Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 706 | 707 | (Page 708) | 709 | 710 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima akisoma Hotuba katika makabidhiano ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari Bariadi uliotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania.
  Mkuu wa shule ya sekondari ya Bariadi Bw. Pawa Lutema akipokea msaada wa vitabu vya sayansi kutoka kwa mkuu wa wilaya Bariadi, Vitabu hivyo vyote vinathamani ya sh milioni 6 na ni vya masomo ya sayansi kutoka kampuni ya simu ya Airtel kupitia mradi wake wa kusaidia elimu wa Airtel Shule yetu.
  Meneja wa Airtel Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi akikabidhi msaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya milioni 6 kwa Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima, vitabu hivyo ni sehemu ya msaada wa Airtel kupitia mradi wake wa Airtel shule yetu.


  0 0


  Na Bashir Yakub
  Mara nyingi nimekuwa nikiandika kuhusu masuala muhimu kuhusu ardhi hasa  namna ya kuandika mikataba  mtu anapokuwa ananunua nyumba/kiwanja , hadhi ya mikataba hiyo kisheria, na ubora wake. 
  Pia nimeandika mambo mbalmbali kuhusu namna ya kununua nyumba au kiwanja kwa usalama ili watu wasitapeliwe. Nikasema suala si tu kununua kile unachokipenda na kuondoka isipokuwa ni kununua  na  kuwa salama  na ulichonunua  bila hatari ya kukumbana na mgogoro mbeleni. 
  Lengo la haya yote ni katika kuhakikisha watu hawatapeliwi na hivyo kupoteza  fedha walizochuma kwa jasho.Lengo lingine ni kuwaepusha wanunuzi  na hatari ya kuingia mahakamani ambako kuna  usumbufu mkubwa na panapoteza fedha na muda sana tena sana, naongea hili kwa uzoefu. 
  Leo pia nasisitiza tena kuwa  ili ununue kiwanja au nyumba  na uepuke kabisa kupata mgogoro hakikisha  unafuata taratibu zote za msingi na za kisheria   ikiwemo kuhakikisha  unaandaa mkataba wenye hadhi  ambao  hata likitokea tatizo basi mkataba uwe ndio mlinzi wako.  Aidha leo naongelea tatizo lingine tena katika  masuala hayahaya ya  manunuzi ya viwanja na nyumba. Naongelea fedha ambayo serikali za mitaa wamekuwa wakiichukua kutoka kwa watu wanaouziana  ardhi.


  0 0

  Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla ametembelea mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mkoani Njombe (NJUWASA) na kutembelea vyanzo vya maji vya Magoda,Hagafilo,Njenga na Kibena pia Amekagua ujenzi wa mradi wa kuboresha maji mji wa Njombe kuanzia kwenye chanzo cha Mto Njenga,ulazaji mabomba na matanki makubwa.

  Mradi wa Njenga utagharimu kiasi cha sh. 3.5 bilioni na tayari umeshagharimu sh 2.2 bilioni na utakamilika mapema machi mwaka huu na kuongeza upataikanaji maji kutoka asilimia 43 hadi asilimia 79,Amewataka wakandarasi wote wa mradi huu kukamilisha kazi hiyo mapema mwezi machi ikiwa ni kuanzia chanzo,mabomba na matanki ili wananchi mji Njombe wapate maji ya uhakika.

  Aidha amefanya mkutano na wadau wote wa maji mji wa Njombe Naibu waziri akipata maelezo ya chanzo cha maji cha Hagafilo kutoka kwa mdau wamazingira na mlezi wa Walei ndg Edwin kilasi.
  Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akielekeza jambo wakati akipatiwa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji mkoa wa Njombe,Ndg. Daudi Majani.
  Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akiangalia uunganishaji na ulazaji wa mabomba maeneo ya airport,kambarage,nzerengerendete na Magereza.  0 0

  Watu wenye uhitaji wa msaada wa sheria sasa wanaweza kupata huduma hiyo kwa kuingia mtandaoni baada ya wakili mmoja Jijini Dar es Salaam kuanza kutoa huduma hiyo.

  Wakili Emmanuel Augustino ameanza kuwafikia wahitaji wa msaada wa sheria kwa kutumia blog yake ya wakiliwangu.blogspot.com.

  "Kupitia blog hii, tunatoa ushauri wa kisheria wa mambo yanayohusu mirathi, ununuzi au uuzaji wa ardhi, kesi za jinai na madai, kuanzisha kampuni na mambo mengine tofauti ya kisheria," alisema Wakili Augustino.

  Wakili Augustino anasema kuwa wazo la kutoa msaada wa kisheria kwa njia ya mtandao lilimjia baada ya kuhudhuria mkutano mkuu wa chama cha wanasheria wa Afrika Mashariki kilichofanyika Kigali, Rwanda mwaka huu.

  "Kule Kigali, kulikuwa na mjadala kuhusu matumizi ya teknologia kuwafikia wateja. Wanasheria maarufu walisema kuwa ni namna bora ya kuwafikia watu, badala ya utaratibu tuliouzowea wa kufuatwa ofisini," alisema.

  "blog ya wakiliwangu.blogspot.com ni kwa ajili ya watu wasio na uwezo. Tunachokifanya ni kutoa ushauri na pia msaada wa kuandika nyalaka tofauti zinazohitajika kukamilisha mchakato wa kisheria kama kuandika wosia, kuandika mikataba, n.k. Tunatoa msaada kwa njia ya simu, e­mail," aliongeza.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchini za Nje na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Mh. Mark Childress walipokutana kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam leo Januari 15,2015.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchini za Nje na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisisitiza jambo wakati akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Mh. Mark Childress walipokutana kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam leo Januari 15,2015.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchini za Nje na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Mh. Mark Childress mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam leo Januari 15,2015.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchini za Nje na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Mh. Mark Childress mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam leo Januari 15,2015.

  0 0

  Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika Takwimu Rasmi kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni Dar es Salaam Bi. Oloumi Olatunde kutoka Nigeria akiwasilisha mada kuhusu Ufundishwaji wa Takwimu Rasmi katika chuo hicho wakati wa Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika unaomalizika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Resort Kampala Uganda.
  Washiriki kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mada kuhusu Ufundishwaji wa Takwimu Rasmi katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni Dar es Salaam iliyowasilishwa na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika Takwimu Rasmi anayesoma katika chuo hicho Bi. Oloumi Olatunde kutoka Nigeria, wakati wa Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika unaomalizika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Resort Kampala Uganda.
  Mshauri wa Sensa ya Watu na Makazi kutoka UNFPA Tanzania Dkt. Collins Opiyo (aliyeinama) akiteta jambo na Meneja wa Sensa ya Watu na Makazi Irenius Ruyobya (katikati) na Meneja Rasilimali watu Gabriel Madembwe wote kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika unaomalizika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Resort Kampala Uganda.
  Wahadhiri Dkt. Tumaini Katunzi (Kushoto) na Dkt. Frank Mkumbo kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini mada kuhusu Ufundishwaji wa Takwimu Rasmi iliyowasilishwa na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika Takwimu Rasmi anayesoma katika chuo hicho Bi. Oloumi Olatunde kutoka Nigeria, wakati wa Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika unaomalizika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Resort Kampala Uganda. (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO – KAMPALA)

  0 0

   Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana ukikatiza katika mtaa wa Daraja Bovu wakati wakielekea kuzindua na kushiriki ujenzi wa Taifa wa Tawi la CCM Kiungani. katika jimbo la Chumbuni,Wilaya ya Amani mkoa wa Mjini Magharibi.
   Mbunge wa Chumbuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh.Pereira Ame Silima akizungumza jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kushoto aliposhiriki ujenzi wa Taifa wa Tawi la CCM Kiungani.  
    Mbunge wa jimbo la Mpendae Mh.Salim Hassan Abdullah Turky  akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakati alipowasili katika jimbo la Mpendae mapema leo katika wilaya ya Amani Mkoa wa Mjini Magharib,ambapo pia alipokea taarifa taarifa ya kazi za chama na Serikali,kuzindua ukumbi wa mikutano wa Jimbo pamoja na kukabidhi Vyarahani na Kompyuta kwa vijana wa jimbo la Mpendae.
   Mbunge wa jimbo la Mpendae Mh.Salim Hassan Abdullah Turky  akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Amani,katika jimbo la Mpendae mapema leo asubuhi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Amani,katika jimbo la Mpendae mapema leo asubuhi,ambapo pia alipokea taarifa taarifa ya kazi za chama na Serikali,kuzindua ukumbi wa mikutano wa Jimbo pamoja na kukabidhi Vyarahani na Kompyuta kwa vijana wa jimbo la Mpendae.
   Mlezi wa mkoa wa Mjini Magharibi na Mbunge wa jimbo la Mwanakwerekwe akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye mara baada ya msafara wa katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kuwasili mkoa wa Mjini Magharibi. 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua Ofisi ya Tawi la CCM Nyerere B,katika Wilaya ya Amani,ndani ya Jimbo la Magomeni Mkoa wa Mjini Magharibi. 

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipiga makofi mara baada ya kushiriki ujenzi na uzinduzi wa Ofisi ya tawi la CCM-Kilimahewa Juu,ambalo lilichomwa moto na kuvunjwa kabisa wakati wa harakati za kundi la Muamsho katika jimbo la Amani.PICHA NA MICHUZII JR-ZANZIBAR

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alisema licha ya juhudi zinazochukuliwa na viongozi katika kuchangia nguvu za kukabiliana na matatizo mbali mbali yanayowakabili wananchi katika maeneo yao lakini bado jukumu hilo litaendelea kubakia mikononi mwa wananchi wenyewe.

  Alisema Viongozi na hata Serikali Kuu huhamasika na kushawishika zaidi kusaidia hata uwezeshaji na hata vifaa kwenye miradi ya Jamii baada ya kuona nguvu za Wananchi zimeanza au kuiendelezwa katika kujikomboa na umaskini au kujitafutia maendeleo yao.

  Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema hayo wakati akikabidhi mabomba 250 ya kusambazia huduma za maji safi na salama yaliyogharimu jumla ya shilingi Milioni 17,000,000/- kwa ajili ya Wananchi wa Kijiji cha Kilombero hapo katika kituo cha Kilimo Kilombero Wilaya ya Kaskazini “ B “ Mkoa wa Kaskazini Unguja.

  Aliwapongeza wananchi wa Kijiji cha Kilombero kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ya kujiondoshea matatizo yanayowakabili ikiwemo kushiriki katika kazi za usambazaji wa huduma za maji safi.

  Aliwaeleza wananchi hao wa Kijiji cha Kilombero kwamba jitihada zitaendelea kuchukuliwa na Uongozi wa Jimbo hilo za kusambazwa huduma za maji safi na salama katika mitaa ya kijiji hicho mara baada ya Bomba za maji hayo kufikishwa katika eneo la Skuli ya Kilombero kutoka kwenye kisima hicho.

  Akitoa shukrani kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji cha Kilombero Msimamizi wa Kamati ya mradi wa Maji ya Kijiji hicho Bwana Moh’d Haji Faki alimuhakikishia mbunge huyo wa Jimbo la Kitope kwamba Wananchi wa Kijiji hicho wako tayari muda wowote kushiriki katika kazi za maendeleo wakati watapotakiwa kufanya hivyo.

  Zaidi ya shilingi Milioni 20,000,000/- zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi zimetumika katika ujenzi wa Kisima cha Maji ya Kilombero kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu wa miaka mingi wa huduma za upatikanaji wa maji safi na salama wananchi wa Kijiji hicho.

  Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Mabomba ya kusambazia maji safi Diwani ya Wadi ya Upenja Bibi Asha Abdulla Mussa kwa ya Kijiji cha kilombero Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kati kati yao ni Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi.
  Mabomba ya kusambazia maji safi katika Kijiji cha Kilombero yenye gharama ya shilingi Milioni 17,000,000/- yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitopo Balozi Seif Ali Iddi.
  Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akishiriki katika kazi ya uchimbaji mtaro kwa ajili ya ulazaji wa mabomba kwa ajili ya huduma za kusambazaji wa maji safi katika Kijiji cha Kilombero. Picha na Hassan Issa wa – OPMR – ZNZ.

  0 0

  Na Chalila Kibuda na Globu ya Jamii 

  Imeelezwa kuwa watahiniwa 2,175 sawa na asilimia 46.9 wameshindwa kufaulu mitihani ya Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA).

  Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA,Pius Maneno ilisema kuwa mitihani hiyo ya kwanza katika mfumo mpya  wa elimu wa mafunzo unaozingatia weledi na matokeo hayo hayalinganishwi  na matokeo ya nyuma ilifanyika katika mfumo wa kukazia maarifa.

  Kwa mujinu wa Maneno,watahiniwa waliojisajili ni 6,464  kati ya hao 678 sawa na asilimia 10.5 hawakuweza kufanya mtihani kwa sababu mbalimbali.

  Taarifa hiyo imesema watahiniwa 1,260 wamefaulu mtihani ngazi husika ,watahiniwa 1,811  wamefaulu baadhi ya masomo  katika ngazi ngzi husika.

  Jumla ya watahiniwa 356  ikiwa wanawake 95  na wanaume 261 wamefaulu mtihani wa shahada ya juu ya uhasibu nchini (CPA)  na kufikia watalaam  wa CPA 6002 tangu ianze mitihani hiyo mwaka 1975.


  0 0

  katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akifafanua jambo mbele ya kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wa vikao vya kamati za Bunge vinavyoendelea katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchuguzi Monica Mwamunyange (katikati) akiwa na baadhi ya Watendaji wa Wizara hiyo pamoja na Maafisa kutoka Mamlaka ya bandari (TPA) mbele ya kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wa kikao cha kujadili taarifa ya Ukaguzi Maalum wa matumizi ya fedha za mamlaka hiyo kwa mwaka 2011/2012
  Mjumbe wa kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Abdul Jabir Marombwa akikisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili taarifa ya Ukaguzi Maalum wa matumizi ya fedha za Mamlaka ya Bandari kwa mwaka 2011/2012.


  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na msako mkali wa kuwakamata na kuwadhibiti vijana wanaofanya uhalifu wa makundi maarufu kwa jina la Panya Road. 

  Msako huo mkali ni endelevu kama ilivyokwishaelezwa tangu awali mpaka tutakapohakikisha uhalifu wa makundi au jina la panya road litakapofutika kabisa. Misako hii inafanyika katika mikoa yote ya kipolisi yaani Ilala, Temeke na Kinondoni na makamanda wa mikoa hiyo wanaendelea kuwa wasimamizi wakuu wa misako hii.

  Misako hii iliyoanza tarehe 03/01/2015 hadi sasa imefanikisha kuwakamata vijana wapatao 1508 wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kujeruhi,wizi, dawa za kulevya, kupatikana na bhangi, wapiga debe na kubugudhi abiria, kucheza kamari, biashara ya ukahaba, mirungi, mikusanyiko isiyo halali katika vijiwe n.k. Uzoefu unaonyesha kwamba maeneo na vitendo tajwa hapo juu huchochea vijana kufanya uhalifu wa aina mbalimbali ambao pia ni kero kwa wananchi.

  Pamoja na watuhumiwa hawa wote  kukamatwa, hadi sasa watuhumiwa wapatao 959 tayari wamefikishwa katika mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa tuhuma zilizotajwa hapo juu. Mashauri yao yanaendelea katika mahakama hizo kwa hatua mbalimbali za kutajwa, kusikilizwa, n.k.

  Aidha, watuhumiwa wapatao 430 wameachiwa kwa dhamana kusubiri kukamilisha upelelezi huku nyendo zao zikifuatiliwa kwa kushirikiana na wazazi wao na viongozi katika maeneo yao. Watuhumiwa 119 wameachiwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha lakini pia nyendo zao zinafuatiliwa na endapo watabainika wanajihusisha na uhalifu basi watakumbwa na msako unaoendelea.

  Natoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhakika kama wanavyofanya hivi sasa ili makundi yanayofanya uhalifu wa aina ya panya road yatokomezwe kabisa ikiwa ni pamoja na uhalifu mwingine wa aina yoyote. Nataka wananchi wa jiji la Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla waishi na kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kwa amani na utulivu uliozoeleka.

  S.H. KOVA,
  KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
  DAR ES SALAAM.

  0 0

  Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania wametakiwa kuchangamkia promosheni ya Jaymillions ambayo ilizinduliwa juzi ili waweze kujishindia mamilioni ya fedha kwa kuwa droo ya kwanza iliyofanyika leo/jana mshindi wa milioni 100/- hakupatikana wakiwemo washindi kumi wa milioni 10/- na washindi mia moja wa shilingi milioni 1/-.

  Mkuu  wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa  alisema leo baada ya kumalizika droo ya kwanza:“Natoa wito kwa wateja wetu kuangalia namba zao kama zimeshinda kila siku kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza  nafasi za ushindi kwa siku. 

  Vodacom  itatoa mshindi mmoja wa Sh.100m/- kila siku, washindi kumi wa Sh.10m/- kila siku na washindi miamoja wa Sh.1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/- hivyo nawasihi wateja wetu kuchangamkia hii fursa muhimu”.Alisema.

  Twissa  aliongeza kusema kuwa  mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.

  Alisisitiza kuwa  kila siku namba zilizoshinda zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa promosheni hii na aliwahimiza wateja kuhakikisha wameangalia kila siku kama namba zao zimeshinda  ili wasipoteze bahati zao iwapo namba zao zitakuwa zimechaguliwa. Bila kufanya hivyo, wanaweza kupoteza mamilioni kama ilivyotokea leo katika droo ya kwanza kwani hawatoweza kujua kama namba zao zilichaguliwa kama washindi ambapo zinachaguliwa kila siku.

  Alimalizia kwa kusema kuwa promosheni hii  inathibitisha dhamira ya  kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi ambao wamekuwa wakiendelea kujiunga na familia ya Vodacom  na kuwataka kushiriki kwa wingi.

  Katika droo ya leo washindi wapatao 116 wameweza kujishindia muda wa maongezi.

  0 0


  0 0

  Rais Mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akila kiapo cha urais kuiongoza nchi ya Msumbiji jijini Maputo Msumbiji leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais Mpya wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi muda mfupi baada ya kuapishwa jijini Maputo Msumbiji leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Mpya wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi pamoja na Rais wa Msumbiji aliyemaliza muda wake Armando Emilio Guebuza katika viwanja vya ikulu ya Maputo baada ya sherehe za kuapisha leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zambia Kenneth Kaunda wakati wa kuapishwa kwa Rais mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi jijini Maputo Msumbiji leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mfalme Letsie III wa Lesotho(Kushoto), Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(wapili kushoto) na kulia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Viongozi hao walihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mpya wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi zilizofanyika jijini Maputo Msumbiji (picha na Freddy Maro).

  0 0

  The East African Community (EAC) and the Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA) have this morning jointly launched Round-Tables for Consolidating Regional Stability through Peaceful Elections in the Republic of Burundi at the Royal Palace Hotel, in Bujumbura, Burundi.

  Themed Peaceful Elections in Burundi for Regional Integration, the COMESA-EAC Roundtables are joint dialogue initiatives/activities geared towards promoting a peaceful environment for elections, prevent elections-related violent conflict and support a smooth transition during and after the 2015 elections in Burundi.

  Launching the Roundtables, the First Vice President of the Republic of Burundi, HE Prosper Bazombanza commended the EAC and COMESA Secretariats for organizing the important dialogue roundtables at the right time when Burundi was heading towards General Elections from May 2015.

  The First Vice President reiterated the region’s a firm desire to see democratic, peaceful and stable elections in the Partner States and commended the two Regional Economic Communities for the role they have played and continue to play in supporting the consolidation of democracy, peace and stability in Burundi.

  The First Vice President welcomed the inclusive roundtable as it gave the Barundi people another opportunity to share experiences, to dialogue on the pertinent issues, and to outline the initiatives that should be taken by various stakeholders as the election approaches “in order for us to achieve the goals we want”.

  “It goes without saying that it is the values of dialogue and inclusion that are of the essence during this period, and which will enhance reconciliation efforts and help to build consensus among Burundians for a better tomorrow” affirmed HE Prosper Bazombanza.

  The Secretary General of the East African Community Amb. Dr. Richard Sezibera noted that Elections were a process, and not an event; thus it was imperative that all the stakeholders stay involved in this process. He called on all stakeholders to fully participate in the Roundtable dialogue and to send out a strong message of peace to the people of Burundi.

  “The EAC calls on all the stakeholders to put the interests of Burundi and Burundians first”, and the focus of EAC and COMESA is to walk alongside the people of Burundi before, during, and after the elections. “Peaceful elections are essential for the country as it integrates more into EAC and COMESA, and together we are committed to achieving the dream of greater social, political and economic development of Burundi” not Amb. Sezibera.

  0 0

  Na Happiness Katabazi (UB)


  MAKAMU wa Rais ,Dk.Mohammed Gharib Bilal anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu  Cha Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Jumamosi Januari 17 katika Kijiji cha  Kiromo, Bagamoyo Mkoani Pwani.


  Akizungumza na waandishi wa Habari  ofisini kwake Mikocheni Dar es Salaam, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtalo  alisema  sherehe hizo zitafanyika Katika Kijiji cha Kiromo    na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao unatarajiwa  kuanza Mwaka huu.


  Dk.Mtalo   alisema Dk.Bilal  ndiye atakuwa mgeni rasmi pia na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa naye anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni walioalikwa katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia linatufundisha kuwa  mji wa Bagamoyo watumwa walikuwa wakiishi.


  "  UB tunaifahamu historia ya Mji wa Bagamoyo ndiyo maana tukaamua kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la University of Bagamoyo.Kupitia   Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, hivyo kupitia   UB  ambayo inajenga makazi yake ya kudumu   katika mji huo, binadamu wote watakuwa  huru kwasababu tutapata elimu" alisema Dk.Mtalo.


  Alisema UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda ,Mikocheni  B, Dar es Salaam  na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu na ajira.

  Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo

  0 0

  MAKALA MAALUMU YA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) .KUONESHA UTEKELEZAJI WA MIRADI MBALIMBALI YA MAJI PAMOJA NA JITIHADA ZA MAMLAKA HIYO KATIKA KUHAKIKISHA INAFIKISHA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA MJI WA MOSHI NA MAENEO JIRANI INAYO HUDUMIA KWA MUDA WA SAA 24.

  Video ya Makala haya imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

   Africa’s biggest sporting spectacle, the 2015 Africa Cup of Nations (Afcon) is coming to DStv.
  From the 17th of January until the 8th of February, all Compact, Compact Plus package subscribers will get special access to an Afcon-dedicated channel, SuperSport 5 (SS5). Furthermore, SS9 East Africa will now also be available on the Family bouquet, further making the tournament available to more subscribers. The channels will only be available on the bouquets for the duration of the Afcon tournament. 

  The activation of the channels on the lower tier bouquets forms part of MultiChoice’s continued efforts to give subscribers access to our exciting range of entertainment content via our different technological platforms while putting a spotlight on the abundance of sports talent on the continent.

  DStv Premium and Compact Plus subscribers will also have access to view all 32 matches from the tournament in both HD and SD across three other SuperSport channels: SS7 which will act as the overflow channel for SS5 at the playoff stage where matches will kick off simultaneously, SuperSport Select and Maximo (where available).    “Afcon is Africa’s biggest football event and we are delighted to offer it to our subscribers on our multiple channels and platforms,” said Peter Fauel, General Manager MultiChoice Tanzania. “The channel that has been dedicated to Afcon will bring our subscribers closer to the soccer action and convey the excitement of the Afcon taking place in Equatorial Guinea.”

  The live Afcon coverage will feature expert analysis from some of the most recognisable faces in the football industry like Ghanaian-born, former France football star Marcel Desailly, former South African national team player Neil Tovey, Ghanaian former international player Samuel Kuffour and the South Africa’s former striker, Benni McCarthy.

  To add to the Afcon excitement, DStv and SuperSport have launched the #AfricaShowYourLove campaign to encourage subscribers to show their support for their favourite teams by uploading pictures of themselves dressed up in their football fan regalia onto the DStv Facebook page to win great prizes.

  SS5 channel 205 will go live on Compact and Compact Plus from 17 January at 14: 00 CAT and will close on until 09 February at 10:00 CAT.
  For more information, visit www.dstv.com.


  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora kuhakikisha umefanya mkutano na wananchi ili kufanya makubaliano jinsi ya kusimamia mradi wa umeme wa kontena ili wananchi waanze kunufaika mara moja.
  Mtaalamu kutoka Kampuni ya Chico – CCC, Luo Xiaoyong (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) juu ya hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika wilaya za Uyui na Urambo mara Waziri alipotembelea eneo palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ya kazi hiyo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijadiliana jambo la kiongozi wa Jopo la Kimataifa la Tathmini (IRP), Rais Mstaafu wa Botswana, Festus Mogae (wa pili kulia) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa jopo hilo kutathmini mwaka mmoja wa utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) Dar es Salaam jana.
  Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa (BRN), Omari Issa akichangia mada wakati wa mkutano wa tathmini ya jopo la kimataifa kuhusu mwaka mmoja wa BRN uliofanyika Dar es Salaam jana.
  Waziri wa Elimu, Dkt Shukuru Kawambwa akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Sekta za Kijamii katika Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa (BRN), Dkt. Linda Ezekiel wakati wa mkutano wa tathmini ya jopo la kimataifa kuhusu mwaka mmoja wa BRN uliofanyika Dar es Salaam jana.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki wakati wa mapumziko kwenye Mkutano wa Jopo la Kimataifa la Tathmini lililokutana Dar es Salaam jana kutathmini Mwaka mmoja wa BRN.

older | 1 | .... | 706 | 707 | (Page 708) | 709 | 710 | .... | 3283 | newer