Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

WADAU TUCHANGAMKIE NAFASI YA KAZI HII HUKO SUMATRA


BREAKING NEWWZZZZ: VIJANA WANAODAIWA KUWA NI PANYA ROAD WAFUNGA MITAA JIJINI DAR NA KUFANYA VURUGU KUBWA.

$
0
0
Sikiliza hapo chini taharuki ya panya Road ilivyozua tafrani na hofu kubwa kwa maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar. Baadhi ya Wadau walikumbana Live na rabsha hiyo ya Panya Road
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar,Kamanda Kova akitoa ufafanuzi wa habari za taharuki katika vyombo vya habari hususani televisheni,kuhusiana na sakata la kundi la Vijana wajiitao Panya Road,amesema suala hilo lilikuwa dogo,lakini baadhi ya watu wamelikuza na kupelekea hofu kubwa kwa Wananchi ''Jiji mpaka sasa liko salama na wananchi watulie wasiwe na hofu kwa sababu jeshi la Polisi liko imara kuhakikisha amani inakuwepo ya kutosha,na hao vijana hawawezi kulishinda Jeshi la Polisi'',alisema.Alisema Wananchi waondoe hofu waendelee na shughuli zao kama kawaida.
 katika hali isiyo ya Kawaida na ya kuogopesha,kumeibuka taharuki kubwa usiku huu kwa Wakazi wa maeneo mbalimabali ya jiji la Dar,ikiwemo,Sinza,Kinondoni,Mwananyamala,Mabibo,Magomeni,Manzese,Kagera na Mburahati kwa kile kinachoelezwa kuwa vijana waitwao Panya Road wamevamia maeneo hayo na kuwajeruhi watu kwa vitu vyenye ncha kali,visu na mapanga na kuwapora vitu (mali zao) walivyokuwa navyo,kama vile haitoshi baadhi yao wamevunjiwa vioo vya magari yao.
Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa vijana hao waitwao Panya Road wameibuka na kufanya uhalifu huo mara baada ya tukio la Mwenzao mmoja kudaiwa kuuwawa na Polisi.

Aidha Chanzo hicho kimebainisha kuwa baada ya taarifa kusambaa kwa haraka,kimeeleza kuwa Jeshi la Polisi limeingia kazini kuwasaka watuhumiwa hao walioibua tafrani kubwa usiku huu. 

Wadau tutazidi kuwaletea taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana.

WAZIRI MKUU AKIWA WILAYANI MLELE

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari ya Usevya wakati alipoitembeklea na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo Januari 1, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Usevya wakati alipoitembeklea na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo Januari 1, 2015.

WANAOKAA KWENYE NYUMBA MBOVU MJI MKONGWE ZANZIBAR WATAKIWA KUHAMA - BALOZI SEIF IDDI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia nyumba iliyoporomoka dari na kujeruhi wakazi wake watatu hapo Mtaa wa Ukutani Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Mmiliki wa Nyumba Hiyo Bwana Mzee Abdulla Juma.
Balozi Seif akiwaagiza watu wanaoishi ndani ya nyumba iliyoporomoka dari Mtaa wa Ukutani kuhama ili kunusuru maisha yao kutokana na uchakavu wa nyumba hiyo. Aliyepo mwanzo kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee.
Balozi Seif akiwa pamoja na Mmiliki wa nyumba iliyoporomoka Dari eneo la Ukutani Bwana Mzee Abdulla Juma na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee wakiangalia hali halisi ya mazingira ya nyumba hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza wananchi wanaoishi kwenye nyumba mbovu na zile zilizochakaa ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar wafanye utaratibu wa kuhama kwenye nyumba hizo mapema iwezekanavyo ili kunusuru maisha yao.

Alisema Serikali kamwe haitakuywa tayari kuachia wananchi wake wanaendelea kuishi katika mazingira ya hatari wakati njia za kuepuka hatari hizo zipo na wala hazina gharama yoyote.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo alipofanya ziara fupi ya kukagua Nyumba ya Bwana Mzee Abdulla Juma ambayo iliporomoka dari sehemu ya sebule na kujeruhi wakaazi watatu wa nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Ukutani Mjini Zanzibar.

Watu waliojeruhiwa ni wadogo wa Mmiliki wa Nyumba Hiyo Bwana Haroun Abdulla Juma na Fahim Abdulla Juma waliolazwa Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu pamoja na Peter Monga aliyetibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Balozi Seif aliutaka uongozi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar kuendelea kuzifanyia uhakiki nyumba zote zilizomo ndani ya mji mkongwe na hatua zichukuliwe mara moja na taasisi zinazohusika katika kuwahamisha wakaazi wanaoishi kwenye nyumba zisizostahiki kuishi watu.

Mapema Mmiliki wa Nyumba hiyo Bwana Mzee Abdulla Juma alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba mkasa huo umetokea majira ya saa 11.00 za asubuhi wkati dari ya nyumba hiyo sehemu ya sebule ilipoporomoka.

Bwana Mzee alisema wakaazi wa nyumba hiyo kwa kushirikiana na majirani walilazimika kuuvunja mlango mkuu wa nyumba hiyo ili kumnusuru Mtoto wa mdogo wake aliyelazwa Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja baada ya kuvunjika mguu.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Mussa Awesu Bakari alisema watendaji wa Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wataalamu wa Taasisi za majengo na ujenzi tayari wameshafanya uhakiki wa Nyumba 75 zilizomo ndani ya Mji Mkongwe .

Nd. Mussa alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba zoezi hilo linaendelea kwa lengo la kubaini nyumba zisizofaa kutumiwa kwa makazi ya kawaida ya binaadamu.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

MAJENGO YABOMOKA MENGINE HATARINI KUWAANGUKIA WATOTO,MH. RIDHIWANI ASIKITISHWA

$
0
0
Na John Gagarini, Kibindu

WANAFUNZI wa shule ya Msingi Kibindu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wako hatarini kuangukiwa na vyumba vya madarasa wanayosomea kutokana na ubovu wa vyumba hivyo ambavyo vimejengwa miaka ya 50.

Mwishoni mwa mwaka jana vyumba vya madarasa mawili na ofisi ya mwalimu vilianguka na kuezua mapaa ya vyumba vine vya madarasa na ofisi ya mwalimu mkuu baada ya kutokea mvua kubwa amabyo iliambatana na kimbunga.

Shule hiyo ambayo ina wanafunzi 970 hawakuwepo shuleni kwani walikuwa wako likizo ya mwisho wa mwaka baada ya shule kufungwa mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete ambaye alitembelea shuel hiyo ofisa mtendaji wa kijiji cha kibindu Juma Athuman alisema kuwa mvua hiyo kubwa iliambatana na kimbunga ilinyesha Desemba 28 mwaka jana  na kuangusha majengo mawili ya madarasa pamojana na kueezua mapaa ya vyumba  vinne vya madasa na  na ofisi ya mwalimu mkuu.

Athuman alisema kuwa kimunga hicho pia kilisababisha ufa katika majengo mengine kadhaa ya madarasa katika shule hiyo na  kuwa katika hatari kubwa ya kuanguka.

“Hali hiyo inatia wasiwasi kwa wanafunzi wnaotarajiwa  kuanza  masomo Januari  14 mwezi huu kuwa hatarini kuangukiwa na majengo hayo endapo hatua za dharura hazitachukuliwa,” alisema Athuman.

Akizungumzia  mara  baada ya kutembelea shule hiyo  Mbunge wa Jimbo la Chalizne Ridhiwani Kikwete amesikitishwa na hali hiyo ya majengo ya shule hiyo  na kusema kuwa anafanya taratibu za kuwasiliana na mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kuona jinsi ya kujenga upya shule hiyo.
Diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya aliyenyanyua mikono juu akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kulia aliyevaa kofia ya kijani kufuatia mvua kubwa kubomoa madarasa ya shule ya Msingi Kibindu.
Moja ya madarasa ya shule ya msingi Kibindu likiwa limebomoka kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa mwaka jana.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa Habari mbele ya jengo la shule ya Msingi Kibindu ambalo lilianguka kufuatia mvua kubwa ziulizonyesha mwishoni mwa mwaka jana kushoto ni diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza wananchi wa Kata ya Kibindu alipofika kuwajulia hali kufuatia mvua kubwa ziulizonyesha mwishoni mwa mwaka jana.

MEMORIAL ANNOUNCEMENT

$
0
0
In Loving Memory
Alice Kidere Rugumyamheto

Oct 6th1947 ~Dec 25th 2013


It is one year exactly since you were called to glory from this world

As we pray for you on this day you are dearly remembered by your

Loving Husband Joseph Rugumyamheto

Son’s Niyongabo, Jerome and Atanasio

 Granddaughter Ella and Grandson Prince.

Beloved brothers sisters and so many of your friends and relatives.

Please Join us for a Memorial Service honoring Alice’s Life

Saturday 3rdJanuary 2015

At 9 o’clock in the morning

at the Anglican Church of St Michael’s, Kunduchi, Dar es Salaam


“ If I say my foot slips, Your mercy, O Lord, will hold me up. 
In the multitude of my anxieties within me, your comforts delight my soul.”


(Psalm 94: 18 & 19)

DKT. SHEIN AZINDUA MAEGESHO NA NJIA YA KUPITIA NDEGE (APRON AND TAXIWAY) ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia Tanzania Monthe Biyoudi wakikata utepe kuzindua maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar(kushoto0 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia Tanzania Monthe Biyoudi wakifungua pazia kwa pamoja kuzindua maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Ndege mbali mbali zikiwa katika Paki ikionesha sura halisi ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar ilivyo ambapo Ndege za mashirika mbali mbali ya ndege zinaouwezo wa kutua hapa nchini na kuweza kukuza pato la Taifa letu.

ZIFF YAWAKUMBUSHA WADAU WA FILAMU NCHINI KUWASILISHA FILAMU ZAO

$
0
0
WADAU wote wa Tasnia ya Filamu nchini,wanakumbushwa kuwa mwisho wa kupokea Filamu kwaajili ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) ni Tarehe 31/01/2015 kwa waandaaji filamu wote wa ndani na nje ya nchi.

"Kama wewe ni Mtanzania na unataka kuwasilisha filamu yako basi wasiliana na Ibra Mitawi +255 713 300997 au +255 783 300997 au mnaweza kutuma ofisini Zanzibar moja kwa moja, hatutapokea filamu yeyote baada ya tarehe hiyo". 

Tunaomba pia mjaribu kuweka filamu ikiwa ndani ya DVD moja na si Part 1 & 2, iwe kwaajili ya Festival. Na wale ambao wanaweza kuweka filamu zao online basi waingie www.ziff.or.tz na unaweza kusubmit online pia unaweza kutuma link ya YouTube au Vimeo katika filmdept@ziff.or.tz

 Nawatakia Heri ya Mwaka Mpya.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA TAHARUKI YA PANYA ROAD

WAGAWA VIPEPERUSHI MABARABARANI

$
0
0
 Makampuni mengi hapa jijini yamebuni utaratibu wa kuwatumia vijana wanaotembea kwa kutumia viatu vya matairi (Roller Skating) katika kusambaza ujumbe na matangazo yao mbali mbali,jambao hilo ni jema sana hasa ukizingatia kuwa sasa hivi swala la ajira ni changamoto.Vijana hawa hufanya kazi ya kugawa vipeperushi kwa wenye magari na watembea kwa miguu katika makutano makuu wa mabarabara hapa jijii Dar,kama walivyokuta na Kamera Mani wa Globu ya Jamii maeneo ya Magomeni Mapipa hivi karibuni.
Mmoja wa vijana hao akipiga misele barabarani.

Mh. Magufuli akutana na Watendaji wa CCM jimbo la Chato

$
0
0
Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Chato,Mh. John Pombe Magufuli (aliesimama) akizungumza na Watendaji mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliochaguliwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivi karibuni kwenye Jimbo hilo,wakati alipokutana nao kwa lengo la kuwapongeza kwa kuaminiwa na kuchaliwa na wananchi.
Sehemu ya Watendaji mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Chato waliochaguliwa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivi karibuni,wakimsikiliza Mh. Magufuli (hayupo pichani).

MSAMA AACHANA NA ROSE MUHANDO.!

$
0
0

HATIMAYE Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ameibuka na kutamka yeye si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kwa waimbaji wengine.
Kwa mujibu wa taarifa ya Msama kwa vyombo vya habari jana, yeye akiwa mlezi wa waimbaji wote wa muziki wa Injili, amekuwa akishirikana nao kwa karibu kutokana
na nafasi yake katika huduma hiyo ya uimbaji kwa kipindi cha miaka 15.
Msama, mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini kutokana na kuandaa matukio ya muziki huo kama Tamasha la Pasaka, uzinduzi wa albamu na Tamasha la Krismas, alisema ameamua kutoa tamko hilo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ambayo amekuwa akipata juu ya Rose. 
“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, kwamba pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayomualika na kushindwa kutokea.
“Lakini, naomba watumishi wa Mungu wanielewe katika hili, sipokei mialiko wala simzuii Rose. Mimi ninapokuwa na matamasha, nimekuwa nikimualika kama wafanyavyo wengine.
“Nimekuwa nikimlipa kiasi cha fedha anachotaka na hakuna zaidi, hivyo mimi sio Meneja wake,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza:

“Agosti mwaka huu, kampuni yangu ilidhamini uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu, haikuwa na maana kwamba ni Meneja wake. 
“Nilimualika uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa ya msanii John Lissu Oktoba mwaka huu, nilimlipa fedha, lakini hakutokea kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wengine ambao wamekuwa wakilalamikia tabia hiyo,” alisema Msama.
“Pia wiki iliyopita nilikuwa na Tamasha la Krismasi tulikubaliana aje katika maonesho hayo, lakini hakutokea na tulishamlipa,” alisema Msama kwa masikitiko na kuongeza kuwa amemsamehe na anamuombea kwa Mungu aweze kubadilika.
Alieleza kuwa hana tatizo na mwimbaji huyo, wala hana ugomvi naye, lakini amekuwa akipata taabu kutoka kwa baadhi ya wachungaji pale Rose anapoalikwa halafu hatokei na inaonekana yeye ndiye amemzuia.
“Sijawahi kupokea mialiko kwa niaba ya Rose, kila kitu anafanya mwenyewe, hivyo ni vyema wadau wakafahamu hilo,” alisema Msama na kusema angekuwa mwepesi wa kulalamika, angeshafanya hivyo muda mrefu dhidi ya Rose.
Aidha, Msama amekana kuhusiana na madai ya Rose kutumia dawa za kulevya na kusisitiza kuwa hajawahi kumuona akijidunga kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti na kuongeza kama ikiwa ni kweli, hilo pia ni suala binafsi.
“Baadhi ya vyombo vya habari vinaandika ni mjamzito, nafikiri pia hayo ni mambo yake binafsi na hakuna mtu mwenye haki au uhalali wa kuhoji hilo.Yule ni mtu mzima na mwenye kujielewa,” alisema Msama.
Rose ni mwimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini aliyejipatia sifa ndani na nje ya ukanda wa Afrika Mashariki ambaye mwishoni mwa mwaka 2013, alisaini mkatabawa kufanya kazi na kampuni ya muziki ya Sony ya Afrika Kusini. 

Miongoni mwa albamu zilizompa umaarufu Rose kiasi cha kuwa alama ya mafanikio ya muziki wa injili nchini, ni ‘Uwe Macho,’ Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, ‘Mungu Anacheka’ na Wololo na Kamata Pindo la Yesu aliyoachia hivyo karibuni.

PBZ WAKABIDHI MABASI YA ABIRIA KWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA ABEID AMANI KARUME,ZANZIBAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour Mohamed akikata utepe kama ishara ya kukabidhi mabasi matatu kwa Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Bi Zaina Ibrahim Mwalukuta (kushoto) yaliyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya kuchukulia abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume yenye thamnai ya shilingi za Kitanzania MIa Tatu na Ishirini Millioni,(kulia) Mkurugenzi Masoko wa PBZ Seif Suleiman.
Miongoni mwa Mabasi yaliyotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) likiwa tayari limeanza kazi kazi ya kubeba abiria wanaokwenda kupanda ndege katika Kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume Kama inavyoonekana Pichani.[Na Mpiga Picha Maalum.]

MH. RIDHIWANI KIKWETE AANZA ZIARA YA KIKAZI KATIKA VIJIJI 40 CHALINZE

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea vijiji 40 jimboni humo.Pia Ridhiwani alishauri shule hiyo yenye majengo yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha maafa zaidi hadi itakapojengwa upya.

taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia kutoka Madimba - Mtwara, SongoSongo - Lindi, na Pwani hadi Dar es Salaam


DJ JERRY KOTTO NDANI YA KIOTA CHA HISAJE PARK BOKO JIJINI DAR

$
0
0
 Dj Jerry Kotto akipata picha na kamera ya Vijimambo ndani ya kiota cha Hisaje Park kilichopo Boko jijini Dar es Salaam kiota maarufu kwa nyimbo za zamani (old school) kila siku kuanzia Jumanne hadi Jumamosi na hakuna kiingilio.dj Jerry Kotto ni moja kati ya maDj wa miaka mingi hapa nchini.
Mitambo ya kisasa ndani ya kiota cha Hisaje Park Karibuni.

Mzinga watokea kwenye makutano ya Shule ya Msingi Oysterbay

$
0
0
 Wasamaria wema wakifanya utaratibu wa kumuokoa Dereva wa Gari aina ya Isuzu Trooper iliyopiga mweleka katika makutano ya Shule ya Msingi Oysterbay jijini Dar es salaam mara baada ya kugongana na gari nyingine aina ya Toyota Vitz iliyokuwa ikitokea upande wa Coco Beach mchana wa leo na kupekea dereva wa Gari hii (alikuwa ni Mama mtu mzima ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) kuumia sehemu ya kiuno na mkono.Gari hii ilikuwa inatokea upande wa St. Peter's kuelekea Morogoro Store na Vitz ilikuwa ikitokea upande wa bahari na kuvuka ghafla barabara hiyo.
 Mashuhuda wakiwa wameizunguka gari hiyo mara baada ya kufanikiwa kumtoa Mama aliekuwa akiendesha Gari hilo.
 Hivi ndivyo ilivyo hii Toyota Vitz baada ya kuhongana na Isuzu Trooper iliyopinduka.Picha na Mdau Pius Micky.

TAMASHA LA KUMUENZI MZEE KAWAWA LAFANA

$
0
0
 Wachezaji  Bao nguli hapa nchini wakioneshana ubingwa katika Tamasha la Kumuenzi aliekuwa Mlezi wa Mchezo huo Hayati  Rashidi Mfaume Kawawa.
 Rais wa Chama cha Mchezo wa Bao mchini Bw Mandei Likwepa akionesha moja ya barua kwa waandishi wa habari hawapo pichani iliyo andika na aliekuwa Mlezi wa Mchezo huo Hayati  Rashidi Mfaume Kawawa enzi za uhai wake.

 Mfanya biashara maarufu nchini Bw Mohamed Sharifu akiongea jambo mbele ya wanahabari, wapenzi na wachezaji wa mchezo wa Bao walioudhuria Tamasha hilo.

 Wajukuu wa Mzee Kawawa kutoka kushoto ni  Mariamu Msemo na wamwisho kulia ni Adam Chacha wakichuana vikali katika mchezo wa Bao walio ucheza katika Tamasha la kumuenzi  Hayati Babu yao Mzee Kawawa.

Mjukuu wa Mzee Kawawa Bi Dora Abdala akichuana vikali na mmoja kati ya chezaji nguli wa mchezo huo katika Tamasha la kumuenzi  Hayati Babu yao Mzee Kawawa.

YANGA YAIZAMISHA SIMBA 4-3 KATIKA MCHEZO WA MWAKA MPYA ULIOANDALIWA NA PSPF

$
0
0
TIMU ya Yanga veterani imeibuka mshindi wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba veterani ulioandaliwa na PSPF, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 4-3 na kubeba kombe. Mchezo huo ulifanyika tarehe 1 Januari 2015 katika uwanja wa chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.

Hadi dakika tisini zinakamilika timu hizo zilitoka sare ya bao moja kwa moja, mabao hayo yaifungwa na Omari kapilima kwa upande wa Yanga na Barnabas Sekolo kwa upande wa Simba.

Bingwa wa mchezo huo alipatikana kwa njia ya matuta, ambapo kwa upande wa Yanga walipata penalty ni Empram makoye, Ngada Shaganga, Ismail Issa na Deo Lucas. Yanga ilikuwa ikifundishwa na Peter Tino Kasongo Athumani kwa Kwa upande wa simu waliozamisha penati ni Athumani Chama, madaraka Selemani na Issa Manofu. Simba ilikuwa chini ya Kasongo Athumani.

Lengo la mchezo lilikuwa kutoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya karibu hususani katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka. PSPF itatumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mpya ambazo Mkopo wa Elimu na Mkopo wa Kuanza Maisha.
Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Simba.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akisalimiana na wachezaji wa Yanga.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akisalimiana na wachezaji wa Simba.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AZINDUA WA BARABARA YA MKAPA AWAMU YA PILI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Zanzibar Seif Ali Iddi akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Barabara ya Amani- Mtoni kwa awamu ya pili ya ujenzi wake katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. (kushoto alievaa kofia ya pama) Katibu Mkuu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Malik Akili.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuzindua Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar (kushoto) Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji.

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images