Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

RIDHIWANI KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA MGOMBEA UNEC, NJOMBE

$
0
0
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM-NEC), Ridhiwani Kikwete akitoa salamu za CCM, wakati wa mazishi ya, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, marehemu Christian Fwalo ambaye alikuwa akiwakilisha mkoa wa Iringa mwaka 2007-2012,  katika makaburi ya Kijiji cha Ihalula, mkoani Njombe juzi. Fwalo pia alikuwa mgombea wa NEC, ili kuziba pengo la marehemu Lupyana Fute aliyefariki mwak jana. (NA MPIGAPICHA MAALUMU)


WANAFUNZI 84 WA PROGRAMU MAALUMU YA DIPLOMA YA UALIMU UDOM MBARONI KWA TUHUMA ZA KUHAMASIHA MAANDAMANO MKOANI DODOMA

$
0
0
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 84 wa chuo Kikuu UDOM kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo Dodoma Mjini leo tarehe 14.01.2015 majira ya 05:30hrs.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – (SACP) ameeleza kuwa chanzo cha wananfunzi hao wa programu maalum ya Diploma ya Ualimu kufanya uhalifu huo ni kikao walichofanya wananfunzi hao tarehe 13.01.201 wakidai kuongezewa posho ya chakula na kwamba hata kiasi ambacho wanapewa wamechelewa kupewa.

Hata hivyo uongozi wa Chuo uliwaeleza kuwa wenye mamlaka ya kuzungumzia swala la kuongezewa posho ni Bodi ya Mikopo na siyo chuo. Hivyo walitakiwa kufuata taratibu za kuwasilisha madai yao. Pia walielezwa kuwa hundi kwa ajili ya fedha za posho zao zimeshasainiwa na kuwasilishwa Benki ili waweze kuanza kupewa posho zao.

Wanafunzi hao  hawakuridhika na usiku wakaanza kuhamasishana kufanya maandamano jambo ambalo ni kosa kisheria. Wanafunzi hao wamehojiwa kulingana na ushahidi ambao umekusanywa na wamefikishwa mahakamani kwa kosa la Kufanya Maandamano yasiyo na kibali. Viongozi waliohamasisha uvunjifu huo wa sheria baadi wamekamatwa na baadhi wanaendelea kutafutwa ili nao waweze kuchukuliwa hatua stahiki. Ushahidi uliokusanywa unaonyesha jinsi viongozi hao wameshiriki kuhamasisha kupitia vikao rasmi na visivyo rasmi, katika vikundi, kupita katika mabweni na kutuma sms.

Kamanda MISIME ametoa wito kwa Wanafunzi hao kutumia taratibu zilizowekwa na Serikali na Chuo kuwasilisha malalamiko yao ngazi kwa ngazi na siyo kufanya vitendo vya kuvunja sheria ambavyo vitawasababishia kukamatwa. Endapo watafanya hivyo wasije kulaumu mtu kwani hatua zitachukuliwa kulingana na Sheria inavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma leo.
Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa kwenye gari ya polisi baada ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma leo.

SIMBA WAREJEA DAR NA KOMBE LA MAPINDUZI

$
0
0
Golikipa chipukizi wa Timu ya Simba Sc,Manyika Peter ‘Manyika Jr’ (wa pili kushoto) wakiwakabidhi Kombe Mashabiki wa timu hiyo mara baada ya kuwasili kutokea visiwani Zanzibar kwenye Mashindano ya Mapinduzi Cup,ambapo Simba waliibuka mabingwa.
Mashabiki wa timu Simba SC wakishangilia ubingwa wao.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na Bakari  Issa ,Globu ya Jamii Dar

Klabu ya Soka ya Simba leo hii imerejea jijini Dar es Salaam toka visiwani Zanzibar ambapo imeibuka kinara wa Kombe la Mapinduzi jana Januari13 katika mchezo uliopigwa usiku katika uwanja wa Amaan.

Akizungumza  mara baada ya kuwasiri jijini Dar es Salaam,Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Klabu ya Simba,Juma Ngambili amesema  vijana wamewapa  mashabiki wao kitu wanachokitaka licha ya kupata ushindi kwa njia ya mikwaju ya penalty 4-3 na kusema kuwa mashabiki wasubiri mambo mazuri toka kwao.

“Tumeupokea ushindi kwa mikono miwili,na tumewapa wapenzi wetu kitu wanachotaka na tunawasihi mashabiki wasubiri mambo mazuri toka kwetu,”alisema Ngambili

Aidha,Ngambili amewatoa hofu mashabiki wa Klabu ya Simba katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na kuwaambia kuwa watakuwa vizuri kwa kuanzia na mchezo unaowakabili siku ya Jumamosi dhidi ya Ndanda.

Kwa upande wake nahodha wa Simba,Nassor Masoud ‘Chollo’ amesema mchezo wao wa fainali dhidi yao na Mtibwa Sugar ulikuwa mgumu na kusema kuwa fainali ni fainali licha ya kuibuka na ushindi.Naye,Golikipa chipukizi wa Klabu hiyo,Manyika Peter ‘Manyika Jr’ amesema siri ya mafanikio yakwake na ya Klabu ni kujituma zaidi na amewaomba mashabiki wa Simba kuiunga mkono klabu yao.

“Katika mchezo wa jana nilitolewa kwenye dakika ya 90 naamini kama Kocha angeniacha nidake mikwaju ya penalti ningedaka,tumenyakua Kombe la Mapinduzi kutokana na wachezaji tulijituma na nawasihi mashabiki wetu kutuunga mkono. 

timu ya wataalam kutoka wizara ya uchukuzi watembelea kituo cha uongozaji ndege Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere (JNIA)

$
0
0
Meneja wa Kitengo cha taarifa za Usalama wa Usafiri wa Anga, Bw. Deodore Mushi akitoa maelezo ya namna ya mashine mbalimbali zinazotumika katika chumba maalum cha kutolea taarifa za usafiri wa Anga zinavyofanya kazi, kwa wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea katika ofisi hizo leo asubuhi kufanya tathimini ya utoaji wa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Wa Kwanza kulia ni Afisa Usafirishaji kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Biseko Chiganga (aliyevaa koti jeusi), wa pili kushoto kwa Chiganga ni Afisa Usafirishaji, Bw Benjamin Mbimbi na tatu kutoka kushoto ni Afisa Usafirishaji, Bw. Said Marusu.
Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo, akifafanua jambo kwa wataalamu kutoka Wizara ya Uchukuzi, waliotembelea kituo cha kuongozea ndege leo asubuhi kufanya tathmini ya utoaji wa huduma katika usafiri wa Anga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).
Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo akiwaonyesha wataalamu kutoka Wizara ya Uchukuzi, karatasi inayoonyesha aina ya ndege, mahali inapokwenda na muda itakaotumia inakokwenda, katika kituo cha uongozaji ndege kilichoko Katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere leo asubuhi wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho.
Meneja wa Kitengo cha Uongozaji Ndege, Mwanajuma Kombo (mwenye kilemba chekundu), akiwaelezaa wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, namna waongoza ndege wanavyotumia rada na kuelekeza marubani sehemu za kupita, wakati wataalam hao walipotembelea kituo hicho leo asubuhi kufanya tathmini ya utoaji wa huduma katika usafiri wa anga katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. (Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).

BREAKING NYUZZZZ...: PCCB YAANZA KUWABURUZA WASHTAKIWA WA ESCROW MAHAKAMANI

$
0
0
Watu  wawili Rugonzibwa Mujunangoma na Theophillo Bwakea wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka ya rushwa baada ya kupokea mgao wa Sh. Milioni 485.1 kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow walizohamishiwa na James Rugemalira.

Katika kesi ya kwanza, aliyekuwa Mwanasheria wa Mamlaka ya Vizazi na Vifo (Rita) Mujunangoma ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Sheria Wizara Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Emmilius Mchauru.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai akisaidiana na Max Ari, ulidaiwa kuwa Februari 5, mwaka 2014 katika benki ya Mkombozi iliyopo Ilala jijini, mshtakiwa akiwa Mkuu wa Sheria wa wizara hiyo, alipokea rushwa.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea rushwa ya Sh. Milioni 323.4 kama zawadi kupitia akaunti yake namba 00120102062001 kutoka kwa Mshauri binafsi wa kimataifa na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL,James Rugemalira baada ya kuwa mjumbe katika menejimenti ya Rita wakati wa machakato wa kuipitisha IPTL kuiuzia Tanesco umeme.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea zawadi hiyo kama ofisa wa muda wa kushughulikia masuala ya IPTL.

Mshtakiwa alikana mashitaka yake.

Swai alidai kuwa upande wa Jamhuri hauna pingamizi la dhamana na kwamba mahakama ijielekeze katika hati ya mashitaka fedha anazodaiwa kuchota mshtakiwa.

Hakimu Mchauru alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kujidhamini kwa Sh. Milioni 160 taslimu au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo ya fedha.

Pia wadhamini wawili wanaofanyakazi serikalini watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni 10 na mshtakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam, bila kibali cha mahakama.

Mshtakiwa alitimiza baadh ya masharti ya dhamana ambapo hakimu alisema mahakama imempa dhamana ya muda hadi Januari 16, mwaka huu hati za mali zake zitakapohakikiwa.

Katika kesi ya pili, aliyekuwa mjumbe wa kitengo cha kuidhinisha Tanesco kununua umeme wa IPTL, Wizara ya Nishati na Madini, Injinia Bwakea kwa sasa mtumishi wa Wakala wa Umeme Vijijini(REA), alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.

Swai alidai kuwa Februari 12, mwaka 2014 mshtakiwa akiwa Injia Mkuu wa REA, alipokea rushwa ya Sh. Milioni 161.7 kupitia akaunti namba 00410102643901 ya Tegeta Escrow kama zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Rugemalira.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea zawadi hiyo baada ya kuwa mjumbe aliyeandaa sera zinazohusu sekta binafsi kuzalisha na kuuza umeme kwa Tanesco.

Mshtakiwa alikana mashitaka yake.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana na kwamba upelelezi umekamilika.

Hakimu Moshi alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka serikalini au wanaofanyakazi katika taasisi zinazotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni 20 kila mmoja.

Pia alisema mshtakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam,  bila kibali cha mahakama.

Mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kesi yake itatajwa Januari 26, mwaka huu.

Jana saa 2:00 asubuhi katika viunga vya mahakama ya Kisutu, watumishi na watu mbalimbali waliingia katika eneo hilo huku kukiwa na minong’ono kwamba wanaotuhumiwa ufisadi wa Escrow watafikishwa mahakamani hapo.

Pia waandishi wa habari waligawanyika katika makundi tofauti huku wakijadili na kutafatuta wadau wao kujua kuhusu ujio wa watuhumiwa hao.

mapema jana saa 5:42 asubuhi vigogo hao walitinga mahakamani hapo na kwenda kusomewa mashitaka yao yanayowakabili.

WATANZANIA WAASWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA UWEKEZAJI

$
0
0
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, Soud Ahmed Al-Rahili akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii ,Dar

Watanzania wametakiwa kuonyesha ushirikiano katika sekta ya uwekezaji ili kuweza kuwavutia wawekezaji wa nje kuwekeza nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, Soud Ahmed Al-Rahili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati walipokuwa wakijadili masuala ya uwekezaji baina ya nchi ya Tanzania na Oman.

Al-Wahili amesema bidhaa za Tanzania zinazotarajiwa kupelekwa nchini Oman ni pamoja na nyama ya ng’ombe (Nyekundu) na Asali.Vitu hivyo vimekuwa na fursa katika soko la Oman hali ambayo watanzania waongeze juhudi ya kuzalisha kutokana na soko hilo kuwa pana na Tanzania ni nchi pekee inayoweza kunufaika na soko hilo.

Aidha  amesema  sekta ya uwekezaji ni pana kati ya Oman na Tanzania na ni wakati mwafaka kutumia fursa ya uwekezaji.

sekeseke la bei za filamu za bongo movie ndani ya danga chee ya michuzi tv part II

sekeseke la bei za filamu za bongo movie ndani ya danga chee ya michuzi tv part I


HASHIM KAMBI KUONGOZA NYOTA BONGO KATIKA FILAMU YA CPU

$
0
0
Hashim Kambi ‘Ramsey’
 Msanii mkongwe katika tasnia ya filamu za Bongo Movie Hashim Kambi ‘Ramsey’ ni moja kati ya wasanii wakubwa Bongo ambaye atawaongoza wasanii nyota na wakongwe katika filamu kubwa ya CPU inayotarajiwa kuingizwa katika DVD baada ya kuonyeshwa katika majumba ya sinema ndani na nje ya nchi.

Filamu ya CPU ni moja ya kazi kubwa sana kutengenezwa na watayarishaji wa ndani na kushirikisha wasanii zaidi ya 200 na  ni filamu  yenye ubora wa kipekee ambayo awali ilionyeshwa katika ukumbi wa sinema Century Cinemax Mlimani City jijini Dar es salaam kwa siku 10 mfululizo na kuacha gumzo kwa wapenzi wa sinema.
Dude
Kwa mara ya kwanza itauzwa katika DVD kwa wapenzi wa filamu walioshindwa kuingia katika majumba ya sinema ilipoonyeshwa  ili waweze kushuhudia teknolojia ya hali ya juu kutumika Bongo na kuwavutia wengi mtaani kwetu ambako ndio soko la filamu za kibongo lilipo.
CPU inawakutanisha wasanii nyota na wakongwe na Kulwa Kikumba ‘ Dude’, Richard Mshanga ‘Masinde’, Dotnata, na nyota wengine kibao ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya filamu wakiongozwa na Hashim Kambi ‘Ramsey’ msanii aliyejijengea mashabiki wengi.

THE FIRST ANNUAL AFRICA DAY 2015 TO BE HELD IN COVENTRY, UK

$
0
0
The  first  annual  African  Day 2015 in Coventry  West midlands to l be   celebrated by many African communities in  the  West  Midlands  is planned to be held on  the 19/20th June  2015  in  Coventry. 
African Day 2015  will  help raise political, social, cultural and  economic  awareness in African communities across West Midlands  especially  Coventry.  The establishment of an annual celebration of Africa Day  is designed to ensure that everyone in  the  community is aware of the invaluable contributions and achievements of African communities in West midlands  and  UK  as  a whole..  
 Originally, It has been a source of information about the struggles for liberation and development. But this year’s theme is  DEVELOPMENT THROUGH DIVERSITY. We  intend  to high  light the  social,  cultural and  Economic  aspects  of  the  African  Diaspora  in  Coventry- West Midlands. We  also  intend  to   honour  and  encourage Diaspora  achievements that  contributes  towards  development  in the  region.This  will  be  possible  with  the  support  of  African  Missions  in  the  UK
Events include:

Formal gatherings with panel discussions, street marches(mini carnival)/Market stalls, speeches by political, cultural ,economic  and social leaders, special university lecture at Coventry  University, rallies featuring cultural entertainment,  poetry, and speakers, the  African  Literature  and  book festival-which  is a lively and interactive panel discussions, where experts will discuss a range of topics to reflect the dynamic changes that are taking place in contemporary African writing.
CREATING GREAT CHARACTERS-How do writers create characters that make stories come alive? Would you or a member of your family make a good hero or heroine? A creative writing workshop for all the family.
THE ART OF STORY-TELLING-What are the essential ingredients of a story? What are the main steps in making one? Come and learn the basics and create a small piece of your own! Aimed at 13-19 year olds.
STORYTIME-Explore the rich and diverse cultures, peoples and places of Africa through these interactive story-telling workshops aimed at 4-7 and 8-12 year olds. Parents welcome too.
 The   event  will   also  host  the  Ambassador’s  Forum ,  which  will  be  an  interactive  forum  focusing  on Tourism,  culture  the significant  economic  growth performance  and  challenges recently  recorded in  Africa, with  particular  emphasis  on  the  contribution  of  the  Manufacturing   sector, to  further  strengthen intra  Africa trade .In  attendance e will be   Ambassadors  and  High  commissioner  accredited  to  the  court  of  St.  James in the UK and Northern Island.
An  exhibition  showcasing  products  and  services  from  Africa   based   small  and   medium  enterprises, large  industries  and  support institutions  will  be  part  of  the  whole  program.
This   event  is  jointly  organised  by  Newdeal  Africa, Ben  Television and  Coventry  City  Council 


INQUIRIES: Email: newdealafrica@yahoo.co.uk

WEAR SWAHILI DESIGNS BY MARIAM IKOA @ DAR FREE MARKET

$
0
0
IMG-20150114-WA0074
Some men shirts and ladies outfit in her own design. The design collection is called WEAR SWAHILI. Her main goal is to promote our own fabric in a modern way and comfortable way. Any age can wear and still look stylish at an effective cost price.
These are a few but also we uniforms in African Attire. Pillow cases, Table mats and throws by order.
Asanteni sana na Karibuni.
The shop is located at Dar Free Market, Masaki 1st Floor, Shop No. 5 or Mobile no +255 784 670089
IMG-20150114-WA0075IMG-20150114-WA0076IMG-20150114-WA0077

ONDOA KITAMBI KWA SIKU KUMI NA NNE!!!

$
0
0
Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic ni wauzaji wa dawa mbalimbali za asili. Tunayo dawa nzuri ya asili inayo ondoa kitambi na kulifanya tumbo lako kuwa flat kabisa ndani ya siku kumi na nne.

Dawa ni ya asili kabisa " Pure Herbal", haijachanganywa na kemikali yoyote na haina side effects kwa mtumiaji.

BEI YAKE NI SHILINGI ELFU HAMSINI TU (Tsh 50,000/=)

Kwa wasio weza kufika ofisini kwetu tunawapelekea dawa mahali walipo (DELIVERY).

Kwa wateja wa mikoani, tunawatumia dawa kwa njia ya mabasi, kwa wateja waliopo Zanzibar tunawatumia dawa kwa njia ya meli na kwa wateja waliopo nje ya Tanzania, tunawatumia dawa kwa njia ya posta au DHL.

Pia tunayo dawa bora kabisa ya nguvu za kiume iitwayo JIKO ambayo inatibu na kumaliza kabisa tatizo la nguvu za kiume ndani ya siku thelathini.

Vile vile tunayo dawa ya asili inayosaidia kurudisha afya na mwili kwa mtu aliye dhoofika kwa magonjwa mbalimbali.

Tunapatikana jijini DarEs salaam,katika eneo la Changanyikeni karibu na Chuo Cha Takwimu.

Kufika ofisini kwetu, panda daladala za UBUNGO-CHANGANYIKENI kisha shuka kituo cha TAKWIMU halafu tembea hatua ishirini mbele kisha tazama upande wako wa kulia.

Kwa maelezo zaidi,wasiliana nasi kwa simu 0766538384 na kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea website yetu kwa kubonyeza hapa.

NYALANDU AKARIBISHA WAFANYABIASHARA WA SAUDI ARABIA KUWEKEZA SEKTA YA UTALII NCHINI

$
0
0
Na Pascal Shelutete, TANAPA 
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Saudi Arabia kuwekeza katika sekta ya utalii nchini ambayo ina fursa nyingi za uwekezaji. 
Mhe Nyalandu alitoa wito huo kufuatia mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara ya Saudi Arabia Dk. Abdulrahman Al-Zamil yaliyofanyika Riyadh, Saudi Arabia jana. 
 Waziri Nyalandu ambaye anaongoza ujumbe wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Saudia alibainisha kuwa mazingira ya uwekezaji nchini yanavutia na kutaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa hoteli na loji za kisasa zitakazoweza kuvutia watalii wengi zaidi katika maeneo ya mijini pamoja na ndani ya maeneo ya uhifadhi. 
 Alisema kuwa utalii wa Tanzania unakua kwa kasi nzuri kutokana jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kutangaza vivutio vya utalii na kuwa juhudi hizo lazima ziende sambamba na upatikanaji wa huduma bora za malazi. 
“Upatikanaji wa huduma nzuri za malazi ya bei nafuu utasaidia kuvutia watalii wengi zaidi nchini na kwa maana hiyo tunawakaribisha kuja kuzitumia fursa zilizopo ili kuweza kukuza uchumi wa nchi yetu”, alisema Nyalandu. 
 Waziri Nyalandu ambaye anaongoza ujumbe wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Saudia, alisema kuwa Tanzania ni ya pili ulimwenguni baada ya Brazil kwa kuwa na vivutio vizuri vya asili vya utalii na kuwa rasilimali hizi zinapaswa sasa kutumiwa vema ili kuinua uchumi na njia pekee ni pamoja na kuvutia wawekezaji na mitaji kutoka Saudia ili kufikia azma hiyo. Kwa upande wake Dk. Al-Zamil aliahidi kuwashirikisha wafanyabiashara wenzake kutikia wito huo na kwa kuanzia timu ya wafanyabiashara pamoja na mawakala wa utalii watafika nchini katika siku chache zijazo ili kuona namna gani wataweza kuzitumia fursa zilizopo kikamilifu. 
Aidha, katika eneo la utalii Al- Zamil alisema kuwa Chemba yake itafanya kila liwezekanalo kubadilisha mtazamo wa Wasaudia wanaotembelea kwa wingi maeneo mbalimbali ya utalii duniani ili waweze kuitembelea Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana nchini. 
 Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru alisema kuwa serikali itaandaa Kongamano Maalum la Uwekezaji nchini Saudi Arabia ili kuweza kutangaza fursa mbalimbali zzilizopo nchini ambazo zikitumika vema zinaweza kuinua uchumi wa taifa. 
 Hivi sasa Tanzania inategemea idadi kubwa ya watalii kutoka Mataifa ya Ulaya na Amerika na kwamba japokuwa idadi ya watalii kutoka nchi za kiarabu haizidi 15,000 kwa mwaka, bado jitihada za utangazaji na uwekezaji zikifanywa vizuri idadi ya watalii kutoka mataifa ya kiarabu itaweza kuongezeka nchini. 
Ujumbe wa Tanzania unajumuisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli, Waziri kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Mchingaji Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo.
 Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa tano kushoto) ukiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudia Dk. Abdulrahman Al- Zamil (wa sita kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya pande mbili jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine pichani kutoka kushoto ni pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori Herman Keraryo; Mkurugenzi Mkuu TANAPA Allan Kijazi; Mhe James Lembeli; Mhe Peter Msigwa; Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru pamoja na maafisa kutoka Chemba ya Biashara ya Saudia.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa pili kushoto) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudi Arabia Dk. Abdulrahman Al-Zamil (wa tatu kushoto) jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mshauri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudia Mohammad Sulayem; Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kushoto) katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudi Arabia Dk. Abdulrahman Al-Zamil jijini Riyadh, Saudi Arabia. 
 Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa (kushoto) akikaribishwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudia Dk. Abdulrahman Al-Zamil jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli (kushoto) akikaribishwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudia Dk. Abdulrahman Al-Zamil jijini  Riyadh, Saudi Arabia. Picha na Pascal Shelutete, TANAPA

RITTA KABATI awataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu

$
0
0
   Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI

Na Mariamu Matundu, Iringa 

Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI  amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
KABATI ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
KABATI amesema kuwa wanawake wawemstari wa mbele kuchukua fomu za kugombea na kwamba wasikatishwe tamaa na baadhi ya watu wanaodhani kwamba wanawake hawawezi kugombea na kuongoza katika nafasi mbalimbali.
Aidha ameongeza kuwa Jamii iachane na mitazamo tofauti kwa wanawake wanao jitokeza kugombea nafasi za uongozi na kuwaasa wanawake wawe na misimamo pindi wanapoingia madarakani, kujiamini na kutokubali
kutumiwa kama chombo cha starehe.
Mbali na hayo KABATI amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Ameendelea kusema kuwa vijana wajotokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.


JK meets Millicom International Cellular SA Executive Vice President for Africa, Mr Arthur Bastings

$
0
0
  President Jakaya Mrisho Kikwete chats  with the Millicom International Cellular SA Executive Vice President for Africa, Mr Arthur Bastings, who paid a courtesy call on him Wednesday January 14, 2015 at the State House in Dar es salaam
 
 President Jakaya Mrisho Kikwete chats with the Millicom International Cellular SA Executive Vice President for Africa, Mr Arthur Bastings, who paid a courtesy call on him Wednesday January 14, 2015 at the State House in Dar es salaam

President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with the Millicom International Cellular SA Executive Vice President for Africa, Mr Arthur Bastings, who paid a courtesy call on him Wednesday January 14, 2015 at the State House in Dar es salaam. Second left is Ambassador Ami Mpungwe and right the Chairman of MIC Tanzania (TIGO)  Mr Diego Gutierrez. Others second right are TIGO's Head of regulatory Ms Sylvia Balwire and extreme left is Tigo's Public Retations Manager MS Halima Okash. STATE HOUSE PHOTOS

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAMJULIA HALI MBUNGE WA NAMTUMBO MHE VITA KAWAWA ALIYELAZWA HOSPITALI YA AMI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mbunge wa Namtumbo Mhe. Vita Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya AMI jijini Dar es salaam Jumatano,  Januari 14, 2015  akipatiwa matibabu ya tumbo. Katikati yao ni Mhe Adam Malima, nai bu Waziri wa Fedha na kushoto ni Daktari katika wodi hiyo.

Polisi Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 84 wa chuo Kikuu UDOM kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo Dodoma Mjini

$
0
0
 Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Dodoma SACP David Misime
---
Polisi Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 84 wa chuo Kikuu UDOM kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo Dodoma Mjini  tarehe 14.01.2015 majira ya 05:30 (kumi na moja alfajiri).
        
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime  ameeleza kuwa chanzo cha wananfunzi hao wa programu maalum ya diploma ya Ualimu kufanya uhalifu huo ni kikao walichofanya wananfunzi hao tarehe 13.01.201 wakidai kuongezewa posho ya chakula na kwamba hata kiasi ambacho wanapewa wamechelewa kupewa.
Hata hivyo uongozi wa Chuo uliwaeleza kuwa wenye mamlaka ya kuzungumzia swala la kuongezewa posho ni Bodi ya Mikopo na siyo chuo. Hivyo walitakiwa kufuata taratibu za kuwasilisha madai yao. Pia walielezwa kuwa hundi kwa ajili ya fedha za posho zao zimeshasainiwa na kuwasilishwa Benki ili waweze kuanza kupewa posho zao.
Hata hivyo wanafunzi hao  hawakuridhika na usiku wakaanza kuhamasishana kufanya maandamano jambo ambalo ni kosa kisheria. 
Wanafunzi hao wamehojiwa kulingana na ushahidi ambao umekusanywa na wamefikishwa mahakamani kwa kosa la Kufanya Maandamano yasiyo na kibali. 
Viongozi waliohamasisha uvunjifu huo wa sheria baadi wamekamatwa na baadhi wanaendelea kutafutwa ili nao waweze kuchukuliwa hatua stahiki. Ushahidi uliokusanywa unaonyesha jinsi viongozi hao wameshiriki kuhamasisha kupitia vikao rasmi na visivyo rasmi, katika vikundi, kupita katika mabweni na kutuma sms.
Kamanda wa Polisi ametoa wito kwa Wanafunzi hao kutumia taratibu zilizowekwa na Serikali na Chuo kuwasilisha malalamiko yao ngazi kwa ngazi na siyo kufanya vitendo vya kuvunja sheria ambavyo vitawasababishia kukamatwa. Endapo watafanya hivyo wasije kulaumu mtu kwani hatua zitachukuliwa kulingana na Sheria inavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
 
Imetolewa na  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. 
 Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma .
Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa kwenye gari ya polisi baada ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma

East African legislative Assembly resumes business next week

$
0
0
New EALA Speaker, Rt. Hon Dan Kidega. 

The East African Legislative Assembly (EALA) resumes business next week by holding its Plenary in Arusha, Tanzania. The Plenary which takes place from Monday, January 19, 2015, to Friday, January 30, 2015 is the Fourth Meeting of the Third Session of the Third Assembly.

The Assembly is to be presided over by the new Speaker, Rt. Hon Dan Kidega. The EAC Supplementary Budget for the Financial Year 2014/2015 is one of the key issues on top of the agenda during the two week plenary.  Another key Bill expected before the House is the EAC Co-operatives Societies Bill, 2013. 


The object of the EAC Co-operative Societies Bill, 2013 is to provide a legal framework for Co-operative Societies in line with Article 128 of the Treaty for the Establishment of the EAC strengthening the role of private sector as an effective force for developing economies. 

The Bill is divided into ten parts. Clause 3 of the Bill lays down objectives of Co-operative Societies which include: solving problems collectively, co-ordinating knowledge and skills and promoting self- reliance amongst Members.  The rest of the areas contained in the Bill deal with the formation, rights and duties of Members and Privileges. Other areas include the assets and liabilities, settlement of disputes and winding up/dissolution of Societies.  The Bill is at the stage of its second reading.


The EALA shall also debate and adopt a number of Reports.The Report of the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution and the African Leadership Centre on the Conference on East African Societies and Regional Security and that of the Inter-Parliamentary Forum on Population, Health and Investment shall be debated.

The Committee on Accounts is also expected to table its Report on the Audited Accounts for the Financial Year ending June 30th, 2013.The Report of the Committee on Legal Rules and Privileges on the EAC Rules of Procedure is also to be tabled.

The Rules of Procedure were first adopted by the first Assembly on 28th November 2001. Thereafter, they were amended in the year 2008, mainly, to take care of expanded membership of the Assembly, following the admission of the Republics of Burundi and Rwanda. 

EALA Members are on record on several occasions to have expressed the need to amend certain provisions of the Rules either for purposes of providing clarity, consistency and/or practicability; or to take into consideration new developments over the years.


Also on the cards at the forthcoming Sitting is the election of Committee Chairs and the EALA Commission which is the decision making body of the Assembly.  This follows the expiry of term of tenure last year.
In his acceptance remarks recently, Rt. Hon Dan Kidega underscored the need to clear the pending bills and backlog of other legislative business.


“My administration will move with haste to tackle the backlog and to introduce new business for the Assembly. The Council of Ministers have also assured me of their support and we expect a number of Council Bills to be brought forth for deliberation this year”, Rt. Hon Kidega said.

MHE. CHIKU GALLAWA AZINDUA MSIMU WA KILIMO KWA MWAKA 2015 KATIKA MKOA WA DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Damai Kondoa alipowasili kijijini hapo Januari 13,2015 kuzindua msimu wa kilimo Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiwaelezea wananchi wa kijiji cha Damai Kondoa malengo ya kuzindua msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiwaelekeza wakina mama wa kijiji cha Damai Kondoa namna bora ya kupanda kwa nafasi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.

RAIS MSTAAFU WA BOTSWANA MH. FESTUS MOGAE ATEMBELEA TAASISI YA UONGOZI

$
0
0
Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae (kushoto) akipokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja pale kiongozi huyo mstaafu alipotembelea ofisi hiyo iliyo chini ya Ofisi ya Rais jana Masaki, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja (wa pili kushoto) akimuelezea Rais mstaafu wa Botswana Mh. Festus Mogae (kulia) kuhusu mradi wa ujenzi wa taasisi ya mafunzo ya UONGOZI Institute unaoendelea katika mji wa Bagamoyo, Pwani. Kutoka kulia ni Dr. Linda Ezekiel Mkurugenzi wa Sekta za Kijamii kutoka Presidential Delivery Bureau (PDB) na Mkuu wa Sera na Utafiti wa UONGOZI Institute Bw. Dennis Rweyemamu.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images