Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 700 | 701 | (Page 702) | 703 | 704 | .... | 3283 | newer

  0 0


  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu na mkewe Mariam Mtemvu na Binti yao Sitti Mtevu -kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja na wagteni wao kutoka vyuo vikuu viwili vya Marekiani vya State University of New York na University  of Buffalo, baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, leo kuanza ziara yao ya siku mbili katika jimbo hilo, kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya kijamii na maendeleo. Kulia ni Mkuu wa Msafara huo Mtanzania, Profesa Dan Nyaronga wa Chuo Kikuu cha Buffalo nchini Marekani.
   Mtemvu akiwa na mdau wa maendeleo katika jimbo loa Temeke, Fiona Barretto wakati wa mapokezi ya ugeni huo kwenda wa mkuu wa wilaya ya Temeke.


  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon pamoja na washiriki wa hafla ya kuwakumbuka walinzi wa amani wakisimama kwa dakika moja kuwaenzi walinzi wa amani na watoa misaada ya kibinadamu ambao ni wafanyakazi wa umoja wa mataifa waliopoteza maisha wakati wa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini Haiti mwaka 2010 na wale ambao wamepoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014.
  Ban Ki Moon akizungumza wakati wa hafla hiyo ambayo iliibua hisia na majonzi makubwa miongoni wa washiriki wa hafla hiyo ya kuwaenzi walinzi wa amani na watoa misaada ya kibinadamu waliopoteza maisha wakati wakitekeleza wajibu wao wa kuwasaidia wananchi waliokuwa matatizoni. Miongoni mwa wahanga hao waliokumbukwa katika hafla hiyo ni Mashuja Watatu Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) waliopoteza maisha wakati wakitimiza wajibu wao katika Misheni ya Kulinda Amani ya MONUSCO katika Jamhuri ya Kidemokraria ya Kongo. Mashujaa hao ni Luteni Rajabu Mlima, Private Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian Msigila.
  Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akitoa heshima zake mbele ya mshumaa mkubwa ambao uliandaliwa kama ishara ya kuwakumbuka na kuwaenzi Walinzi wa Amani na Watoa Misaada ya kibinadamu waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao katika kipindi cha tetemeko la aridhi lililotokea mwaka 2010 huko Haiti na wale waliopoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014. katika kipindi hicho Tanzania ilipoteza mashujaa wake watatu waliokuwa wakihudumu katika Misheni ya MONUSCO huko DRC.

  Na Mwandishi Maalum

  Umoja wa Mataifa jana Alhamisi umewakumbuka walinzi wa Amani   na  wafanyakazi ya umoja wa mataifa waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yako katika kipindi cha Octoba 2013 na November 2014.

   Kumbukumbuka hiyo  imefanyika  katika siku  kama ya jana ( January 8) miaka mitano iliyopita  palitokea   tetemeko kubwa la ardhi huko Haiti na  kupoteza  maisha ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo  pamoja  na  uhalibifu  mkubwa wa  mali ilivuta hisia za waliohudhuria hata baadhi yao kutokwa na machozi

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki  Moon akizungumza katika hafla hiyo amesema,  anasikitishwa sana na  ongezeko  la mashambulizi yanayofanywa  dhidi ya walinzi wa Amani pamoja na watoaji wa misaada ya kibinadamu ambao ni wafanyakazi wa  mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.

  Jumla ya  wahanga 102 walipoteza maisha nchi Haiti   wakati lilipotokea tetemeko hilo mwaka 2010,  huku wengine 100 walipoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014. Wahanga hao  ni walinzi wa Amani na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa  kutoka mataifa mbalimbali duniani  na walikuwa wakihudumu katika Misheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa  na Mashirika yake.
  Kati ya   waliokumbukwa jana wapo walinzi wa Amani watatu kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walipoteza maisha huko  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walikokuwa wakihudumu katika Misheni ya MONUSCO.

  Mashujaa hao wa kitanzania   na ambao majina yao yalisomwa moja  baada ya jingine sambamba na  mashujaa wenzao wengine. Ni Luteni Rajabu  Mlima,  Private Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian Msigila.

  Ban Ki Moon amesema   walinzi  wa Amani na watoaji wa misaada ya kibinadamu wamekuwa wakipoteza maisha katika mazingira ambayo ukiacha yale yatokanayo ya majanga asili yakiwamo magonjwa ya milipuko na ajali, wengine wamepoteza maisha kwa mashambulizi yanayofanywa kwa makusudi. 

  Na kwa sababu hiyo Katibu Mkuu anasema,  Umoja wa Mataifa unaendelea na jitihada zake za kuimarisha   ulinzi wao    ikiwa ni  pamoja na kuwajengea mazingira salama ya utendaji kazi  yakiwamo  mafunzo na vifaa 

  Ameongeza kuwa  ushirikiano na michango kutoka nchi wanachama wa umoja wa mataifa ni  muhimu sana  hasa katika kipindi hiki ambapo siyo tu pamekuwapo na ongezeko kubwa la mahitaji ya walinzi wa Amani na watoaji wa misaada ya kibinadamu, lakini pia kutokana na ongezeko la  mashambulizi  dhidi yao na mazingira magumu ya kazi.

  0 0

  Katika HUYU NA YULE Jumatatu ijayo tunakuletea mahojiano yetu na Dr Talib Ali.


  0 0

  Siku ya warembo ni usiku unaowakutanisha pamoja warembo wote wa mjini ambao hufanyika kila Alhamis ndani ya Kiota cha Samaki Samaki City centre Jijini Dar,ambapo huduma kama zile za  sangria kwa kila mrembo na shot ya Baileys pamoja ua rose hutolewa kwa warembo hao ikiwa ni kuonyesha kuwa bila warembo hakuna kinachoendelea.Katika usiku huo magoma ya nguvu huporomoshwa na maDJ wakaji wa Samaki Samaki ambao ni  Dj Sinyorita the hottest female DJ in town na DJ Vasley.
  Dj Vasley akizungusha ngoma siku ya warembo.
  Mmoja wa wahudumu wa katika kiota cha Samaki Samaki akipeleka huduma kwa Mteja.

  0 0


  0 0

  Umoja wa klabu za michezo za maveterani Dar es salaam,  chini ya uratibu wa klabu za Singasinga na Tazara,  unatangaza rasmi kwamba  shughuli ya kurehemu wanachama wenzetu ambao wametangulia mbele ya haki itafanyika JUMATATU 12/1/2015, ikiwa pia ni  sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi.

  Ratiba itaanza  Saa 7 mchana katika viwanja vya Leaders club jijini Dar es salaam. Dua zitafanyika  kutoka kwa Father Oscar na Sheikh Kipoozeo. Dua hizo zitafuatiwa na Chakula cha pamoja cha mchana kitachoandaliwa na Mpishi maarufu nchini, Chef  Saidi Bajia,  na  baadae burudani mbalimbali za  nguvu zitaendelea. 

  Karibuni tujumuike wote... 

  Pichani chini ni shughuli kama hii zilizofanyika miaka iliyopita.
  - Imetolewa na Balozi Cisco Mtiro, Mratibu mkuu wa shughuli hii.
  wanachama wa klabu za michezo za maveterani Dar es salaam wakiwa katika shughuli hiyo ya kuwakumbuka wenzao miaka ya nyuma
  Mapochopocho
  wadau
  Kila mtoto wa mujini alikuwepo
  Vilaji

  0 0

  Nimesoma katika gazeti la Habari leo la tarehe 9 Januari,2015,toleo la 02942,Ukurasa wa 8 habari na mwandishi Prisca Libaga,Arusha ,habari yenye kichwa cha habari "Mradi wa Maji wadaiwa kutoa Tope".

  Mwandishi amenukuu malalamiko ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Nangoro akiongea kwenye kikao cha Kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika juzi kuwa mimi Amos Makalla,Naibu Waziri wa Maji nilidanganywa nikazindua mradi wa maji wilaya ya Longido uliogharimu shilingi milioni 300 na kwamba mradi huo uliwekwa tanki la bandia na sasa mradi huo unatoa tope na siyo maji.

  Naomba nitumie fursa hii kukanusha habari hiyo kuwa siyo ya kweli mimi kama naibu waziri maji sijafanya ziara wilayani Longido na umma uelewe sijawahi kuzindua mradi unaotajwa.

  Aidha nimekuwa na ziara mkoa wa Arusha kuanzia tarehe 15 desemba hadi 18 mwaka jana kwa kutembelea wilaya ya Karatu,Arusha jiji, halmashauri Arusha Dc na Meru na ieleweke kuwa wilaya ya Longido zikufanya ziara tarehe 19 kutokana na maombi ya mkuu wa wilaya na mbunge wa Longido kuniomba nihairishe wilaya yao kutokana na wilaya kuwa na mgeni wa kitaifa ni hivyo waliniomba niwapangie wakati mwingine.

  Hivyo kauli ya mwenyekiti wa mkoa ilichukuliwe kuwa waliompatia habari hizo kuwa mimi nilizindua mradi wamempotosha na si za kweli.

  Mwisho wizara yangu imepokea taarifa hii na itaifanyia kazi ili kuona mradi huo unatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa na niwaombe wananchi wa Longido wawe watulivu wakati jambo hili linashughulikiwa.

  Amos G Makalla(mb)
  Naibu waziri maji
  9 Januari,2015

  0 0

  On Friday 9 January British High Commissioner, Dianna Melrose, handed over medical equipment to Dr. Seif S. Rashid, Minister of Health and Social Welfare at the Ministry of Health and Social Welfare offices in Dar es Salaam. She did this on behalf of the British charity UK Police Aid Convoys.

  Speaking at the event, Ms Melrose said:“This medical equipment was donated by the British Ambulance Service and hospitals across the United Kingdom. We hope that the equipment will prove useful to Tanzanian medical institutions and benefit the people of Tanzania. The donation is a symbol of the close partnership between the UK and Tanzania in the health sector. The Department of International Development [UK Aid] supports programmes in Tanzania in reproductive health, water and is finalising a new £32.96 million Nutrition programme to reach over 3 million mothers and children.”

  The medical equipment was sent to Tanzania, along with equipment for the Fire and Rescue Services and Police in a 42 feet container, organised by National Police Aid Convoys.  It is a UK based charity, staffed by volunteers, that collect, sort and then dispatch this sort of equipment as donations to partner agencies all over the world.

  On 11th December 2014 the High Commissioner presented equipment for fire fighters and Police and on the mainland to Home Affairs Minister Mathias Chikawe. 
  This included protective clothing for fire fighters, breathing apparatus, medivac chairs and traction splints.

  On Wednesday 7th January, she presented equipment from another container sent to Zanzibar to the Zanzibar Police Commissioner and the Fire and Rescue Service Commissioner.  We were delighted to hear that the equipment proved useful in the rescue of people injured following the collapse of a building in Stone Town. 

  DFID is supporting a new £32.96 million Nutrition Programme (ASTUTE) to combat stunting in children aged under 5.  ASTUTE is a 5 year programme (from 2014/15 to 2019/20) with of funding. This will support interventions to improve early childhood development and reduce the prevalence of stunting (low height for age) in Tanzanian children under 5 years old. It will focus on the first 1000 days of life from conception.

  The UK is funding UNICEF in two regions and another group of organisations working in 5 regions. The programme will reach over 3 million mothers and children. The aim is to ensure that over 50,000 children under five years will not be stunted and have enhanced overall development. It should reduce the prevalence of stunting in Tanzanian children aged five by at least 7 percentage points in 8 target regions. 

  DFID is also providing £22 million for the Family Planning Programme Phase II over a four year period (2014-2018). This is designed to increase women’s use of family planning and the availability of comprehensive post-abortion care services across Tanzania.  The programme is expected to reach over 1 million women by 2018 and result in over 916,000 fewer unintended pregnancies and 2,300 fewer maternal deaths.

   It will include training for health workers, outreach services to rural areas, and provide contraceptives to 80,000 young women to avoid unwanted pregnancies and reduce risk of unsafe abortions. Support will also be given for 28,000 women who have suffered sexual violence to both recover and to be able to advance their court cases, making the environment more supportive for women.
  HE Dianna Melrose The British High Commissioner hands over an adult hand training model to Hon Seif Rashid Minister of Health and Social Welfare.
  HE Dianna Melrose The British High Commissioner hands over Protective suits to Hon Seif Rashid Minister of Health and Social Welfare.
  HE Dianna Merlose the British High Commissioner hands over Pediatric Leg traction to Hon Seif Rashid Minister of Health and Social Welfare .

  0 0
 • 01/09/15--07:42: Bei ya Madafu


 • 0 0  0 0

  DSC_0019
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) alipoitishia mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza mara baada kuhitimisha ziara zake Kanda ya ziwa. Kushoto ni Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya mratibu mkazi wa UN Tanzania, Bi. Chitralekha Massey.

  Na Mwandishi wetu, Mwanza
  MRATIBU wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la maendeleo la Umoja huo, UNDP, Alvaro Rodriguez ameutaka uongozi mkoa wa Mara kuanzia Polisi hadi serikali ya mkoa kuweka kipaumbele kumtafuta binti albino ambaye ametekwa na watu wasiojulikana siku 14 zilizopita.

  Hayo aliyasema jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini

  Mwanza baada ya kutembelea mkoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mara, Shinyanga na Mwanza kuangalia miradi inayotekelezwa na Umoja wa Mataifa pamoja na masuala ya haki za binadamu.

  Alisema serikali kupitia Mkuu wa mkoa na Kamanda wa polisi mkoa wahakikishe wanaendelea kumtafuta na kulipa suala la Pendo Emmanuel (4) kipaumbele .

  Pendo alitekwa na watu wasiojulikana baada ya mlango wa nyumba yao kuvunjwa Desemba 27,2014 kwa jiwe la fatuma katika kijiji cha Ndami tarafa ya Mwamashinda,wilayani Kwimba mkoani hapa ambapo hadi sasa bado hajapatikana.

  Aidha aliwataka wananchi na viongozi kuhakikisha usalama wa watu wenye ulemavu kwani wao ni binadamu kama binadamu wengine na wanahitaji haki yao ya msingi ya kuishi bila hofu na manyanyaso kutoka kwa jamii inayowazunguka.

  Mwakilishi huyo wa Umoja wa mataifa alisema katika mkutano huo kwamba hata kurundikana kwa watoto walemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga ni matokeo ya mauaji yanayoendeshwa dhidi yao na kusema suluhisho la tatizo hilo ni jamii kuwakubali watu wenye ulemavu wa ngozi.

  Tayari watu 15 wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wa kuhusika na uporwaji wa mtoto huyo akiwemo baba mzazi, Emmanuel Shilinde.

  Pamoja na kuzungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza, kuelezea ziara yake katika Ukanda wa Ziwa, Mwakilishi huyo pia alizuru wilaya ya Magu na kukagua mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ,UNICEF, wenye lengo la kuhakikisha haki inatetendeka dhidi ya wale wanaonyanyasa watoto na haki zao za kibinadamu zinahesmiwa.
  DSC_0095
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.


  0 0

  Kufuatia kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji na hivi sasa kuendelea kwa zoezi la kuapishwa kwa viongozi hao katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kumejitokeza tabia ya baadhi ya wananchi kufanya vurugu na fujo katika zoezi hilo.

  Baadhi ya wananchi wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kufanya fujo na vitendo vya vurugu ikiwemo kuwapiga baadhi ya watendaji wanaosimamia zoezi la kuapisha na kuwapiga viongozi wateule waliochaguliwa kihalali na wananchi kwa madai kuwa hawakushinda kihalali katika uchaguzi huo jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni  na taratibu za nchi.

  Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kwa wananchi wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake kama mtu hakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo, afuate utaratibu wa kuwasilisha malalamiko yake kwenye ngazi husika ili yaweze kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria. 


  Aidha, Jeshi la Polisi linawata Wakurugenzi na Maafisa watendaji wenye dhamana ya kusimamia mchakato wa kuwaapisha wenyeviti waliochaguliwa, kufuatilia kwa karibu migogoro inayojitokeza na kuitatua migogoro hiyo mapema ili kuepusha migongano inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

  Jeshi la Polisi halitamvumilia mtu ama kikundi chochote kitakachofanya vurugu ama fujo kwa kisingizio cha ushabiki wa siasa na badala yake atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

  Imetolewa na:
  Advera J. Bulimba - SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.

  0 0  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kufungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo (kushoto) Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na Prof,Dk. Mahmoud Quresh Mwakili wa taasisi ya ND kutoka Spein sherehe hizo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pilikushoto) na Makamo wa Kwanza wa Reais maalim Seif Sharif Hamad wakipata maelezo kutoka kwa Prof,Dk. Mahmoud Quresh Mwakili wa taasisi ya ND kutoka Spein wakati alipotembelea mashine za upasuaji baada ya kulifungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo (kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dk.Jamala Adam Taibu pia sherehe hizo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange alipokuwa akimshukuru kwa kutoa vitabu  kwa Chuo cha Ulinzi na makataba zingine za JWTZ wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa January 9, 2015.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi baadhi ya vitabu   na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. Rais Kikwete amekabidhi vitabu hivyo 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa January 9, 2015. Rais kikwete, ambaye ameshachangia jumla ya vitabu 2752 katika maktaba ya chuo hicho na maktaba zingine za JWTZ  katika vipindi tofati, amesema elimu imo vitabuni, na ili kuelemika yapaswa mtu usome vitabu, na kwamba taasisi ya elimu inakamilika ikiwa na vitabu.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na maafisa waandamizi wa JWTZ wakiangalia vitabu wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa January 9, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhe Jacky Zoka, Balozi wa Tanzania nchini Canada na Mhe Ali Siwa, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, walipofika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa January 9, 2015 kuaga rasmi kabla ya kwenda kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi. 
  PICHA NA IKULU.


  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu.

   Wakazi wa kijiji cha Ndoleleji  wilayani Kishapu wakimsikiliza kwa makini  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Profesa Muhongo ameahidi kuwapatia umeme kabla  ya tarehe 30 Aprili, mwaka huu.

   Wakazi wa Bubiki wilayani Kishapu wakimkabidhi  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)  zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri  ya kusambaza umeme katika kata hiyo.

   Wakazi wa Kata ya  Seke Ididi wilayani  Kishapu  wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) mara baada ya kumkabidhi  zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri  ya kusambaza umeme katika kata hiyo.

   Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Nchambi akisisitiza jambo wakati  wa mkutano huo

   Wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani  Kishapu wakimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa tatu kutoka kulia)  zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri ya kusambaza umeme katika kata hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0


older | 1 | .... | 700 | 701 | (Page 702) | 703 | 704 | .... | 3283 | newer