Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

MISS SINGIDA 2014 DORICE MOLLEL ATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WODI YA WATOTO NJITI

$
0
0
DSC03176
Miss Singida 2014 Dorice Mollel akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa mjini Singida. Miss Singida huyo ambaye mwaka jana alikuwa pia mshindi wa kwanza Miss kanda ya kati na kushika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema ametoa msaada huo kwa sababu na yeye alizaliwa mapacha njiti.

Na Nathaniel Limu, Singida
JUMLA ya watoto 284 hadi 300, huzaliwa kila mwaka katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini Singida wakiwa hawajatimiza umri wa kawaida wa kuzaliwa (njiti).

Kati ya watoto hao,inakadiriwa 60 hadi 83 hufariki kutokana na sababu mbalimbali kila mwaka ikiwemo ya tatizo la kupumua.

Hayo yamesemwa na kaimu mganga mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida,Dk.Daniel Tarimo,wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba vitakavyotumika kwenye wodi ya watoto njiti katika hospitali ya mkoa mjini hapa.

Kuhusu watoto hao njiti wanaofariki dunia,Dk.Tarimo alisema vifo vingi vinachangiwa na baadhi ya akina mama wajawazito kujifungulia nyumbani mahali hakuna wataalamu wa huduma ya afya.

“Watoto wa aina hii kwa kawaida wanakuwa na matatizo ya kupumua.Sasa mama akijifungulia nyumbani,wakiwa njiani kukimbiza watoto/mtoto wa aina hiyo hospitalini,mtoto/watoto husika hupata tatizo la kupumua linalopelekea vifo vyao”,alifafanua zaidi Dk.Tarimo.
DSC03187
Miss Singida 2014 Dorice Mollel akimkabidhi Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, msaada wa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwa wodi ya watoto njiti.


YAMOTO BAND LIVE KWA MARA YA KWANZA KWENYE JIJI LA LONDON

$
0
0
 Confirmed...21Feb2015..Yamoto! Yamoto! Yamoto Band Live in the UK For the first Time Ever...When we Say Live, we mean 

Live with Full Band & Dancers...
This is one show that's not to be Missed... Sponsored by @officialjestinageorgeblog @bongodeejays@zuriihouseofbeauty

 Zurii House of Beauty CEO akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa yamoto band Maromboso na Aslay  baada ya makubaliano ya kuwadhamini band hiyo kuja  kufanya show yao jijini London @maromboso @aslayisihaka
 Zurii House of Beauty CEO akiwa kwenye picha ya pamoja na mameneja wa yamoto band
 It's gonna be bigger and better! UK & Europe people Save the Date. Their Live Performance is a must see..If you love live music
Make sure you get your tickets mapemaaaa...Hili ni Bonge la show kuwahi kutokea na watoto wameahidi kuweka historia

Rais amteua George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju (pichani) kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.



3 Januari, 2015

DKT. MAGUFULI AWAPONGEZA CCM CHATO KWA USHINDI MKUBWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwasalimia baadhi ya Wajumbe waa Chama cha Mapinduzi CCM waliofika katika hafla ya kupongezwa baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akihutubia mamia wa wanachama wa CCM wilaya ya Chato waliojitokeza katika mkutano huo wa kupongezana.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akipakua wali kwa ajili ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo wa kujipongeza kwa ushindi.

MH. RIDHIWANI KIKWETE KUHARAKISHA MAENDELEO CHALINZE

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Changarikwa wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kuchagua viongozi wa Seikali ya Kijiji wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.CCM imepata ushindi wa Vijiji vyote katika 74 katika jimbo hilo.
 Ridhiwani akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika kijiji hicho ambapo aliwataka kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa ama sivyo vijiji vitageuka jangwa.
 Mkazi wa Kijiji cha Kwaluhongo, Dustan Sangi akiuliza swali kwa Mbunge wake Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano  uliofanyika kijijini hapo.

mtoto wa Raila Odinga afariki Dunia leo

$
0
0
Mtoto wa aliekuwa Waziri Mkuu wa Kenya,Raila Odinga aitwae Fidel Odinga (pichani) amekutwa akiwa amefariki nyumbani kwake huko Karen,jijini Nairobi mapema leo asubuhi.

Taarifa za awali zilieleza kuwa, Fidel alitoka nyumbani kwake jana usiku kwa lengo la kujumuika na marafiki zake kwa matembezi na burudani za mwisho wa wiki na alirejea nyumbani kwake alfajiri ya leo na haijulikani ni nini kilichosababisha kifo chake.

Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini Kenya,wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo hicho.

Kundi la wabunge pamoja na maseneta wa Kenya waliwasili nyumbani kwa Mh. Raila Odinga baada ya kupata habari hizo. Maafisa wanaosimamia kesi hiyo wanasema kuwa wanataka kujua ni wapi Fidel alikuwa usiku wa jumamosi na alikuwa na nani.

JKT KANEMBWA YAIOMBA HALMASHAURI YA KIGOMA KUMALIZA MCHAKATO WA KUKIPATIA HATI MILIKI YA MAENEO YA KIKOSI

$
0
0
Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,Kigoma

KAMANDA wa Kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa (JKT) 824 KJ cha Kanemwa wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma Luteni Kanali Erasmus Bwegoge ameomba Halmashauri ya wilaya hiyo kutilia mkazo na kuhitimisha mchakato wa kupata hati miliki ya maeneo ya kikosi hicho ili kuondoa uwezekano wa wananchi kuvamia maeneo hayo jambo ambalo linaweza kuzua migogoro na kuhatarisha mahusiao baina ya Jeshi na wananchi.

Luteni kanali Bwegoge ametoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni kanali mstaafu Issa Machibya wakati wa mahafali ya nne ya kuhitimu mafunzo ya jeshi kwa mujibu wa sheria .

''Mgeni rasmi tunaomba Halmashauri yetu ya Kakonko suala la kupata hati miliki ya maeneo ya kikosi chetu hiki,hii itatusaidia sana kuondoa migogoro ya ardhi baina ya wananchi na jeshi,pia itasadia kutokuwepo na wananchi wanaovamia katika maeneo ya jeshi''alisema.

Alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoo hiyo ya ardhi kikosini hapo pia kuna changamoto za huduma bora za afya alisema jumla ya vijana 1127 wa oparesheni ya miaka 50 ya muungano wamehitimu mafunzo hayo ambao ni wahitimu wa kozi ya ualimu na wale waliomaliza kidato cha sita .

Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa nchini(JKT) Meja Abdulrahmani Dachi na mgeni rasmi katika maafali hayo Mkuu wa M koa wa Kigoma Luten Kanali mstaafu Issa Machibya wamewataka vijana hao kutumia mbinu walizojifunza kudumisha ulinzi na usalama wa nchi pamoja na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika jamii na si kulihujumu Taifa kwa namna yeyote.

''Muende mkawe mfano wa kuigwa katika jamii pia mtumie mbinu mlizofundishwa katika kudumisha ulinzi na usalama wa nchini pia mkawe mfano katika shughuli za maendeleo katika jamii''alisema Mkuu wa Mkoa
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa wakiwa tayari kwaajili ya Gwaride.
Wahitimu wakipita mbele ya mgeni (hayupo pichani)Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya rasmi kwa mwendo wa pole.

Kwanini Bei ya mafuta kwa walaji haishuki kwa kasi? - Mh. Zitto Kabwe

$
0
0
Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa. Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40% haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta ikiwemo wenye daladala na kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua. Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli, bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.

EWURA,inasemekana, wamesema kuwa bei za hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu waagizaji huagiza kwa ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo la bei. Hata hivyo bei zimeanza kushuka toka mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa wananchi. Ingekuwa bei ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na sababu za kununua ' bulky' huwa hazitolewi.

Ni kweli kwamba Tanzania hununua mafuta yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo. Lakini hao wasafishaji hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo ni dhahiri lazima bei za pampu zipungue. Vile vile ni kweli kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi hawawezi kuona unafuu wa bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za kigeni na kuuzwa kwa Sarafu yetu. Hata hivyo kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta ni 40% wakati shilingi imeshuka kwa chini ya 10%. Katika hali ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.

Ni dhahiri mamlaka za nchi na hasa EWURA wanapaswa kueleza kwa umma ni Kwanini bei za mafuta hazishuki kulingana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia. Wananchi wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo basi bei hizo zishuke na wananchi wafaidike na punguzo hilo.

Zitto Kabwe, Mb

DKT. SHEIN AFANYA UFUNGUZI WA BARABARA UMBUJI,ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Viongozi mbali mbali wakitembea katika Barabara ya Njia NNe -Umbuji Wilaya ya Kati Unguja mara baada ya kuifungua rasmi leo ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kufungua Barabara ya Njia Nne-Umbuji Wilaya ya Kati Unguja leo iliyojengwa na Serikali kupitia kitengo cha Idara ya ujenzi Barabara UUB ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar (kulia) Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji na (kushoto) Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya kufungua Barabara ya Njia Nne-Umbuji Wilaya ya Kati Unguja leo iliyojengwa na Serikali Mapinduzi kupitia kitengo cha Idara ya ujenzi Barabara UUB ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija.

WAENDESHA BODABODA WAJINAFASI KWA MIPASHO DAR LIVE

$
0
0
WAENDESHA bodaboda na wamiliki wake walijimwaya na bonge la burudani kutoka kwa Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa na kundi lake la Ogopa Kopa Modern Taarab sambamba na mkali wa muziki wa Kigodoro, Msaga Sumu, kwenye tamasha lao lililofanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhiem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Khadija Kopa akijipinda kimadaha wakati akifanya ‘mavituz’ stejini.
Kundi la Ogopa Kopa kazini
Shadya Chotara naye akionesha makali yake.
Mashabiki wakifurahia burudani.

WAENDESHA  bodaboda na wamiliki wake walijimwaya na bonge la burudani kutoka kwa Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa na kundi lake la Ogopa Kopa Modern Taarab sambamba na mkali wa muziki wa Kigodoro, Msaga Sumu, kwenye tamasha lao lililofanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhiem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
PICHA : RICHARD BUKOS/GPL. 
Picha zaidi BOFYA HAPA

Usiku wa Old is Gold taarab kila Jumapili ndani ya Safari Carnival, Kawe.Dar es salaam

$
0
0
Na Andrew Chale
USIKU wa Old is Gold taarab  unatarajiwa kurindima ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikochezni B, kwa wadau kupata burudani ya muziki wa mwambao wa kizamani.
Kwa mujibu wa waandaji wa usiku huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin alieleza kuwa  ni kila Jumapili  ndani ya ukumbi huo utakuwa na burudani ya kipekee kwa nyimbo za mwambao pamoja na ‘surprise’ mbalimbali kwa watakaofika hapo.
“Kila jumapili  kwa kiingilio cha sh 5,000 tu. Wapenzi wa muziki wa wambao  watashuhudia shoo ya Usiku wa Old is Gold ndani ya Safari Carnival” Alisema Asia Idarous.
Aliongeza kuwa, mbali na burudani ya taarab za zamani  pia kutakuwa na ‘Surprise’ mbalimbali" kwa wadau watakaojitokeza kwenye usiku huo.
Aidha,  Asia Idarous alisema usiku huo, pia umedhaminiwa na  Safari Carnival, Fabak fashions, Clouds
Fm, Gone Media, Maji Poa, Michuzi Media Group na wengineo.

DIAMOND ATEULIWA KUTUMBUIZA TUZO ZA MWANASOKA BORA CAF

$
0
0
Na Saleh Jembe
Msani Nasib Abdul ‘Diamond’ amechaguliwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye hafla ya utoaji tuzo za mwanasoka bora Afrika 2014. Diamond atatumbuiza katika tuzo hizo ambazo wachezaji 25 nyota barani Afrika wamechaguliwa kugombea tuzo hizo. Hafla hiyo itafanyika Januari 8, 2015 jijini Lagosi Nigeria. Mwanasoka Bora, Yaya Toure raia wa Ivory anayeitumikia Manchester City ya England ni kati ya watakaowania nafasi hiyo. 

Wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika:

1.    Ahmed Musa                          (Nigeria, CSKA Moscow)
2.    Asamoah Gyan                       (Ghana, Al Ain)
3.    Dame N’doye                         (Senegal, Lokomotiv Moscow)
4.    Emmanuel Adebayor               (Togo, Tottenham)
5.    Eric Maxim Choupo-Moting          (Cameroon, Schalke 04)
6.    Fakhreddine Ben Youssef            (Tunisia, CS Sfaxien)
7.    Ferdjani Sassi                          (Tunisia, CS Sfaxien)
8.    Yao Kouassi Gervais ‘Gervinho’ (Cote d’Ivoire, AS Roma)
9.    Islam Slimani                          (Algeria, Sporting Lisbon)
10. Kwadwo Asamoah                   (Ghana, Juventus)
11. Mehdi Benatia                         (Morocco, Bayern Munich)
12. Mohamed El Neny                   (Egypt, Basel)
13. Pierre-Emerick Aubameyang        (Gabon, Borussia Dortmund)
14. Raïs M'Bolhi                           (Algeria, Philadelphia Union)
15. Sadio Mané                            (Senegal, Southampton)
16. Seydou Kieta                          (Mali, As Roma)
17. Sofiane Feghouli                     (Algeria, Valencia)
18. Stephane Mbia                       (Cameroon,  Sevilla)
19. Thulani Serero                        (South Africa, Ajax)
20. Vincent Aboubakar                  (Cameroon, Porto)
21. Vincent Enyeama                    (Nigeria, Lille)
22. Wilfried Bony                          (Cote d’Ivoire, Swansea)
23. Yacine Brahimi                       (Algeria, Porto)
24. Yannick Bolasie                       (DR Congo, Crystal Palace)
25. Yaya Toure                            (Cote d’Ivoire, Man City)

Wanaowania tuzo za Mwanasoka Bora Afrika( Kwa wachezaji wanaocheza Afrika)

1.    Amr Gamal                     (Egypt, Al Ahly)
2.    Abdelrahman Fetori          (Libya, Ahly Benghazi)
3.    Bernard Parker               (South Africa, Kaizer Chiefs)
4.    Bongani Ndulula               (South Africa, Amazulu)
5.    Akram Djahnit                 (Algeria, ES Setif)
6.    Ejike Uzoenyi                   (Nigeria, Enugu Rangers)
7.    El Hedi Belamieri              (Algeria, ES Setif)
8.    Fakhereddine Ben Youssef   (Tunisia, CS Sfaxien)
9.    Ferdjani Sassi                    (Tunisia, CS Sfaxien)
10. Firmin Mubel Ndombe          (DR Congo, AS Vita)
11. Geoffrey Massa                  (Uganda, Pretoria University)
12. Jean Kasusula                     (DR Congo, TP Mazembe)
13. Kader Bidimbou                  (Congo, AC Leopards)
14. Lema Mabidi                       (DR Congo, As Vita)
15. Mudathir Al Taieb                (Sudan, Al Hilal)
16. Roger Assalé                     (Cote d’Ivoire, Sewe Sport)
17. Senzo Meyiwa                    (South Africa, Orlando Pirates)
18. Solomon Asante                 (Ghana, TP Mazembe)
19. Souleymane Moussa            (Cameroon, Coton Sport)
20. Yunus Sentamu                  (Uganda, AS Vita)


Naibu waziri wa maji Mhe Amos Makalla avamia mkoa wa Dar es salaam, abaini wizi mkubwa wa maji

$
0
0
Naibu waziri Maji Mhe Amos Makalla leo amefanya ziara ya kustukiza mkoa Dar es salaam, ambapo amekamata wezi wa maji 12, amewatimua kazi mameneja wa maji Boko na Kimara na pia ametangaza operasheni kubwa zaidi ya kusaka wezi wa maji jijini Dar es salaam
 Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akiangalia miundombinu ya wizi wa maji Magomeni
 Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akitembelea kitongoji cha Manzese kusaka wezi wa maji
 Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla  akiangalia matenki yanayoingizwa maji ya wizi manzese
 Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla  akimsikiliza Mwananchi akielezea jinsi wizi wa maji unavyoendelea Manzese
Naibu waziri wa Maji Mhe Amos Makalla  akiwa katika operesheni ya kusaka wezi wa maji Boko

JK AKIREJESHA KIWANDA CHA CHAI CHA MPONDE LUSHOTO KWA WANANCHI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano ulioandaliwa rasmi kuwaambia wananchi wa Mponde, Halmashauri ya Wilaya ya Bumburi, Lushoto mkoani Tanga, kuwa Rais Jakaya Kikwete amekubali kukirudisha Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi baada ya mgogoro dhidi mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mula uliodumu kwa takribani miaka 10 na kusababisha kiwanda hicho kufungwa maiaka miwili iliyopita na kuwaacha wananchi kwenye lindi kubwa la umasikini.

Hayo ni Mafanikio ya Katibu Mkuu wa CCM,  Abdulrahman. Kinana ambaye katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba mwaka jana katika Kijiji cha Mponde, aliahidi kupata suluhu ya mgogoro wa kiwanda hicho ulioshindikana kutatuliwa kwa muda mrefu kwa kuupeleka kujadiliwa katika Kamati Kuu ya CCM na kupata ufumbuzi ndani ya mwezi mmoja, ahadi ambayo aliitimiza.

Kiwanda hicho kilifungwa baada ya wananchi kususia kuendelea kulima mashamba ya chai kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutatua haraka mgogoro dhidi ya Mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mulla, ambaye walidai kuwa alikuwa anawanyanyasa wakulima wa zao hilo pamoja na wafanyakazi kuwalipa ujira mdogo.

Kinana amesema Serikali itanunua hisa za mwekezaji ili aondoke na kuwaachia wananchi kiwanda hicho.Pia Serikali itatuma jopo la wataalamu watakao tathmini hasara iliyopo, na kutafuta mtaji wa kukifufua kiwanda  ili kianze kufanya kazi
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamba akiishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kukirudisha kiwanda hicho kwa wananchi ambapo pia alimshukuru Rais Jakaya Kiwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman kwa kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata haki yao hiyo walioisotea kwa takribani miaka 10.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba wakati alipowasili jimboni humo katika wilaya ya Lushoto, akiwa katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Mponde na kuwataarifu wananchi na wakulima wa Chai kuhusu maagizo ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kukirejesha kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi .
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Mh.Majid Hemed akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika kijiji cha Mponde,mkoani Tanga.
 Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini.
 Mkutano ukiendelea katika uwanja wa Mponde,katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga jioni ya leo.

PICHA NA MICHUZI JR -BUMBULI-TANGA.

AWARD WINNING FASHION DESIGNER LINDA BEZUIDENHOUT IS THE DESIGNER OF YEAR (2014) FOR VIVA INTERNATIONALE MAGAZINE

$
0
0
Award Winning Fashion Designer Linda Bezuidenhout is the Fashion Designer of the Year (2014) for VIVA INTERNATIONALE MAGAZINE and will be featured in the upcoming issue. For more CLICK HERE

SERIKALI YAREJESHA KIWANDA CHA CHAI CHA MPONDE MIKONONI MWA WANANCHI.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano ulioandaliwa rasmi kuwaambia wananchi wa Mponde, Halmashauri ya Wilaya ya Bumburi, Lushoto mkoani Tanga, kuwa Rais Jakaya Kikwete amekubali kukirudisha Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi baada ya mgogoro dhidi mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mula uliodumu kwa takribani miaka 10 na kusababisha kiwanda hicho kufungwa maiaka miwili iliyopita na kuwaacha wananchi kwenye lindi kubwa la umasikini.

3 apartments for rent Located at Tegeta Namanga

$
0
0
3 apartments for rent Located at Tegeta Namanga near Latham school not far from kibo complex. Easily accesible from bagamoyo road also from bahari beach. Rent usd 500 per month each.  Contact 0788400101 or 0715744522.  


Article 15

IPTL yashusha bei ya umeme kwa asilimia 20

$
0
0
KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwa chini ya uongozi wa kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP) imetangaza kufikia kwa punguzo la bei ya umeme la asilimia 20 baada ya kufanya marekebisho makubwa ya injini za mtambo huo ya masaa 36,000 ikifanya kazi, zoezi iliyokamilika ndani ya mwanka 2014. IPTL pia imetangaza kuwa bei yao ya umeme ikitarajiwa kushuka zaidi kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta mazito. 

Marekebisho hayo yaliyotumia zaidi ya Dola za kimarekani milioni 25 yameiwezesha mitambo ya IPTL kuwa katika nafasi nzuri ya kuzalisha umeme wa uhakika kwa kufikia megawati 100 na kuingiza katika gridi ya Taifa mara to baada ya kukamilika kwa zoezi hilo mnamo Desemba mwaka 2014.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Harbinder Singh Sethi, IPTL sasa imepunguza bei ya umeme wake inaoutoza kwa Shirika la ugavi wa umeme Tanzania (Tanesco) ambao sasa utakuwa chini ya bei ya awali iliyokokotolewa ya senti 23 dola za kimarekani kwa Kilowati; huku ikihakikisha kupatikana kwa umeme wa uhakika.

"Tukiwa tunaukaribisha mwaka 2015, IPTL inajivunia kutangaza kuwa imefanikiwa kufanya marekebisho makubwa ya mashine zake ya masaa 36,000 ya kufanya kazi, zoezi iliyokamilika ndani ya mwaka wa 2014. Nimeiomba timu ya IPTL kupanga mapema jinsi gani wanaweza kuongeza juhudi zaidi kufikia marekebisho ya masaa 48,000, katika awamu inayofuata katika mwaka 2015. Tunatarajia uwepo wa IPTL kuwa bora zaidi kwa kuwa sasa tunajipanga kuongeza rasilimali zaidi.

"Hii ni sehemu ya ahadi ya PAP kuhakikisha kuwa IPTL inaendeshwa vizuri na kwa ufanisi. Wakati sasa umefika kwa TANESCO kuwa na uhakika wa kupata umeme wa uhakika wa megawati 100 katika gridi ya taifa wakati wowote utakapohitajika.

"IPTL chini ya PAP haiangalii tu uzalishaji wa umeme wa kutosha, lakini pia ipo makini kuhakikisha kuwa umeme huo wa kutosha unakuwa nafuu. Kwa maana hiyo, tumeamua kushusha bei zetu za umeme kufikia chini ya bei iliyokokotolewa ya hapo awali ya senti 23 dola za kimarekani kwa uniti, ambayo sasa inaleta jumla ya punguzo la bei la asilimia 20 kwa ile iliyokuwa ikitozwa na IPTL  kabla ya PAP kuchukua uongozi," alisema.

Bw. Sethi aliongeza kuwa TANESCO itarajie punguzo zaidi la bei ya umeme kufikia kiwango cha chini ya Senti 8 Dola za kimarekani kwa kila uniti ya umeme mara baada ya mitambo ya IPTL kupanuliwa na kufikia uzalishaji wa megawati 500 mitambo yake ikitumia gesi asilia.  

Alisema kuwa mpango wa upanuzi wa mitambo hiyo unaendelea vizuri, akiongeza kuwa iko katika hatua za awali za uchanganuzi na upimaji wa udongo.

"Tunatarajia hatua za upanuzi kwenda haraka ili kuhakikisha kuwa IPTL inatoa huduma bora, ya uhakika na nafuu katika taifa hili. Ningependa kutoka shukrani zangu kwa uongozi wa TANESCO na Gridi ya Taifa kwa kukubali umeme unaozalishwa na IPTL,"alisema.

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali kutoka TANESCO, bei za umeme zinazotozwa na IPTL kwa sasa zimeshuka na kufikia chini ya Senti 19 Dola za kimarekani kwa uniti za umeme kutokana na kushuka kwa bei ya Mafuta mazito wakati wa kipindi cha ukokotoaji wa bei hizo.


Upatikanaji wa umeme wa uhakika kutoka IPTL tayari umeshathibitika wakati wa kipindi cha sikukuu kilichopita ambapo nchi haikukumbana na mgawo wowote ikilinganishwa na miaka iliyopita ambapo ilikuwa ni kawaida kwa umeme kukatika katika wakati wa msimu wa sikukuu ambapo kunakuwa na mahitaji makubwa.

MAALIM SEIF AKIZINDUA MRADI WA MAJI SAFI,PEMBA

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, alipofika eneo la Vikunguni kwa ajili ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika eneo hilo.
Bango la mradi wa maji Vikunguni baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo.
Baadhi ya wananchi pamoja na wakandarasi wa kampuni ya SINO-HYDRO LTD ya China, wakimsikiliza Maalim Seif wakati akiwahutubia wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika eneo la Vikunguni.

Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images