Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

Mashindano ya Upigaji Picha


Rais Kikwete aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Mjini Unguja

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) alipokuwa akiongoza Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja (kushoto) Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU WAGANGA WA JADI WANAOPIGA RAMLI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu maalumu ya kutembelea maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino nchini ambapo timu hiyo inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa kuanza na mikoa sugu ya matukio hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora na Shinyanga na baadaye itafuata mikoa mingine. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Picha na Emmanuel Massaka

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

Serikali imewapiga marufuku waganga wa jadi wanaotumia ramli kutokana na kuwa chanzo cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Mambo Ndani ,Mathias Chikawe wakati alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam,Chikawe amesema waganga wa jadi wanaotumia ramli wamekuwa wakiwaambia watu kuwa kuua au kupata kiungo cha albino ni utajiri,kuwa mvuvi wa mwenye mafanikio.

Chikawe amesema Jeshi la Polisi na Chama Cha Wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) wameunda timu maalum ya kufanya operesheni kwa waganga hao katika mikoa mitatu ikiwa lengo ni kutokomeza mauji ya albino.

“Tunataka kutokomeza mauaji ya Albino kwa timu hii ambayo tumeiunda itapita kila sehemu na wale wote ambao watabainika watachukuliwa hatua na kesi hizo zitapewa kipaumbele na Mwendesha Mashitaka Nchini (DPP)”alisema Chikawe.

Operesheni hiyo ya kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) itafanyika katika Mikoa mitano ambayo inaonekana ni sugu katika matukio hayo, nayo ni Mwanza,Tabora,Simiyu,Shinyanga pamoja na Geita.

Aidha alisema kuhusu serikali kutoamini ushirikina wa kazi hiyo pia itafanywa pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Mikoa na Tawala za Mitaa (Tamisemi) ambapo sheria ya  kuwabana itakapopatikana.

Mh. Mahiza Apania kuokoa miradi ya vijana na wanawake lindi

$
0
0
Na Abdulaziz Video,Globu ya Jamii - Lindi

Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mwantumu Mahiza ameitaka halmashauri ya wilaya Ruangwa na halmashari nyingine za wilaya,miji,manispaa zilizopo mkoani Lindi ambazo hazijachangia na zisizo kamilisha kuchangikia mifuko ya vijana na wanawake zikamilishe kuchangia michango hiyo haraka.Mahiza alitoa agizo hilo mjini Ruangwa baada ya kupokea taarifa ya kazi za maendeleo katika wilaya hiyo iliyosomwa na kaimu mkuu wa wilaya hiyo,Regina Chonjo.

Mahiza alisema halmashauri za wilaya zinawajibu wa kuchingia mifuko hiyo kwa mujibu wa sheria badala ya kutafuta visingio vinavyosababisha kutimizwa nia njema ya serikali kwa makundi hayo maalum ya kijamii.Mkuu huyo wa mkoa ambaye yupo katika wilaya hiyo kwa ziara ya siku mbili ili kukagua na kuhimiza utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

Alibanisha kuwa suala la halmashauri za wilaya kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani ili kuchangia mifuko hiyo siyo jambo la hiari bali ni lazima.Hivyo halmashauri hiyo na nyingine zilizopo katika mkoa huu ambazo hazijachingia au zisizokamilisha michango hiyo zikamilishe michongo yake haraka."

mnatakiwa mtambue kuwa vijana na wanawake kupewa fedha hizo siyo zawadi bali ni haki yao,na ndiyo nia ya serikali wajiendeleze kiuchumi," alisema Mahiza.

Awali akisoma taarifa hiyo kaimu mkuu wa wilaya ya Ruangwa,Regina Chonjo alisema halmashauri ya wilaya ya Ruangwa katika mwaka wa fedha 2014/2015 imechangia shilingi 20,000,000.00 kutoka katika mapato yake ya ndani yaliyokusanywa hadi sasa,yenyejumla ya shilingi 946743451.72.

Ambapo katika kipindi hicho(2014/2015) imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 6000000.00,kwa vikundi 16 vya wanawake vyenye wanachama 80.Huku ikiendelea kupokea maombi ya mikopo kutoka kwa vikundi mbali mbali vya vijana na wanawake
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mh. Mwantumu Mahiza (wa pili kushoto) akiangalia namna ya kushuka kwa usalama baada ya kukagua mradi wa Umwagiliaji katika kijiji cha Chinokole wilayani Ruangwa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AMPANDISHA CHEO CHA SAJIN WA MAGEREZA ASKARI WA KIKE, MWANARIADHA WA KIMATAIFA JIJINI DAR

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimvisha cheo cha Sajin wa Magereza, Askari Mwanariadha wa Kimataifa, CPL. Catherina Lange(hivi sasa cheo cha sajin) wa Gereza Kuu Arusha ambaye ambaye hushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla. hafla hiyo imefanyika leo Januari 13, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza Sajin wa Magereza, Askari Mwanariadha wa Kimataifa, wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla rasmi ya kumvalisha cheo hicho ambapo askari huyo hushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(Meza kuu) akitoa maelezo mafupi kwa Waandishi wa Habari(hawapo pichani) namna Askari Mwanariadha wa Kimataifa, CPL. Catherina Lange(hivi sasa cheo cha sajin) wa Gereza Kuu Arusha alivyoshiriki kwa mafanikio makubwa katika mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla.

IJUE CYBER SECURITY - SEHEMU YA I NA VIDOKEZO

Treni ya abiria imeahirishwa kuondoka hadi kesho Januari 14, 2015

$
0
0
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho saa 11 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea leo Jumanne Januari 13, 2015 saa 9 alasiri maeneo ya Stesheni ya Pugu Mpiji ambapo mabehewa matatu ya treni ya mizigo iliyokuwa inasafiri kwenda Bara yaliacha njia na moja kuanguka kabisa.

Tayari Wahandisi wa TRL wako eneo la ajali kufanya tathmini na kuanza zoezi la uokoaji, ikiwemo kazi ya kuyanyanyua mabehewa yaliyopata ajali na kisha kukarabati njia ili iwezwe kupitika mapema hapo kesho.

Uongozi wa TRL inawaomba radhi wananchi na wateja wake wote nchini kwa usumbufu utakaojitokeza.


Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam,
Januari 13, 2015.

RIPOTI KAMILI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KILICHOKETI ZANZIBAR KUJULIKANA LEO.

$
0
0

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu Adam Kimbisa,wakati akitoka nje mara baada ya kumaliza kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa usiku huu,kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja,Zanzibar,kikao hicho kilianza mnamo majira ya saa sita mchana na kumalizika usiku mnamo saa mbili na ushehe hivi huku mambo mbalimbali yakiwa yamejadiliwa ikiwemo suala la sakata la Akaunti ya Escrow, hali ya kisiasa nchini, uchaguzi Mkuu na mambo ya Maadili na mengineyo.
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari usiku wa kuamkia leo baada ya kikao cha kamati kuu cha CCM kuisha nje ya ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Unguja kisiwani Zanzibar.Nape ameeleza kuwa taarifa rasmi ya yaliyohusu kikao hicho atayaweka wazi  asubuhi hii.

KUMBUKUMBU

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Miono,Saleh Mpwimbwi afariki Dunia leo

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Miono,Ndg. Saleh Ramadhan Mpwimbwi (pichani) amefariki Dunia asubuhi ya leo kwa ajali ya Gari alilokuwa akiendesha mwenyewe, maeneo ya katikati ya Kijiji cha Hondogo na Miono.

Chanzo cha ajali hiyo,kinaelezwa kuwa ni kupasuka kwa tairi ya nyuma wakati akiwa kwenye mwendo na kushindwa kuliongoza gari hilo na kupelekea kupinduka.

Mwili wa Marehemu umepelewa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.

Taratibu zote za msiba huo,zinafanyika Nyumbani kwake Miono,Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Tunamuombea kwa Mungu aiweke Roho yake mahala pema peponi

-Amin

AFRIKA ARISE - JHIKOMAN AND PEETAH MORGAN

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi afanya ziara katika Wilaya ya Momba na Mkoa wa Rukwa

$
0
0
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Kamani (wa tano kushoto) akipewa maelezo alipoenda kukagua eneo linalotegemewa kujengwa soko la kimaifa la samaki eneo la Tunduma katika Wilaya ya Momba. (Picha na Mwakipesile).
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Kamani (kati), akipewa maelezo alipotembelea kiwanda cha kusindika nyama cha SAAFI kilichopo Sumbawanga. Kulia kwake ni Mhe. Chrisant Mzindakaya mmiliki wa kiwanda cha SAAFI. Kiwanda hicho kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 300 kwa siku.
Shughuli za uchinjaji zikiendelea katika kiwanda cha SAAFI kilichopo katika Wilaya ya Sumabwanga mkoani Rukwa

TANZANIA NA CANADA KUUNDA KUNDI LA NCHI MARAFIKI KUHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO

$
0
0
Mhe. Rais Jakaya Kikwete ambaye amekuwa mstari wa mbele katika juhudi za kuboresha afya ya mama, mtoto mchanga na mtoto anaoneka katika picha hii kutoka maktaba akimjulia hali mama mzazi pamoja na watoto wake. Mhe. Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada ni wenyeviti wenza wa Kamisheni ya Habari na Uwajibikaji katika masuala ya Afya ya Mama na Mtoto. Juhudi za Rais na Waziri Mkuu katika eneo hilo zitapatiwa msukumo zaidi wakati wa majadiliano ya ajeda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. jana Jumanne Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Canada katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manoni pichani chini na Balozi Guillermo Rishchysnk wamekubaliana kuunda kundi la nchi marafiki litakalosukuma mbele juhudi hizo.
" Tuko pamoja katika hili" ndivyo wanavyoelekea kusema Mabalozi Tuvako Manongi na Guillermo Rishchynsk mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania ambapo wamekubaliana kuundaa kundi la nchi marafiki kuhusu afya ya mama na mtoto ambapo pia watakuwa wenyevita wenza wa kundi hilo.

Na Mwandishi Maalum, New York

Jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada,Bw. Stephen Harper kuhusu afya ya mama, mtoto mchanga na mtoto, zitapata msukumo zaidi katika kufafanua ajenda mpya ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Ili kufanikisha azima hiyo Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Canada katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Balozi Guillermo Rishchynsk wanakusudia kuunda Kundi la nchi marafiki ambalo litatoa fursa kwa wajumbe kufanya tathmini ya hali ya sasa kuhusu afya ya mama na mtoto , tathmini ambayo itakuwa kiini na msingi wa majadiliano mapana zaidi ya nini kifanyike ili kuongeza msukumo katika suala hilo

Mabalozi hao wawili katika mazungumzo yao yaliyofanyika siku ya Jumanne katika Uwakilishi wa Tanzania pia wamekubali kuwa wenyeviti wenza wa kundi hilo mara litakapoundwa.

Wawakilishi hao wamesema, kundi hilo litatarajiwa pia kujadiliana mwelekeo wa baadaye katika eneo la uwajibikaji ambao utasaidia na kuhakikisha ahadi kuhusu afya ya mama na mtoto zinatekelezwa na uzoefu uliopatikana utatumika katika majadiliano ya kina ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Kwa mujibu wa Mabalozi hao wa Tanzania na Canada kundi hilo linatarajiwa kuwa na washiriki au wajumbe kati ya 20 na 30 ambao watatokana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa.

Mwezi Mei mwaka 2014 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu Stephen Harper ambao ni wenyeviti wenza wa Kamisheni ya Habari na Uwajibikaji kuhusu afya ya mama, mtoto mchanga na mtoto waliongoza huko Toronto Canada, mkutano maalum wa wakuu wa nchi ambapo ilikubalika kwamba suala hilo lipewe kipaumbele katika kukalimisha Malengo ya Millennia yanayofikia ukiongoni mwaka huu.

Waumini wa Mwembetanga kwa Karagosi waadhimisha Maulidi ya Mfungo Sita

$
0
0
Vijana na wazee wa kiIslamu wa MwembeTanga wamefanikisha kuadhimisha Maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yaliosomwa Siku ya Jumanne Jan 13 ,2015 sawa na Rabii Awal 1436
Maulidi hayo walioaza rami mida ya Saa tatu usiku maraa tu baada kusaliwa sala ya Ishaa, katika Mtaa wa Mwembetanga maarufu (Kwa Karagosi) Zanzibar ambapo Wazee na vijana hao huuandaa maulidi kila mwaka, ifikapo mwezi wa kuzaliwa Mtume Muhammed S.A.W.
Muongozaji Maulidi ya Mwembetanga kwa karagosi MC Imam Sadat Fadhil Abdullah akiongea Mipangilio ya maulid kwa ratiba maalumu iliopangwa na wana kamati Ya maandalizi ya Maulidi hayo.
Wazee wa mtaa wa M/Tanga Hajji AbdulAziz akiea na Sheik Ahmed wakiwa makini kusikiliza maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa MwembeTanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar.
Waumini wa kiIslamu kutoka maeneo mbali mbali wakiwa katika  maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa MwembeTanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NAPE AYATAJA MAAZIMIO KAMILI YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KILICHOFANYIKA JANA MJINI UNGUJA

$
0
0
 Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari mapema leo akifafanua kuhusiana na ripoti na maazimio ya kikao cha kamati kuu cha CCM kilichofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Unguja kisiwani Zanzibar.PICHA NA MICHUZI JR-ZANZIBAR.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Jana tarehe 13/01/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya kikao chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-

1. SAKATA  LA  AKAUNTI  YA ESCROW.
 
Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na sakata hili. Baada ya kulijadili kwa muda mrefu na kwa kina Kamati Kuu imeamua yafuatayo:-,
i). Pamoja na yale ambayo yameshatekelezwa na serikali, Kamati Kuu imeitaka serikali na vyombo vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge juu ya swala hilo.

ii). Kamati Kuu imewataka wote wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa dhamana zao, na wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za kuwawajibisha.

iii). Aidha Kamati Kuu imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili kwa wale wote waliohusika na ukiukwaji wa maadili kwenye sakata la Escrow na wako kwenye vikao vya maamuzi vya Chama. Kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili kitafanyika tarehe 19/01/2015 kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.

2. WALIOPEWA  ADHABU KWA KUKIUKA MAADILI YA CHAMA.
 
Itakumbukwa kuna makada sita wa CCM walipewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais, watamaliza muda wa adhabu zao mwezi wa pili mwaka 2015.

Baada ya muda wa adhabu zao kuisha, itafanyika tathimini kuona kama walizingatia mashariti ya adhabu zao. Na kama kuna ambao watakutwa hawakuzingatia mashariti ya adhabu zao wataongezewa adhabu.

3. SOKO LA MAHINDI.
 
Kamati Kuu imepokea taarifa ya mwenendo wa soko la mahindi nchini. Baada ya tathimini na uchambuzi,  pamoja na kazi iliyofanywa na serikali, Kamati Kuu imeiagiza serikali kuangalia upya mfumo unaotumiwa na Hifadhi ya Taifa ya Chakula ( NFRA)katika ununuzi wa mahindi, ili unufaishe zaidi wakulima badala ya utaratibu wa sasa ambao kwa kiasi kikubwa unanufaisha zaidi mawakala badala ya wakulima moja kwa moja.

4. RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA.
 
Kamati Kuu imepitisha ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama kwa mwaka 2015.Aidha ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM ndani ya dola utapangwa na vikao vijavyo  vya Chama.

Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity.

MFUKO WA PENSHENI WA GEPF WASHEREHEKEA MWAKA MPYA NA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA WASIO NA MAKAZI MAALUM (CHAKUWAMA) KILICHOPO SINZA

$
0
0
Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF,Bw Aloyce Ntukamazina (shati draft) akimkabidhi Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha Chakuwama,Bw. Hassan Hamisi msaada wa mahitaji mbali mbali ya chakula kwaaajili ya watoto wa kituo hicho.katikati ni Afisa Masoko Msaidizi wa Mfuko wa GEPF,Bw. Adam Hamza.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha Chakuwama,Bw. Hassan Hamisi akipokea moja ya ‘pampers’ maalum kwaajili ya watoto wachanga kutoka kwa Afisa Mafao Mwandamizi wa Mfuko wa GEPF,Bi. Salma Mtaullah.
Baadhi ya watoto yatima na wasio na makazi maalum watunzwao na kituo cha Chakuwama wakifurahia ujio wa maafisa wa GEPF.
Mwakilishi wa watoto wa kituo cha Chakuwama akitoa neno la shukurani kwa niaba ya watoto wenzake na kuwashukuru GEPF kwa kuwakumbuka katika kipindi muhimu cha mwaka mpya.

madarasa mawili ya shule ya msingi Loorng'oswani wilayani Simanjiro yakabidhiwa

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka pamoja na Kamanda Mteule wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Daniel Ole Materi wakikata utepe kuashiria kuzindua madarasa mawili ya shule ya msingi Loorng'oswani iliyopo Kata ya Terrat ambayo Kamanda Ole Materi, aliyajenga na kutoa msaada kwa shule hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara wakiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Christopher Ole Sendeka na Kamanda Mteule wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Daniel Ole Materi wakipiga picha ya pamoja baada ya kukabidhi madarasa mawili ya shule ya msingi Loorng'oswani ya kata ya Terrat.


Promosheni ya Jaymillions yaanza kwa kishindo jijini dar

$
0
0
Mtangazaji wa kituo chatelevisheni ya Taifa (TBC), Bavon Benjamin (wa kwanza kulia) akimsikiliza balozi wa promosheni ya JayMillions Hillary Daud “Zembwela” (wa tatu kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa (kulia) akitoa maelezo juu ya promosheni ya JayMillions iliyozinduliwa na kampuni hiyo jana wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana. Pamoja naye ni balozi wa promosheni hiyo, Hillary Daud “Zembwela” (kushoto). Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

MH. MEMBE ZIARANI NCHINI URUSI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) ameondoka nchini tarehe 13 Januari 2015 kwenda Urusi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Mhe. Sergey Lavrov.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha na kupanua ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.

Mhe. Membe anatarajiwa kutumiafursa hiyo kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na Urusi, hususan katika maeneo ya biashara, uwekezaji na ubadilishanaji wa teknolojia.  Tanzania inaweza kufaidika na utaalamu wa Urusi katika sekta za uzalishaji wa nishati, uvuvi, afya, kilimo na huduma. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Tarehe 14 Januari, 2015.

APPOINTMENT TO THE DIRECTOR GENERAL OF THE TANZANIACOMMUNICATION REGULATORY AUTHORITY (TCRA)

Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images