kushiriki  katika kupanga, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.

·        Kujenga mshikamano miongoni mwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Maji.

·        Kutoa ujumbe kwa wadau  kuhusu Kauli Mbiu ya Wiki ya Maji na Siku ya Maji Duniani.

Madhumuni  hayo yanalenga kuboresha  utoaji wa huduma  ya Maji, Usafi na Uhifadhi wa Mazingira, pamoja na usimamizi na utunzaji wa rasilimali za Maji nchini (vyanzo vya maji na miundombinu ya kufikisha huduma ya maji kwa watumiaji).

3.   Maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Maji mwaka 2013;

Maandalizi ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji yanaendelea vizuri na uzinduzi na kilele cha maadhimisho kitawahusisha viongozi wa Kitaifa. 

Maadhimisho ya mwaka 2013 yanakusudia kuwashirikisha wananchi katika:-

·        kupanga, kujenga, kuendesha na kufanyia matengenezo miradi ya maji na kuimarisha usafi wa mazingira,

·        kutunza vyanzo vya maji na kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi endelevu ya rasilimali za maji.

Matukio haya yataenda sambamba na kutoa ujumbe (maudhui) wa  Siku ya Maji Duniani ya mwaka 2013 ambao ni  “MWAKA WA USHIRIKIANO WA MAJI KITAIFA”.

Shughuli zitakazofanyika katika Wiki ya Maji hapa Mkoani Lindi ni pamoja na:-

·        Kuzindua miradi 3ya Maji vijijini ambayo ujenzi wake umekamilika.

Vijiji hivyo ni Mtandi (Wilaya ya Kilwa), Rondo Mnara (Halmashauri ya Wilaya ya Lindi) na Luchelegwa (Wilaya ya Ruangwa).

Miradi hii imetekelezwa kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji na wadau mbalimbali.

·        Kuzindua Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Maji katika Mji wa Lindi kutoka chanzo kilichopo katika eneo la Kijiji cha Sinde.

·        Kutakuwa na Mikutano ya Hadhara maeneo yote ya Uzinduzi

Miradi yote itakayozinduliwaitawanufaisha wananchi wapatao 134,108.

 4.   Kugharamia Maadhimisho;
Ili kuweza kugharamia maadhimisho ya Wiki ya Maji mwaka 2013, Wadau mbalimbali wameombwa kutoa michango ya hali na mali ili kufanikisha maadhimisho haya.

Maadhimisho ya kitaifa  ya Wiki ya Maji yanagharimiwa na Wizara ya Maji , Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mamlaka za Maji Safi na Maji taka nchini, Halmashauri, Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Kiserikali na yasiyo ya Kiserikali na Watumiaji Maji.

Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba wadau wote kutoa michango ya hali na mali ili kuweza kufanikisha maadhimisho haya ya Wiki ya Maji Kitaifa yatakayofanyika hapa Mkoani kwetu mwaka huu wa 2013.

 5.   Wito kwa Wananchi wa Lindi;
Nitoe wito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi kuwapokea na kuwakaribusha wageni wote ambao watakafika Mkoani kwetu kwa nyakati mbalimbali katika Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani. Kipekee ninawaomba Wananchi/Wakazi wa Manispaa ya Lindi kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania atakapowasili tarehe 21 Machi, 2013 na kuendelea kuwa nae mpaka siku ya Kilele cha Maadhimisho katika Uwanja wa Ilulu tarehe 22 Machi, 2013.



ngoma azipendazo ankal

0
0
Ngoma ya 'Love Come Down' ya Evelyn Champagne King ilikuwa moto!

Twanga Pepeta kusindikiza utambulisho Miss Tabata 2013 Pasaka

0
0
Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tabata 2013, watatambulishwa siku ya sikukuu Pasaka katika ukumbi wa Dar Wes Park, Tabata. 

Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga amesema jana kuwa utambulisho huo utasindikizwa na burudani kababembe kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”. 

Kalinga alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya fainali itakayofanyika Mei. 

Utambulisho wa Miss Tabata 2013 imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti 5 na Kitwe General Traders na kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

 Mratibu huyo alisema warembo 25 wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata. 

Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala baadaye mwaka huu. Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael (pichani katikati) ambaye pia ni Miss Ilala.

Serikali kuendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha utambuzi cha kiwanda cha simenti cha Tanzania (TPCC) kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun (kulia) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha ni Waziri wa Uchumi wa Ujerumani, Ms. Anne Ruth (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TPCC, Bw. Pascal Lessoine (wa tatu kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto).

TPSF yahamasisha umoja sekta binafsi

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Geofey Simbeye akisisitiza jambo kwa wanachama wa taasisi hiyo wa kanda ya ziwa katika mkutano maalumu wa uelimishaji na uhamasishaji wa muundo wa uwakilishi katika kongano ( clusters). Kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya TPSF Bw. Gideon Kaunda. Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Geofey Simbeye akizungumza na wanachama wa taasisi hiyo kutoka kanda ya ziwa katika mkutano maalumu wa uelimishaji na uhamasishaji wa muundo wa uwakilishi katika kongano( clusters) mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.

wilaya ya hai yaweka mikakati kupambana na ugonjwa mpya wa mahindi ulioibuka

0
0
Mtaalamu mtafiti wa kilimo Dk Peter Matowo akionyesha mmoja ya mmea wa mahindi uliothiriwa na ugonjwa mpya wa mahindi katika wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro

Mtaalamu wa kilimo kutoka wizara ya kilimo na chakula Bwana Kitenge akiwaonyesha aina ya mmea wa mahindi ulioathirika na ugonjwa hatari wa mahindi ambao umeingia katika baadhi ya mikoa hapa nchini



Na Mwandishi wetu Hai,Machi 17,2013

Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga amewataka viongozi kuanzia ngazi  za vijiji,kata,tarafa mpaka wilayani pamoja na wataalamu wakiwemo maofisa ugani kuhakikisha wanatumia mwezi huu wa mwanzo wa mvua za masika kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mbinu za kukabiliana na ugonjwa mpya na  hatari wa mahindi.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo wakati anafungua kikao cha dharura cha kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo  kilichowashirikisha watalamu wa kilimo kutoka vituo vya utafiti nchini pamoja na wadau,viongozi wa ngazi mbalimbali,maofisa ugani wa vijiji,viongozi wa dini pamoja na viongozi wa siasa wakiwemo madiwani.

Makunga ameeleza baada ya kikao hicho viongozi wa ngazi ya vijiji wanatakiwa kuitisha mikutano ya vijiji na wale wa kata kukaa katika vikao vya maendeleo ya kata ndani ya wiki mbili ili kuweka mkakati wa kuelimisha wananchi jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari wa mahindi unaofahamika kama Lethal Necrosis Disease

Aidha amewaagiza wataalamu wa ugani kutumia muda wa siku saba kufanya tathimini ya maeneo yao endapo kuna ugonjwa huo na kuwashilisha taarifa hizo katika vikao vya Halmashauri za vijiji na Kamati za maendeleo za kata na baadaye mwisho wa mwezi katika halmashauri ya wilaya ya Hai.

Ameonya kuwa endapo kila mdau atazembea katika kuhakikisha anatimiza wajibu wake kuwepo kwa ugonjwa huo litakuwa janga kubwa kutokana na idadi kubwa ya wananchi katika wilaya hiyo kutegemea zaidi mahindi kwa matumizi ya family,kipato pamoja na malisho ya mifugo

Makunga pia ameitaka halmashauri ya wilaya kuhakikisha inasambaza kwa wingi vipeperushi vinavyohusiana na ugonjwa huo ili elimu iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi badala ya kuendelea kubaki navyo katika maofisi.

Awali mtaalamu mtafiti kutoka kituo cha utafiti wa kilimo cha Selian cha Arusha Dk Peter Matowo ameeleza kuwa madhara makubwa ya ugonjwa huo ni pamoja na uharibifu shambani unaoweza kufikia asilimia mia moja kwa mimea kufa na kukosa mavuno,magunzi na punje zilizoathirika kuwa na sumu ya magonjwa hatari ya ukungu kwa binadamu na kutofaa kwa malisho ya mifugo.

Ameeleza kuwa ugonjwa huo unaenezwa na virusi na kwamba hauna tiba wala mbegu kinzani na hivyo njia pekee ya kudhibiti ni kwa wakulima kuzingatia kanuni zinazoshauriwa zikiwemo za kung’oa mara moja mimea iliyoathirika,kupiga dawa za kuua wadudu aina ya thrips,beetles,leafhoppers na aphids waenezao ugonjwa huo,kupanda mazao mara tu mvua zinyeshapo pamoja na kilimo cha mzunguko wa mazao.

Ugojwa huo ulianza nchini Marekani mwaka 1976 na kuingia katika nchi za Kenya mwaka 2011 na Tanzania mwaka 2012 na kuenea katika wilaya za mkoa wa Kilimanjaro,Arusha na Mwanza

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MITI KUFANYIKA TANZANIA - TAREHE 21 MACHI 2013

0
0

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Siku ya Kimataifa ya Miti (World Wood Day) ambayo huadhimishwa tarehe 21 Machi kila mwaka. Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Khamis Suedi Kagasheki atakuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ambayo yatafanyika kwenye Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.

Siku ya Taifa ya Miti huadhimishwa duniani kote kuhamasisha watu kuhusu manufaa ya miti katika maisha ya kila siku ya binadamu ili waweze kuitunza na kuitumia kiuendelevu.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni: Mbinu za kitamaduni za kutumia miti ni nzuri (A cultural approach to achieve wood is good).

Tarehe 21 Machi itakuwa ni siku ya kilele cha maadhimisho hayo ambayo yataadhimishwa kwa siku nne mfululizo tangu tarehe 19 hadi 22 Machi kwa kufanya shughuli mbalimbali zilizopangwa.

Baadhi ya shughuli hizo ambazo zitaanza tarehe 19 Machi katika viwamja vya Karimjee ni:

·         Maonyesho ya bidhaa zitokanazo na miti;

·         Mashindano ya bidhaa zitokanazo na miti, za hapa nchini na za kutoka nje;

·         Kutoa na kujadili mada kuhusu Utamaduni wa Kupenda Miti;

·         Kupanda miti katika wilaya ya Kisarawe;

·         Kutembelea VETA Chang’ombe;

·         Mashindano ya uchoraji kwa watoto.

Maadhimisho haya huratibiwa na Chama cha Kimataifa cha Utamaduni wa Miti (International Wood Culture Society) ambacho kiliasisiwa nchini Marekani mwaka 2007 kwa nia ya kuwatia moyo watu wajenge utamaduni wa kupenda miti.

Mwaka huu Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa siku Siku ya Kimataifa ya Miti kwa kuwa imeonyesha juhudi za kuwashirikisha wananchi wake katika kuhifadhi na kupanda miti.

Wananchi wanakaribishwa kuhudhuria mikutano na maonyesho yote yaliyopangwa katika viwanja vya Karimjee maana hakutakuwa na kiingilio chochote.

[MWISHO]

George Matiko

MSEMAJI

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

17 Machi 2013


introducing rasello

0
0
Hi,

I wanted to take this chance to introduce Rasello as a system that is changing how Businesses and Organizations automatically manage and retain their clients better. 

Being a cloud based software, Rasello simplifies how businesses manage client information, understand their trends using Rasello analytics and communicating to them more strategically via SMS and Email.

Please visit rasello.com/aboutus to learn more or use it for free rasello.com/register to manage up-to 100 clients before upgrading to our premium accounts. If needed, i can also schedule a call to tell you more about the system.

Malindi yainyuka timu ya Mundu Bao 2-1 Zanzibar

0
0
Timu ya Malindi ya Zanzibar huku ikiwa pungufu kutokana na mchezaji wa ke mmoja kulimwa kadi nyekundu mapema dakika za mwanzo wa mchezo, jana iliibuka mshindi kwa kuinyuka Mundu mabao 2-1 ligi kuu ya Grand Malt ya Zanzibar kwenye uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Mundu, Ulrasa Juma akimtoka mlinzi wa Malindi, Nadir Rashid (kushoto) wakati wa mchezo wa wa ligi kuu ya Grand Malt,Zanzibar uliochezwa jana jioni kwenye uwanja wa Mao Tse Tung.
Abdalla said wa Malindi (kushoto) na Thabit Khamis wa mundu wakiwania mpira.

Urembo ni asili ya Mwafrika

taarifa toka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo

IGP MWEMA KUFUNGUA MKUTANO WA MAKACHERO WA POLISI JIJINI DAR

0
0
Na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi.

Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI’s) kutoka Umoja wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kesho jumatatu wanatarajia kuanza mkutano wa siku mbili jijini Dar Es Salaam chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa Jeshi la Polisi Advera Senso amesema Mkutano huo wa siku mbili utafunguliwa na Mwenyekiti wa sasa wa SARPCCO ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema.

Amesema katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya operesheni za pamoja na ushirikiano baina ya SARPCCO na umoja wa Wakuu wa Polisi wa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO).

Advera amesema mkutano huo pia utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na wakuu wa Polisi wa SARPCCO katika mkutano uliofanyika Zanzibar mwezi Septemba mwaka 2012.

Aidha amesema Kamati Tendaji za SARPCCO ambazo zinajumuisha wajumbe kutoka nchi wanachama katika nyanja za Sheria, Mafunzo na kamati tendaji inayoshugulikia mambo ya wanawake na jinsia zitajadiliana ili kutoka na maazimio ambayo yatapelekwa katika mkutano wa Wakuu wa Polisi wa SARPCCO mwezi Mei mwaka huu.

Tayari wajumbe wa mkutano huo wameanza kuwasili hapa jijini Dar Es Salaam kuhudhuria mkutano huo.

RAI YA JUMAPILI TOKA KWA BARAKA WA CHIBIRITI

0
0
Chakula kizuri kuliko vyote duniani ni: UPENDO.
Sahani yake nzuri kuliko zote ni: UAMINIFU.
Mchuzi wake nzuri ni; HESHIMA.
Kachumbari yake nzuri ni; AMANI.
Utamu wake ni; KUKUMBUKANA.
- Nami nawakumbuka sana ninyi nyote na kuwatakieni Jumapili njema!
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images