Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MOTO WATEKETEZA GHALA LA KUHIfaDHIA RANGI,KIJITONYAMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Askari wa Kikosi cha zima moto wakiendelea na zoezi la uzimaji moto katika ghala la kuhifadhi rangi za kampuni ya Colar Paint lililopo katika Mtaa wa Kenya,Kijitonyama usiku huu.Chanzo cha moto huo hakijafahamika mpaka sasa na eneo kubwa la ghala hilo limeteketea kabisa kwa moto huo.hakuna mtu yeyote alieripotiwa kupoteza maisha au kujeruhiwa katika moto huo.Mpaka Globu ya Jamii inaondoka eneo la tukio,eneo kuwa la moyo huo lililiwa limeshazimwa.

Sehemu ya Maduka yaliyokuwa yamezunguka nje ya ghala hilo kama yanavyoonekana,hakuna alieweza kuokoa chochote.
Maafisa wa vikosi vya zimamoto wakijadiliana jambo mara baada ya kufanikiwa kuzima moto kwa asilia kubwa.


WZIRI MKUU AHITIMISHA ZIARA YAKE WILAYANI MPANDA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na viongozi wa mkoa wa Katavi kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya ziara yake ya jimbo la uchaguzi Januari 9, 2015. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Pazi Mwamlima, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Emmanuel Kalobelo na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Kanali Ngemera Lugunga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia msokoto wa rasta isiyokuwa ya kawaida aliosuka Bwana huyo, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa shule ya ufundi ya Mamba wilayani Mlele kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 9, 2015. 

WAZIRI WA VIWANDA ATEMBELEA MACHIMBO YA CHUMA LIGANGA NA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA

$
0
0
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kiogoda (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources Ltd, Erick Mwingira juu ya miradi hiyo ya makaa ya mawe, alipotembelea miradi ya Chuma cha Liganga na Makaa ya mawe ya Mchuchuma. Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mligi Mkucha.
 Picha ya pamoja ya Mh. Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na watafiti na Viongozi wa serikali.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TANZANIA YAOMBOLEZA NA WAFARANSA KUFUATIA MAUAJI YALIYOTOKEA HIVI KARIBUNI

$
0
0
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,Balozi Tuvako Manongi akibadilishana mawazo na Mabalozi wenzie muda mfupi kabla ya kusaini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, kufuatia tukio la jumatano ambapo watu kumi na mbili wakiwamo waandishi wa gazeti la Charlie Hebdo walipoteza maisha
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akiandika salamu za rambirambi kufuatia tukio linaloelezwa kuwa la kigaidi ambapo watu kumi na mbili wakiwamo waandishi wa gazeti la Charlie Hebdo waliuawa.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATEMBELEA VIWANDA VYA GENERAL TYRE NA A TO Z JIJINI ARUSHA

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akiongozana na  Meneja Ufundi wa Kiwanda cha Magurudumu cha General Tyre cha jijini Arusha, Elias Pallangyo,alipofanya ziara kutembelea kiwanda hicho.
Meneja Ufundi wa Kiwanda cha Magurudumu cha General Tyre cha jijini Arusha, Elias Pallangyo,akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene , sehemu ya kiwanda hicho ambayo ipo katika ukarabati tayari kwa ajili ya uzalishaji wa Magurudumu mapema mwaka huu. Kiwanda hicho kitafufuliwa baada ya kufungwa tangu mwaka 2009.
Meneja Masoko wa Kiwanda cha A to Z cha jijini Arusha, Binnesh Harrier, akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Janeth Mbene, namna fulana zinavyozalishwa kiwandani hapo juzi. Kiwanda hicho kinazalisha vyandarua, fulana zikiwemo bidhaa nyingine muhimu ambazo usafirishwa katika nchi zaidi ya 25 duniani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha A to Z cha jijini Arusha kujionea hali ya uzalishaji .Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

ZURIEL ODUWOLE STARTS 2015 ON AFRICAS PREMIUM WEB TV

$
0
0
Zuriel Oduwole Unveils New Computer LAB Dedicated To  her in   Tanzania.
Africa's most influential child and now as the worlds youngest movie producer to show her work in a commercial cinema - 12 year old Zuriel Oduwole has started 2015 on a bright note. Colorful Ndani TV [Swahili for Inside], Africa's second largest and Nigeria's biggest web based TV, has launched its 2015 programs, by featuring Zuriel in prime time on its coveted "Spotlight" program.

In the edition, Zuriel talks about her journey, her focus, her experiences after meeting more than 14 Presidents & Prime Ministers, the effect of her Dream Up, Speak Up, Stand Up project, which she has now delivered in Malawi, Tanzania, Nigeria, Ethiopia and Mauritius, and her new documentary titled A Promising Africa. Focusing first on Nigeria, it premiered in Lagos on November 29th last year, and moved to London in December 2014, with critical reviews already.

A firm believer in the African renaissance and the need to show the world the positive aspects of the continent, her next countries of focus as part of her 'A Promising Africa' documentary series include Tanzania, Ethiopia and South Africa. Zuriel, who is an honorary Ambassador for East Africa's largest women's assist foundation; WAMA, started by the First Lady of Tanzania - H.E Salma Kikwete, is already looking forward to visiting the land of Kilimanjaro. It is a country which is very special to her, and where almost a quarter of her nearly 3000 followers on social media reside.
Zuriel Presents PC to Olympio School in Partnership with  Computer Mart.
 As a way of recognizing her work in the area of children's education across Africa, a new computer lab was named after her in October 2013, when she visited Tanzania. True to her mission of supporting "everything" education, she used her growing influence to invite Computer Mart, a local Tanzanian PC distributor who partnered with her to donate the schools first brand new computer, 2 days after the opening.

With these new generation of Africans, the continents future is indeed, exceptionally bright !!

TATIZO LA KUTOAMINIANA LITAATHIRI UTEKELEZAJI WA SDGs- –TANZANIA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Elliason akiwa pamoja na baadhi ya washiriki wa majadiliano hayo kushoto kwake ni Balozi Tuvako Manongi anaonekana pia Balozi wa Finland mwenye Tai nyekundu Bw. Kai Sauer
Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akizungumza wakati wa majadiliano baina ya wajumbe wa Bodi ya Global Impact ambayo ni Taasisi ya Umoja wa Mataifa na Wawakilishi wa Balozi mbalimbali na kumshirikisha pia Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw, Jan Elliason.
Bw. Paul Polman CEO wa Unilever akizugumza wakati wa majadiliano hayo ambapo katika maelezo yake, alitambua juhudi za Serikali ya Tanzania za kujenga mazingira yanayoziwezesha sekta binafsi kukua na kuchangia maendeleo ya nchi.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

DK. MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA MTOTO WA RAILA ODINGA,NCHINI KENYA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli yupo nchini Kenya akiiwakilisha Tanzania kwenye mazishi ya mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga aitwaye Fidel Odinga aliefariki mwishoni mwa wiki iliyopita,yanayofanyika huko Bondo, Kisumu, Kenya. 
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mfiwa, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga wakiongozana kuelekea sehemu maalum ya kuaga mwili wa Marehemu Fidel Odinga kabwa ya kuzikwa kwake.
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Fidel Odinga kabwa ya kuzikwa kwake.Kushoto ni Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga ambaye ni baba wa Marehemu.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya,Mh. Raila Odinga ambaye ni baba wa Marehemu akimuombea mwanae.

DANGA CHEE YA MICHUZI TV NA SAKATA LA BEI YA BONGO MOVIE PART 2

DANGA CHEE YA MICHUZI TV NA SAKATA LA BEI ZA BONGO MOVIE NCHINI PART 1

TANESCO YASHEREHEKEA MWAKA MPYA NA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA CHAKUWAMA,SINZA JIJINI DAR

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki akizungumza na wanahabari mara baada ya kutembelea maeneo mbali mbali ya kituo cha cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,ambapo amefarijika sana kuona maendeleo ya watoto katika kituo hicho.ambapo waliweza kuwapatia watoto hao vifaa vya shule na vyakula kama sehemu ya mchango wao.Kituo hicho kipo Sinza Mori,Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulea Watoto Yatima cha CHAKUWAMA,Hassan Hamis (kulia) akitoa maelezo ya kituo hicho kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki wakati alipokuwa akimtembeza kwenye maeneo mbali mbali ya Kituo hicho.Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Leila Muhaji.
Afisa wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Khadija Ahmed (kati) akimnyesha maziwa Mtoto Badra mwenye umri wa miezi saba (7) anayelelewa kwenye kituo hicho baada ya kutupwa na Mama yake nje ya kituo hicho akiwa na miezi mitano (5).wanaoshuhudua ni Queen Mwashinga (kulia) na  Henry Kilasila.
Mmoja wa maafisha wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Lusajo Mwakabuku akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Decklan Mhaiki (mwenye shati jeupe walioketi mbele) wakati walipowatembelea na kusherehekea nao mwaka mpya 2015,watoto wanaolelewa kwenye kituo cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori,jijini Dar es salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAFAHAMU ZAIDI TANESCO KUPITIA LINK ZIFUATAZO:-

www.umemeforum.blogspot.com
www.twitter.com/tanescoyetu
www.facebook.com/tanescotz

BREAKING NYUUZZZZ.......: MH. SUGU APATA AJALI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akifanya mawasiliano kwa ndugu na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo,ajali hiyo imetokea eneo la Mlima Kitonga Mkoani Iringa mchana wa leo.kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa Mh. Mbilinyi alikuwa safarini akitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar akiwa na jamaa zake Wanne katika gari hilo lenye namba za usajili T 148 BQE. katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.
Gari hiyo inavyoonekana.

SHEREHE YA MAOFISA MAGEREZA KUUAGA MWAKA 2014 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2015 YAFANA JIJINI DAR

$
0
0
Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika sherehe ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015. sherehe hiyo imefanyika Januari 9, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(wa tatu kushoto) atoe hotuba yake (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Bw. Daud Msangi(wa pili kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa tatu kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. Dickson Mwaimu(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa) .

MAALIM SEIF AFUNGUA ICU HOSPITALI YA MNAZI MMOJA,ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Bw. Xie Yun Liang, wakifurahi baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU), katika hospitali ya Mnazi Mmoja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akitembelea wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU), katika hospitali ya Mnazi Mmoja, baada ya kuifungua rasmi.

MHE. CHIKU GALLAWAAKAGUA MACHINJIO YA KISASA KIZOTA MKOANI DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akifanya ziara ya ukaguzi kwenye machinjio ya Kisasa Kizota Mjini Dodoma Januari 9, 2015.
Muu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akikaga vifaa vinavyotumika kwenye uchinjaji mifugo na uandaji wa nyama kwenye machinjio ya Kisasa Kizota Mjini Dodoma Januari 9, 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akikagua utunzaji wa nyama kwenye chumba maalumu cha kutunzia nyama zinazosubiri kusafirishwa kwenye machinjio ya Kisasa Kizota Mjini Dodoma Januari 9, 2015.


KARIBU ZuRii House of Beauty Dar Free Market complex 1st Floor Shop No F4.

$
0
0

Karibu ZuRii House of Beauty duka jipya na la kisasa la vipodozi litakalo funguliwa rasmi Jumatatu 12 Jan 2015. 
Duka lipo Dar Free Market 1st Floor Shop No F4. 

Wako wazi kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa nne usiku.
Hapo utapata kila kitu kuanzia Lotions, Dawa Za Nywele za watoto na watu wazima, Mafuta mazuri ya nywele na mwili kwaajili ya watoto, Queen Elisabeth (Jumla na Reja Reja), Make Ups, Perfumes yaani cosmetics na urembo wa kila aina.  Vitu vyao ni 100% original na vyote vinatokea UK na MarekaniOk hand signOk hand sign Bei zao ni very affordable. 


Pia Kuna nywele aina zote kuanzia huma hair za kawaida na Natural Human Hair like Brazilian, Peruvian, Closures na ma lace wig ya ukweli. Bei zao ni nafuu sana karibuni mjionee wenyewe. 

Wamiliki wa masalon ya kike, kiume na kucha pia mnakaribishwa kujipatia bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. Wasiliana nao kwa kuwafollow kupitia acc yao personal ya  

Instagram
@officialjestinageorgeblog au @zuriihouseofbeauty
Contact details +255 752 019 597 au +255 65 918 9769 Whatsapp ni+447557304940 (Business Enquires Only Please).....

MSIKOSE SIKU YA UZINDUZI BEI ZA SALE! Karibuni!!!

Lowassa asalimiana na wananchi baada ya kusimikwa uaskofu mchungaji Solomon Jacob Masangwa jijini arusha

$
0
0
 Waziri mkuu wa mstaafu na  mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akisalimiana na mamia ya waumini wa  kanisa la KKKT Kimandolu jijini Arusha baada ya Ibada ya kusimikwa uaskofu mchungaji Solomon Jacob Masangwa kuwa askofu wa dayosisi ya kaskazini Kati leo Jumamosi  Waumini hao walipigana vikumbo kumpiga picha na simu zao.


VIJANA 500 (UVCCM) WA MIKOA YA ZANZIBAR NA TANZANIA BARA WASHIRIKI MATEMBEZI YA MAPINDUZI

$
0
0
Baadhi ya vijana 500 wa Chama cha Mapinduzi wakiwa wameshika picha za waasisi wa Tanzania na Marais wa Sasa katika matembezi ya siku tatu kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika eneo la Rahaleo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mhe. Mboni Mhita akiongoza matembezi ya siku tatu ya Vijana mia tano kutoka mikoa mbali mbali ya Zanzibar na Tanzania bara kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo vijana hao walitembea mikoa yote mitatu Unguja.
vijana 500 wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika matembezi ya siku tatu kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika eneo la Rahaleo.Picha na Haroub Hussein.

JK AZINDUA NYUMBA ZA KISASA ZA MAKAZI YA WANAJESHI GONGO LA MBOTO, DAR ES SALAAM, LEO

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuzindua nyumba za kisasa za makazi ya wanajeshi akisaidiana na Balozi wa China nchini Mhe Lu Youqing, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange Gongo la Mboto jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 10, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili tayari kuzindua nyumba za kisasa za makazi ya wanajeshi Gongo la Mboto jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 10, 2015.

BONANZA LA WATUMISHI TAMISEMI LAFANYIKA UWANJA WA JAMHURI DODOMA

$
0
0
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) walijumuika kwa pamoja katika uwanja wa jamhuri mjini Dodoma kwa ajili ya kushiriki tamasha maalum kwa ajili ya kuwapongeza watumishi wenzao ambao waliiwakilisha vyema wizara katika mashindano ya SHIMIWI na SHIMISEMITA iliyofanyika mwaka jana.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bwana Mohamed Pawaga. Tamasha hilo liliambatana na kufanyika kwa michezo mbalimbali kama vile Mpira wa Miguu, Netiboli, Kuvuta kamba na Riadha.
Katika mchezo wa mpira wa miguu, timu ya mpira wa miguu kutoka jengo la SOKOINE ilifanikiwa kuilaza timu kutoka jengo la Mkapa kwa mabao mawili kwa bila. Mabao ya washindi yakiwekwa wavuni na Abdallah Mbuguni na Ally Kiama. Kwa upande wa Netiboli, timu ya Jengo la Mkapa iliigalagaza timu ya Sokoine kwa magoli 19 kwa mawili. Katika mchezo wa kuvutana kamba, timu hizo zilitoshana nguvu kwani kila timu ilishinda awamu moja.

Katika mchezo wa riadha wanaume, mkimbiaji Philbert Rwakilomba kutoka jengo la Mkapa alishinda mbio za mita 200, na kufuatiwa na Ebeneza mlinga pia wa jengo la Mkapa na nafasi ya tatu ilishikwa na Felix changwe kutoka jengo la Sokoine. Kwa upande wa wanawake florah Odilo alishika nafasi ya kwanza, na kufuatiwa na Yadesi Katamba na chiploe Mpelembe wote kutoka jengo la Mkapa.
Katika mbio za mita 100 wanaume, nafasi ya kwanza ilishikwa na Christopher masomapya kutoka jengo la Mkapa, huku nafasi ya pili ikienda kwa Donath kambanyuma na nafasi ya tatu Jeremiah Mtawa wote kutoka jengo la Sokoine
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images