Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 703 | 704 | (Page 705) | 706 | 707 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Karibu katika kipindi cha HUYU NA YULE ambapo wiki hii tumeongea na Dk Talib Ali
  Yeye ni mwanzilishi wa Avatar Dental Care iliyopo Leesburg Virginia.
  Ameeleza mengi kuhusu kazi zake na mikakati aliyonayo baadae Pia, ametoa punguzo la 50% kwa waTanzania watakaoenda kutiiwa kwake, pamoja na mpango wa malipo ya awamu kuwzesha watu kumudu gharama hizo
  Karibu
  Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production
  Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com .

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla amefanya ziara ya vijiji mbalimbali Mbeya Vijijini ambako amezindua mradi mkubwa maji vijiji vya Shongo na Igale maelfu wafurahia. Katika ziara hiyo kaagiza wakala wa visima (DDCA) kuchimba kisima kirefu kijjiji cha Mjele kutekeleza ahadi ya mhe Rais Jakaya Kikwete kuwaokoa wananchi maelfu kufuata maji umbali wa kilomita 7. Pia ametoa ahadi ya kuanza utekelezaji wa mradi wa maji wa maji vijiji vya Iwindi,Mwashiwawala na Izumbwe ambao ulisimama baada mkandarasi kusimamishwa kwa kushindwa kazi.
  Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akikwepa utelezi  wakati akikagua chanzo cha maji ya chemchemu  ya Ndoba kijiji cha Galijembe

  Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akipokea zawadi kijiji cha Shongo

  ambako wananchi  wakimlaki kwa furaha 
  Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla katika Akipanda mti chanzo cha Ndoba- kijiji cha Galijembe

  Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akizindua rasmi mradi kijiji cha shongo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Bashir Yakub
  Wakati mwingine migogoro ya ardhi inasababishwa na kutojua. Wengi hawajui taratatibu na ndio maana hujikuta wanainga katika matatizo. Moja ya maeneo ambako watu wamekuwa wakipatia matatizo ni huu wakati wa kununua.  
  Yapo mambo mengi unapoununua ardhi, nyumba au kiwanja ambayo wewe kama mnunuzi unatakiwa kuyajua na kuyazingatia ili usiingie katika matatizo.  Nimefanya utafiti katika  kesi za  ardhi mahakamani na kugundua kuwa  moja ya eneo baya linalowaingiza watu mkenge ni hili la  mume kuuza nyumba au kiwanja  bila kupata ridhaa ya  mke wake.
  Ikumbukwe kuwa  suala la ridhaa hapa sio suala la hiyari isipokuwa ni suala la lazima na la kisheria ambalo kutolitekeleza kwake kunaweza kupelekea mnunuzi kupoteza kile alichokinunua. Ni hatari ndugu na umakini unahitajika.Mume anapouza nyumba/kiwanja kuna kitu huitwa ridhaa ya mwanandoa ambacho ni lazima akisaini, tutaona.  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa ACT-Tanzania ,Bara ,Shabani Mambo Akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Kagame Jijini Dar es Salaam.
   Wanachama wa ACT wakiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa  kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kagame Jijini Dar es Salaam wakipata taarifa ya Chama kwa kipindi cha miezi sita na tathimini ya uchaguzi wa serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni.
   Aliyekuwa Mwanachama wa TLP ,Ahmad Tao akionyesha kadi mpya uanachama wa ACT katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama  hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa hoteli ya Kagame jijini Dar es Salaam.
   Katiku mkuu wa wa Chama cha ACT-Tanzania,Samsoni Mwigamba akifafanuwa jambo katka kikao cha halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
  Aliyekuwa Mwanachama wa TLP ,Ahmad Tao akipokea kadi mpya uanachama wa ACT katika

  0 0

   
   Sheikh Hilal Shaweji akitoa neno kwa wadau wa michezo katika ibada ya kuwakumbuka wasanii na wanamichezo mbalimbali waliotangulia mbele ya haki, ibada hiyo imefanyika katika viwanja vya Leaders Club kinondoni jijini Dar leo.
  Padre John Solomon akitoa neno kwa wadau na wanamichezo katika ibada ya kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki  iliyofanyika leo katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.
  Balozi Mstaafu  Sisco Mtilo Akiwakaribisha wadau katika ibada ya kuwaombea waliotangulia mbele ya haki na Ibada  hiyo imefanyika katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.
   Padre John Solomon akiongoza ibada ya kuwaombea wasanii na wanamichezo mbalimbali waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika kaika viwanja vya leaders Club.
  Wadau wakiwa wamesimama katika ibada ya kuwaombea wasanii na wanamichezo waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
   Wadau wakifuatilia ibada maalumu ya kuwaombea wa wanamichezo na wasanii waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.
   Wadau wakifuatilia ibada maalumu ya kuwaombea wa wanamichezo na wasanii waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akiwasili kwenye uwanja wa Aman tayari maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Januari 12, 2015.
  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akipokea salamu za kijeshi mara baada ya kuwasili kwenye uwanjwa wa Aman tayari maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Januari 12, 2015.
  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akikagua gwaride la vikosi mbali mbali vya kijeshi wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yaliyofanyika  leo Januari 12, 2015 kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.
   Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yaliyofanyika  leo Januari 12, 2015 kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa kwenye maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yaliyofanyika  leo Januari 12, 2015 kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar.

  BOFYA HAPA  KWA PICHA ZAIDI 

  0 0
 • 01/12/15--23:32: in loving memory
 • The Late Christopher Joseph Mnzava.
  29/01/1944- 13/01/2013

  Dad, it has been two years since you were called by God on 13th January 2013. 

  Even though you are not with us physically, we know that you are always with us in spirit. 

  We miss your love, kindness and suble strength that could move mountains.

   May your soul rest in External Peace. 

   Dearly remembered by your wife, children, grand children, inlaws, as well as extended family, relatives and friends.

  0 0

  Kijana Andrew Mlaki kutoka kikundi cha Akili ni Mwanga akielezea vijana wenzake (hawapo pichani) shughuli zinazofanywa na kikundi chake baada ya kikundi hicho kutembelewa na wawezeshaji waliofika Wilaya ya Mwanga kuhamasisha vijana na kuwapa elimu kuhusu ujuzi na stadi za maisha. Kushoto ni mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa.
  Afisa Vijana wa Wilaya ya Mwanga Bibi Subira Mfanga akizungumza na vijana walioshiriki semina ya uhamasishaji kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana Mkoani Kilimanjaro katika Wilaya ya Mwanga.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Serikal ya Mapinduzi ya Zanzibar ina nia ya kutaka kujenga Wodi maalum kwa ajili ya kulazwa watoto wadogo wanaopatwa na majanga mbali mbali ya kuunguwa kwa moto.

  Balozi seif alisema hayo wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua watoto walioungua moto ambao wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa kilele cha maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

  Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaelewa vizuri matatizo yanayowakumba watoto wanaopatwa na majanga hayo ya moto ambao hulazimika kulazwa zaidi ya mtoto mmoja kwenye kitanda kimoja.

  Balozi Seif alisema hali hiyo mbali ya kwamba haipendezi kuonekana lakini pia inaweza kusababisha maambukizi ya maradhi mbali mbali kwa watoto wanaolazwa pamoja.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wazazi na walezi kuwa waangalifu na matukio ya majanga ya moto ambayo huonekana kushamiri zaidi katika baadhi ya vipindi na kusababisha vifo na hata vilema kwa watoto wao.

  Mapema Muuguzi wa Zamu wa Wodi ya Watoto katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Bibi Mary Jadi alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ajali za moto zinazowakumba watoto katika maeneo mbali mbali hapa nchini zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku.

  Bibi Mary alisema ipo haja ya kufanywa kwa utafiti wa kina kuelewa sababu zinazopelekea kuongezeka kwa majanga hayo na juhudi zifanywe kwa makusudi ili kupunguza au kuondosha kabisa tatizo hilo ambalo huonekana kushamiri zaidi katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
  Muuguzi wa Zamu katika Hopitali kuu ya Mnazi Mmoja wodi ya Watoto Bibi Mary Jadi akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif msongamano wa watoto wanaoungua moto ambao hulazimika kulazwa wagonjwa watatu kwa kitgand kimoja.
  Balozi Seif akimpa pole Bibi Wanu Rajab aliyelazwa Hospital Kuu ya Mnazi mmoja yeye na Mtoto wake baada ya kibanda wanachoishi katika shughuli za Kilimo kuwaka moto katika Kijiji cha Kirombero.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole Mtoto mgonjwa Nasrya Kombo aliyelazwa Hospitali kuu ya Mnazi mmoja baada ya kuungua kiwa moto. Pembeni ya Balozi Seif ni Muuguzi wa Zamu katika Hopitali kuu ya Mnazi Mmoja wodi ya Watoto Bibi Mary Jadi.

  0 0

   Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige  akikata utepe katika ufunguzi wa ZuRii House of Beauty duka jipya na la kisasa la vipodozi lililofunguliwa rasmi Jumatatu 12 Jan 2015 . kulia ni Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George. 
     Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George  akitoa ufafanuzi kwa Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige kuhusu bidhaa zilizopo kwenye duka la ZuRii Fashion & Beauty Boutique.
   Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George( kulia) akiwa na mwana harakati mwenzake Shamim Mwasha mmiliki wa blog ya 8020.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro,Mhe. Chabaka Kilumanga ameshiriki katika shughuli ya kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa katika Ofisi za Charlie Hebdo, jijini Paris, Ufaransa. Shughuli hiyo, iliyoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Comoro na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro, Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa pamoja na watu mashuhuri, iliambatana na kusaini kitabu cha maombolezi.
  Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga akisalimiana na Mhe. Ahmed Abdallah Mohamed Sambi, wakati akiwasili katika maombolezi ya mashambulizi ya Charlie Hebdo.
  Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga akisaini Kitabu cha Maombolezi ya Wahanga wa Mashambulizi ya Charlie Hebdo. Kushoto, aliyesimama ni Balozi wa Ufaransa nchini Comoro.

  0 0

  "Karibu" ndiyo anavyosema Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi wakati akimkaribisha mgeni wake Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Ujerumani katika Umoja wa Mataifa Balozi Harld Braun alipofika kwa mazungumzo katika Uwakilishi wa Tanzania siku ya jumatatu. Wawakilishi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali yenye maslani kwa mataifa hayo mawili, na moja ya masuala hayo ni namna gani Tanzania na Ujerumani kama sehemu ya kundi la nchi ambazo ziko mstari wa mbele kupinga na kukemea uharamia dhidi ya wanyamapori zitakavyoshirikiana katika majadiliano na maandalizi ya rasimu ya Azimio kuhusu uharamia dhidi ya wanyama pori. Katika mazungumzo hayo Balozi Harld Braun alitambua juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete za kuongoza na kusimamia mipango ya serikali katika kudhibiti uwindaji haramu wa wanyamapori na hususani Tembo. Ni kwa kutambua Juhudi hizo za Rais Kikwete ndiyo maana Ujerumani inaiomba Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu kuwa moja na nchi zitakazo dhamini Azimio hilo.


  0 0

  Siku ya tarehe 11.01.02 wadau wa "Social Media Network Citizens", ambao ni watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Twitter walifanya awamu ya pili ya zoezi la kukabidhi madawati 241 kwa shule ya msingi ya Mjimwema iliyopo kwenye kata ya Mjimwema, Jimbo la Kigamboni.

  Katika awamu ya kwanza, wadau hawa walikabidhi madawati 45. Jumla ya Tsh 30.5 millioni zimechangwa na wadau hawa na zimetumika kutengeneza madawati 286 yaliyotolewa hadi hivi sasa.

  Mchango huu wa madawati umewezesha kutatua tatizo la madawati kwenye shule hii kwa asilimia 80% na kuwezesha wanafunzi 858 ambao ni asilimia 75% ya wanafunzi wote kukaa kwenye dawati.

  Mgeni Rasmi kwenye makabidhiano haya alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dkt Faustine Ndugulile.

  Shule hiyo bado inahitaji madawati 70 ili watoto wote waweze kuwa na dawati. Vile vile Ofisi za walimu zina upungufu wa samani. Wadau wameanza raundi ya tatu ya michango kwa ajili ya kumaliza tatizo la madawati kwenye shule hii.

  Wadau wanaotaka kuchangia wanakaribishwa kuwasiliana na waratibu (@AnnieTanzania na @IrineiKiria) kupitia mtandao wa Twitter.
  Mbunge wa Kigamboni,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akikabidhi moja ya dawati kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo (Kushoto) huku wakishuhudiwa na Bw Irinei Kiria (Mbunifu wa harambee hii), Bi Germana Ibreck (Mtunza fedha), Dkt Mwele Malecela na Afisa Elimu toka Manispaa ya Temeke.
  Mtunza fedha wa Social Media Network Citizens Bi Germana Ibreck akiwa na wanafunzi wa shule ya Mjimwema.
  Mgeni Rasmi, Mbunge wa Kigamboni, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Social Media Network Citizens na walimu.

  0 0

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza ukarabati katika Uwanja wa Kaitaba uliopo mkoani Kagera kuanzia Januari 12,2015.

   Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kuwa kutokana na ukarabati huo tayari Kagera Sugar imeshaomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa ajili ya mechi zake za nyumbani. Katika hatua nyingine, Malinzi alisema kutokana na kikao cha Kamati ya Utendaji cha FIFA kilichokutana hivi karibuni kiliweka wazi kila Mwanachama wa FIFA ataendelea kupata dola za kimalekani 600,000 kwa mwaka kwa ajili ya maendeleo ya Soka. 
  Muonekano wa Uwanja wa mpira wa Kaitaba Stadium wa Bukoba baada ya kuanza ukarabati huo.
  Ukarabati huu wa Uwanja wa Kaitaba umeifanya mechi ya Kagera Sugar na Mbeya City kuhamishiwa kwenye Jiji la Mwanza na utachezwa siku ya Jumamosi tarehe 17.01.2015 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.


  0 0

  DSC_0499
  Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akionyesha gazeti la "Tuwasiliane" linalochapishwa na UTPC na kusambazwa kwa wadau na maeneo mbalimbali ya jijini Mwanza kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyetembelea makao ya ofisi hizo kwa ajili ya mazungumzo na kuboresha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa Umoja huo wa vilabu vya waandishi wa habari nchini.

  Na Mwandishi Wetu
  WIMBI kubwa la kuwa na vijana wasiokuwa na kazi limeelezwa kuwa tatizo duniani kote na serikali mbalimbali zinatakiwa kuliangalia hilo kwa undani na kulitatua.

  Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.

  Mratibu huyo alisema hayo katika mazungumzo yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC) Abubakar Karsan.

  Alisema ukosefu wa kazi kwa sasa ni tatizo la kijamii na kwamba, shauri hilo lisipoangaliwa kwa makini linaweza kuwa chanzo cha matatizo makubwa ya usalama na amani katika taifa.

  Alvaro Rodriguez ambaye alifika katika ofisi za UTPC kuangalia mambo yanayofanyika katika ofisi hiyo wakati akiwa ziarani Mwanza wiki iliyopita, alisema kama tatizo la ajira litaendelea kuwapo, vijana wanaoathirika wanaweza kufikiria njia nyingine isiyo ya kistaarabu kufanikisha mambo yao.
  DSC_0440
  Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akizungumza na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya mratibu mkazi wa UN Tanzania, Bi. Chitra Massey (kulia) alipotembelea makao makuu ya ofisi hizo jijini Mwanza.


  0 0
 • 01/13/15--03:53: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

  Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia. Wengine katika picha kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi;Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo na Afisa wa Ubalozi Ndg. Sufian.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) akisisitiza jambo katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia.


  0 0

  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Ushirika cha Ujenzi wa Nyumba Mwenge (MHCS Ltd), Hillaly Mdaki akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo, uliofanyika Afrika Sana Mwenge jijini Dar es Salaam.Kulia ni makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Hellena Khamsini.
  Mjumbe mmojawapo wa bodi ya hiyo, Ndesumbuka Merinyo akisaini hati ya kiapo cha kuitumikia nafasi hiyo katika hafla iliyofanyika Sinza, Afrika Sana jana.


  Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Chama cha Ushirika cha Ujenzi wa Nyumba Mwenge (MHCS Ltd), imezinduliwa rasmi jana ambayo pamoja na mambo mengine, imejizatiti kuhakikisha inatekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya wanachama wake.

  Akizungumza mara baada ya kuapishwa, mwenyekiti wa bodi hiyo Hillaly Mdaki alisema kuwa pamoja na mambo mengine itahakikisha inatekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya ujenzi wa majengo pacha yenye urefu wa ghorofa 32 katika kiwanja ilipo Afrika Sana, Sinza jijini Dar es Salaam.

  Pia ujenzi wa nyumba za wanachama na vitegauchumi vingine kupitia mikopo ya mabenki katika eneo la kiwanja chenye ukubwa wa ekari 800 katika eneo la Kibiki, Chalinze mkoa wa Pwani. Mdaki alisema serikali kupitia mrajisi wa vyama vya ushirika imewakabidhi eneo hilo Chalinze na wanachama 378 tayari wamekabidhiwa viwanja na hati za umiliki wa viwanja hivyo na awali waliomba Bagamoyo lakini wakapatiwa Chalinze, jambo ambalo alisema ni jema.

  “Lengo ni kuhakikisha wanachama ambao wengi wao ni wastaafu wa serikali wananufaika na ushirika” alisema na kuongeza kuwa bodi iliyozinduliwa pamoja na mambo mengine ina jukumu la kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo za wanchama unakamilika na kupitia mikopo ya mabenki.

  “Pia bodi ina jukumu la kuhakikisha mradi wa majengo pacha yatakayokuwa na jumla ya ghorofa 32 ikiwa ni idadi ya 16 kila upande unakamilika” alisema na kuongeza kuwa michoro kwa ajili ya ujenzi huo imekamilika.

  Alibainisha kuwa majengo hayo pacha yatajengwa katika kiwanja hicho ilipo Afrika Sana, eneo ambalo walipewa na Rais wa Awamu ya Kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1971 na pia wamelenga kutekeleza miradi kadhaa ya ujenzi mikoani pia.

  Tupo Mwenge ambayo ni alama ya mwangaza kwa nchi nzima hivyo nasi tutatekeleza miradi hiyo ya ujenzi katika mikoa mingine 10 nchini kwa kuanzia lengo kufanya hivyo nchi nzima” alisema na kuongeza kuwa viwanja 77 vitagawiwa kwa wakazi wengine wa jiji ambao watahitaji.

  Awali mwenyekiti anayemaliza muda wake, aliwataka wajumbe na mwenyekiti mpya kufanyakazi kwa kufuata kanuni, sheria ya vyama vya ushirika na katiba na alibainisha kuwa hadi kufikia ulipo huo ushirika ni jitihada binafsi za wanachama.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni mpya inayojulikana kama JayMillions itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku.Kushoto ni Balozi wa promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” na kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
  Balozi wa promosheni ya JayMilions Hilary Daud ”Zembwela” (kushoto) akionesha bango linaloelezea jinsi ya mteja kujua kama ameshinda katika Promosheni hiyo iliyozinduliwa na Vodacom Tanzania leo itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu kila siku yenye neno “JAY” kwenda namba 15544.Wengine kutoka kulia Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa.


older | 1 | .... | 703 | 704 | (Page 705) | 706 | 707 | .... | 3272 | newer