Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 702 | 703 | (Page 704) | 705 | 706 | .... | 3278 | newer

  0 0


  Na Harriet Shangarai

  Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko  katika shingo ya kizazi.Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.  Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani ya nne inayoongoza kwa kusababisha vifo vya  wanawake katika nchi zinazoendelea. Repoti ya 2012 ya shirika la afya duniani 'WHO' imesema kati ya matukio 75,000 ya waathirika wa saratani ya kizazi barani Afrika, 50,000.Namba za matukio haya zinawakilisha waathirika waliopata fursa ya utafiti.


  NINI KISABABISHACHO SARATANI YA SHINGO YA UZAZI ?

  Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99%  ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya  kujamiana.

  BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA  HATARI  ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?

  • Kushiriki tendo ndoa katika  umri mdogo au chini ya miaka 18
  • Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofauti
  • Utumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system)
  • Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama Ukimwi
  • Uzazi wa mara kwa mara


  BAADHI YA DALILI ZA SARATANI YA KIZAZI

  • Kutokwa na majimaji au uchafu wenye harufu kali ukeni.
  • Kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa
  • Maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( pelvic area)
  • Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
  • Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudia
  • Mkojo wenye matone ya damu


  JE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTIBIKA ?
  Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema.

  PAP TEST (PAPANICOLAOUS TEST);
  Pap-Smear ni test ambayo hutumika  kuchunguza  mabadiliko ya chembe zilizoko katika mlango wa kizazi   ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo na hivyo kuwahi kuyakabili mapema.

  UMRI WA KUPATA PAP TEST
  Test hii hushauriwa kwa wanamke wa umri wa miaka 21 hadi 65  na chini ya umri wa miaka 21 endapo umeingia katika tendo la ndoa kwa kipindi cha kisichopungua miaka 3.

  KUPUNGUZA HATARI ZA
  SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?

  • Pap tests.  Waweza kupata Pap test mara 1 kwa mwaka au mara 1 kwa miaka 2- 3,hii itategemea ushauri wa daktari,umri,hali yako ya afya kwa ujumla, na majibu uliyoyapata katika testi zilizotangulia na mfumo wako wa maisha.

  • Pata HPV vaccine (hii yashauriwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26 chini ya mwongozo wa daktari)

   • Kuwa na mpenzi mmoja. Mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magojwa ya zinaa.

   • Tumia kinga (condoms). Hii husaidia kupunguza maambukizi ya magojwa ya  zinaa  


   Shukrani/Thanks;

   Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-Centered Collaborative Care (6th ed.).
   (WHO/ICO HPV Information Centre 2010)
   https://www.imaworldhealth.org/archive/cervical
   (WHO/ICO HPV Information Centre 2010)
   http://cip.cornell.edu/dns.gfs/1343074824
   Story;NesiWangublogspot.com

   0 0


   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko Ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania.
   Baadhi ya wageni waalikwa wakiongozwa na Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakhia Bilal (wa kwanza kushoto) wakisikiliza hotuba ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati wa tarfija ya mwaka mpya aliyowaandalia wenza wa mabalozi wa nchi za nje waliopo hapa Tanzania tarehe 10.1.2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Anna Mkapa wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nje hapa nchini.

   BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

   WAMA yajivunia mafanikio katika sekta ya elimu
   Taasisi ya WAMA Foundation imefanikiwa kupanua fursa za elimu kwa mtoto wa kike kwa mwaka 2014.
   Hayo yamesemwa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete wakati Akiongea na wenza wa mabalozi kutoka nchi mbalimbali katika ghafla fupi ya kuukaribisha mwaka mpya 2015 iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam,
   Mama Salma alisema kuwa baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na Taasisi ya WAMA ni kukamilika kwa sekondari ya WAMA Sharaf katika Manispaa ya Lindi.
   “Ninayo furaha kuwataarifu kwamba ujenzi wa shule ya sekondari ya WAMA Sharaf umekamilika, shule ambayo itaongeza idadi ya wasichana wanaofaidika na WAMA” Alisema Mama Salma.
   Aidha, aliitaja Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama kuwa sehemu ya mafanikio ya Tasisi hiyo ambayo ina idadi ya wanafaunzi zaidi ya 400 na inatarajia kuchukua wanafunzi 90 mwaka 2015, ambao ni yatima na wanaotoka kwenye mazingira magumu.
   Akiongelea kuhusu mafanikio mengine Mama Salma alisema ni pamoja na kuimarisha afya ya mama wajawazito na watoto ili kupunguza vifo, kupunguza mimba za utotoni, na kupunguza kasi ya maambukizi ya HIV toka kwa mama kwenda kwa mtoto
   Mama Salma aliwashukuru wadau wote wanaofanya kazi kwa kushirikiana na WAMA wakiwemo Mashirika yasiyo ya Serikali kwa misaada na kuwaomba waendelee kushirikiana ili kutoa mabadiliko chanya katika jamii husika.

   Aidha, kwa niaba ya wenza wa mabalozi waliohudhuria ghafla hiyo, Mke wa kiongozi wa mabalozi nchini Bi Celine Mpango alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa juhudi anazofanya katika kumkomboa mtoto wa kike na mwanamke kwa ujumla.

   0 0

   Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchi ujerumani,inawatakia kila heri na fanaka wadau wote katika kuadhimisha miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzibar,mapinduzi yaliyofanyika 12 Januari 1964 ambayo  yaliwakomboa Wanzibari  kutoka katika makucha ya Sultan,Mapinduzi yaliyomng'oa Sultan hadi kusahau kilemba kitandani.
   Tunawapongeza Wanzabari katika kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu. Amani,Upendo ,Umoja na mshikamano ndio msingi wa maisha bora kwa wanadamu wote.
   Yadumu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ! 
   Zidumu fikira za waasisi wa mapinduzi !
   Mapinduzi haya ni yetu sote watanzania


   0 0

   Mwanalibeneke wa Demasho.com Hamza Juma akiwa anawajibika , leo hii anasherehekea siku yake ya kuzaliwa .


   Wahenga wanasema maisha ni Safari na siku hazigandi, nakama maisha ni safari basi kila kukicha twakumbana na masaibu ya kukatisha tamaa  ya kukupa moyo wa kusonga lakini jibu pekee ni kupambana nayo tu sikurudi nyuma. Nakama siku hazigadi basi ni dhahiri shairi kuwa umri unasonga siku hadi siku na huwezi kuurudisha nyuma.

   Basi katika siku hii muhimu ya kukumbuka kuzaliwa kwako, NAPENDA KUKUTAKIA KILA LILILO JEMA na kumbuka kuwa yote yatokeayo yana sababu. Mungu Akulinde, akufungulie lililojema ,
   "Tupo pamoja na tutaendelea kuielimisha jamii yetu."

   0 0

   Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi jijini Mbeya na kufanikiwa kutembelea vyanzo mvali mbali vya maji vilivyo chini ya Mamlaka ya Maji Safi jijini humo.

   Mh. Makalla amevutiwa sana na utendaji kazi wa Mamlaka hiyo na kuupongeza kwa kuongeza idadi kuwa wateja wa maji kutoka 9000 mwaka 2002 na kufikia 40,000 hivi sasa na pia kuwa mamlaka ya tatu kitaifa kuwa na miundombinu ya majitaka.

   Mh. Makalla ameiagiza Mamlaka hiyo kuhakikisha inadhibiti upotevu wa maji kutoka asilimia 34 ya sasa na wafikie kiwango cha kimataifa asilimia 20.
   Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla  (katikati) akimsikiliza Ing. Martin Kimambo wakati akimwonyesha na kumpa maelezo kuhusu miundombinu ya maji taka eneo la Kalobe.
   Naibu Waziri wa Waji,Mh. Amos Makalla akiangalia chujio la maji eneo la Swaya.

   BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

   0 0

   Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wakiwa wamebeba Bendera na Picha za Viongozi wakati wa kilele cha matembezi ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyopokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akikagua gwaride la Chipukizi wa UVCCM wakati alipofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo Mjini Zanzinar kupokea matembezi ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wakiwa katika matembezi ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyopokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibarleo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.


   0 0


   Wananchi wa Mkoa wa Njombe wametakiwa kupanda miti kibiashara  ili hatimaye kuongeza kipato katika familia zao. Wameagizwa pia kuitunza miti wanayoipanda na kusubiri ifikie umri wa kuvunwa ndipo ikatwe.

   Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi (pichani) jana tarehe 10 Januari 2015 alipozungumza kama Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupanda Miti katika ngazi ya Mkoa.

   Katika maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yalifanyika wilayani Makete jumla ya miti 3,000 ilipandwa katika kitongoji cha Dombwela kilichoko katika  mji wa Makete. 

   Dr. Rehema Nchimbi aliitumia fursa hiyo kuagiza  Halimashauri zote za Mkoa wa Njombe kutenga maeneo maalum ya kupanda miti kwa ajili ya watu wasiojiweza.  Miti hiyo itachangia baadaye katika upatikanaji wa fedha za  kuwasomesha watoto wa familia hizo. 

   Vilevile Mkuu wa Mkoa alizitaka Halimashauri zote za Mkoa wa Njombe kustawisha miche ya kutosha na kuwapatia wananchi waipande kwa wingi kwa nia ya kuifanya miti kuwa zao maalum la uwekezaji katika mkoa huo. Aidaha aliwataka wananchi wa Njombe wanaoishi nje ya mkoa kuwekeza pia katika mkoa wao husuan katika upandaji miti ili kukuza uchumi mkoani mwao.

   Kwa namna ya pekee Dr. Nchimbi  aliwapongeza wananchi wa mkoa mzima wa Njombe kwa kuwa na utamaduni wa kupandamiti. Hata hivyo akawataka kuipalilia inapokuwa midogo, kuitunza kitaalam na kuilinda dhidi ya moto kichaa .

   Aina ya miti iliyopandwa katika maadhimisho hayo ni Mizambarao na Miturunga ambayo inafaa kuhifadhi vyanzo vya maji. Mkuu wa Mkoa alichagua kupanda miti ya Miturunga kwa kuwa ni miti imara inayotoa mbao zisizochakaa upesi. 

   Alipokuwa akipanda mti hiyo Mkuu wa Mkoa alichukua fursa hiyo kuwataka wananchi wa mkoa wa Njombe, pamoja na kupanda miti ya biashara, kuviimarisha vyanzo vyote vya maji katika mkoa wa Njombe kwa kupanda miti inayofaa  kuhifadhi maji.

   Maadhimisho yaliyofanyika mkoani Njombe ni sehemu ya sherehe  za SIKU Ya TAIFA YA KUPANDA MITI ambazo huadhishwa kitaifa  tarehe 1 Aprili kila mwaka. Kaulimbiu ya mwaka huu nii:‘Panda Miti Kibiashara’.

   0 0

   Meneja Uhusiano wa Umma wa
    Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu
   Wadau wa soka nchini na wateja Vodacom Tanzania kwa ujumla   wanaendelea kupata habari za soka  zinazohusiana na   ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara(VPL)Ligi kuu ya Uingereza,na masuala mengine mengi yanayohusiana ya burudani kupitia simu zao za mkononi kupitia huduma  maalum iliyozinduliwa mwaka juzi.
   Katika huduma hiyo ambayo inawafanya wateja kupata burudani ili kupata  taarifa  hizo za michezo na burudani anachotakiwa kufanya mteja ni kutuma  neno SPORTS kwenda namba 15778 na hapo mteja atajipatia habari motomoto na burudani kwenye simu yake ya mkononi mahala popote pale aliko. 
    Akiongea kuhusu huduma hii Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amewasihi wapenzi wa soka na watanzania kwa ujumla kuitumia huduma hii ambapo itawarahisishia kujipatia habari motomoto za michezo na burudani kwa urahisi bila kupoteza muda mwingi. 
   “Ni rahisi kupata  habari za michezo kwa pamoja kupitia simu yako ya mkononi kupitia  huduma hii ukiwa popote pale badala ya kupoteza muda mwingi wa kusubiri kusoma magazeti au kufika manyumbani kusikiliza radio na kuzitafuta kwenye intanent,kwa kujiunga na huduma hii utaona maisha yanakuwa murua na tunawaaidi wateja wetu tutaendelea kuboresha huduma zetu na kuwaletea huduma zilizo bora na zenye manufaa kwao”.Alisema Nkurlu. 
   Vodacom imekuwa ikiboresha huduma mbalimbali  ili ziweze kwenda na wakati na kuwanufaisha na kuwapatia  burudani wateja wake ambapo mwaka jana ilizindua huduma ya kipekee ya shinda na kabumbu ambayo iliwawezesha wateja wengi kujishindia zawadi za kila aina ikiwemo fedha taslimu.Mbali na huduma kama hizo za michezo  Vodacom imekuwa ikiandaa promosheni za kubadilisha maisha ya wateja mojawapo ikiwa ni ile ya Timka na bodaboda na Vodacom milionea ambapo  washindi  waliweza kujishindia pikipiki na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 100.

   0 0

    Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akipunga mkono kusalimia katika ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Massangwa jana kwenye Usharika wa Kimandolu.
    Viongozi waliohudhuria ibada hiyo katika Usharika wa Kimandolu,kutoka kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu,Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Eraston Mbwilo,Balozi wa Tanzania nchini Nigeria,Daniel Ole Njolay na Waziri Mkuu mstaafu,Frederick Sumaye.
    Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Massangwa akipongezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu baada ya ibada ya kumsimika kuongoza dayosisi hiyo.
    Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akisaliana na waumini waliohudhuria ibada maalumu.

   Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu(kulia)akiwa na Mbunge wa Arumeru Magharibi wakisalimiana na wananchi na waumini waliohudhuria ibada maalumu.Picha na Filbert Rweyemamu

   0 0
  • 01/11/15--03:50: CAR FOR SALE
  • LAND ROVER  DISCOVERY 2/3 TD5 
    MODEL: 2004 ,DIESEL 2.8
   ,MANUAL, 
   MILEAGE: 87000
   FULL A/C, POWER WINDOW, CENTRAL LOCK, 
    FOUR WHEEL DRIVE IN VERY GOOD CONDITION. 
   JUST BEEN  IMPORTED  FROM THE UK 
    CAR LOCATION : DAR ES SALAAM , 
    DUTY HAS BEEN PAID 
    PRICE: TSH 35 > MILLION , USD 22 THOUSAND 
   FOR MORE INFORMATION CONTACT :  0718-736-213 OR 0788-741-125
   Front
   Side
   Rear

   0 0
  • 01/11/15--12:30: iringa international school

  • 0 0


   0 0
  • 01/11/15--12:30: Tahadhari ya mvua kubwa


  • 0 0


   0 0


   0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akipokelewa na Viongozi wa BAKWATA Dodoma na baadhi ya taasisi zilizo chini yake alipofanya ziara ofisini kwao Januari 9, 2015.
   Mkuu wa Mkoa Dodoma Chiku Gallawa (kulia) akizungumza na viogozi wa Kanisa la Kiinili Kilutheri Tanzania Mkoa wa Dodoma alipofanya ziara kutembelea taasisi za dini Januari 9, 2015.
   Mzee wa Kanisa la Sabato Dodoma Wallace Lusungwi akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Dodoma Chiku Gallawa zawadi ya vitabu wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa kutembelea taasisi za dini Januari 9, 2015.

   BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

   0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mkazi wa Bagamoyo mjini Bwana Mohamed Amani anayeugua ugonjwa wa Kiharusi kutokana na maradhi ya moyo.Rais kikwete aliyekuwa katika mapunziko ya mwisho wa wiki nyumbani kwake mjini Bagamoyo alimwona mgonjwa huyo  na kuamua kusimama kumjulia hali na kuahidi kumpatia msaada wa matibabu Picha na Freddy Maro

   0 0

    Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga (wa pili kutoka kulia) akizungumza jambo na ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli. Ujumbe huo ulikwenda kumpa pole nyumbani kwake Bondo nje kidogo ya mji wa Kisumu nchini Kenya kufuatia kifo cha mtoto wake Fidelis Castro Odhiambo Odinga aliyefariki ghafla mapema mwezi huu.

    Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akimfariji mama mzazi wa marehemu Fidelis Castro Odhiambo Odinga

    Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akizungumza na wafiwa, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pamoja na Mkewe Mama Ida Odinga

    Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais wa zamani wa Uganda Mama Miria Obote aliyehudhuria pia katika msiba huo Bondo nchini Kenya.

    Shabiki maarufu wa Timu ya Gor Mahia ya Kenya akilia kwa uchungu katika ibada ya kumuombea marehemu Fidelis Castro Odhiambo Odinga mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu.

   Taaswira katika jukwaa kuu.

   Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akihutubia maelfu ya Wakenya waliofika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha JOOUST  kwa ajili ya ibada ya Mazishi ya Fidel Odinga.   0 0

   Padri John Wotherspoon anayechapisha barua mbalimbali za 
   wafungwa wa Kitanzania waliofungwa katika magereza ya Hong Kong.

   Padri John Wotherspoon anayechapisha barua mbalimbali za wafungwa wa Kitanzania waliofungwa katika magereza ya Hong Kong baada ya kukamatwa na dawa za kulevya anafanya ziara nchini Tanzania kutembelea familia za wafungwa hao. Padri Wotherspoon alianza ziara yake mwishoni mwa mwaka jana na anaendelea na ziara ya kutembelea familia hizo hadi hivi sasa.

   John Wotherspoon anasema aliwasili nchini akiwa na fedha za wafadhili kutoka Hong Kong kwa ajili ya kusaidia familia za wafungwa walio magerezani Hong Kong. Lakini fedha hizo zimeishia kwenye familia 5 tu huku bado akiwa na familia nyingine kama 30 za kutembelea na kuzijulia hali.

   Padri huyo ambaye anayeendesha kampeni yake dhidi ya madawa ya kulevya kwenye tovuti yake ya Pope Francisamekuwa akichapisha barua nyingi kutoka kwa wafungwa wa Kitanzania walioko magerezani huko Hong Kong baada ya kukamatwa na dawa za kulevya. Barua hizo zinapatikana hapa ==>2013).

   0 0

   Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (katikati) akikabidhi gari jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance), kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Dk. Mastidia Rutaihwa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chalinze, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jioni hii. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk. Bamba Victor na Diwani wa Kata ya Bwilingu, Nasa Karama. 
   Muumini wa Dini ya Kikiristo, Heema Said akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete 9aliyevaa koti kushoto) alipokabidhi ambulance hiyo. Ridhiwani alisema kuwa yeye hivi sasa ni mbunge wa vyama vyote jimbo humo hivyo ambulance aliyoitoa itoe huduma kwa wakazi wote wa jimbo hilo bila kubagua watu kutokana na itikadi zao. Pia aliuasa uongozi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanatunza vizuri gari hilo.
   Dok Rtaihwa akimkabidhi ufunguo wa gari hilo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Chalinze, Dk.Victor baada ambulance hiyo kukabidhiwa na Mbunge Ridhiwani.
   Dk. Victor akitoa shukurani kwa Mbunge Ridhiwani kwa msaada huo wa ambulance. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  older | 1 | .... | 702 | 703 | (Page 704) | 705 | 706 | .... | 3278 | newer