Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 692 | 693 | (Page 694) | 695 | 696 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza matembezi ya Siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa akiwa na Viongozi wengine yaliyoanzia katika Uwanja wa Tumbaku hadi Uwanja wa Amaan Studium leo asubuhi ambapo yamejumuisha Vikundi mbali mbali vya Unguja na Pemba.
  Miongoni mwa vikundi vilivyoshiriki katika matembezi ya Siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa ni kikundi cha KVZ Fitness Group kikiwa katika hali ya ukakamavu na nidhamu ya juu wakipita katika barabara Kariakoo kuelekea Komba wapya ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyaongoza matembezi hayo leo asubuhi.
  Kundi la Mazoezi Zoni C wakiwa na bango lao linalosomeka "Siku ya Mazoezi Kitaifa 01Jan 2015 Mazoezi ni Tiba Mbadala",kama wanavyoonekanwa wakiwa katika matembezi ya Siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa leo yaliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).


  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

  Jumla ya watoto 63 wamezaliwa katika mkesha wa mwaka mpya 2015 katika hospitali za Temeke,Kinondoni pamoja na Ilala jijini Dar es Salaam.

  Hospitali ya Temeke wamezaliawa watoto 19,Muuguzi wa zamu ,Rolester Kinunda alisema watoto 10 ni wakiume na tisa (9) ni wa kike  na wazazi wa watoto hao wamejifungua salama na wameshapewa ruhusa .

  Hospitali ya Amana Ilala watoto 21 wamezaliwa 11 wakiwa ni watoto wa kike  na wakiume 10 na  mapacha moja na kati ya watoto hao 21 wawili walifariki dunia.

  Katika hospitali ya Mwananyamala iliopo kwenye Wilaya ya Kinondoni watoto 23 ambao kati yao watoto nane (8) ni wa kike na 15 ni wakiume  ambapo  wazazi pamoja na watoto waliruhusiwa.

  Wauguzi katika Hospitali zote walitueleza kuwa watoto wote wamezaliwa wakiwa na afya bora na hakuna mtoto aliyezaliswa kabla ya siku zake (Njiti)

  0 0

  Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu, katika picha ya pamoja , Desemba 31, 2014 na baadhi ya wazee wasiojiweza wa Kambi ya Funga Funga iliyopo Manispaa ya Morogoro.
  Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu, akimkabidhi zawadi ya vyakula na mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya 2015 kwa Wazee wasiojiweza wa Kambi ya Funga Funga iliyopo Manispaa ya Morogoro, mnamo Desemba 31, 2014, zawadi hiyo ilipokelewa na Mwenyekiti wao Joseph Kaniki. ( Picha na John Nditi).

  Na John Nditi, Morogoro

  VIJANA wa chama cha Mapinduzi UVCCM wameshauriwa kujenga tabia ya kusaidi wazee wasiojiweza, kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwa lengo la kuwapa faraja badala ya kuachia jukumu hilo kwa serikali pekee kama  ilivyo sasa.

  Kauli hiyo ilitolewa Desemba 31, 2014  na Mjumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) wilaya ya Morogoro vijijini, Lulu Mtemvu,wakati alipotembelea kituo cha kuwatunza wazee wasiojiweza cha Fungafunga cha Kichangani Manispaa ya Morogoro.


  0 0


  0 0


  0 0

  KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, kesho kinajitupa kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kuvaana na timu ya African Lyon, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza. 
  Ofisa habari wa Friends Rangers, Asha Kigundula, alisema kuwa mchezo huo wa pili kwa timu hizo ikiwa ni mzunguko wa pili wa ligi hiyo. 
   Kigundula alisema kuwa kikosi chao kipo katika hali kubwa ya kuhakikisha haitapoteza mchezo huo. 
   Alisema kikosi chao chini ya kocha wao Ally Yusuph 'Tigana' kina matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo. 
   Kigundula alisema licha ya kutambua ugumu wa mchezo huo, lakini wana matumaini ya kufanya vizuri. 
   Alisema endapo watafungwa au kutoka sare timu yao itakuwa imepoteza mwerekeo wa kupanda daraja. 
   "Mchezo huo ni lazima tushinde; tusiposhinda tutakuwa tumejiweka pabaya zaidi katika kupanda ligi kuu msimu ujao"alisema Kigundula. 
   Rangers inashika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi daraja la kwanza baada ya kupoteza mechi yake dhidi ya Lipuli, kwa kufungwa bao 1-0, kwenye Uwanja wa Samora Mkoani Iringa.
   African Lyon
  Friends Ranger

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakijumuika na wananchi katika kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukurani kwa Mashekhe wa Bagamoyo na wananchi kwa kumuandalia hafla ya kumuombea dua katika mkesha wa mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiomba dua pamoja na Mashekhe wa Bagamoyo na wananchi wakati wa hafla ya kumuombea dua katika mkesha wa mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa jamii ya wamasai wanaoishi mkoa wa Pwani. Kiongozi mkuu wa jamii hiyo, Laiboni Tikwa Moreto (wa pili kushoto), Majaliwa Lihalei na Zuberi Tangono katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani. PICHA NA IKULU

  0 0

  Mrakibu msaidizi wa Jeshi la polisi (ACP) mkuu wa kitengo cha elimu kwa umma makao makuu ya usalama barabarani jijini Dar-es-salaam,Abel Swai,akiwahamasisha abiria wa basi la kampuni ya France line lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Arusha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi endapo watagundua dereva mlevi au akiendesha gari vibaya,ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya"Wait to send"inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
  PC.Abdalah Ramadhani kutoka trafiki makao makuu Dar-es-salaam,akitumia chombo maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati zoezi la kampeni ya"Wait to send" lililofanyika katika kituo cha mabasi cha Misuna Singida mjini inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.


  0 0

  Kikosi cha Timu ya Mara (jezi Nyekundu) wakisalimiana na Marefa wa mchezo huo tayari kwa Mtanange wa Women Taifa Cup kuzinduliwa leo jijini Mwanza kwa Kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Mh Jamal Malinzi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Mara kabla ya Mechi ya Uzinduzi wa mashindano ya Mpira wa Miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Women Taifa Cup kuanza katika dimba la CCM kirumba leo Jijini Mwanza
  Baadhi ya Viongozi wa Mpira wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Viongozi wa TFF na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo Wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Mechi ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Women Taifa Cup kuanza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
   Kikosi Cha Timu ya Mwanza kikiwa tayari kukabiliana na Timu ya Musoma
   Kikosi cha timu ya Mara. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
    

  0 0  0 0


   Komandoo Hamza Kalala bosi wa Utalii Band
  Bwa' Chuchu (RiP)


  0 0

  1
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akizunguza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya tume ya uchaguzi jijini Dar es salaam wakati alipozungumzia maandalizi ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura, kura ya maoni ya Katiba mpya na uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu, kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Julius Mh.Julius Mallaba.
  2
  Baadhi ya waadishi wa habari wakiwa katika kutano huo.


  NA CHALILA KIBUDA ,GLOBU YA JAMII DAR


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutumia Bilioni 293 kwa ajili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa mwaka huu ikiwa ni lengo kukuza demokrasia nchini.


  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo ,Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema wamejipanga kuhakisha watu wenye sifa za kupiga kura wanajiandikisha ili waweze kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa  pamoja na kupiga kura ya uchaguzi mkuu   Oktoba mwaka huu.


  Lubuva alisema kuwa suala la kuwepo wanajeshi katika uchaguzi , wataangalia jinsi gani  ya kufanya  na kazi ya ulinzi ibaki mikononi  mwa jeshi la polisi.


  ‘’Suala la ulinzi wa jeshi  tuliweke na kuangalia jinsi gani tutafanya katika kuhakikisha wananchi wanapiga kura kwa amani na usalama wa mali bila kuwa na hofu ya watu wanaowalinda’’alisema  Jaji Mstaafu Damian Lubuva.


  Aidha alisema uandikishaji wa majaribio, utambuzi wa alama ya mpiga kura kwa kifaa cha BVR ulikwenda vizuri na mapungufu yaliyojitokeza wataendelea kuboresha ili kila mtanzania aweze kujiandikisha na kupiga kura.


  Alisema uandikishaji wa kanda ya kwanza utaanza Februari 16 hadi Machi 15 ambapo hakutaja mikoa gani itaanza hivyo wanaandaa orodha ya mikoa na kanda katika jinsi ambavyo daftari la kudumu la mpiga  litavyoweza kupita  kuandikisha.


  ‘’Mambo yote yatakwenda sawa baada kukamilika kwa daftari la mpiga kura likiwemo upigaji kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa  na maoni ya wadau yataendelea kupokelewa katika ofisi yetu’’alisema Jaji Lubuva 


  0 0

  Mwanasheria wa uhamiaji Fatmata Barrie akizungumza na wanaDMV kwenye mkesha wa mwaka mpya
  Katika mkesha wa mwaka mpya (2014-2015), Jumuiya ya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia , kulikuwa na matukio mbalimbali.
  Moja wapo lilikuwa ni maelezo ya mwanasheria wa uhamiaji Fatmata Barrie kuhusu maamuzi mapya ya serikali ya Marekani kwenye sheria za uhamiaji.
  Karibu umsikilize

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akizindua Tawi la CCM la Wajasiriamali Bodaboda na Mama lishe lililopo Mgulu wa Ndege Kata Ya Mkundi Manispaa ya Morogoro.Mara Baada ya Kuzindua Tawi Hilo Mh Abood Aliongea na Wanachama wa Tawi Hilo Kisha Kuwaelekeza Kujiunga Kwenye Vikundi vya Wajasiriamali Yeye Atakuwa Tayari kuwawezesha Mitaji ya Kufanya Shuguli za Kujiletea Maendeleo.

   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Meza Kuu Sambamba na Katibu wa CCM Kata Ya Mkundi tayari Kusikiliza Kero zinazowakabili wakati wa Kata hiyo,ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na Barabara.

  Aidha Mh Abood ametoa majibu Kuhusu Kero hizo na kusema kuwa Serikali imeiweka Kata hiyo Kwenye Bajeti ya Serikali ya Mwaka huu .Kuhusu Maji Mh Abood alitoa Shilingi Milioni 11 Kwa jili ya Kununua Vifaa vya Kuwezesha Kufikisha Maji katika eneo la Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi.Pia Alitoa Shilingi Milion 2 kwa ajili ya kuhakikisha barabara zote za Kata hiyo zinachongwa.
   Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi Jimbo la Morogoro Mjini Akisoma Risala yake Kwa Mbunge wa Jimbo Hilo Mh Aziz Abood.

  0 0  0 0  Sikukuu ya Maulid kitaifa inaratajia kufanyika wilayani Korogwe mkoani Tanga Januari 4 Mwaka huu. 

  Kwa taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (Bakwata),Suleiman Said Lolila ilisema Maulid itaanza Januari 3 na kumalizika Januari 4.


  Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania ,Issa  Bin Shaaban Simba anawatakia waislaam na wananchi kwa ujumla maulid njema.


  Hata hiyo Katibu Mkuu Lolila aliwataka waislam wote nchini kushirikia kikamilifu katika mazazi ya M.tume mohamad (S. AW)

  Wabillah Tawfiq.  0 0

  Gwiji la Muziki wa Kizazi Kipya, Profesa J. akiwapagawisha mashabiki waliofika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kushuhudia Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua” lililofanyika jijini Dar es Salaam mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015  jana.
  Wasanii wa Kundi la Wanaume Family wakitoa burudani kali wakati wa Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua” lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jijini Dar es Salaam jana.
  Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki, akiwapagawisha mashabiki wake waliofurika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kwenye Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua”lililofanyika jijini Dar es Salaam,Mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jana.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Ndg Phares Magesa akiwa na kiongozi wa chama cha wachezaji wa soka Temeke Ndg. Kapilima akimkabidhi mchango kusaidia kuimarisha chama hicho wilayani Temeke.

  0 0

  Na Chalila Kibuda
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dk.Mighanda Manyahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Kwa taarifa iliyotolewa leo na kwa vyombo vya habari  na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini ilisema ,kufuatia uteuzi huo,Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter  Muhongo amewateua Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO .

  Wajumbe wa bodi walioteuliwa ni Kissa Vivian Kilindu,Juma Mkobya,Dk.Haji Semboja,Shabaan Kayungilo,Dk.Mtesigwa Maingu,Bodi Mhegi,Felix Kabodya pamoja na Dk.Nyamajeje Weggoro.

  Taarifa hiyo ilisema bodi hiyo imeanza kazi Januari 1 na itaishia Februari 31 Mwaka 2017


  0 0

  Na Mdau Sixmund J.B

  Shirikisho la mchezo wa Bao nchini (SHIMBATA) nilatarajia kufanya Tamasha kubwa la mchezo huo kwa ajili ya kumuunze aliekuwa mlezi wa mchezo huo hapa nchini Hayati Mzee Rashidi Mfaume Kawawa kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka mitano ntangu afariki Dunia.

  Tamasha hili ambalo litaudhuriwa na wanafamilia ya Mzee Kawawa wakiwemo watoto wake Mh Vita R. Kawawa Mbunge wa Namtumbo (CCM) na Mh Zainabu R. Kawawa Mbunge viti maalumu (CCM) linatarajiwa kufanyika hapo kesho Tarehe 3/01/2015 katika viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM.

  “Tamasha hili ni kubwa na nimahususi kwa kumuenzi Mzee wetu Mlezi wetu ambae pia ni Muhasisi wa Taifa hili Mzee Kawawa, kwani mchango wake kwa maendeleo ya mchezo huu ni mkubwa sana, na pia Mjane wa Hayati Mzee Kwawa atakuja kuungana nasi, yeye atakuja mchana saa sita hadi saa nane.

  Nichukuwe nafasi hii kuwaalika watanzania wote, wanahabari na wafadhili mbali mbali wajitokeze kuupa heshma mchezo huu kama sehemu ya kumuenzi Mzee wetu Kawawa”. Alisema Rais wa Bao nchini Bw Mandei Likwepa.

  Mchezo wa Bao ni moja ya michezo mikongwe hapa nchini na ambao unahistoria kubwa hasa katika ukombozi wa Taifa hili la Tanzania, na umekuwa ukichezwa sana na Hayati Baba wa Taifa Mwl J.K.Nyerere enzi za uhai wake.

older | 1 | .... | 692 | 693 | (Page 694) | 695 | 696 | .... | 3282 | newer